Namshukuru Mwanangu Kufanana na Mimi, Amenistiri :-Ray

Msanii wa maigizo nchii ray kigosi  anasema kuwa ansshukuru sana baada ya mtoto wake kufanana sana na yeye kuliko mama yake kwa sababu kama mtoto angefanana sana na mama yake basi inawezekana watu wangeanza kusema kuwa  ameibiwa mtoto.

ray anasema kuwa walimwengu wamekuwa ni watu wa kusema maneno mengi sana kiasi kwamba wamekuwa wakisema maneno mengine bila kujua kuwa yanapomfikia mlengwa yanaweza kumuumiza kiasi gani.

walimwengu bhana wamekuwa watu wa ajabu sana, ingetokea kuwa mtoto kafuata kwa mama  bila kufuata kwangu wangesema kuwa huyo mtoto sio wangu  na yangeibuka mengi sana,Namshukuru mungu mwanangu kafuata kwangu amenifichia maneno mengi sana kufanana na mimi Jaden –Alisema Ray

Chuchu Hans :-Mashabiki Walilazimisha Penzi Langu na Ray

Mwanadada Chuchu Hans amefunguka na kuelezea kwa undani juu ya swala la kuachana kwake na mzazi mwenzie ambae  Ray kigosi ambapo hvi karibuni ziliibuka tetesi kuwa waili hao wameachana na kwamba Ray ameamua kumuachia nyumba mwanadada huyo.

Chuchu anasema kuwa kitu kikubwa wanayakiwa wat kujua ni kwamba wao hawakuwahi kuwa katika mahusiano lakini baada ya mashabiki kuzsha sana maneno wakaone isiwe tabu na kuamua kufanya kweli kama walivyotaka iwe.

Hata hivyo akiongea kwa hamaki kabisa, mwanadada huyo anasema kuwa sio kweli kuwa walikuwa wakiishi nyumba moja na ray  bali ray alimpangia nyumba pindi walipoingia katika mahusiano na alipopata mimba ya mtoto wake wa kiume.

Chuchu anasema kuwa watu wanatakiwa waelewe kuwa mashabiki ndio waliolazimisha pezi lake na ray na wala sio vinginevyo.

Uongozi wa Airport Wajibu Tuhuma za Ray Kuibiwa Mizigo

Uongozi wa uwanja wa ndege  wa mwl julius kambarage nyerere wamejibu tuhuma za kuibiwa kwa msanii ray kigosi baada ya msanii huyu kulalamika sana kuwa aliibiwa mizigo yake baadhi akiwa uwanja wa ndege.

Uongozi wa uwanja wa ndege unasema kuwa mtu yoyote anapopata tatizo lolote ni vizuri zaidi kama watatoa taarifa moja kwa moja kwa uongozi na sio kuandika katika mitandao ya kijamii kama ambavyo wamekuwa wakifanya baadhi ya watu.

katika ukurasa wa insta wa msanii Ray kigosi aliandika ”

Ray Kigosi-Wema Anastahili Adhabu Ya Kufungiwa

Msanii mkongwe wa sanaa ya Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’  amefunguka na kuweka wazi kuwa msanii mwenzake Wema Sepetu anastahili kabisa adhabu aliyoipata ya kufungiwa kufanya filamu kwa miaka miwili.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Sammisago Tv, Ray ameweka wazi kuwa ni sawa tu kwa adhabu aliyoipata Wema kwani kitendo alichofanya hakikuwa kizuri kabisa hasa kama msanii ambaye ni kioo cha jamii;

Wema alistahili mkupewa adhabu ya kufungiwa unajua tatizo la Watanzania wanapenda tuambiane vitu vya kusifiana sifiana tu lakini tusiseme pale mtu anapokosea kwaiyo mimi nikiwa kama msanii mkongwe ambaye nimekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu nasema kabisa kuwa Wema alikosea sana sana kwa sababu ukiangalia Wema ni Brand kuna watu wengi wengi sana ambao wanamuangalia hao wanaomuangalia wafanye nini yeye ni kioo cha jamii  kimsingi kabisa amefanya kosa lakini tumeshamuona Wema akiomba msamaha mara nyingi sana imefika wakati sasa abadilike”.

