Linah- Siwezi Kuwa na Mwanaume Asiyekuwa na Hela

Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea kuwa na mwanaume ambaye ana hela na kamwe hawezi kuwa na mwanaume ambaye hana pesa.

Siku mbili hizi Linah amekuwa aki trend sana kwenye vyombo vya habari na social media hii inatokana na mahojiano anayokuwa anafanya kwa ajili ya kuitangaza ngoma yake mpya aliyomshirikisha Rachel Kizunguzungu inayoitwa ‘same boy’.

Linah amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv Kupitia kipindi chao cha Kikaangoni ambapo ameongelea sifa za mwanaume ambaye angependa kuwa naye huku akitia msisitizo kwenye suala la kuwa na pesa.

Kwanza mwanaume ambaye naweza kuwa naye awe mrefu kwangu maana mimi ni ka shotii alafu mimi napenda mwanaume mweusi ambaye giant wale wenye miili mikubwa alafu cha pili na cha muhimu awe na pesa ili aweze kunitunza kwa sababu tutake tusitake mtoto wa kike anahitaji kutunzwa sio lazima awe milionea hapana lakini kulingana na kazi yangu na status yangu nje mashabiki zangu wanapenda nizidi kupendeza unapochuja anakuponda huyu naye vipi anakutupa kule”.

Lakini pia Linah amezidi kusisitiza kuwa mwanaume huyo awe smart na anajielewa na anajiongeza na pia amesisitiza kuwa kikubwa ni upendo lakini ameweka wazi hawezi kuwa na mwanaume ambaye atamtegemea yeye hata siku moja.

Linah: Siko Tayari Kufunga Ndoa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga amerudi kwenye ramani ya muziki hivi karibuni na kutoa wimbo wake mpya unaoitwa ‘Same boy’ aliomshirikisha msanii mwenzake Rachel Kizunguzungu.

Linah alikuwa amepumzika kufanya Muziki kwa kipindi kirefu hakusikika hasa baada ya kuwa mjamzito mwaka jana na kujifungua mtoto wake wa kwanza wa kike aitwaye Tracey ambapo alipokuwa mjamzito Linah aliweka wazi kuwa anapumzika kufanya mziki.

Katika kuitangaza nyimbo yake mpya Linah amefanya Interview na kituo East Africa Tv kupitia kipindi cha Kikaangoni ambapo Linah alifunguka na kusema kuwa hana mpango wa kuolewa pamoja na kuzaa mtoto na jamaa yake anayeitwa Shabani au kwa jina jingine Director ghost.

Kwenye Interview hiyo Linah alifunguka na kusema:

Hilo suala la ndoa ni zito yaani ulivyotaja ndoa mpaka nimeshtuka unajua ndoa ni kitu nyeti sana siwezi kukisema tu of course napenda na ninatamani kuolewa mimi ni mtoto wa kike lakini sidhani kama niko tayari kwa sasahivi kuolewa yaani Mungu atusamehe tu tunazaa nje ya ndoa sawa lakini suala la ndoa ni la kujipanga sana”.

Lakini pia Linah amefunguka na kusema Baba mtoto wake yuko tayari kabisa kumuoa lakini yeye ndio hayupo tayari ingawa ameongezea mbali na sababu zote hizo bado kuna mambo yao makubwa yanaowafanya wasioane ambayo wote wanayaju.

Kumekuwa na tetesi kuwa wawili hao hawawezi kufunga ndoa kutokana na tofauti za kidini ambapo Linah ni mkristo lakini mpenzi wake ni muislamu.

 

Linah Ataja Orodha ya Wanaume Aliowahi Kubanjuka Nao

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kutaja idadi ya wanaume ambao ametembea nao tangu amekuwa supastaa na hata kabla hajawa staa.

Linah ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris alipata umaarufu miaka ya nyuma baada ya kuanza Sanaa yake kutokea katika jumba la vipaji Tanzania house of talents(THT).

Ingawa Linah kukiri kutulia kwa hivi sasa na mtoto wake na Baba wa mtoto wake, amekiri kuwa miaka ya nyuma kidogo ameshawahi kubanjuka na watu kadhaa ambao kwa sasa wamebaki kama historia tu katika maisha yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv, Kikaangoni Linah amefunguka na kutaja kuwa tangu amekuwa maarufu amekwisha wahi kutembea na wanaume watano tu mbali na mwanaume ambaye amezaa naye na anaishi naye kwa sasa:

Kwa haraka haraka naweza kusema nimeshatoka na wanaume watano tu toka watu wamenifahamu kama Linah sina idadi kubwa sana”.

