“Chiddi Ameletwa na Mungu ‘Special’ Kwaajili Yangu”- Shamsa Ford

Msanii wa filamu za Bongo movie mwanadada shamsa Ford ameibuka na kudai anampenda sana mumewe huyo na anaamini ameletwa maalumu kwa ajili yake.

Lakini pia Shamsa amedai kuwa anaamini kama bila kumuweka ndani huenda hadi leo angekuwa amedoda kwa kitoolewa kwani kwenye ulimwengu huu haoni kama kuna mwanaume aliyestahili kuwa mumewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Shamsa alisema kuna sababu nyingi za kumfanya aseme hivyo kubwa ikiwa ni jinsi mwanaume huyo anavyompenda kwa dhati kiasi kwamba anaamini ame­letwa na Mungu spesho kwa ajili yake.

Hata kama dunia ingeisha leo na tukarudi mara ya pili mimi bado nin­gemchagua mume wangu Chid kwa sababu naona ndiye mwanaume pekee aliyekuja kwa ajili yangu. Ananipa furaha isiyo kifani kiasi kwamba naamini kama asingetokea yeye, mpaka leo ningekuwa sijaolewa, yaani ningekuwa bado nas­ubiri aje hata angechelewa vipi”.

 

“Wanawake Wenye Mapenzi Ya Dhati Tunaonewa Sana”-Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie staa Shamsa Ford Ameibuka na kutoa ujumbe wenye utata na kusababisha minong’ono juu ya ndoa yake na mfanyabiashara Chiddi Mapenzi Kuzidi.

Kama utakumbuka siku za nyuma kidogo Chiddi Mapenzi alikamatwa hadharani na mke we Shamsa Baada ya kuchepuka na mrembo wa Instagram na kusababisha mtikisiko katika ndoa yao.

Lakini baadae kidogo Shamsa aliweka wazi kuwa ameamua kumsamehe mume Wake na hata kusema hadharani kuwa hawezi kumuacha mume Wake Kisa ana wanawake wa kando.

Na kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za kutokuwa na maelewano kati ya Shamsa na mumewe kutokana na maneno ya utata anayoweka kwenye Mitandao ya kijamii yenye mafumbo.

Siku ya jana Shamsa ameibua tena gumzo na kusababisha watu kuhoji labda huenda mume Wake Chiddi amechepuka tena ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shamsa aliandika maneno haya:

Wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati huwa tunaonewa sana, Wanawake ambao tunaishi maisha ya Uhalisia huwa tunaonekana washamba, Lakini wale Wanawake wachunaji ndio huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa”.

 

Napenda Kumpumzisha Mke Wangu- Chiddi Mapenzi

Mfanyabiashara maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Chiddi Mapenzi Ambaye pia ni Mume wa staa wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai anapenda kumpunzisha mke wake.

Chiddi Mapenzi na mke Wake Shamsa wanamiliki duka la nguo ambalo ndilo linawaingizia kipato na mara nyingi Shamsa amekuwa akionekana kama ndio msimamizi wa duka hilo.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Chiddi ameweka wazi kuwa hapendi kabisa kumchosha mke wake  kwa kumuweka dukani kila siku badala yake anapenda kumuona akiwa amepumzika nyumbani.

Ukiona Shamsa yupo dukani ujue kabisa mimi sipo, nimesafari, lakini kama nipo mjini, siwezi kumruhusu kukaa dukani.

Namuonea huruma sana, kuna kipindi anachoka halafu yeye ni mama, ana majukumu mengine anafanya ya nyumbani hivyo anapopumzika ni vizuri”.

Lakini pia Chiddi amezima kabisa tetesi za wawili hao kuachana ambazo zilizuka baada ya Shamsa kuweka kauli tata kwenye social media.

