Wadukuzi Wamliza Aika wa Navy Kenzo

Mwanadada kutoka katika kundi la Navy kenzo, Aikah amejikuta analizwa na wadukuzi wa mitandao baada ya akaunti yake ya instagram kuibiwa na wabbobezi wa mambo na kumfanya ashindwe kuwa na access na akaunti hiyo kwa zaidi ya masaa sasa.

Hata hivyo mwanadada huyo ameomba mashabiki zake kuwa na subira ili aweze kulishughulikia swala hilo huku akiwataka wasije kudanganywa na kujikuta wakitapeliwa kupitia jina  lake.

Swala la wasanii kuibiwa kaunti zao katika mtandao wa instagram imekuwa swala la kawaida huku ikishndikana kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwa sababu msanii na kosa baadhi ya mambo hasa anapokuwa anashindwa kuwa karibu na akaunti hiyo kwa muda

Navy Kenzo Waibuka Kidedea Katika Tuzo za Soundcity

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda  Kundi la Navy kenzo, Nahreel na Aikah Marealle wameonekana kidedea katika tuzo za Soundcity Awards za nchini Nigeria.

Navy kenzo walikuwa moja kati wasanii sita waliotajwa kutoka Tanzania na ndio waliofanikiwa kupata tuzo ambapo wameshinda kipengele cha Best Group or Duo.

https://www.instagram.com/p/BsSlddNASqp/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=kbwrq7qnvxfc

Wasanii wengine waliochaguliwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platnumz, Mbosso, Lava Lava na Harmonize kutoka WCB Lakini pia Maua Sama na Navy Kenzo.

Katika tuzo hizo Msanii Burna Boy ameshinda tuzo hizo kwenye vipengele vya Msanii Bora wa kiume Afrika, Wimbo bora wa mwaka (YE), Listeners Choice Awards na Best Male MVP.

Kwenye vipengele hivyo vyote alivyoshinda, alikuwa anapambana na wasanii wakubwa kama Diamond, Wizkid, Davido, AKA, Cassper Nyovest na wengineo.

Navy Kenzo Wagoma Kufanya Kazi na WCB

Wasanii wanaounda kundi la Navykenz wakiwa ni wapenzi wa muda mrefu Aika na Nahrelly wamekanusha taarifa za wao kujiunga na lebo ya Wasafi.

Wakiwa kwenye mahojiano walipoulizwa kuhusu tetesi zinazosambaa za wao kujiunga na lebo ya wasafi walijibu kuwa „hatujajiunga na lebo ya wasafi sisi tuko chini ya Manager Sallam SK ndie anasimamia kazi zetu hizo habari za mitandao sio za kweli”

Story za Navkenzo kujiunga Usafini zilienea baada ya kundi hilo kutoa ngoma iitwayo ‘katika’ ambayo wamemshirikisha Diamond Platnumz, ngoma ambayo kwa sasa imekuwa gumzo katika mitaa mbali mbali.

Navy Kenzo Wafungukia Tetesi Za Kijamii WCB

Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii  ambao ni Producer na msanii Nahreel na mpenzi wake Aikah limefungukia tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wamesiniwa na lebo ya WCB.

Navy Kenzo walitengeneza headlines wiki iliyopita baada ya kutotoa ngoma kali waliomshirikisha Diamond lakini baadae kuna tetesi zilisambaa kuwa kundi hilo linasiniwa na linakuwa chini ya WCB.

Tetesi hizo zilishika kasi mara baada ya Harmonize kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anawakaribisha kundi hilo katika Label ya WCB na Nahreel alionekana kukubaliana na Harmonize.

Lakini Navy Kenzo wamekanusha taarifa hizo na kuweka wazi kuwa wenyewe wako chini ya Meneja Salaam SK ambaye pia ni Meneja wa Diamond lakini sio chini ya WCB na kama siku wakijiunga WCB tamko litatoka rasmi kwao.

Navy Kenzo wanafanya vyema sana na wimbo wao mpya wa ‘Katika’ waliomshirikisha Diamond Platnumz ambao mpaka hivi sasa wanashikilia nafasi ya kwanza katika kutrend Kwenye Media mbali mbali.

