Hamisa Mobetto na Lulu Wazika Bifu Lao

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wameonyesha kuwa hawana Bifu na kila mtu hana kinyongo na mwenzake.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi Februari 23, 2019 katika utoaji wa tuzo za  Filamu Zetu International Festival Film (SZIFF) mwaka 2019  ambapo Lulu alimuita kwa mbwembwe jukwaani Hamisa Mobeto.

Lulu ambaye alikuwa Mshehereshaji (MC) kwenye Shughuli hiyo aliyofanya katika ukumbini wa Mlimani City, alimuita kwa mbwembwe na kusababisha kuibuka kwa shangwe kwa watu waliokuwa ukumbini hapo.

Ninamleta kwenu mrembo, model, mama wa Watoto wawili jukwaani na si mwingine bali ni Hamisa Mobetto”.

Baada ya kupanda stejini Hamisa alienda kukabidhi tuzo kwa moja ya washindi na kurejea kukaaa katika siri yake.

Siku za nyuma Hamisa na Lulu walishawahi kuingia kwenye Bifu zito Baada ya Hamisa kumtuhumu Lulu kwa kumuibia aliyekuwa Mpenzi Wake Majizzo lakini Hamisa alitangaza kuwa hana kinyongo na Lulu Baada ya kufungwa gerezani.

Lulu Afungukia Tetesi Za Kubeba Mimba Ya Majizzo

Muigizji wa Filamu za Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuanika ukweli wote kuhusu tetesi za yeye kuwa na ujauzito wa mchumba wake Majizzo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Play List cha mtangazaji Lily Ommy wa Radio Times FM, Lulu amesema kuwa hana ujauzito kama watu walivyodhani, bali alinenepa mno kiasi cha watu kuhisi hivyo kutokana na unene wake kumfanya aonekane kama mjamzito.

Lulu Micheal

Unajua mimi nikinenepa ni asili ya mwili wangu, nina mguu mnene sana hivyo uliongezeka, mwili pia uliongezeka kwa kiasi kikubwa kwani niliongezeka kilo 20 hivyo kila mtu aliamini nina ujauzito, sikuwa na ujauzito”.

Lakini pia Lulu alifungukia Tetesi Za kufunga ndoa walipoenda China  kwa kusema kuwa yeye hajafunga ndoa nchini China kama watu wanavyodai, bali alikwenda kwa ajili ya matembezi tu.

Mimi sijafunga ndoa China kama watu wanavyodai na watu wanaongea kwa sababu sina kawaida ya kutangaza mahusiano yangu“.

 

Siwezi Kuitangaza Ndoa Kwenye Mitandao- Lulu

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kusema kuwa haweiz akaianika ndoa yake au mipango ya ndoa yake hadharani.

Lulu alivalishwa pete na mchumba wake Mkurugenzi wa EFM Majizzo mwaka jana mwishoni Baada ya kutoka gerezani, Lakini badala ya kusikika mipango ya ndoa kumekuwa kunasikika Tetesi za kuachana.

Skendo kubwa ambayo ilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii ni kuwa Majizzo alimpa kipigo Lulu na kupelekea mrembo huyo kuvua pete yake na hata tetesi zinadai ndoa hiyo haipo tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Lulu amesema wazi kuwa ndoa ipo Lakini hawezi akaanza kuitangaza kwani ni mambo ya binafsi.

Lulu amesema anataka mashabiki wamsapoti kwenye kazi zake kama ni filamu wanunue na vitu vingine Lakini kuhusu harusi yake haina umuhimu wa kufuatilia kwani hawezi kuwaangalia.

Lakini pia Lulu ameweka wazi kuwa ndoa yake na Majizzo Iko pale pale na maandalizi yanaendelea .

“Tetesi Za Kupigwa na Kuvua Pete Zinataka Kuniharibia Lengo Langu”-Lulu

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael amefunguka na kuweka wazi kuwa tetesi zilizoenezwa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amepigwa na mchumba wake sio za kweli.