Kila msanii wengi amekuwa na maoni yake juu ya sakata la Wema wapo ambao wamemchana laivu kuhusu kosa lake lakini wapo ambao wamemkingia kifua kama vile Wolper.

Ray Kigosi Awapa Somo Viongozi wa Wasanii Walioteuliwa na BASATA.

Msanii wa filamu nchini, Vincent Kigosi (Ray Kigosi) amewataka wajumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mwana FA pamoja na single Mtambalike ‘Richie’ ambao wameteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, kutojisahau kwa nafasi walizopewa.

Akiwa kwenye interview Ray amesema “nimefurahi kwa uteuzi huu lakini ningefurahi zaidi kama pale BASATA na Bodi ya filamu wangekaa watu ambao wanajua kila kitu kuhusu sanaa, nimshukuru sana Waziri kwa kuwateua Mwana FA na Richie, ila niwaambie tu wasijisahau watusemee sisi na sio wajisemee wao ili tuweze kupiga atua kisanaa

Wasanii hawa wameteuliwa wakiwa kama wawakilishi wa wasanii wengine kaatika bodi ya BASATA ili kufanikisha utatuaji wa matatizo ya wasanii.

Ray kwasasa amekuwa kimya sana kwenye gemu ya filamu lakini amewaahidi mashabiki zake kuwa anawaletea kitu kipya hivi karibuni

Ray Atamani Mtoto Wake Kupata Elimu Nje ya Nchi.

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo Movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka na kukiri kuwa anatamani sana mtoto wake Jaden aende akapate elimu katika nchi za nje.

Ray amefunguka kuwa yupo katika mapambano makubwa ya kufa na kupona ili kuhakikisha mtoto wake wa kipekee Jaden anaenda kupata elimu bora kabisa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Dimba, Ray alisema si kwamba Tanzania hakuna shule bora kwa hapa nyumbani lakini ndoto zake anatamani mwanawe asome nje ya Tanzania kama ambavyo amejiwekea toka awali.

Nilitamani sana mwanangu akasome nje na akikua kidogo tu atasoma moja ya shule bora kabisa, natamani abadilishe mazingira, natambua zipo shule bora sana hapa lakini si mbaya pia akazoee na mazingira mengine, napambana kuhakikisha namwekea akiba ya kutosha ili asipate tabu katika kupata elimu yake”.

Jadrn ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Msanii mwenzake wa Bongo movie mwanadada Chuchu Hansy

Ray Atamani Kumpeleka Mtoto Wake Kusoma Majuu

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo Movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka na kukiri kuwa anatamani sana mtoto wake Jaden aende akapate elimu katika nchi za nje.

Ray amefunguka kuwa yupo katika mapambano makubwa ya kufa na kupona ili kuhakikisha mtoto wake wa kipekee Jaden anaenda kupata elimu bora kabisa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Dimba, Ray alisema si kwamba Tanzania hakuna shule bora kwa hapa nyumbani lakini ndoto zake anatamani mwanawe asome nje ya Tanzania kama ambavyo amejiwekea toka awali.

Nilitamani sana mwanangu akasome nje na akikua kidogo tu atasoma moja ya shule bora kabisa, natamani abadilishe mazingira, natambua zipo shule bora sana hapa lakini si mbaya pia akazoee na mazingira mengine, napambana kuhakikisha namwekea akiba ya kutosha ili asipate tabu katika kupata elimu yake”.

Jadrn ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Msanii mwenzake wa Bongo movie mwanadada Chuchu Hansy.

Sitaki Kutumika Kwenye Kampeni 2020, Niliona Madhara Yake- Ray

Muigizaji wa Bongo movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray amefunguka na kuweka wazi kuwa hataki tena kutumiwa na Vyombo vya siasa Kwenye kampeni za uchaguzi.

