Nikki wa Pili Awatolea Uvivu BASATA.

Ikiwa bado sakata la kufungiwa kwa wasanii likiwa bado linashika kasi katika mitandao ya kijamii huku wengi wao wakingngunika kwa jinsi msanii wa bongo hip -hop ,Roma Katoliki alivyopewa adhabu kubwa ilhali muda wake wa kufanya marekebisho ya nyimbo hiyo yakiwa bado haujaisha msanii ,mwenzake Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi ameilalamikia BASATA kuhusu hatua kali wanazochukua wa wasanii huku akiwakumbusha mambo ya nyuma yaliyopita hasa kipindi cha siasa jinsi kulivyokuwa kumetapakaa kwa nyimbo za matusi lakini zilikuwa hazifanywi kitu chochote..

Niki wa Pili ambae amekuwa msemaji mzuri katika kitandao ya kijamii kuhusu maswala mbalimbali yanayotokea katika jamii anasema kuwa imekuwa  basata wamekuwa wakifumbia macho baadhi ya vitu na kuibuka na baadhi ya vitu kitu kinachowafanya watu waone kama vile hawatendi haki.

Akihoji kuhusu maamuzi ya BASATA , Niki  wa Pili amehoji kwanini kipindi cha kampeni kulikuwa na nyimbo nyingi za siasa zilizokuwa na matusi mengi lakini hazikuwa zikifungiwa lakini wameanza kuwakamta wasanii wenzao.

tukizungumzia nyimbo za matusi bwana zilizotoka wakati wa kampeni , bwana we matuzi ya nguoni,tena takitukana watu wazima  na heshima zao,hapa walezi wetu wakikaa kimya bBASATA kama walezi  wetu msisahau kuwa kuyalinda maadili yetu kiuchumi , kama mlezi  halafu watoto wako wanakuwa wanaishia kufa , inamaanisha hawakulelewa vizuri kiuchumi pia-Aliandika Niki wa  Pili akitaka BASATA kwaangalia pia wasani wake katika swala la kiuchumi.

Maneno ya Nikki wa Pili Kuhusu Upendo na Mahusiano.

Msanii wa bongo fleva kutoka kundi la Weusi nchini , Nikki wa Pili ambae amekuwa ni moja ya wasemaji wazuri sana hata kuwasemea vijana kuhusu maisha wanayoishi na kutoa manen mengi ya hamasa na kujenga kwa vijana , siasa na hata katika maswala ya uchumi amefunguka na kuweka wazi kuhusu kile anachokifikiria kuhusu upendo na mahusiano.

Nikki ambae mara yingi katika nyimbo zake amekuwa akitoa maneno yanayoumiza moyo hasa kwa vijana kama unaishi yale maisha aliyoimba katika nyimbo zake , amekuwa ni moja ya wasanii aanependa kutoa ukweli kuhusu wasichanaau vijana wanaojiingiza katika mahusiano bila kujua dhumuni la mahusiano hayo au ambao wapo kimaslahi zaidi.

upendo ni msaada , kusaidiana katika uchokoraa wenu na tabia zenu, ulemavu wa matendo yenu  na uyatima wa mioyo yenu.

upendo ni uvumilivu kupeana muda wa kutambuana na kurekebisha makosa,muda wa kukua na muda wa kujifunza.

upendo ni msamaha, kujisamehe mwenyewe kwanza ili usiwe na sumu ndani yako na kumrekebisha mwenzako.

upendo ni ndoto na maono.kuota maisha ya mwenzakoalivyozaliwa,kukua na kujua kwanini yuko vile alivyo.upendo sio kumpenda kama unavyojipenda kwa sababu hata wewe uanamambo yako mengi usiyo yapenda, so ukimpenda kama unavyjipenda yale usiyoyapenda kwako pia hutayaenda kwake…upendo ni ahadi ya kuendelea kuwa mkarimu hata kwa mambo yanayokuwa ndimu.

Nikki wa Pili yuko katika mahusino ya kimapenz na mwanadada mmoja ambae amekuwa akiweka picha zake katika ukurasa wake wa instagram kwa muda mrefu.

Nikki Wa Pili Amewatolea Uvivu Watu Wanaotoa Msaada na Kamera Nyuma

Mwanamuziki wa hip hop ya Bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa pili amewatolea povu kali watu wanaodai ni wasamaria wema ambao wanaenda kutoa misaada lakini wanabebea makamera ya kuwarekodi.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kwenda kwenye maeneo mbali mbali ambamo inajulikana wanaishi watu fulani wenye maisha magumu inaweza ikawa kituo cha watoto yatima ama hata vituo vya kuishi wazee na kutoa chochote alicho nacho lakini pia ni desturi kwa watu wengi kuita waandishi wa habari.

