Sugu Amlilia Mama Yake, Asema Mama Yake Aliamini Alifungwa kwa Kuonewa.

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini ambae pia ni mwanasiasa na mbunge kupitia chama cha upinzani chadema kutoka katika jimbo la Mbeya Sugu ameshindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi muda wote wa kusoma risala ya mama yake mzazi aliywafiki mapema wiki hii katika hospitali ya Muhimbili.

Mama wa msanii Sugu alikuwa wiki hii akiwa na miaka 61, huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua ukiwa ni figo na kushinikizo la damu.

Akisoma risala hiyo huku akilia, Sugu anasema kuwa kitu kikubwa ambacho mama yake aliamini kipindi yeye amefungwa ni kwamba alikuwa hana kosa basi alifungwa kwa kuonewa hata hivyo Sugu anasema kuwa pamoja na kwamba mama yake alikuwa na ugonjwa wa figo alkini alizidi kuumwa baada ya kugundua kuwa mtoto wake yuko jela.

Mama mazazi wa Sugu alikuwa akijishughulisha na kilimo  kidogo nyumbani kwao na alikuwa mjane tangu mwaka 1992 baada ya kufiwa na mme wake na hakutaka kuolewa tena bali alijikita kusali katika kikundi cha karismatiki katika kanisa la Roma.

Baaada ya mwili huo kuagwa katika kanisa la Roma katika hopitali y Muhimbili , mwili huo utasafirshwa na kwenda kuzikwa mkoani Mbeya.

Faiza- Sijaenda Kwenye Msiba Wa Mama Sugu Sababu Alikuwa Hanipendi

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa Msanii wa Bongo fleva na Mbunge wa Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi sababu zilizompelekea mpaka kushindwa kuhudhuria msiba wa Mama Mkwe wake.

Siku chache zilizopita Mama mzazi wa Sugu Bi. Desderia Mbilinyi aliaga dunia baada ya kugua kwa muda mrefu ambapo siku ya jana ilifanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Muhimbili hospitali.

Lakini siku ya jana hapo kanisani Faiza hakuonekana kabisa na badala yake alionekana mtoto wake aliyezaa na Sugu hali iliyoibua maswali ya kwanini hakuhudhuria msiba.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Faiza amefunguka kuhusu kutohudhuria Kwenye msiba:

Sijaenda wala sijashiriki Kwenye msiba lakini Sasha ameniwakilisha yupo pale kwa ajili yangu kila mtu akimuona Sasha pale atajua amemuwakilisha Faiza.

Sikujisikia kwenda pale kwa mtu ambaye hajawahi kunipenda na mimi naamini ukienda Kwenye msiba wa mtu ambaye hajawahi kukupenda naamini unaenda kupata dhambi unatakiwa ukifika pale uwe na majonzi na mapenzi kwaiyo sikuhitaji kuwepo sehemu ambayo sijutakiwa kuwepo”.

Faiza amekuwa Kwenye mgogoro wa muda mrefu na Sugu pamoja na Familia yake yote kutokana na malezi ya mtoto wao Sasha.

 

Tanzia- Sugu Afiwa na Mama Yake

Mnunge wa Mbeya Mjini na msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amedaiwa na mama yake mzazi.

Mama yake na Sugu alifariki siku ya jumapili Agosti 26, 2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu.

Taarifa ya kifo hicho, imethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano ya umma na huduma kwa wateja katika Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.

Sugu Akiwa na Mama yake enzi za unaishi wake

Mwenyezi Mungu Ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

Sugu Aapa kuiburuza BASATA Mahakamani, Asema Wasimfananishe na Roma

Baada ya kupokea  barua kutoka BASATA msanii wa hip-hop wa muda mrefu Sugu amefunguka na kuongea akiwa bungeni Dodoma anasema kuwa anaona kama BASATA  wanafanya uonevu kwa sababu hata sasa wimbo huo uliofungiwa bado alikuwa anautoa rasmi bali ulikuwa umevuja lakini kitu cha ajabu ulishafunguiwa kabla haujatoka.

Lakini pia sugu amewaomba BASATA wasimfananishe na Roma ambae waliweza kumfungia na baadae kusema wamemsamehe kwa sababu waliweza kumuonea huyo.

Wimbo umevuja wao wanatoa statement ya kufungiwa,hawajawahi hata kuingia studio , hawajui hata gharama za wimbo na kutengeneza hayo,wanataka tuimbe nyimbo za matusi..mimi sio kama Roma ,,ninaiburuza mahakamani BASATA , mimi wimbo sijatoa bado ila umevuja tu , nina mawakili sita na nitawaburuza mahakamani ndio watakoma.

 

BASATA Waupiga Stop Wimbo Mpya Wa Sugu

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kuufungia rasmi Wimbo Mpya wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Sugu ameachia wimbo huo unaoitwa #219 ambayo  ni namba yake ya kifungo jela alipokaa kwa miezi kadhaa.

BASATA wameufungia wimbo huo huku wakiweka wazi sababu kubwa ni maudhui yake ambayo yanaleta uchochezi katika jamii na kuhatarisha Amani ya nchi.

Mbali na kuufungia wimbo huo, Basata wamemuonya msanii huyo kwa kumtaka kuacha mara moja kuutangaza na kuisambaza ngoma hiyo.

