Kifesi Adai Diamond Amepoteza Kitu Cha Thamani Maishani Kwa Kumpoteza Zari

Aliyekuwa mpiga picha wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Kifesi amevunja ukimya na kufunguka kuhusu kuvunjika kwa Penzi la Diamond na Zari.

Kifesi aliacha kazi WCB Miezi michache iliyopita lakini ilisemekana kuwa amefukuzwa kazi na Diamond baada ya kuingilia kati Penzi la Diamond na Zari.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kifesi amefunguka na kuweka wazi kuwa Diamond amefanya makosa kuachana na Zari kwa sababu ni mwanamke anayejielewa sana.

Mimi naamini Diamond amefanya makosa sana kuachana na Zari kwa sababu Mwanaume yoyote mwenye akili na Basara atamuona Zari kama aina ya mwanamke ambaye anatamani awe naye kujenga maisha na kujenga familia.

Kwaiyo Diamond atakuwa ni wa ajabu kama akisema eti hajapoteza kitu cha thamani kwa kumpoteza Zari nitamshangaa halafu hata yeye anaelewa umuhimu wake ukilinganisha na wanawake ambao ameshawahi kuwa nao na hata alionao huwezi ukawalinganisha na Zari”.

Kifesi pia amekiri kuwa hana mawasiliano yoyote na Diamond tangu aache kazi WCB Miezi michache iliyopita lakini bado ana ukaribu na urafiki na Zari na anaongea naye kila siku.

Diamond kwa Zari apindui, Ningetaka Kurudi WCB Ningeongea na Zari.:-Kifesi

Aliyewahi kuwa mpiga picha maarufu wa diamond platinumz, kifesi amefunguka na kusema kuwa endapo angekuwa anataka kurudi WCB basi wala isingekuwa shida kwake kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuongea na zari na angeweza kurudi kazini.

Kifesi anasema kuwa yeye ndie aliyekuwa mtu aliyekuwa akisikilizwa sana na  diamond na zari pia hivyo kwake isingekuwa kazi kufanya hivyo kwa diamond latinumz.

Kwa kujiamini kabisa kifesi anasema kuwa kama angeweza kuongea na zari wala hasingepata shida kwa sababu zari angemwambia diamond kuwa kama anataka kurudiana nae basi amsamehee yeye.

Diamond hapindui kwa zari, ningeweza kuongea na zari nikamwambia kuwa hii kazi mimi nimefukuzwa na ingekuwa rahisi kwa zari kwa sababu ni dada yangu,na angeweza hata kumwambia kuwa kama unataka kurudiana na mimi basi msamehe kifesi.

Kifesi-Tangu Nimeacha Kazi WCB Diamond Hajawahi Kunitafuta

Aliyekuwa mpiga picha wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kifesi amefunguka na kudai tangu ameacha kazi WCB, Diamond hajawahi kutafuta zaidi alim-block Instagram.

Miezi michache iliyopita Kifesi alitangaza kuwa anaacha kazi WCB baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu ambapo alidai sababu kubwa ilikuwa ni kutaka kufungua biashara zake na kujikita Kwenye mambo yake kidini.

Baadae kuna taarifa zilisambaa kuwa Kifesi hajaacha kazi WCB bali alifukuzwa kazi na Diamond  kwa utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kuingilia mapenzi ya bosi wake (Diamond na Zari).

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Kifesi amefunguka na kuweka wazi kuwa tangu ameacha kazi WCB, Hajawahi kuwasiliana na Diamond na pia kukiri kuwa Diamond amemblock Instagram.

Lakini pia Kifesi amesema yeye binafsi hana beef na Diamond na hawezi kuongelea mabaya yake kwa sababu tu hayupo naye karibu na kudai yeye ni mtu mwaminifu na anampenda Diamond kama shabiki.

Kwenye Interview hiyo Kifesi aliongelea Tetesi za yeye kufukuzwa kazi ambapo amedai kama kweli angekuwa amefukuzwa basi watu wangemuona amempigia magoti Diamond amrudishe kazini na kama haitoshi angemtumia Zari ambaye amekiri Diamond hapindui kwa Zari.

Kifesi ameongelea biashara zake mpya ambapo amefungua studio ya upigaji picha na yupo mbioni kuanza kipindi chake cha mapenzi redioni lakini pia anafungua kampuni yake ya kuuza chakula.