Lakini pia Linah amesema wanaume hao watano ni baada ya kupata jina wakati tayari watu wanamfahamu kama msanii kabla hajajulikana ameshatembea na wanaume kama 10 au 15 ingawa hawakumbuki.

Penzi la Linah na Mumewe Ladaiwa Kulega Baada ya Kuzaa

Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amerudi tena kwenye vichwa vya habari huku safari hii sababu ikiwa ni mapenzi, ambapo inadaiwa penzi la Linah na mpenzi wake limeingia shubiri kidogo tangu azae.

Linah ana uhusiano wa kimapenzi na Shaban Mchomvu ambaye ni maarufu kama Director Ghost ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

Lakini tetesi zilizosambaa chini chini ni kwamba inadaiwa mapenzi yamepungua kati ya Linah na mumewe tangu ajifungue mtoto wao mwaka jana lakini pia inadaiwa Director ghost anajitahidi kumpa kila kitu mpenzi wake Linah ikiwa ni pamoja na kutengeneza studio ndani ya nyumba yao ili Linah asitoke nje ya nyumba.

Kwenye interview na ENews ya East Africa Tv, Linah amefungukia tetesi hizi na pia inadaiwa penzi limeisha kwani amekuwa hamposti Tena mumewe kama zamani:

Kwanza nitamposti niijisikia unajua kile kitu unatakiwa ufanye kwa kujisikia sio usukumwe na watu eti kisa unaogopa watu watafikiria mmeachana sababu mimi na yeye sahivi tuna miaka miwili na kitu kwenye mahusiano tumeshajuana tushakuwa tayari kama mume na mke kwaiyo kuna vitu vingine tunaona ni utoto tu havina faida labda tuseme nimempunguzia kasi lakini sio kwamba ndio simpendi au nini ila yeye ni mtu simple na ana mambo yake binafsi hana muda wa kufanya mambo ya kitoto”.

Linah amekana tetesi za yeye kuwa na ugomvi na mumewe na kusema wanafanya mambo yao private lakini pia amekiri kuwa hapendi kumposti sana kwani anavyojigamba naye sana kuna nyaku nyaku wanapata wivu na kuna wasichana wengine watataka kutembea na bwana wa mtu ilimradi wamkomeshe mke wake sababu ya kuringa.

Alichosema Linah Kuhusu Ku-Copy Wimbo wa Vannesa na Maua

Hivi karibuni wasanii wawili wa kike Linah pamoja na Recho wametoa wimbo wao mpya uliokwenda kwa jinala same boy wimbo ambao inasemekana kuwa umekopiwa kutoka katika wimbo wa Maua na Vannesa mdee uliotoka miezi kadhaa iliyopita.

Hata hivyo moja ya wasanii hao, Linah Sanga amekanusha  tetesi hizo za kuiba idea ya wimbo huo  na kusema kuwa nyimbo hizo ziko tofauti na hata idea zake ziko tofauti wanachowaomba mashabiki kukaa na kuzikiliza vizur na watagundua kitu.

Akiongea katika kipindi cha Playlist cha Efm, Linah anasema kuwa wimbo wao na Recho ulitengenezwa siku nyingi kabla hata wimbo wa Bounce haujatoka lakini walikuwa wamechelewa kuuachia wa sababu ya vitu tofauti tofauti tu.

hii ya kwetu inazungumzi kuwa sisi wote kwa pamoja tunamtaka mwanaume mmoj lakini ile ya kwao inaelezeaa kuwa wao wanatembea na mwanaume mmoja na bado  hawajuani lakini kwa upnde wa ya kwetu ni kwamba tunajuana kuwa tunamtaka mwanaume mmoja.

Wimbo huu wa Linah na Recho unakamilisha nyimbo mbili kwa wasanii hao kufanya pamoja ambapo walifanya wakwanza wakiwa na Makomandoo.

Recho anaanza kurudi kwa kasi sasa baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya kazi za muziki kutokana naathari alizokuwa amezipata baada ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Linah:Hutakiwi Kumuachia Mwanaume Wako Mwanamke Mwingine

Msanii wa muziki bongo ambae alikaa kimya kwa muda baada ya kupata ujauzito na kuingia katika majukumu ya kulea , Linah Sanga amefunguka na kuongelea swala lake yeye na baba mtoto wake kufunga ndoa kama ilivyotokea hivi karibuni kwa msanii mwenzake wa kike Shiloleh,Linah anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuuliza na yeye anafunga ndoa lini lakini anachojua yeye ndoa ni mipango ya Mungu hivyo hawei kupanga kitu.

