“Namtambua Young killer toka zamani” Lava Lava

Mkali mpya wa Wasafi Records Lava Lava amedai kuwa anamtambua Young Killer toka zamani wakati alikuwa aki hustle na THT.

Lava Lava ambaye kwa sasa amepata maarufu tangu kuachia wimbo wake mpya ‘bora Tuachane’ alifunguka kwa kusema kuwa wakati bado alikuwa anatafuta njia ya kuingia kwenye Bongo Industry aliweza kukatana na young killer ambaye kwa hivi sasa hamkumbuki kwa kuwa wakati huo hakuwa maarufu.

Akizungumza na Bongo 5, Lava Lava alisema,

“Msodoki mimi namkubali sana lakini pia ni mtu ambaye nilikuwa nakutana naye. Young Killer hanijui mimi lakini leo namwambia, kipindi nahustle THT alikuwa kwenye Super Nyota walikuwa wanakuja sana THT kuweka kambi hadi tukafanya tangazo fulani wote, lakini hakumbuki, yeye akaweka sauti yake mimi nikaweka yangu. Kwa hiyo mimi namjua kwanzia kule chini kabisa lakini yeye katika kutokumbuka kwake tukikutana tunaheshimiana.”

Lava Lava awatetea wasanii wa Wasafi records baada ya wengi kudai kuwa wanamuiga Diamond Platnumz

Lava Lava ambaye ni msanii mpya wa Wasafi records kwa hivi sasa anatamba kwa wimbo wake mpya ‘bora tuachane’ ambao umempa mashabiki wengi kwa muda wa wiki moja.

Baada ya kuingia Wasafi msanii huyu amepata interview kadhaa kwa redio na hivi karibuni tunatarajia kumuona kwenye televisheni.

Lava Lava
Lava Lava

Hata hivyo kama wasanii wenzake, msanii huyu ameweza kupata changamoto ambazo zinaweza kuiletea career yake shida. Hivi karibuni akizungumza kwenye interview na Bongo 5 msanii huyu alikana kuwa hakuna msanii yoyote kutoka Wasafi Records anayemuiga Diamond Platnumz. Kulingana na yeye kila mtu ananjia tofauti ya kuimba na iwapo saa zingine wengi wanaona kuwa wanaimba kama mkubwa wao…hii sio ukweli.

Alisema,

“Naona watu wanazungumza lakini watu wawe na masikio ya kusikiliza kitu. Sio watu wote wanaweza kufanana ya Diamond japokuwa kuna vitu tunaweza kufanana kwa sababu ni watu ambao tunakaa pamoja kwa muda mrefu. Pia watu wakiwa wanaishi muda mrefu pamoja huwa wanafanana, kwa hiyo kuna muda mkikaa pamoja kuna vitu mnaanza kushare lakini ukichunguza ndani yake kila mtu ana kitu chake,”

Lava Lava afunguka kuhusu bosi wake wa Wasafi Records

Lava Lava ndiye msanii mpya kwenye label ya Wasafi Records na baada ya kuachia wimbo wake mpya bora Tuachane msanii huyo ameonyesha kuwa anatalanta ambayo itampeleka mbali.

Hata hivyo hivi karibuni akizungumza na Mzazi Willy M Tuva kwenye kipindi cha Radio Citizen, Lava Lava alisema kuwa ilimchukua muda wa mwaka mmoja kukutana na Diamond Platnumz macho kwa macho.

Kulingana na Lava Lava hii ilikuwa kama mtihani kwake kwa sababu kuna wakati akate tamaa. Alimwambia Willy

“Ilikuwa inanivunja moyo sana, kwamba sasa itakuwaje na ndoto zangu ni kumuona Diamond kwa sababu ni kioo chetu mtaani tunamuangalia nikaona kama itakuwa hanifuatilii kumbe yeye anafuatilia stori zangu sema ni katika kuniona kama nina moyo na uvumilivu,”

Msanii mpya wa Wasafi Records Lava Lava azindua video ya wimbo wake-Bora Tuachane

Lava Lava ameachia wimbo mpya Bora Tuachane ambao unawazingua wengi Afrika Mashariki. Tangu Diamond Platnumz kumtambulisha kama msanii wa Wasafi…Lava Lava amepata mashabiki wengi kwa muda mfupi kuonyesha kuwa yuko tayari kuwatumbuiza wengi.

Hata hivyo Lava Lava ameachia video yake ya kwanza tangu kuingia Wasafi. Video hii imekuja siku mbili tangu kuachia audio.

Mashabiki nao pia wameonekana kumpa support msanii huyu ambaye kwa hivi sasa anawazingua wengi. Sauti yake pia ni ya kumtoa nyoka pangoni na inaonekana kuwa atawapa Harmonize, Rayvanny na Rich Mavoko competition ya kutosha. Tazama video hiyo hapa.