Soudy Brown na Maua Sama Watiwa Mbaroni

Mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv, Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Iokote’ wamekuwa mbaroni mapema jana.

Soudy Brown na Maua Sama wanadaiwa kukamatwa na Polisi Kinondoni lakini mpaka jana jioni tayari walikuwa wameshahamishiwa Central Polisi.

Bongo 5 wanaripoti kuwa wawili hao walishikwa siku ya jana baada ya kupost video mtandaoni inayowaonekana watu wakicheza wimbo ‘Iokote’ wa Maua Sama huku wakiwa wanakanyaga hela.

Kamanda wa polisi kanda maalumu Dar, Mambosasa amefunguka na kuweka wazi kuwa Polisi inamshikiria mtangazaji Soudy Brown na mwanamuziki Maua Sama  kwa kosa la uharibifu wa mali. Inadaiwa wameonekana mtandaoni wakirusha hela na kuzikanyaga jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Maua Sama Afungukia Tetesi Za Kumwagwa na Mzungu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Maua Sama Amefunguka na kuongelea tetesi zilizosambaa nwneye mitandao ya kijamii kuwa hivi Karibuni ametoswa na mpenzi wake.

Maua Sama ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma na ngoma yake ya Amen hivi sasa bado yupo Kwenye gemu na anatamba na ngoma yake ya Iokote ambayo inasikika kila kona.

Pamoja na kufanya vizuri katika muziki wake lakini inadaiwa Msanii huyo hafanyi vizuri sana Kwenye maisha yake binafsi hasa upande wa mapenzi kwani inasemekana Msanii huyo ana ametoswa na mpenzi

Maua ambaye alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mzungu fulani inadaiwa kuwa amejikuta katika kipindi kigumu baada ya kumwagwa.

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers Maua amekana tetesi hizo na kudai ni maneno ya watu kwani yeye hajaachwa na mtu yoyote:

Hakuna kitu kama hicho. Ujue Wabongo bwana wape picha tu ‘caption’ wataandika wenyewe! Yaani wamejaa kufuatilia mambo ya mtandao na kuyaamini. Kwa sasa nipo katika uhusiano na sipendi kuuweka hadharani“.

 

Solo Thang Akiri Kuzimika na Maua Sama

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva aliyetamba kwa miondoko yake ya kuchana miaka hiyo Msafiri Kondo maarufu kama Solo Thang amefunguka na kukiri kumkubali msanii mwenzake Maua Sama.

Solo Thang ambaye amekuwa kimya kwa miaka mingi baada ya kuhamia nchini Uongereza amekiri bado anafuatilia kwa ukaribu Bongo fleva na msanii wa kike anayemkuna ni Maua Sama.

Solo Thang

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Solo Thang amesema katika wasanii wa kike Maua ndio anajua muziki pia ni miongoni mwa wadada wa Bongo fleva wanaomkuna sana.

Kiukweli ninapenda anachokifanya Maua Sama, ni mwanamuziki mzuri, ingawa nipo nje namsikiliza sana na anasikilizwa sana pia, lakini mbali na yeye wanamuziki wengine kama Diamond, Ally Kiba, A.Y, Fid Q, kazi zao zinatufikia na tunapata nafasi ya kuzisikiliza“.

Maua Sama anafanya vizuri na wimbo wake unaoitwa Amen aliomshirikisha mkali wa RnB Ben Paul.

Maua Sama Atangaza Ndoa.

Huenda ikawa kweli mwanadada Maua Sama ameamua kufunga pingu za maisha na yule ampendae kutokana na caption zake nyingi katika ukurasa wake wa instagram akionyesha kuwa ana dalili za harusi hivi karibuni.

Lakini pia inawezekana ikawa ni kiki ya wimbo wake mpya kama wanavyojua kufanya wasanii wengi  pale wanapotaka kuachia ngoma mpya kwa kuamua kutengeneza attention kwa mashabiki wao ili ngoma iuze na waweze kufanya vizuri.

basi katika ukurasa wake wa instagram, maua ameweka zaidi ya mara mbili picha zeney caption ya kuashiria jambo fulani linakaribia.akiwa amevalia gauni ya harusi (shela) mau sama aliweka picha hiyo na kuandika “wahenga wanasema utamu wa ngoma ingia ndani mwenyewe ucheze,wacha na mimi nikachze yangu”

Na baada ya maneno hayo katika ukurasa wake wa instagram alianza kuweka picha zinazomuonyesha akiwa karibu na msani mwenie Ben pol na kuandika baadhi ya maneno yaliyoashiria ndoa.

