Nay Wa Mitego Akumbwa na Skendo Ya Kufilisiwa na Benki

Staa wa muziki wa Bongo fleva Emmanuel Elibariki. maarufu kama Nay wa Mitego amefungukia skendo ambayo imekuwa ikimuandama kuwa amefikisiwa na benki baada ya kukopa na kushindwa kulipa kwa wakati.

Nay ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo fleva ambaye amewahi kutajwa kuwa na mafanikio sana kwaiyo ilipotokea anaonekana anatembea kwa miguu na kupanda boda boda na bajaji ilisemekana mali zake zote zimefilisiwa na benki.

Kwenye mahojiano na gazeti la Ijumaa Wikienda Nay amefunguka kuwa,habari hizo  siyo za kweli kwani mali zake zote zipo na hajawahi kuwa na mkopo kwenye benki yoyote.

Ni stori tu ambazo watu wameamua kuzungumza na watu kuzungumza siyo dhambi kwa sababu mimi ni staa, kwa hiyo watu wakiwa wanaongea vitu kama hivyo huwa sishtuki, nawaa-ngalia tu”.

Ishu ya Nay kufilisiwa ilianza kusambaa mitandaoni baada ya mashabiki kudai msanii huyo kwa sasa hana jipya kwani benki hiyo walikwenda nyumbani kwake na kutaifisha mali zake zote zikiwemo nyumba na magari anayomiliki baada yakushindwa kulipa deni.

Nay alisema hakuna ishu kama hiyo na hakuna mali yake yoyote iliyopigwa mnada kwa sababu mali zake zote zipo na hafikirii kwenda

“Bado Nampenda Nini, Akitaka Kurudi Niko Tayari”- Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa bado anampenda sana aliyekuwa mpenzi wake na msanii mwenzake Nini.

Wiki chache zilizopita Nini aliweka wazi kuwa Mahusiano Yake na Nay wa Mitego yamefika mwisho na alidai ameamua kumuacha rapa huyo kwa madai amekuwa na michepuko mingi.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Nay amefunguka na kudai bado anampenda sana Nini na kama atakuwa tayari kuwa naye Tena basi yeye Yupo Tayari.

Nay wa Mitego amekiri kuwa ni kweli alifanya makosa ambapo alikuwa ana michepuko kadhaa na Nini alipogundua alimpiga kibuti na hata alipomuomba msamaha hakutaka kumsamehe.

Nay amesisitiza kuwa bado anampenda sana Nini na kama atakuwa tayari kumsamehe hata leo hii basi Yupo Tayari kuwa naye Tena.

Nay amekiri kuwa ingawa yeye na Nini walikataa kuwa hawakuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini walikuwa pamoja kwa miaka zaidi ya miwili na hata kudai walianza Mahusiano kabla hata hajajua kuwa Nini anaimba.

“Shilole Angetaka Kiki Angeenda Beach na Uchebe Wake na Kuvua Nguo Zote”-Nay Wa Mitego

Msanii wa MuzikiSana wa Bongo fleva Nay wa Mitego amemjia juu Msanii mwenzake Shilole baada ya kuingilia kati sakata la Muna na kumrushia maneno katika Interview mbali mbali.

Nay ameibuka na kumkingia kifua Muna na kumtolea povu Shilole na kudai anatafuta kiki Kupitia ishu ya Muna na hana lolote kingine linalomsumbua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nay wa Mitego alimuandikia ujumbe huu Shilole:

Shiloleeee Zainabuuu nadhani ulimiss tu Media dada yangu nadhani umefanikiwa kwa kiasi chake. Ulichokosea ni ishu uliyoingilia yaani gear  yako. Sioni alichokosea huyo unayemuita mdogo wako Muna ameongea mengi ambayo watu walitaka kujua nini kilichokuwa kinamsumbua Patrick.

Sasa ungetaka kiki mngeenda Beach na Uchebe wako mnavuana nguo zote alafu mbapiga picha halafu mnaposti bila hata caption halafu mtaona kiki yake ingekuwa noma.Lakini hili la Muna umejichoresha tu umeonekana ulikuwa unatafuta…..Mtazamo wangu tu”.

