Gabo Hana Hadhi ya Kuwa na Bifu Na Mimi- Duma

Muigizaji wa Bongo movie Daudi Michael maarufu kwa Jina la usanii kama Duma amefunguka na kudai kuwa hana bifu na msanii mwenzake Gabo na wala hana hadhi hiyo.

Kwa muda mrefu kumekuwa na kama ugomvi fulani kati ya Duma na Gabo na hata juzi juzi tu wawili hao wameonekana wakirushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii na hata vyombo vya habari.

Lakini Duma amedai hana bifu na Gabo na taarifa zinazoendelea kusambaa Kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii sio za kweli.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Duma alisema hayupo katika bifu na Gabo kama watu wa mitandao wanavyovumisha ingawa hana mawasiliano naye kwa sababu hana kitu cha kuongea naye ila akiwa na kazi anaweza kufanya naye na akamlipa.

Sina bifu naye kabisa na wala hatuna mawasiliano kwa sababu mimi ni bosi wa kampuni yeye ni msanii wa kuigiza sasa tutaongea kuhusu nini? Labda nikiwa na kazi nitamwita afanye na nitamlipa ila najua yeye hawezi kuniita kwa sababu hajawahi kuzalisha filamu”.

Kwa muda mrefu sasa wasanii hawa wamekuwa wakisikika wakirushiana madongo kama hayo lakini sababu kamili ya kutoelewana haijulikani.

Faiza Adai Gabo ni King’asti Kwani Alimtafutia Jimama La Kumlea

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally amefunguka mazito na kudai kuwa msanii mwenzake Gabo ni king’asti na hata kudai alimtafutia mwanamke mwenye hela ili amlee.

Bifu la Faiza na Gabo lilianza siku za nyuma baada ya kuigiza movie moja ambayo haijatoka mpaka leo ambapo Faiza ameonyesha kumlaumu Gabo na kudai amemtapeli.

Kwenye mahojiano na Kiss Fm Radio Faiza amefunguka na kukataa tetesi za yeye kuwahi kuwa Kwenye Mahusiano na Gabo na kuweka wazi kuwa Gabo alikuwa King’asti wa rafiki yake:

Ukweli ni kwamba Gabo alikuwa king’asti nilimpa  rafiki yangu anaitwa Karima yaani mtu ambaye nilimpa kazi na nikampa na demu ambaye ana hela”.

Faiza amedai mwanamke huyo ambaye alimpa Gabo ni mwanamama wa kizungu ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona Gabo na mara moja wakaanzisha mahusiano na kudai kuwa Gabo amehongwa sana.

Gabo na Duma Watoleana Maneno Kisa Kauli Ya ‘Kanumba Wapya’

Staa wa Bongo movie aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa kiume Gabo amejikuta katika vita ya maneno a Msanii mwenzake Duma baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu Marehemu Steven Kanumba.

Gabo alipofanya Interview na kituo kimoja cha habari, Gabo alisema ili kuiokoa Bongo Movie wanahitajika kuandaliwa wakina Kanumba wengine watakaoweza kuikoa tasnia hiyo.

Baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Gabo, Duma amemjia juu na kusema hajapendezwa na kauli hiyo kwani yeye na wasanii wenzake wana uwezo sana na watu waache kumtaja Steven Kanumba.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Duma alimwaga povu hili:

Kama kweli wewe unajiamini ni msanii mzuri Ian uwezo unapambana na unajituma huwezi ukasema tunahiyaji kanumba wengine kwani sisi hataweza kufanya alichofanya Kanumba? TUnaweza ila cha muhimu ni kujituma na kujua wapi tunapokosea.

Lakini pia Duma aliendelea kumtolea povu zito Gabo ikiwemo kumtolea maneno makali:

Unajua sio kila staa ana akili timamu kuna wengine mitambo tu tupo nao Kwenye Industry lakini ndio uwezo wao umeishia hapo lakini kama unajiamini uwezo wako unaweza kufanya kazi kubwa zaidi”.

Lakini pia Duma amewataka watu waache kumtaja taja Marehemu Kanumba lakini badala yake waelekeze juhudi zao Kwenye kupiga kazi nzuri zaidi.

Faiza Ally Amtolea Povu Zito Gabo Adai Amechelewesha Mafanikio Yake

Msanii wa Bongo movie Faiza Ally amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Gabo na kudai amemfelisha na kumkosesha kupata mafanikio aliyoyategemea.

Siku ya Jumapili kwenye Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) Gabo aliibuka kidedea na tuzo tatu ikiwemo msanii bora wa kiume  na kupelekea watu kadhaa kumpongeza huku wengi wakisema amestahili ushindi Ule.