 

Aikah Afungukia Miaka 10 Ya Mahusiano na Nahreel

Msanii kutoka kundi la Navy Kenzo, Aikah Mareale amefungukia na kuongelea Mahusiano Yake yaliyodumu kwa miaka 10 na mpenzi wake Msanii na mtayarishaji wa muziki Nahreel.

Wiki iliyopita Nahreel na Aikah walisheherekea miaka kumi ya kuwa pamoja tangu walipokutana kwa mara ya kwanza nchini India walipokuwa kimasomo.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika alifunguka kwamba ndani ya miaka hiyo waliyoishi pamoja kama marafiki wakubwa, wapenzi na watu wanaosi-kilizana, imeweza kuwafundisha vitu vingi kwa sababu wamepitia changamoto nyingi hadi kufika hapo.

Ulishawahi kukaa na mtu miaka 10, lakini unaona ni kama jana tu? Hii ni kutokana na jinsi mlivyoishi katika upendo na urafiki mkubwa, ndivyo tulivyo mimi na Nahreel na tunaunganishwa zaidi na mtoto wetu, Gold“.

Pamoja na kwamba Aikah na Nahreel wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Gold lakini wameweka wazi hawana papara ya kuoana kwa sasa endapo muda Ukiwa tayari watafunga ndoa.

Aikah na Nahreel Washeherekea Miaka Kumi Ya Mahusiano

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao wamehusika kutoa hit songs kama Game na Kamatia chini,Producer Nahreel na Aikah Mareale wanasheherekea miaka kumi ya Mahusiano.

Baada ya kuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka kumi Nahreel na Aikah  tayari wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume mapema mwaka huu anayeitwa Gold.

Wasanii hao walikutana miaka kumi iliyopita nchini India ambapo wote walikuwa wameenda kimasomo na kuanzisha Safari yao ya mapenzi pamoja na kufanya Muziki pamoja.

Pamoja na kuwa wote kwa miaka kumi sasa wasanii hao wameweka wazi kuwa hawana haraka ya kufunga ndoa kwa sababu tu maneno ya watu bali watafunga ndoa pale watakapokuwa tayari.

Wapendanao hao wameonekana wakila bata katika viwanja mbali mbali katika visiwa vya Zanzibar na hata kuandikiana posti za kimahaba Kwenye mitandao ya kijamii:

https://www.instagram.com/p/BnTQZxIARXF/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rwp3x59l4rn8

https://www.instagram.com/p/BnUCar7nctO/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=167fp4g7z53ei

Aikah Navykenzo Afungukia Ndoa na Nahreel

Mastaa wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika kundi la Navy kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wana mipango ya ndoa.

Wasanii hao ambao wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa zaidi ya miaka 10 walibahatika kupata mtoto wao wa kwanza mapema mwaka huu anayeitwa Gold Navykenzo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aikah amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kwamba wameshazaa nje ya ndoa lakini anaona ni jambo la kawaida na wana mipango ya ndoa.

Kwangu ninaona ni kawaida. Sisi siyo watu wa kwanza kupata nje ya ndoa mtoto, lakini mipango ya kufunga ndoa ipo na muda ukifika tutafunga ndoa.

Lakini pia Aikah ameanika changamoto wanazopitia katika kulea mtoto wao na kufanya muzikI katika wakati mmoja:

Kuna changamoto sana na si jambo rahisi hata kidogo kulea mtoto na kufanya muziki. Tangu tupate mtoto mambo mengi yamekwama kiasi kwamba kuna ‘interview’ nyingi tumezipiga chini ili tu kudili na mtoto. Unajua sisi ni wazazi wapya kwa hiyo mambo mengi tunajifunza“.

Jibu La Navy Kenzo Kuhusu Ndoa Yao

Wasanii wawili wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao ni Aikah na Nahreel ambao pia ni wapenzi wa muda mrefu wamefunguka kuhusu mipango yao ya kufunga ndoa.

Nahreel wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya kumi na wamejikuta kupata mtoto mmoja Mwanzoni mwa mwaka huu na sasa wanafunguka kuhusu mipango yao ya kufunga ndoa.

Kwenye mahojiano waliyofanya na Friday Night Live ya East Africa Tv, Nahreel ameweka wazi kuwa ndoa ipo lakini anaamini muunganiko wao kimapenzi ni muhimu zaidi na ukaribu wao:

Mimi na Aika nadhani the bond ni special, wedding ni important kufanyika katika maisha lakini Bond yangu na Aika is very special”.