Sakata kati ya Muna na Shilole lilianza baada ya Muna kufanya Interview na kuweka wazi kuwa Casto ndiye Baba halali wa marehemu mtoto wake Patrick na mambo mengine ambayo yalionekana kutompendeza Shilole.

Nini Akiri Kuvunjika Kwa Penzi Lake na Nay Wa Mitego Kisa Michepuko

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nini amefunguka na kuweka wazi kuwa penzi lake na msanii mwenzake Nay wa Mitego limefikia ukingoni hivi karibu.

Nay wa Mitego na Nini walidaiwa kuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini walikuwa wanakataa kila wakiukizwa walidai kuwa ni marafiki tu lakini wamethibitisha walikuwa wapenzi baada ya kuachana.

Nini ameibuka na kukataa tetesi zinazoendelea kusambaa kuwa kisa chao wao kuachana ni baada ya familia yake kumlazimisha Nay amuoe baada ya kumchukua mtoto wao na kuishi naye bila kujitambulisha wala kumuoa.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv,Nini amesema ameamua kuachana na Nay wa Mitego kutokana na kumchukulia poa na kuwa na mahusiano na wanawake wengine.

Ni kweli nimeachana na Nay na niweke hili sawa sijawahi kuishi nyumba moja na Nay na hata hiyo ishu ya wazazi wangu kwenda kwa Nay sio kweli.

Unajua kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana na mtu kama mwanaume unaweza ukampenda, ukamuheshimu akawa anakuchukulia poa, anakufanyia drama anakuletea wanawake“.

 

Nay Wa Mitego Adaiwa Kuvunja Mahusiano na Nini Baada Ya Familia Yake Kutaka Ndoa

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amedaiwa kuvunja Mahusiano na mpenzi wake Nini baada ya familia ya Nini kutaka afunge ndoa na binti yao.

Shilawadu wanaripoti kuwa Nay wa Mitego na mpenzi wake Nini wamejikuta katika wakati mgumu baada ya familia ya Nini kumkalia kooni Nay na kumtaka amuoe Nini.

Nay na Nini wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa muda kidogo Lakini sasa inadaiwa Familia ya Nini imekuja juu na kumtaka Nay amuoe binti yao baada ya kukaa naye nyumbani kwake.

Inadaiwa Nini alihamisha makazi yake nyumbani kwa Nay na kila Familia yake ilikuwa ikimtafuta arudi nyumbani alikuwa anagoma ndipo walipoamua kumsaka na kumtaka afunge ndoa.

Lakini inasemekana kuwa Nay alikuwa anawapiga chenga kila wakimtafuta anajificha hataki kabisa kuonana na Familia ya Nini.

Siku ya leo Nay wa Mitego Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kumtosa Nini na kudai yupo single ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema “It’s Official I am Single”.

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Nay wa Mitego Amshauri Diamond Amuoe Zari Aachane na Hamisa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amemtaka Msanii mwenzake Diamond Platnumz amtupie kule mpenzi wake wa sasa na arudishe majeshi kwa Mama watoto wake Zari.

Suala hili lilikuja siku chache zilizopita baada ya Diamond kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Iyena ambao ndani yake video queen ni Ex wake Zari.

Nay wa Mitego ambaye alishawahi kuweka wazi tangu Diamond alipoachana na Zari kuwa yeye anampenda Zari awe na Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego aliandika ujumbe huu kuhusu wimbo huo na ZAri:

Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.(Yamoyoni) Haya Fanya Muende YouTube”.

Nay wa Mitego na Diamond walitoa hit iliyokwenda jina la Muziki gani, hata hivyo hawakuishia hapo baadaye walitoa ngoma nyingine inaitwa ‘Mapenzi Pesa’.

Sina Mpango wa Kuoa Mimi:-Nay wa Mitego

kumekuwa na tetesi zinasambaa katika mitandao kwamba msanii nay wa mitego kwa sasa ana mpenzi mpya ambae ni mzuri na mkali zaidi ya yule mama wa watoto wake aliyewahi kuwa nae mara ya kwanza aliyejulikana kama siwema.

akiongea huku akikataa jina lake kuwekwa wazi, moja ya mapaparazi alisema kuwa kwa sasa nay ana chombo kipya kizuri kuliko hata siwema aliyekuwa nae mwanzo,’hivi mna habari kuwa nay saa hivi ana chombo kpya kisu kuliko siwema,ni mjasiriamali na ana karibia kumuoa na mara nyingi anakuwa nae pale kimara nyumbani kwake.’

mimi nakuibia siri ya familia kwa sababu huyo dada amechukua sehemu kubwa ya siwema kwaio wamemwambia kuwa lazima amuoe huyo dada.