Lakini Faiza amejitokeza na kumpongeza Gabo Lakini pia amemtolea povu zito huku akimtuhumu kwa kumfanyia dhuluma ambayo imemfanya apoteze hela na jitihada zake kurudi nyuma na kushindwa kupata mafanikio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza amemtolea povu zito sana Gabo:

 

 

 

Gabo: Bongo Movie Wameacha Kazi

Muigizaji kutoka tasnia ya Bongo movie Gabo ameibuka na kudai kuwa wasanii wenzake wa Bongo movie wameacha kazi.

Kiukweli kwa mwaka huu tumeshuhudia jinsi Bongo movie ilivyoporomopa ingawa hatua za kufa kwa Bongo movie hazijaanza sasahivi lakini huu mwaka umeshinfilia kabisa like kinachosemwa kila siku kuwa tangu Kanumba amekufa Bongo movie nayo imekufa.

Mwaka huu mzima vipaji vya wasanii wengi wa Bongo movie zimeelekezwa kusiko sanaa kwani kuna mambo mengi yamefunika sanaa ikiwemo skendo za mahusiano kwa wasanii wengi, suala la siasa ndio kabisaa limepoteza wengi na pia skendo zimekuwa nyingi kuliko kazi.

Gabo ni moja kati ya wasanii wa Bongo movie anayefanya vizuri kwenye tasnia hii lakini pia amekiri kuwa wasanii wengi wa Bongo movie wamesahau kazi yao ya kuigiza lakini wameingia na kufanya kazi za watu wengine ambazo ni mbali kabisa na uigizaji wa filamu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa katika kipindi cha Enews amefunguka haya kuhusiana na ishu hiyo:

Ningezungumza kimapana zaidi ingawa najua ikawa inawagusa baadhi ya watu lakini wasisikitike lakini wachukue kama namna ya kujifunza wengi wetu tumeacha kazi zetu na kufanya kazi za watu wengine hivyo imepelekea kazi zetu kuharibika kuacha kazi yako kufanya kazi za wenzako unachanganya mashabiki ninachopenf kuwashauri wasanii wendaangu ni kuwa tubaki kufanya kazi zinazotuhusu na hii itatusaidia kukuza zaidi Industry yetu”.

 

Bifu La Gabo Na Duma Bado Linafukuta

ingawa wenyewe wanasema kuwa hawana ugomvi lakini kumekuwa na kurushiana kwa maneno baina ya wasanii wa Bongo movie kati ya Duma na Gabo Zigamba, bifu ili lilianza pale ambapo Duma alianza kwa kumponda sana Gabo na kumwambia kuwa hajui kuvaa, hata hivyo Duma amekuwa akikerwa na tabia ya Gabo kukaa kimya kwa muda mrefu bila kufanya filamu ili kikudhi kiu ya mashabiki zake.

Duma amekuwa akisema kuwa hana ugomvi wowote na Gabo ila tu anajaribu kumuweka sawa msanii mwenzie kwa sababu ni moja ya wasanii wa Bongo movie mwenye mashabiki wengi wanaopenda kazi zake, lakini ili aendelea kuwaweka msahabiki zake na kuwaongeza ni lazima  ajitaidi kutoa filamu mpya ili kuwafanya mashabiki waaendelee kumsapoti.

Hivi karibuni Duma alifunguka na kusema tena kuwa msanii Gabo amekwa akibweteka tu katika kufanya kazi, hayo yamekuja baada ya msanii Duma kufanya uzinduzi wa filamu yake ya ‘bei kali’, ambapo Duma alimualika Gabo katika uzinduzi huo lakini Gabo hakutokea.Akiongea na waandishi wa habari Duma nasema kuwa kilichomsikitisha ni kwanini Duma aliamua kutokutokea katika uzinduzi huo ilhali alipewa mwaliko.Kwa mujibu wa Duma, anasema kuwa katika sehemu kama hizo ndipo wasanii wanapopata nafasi ya kukutana na mashabiki wake na kujifunza mambo mengi anayohusiana na filamu kwa sababu kuna kuwa na mkusanyika wa watu wengi hivyo kuna mengi ya kujifunza.

alipopata nafasi ya kuongea na kuelezea kwanini gabo hakuonkana katika uzinduzi huo, msanii duma alisema “yeye kutokuwepo anakosa vitu vingi sana,gabo anashuka kimasoko,mimi na yeye hatuna mugogoro wowote ila tu tunaelezana ukweli wa mambo ilitueze kutoa tasnia hapa ilipo na  kuipeleka sehemu nyinginw.mimi simkosei heshima kwa sababu sijamkosea kitu chochote kwa sababu sijawai kumtukana tusi hata moja,Gabo ana mashabiki wengi  sana yeye anabweteka  tu, no man, fanya kazi” ameongea Duma

Inawezekana ikawa ni njia ambayo Duma anaitumia kukuza tasnia ya filamu lakini, nadhani njia inayokuwa bora zaidi ni wawili hao kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao ili kuunda mbinu itakayokuwa bora ya kukuza tasnia hiyo kwa pamoja.