Lakini pia na Aikah alimfunza mkono mpenzi wake na kuweka wazi umuhimu wa kutengeneza bond baina ya wapenzi kabla ya kufunga ndoa ili hata ndoa ikifungwa wanandoa wewe na ukaribu zaidi utakaowasaidia kudumu Kwenye ndoa:

Na tusiwafundishe watu wengine kuwa walazimishe kuingia kwenye ndoa kabla mtu hajawa tayari kuwa na ile bond, ni muhimu sana”.

 

Nahreel Afungukia Ishu Ya Rosa Ree Kuondoka The Industry

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo, Nahreel amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu msanii Rosa Ree kuondoka Kwenye label yake ya The Industry.

Msanii wa kike anayefanya vizuri kwa hivi sasa Rosa Ree alianza kujulikana baada ya kusainiwa chini ya label ya The Industry inayomilikiwa na Nahreel ambaye pia ni producer.

Rosa Ree alitangaza kuondoka kwenye label hiyo mapema mwaka jana baada ya kuwepo humo kwa muda mrefu huku akidai sababu pekee iliyomuondoa ni kuisha kwa mkataba wake na kusisitiza hana ubaya nao.

Lakini baadae Rosa Ree aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yalifanyika ndani ya label hiyo ambayo hayakumfurahisha ikiwemo kukataa kumpa akaunti yake ya Youtube hali iliyoashiria kulikuwa na kabifu fulani.

NAhreel anefunguka kwa mara ya kwanza na kumuongelea Rosa Ree tangu alipoondoka The Industry ambapo kwenye kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv ameweka wazi hakukuwa na bifu baina yao bali mwenyewe aliomba kuondoka.

Rosa Ree watu wamemjua Kupitia The Industry na kama alivyosema yeye time ilivyofika alitaka kuondoka na sisi tukamuacha aende but hatuna tatizo Rosa”.

 

Rosa Ree Awatolea Povu The Industry na Kusema Hawawezi Kumshusha

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap na hata kupewa jina the rap Godess Rose Kimario ‘Rosa Ree’ amewatolea povu zito wale wote wanaotaka kumshusha hawataweza kushusha kipaji chake kikubwa.

Rosa Ree alipata umaarufu kwa mara ya kwanza baada ya kuwa chini ya uongozi wa The Industry ambao uko chini wa Nahreel na Aikah Navykenzo.

Tangu alipoondoka kwenye label hiyo na kuanza kufanya muziki kama Solo artist Miezi michache iliyopita siku zote amekuwa akisisitiza kuwa hana bifu wala ubaya na Navykenzo.

Lakini siku chache ziliopita Rosa Ree aliibuka na kuongelea mchezo mchafu aliofanyiwa na Uongozi wake wa zamani ambapo amedai wamefuta baadhi ya video za nyimbo zake YouTube ambazo zilikuwa kwenye kurasa yao lakini pia amesema nyingine wamezishusha wameziweka private jambo ambalo amedai limemrudisha nyuma.

Rosa Ree amefanya Interview na Enews ya East Africa Tv amekiri pamoja na kwamba kitendo hiko kimemrudisha nyuma lakini hakijamkatisha tamaa na hakiwezi kushusha kipaji chake:

Kusema ukweli walivyoshusha video zangu kuna thamani ambayo imeshuka kidogo na ninajikongoja kuweza kupita ile sehemu ambayo ilikuwa zinaweza kunifikisha lakini siamini kama video zikishushwa kwenye YouTube na kipaji changu kimeshushwa kwaiyo nina iyo imani kwamba bado kipaji changu kipo na bado uwezo wangu upo na nitaendelea kufanya vyema”.

Pia Rosa Ree aliulizwa kuhusu uhusiano wake na Navy Kenzo kwa sasa endapo kuna bifu lolote ambalo linapelekea wao kumfanyia hivyo yeye na alisema:

Sina mawasiliano yoyote na Navykenzo kwa muda mrefu Lakini naamini ni kwa sababu ya majukumu mimi niko busy na muziki wangu hivyo sijaweza kuwasiliana nao lakini na wao wamepata mtoto ambalo ni jukumu kubwa naamini hivyo siwezi kujiuliza kwa nini hatuwasiliani”.