 

Maua Sama Kufunga Ndoa Mwakani

Ndoa ni jambo la kheri sio kwa mwanamke tu, ila hata kwa wanaume, wasanii wengi wa Bongo wamekuwa hawadumu katika mahusiano na kuachana kila baada ya miezi michache,hii imefanya wasanii wengi washindwe kuingia katika ndoa , bado sababu haiko wazi lakini ni wasanii wachache wenye kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu  na kufikia hatua ya  kufunga ndoa.

Mwanadada mrembo kabisa katika tasnia ya  muziki wa Bongo fleva nchini, Maua Sama ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha” Katukatu’ amefunguka na kusema kuwa ndoa yake na mwanaume aliyemchumbia hivi karibuni inaweza kufanyika hapo mwakani lakini kwa sasa bado kidogo mipango  ya harusi haijafanyika.Msanii huyo ambae miezi kadhaa hivi iliyopita alichumbiwa na mchumba wake mwenye asili ya kizungu anasema kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwakani.

Maua Sama akiongea katika Over the Weekend ya gazeti la Ijumaa, alisema kuwa ana uhakika michongo yote ya harusi itaenda vizuri lakini kwa utaratibu wake na kazi zake kwa sasa  hana mpango wa kufunga ndoa  mwaka huu hadi mwakani.’Bado sana mipango ya ndoa kwa sasa mpaka mwakani.Sasa hivi ninaangalia zaidi muziki wangu,” aliongea Maua

Hata hivyo msanii Maua anasema kuwa anamshukuru sana Mungu maana ameweza kumsimamia na kuweka kukaa kwenye game muda mrefu huku nyimbo zake zikifanya vizuri ,lakini pia ameelezea sababu za msanii kukaa katika game la muziki  kwa muda mrefu ni vile ambavyo msanii anaamua kujiweka  “nashukuru nimeweza  kukaa kwa muda mrefu  bila kuchuja  na hii ni kutokana  na hii ni kutokana na msanii unavyojiweka” aliongezea Maua

Maua SaMa ambae pia ni zao zuri kutoka katika jumba la kulea wasanii wenye vipaji  nchini la THT , amekuwa mmoja wa wanadada wanaofanya vizuri kuanzia katika wimbo wake wa ‘Mahaba niue’ ambao ulikaa muda mrefu kwenye chati, lakini hata baada ya wimbo huo nyimbo zilizofuata ziliendela kufanya vizuri na kupokelewa vizuri na mashabiki wake, akiwa pia ni mmoja wa wasanii wanaozunguka mikoani katika tamsha la Fiesta , maua amekuwa akipokelewa vizuri katika jukwaa la Fiesta.

“Hamna bhana, mimi na Ema tunafanya tu kazi, mimi siko na Ema” Maua Sama

Kwa muda mrefu sasa, imekuwa inadaiwa Maua Sama amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na producer wake Ema the Boy.

Maua Sama alizungumzia jambo hili na Soudy Brown na kukana hili jambo. Alieleza uhusiano wao ulikuwa wa kazi tu na hamna jambo lingine kati yao.

”Hamna bhana, mimi na Ema tunafanya tu kazi, mimi siko na Ema na watu wanatangaza tu kwani mimi ni mtu wa kwanza kutangaziwa vitu vya namna hiyo..?” Alinena.

Ema pia alimuunga mkono na kusema hivi;

“Sijui chochote kuhusu hizo habari. Mara nyingi tunakuwa tunarecord hamna kitu cha zaidi ya hapo. Wewe unajua mambo ya muziki yanavyokuwa, muda mwingine mnaweza kutoka asubuhi ukamrudisha anapokaa au usiku mkaenda wote kutafuta chakula lakini hamna chochote ni muziki tu.”

Na ndio hiyo sasa.