Linah anasema kuwa anapenda sana kufunga ndoa na kukaa kinyumba na mwanaume wake aliyezaa nae mtoto kwa sababu hapendi kuzaa mtoto kila mtu na baba yake labda itokee sababu ya kumfanya kuachana na baba wa mtoto wake iwe kubwa lakini sababu haiwezi kuwa ni mwanamke mwingine.

Siwezi kujipangia nafunga ndoa lini, kwa sababu hata shiloleha hakuna aliyejua ataolewa lini .lakini kama mwanamke napenda kuolewa na ninapenda kuolewa na baba wa mtoto wangu kwa sababu katika maisha yangu nilisha apa sitatka kuzaa zaa nje huko  na baba tofauti tofauti napenda watoto wangu wawe na baba huyohuyo na mimi mama yao.

yaan labda kuwe na sababu kubwa sana ya kunifanya niachane nae na watu waone kabisa hapa linah alikuwa anafaa kuachana na huyu kuzaa na mtu mwingine.lakini so far utakiwi kumuacha mwanaume wako uanempenda kwa sababu ya mwanamke mwingine yoyote, yaani hiyo sio reason kubwa sana.unless na wewe uwe na mambo yako mengine  lakini huwezi kumuacha mwanamke wa malengo yako.

Akiongelea kuhusu kurudi katika muziki Linah anasema kuwa  kwa sasa anaanza kujipang kurudi katika muziki  kwa sababu ameshamaliza kulea na atakuja vizuri.akiongelea kuhusu tamko la kuvaa uchi linah anasema kuwa  inabidi ifafanuliwe kuvaa uchi kukoje kwa sababu kuna nguo unavaa zinakuwa za kawaida tu lakini inaweza kutasfiriwa kuwa ni nguo za uchi.

 

Kisa Umbile,Linah Sanga Amtolea Povu Shabiki.

Msanii wa bongo fleva nchini  Linah Sanga amejikuta akiingia katika vita na shabiki baada ya kuweka picha ikimuonyesha umbile lake na shabiki huyo kumsema kuwa umbile hilo ni la ku-fake kamailivyo kawaida kwa wasanii kuwa wana-fake maumbo ili waonekane.

Baada ya kuweka caption iyo,shabiki aliamvamia Linah Sanga kwa kumwambia kuwa umbile alilonalo sio lake ila ni la kubambika.lina alionekana kukerwa  na maoni ya shabiki huyo ndipo alipoamua kumtolea maneno mazito na kufika hatua ya kumwita kunguru.

we kunguru umwetumwa eeh,sijawahi kufake shape yangu hata siku moja.usinichukulie poa mbwa wewe.

                                        

Hata hivyo baadhi ya mashabiki waliendelea kumshambulia linah kwa maneno na kumfananisha na wasanii wengine wa kike ambao wamekuwa wakitengeneza maumbo yao kwa madawa au kwa kuvaa nguo za kufanya shape ionekana sana.

 

Linah Sanga: Namiliki Studio Lakini Siwezi Kuwa Producer

Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga ameongelea hali yake ya kimziki na kufunguka kuwa pamoja na kwamba anamiliki studio ya mziki lakini hajawahi kufikiria wala kudhani kuwa anataka kuingia studio na kuwa producer.

Linah amefunguka na kudai kuwa kwa msanii kufanya kazi ya kuimba na kuwa producer inakuwa ngumu ndio maana kuna watu wako maalumu kama mproducer na wengine wako maalumu kama wasanii. Ingawa kuna wasaniiambao wanafanya vyoye viwili nikimaanisha ni ma-producer na wakati huo huo ni wasanii kama msanii kutoka kundi la Navykenzo Nahreel ambaye mbali ya kuwa msanii kutoka kundi hilo lakini pia ni producer kutoka katika lebo yake ya The Industry ambayo inasimamia wasanii mbalimbali.