Siku chache zilizopita kuna Stori zilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Lulu havai pete yake ya uchumba Baada ya kutembezewa kichapo cha Hana na mchumba wake Majizzo.

Kwenye mahojiano aliyofanya jana Januari 29 katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio E FM, Lulu amesema habari hizo zilianza kuenea baada ya kutangaza kampeni yake ya Save my Valentine wiki iliyopita.

Suala la Mimi kuvua pete na kupigwa linalosambaa kwenye Mitandao ya kijamii ni kama kuniharibia lengo langu la #Save my valentine wala siwezi kulizungumzia na kulipa airtime”.

Lakini pia Lulu ameongeza kuwa Ameongeza kuwa utakapofika wakati sahihi atalizungumzia hilo na kwamba kwa wakati huu angependa kuendelea na kampeni yake ya kusaidia wasiojiweza.

Lulu Adaiwa Kuwekewa Bodyguard Baada Ya Kuvishwa Pete

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amedaiwa kuwekewa ulinzi mzito na mume wake mtarajiwa Majizzo Baada ya kumvalisha pete.

Gazeti pendwa la Amani linaripoti kuwa tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.

Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone“.

Gazeti hilo lilithibitisha taarifa hizo wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.

Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.

Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa“.

Tangu ametoka gerezani miezi Michache iliyopita Lulu amekuwa na upepo wa bahati nzuri kwani amechumbiwa na Mpenzi Wake wa muda mrefu Majizzo na kumaliza kifungo chake rasmi.

Siwezi Kuwa Video Queen- Lulu

Msanii mkongwe wa Bongo movie Mrembo Elizabeth Michael amefunguka na kudai hawezi kuwa mtumwa wa pesa kwa kufanya kila kazi iliyopo mbele yake.

Lulu ambaye alijipatia umaarufu tangu akiwa na miaka nane Kupitia uigizaji amefunguka na kudai hawezi kutaka kufanya kila sanaa kwa sababu tu ni msanii bali ameridhika kuwa muigizaji basi.

Lulu aneweka wazi kuwa tofauti na wasanii wengi wa Bongo movie yeye binafsi hawezi kabisa kufanya kazi kama video queen Kwenye video mbali mbali za wasanii.

Nadhani kwa kiwango nilichofika ni wakati wa kushika hiki hiki, siwezi kuwa Video Queen na Actress. Siwezi kuwa mtumwa wa pesa kwa kufanya hivyo Some times ni kuweka tu mipaka ya kazi zako”.

Anasema kama ni suala la kupata kwa njia ya sanaa, uigizaji unatosha na anafikiria anahitaji kujikita zaidi huko kuliko fani nyingine, kwani anaamini ameandikiwa kupata kupitia huko na si kuhangaika huku na huko akiendekeza pesa na anaamini bila kuwa na msimamo ni rahisi kufanya hata kazi mbaya.

Mama Kanumba- Siwezi Kuhudhuria Harusi Ya Lulu na Majizzo

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ ametoa povu zito hivi karibuni baada ya kuulizwa Kuhusu Ndoa ya Lulu na Majizzo.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na mpenzi wake Majizzo wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Mama Kanumba amefunguka kuwa, endapo atapelekewa kadi ya mwualiko wa harusi hiyo hawezi kwenda kwa sababu tangu atoke gerezani hawajawahi kuonana na Lulu wala kusalimiana naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mama Kanumba amedai kuwa, hata hiyo habari yenyewe ya Lulu kuolewa na Majizo anaisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba hajui lolote.

Kwanza hiyo habari yenyewe nimeisikia kwenye vyombo vya habari, lakini mimi sijui kabisa kama wanaweza kuniletea hiyo kadi ya mwaliko na hata wakiniletea siendi.

Najua itakuwa ngumu tu katika mazingira tuliyopitia sisi, kwanza mimi sasa hivi muda mwingi ninajikalia nyumbani tu kutoka na maradhi yangu haya presha”.

Mama Kanumba aliweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kutoka jela mapema baada ya kupata msamaha wa Raisi na kupewa kifungo cha nje mapema mwezi uliopita.