Ray amefunguka na kusema anaunga Mkono Kauli na Katibu kuwa hawataki kutumia tena wasanii Kwenye kampeni za siasa kwani na yeye ameona madhara ya kutumika Kwenye kampeni hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Ya, Ray amefunguka zaidi na kusema

Kimsingi yeye alichozungumza Katibu mimi siwezi kukataa alichozungumza cha muhimu tusubiri tuone kama kweli wasanii hawatotumika kwa ajili ya kampeni lakini mimi binafsi sitaki wanaitumie kwa sababu nimeona madhara ya kutumika Kwenye kampeni lakini dunia nzima hata Marekani tunaona wakina Trump wanatumia wasanii kufanya kampeni lakini kama Katibu Bashiru kazungumza basi atakuwa ana target kwaiyo naheshimu maamuzi yake lakini kama wakitumia wasanii basi tutawasuta kwa Kauli waliyotoa”.

Wasanii wengi waliotumika kupiga kampeni 2015 walikosolewa sana kutokana na baadhi yao kuhama hama vyama kwa maslahi yao binafsi ya kujiingizia kipato.

“Nikifa Nizikwe na Ray na Awasomeshe Watoto Wangu”- Steve Nyerere

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanaharakati wa siasa Steve Nyerere ameibuka na kudai hawezi kuacha kusimamia misiba ya watu na msiba wake anataka msanii mwenzake ausimamie.

Steve ameibuka na hili baada ya sakata lake lililompata siku chache za nyuma baada ya kugubikwa na skendo ya kuiba pesa za Michango ya rambirambi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Steve amesema kitendo hicho cha kusimamia misiba kimeweza kwa namna moja au nyingine kumfanya pia awe karibu na watu wazito nchini ambao wanamuunga mkono kwenye kujitolea kwake.

Sitaacha kusimamia misiba ng’o, wanaosema waache waseme watachoka. Ninasimamia misiba kwa sababu ninafahamu na mimi ipo siku nitaondoka na watu watasimamia msiba wangu. Niseme tu wazi hata kama nikiondoka leo nataka Vincent Kigosi ‘Ray’ asimamie na kuwasomesha wanangu“.

Steve Nyerere amekana kabisa skendo za yeye kudhulumu pesa za rambirambi na kudai akikusanya basi hufikisha kwa wahusika.

Ray Kigosi- Nisingefanana Na Mwanangu Walimwengu Wangenipa Tabu Sana

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Vincent Kigosi maarufu kama Ray amefunguka na kuweka wazi kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kuwa anafanana copyright na mtoto wake Jayden.

Kabla Ray hajazaa mtoto na Muigizaji mwenzake Chuchu Hansy kulikuwa na tetesi kuwa Msanii huyo Hana uwezo wa kuzaa (Tasa/ Mgumba) kwani alikuwa Kwenye Mahusiano na wanawake wengi lakini hakuwa na mtoto.

Lakini mwaka juzi Ray na mpenzi wake wa siku nyingi Chuchu Hansy walifanikiwa kumkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja na kwa bahati nzuri mtoto huyo ni kipindi kabisa ya Baba yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ray amefunguka na kusema anamshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kufanana naye kwani vinginevyo walimwengu wangemsumbua kwa maneno ya kejeli.

Walimwengu bwana wanaongea sana. Ingetokea mtoto labda kafuata kwa mama kila kitu halafu kwangu hamna kitu, yangeibuka ya kuibuka hadi ungeshangaa, nashukuru sana Jaden amenifichia maneno kwa kufanana na mimi”.

 

Monalisa na Ray Kigosi Wang’aa Kwa Tuzo Nchini Ghana

Muigizaji wa Bongo movie Yvonne Cherry kwa Jina maarufu la usanii kama Monalisa ameng’aa kwenye tuzo za African Prestigious Awards (APA) zilizofanyika nchini Ghana.

Monalisa ameshinda tuzo kwenye kipengele cha Muigizaji bora wa kike nchini Africa. Tuzo hizo zilitolewa Siku mbili zilizopita.