Hii ndio barua rasmi iliyotolewa na BASATA:

“Sina Sababu ya Kusema Namuhurumia Kapata Matatizo Shauri Zake”. Amefunguka Faiza Baada ya Sugu Kufungwa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally ambaye amejipatia umaarufu zaidi kutokana na kuwa mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Uhusiano wa Sugu na Faiza sio mzuri siku zote kwani ni mara nyingi wamekuwa watu wa kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii huku Faiza akimtuhumu Sugu kwa kukataa kumlea mtoto wao na kupelekea vita kali kati yao.

Siku ya Jumatatu Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano Jela baada ya kukutwa na hatia na mahakama ya hakimu mkazi Mbeya ambapo Sugu alihukumiwa kwa kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi na lugha ya fedheha dhidi ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. J.P Magufuli.

Baada ya hukumu hiyo hatimaye mzazi mwenza wa Sugu, Faiza amefunguka kuhusiana na hukumu hiyo na kusema amechukizwa na kitendo hicho kilichofanyika maana hakikuwa cha haki kabisa.

Faiza amesema hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Radio 5 ambapo amedai kitendo hicho kimemuuma kama mzazi mwenzake ingawaje maisha yake yanakuwaga magumu zaidi Sugu akiwa uraiani.

Nikimuangalia kwenye maisha yangu namuona kama adui ambaye hana neno kwangu, kwaiyo mimi sina sababu ya kusema sijui namuhurumia sijui kapata matatizo shauri zake, Hayo matatizo kwa kweli naona akiwa uraiani maisha yangu yanakuwa magumu sana, sijali japo siombi akae jela hivyo lakini saa nyingine naona inabidi aah sijali kwa kweli”.

 

Nikki wa Pili Amjibu Mh.Nasarri Kuhusu Mh. Sugu

Msanii wa muziki nchini Nikki wa Pili amemjibu Mh Joshua Nassari baada ya kuwatuhumu wasanii kwa kukaa kwao kimya baada ya Mh.Sugu kukamatwa na kuweka polisi kwa zaidi ya siku kumi sasa wao wakiwa wamekaa kimya ilhali mbunge huyo alikuwa mstari wa mbele kuwatetea wasanii katika kupata maslahi yao.

Mh. Nasari anawataka wasanii wakumbuke kuwa Sugu ndie msanii wa kwanza kupigania haki zao kwa uda mrefu na kukataa kufanya kazi za muziki  bila kulipwa na haki hiyo.

wasanii wa bongo fleva mmesahau kabisa harakati za sugu kupigania muziki wenu kusimama.sugu yupo selo siku ya kumi sasa wasanii mmepiha kimya,courtin hamtokei,jela hamji kumuona , mmeamua kumtumikia kafiri.mmesahau kuwa alianzisha harakati za kugoma kuimba bure.

Katika kumjib Mh. Nassari nikki wa pili amemwambia kuwa wasanii wanaogopa kupaza sauti ya kutetea jambo kwa sababu hakuna umoja kati yao na hata wanapotaka kusimama kutetea jambo fulani mtu anaweza kujikuta peke yake.

Wasanii hawna umoja na chama chao hakina nguvu kwaio hata kinapotokea kitu  wasanii wakatakiwa kulitolea sauti hakuna platform   ya kulishikilia jambo hilo  na kujikuta kila msanii huyo yuko peke yake  na kupaza sauti peke yae wasanii wengi wanaogopa hilo.-Aliandika Nikkki wa Pili.

Mheshimiwa joseph mbilinyi jina la usanii sugu aliwekwa jela siku kama 10 zilizopita kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi kwa wananchi juu ya serikali iliyopo madarakani.

 

Sugu Avunja Ukimya Juu ya Swala la Malezi ya Mtoto

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya mjini amevunja ukimya na kufunguka kwa mara ya kwanza juu ya shutuma zinazomkabili  dhidi ya mzazi mwenzie Faiza Ally.

Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kumshutumu Sugu kwa kukataa kumlea binti yao mdogo Sasha. Baada ya juzi kumsema Sugu kuwa hamjali mtoto wake na kukataa kumlipia mtoto huyo ada ya shule hadi kufikia hatua ya Sasha kurudishwa nyumbani.

Kwa mara ya kwanza Sugu kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kusema anamlipia ada binti yake huyo lakini mwenye matatizo ni mama yake kwani humkataza kumuona, aliandika yafuatayo juu ya tuhuma hizo:

“Huwa sipendi kuposti hivi vitu lakini imenibidi,  hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwaajili ya Sasha na ilikuwa mwezi huu wa tisa nimuanzishe shule ya Feza Nursery pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema hahitaji nilipe ada na kunizuia nimsomeshe tena Sasha! Na kwamba ana uwezo wa kumsomesha mwenyewe shule yoyote anayotaka na ndo kumpeleka huko Hazina international ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu. Hivi kama nyie mngefanyaje?

Hata hivyo mara baada ya kusema hayo Faiza alikuja juu na kumuita Sugu muongo na amewahi kulipa ada mara mbili tu tangu mtoto wao aanze kusoma na miaka yote hiyo Faiza ndo alikuwa analipa ada.