 

Chiddi Mapenzi Ajibu Tetesi Za Kumwagana na Shamsa Ford

Mfanyabiashara maarufu kwenye mitandao ya kijamii Chiddi Mapenzi amefungukia tetesi za kuachana na mke wake  ambaye ni muigizaji wa  Bongo movie Shamsa Ford.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha FNL cha East Africa Tv, Chiddi amesema kuwa msanii huyo bado ni mke wake na hajaamua kumpost kwasababu yuko busy kwasababu anatarajia kufungua duka lake mwezi ujao.

Shamsa ni mke wangu sio kwamba hapost, labda mwenyewe kaamua ana mambo yake lakini by the way anafungua duka lake soon mwezi ujao la kike kwahiyo hakuna tatizo lolote la kike nipo nae mama”.

Lakini pia Chiddi aliendeleq kutetea mahusiano yake na Shamsa:

Unajua watu wengine wamezoea kupostiana sasa mimi siko hivyo wewe unanijua ndugu yangu, mimi mtu mzima siko hivyo mimi niko nae sema nilikuwa sipo nilikuwa safari juzi kati tu, kwahiyo mama niko nae sema yuko busy anataka kufungua ofisi yake anashinda dukani kwake”.

Tetesi Za Shamsa kuachana na Chiddi zilianza Baada ya Msanii huyo kujiposti akiwa na majeraha usoni yaliyopelekea Tetesi Za kupigwa na Mume Wake Lakini pia amekuwa akiweka vijembe vinavyozaniwa kumuelekea Mume Wake huyo.

Shamsa Ford Akiri Kusumbuliwa na Wapenzi Wa Zamani Wa Chiddi Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Shamsa Ford amefunguka na kudai anapata sana usumbufu kutoka kwa Wanamaker ambao wamewahi kuwa wapenzi wa mume wake Chiddi Mapenzi.

Shamsa amedai usumbufu ambao amekuwa akikumbana nao ni mkubwa sana kwani wamekuwa wakimfanyia visa yeye kwa wivu kwa kuwa yeye ndio mke halali wa ndoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shamsa alisema amekuwa akisumbuliwa na wanawake ambao waliwahi kutoka kimapenzi na mumewe ambapo kila anapokutana nao wamekuwa wakimfanyia visa kama kumpiga vikumbo na fujo nyingine za hapa na pale.

Kiukweli wanawake wa zamani wa mume wangu wananisumbua sana, kila ninapokutana nao wananipiga vikumbo, wananifanyia visa na maneno kibao yakiwatoka huku wakitaja jina la Chid, naomba niwaambie tu kuwa wanatakiwa kukubaliana na hali halisi maana aliniona ninamfaa ndiyo akanioa na kuniweka ndani hivyo fujo wanazofanya hazisaidii bali wanatakiwa watafute wa kwao”.

 

Sitaachika Kwa Mume Wangu Ng’oo-Shamsa Ford

Msanii wa filamu za Bongo Movie Shamsa Ford amefunguka na kuungelea tetesi zilizozuka wiki iliyopita kuwa yeye na mume wake mfanyabiashara Chid Mapenzi wameachana.

Tetesi za Shamsa na Chid kuachana ziianza baada ya Shamsa kuweka status iliyosomeka:

Mapenzi au kumpenda mtu, kusikufanye uwe mtumwa… ukiona unampenda mtu halafu anakuchukulia poa achana naye. Maisha ya sasa hivi, siyo ya kujipendekeza au kulazimishana… mtu uwaze maisha magumu bado mapenzi yakusumbue? Acha ujinga na usikubali kuwa mtumwa… wewe funika sura fanya kama huoni..”.

Kwenye mahojiano Gazeti la Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kila akiweka ‘status’ kwenye ukurasa wake wa Instagram inayohusu ishu za kuachana, kuna wanaodhani inamhusu yeye, wakati huwa kuna ambao wamekuwa wakiomba ushauri na kwa sababu hawezi kumshauri kila mtu kwa wakati wake, huamua kuandika kwenye ukurasa wake.