Baada ya hapo Ney alitafutwa ili kuweka ukweli juu ya jambo hilona kutuweka wazi kuhusu kila kitu kuhusu mahusiano yake, ndipo nay alipojibu kuwa kwa sasa hana mpango wakuoa.

Sina mpango wa kuoa mimi, na  mmepata wapi picha,sema kwanza picha umezitoa wapi na nani kakutumia ndipo nitakujibu kama ni mpenzi , mchumba au vipi.

mimi huyu sio mwanamke wangu aisee, mimi nina mahusiano yangu mengine kabisa.

Hata baada ya kuulizwa hivyo Ney wa Mitego hakutaka kujibu tena swali lngine lolote zaidi ya hilo.

B Gway Adai Nay wa Mitego ni Mchawi

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva B Gway alijipatia umaarufu baada ya kutoa wimbo wake unaoitwa unajichukia aliomshirikisha Nay wa Mitego amemgeuka Msanii huyo na kudai ni mchawi.

B Gway alikuwa msanii chini ya label ya Nay Free Nation lakini baada ya kuzinguana na kuondoka Kwenye label hiyo B Gway amedai hivi sasa Msanii huyo ameanza harakati za kumpoteza Kwenye gemu.

Kama utakumbuka siku za nyuma NAy alifanya shoo iliyotwa Nguvu ya kitaa maalumu kabisa kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Dar lakini unaambiwa siku ya shoo mvua kubwa ilimyesha na B Gway anadai Nay alitumia nguvu za Giza kufukuza

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, B Gway alifunguka haya:

Ile Nguvu ya kitaa tu vitu vingi viliendelea maana kulikuwa kuna bonge la mvua lakini pale TAnganyika Packers kulikuwa kukavuu.

Unajua mimi naamini sana katika uwezo wa Mwenyezi Mungu yaani naamini sana kwamba nitafika kwa iyo kama yeye ana Imani atatia ubani mambo yangu yaharibike basi amekosea sana”.

 

Nay Wa Mitego- Nagombea Uraisi Mwaka 2020

Mwanamuziki wa Bongo fleva amefunguka na kusema sababu pekee inayomfanya awe kimya kwa hivi sasa ni mipango yake ya kugombea uraisi mwaka 2020.

Nay wa Mitego ni msanii ambaye anajulikana kwa vituko Chake ikiwemo Uwezo wake wa kuwachana watu kwenye jamiii hasa wasanii wenzake kuhusu mambo mbali mbali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes, Nay alisema kwa sasa ameamua kujitenga na skendo kwani anajiandaa kugombea urais mwaka 2020 japokuwa hawezi kuweka wazi atagombea kwa chama gani hivyo akaona ni vema aachane na skendo zisizokuwa na maana.

Nimeamua kutulia na kuachana na skendo zisizokuwa na maana kwa sababu nina mpango wa kugombea urais mwaka 2020 sasa nikiwa na skendo chafu zitaniharibia“.

Hivi sasa kumekuwa na trend kubwa ya wasanii mbali mbali kujiingiza Kwenye mambo ya siasa na kugombea nafasi mbali mbali kama vile Wasanii wakongwe wa Bongo fleva Profesa Jay na Sugu ambao wote ni wabunge.

Nay wa Mitego Atupa Dongo Gizani Kwa Wasanii Wanaopenda Kiki

Mwanamuziki Ney wa Mitego ametupia gongo gizani bila kutaja ni nani amemlenga katika maneno yake yaliyokuwa yakimaanisha kuwakaribisha mashabiki zake katika kuungalia na kuusapot wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la amsha popo.