Wasanii wengi kwenye jamii yetu hawaoni shida kuanika mambo mema waliyofanya katika jamii ni jambo zuri ndiyo lakini sio lazima ujionyeshee kweli umetoa kama kweli ulitoa kwa moyo mmoja hutahitaji kila mtu ajue ingawa huo ni mtazamo wangu tu binafsi.

Lakini inaelekea Nikki wa pili ana mtazamo kama wangu ambapo amewapa makavu watu wote ambao hawaridhiki na kutoa msaada tu lakini watataka waanike kila kona ili waonekane na kila mtu kwaiyo inakuwa ngumu kumtambua yupi ana nia gani ya kweli au yupi ana nia ya uongo:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo:

Ukitoka na marafiki au familia au wafanyakazi wenzako mkaenda kutoa msaada kwa wenye uhitaji mkifanya nyie na wao mnakuwa mmefanya kazi ya Mungu , maana alisema ukitoa sadaka na mkono wa kushoto mkono wa kulia usijue, lakini ukienda kutoa msaada umembatana na makamera kuandaa mapicha na mavideo kusambaza mtandaoni na kwingineko utakuwa umeenda kufanya kazi ya shetani…..kuwatumia watu wenye shida kujenga jina au brand au kutafuta ushawishi au kifaa cha kufanyia propaganda…saidia kama habari zitasambaa acha zisambae zenyewe ni maoni yangu lakini naweza nisiwe sawa pia”.

 

Nikki wa Pili Amjibu Mh.Nasarri Kuhusu Mh. Sugu

Msanii wa muziki nchini Nikki wa Pili amemjibu Mh Joshua Nassari baada ya kuwatuhumu wasanii kwa kukaa kwao kimya baada ya Mh.Sugu kukamatwa na kuweka polisi kwa zaidi ya siku kumi sasa wao wakiwa wamekaa kimya ilhali mbunge huyo alikuwa mstari wa mbele kuwatetea wasanii katika kupata maslahi yao.

Mh. Nasari anawataka wasanii wakumbuke kuwa Sugu ndie msanii wa kwanza kupigania haki zao kwa uda mrefu na kukataa kufanya kazi za muziki  bila kulipwa na haki hiyo.

wasanii wa bongo fleva mmesahau kabisa harakati za sugu kupigania muziki wenu kusimama.sugu yupo selo siku ya kumi sasa wasanii mmepiha kimya,courtin hamtokei,jela hamji kumuona , mmeamua kumtumikia kafiri.mmesahau kuwa alianzisha harakati za kugoma kuimba bure.

Katika kumjib Mh. Nassari nikki wa pili amemwambia kuwa wasanii wanaogopa kupaza sauti ya kutetea jambo kwa sababu hakuna umoja kati yao na hata wanapotaka kusimama kutetea jambo fulani mtu anaweza kujikuta peke yake.

Wasanii hawna umoja na chama chao hakina nguvu kwaio hata kinapotokea kitu  wasanii wakatakiwa kulitolea sauti hakuna platform   ya kulishikilia jambo hilo  na kujikuta kila msanii huyo yuko peke yake  na kupaza sauti peke yae wasanii wengi wanaogopa hilo.-Aliandika Nikkki wa Pili.

Mheshimiwa joseph mbilinyi jina la usanii sugu aliwekwa jela siku kama 10 zilizopita kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi kwa wananchi juu ya serikali iliyopo madarakani.

 

Nikki wa Pili Azungumza na Baraza la Sanaa.

Msanii wa muziki Tanzania Nikki wa Pili amefunguka na kuhoji juu ya vitendo wanavyovifanya baraza la sanaa vya kuwafungua wasanii kama ni vya halali bila kuzingatia mambo mengi na kujikuta wakijikita katika mavazi tu ilhali swala la maadili linakuwa linapande nyingi na sio swala la mavazi tu.

Nikki wa Pili alizungumza hayo alipokuwa naongea na mtangazaji wa EATV na kusema kuwa baraza linatakiwa kuangalia swala la maadili kwa upana sana na sio katika mavazi tu kwa sababu hata kwa upande mwingine ukiangalia utakuta kuwa hata wao kama baraza wanakuwa hawatimizi majukumu yao wa wasanii.

Nikki amesema kuwa Baraza wanakosea wanapokuwa wanawafungia wasanii tena hasa wa kike kwa sabau ya maadili ili hali wanapaswa kuangalia vitu vini kabla ya kutoa uamuzi huo,lakini pia yapo mambo mengi baraza wanatakiwa kuyanyoosha na kuyyaweka katika mstari kabla hawajaanza ku-judge kuhusu mavazi na maadili yao.