Unajua nilipoweka ‘status’ kila mtu alinihoji na wengine kunifuata ‘DM’ wakitaka kujua nini kimenikuta, niwaambie tu kwamba sitaachika mpaka Mungu atakapotutenganisha ingawa wapo wanaoniombea hilo kila siku”.

 

Shamsa Ford Adai Hajali Kuchukiwa na Watu Ilimradi Anapendwa na Mumewe

Msanii wa filamu za kibongo Shamsa Ford amefunguka na kusema hajali kama watu  watamchukia kwa muonekano wake au hata kusema ukweli inapobidi ilimradi anapendwa na mume wake Chidi Mapenzi inatosha.

Shamsa amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii tangu avae gauni lililokuwa fupi sana Kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi Mketema wiki iliyopita.

Kwenye mahojiano na gazeti  Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako.

Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu”.

 

Penzi Langu na Shamsa Ford Halina Dalili Ya Kuvunjika- Chidi Mapenzi

Mfanyabiashara maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Rashid maarufu kama Chidi Mapenzi ambaye pia ni mume wa msanii wa Bongo movie Shamsa Ford ameweka wazi kuwa hana Mpango wa kuachana na mke wake.

Chidi Mapenzi amekanusha tetesi zinazodai  kwamba penzi lao lipo hatarini kuvunjika huku akidai kwa sasa wapo vizuri na wanafurahia maisha yao.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv,  Chidi amedai kuwa siri ya kudumu kwao ni kutambua kosa lake na kuamua kujishusha mara moja:

Mimi ni mke wangu huwa hatugombani, nikimkwaza lazima niwe chini nitafanyaje Mke wangu nikimkosea huwa anakuwa na hasira lakini baadaye hasira zinaisha na maisha yanaendelea”.

Chidi amesema sio kweli kwamba ndoa yao ilikuwa ivunjike, yote ambayo yalikuwa yanazungumzwa na mitandao ya kijamii kwamba ndoa yao ipo mbioni kuvunjika sio ya kweli.

Shamsa Ford: Sina Bifu na Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kusema hana bifu lolote na staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize hata baada ya kumdhalilisha mume wake .

Wiki chache zilizopita Harmonize alikuwa kwenye vita kali ya Ex wake Jacqueline Wolper na katika ugomvi wao alimtaja mume wa Shamsa Chidi Mapenzi kama mmoja wa mpenzi wa zamani wa staa jambo ambalo lilimkera Shamsa.

Shamsa aliweka wazi kuwa hajafurahishwa na maneno ya Harmonize kumuingiza mume wake Kwenye bifu lake na Wolper na kumdhalilisha wakati anajua wazi kuwa ameoa tayari.

Kwenye mahojiano na FNL ya EATV, Shamsa amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.

Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao.

Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu”.

 

“Bila Wewe Sijiwezi Rashid Wangu” Shamsa Ford Afunguka Baada ya Kutangaza ni Mjamzito

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amezidi kushika kasi katika mitandao ya kijamii baada ya kutangaza rasmi kuwa yeye na mume wake Rashid ‘Chiddi Mapenzi’ wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Shamsa amekuwa muwazi kuwa anampenda sana mume wake pamoja na changamoto wanazopitia ambapo ni juzi tu Shamsa alisema rasmi kuwa hata kama mume wake akichepuka na kutembea na wanawake wengine hawezi kumuacha.

Miezi michache iliyopita Chiddi Mapenzi alikumbwa na skendo mitandaoni baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na moja ya wasichana maarufu instagram ambaye anaitwa Irene lakini Shamsa alisema pamoja na kuchepuka hawezi kumuacha.

Shamsa ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mumewe Chiddi baada ya kumuita baba kijacho ambapo aliandika ujumbe huu:

I wish ningekuwa na neno la ziada la kukwambia zaidi ya nakupenda…… Bila  wewe sijiwezi Rashidi wangu….. Mwenyezi Mungu mume wangu halali baba K wangu”.

Wiki chache zilizopita Shamsa aliweka wazi kuwa alibeba mimba ya kwanza ya Chiddi lakini kwa bahati mbaya ikatoka kutokana na kupata stress za hapa na pale.