Bahati Kutoka Kenya Bado Yupo Na Lulu Kichwani Kwake

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Kenya Bahati amekiri Elizabeth Michael maarufu kama Lulu bado anamchanganya kichwani baada ya kuharibu makubaliano yao siku za nyuma.

Bahati alishawahi kufunguka na kusema mwaka 2016 alitoka nchini Kenya mpaka Tanzania kwa ajili ya kumtaka Lulu awe Video vixen Kwenye wimbo wake unaoitwa Maria lakini alipofika hotelini ambapo walipanga kukutana kwa ajili ya kikao Lulu hakufika

Bahati alidai baada ya Lulu kumgeuka na kukataa kutokea mwishoni kabisa hivyo ikabidi amuweke Jokate kwenye video ya wimbo huo ingawa chaguo lake lilikuwa Lulu.

Safari hii  Bahati amerudi tena Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi na msanii wa WCB, Mbosso, hata hivyo bado anakumbuka alichofanyiwa na Lulu.

Ilikuwa meeting ya video vixen, kama alinifanyia hivyo je anayempenda inakuwaje?, na mimi nilikuwa nimeweka shilingi kidogo, naongea kwa uchungu”.

Siku za nyuma msanii huyo alishawahi kukiri kuwa anampenda Lulu na kama angepata bahati ya kuwa naye basi bila Shaka angejiona mwenye bahati.

RC Makonda Atangaza Ndoa Ya Majizzo na Lulu

Mkui wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza rasmi kuwa Muigizaji wa Bongo movie Lulu Michael na Mkurugenzi wa EFM Majizzo watafunga ndoa hivi karibuni.

Kumekuwa na tetesi nyingi tangu Lulu atoke gerezani wiki chache zilizopita ikiwemo kuwa ni mjamzito na kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Majizzo.

Hatimaye Paul Makonda amethibitisha taarifa hizo baada ya kuandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ni mwenye kati wa shughuli hiyo ambayo itafanyika hivi karibuni lakini hajweza kutaja tarehe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram RC Makonda kaandika maneno haya:

Nikiwa mwenyekiti wa  kamati ya Harusi ya bwana Majizzo na Bi Elizabeth Michael (Lulu) nimeupitisha huu wimbo wa Mrisho Mpoto na Harmonize kuwa ndio winbo rasmi wa Harusi yao, kuhusu tarehe za harusi endelea kufuatilia 92.5 Dodoma”.

Mpaka sasa Maharusi Watarajiwa hawajathibitisha taarifa hizo.

Lulu alifungwa jela mwaka jana mwishoni baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia marehemu Steven Kanumba.

Baba Kanumba Afurahishwa na Kitendo Cha Lulu Kutoka Gerezani

Baba mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka na kuweka wazi furaha yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani kupewa kifungo cha nje.

Tofauti na Mama Kanumba ambaye aliweka wazi kuwa alikasirishwa na Kitendo Cha Lulu kuachiwa huru, Baba Kanumba ameweka wazi kuwa hana neno na Lulu na amefurahi alivyotoka kwani hata kama angefungwa miaka 100 mwanaye hawezi rudi.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ijumaa Wikienda Baba Kanumba amesema yeye ni mcha Mungu hivyo hawezi Kubeba kinyongo dhidi ya Lulu.

Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu na kila kinachotokea ni mapenzi yake, siwezi kulaumu kwa nini Lulu ametoka bali nimefurahi kwa sababu hata angefungwa miaka mia moja, Kanumba tayari alishafariki dunia, hawezi kurudi duniani.

Silaumu kwa sababu mimi ni mcha Mungu hivyo Mungu ndiye amesema suala hilo lifikie tamati kwa namna hiyo, wanaopinga na kusema siyo haki, hayo ni mawazo yao maana kama ni kifo cha mwanangu kiliniuma sana, lakini sasa siwezi kumlazimisha Mungu afanye mimi binadamu ninavyotaka maana hata neno lake linatufundisha kwamba tusamehe“.