Ney wa mitego ambaye aliandika katika ukurasa wake wa instagram ameno yaliyoanshiria kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa hawaachi ngoma mpaka wapate kiki kwanza anasema kuwa kwa uapnde wake huwa hasubiri kiki ia  nyimbo yenyewe ndio italeta kiki.

no hatuogopagi kiki hata siku 1,ukijua unachokifanya  raha sana.nikiamua kudondosha chuma mi nadondosha tu, wao ndio wanaogopa kiki…huku kwetu sisi hatupeleki siku mbele.’–Aliandika Nay katika ukurasa wake wa instagram.

Ukifuatilia kama wiki moja nyumba kuna wimbo wa diamond na harmonize ulitakiwa kutoka lakini wimbo huo ulishindwa kutoka huku kukiwa hakujatajwa sababu  husika lakini wimbo huo ulitoka hivi karibuni.

Kwa inavyoonekana ni kama Ney wa Mitego amekuwa akiwaponda na kuwasema watu ambao wamekuwa na tabia ya kutangaza kutoka kwa nyimbo kisha nyimbo hizo kushindwa kutokwa kwa kuogopa kutofanya vizuri kutokana na kwamba wanakuwa hawajaitengenezea skendo ya kuifanya kusamba kwa haraka.

Hata hivyo kiki imekuwa ni kama mazoea kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakifanya jambo kubwa la ajabu ili kuongelewa katika mtandao ili wanapotoa nyimbo iweze kusikilizwa sana.

Nay wa Mitego Awasilisha Kazi Yake BASATA

Msanii anejulikana kwa shida ya kuwa mbishi na mkorofi inapofikia kwenye swala la kazi zake,nay wa mitego amesalimu mari baada ya kuamua kupeleka kazi yake ya muziki BASATA kukaguliwa kabla ya kutolewa katika vyombo vya habari.Ney ambae pamoja na kwamba amepelaka nyimbo hiyo kwenda kukaguliwa lakini anasema kuwa hiyo haimzui yeye kufanya lolote atakalo katika muziki wake.

Nay wa mitego amesema kuwa kilichomsukuma kupeleka nyimbo yak BASATA ni kukwepa lawama za serikali lakini haimapngii au kubadilisha kile anachokiimba kwa sababu hicho ndicho kinachomwingizia ela na kinampa mashabiki.

Najaribu kufuata utaratibu na nadhani hii ndio ngoma yangu ya kwanza kabisa kuwatumia BASATA , nafanya muziki wangu kama vile nilivyokuwa nafanya , nimepunguza vitu kidogo tu , siwezi kuhama kwenye muziki wangu , yaani nitaendelea kufanya muziki wangu ule ule.Nimewafikishia wimbo wangu sio kwa sababu nataka wanipangie mashairi ya kuimba  ila tu sitaki kuanza kuzuiliwa nyimbo zangu.

Maamuzi ya Nay yanakuja baada ya kuwa na wimbo kubwa la wasanii wanofungiwa nyimbo zao kwa sababu ya nyimbozao kukosa maadili katika jamii.

Nay wa Mitego: Naendelea na Mziki Wangu Ule Ule Sina Mpango Wa Kubadilika

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kubadilisha aina ya muziki anaofanya kwani ndio mziki unaopendwa na mashabiki zake.

Wiki chache zilizopita Nay wa Mitego alikuwa mmoja kati ya wasanii waliofungiwa nyimbo kumi na tano na BASATA kwa ukosefu wa maadili ya Kitanzania kwenye nyimbo hizo.

Nay wa Mitego alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao waliofungiwa nyimbo mbili na BASATA hivyo utategemea kutokana na hilo basi atakuja kuchukua kila jitihada ya kufanya nyimbo sahihi ili zisifungiwe Tena lakini sivyo hivyo.

Nay wa Mitego ameweka wazi kuwa hana hata mpango wa kubadilisha mziki wake anaoufanya ili kuwa ridhisha BASATA kwani huo ndio mziki unaopendwa na mashabiki zake na kukubali kila hivyo nyimbo yake mpya anayotoa itakuwa hivyo hivyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego aliandika maneno haya kuhusiana na wimbo wake mpya unaoitwa ‘Amsha Popo’:

Mwandishi: Kesho unaachia wimbo mpya kuna mabadiliko gani katika wimbo huo mpya kuepuka kufungiwa tena?