Linah alipofanya mahojiano na Dizzim online alifunguka yafuatayo kuhusu mziki wake na kikataa kuwa producer :

Mimi ninachoamini kwenye fani hii kama muimbaji basi imba kwa sababu huwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, yaani ukifanya huku unaimba na huku una-produce basi lazima sehemu moja kati ya hizo mbili utajikuta unaharibu kwa sababu utajikuta mwisho wa siku unaegemea upande mmoja, kwa iyo mimi sijawahi kufikiria kuwa kama nataka kuwa producer muda wowote kuanzia sasa mimi nataka tu kubaki kuwa mwanamuziki na kuendelea kuimba na kuwaachia kazi ma-producer wenyewe”.

Linah alijifungua mtoto wake wa kwanza wa kike miezi michache iliyopita jambo lililosababisha ukimya wake kwenye muziki kwa kipindi kirefu lakini Linah amehaidi kurejea studio mapema mwakani mwezi wa kwanza.

Alichojibu Linah Kwenye Comment ya Hamisa Ni Utata

Instagram sasa imekuwa mtandao usiokuwa na siri , watu wanaotumia mtandao huo wanazidi kuongezeka siku hadi siku, hivyo mambo mengi yanayofanyika yanakuwa yanaonekana kwa watu wengi, mara nyingine unaweza kuhisi hakuna hatakaeona, au watakaona ni wachache kuhusu kile unachoandika au kupost lakini si kweli.

kuna screenshot zinazosambaa katika mtandao wa instagram zikionyesha comments za Hamisa na Linah katika moja ya picha Linah alizopost hivi karibuni akiwa na baba wa mtoto wake,katika posti hiyo ambayo inaonekana kama kama kuna siri chini ya kapeti kuhusu uwepo wa mwanamke mwingine mjamzito mwenye mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie na Linah.

Katika post hiyo Hamisa aliandika”lv unajua kuwa kuna mwenzio ana mimba$$$ mdomo koma lakini” maneno haya yanayoonyesha kama kuna kitu Hamisa anajua kuhusu mwanamke huyo mwingine mwenye mimba hivyo inakuwa kama anatoa tarifa kwa Linah.

Lakini kitu cha kushangaza ni jinsi Linah alivyamua kumjibu Hamisa kuhusu taarifa hizo ambapo anaonyesha kujua kwa taarifa hizo na anaonekana kutokujali kuhusu maneno hayo” @ hamisamobetto, Najua, tulishayaongea kuna lingine” alijibu linah

Linah Sanga ambae miezi michache iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kike mwenye jina TracyParis aliezaa na mpenzi wake  , alisikika hivi karibuni akisema kuwa yeye na mzazi mwenzie huyo wanategemea kufunga ndoa ukiachalia mbali tofauti zao za kidini .

Comment ya Hamisa kwa Linah.

Hata hivyo bado kunakuwa na mishangao kwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huu wa kijamii , tena wengine wakimtolea mapovu mwanadada Hamisa mobeto kwa kitendo chake cha kuandika kitu kama hicho ambacho pengine ilipaswa kuwa siri ya familia tu, hii ina maanisha nini kuwa watu hawa wawili wapo katika , je Hamisa alishindwa kuongea na mwanadada Linah nje ya hapo.Je swala hili linapokelewaje na mwanaume aliyehusika katika jambo hili?

Hamisa Mobeto ambae hivi karibuni alikuwa na kashfa nzito ya kuvujisha picha za faragha na msanii mkubwa Tanzania na Duniani kwa ujumla Diamond Platinumz, baada ya msanii huyo kukataa katika vyombo vya habari kuwa mimba na mtoto aliyejifungua Hamisa sio wake , lakini baada ya hapo msanii huyo aliamua kukiri hadharani katika media na kusema kuwa mtoto huyo ni wa kwake.

 

Linah Aongelea Mimba Ya Mtoto Wake Wa Pili

Msanii wa Bongo Fleva ambae amekuwa kimya kwa muda kidogo kutokana majukumu ya kujifungua na kulea, EsterLinah Sanga amefunguka na kusimulia jinsi mimba  ya mtoto wake wa pili itakavyokuwa. Linah ambae alifanya arobaini ya mtoto wake wa kike anaejulikana kama Tracy Paris kama wiki mbili zilizopita amesema kuwa yeye hana mpango wa kuzaa watoto wengi bali watoto wawili tu huyo wa kwanza na ataongeza wa pili atakayekuwa wa mwisho.”Niko na mpango wa kupata watoto wawili tu , huyu wa kwanza na wapili atakuwa wa mwisho , sikuwa na  plan za kupata watoto wengi kabisa”alisema Linah