Lakini pia Baba Kanumba amempa masharti mazito  kwamba kama anataka maisha yake yaende vizuri, awe na familia nzuri kama watu wengine na amani moyoni, anatakiwa kwenda kufanya usafi kaburi la Kanumba kama ni kulia, alie na hapo atakuwa ameacha balaa na mikosi yote.

Kwa mila za kabila letu la Kisukuma ni kwamba, Lulu alitambulika kama mke wa Kanumba maana hakuna mwanamke mwingine tunayemfahamu sisi hivyo natamani angeachiwa huru kabisa asiwe na kifungo cha nje na aende tu kufagilia kaburi la mumewe Kanumba na hapo atakuwa amemaliza na kuwa huru.

Sababu Za Lulu Kutokuwepo Katika Msamaha Wa JPM Zatajwa.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amefunguka sababu za Lulu Michal  kutokuwepo katika listi ya majina ya wafugwa waliopewa msamaha wa Mh.rais tarehe 9 December mwaka huu kama vile ambavyo watu wengi walivohisi  itakuwa.Lulu  alianza kifungo chake November mwaka huu baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

Mapema mwaka huu Mh.Rais alitoa tamko la kuwasamehe wafungwa  kwa vigezo mbalimbali huku mashabiki wa msanii Lulu Michael wakiwa na matumain ya kumuona msanii wao akiwa katika moja ya wafungwa watakao pewa msamaha huu kwa sababu wasanii wengine wakongwe walipewa msamaha huo.Hata hivyo kamishna huyo alisema kuwa lulu michael aliingia gerezani kipindi ambacho mchakato wa kutafuta wafungwa wa kupewa msamaha wa Raisi ukiwa tayari ulishaaanza hivyo isingekuwa raisi kuwekwa katika list hio kama watu wanavyofikiria.

Msamaha huu haukumuhusu kwa sababu kipindi anaingia magereza mchakato wa kupata wafungwa wa kupewa msamaha tayari ulikuwa  umeshaisha.Kwaio labda misamaha mingine ijayo kama itakuwepo  lakini huu haukumuhusu kabisa.

Hata hivyo Kamishna Malewa amesema kuwa kuna vigezo vingi ambavyo huwa vinaangaliwa mpaka mfungwa kupewa msamaha au kupunguziwa kifungo chake, kwa kuangalia muda wa kifungo chake na kosa lake pia na jinsi hukumu ilivyotoka , lakini pia wanaangalia jinsi mfungwa anavyokuwa anafuata masharti ya kifungo chake na jinsi gani kifungo hicho kimeweza kumfunza kitu.

Baada ya Mh. Rais kutoa msamaha kwa watu wnegi ikiwepo Babu Seya na Nguza Viking mashabiki walianza kuhoji kwanini Lulu Michael hakuhusishwa katika msamaha huo, lakini Kamishina ameona bora kufunguka na kuelezea kwa undani swala hilo.

Lulu Michael amepewa kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Kanumba Steven aliyekuwa mpenzi wake baada ya kuwa na ugomvi uliosemekana kuwa ni wa wivu wa mapenzi.

Mafanikio Ya Lulu Michael Yazidi Kuonekana

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Lulu Michael, anazidi kuonyesha mafanikio anayoyapata katika kazi zake baada ya kupata tena donge nono kutoka katika televisheni ya Sinema Zetu inayopatikana Azam Tv inayohusika na filamu za Afrika Mashariki.Msanii huyo wa kike ambae pia ni moja wa warembo wanaosifika kwa kupendeza Bongo na inawezekana ndio msanii wa kike anaewazidi wasanii wengine, amesaini dili nono la kuwa balozi  wa (SZIFF) Sinema zetu international  festival kwa mwaka 2017/2018.

Msanii huyo wa kike ambae mwaka jana (2016) alipata tuzo ya AMVCA katika kategoria ya filamu  bora ya mwaka kupitia  filamu yake iliyojulikana kama ‘Mapenzi ya Mungu, alidhirisha kuwepo kwa mkataba wake na Sinema Zetu kwa kuandika maneneo ya kuwashukuru watu hao na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kukuza filamu za Afrika.

Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram kuelezea kwa undani juu ya tamasha ilo ambalo limeanzishwa na Azam Tv  kupitia channeli ya Sinema Zetu lenye lengo la kutoa Tuzo kwa Filamu za Afrika Mashariki Lulu Michael aliandika  “Oct 2/2017….Azam tv kupitia channel ya Sinema Zetu imezindua rasmi tamasha la tuzo za filamu  kwa upande wa Afrika Mashariki  SINEMA ZETU INTERNATIONAL FESTIVAL (SZIFF).Hizi ndizo tuzo zitakazo husisha waandaaji na wadau wa Filamu Tanzania .Ni Tuzo za Filamu kupitia Televisheni zenye nia ya  kuleta Mapinduzi katika soko la Filamu nchini Tanzania ”  alifunguka kwa undani.

Pia alionyesha shukrani zake za dhati kwa waandaji wa filamu izo kwa kumchagua yeye kuwa kama balozi kwa tanzania kuwakilisha wadau wengune wa sanaa    “Nitoe shukrani zangu za dhati kabisa kwa uongozi mzima wa  azam tv kwa heshima niliyopewa ya kuwa balozi wa tuzo hizi.hii ikimaanisha kuwakilisha  tasnia nzima ya filamu  katika tuzo hizi.”    aliongezea Lulu.

Hata hivyo Lulu alichukua jukumu la kuwa kama balozi kuhamasisha wadau wote na waandaaji wa Filamu nchini kujitolea kushiriki katika tuzo izo “mwisho nitoe  kwa waandaaji  pamoja na wadau wa filamu  kufatilia na kushiriki  katiak tuzo hizo. CC@ sinema zetu #hakikanizakwetu” alimalizia Lulu.Pongezi nyingi zimfike Lulu Michael!!!!

 

Muigizaji Elizabeth Michael akana taarifa za ndoa yake na Majay

Elizabeth Michael hivi karibuni alikuwa anasemekana kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Majay ambaye pia ni bosi wa EFM na TVE. Taarifa hii ilienea baada ya magazeti kadhaa ya Tanzania yalioandika kusema kuwa walifanya mahojiano na mrembo huyo.

Hata hivyo Elizabeth Micheal anaejulikana kama Lulu amekana taarifa hizi kupitia mtandao wa Twitter baada ya kuandika ujumbe uliosema…

“Hivi kwa Akili yenu Ndoa inatangazwaga Kwenye Magazeti!??Muwege mnajiongeza kabla ya kuparamia Story…!.”

Hii inakuja baada ya gazeti la Mtanzania lilikiri kwa kumnukuu muigizaji huyo…

“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni.”

Kwa hivi sasa inaonekana kuwa Lulu hana mipango ya kuolewa.

Alichosema staa wa filamu Bongo,Lulu kuhusu ‘kuachana’ na mchumba wake

Stori za mitaani kuhusu uchumba wa Elizabeth Michael,ajulikanaye kwa jina Lulu,mkali wa filamu Tanzania,kukatika zimemkwaza na kumpandisha hasira sio mchezo.

Inaripotiwa kua sio mapenzi mubashara tena kati yake na mpenzi wake,baada ya wawili hao kutemana kama big G.

Elizabeth Michael na Majizo

Kwa mujibu wa taarifa hii,mambo sio kama kawaida kwani pendo limevunjika huku kila moja akiongea lake.

Madai kuwa staa huyo wa filamu na mpenzi wake kuonyeshana kisogo yalienea kwenye mitandao ya kijamii huku wadaku wa town wakiongeza makali na pilipili zaidi na kudai kuwa, Lulu karejea nyumbani kwao na ana mpango wa kuanzisha maisha yake upya.

Staa huyo amekereka kuhusu stori hii,haya ndio maneno yake kwa wanahabari wanaotaka kujua kulikoni.

“Sitaki kuongelea chochote…sitaki kuongelea chochote, pliz…unajua mimi siyo mtu wa magazeti kabisa na unanijua vizuri…” amesema Lulu.

Kumbe hapendi stori za magazeti?