Baba Yaga: Hakuna mabadiliko yoyote naendelea na mziki wangu ule ule Cox mashabiki zangu ndio wanaishi upenda na ndio walionipokea nao #Amshapoo”.

 

Edu Boy Akiri kumpora Nini Kwa Nay Wa Mitego.

Msanii wa hip-hop nchi edu boy ambae siku za hivi karibuni amekuwa ni moja ya wasanii wasiogopa kutoa makavu live kwa wasanii wenzake amefunguka na kumpondea msanii mwenzake Ney wa Mitego kwa madai kuwa  amempokonya aliyekuwa mpenzi wake Nini.

Nini na Ney wa Mitego walisemekana kuwa katika mapenzi kwa muda mrefu na hivi karibuni waliamua kutoa wimbo lakini kama kawaida ya wasanii walikuwa wakikana kabisa kuwa hawapo katika mapenzi.

Edu Boy amesema kuwa Ney hawezi kujilinanisha nae kwa sababu yeye ni mtoto  wa kisukuma na anakula vizuri hivyo kumpokonya mtu mwanamke kwake ni swala la kawaida kama mwanaume aliyenae hamridhirishi.

Unajua kuwa mimi ni mtoto wa kisukuma kwaio nakula vizuri sana,kwaio najua namna ya kumridhirisha mwanamke  katika tendo kwa sababu tuna nguvu za kutosha.kumpora mtu mpenzi ni jambo la kawaida.

Kwa Roma Naomba Wamfikirie Mara Mbili: Nay wa Mitego.

Msanii Ney wa  Mitego amefunguka kuhusu kupewa onyo baada ya nyimbo zake kufungiwa katika vyombo vya habari.Ney wa Mitego ni msanii anaeongoza kuwa na nyimbo nyingi  katika orodha ya nyimbo zilizotolewa na Baraza la Sanaa.

Akizungumza na Cloud e, Ney wa Mitego anasema kuwa kwa upande wake anaona kabisa kuwa nyimbo yake mpya ya mikono juu haikustahili kuwepo katika orodha hiyo kwa sababu ukisikiliza ngoma hiyo iko tofauti na nyimbo zake za nyuma ambazo amekuwa akiimba.

wimbo wangu mmoja upo pale kimakosa, haukutakiwa kufungiwa kabisa ukimsikiliza ney huyu wa mikono juu sio yule wa zamani, audio ya makuzi tulishairekebisha , nilikaa na baraza na tukaongeana na  tulishamaliza.

Nay wa mitegoanasema kuwa amekuwa akitumia tasfida katika muziki wake kila mara lakini kitu kinachomkosesha amani ni kwamba watu wanafumbua tasfida na yanakuwa maneno ya kawaida.

natumia tasfida sana,kama unafumbua tasfida hilo ni tatizo lako na kama nispotumia tasfida nitatumia nini sasa.

Hata hivyo Nay wa Mitego anasem akuwa wimbo wa mikono juu ni wimbo mpya ambao ndo kwanza unaanza kupokelewa,baraza limeshindwa kutambua na kuniambia tatizo la wimbo wangu labda tukikutana tena wiki ijayo.

Tumezungumza kuhusu mabadiliko na mpaka nimetaka kujua tatizo la mikono juu na tumekubaliana nibadilishe.nina imani hauna tatizo na wao hawajasema  tatioz liko wapi ila kila list imeshazoeleka kwa ni lazima ney wa mitego atakuwepo.tumeyamaliza na tumekubaliana kufanya muziki mzuri na kufanya mabadiliko katika muziki.

Nay wa Mitego pia alipata nafasi ya kuzungumzia swala la Roma ambae yeye pia amefungiwa muziki wake na pia hapaswi kufanya kazi kwa muda wa miezi sita.

tunaishi kupitia muziki, pengine labda tungekuwa vibaka, wezi, au jela au hata tushakufa.mtu anakosea lakini kwa sababu tuna wazazi inabidi wawepo kuturekebisha lakini kwa kutuambia pale tunapokosea na mtu ajiridhishe na kosa lenyewe kwanza.Nimewahi kufungiwa najua maumivu yake, sitaki kuliongelea sana hili lakini kwa Roma naomba wamfikirie mara mbili.