Maneno ya nikki yanakuja baada ya Baraza la Sanaa kuwafungia baadhi ya wasanii wa kike kwa madai kuwa wasanii hao wamekuwa wakitoa video na kuchapisha picha za uchi katika mitandao na kutoa ahadi kuwa yeyeto atakae toa wimbo usiokuwa na maadili ya kitanzania basi wimbo huo na kazi zake zitafungiwa.

Wasanii waliofungiwa hivi karibuni kutokana na utovu wa nidhamu katika kazi za muziki ni pamoja na Gigy money na Pretty kindy huku wengine wakiambiwa kuripoti katika ofisi za baraza lakini pia wimbo wa Rostam wa Kibaa100 pia umfungiwa mpaka utakapofanyiwa marekebisho katika baadhi ya vipengele.

Hivi Ndivyo Zitto Kabwe Alivyomkaribisha Nikki Wa Pili Kujiunga na ACT Wazalendo

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe hajaona hiyana kumkaribisha Mwanamuziki wa Bongo fleva Nikki Wa Pili kujiunga na chama hicho.

Nikki Wa Pili ni mmoja kati ya wasanii wasomi nchini anayemiliki degree kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, tofauti na wasanii wengine wengi Nikki Wa Pili ni msanii anayependa kutoa maneno ya kizalendo ambayo yanalenga kujenga nchi yetu.

Zitto Kabwe baada ya kuvutiwa na upeo mkubwa wa Nikki Wa Pili alimuandikia ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter huku akimsihi kujiunga na ACT Wazalendo.

Njoo ACT Wazalendo ujenge chama cha kijamaa acha mambo yako”.

Baada ya Tweet hiyo ya Zitto Kabwe kumuomba Nikki Wa Pili ajiunge na chama chake ili akajenge ujamaa, Nikki alimjibu kuwa chama cha kijamaa kinajengwa na watu wanyonge bali yeye kama mtu Vyombo vya habari sio wa kuaminika kwani hachelewi kuwauza.

Chama cha Kijamaa hujengwa na Vugu vugu la wanyonge wenyewe, ni muwe tu na mkakati wa kuwaunganisha ki-ideoligia umoja zao hizo za boda boda, machinga, wakulima, sisi watu wa media hatukawii kuwauza sokoni kama nyanya”.

Wasanii wengi wa Bongo movie na hata Bongo fleva wamekuwa wakijiingiza katika vyama mbali mbali vya siasa lakini mpaka sasa Nikki Wa pili hajaweka wazi kuwa yeye ni mfuasi wa chama gani.

 

Mambo Atayoyafanya Nikki Wa Pili Akiwa Raisi

Mwanamuziki  Nikki wa pili kutoka katika  kundi la Weusi, ambalo linaundwa na wasanii watatu Joh Makini, G-Nako na Nikki wa Pili ,amefunguka na kuendelea kuonyesha nia yake ya kutaka kuingia kwenye siasa kwa spidi ya ajabu,Nikki wa Pili ambae anafanya vizuri wa kibao chake cha kihasara na quality time ambazo zinafanya vizuri zaidi katika vituo mbalimbali vya habari.

Nikki wa pili ametaja baadhi ya mambo muhimu atakayoyafanya endapo atakuwa raisi.Mwanamuziki huyo ambae alishawahi kusema kuwa anampango wa kuingia kwenye siasa anaendelea kuthibtisha nia yake hiyo kupitia maneno yake.Katika vitu alivyoviorodhesha ni pamoja na :

1.Kikao kikubwa cha serikali yangu itakuwa sio baraza la mawaziri bali  mkutano mkuu wa kijiji au mtaa(kitaa kitaongea)

2.Kipimo kikubwa cha maendeleo itakuwa ni kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi au makusanyo ya fedha.

3.Mfumo wa elimu utajikita katika kupima learning na sio ufeli au kufaulu

4.Vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa vikifanya mikutano na kuhoji serikali sio vyama vya siasa  bali vyama vya wakulima, wafanyakazi ,walimu, machinga , bodaboda madaktari na kadhalika.

5.Serikali itakuwa mdau mkubwa  uchumi na mukewezaji  atakuwa ni mkulima,mfugaji, mchimbaji mdogo,wavuvi wadogo na wafanyabiashara wadogo.

6,Ardhi, maji ,elimu ,afya, havitakuwa bidhaa bali hifadhi za jamii

7.Maisha bila maadili hayana maana , kila mtoto ni lazima afundishwe kuwa na  maadili , uaminifu,heshima,ujamii,upendo, bidii, na kujiamini.

8,Mahusiano na mataifa ya afrika  hayatakuwa na neno wahamiaji haramu , mwafrika hawezi kuwa haramu maana Afrika ni nyumbani kwake.

Nikki anasema kuwa maswali ataulizwa kipindi cha kampeni kikifika lakini anampango wa kuwa mgombea binafsi.