Hata hivyo katika mahojiano hayo na kituo cha Televisheni cha Eatv, Linah aliulizwa kuhisu kupiga picha kama alizopiga katika mimba yake ya kwanza “siwezi kujua,mimba itakavyokuja itanipeleka vipi maana kila mimba ina mambo yake, itategemea na muda pia,ila mimi ni msanii siwezi kuficha maana ntaenda hapa na pale , ntajulikana tu, picha ntapiga” alisema

Alipoulizwa kama kelele za mara ya kwanza zinaweza kumzuia linah kupiga picha kama zile za mwanzo linah anajibu kuwa “kelele zile hazikuniboa,kwa sababu hata nikifanya kitu kizuri kuna watu watapenda na watu wengine wataponda tu huwezi kumridhisha kila mtu,, ukipiga picha na gauni refu watakwambia mshamba, likiwa fupi watakwambia gauni fupi”

Hivi karibuni kunakuwa na tabia ya watu kupiga picha za ujauzito huku wakiacha miili yao yote nje, ambapo haikuwa tamaduni za kitanzania lakini kwasababu wanasema wanakwenda na wakati imekuwa kawaida kwao, Linah ni mmoja wa wasanii ambao walipiga picha za ujauzito akiwa ameacha wazi badhi ya maungo yako , na baadhi ya mashabiki walimtupia maneno katika mitandao kuhusu picha hizo.Kwa Linah anasema hakukerwa kabisa na kelele hizo

Linah anaendelea kuelezea kuwa kuna baadhi ya watu walikuwa wakisema amechelewa kujifungua, ila yeye mwenyewe anasema hakuchelewa kujifungua bali watu walijua mapema kuhusu ujauzito wake, alikuwa na mimba ya miezi mitatu watu wakawa tayari wamejua lakini alijifungua mimba ikiwa na wiki 36 na siku 5 ivyo huwa ni kawaida kwa baadhi ya watu ila tu alikuwa na tumbo kubwa.

Linah afunguka kuhusu ndoa yake

Mwanadada mrembo ambae kwa sasa amepotea kidogo katika muziki wa Bongo Fleva kutokana na pilika pilika za uzazi mwanadada Esterlina Sanga amefunguka na kusema kuwa tutegemee ndoa siku yoyote kuanzia sasa,Linah ambaye alibamba na vibao vingi ikiwa ni pamoja na  kile cha malkia wa nguvu.

Mwanadada huyo ambae pamoja na kuwa mjamzito ,alionekana kuwa mrembo siku zote bila kuchoka na hata baada ya kujifungua amezidi kunawiri na kupendeza zaidi,lLnah kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike   amejifungua kama mwezi tu umepita,na mtoto huyo  amepewa jina la Tracy Paris.

Linah amezaa na mchumba wake ambae anajulikana kwa jina la Shaban na wala hausiani kabisa katika tasnia ya muziki , amesema kuwa wapo katika harakati za ndoa ingawa baba wa mtoto huyo wana utoufati wa kiimani.

Imekuwa ni desturi kwa wanamuziki wengi wakike kujishauri sana katika swala la kubeba mimba na kuzaa huku wengine wakikataa eti wataharibu miili yao, lakini hii ni tofauti na kwa mrembo huyo Linah ambae yeye anasema kuwa alikuwa ameshaamua kwa moyo mmoja  na wala hakusita kubeba mimba kwa sababu alikuwa anatamani mtoto ivyo kubeba mimba haikumpa shida.

Akielezea kuhusu baba huyo wa mtoto ,Linah anasema kuwa “Unajua huyu mchumba wangu alinipenda tangu 2009, ndio kwanza naanza kutoka lakini hakupata muda wa kunifikia hivyo anajua kazi yangu na ndio maana niko nae amekubali kila kitu changu’

Akiongelea swala la ndoa anasema kuwa ndoa ipo karibuni, na kuhusu swala la yeye kuwa dini tofauti na baba mzazi wa mtoto wake ambae wanaimani tofauti Linah anasema kuwa yeye wala haoni shida yoyote kuolewa na mtu wa dini tofauti,

Msanii huyu wa kike ukiacha katika kupitia katika mahusiano tofauti mpaka kufika hapa alishawahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzie kutoka THT Amini lakini waliachana, na alipoulizwa kuhusu amini linah alijibu “Mimi na Amini tunaheshimiana sana kwa kuwa tayari ana mke wake na mimi nina mtu wangu”