Lakini pia Ray Vicent Kigosi pia ameibuka kidedea baada ya kukwapua tuzo ya Muigizaji bora wa kiume barani Africa huku wasanii kama Mzee majuto alibahatika kuchaguliwa kushindania Tuzo hizo.

Lakini pia Monalisa alipokea tuzo kwa niaba ya Raisi John Pombe Magufuli ambaye ameshinda tuzo kwenye kipengele cha Uongozi bora.

Kwa upande mwingine, Mtanzania Moise Hussein ameshinda tuzo hizo kwenye kipengele cha mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

 

Ray Kigosi:Niko Tayari Kumuita Dogo Janja Shemeji kwa Uwoya

Msanii Vicent Kigosi maarufu kama Ray, amefunguka na kusema kuwa yeye hana wivu wowote na msanii mwenzie Irene Uwoya ambae hivi karibuni alifunga ndoa na msanii wa bongo fleva Dogo Janja.Ray ambae ndie alikuwa mtu wa kwanza kumfungulia Irene Uwoya milango ya sanaaa katika tasnia hiyo anasema kuwa hana wivu kabisa na mwanadada huyo kuolewa kwa sababu kati yake na Dogo Janja yeye ndie alikuwa wa kwanza kumuona hivyo kama angetaka kuwa nae katika mahusiano angekuwa ameshamchukua siki yingi kabla yake .

Mimi siwezi kuwa na wivu  nilianza kumuona irene uwoya kabka hata ya Dogo Janja, Dogo Janja ni mdogo wangu lakini pia naheshimu maamuzi yake ya kumuoa Irene Uwoya.Mimi yule ni dada yangu ambae tumetoka nae mbali sana kwenye sanaaa, na mimi ndie nilimu-introduce Irene  kwenye sanaa nikiwa na marehemu Kanumba.Kama ningekuwa nimemuona na ningekuwa nimemtamnai basi ningekuwa nae  lakini niliamua kufanya nae kazi tu, wengine wamemuona na wamemchukua ilo ni jambo zuri hata Mungu pia anafurahi. -Alifunguka Vicent Kigosi

Lakini pia Ray ameongezea kuwa kwake yeye yupo tayari kumuita Dogo janja shemeji kwa sababu alishachukua jukumu la kumuoa dada yake Irene Uwoya hivyo hana kipangamizi chochote na hana sababu ya kukataa kwa sababu ndoa ni jambo la kheri.

Mapenzi ni kipenda roho na kipenda roho hula nyama mbichi,kama wamependana wenyewe inatosha .mimi niko tayari kumuita shemeji kwa sbabu tayari kamuoa dada yangu -Aliongezea Ray Kigosi

Dogo Janja na Irene Uwoya waliingia katika headlines za vyombo vya habari baada ya kufunga Oktoba 28 mwaka huu  , ambapo watu wengi wameshikwa na butwaa kwa ndoa iyo kutokana na umri wa wawili hao kuwa umetofautiana sana ,lakini pia wawili hao walikuwa wakikanusha kabisa kipindi cha nyuma kuhusu mahusiano yao.Hata hivyo wenyewe wamethibitisha kupendana hata kama kuna utofauti wowote uliopo.

Ray ambae pia yupo katika mahusiano na msanii mwenzie wa filamu Chuchu Hans wamefanikwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

Maoni ya Ray Kigosi kuhusu madai ya kwamba Diamond na marehemu Kanumba ni Freemason

Ray Kigosi amechoshwa na umbea wa Tanzania kusema mojawapo ya anayefanikiwa ni Freemason.

Alipeana mfano wa marehemu Kanumba na pia Diamond ambao ni wasanii waliofanikiwa sana Tanzania. Na hiyo ilipofanyika, wakaanza kutaniwa wamejiunga na kanisa la freemason ambalo lilieneza sanaa yao.

Hivi ndivo alivosema kwenye instagram:

1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!

2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!

3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.

Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.

5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.