Nikki akiwa kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa na impact kubwa kwa jamii, atakapojiingiza katika siasa atakuwa amevumbua na kusaidia vijana wengine wengi wanaompenda na kumuamini pia.

Ukiachana na kazi za muziki anazofanya Nikki na wenzake lakini pia msanii huyu amekuwa akitumiwa na mashirika katika mikutano mbalimbali ya uhamasishaji wa vijana katika jamii.

 

Nikki Wa Pili Azungumzia Bifu La Dogo Janja Na Young Dee

Wakiwa bado wanavuma sana katika vichwa vya habari sehemu mbalimbali wasanii  wawili wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) msanii Dogo Janja kutoka Arusha na Young Dee kutoka wa Dar Es Salaam kutokana na bifu linaloendelea kati yao katika mitandao na vyombo vya habari , msanii mkongwe na mwenye mafanikio  kutoka kundi la Weusi ameamua kulizungumzia  bifu ilo ambalo linaonekana ni tatizo .

Nikki amekuwa ni mmoja wa wasanii ambao amekuwa akishauri na kusaidia watu wengi katika tasnia ya muziki na nje ya muziki pia, ukiachana na kipaji cha muziki alichonacho Nikki  akiaminika sana katika jamii kutokana na ushawishii wake mkubwa kwa vijana wenzake katika swala zima la maendeleo

Akiongean na  eNews ya EATV, Nikki wa Pili anaona kuwa bifu ilo linaendelea na linaweza kufika pabaya ilhali wasanii hao wameanza kuingia katika  maisha yao binafsi badala ya kuwa na ushindani wa kikazi “mimi naona kama kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi,kwaiyo ningefurahi kuona wanashindana  kumuziki zaidi.” alisema Nikki wa Pili

Kwa kuongezea pia Nikki aliwashauri kuwa wao kama wasanii maneno mengi wanayoyasema huwa yanabaki kuishi katika jamii na ni vigumu kuyapoteza kwa mara moja hivyo kwa kila jambo wanalofanya au kuongea ni lazima wachagulie lile lililo sahihi ” maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kirahisi kwa hiyo  ni vizuri zaidi kama watachagua maneno ya kutumia kila mara” aliongezea Nikki wa Pili

Dogo Janja na Young Dee waliingia katika bifu zito baada ya Young Dee kukataa kufananishwa na msanii mwenzie Dogo Janja, huku akitoa sababu kuwa yeye ni mkubwa kimuziki kuliko msanii mwenzie huyo, lakini haikuwa rahisi kwa Dogo Janja kukubaliana na kauli ya mwenzie hivyo aliamua kumjibu, katika majibu yake Dogo Janja alimwita Young Dee ‘mteja’ na kwamba hata yeye hawezi kulinganishwa kimuziki  na mtu anaekula unga, kitu kilichofanya wawili hao kundelea kuzozana.

Nikki Wa Pili: Ipo siku nataka kugombea uraisi

Mwanamuziki na Rapa maarufu Tanzania kutoka kundi la Weusi anayejulikana kama Nikki wa pili amekiri kuwa moja kati ya ndoto yake kubwa maishani ni kuja kugombea uraisi ili kusaidia nchi yake ya Tanzania kutokana na matatizo ambayo wananchi wanayo na wimbi kubwa la umaskini unaolikabili taifa hili.

Kukiwa na wimbi kubwa la wasanii wa muziki wa Bongo fleva kujiingiza katika fani ya siasa ambayo hayo yameonekana kwa wasanii wakubwa kwenye tasnia hii ikiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo maarufu kwa jina la sanaa kama “Sugu” ambaye aliachana na muziki na kuamua kuingia kwenye siasa. Pia mfano mwingine ni Proffesor Jay ambaye alikuwa ni rapa maarufu sana kwa nyimbo zake naye pia aliamua kuukacha muziki na kuamua kuingia katika siasa ambaye sasa ni Mbunge wa Mikumi lakini pia wasanii wengi wamejaribu kuingia katika siasa kama Wema Sepetu lakini hawakufanikiwa.

Katika mahojiano aliyoyafanya Nikki wa pili hivi karibuni alisema kuwa ni vizuri kwa wasaanii hawa kuingia katika siasa kama wabunge ili kusaidia jamii zao na Watanzania kwa ujumla lakini yeye kwa ubinafsi wake ameona kuwa hatogombania ubunge bali anataka moja kwa moja anataka akagombanie uraisi wa nchi ili apate nafasi kubwa zaidi kutatua matatizo ya wananchi. Mwanamuziki huyo alisisitiza:

“Ipo siku nataka nataka kugombea uraisi kwasababu nitakuwa na nafasi kubwa ya kutatua matatizo ya Watanzania kuliko kuwa mbunge”.