Kifesi Afukuzwa Kazi na Diamond Baada Ya Kumshauri Arudiane na Zari

Mpiga picha maarufu wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kifesi amedaiwa kufukuzwa kazi WCB baada ya kumshauri bosi wake arudiane na Zari.

Kifesi alitumia ukurasa wake wa Instagram na kutangaza kuwa ameamua kuacha kazi kama mpiga picha wa Diamond na kujiajiri mwenyewe na kudai anataka kuwa karibu zaidi na Mungu wake kwa kupitia dini yake.

Lakini Mara tu ya habari hiyo kusambaa taarifa mbali mbali kutoka kwa watu wa karibu wa WCB walianza kudai kuwa Kifesi hajaacha kazi bali ametimuliwa na Diamond kwa tabia yake ya kupenda kuingilia maisha binafsi ya bosi wake Diamond.

Kifesi ni mtu ambaye huweka wazi siku zote kuwa anampenda Zari name hata siku alipomuacha Diamond alidai hata Kama wameachana lakini yeye bado anampenda Mama T na kumkubali.

Sasa juzi juzi baada ya Zari kuja Tanzania kusaini dili lake jipya Kifesi alitumia nafasi hiyo kumshauri tena Diamond arudiane na Zari kitendo kinachisemekana kuwa hakikukaa vizuri na Diamond ambapo aliishia kumfukuza kazi.



Kifesi Amjibu Esma Kuhusu Kufukuzwa Kazi Wcb

Aliyekuwa mpiga picha maarufu kutoka kundi la Wcb ambae aliajiriwa kwa kazi maalum ya kupiga picha alitangaza kuacha kazi hiyo kwa madai kuwa anataka kuendelea na kufanikisha ndoto za maisha yake ambazo anaona kabisa hawezi kufanikiwa kama atakuwa hapohapo kila siku, lakini pia alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anataka kumrudia mungu wake kwa sababu kwa muda mrefu  amekuwa akifanya kazi kinyume na maadili ya dini yake.

Lakini cha kushangaza  na kwamba baada ya kifesi kutangaza na kutoa tamko ilo, dada wa msanii Diamond Platinumz aliweka comment chini ya post ya Kifesi katika ukurasa wake wa instagram na kufichua siri kuwa , kifesi ni muongo ajaacha kazi bali amefukuzwa na bosi wake.

acha uongo kifesi, umefukuzwa kazi kwa kucha kufatilia maisha ya bosi wako, yametushinda sisi wewe mtu baki utayaweza-Aliandika hivyo Esma.

Hata hivyo kifesi aliamua kujibu tuhuma hizo na kukanusha kuwa hajawahi kufukuzwa kazi WCB na hata swala la kuktetea zari hajaanza kulifanya leo.

Hapana sijawahi kuachishwa kazi na kama niliachishwa kazi basi sikuwahi kupewa taarifa,ninachofahamu ni kwamba nimechukua maamuzi haya na nai kitu nilichokuwa nimekipanga tangu siku nyingi, so jana nikasema i think its aright time to do this.

kumtetea zari sijaanza leo na hata ukiangalia katika post zangu za insta utaona,nilikuwa nafanya hivyo ingawa pia ni swala gumu kulielezea.

Kifesi alimtetea Zari kwa Diamond na kusema kuwa kitendo cha Diamond kuachana na zari atakuja kukijutia maishani.

 

 

Hili ndilo onyo Kifesi alimpea Zari Hassan kumhusu Diamond linalozingua mitandao

Kifesi, mpiga picha official wa Wasafi amekuwa kizungumzio kikubwa sana Tanzania baada ya ujumbe alioutoa unao aminiwa kuelekezwa Zari Hassan.

Kifesi bila kutaja majina alipea onyo wsichana wa bongo wasifikirie kuwa kwenye instagram na kupelekwa safari ndio mapenzi rahisi.

Alieleza kuna wasichana kwenye maisha ya huyo unaye mtambua kama bwana yako ambao hawataki sifa yoyote na wanafurahia kuwa nambari mbili.

Alivyi tamka maneno yake ilionekana ni kama alaikuwa anaelezelea kuhusu Zari na Hamisa Mobetto ambao wanaminiwa kuwa wapenzi wa Diamond.