Huyu atakuwa mtoto wa pili kwa Shamsa ambaye tayari ana mtoto mwingine anayeitwa Terry aliyezaa na mumewe wa zamani lakini atakuwa mtoto wa kwanza kwa Chiddi na Shamsa.

Shamsa: Mume Wangu Kanikataza Kujichanganya na Marafiki

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa imekuwa ngumu sasa yey kutoka na kujichanganya na marafiki kama zamani kwani mumewe Rashid ‘Chid Mapenzi’ kampiga stop.

Kama ilivyo kwa kazi yoyote ni muhimu kujichanganya ndivyo ilivyo kwa wasanii wa Bongo movie hupenda kufanya matukio mbali mbali pamoja lakini safari hii imekuwa tofauti kwa Shamsa kwani tangu ameolewa amepunguza kabisa ushirikiano na wasanii wenzake.

Shamsa amefunguka na kusema yeye kupunguza muingiliano kwenye shughuli mbali mbali ni maagizo kutoka kwa mume wake ambayo hawezi kupuuzia ambayo anaelekezwa na mumewe.

Shamsa amepiga stori na Motomoto News, na kudai mara ya kwanza alikuwa akijichanganya mno kwenye ishu tofauti lakini kwa sasa anashindwa kutokana na kupigwa marufuku na mumewe baada ya kuwa na ujauzito mchanga uliochoropoka kutokana na kuzurura:

Mume wangu alinipiga marufuku kutoka toka licha ya kwa mbali mara ya kwanza nilikuwa natoka kibishi bishi tu lakini kwa sasa imebidi nimsikilize mume wangu zaidi maana mimba yangu changa ilitoka kwa sababu ya kutoka toka ovyo kwenda kwenye shughuli”.

 

“Nilipata Matatizo Mimba Yangu Ikaharibika”-Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka mazito kuhusu jitihada zake za kushika mimba ambapo amesema alishika ujauzito mwaka jana lakini kwa bahati mbaya mimba ikatoka.

Shamsa amefunguka na kuelezea janga hilo lililomkuta miezi michache iliyopita ambapo alidai kutoka na matatizo aliyoyapata mume wake Chidi ambaye aliwekwa rumande kwa tuhuma za kuuza na kuingiza nchini madawa ya kulevya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Lemutuz Online Shamsa Ford amefunguka zaidi haya:

Mimi naamini watoto wanaletwa na Mwenyezi Mungu kwa bahati mbaya au bahati nzuri nilishika ujauzito kipindi kile mume wangu kapata matatizo yale ya kuwekwa ndani na mimi mimba yangu ikatoka naona ilikuwa hofu ndio maana, unajua hapa mjini mume wangu hana ndugu kwaiyo mimi ndio nilikuwa kila kitu yaani nihahakikishe biashara zinaenda vizuri muda huo huo nikamuangalie Mume wangu ana hali gani kule polisi kwaiyo nilikuwa very stressed kwaiyo nikajikuta mwisho wa siku mimba yangu ya wiki tatu ikatoka”.

Shamsa ameolewa na Chiddi Mapenzi ambaye ni mfanyabiashara maarufu Lakini tangu wanafunga ndoa yao mwaka jana maneno mengi sana yalisemwa juu ya Mahusiano yao ikiwemo wapo waliodai hawatodumu jambo ambalo Shamsa amesema halitakuja litokee kwani wapo wote mpaka kifo kitakapowatenganisha.

Shamsa Ford: Mwanamke Mwingine Hatosababisha Nimuache Mume Wangu

Mwigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa kamwe hatokaa amuache mume wake Chiddi Mapenzi kwasababu ya yeye kuwa na mwanamke mwingine.

Katika siku chache zilizopita kumekuwa na tetesi za wawili hao waliooana miezi michache iliyopita kuachana kutokana na kukosekana kwa uaminifu baina yao baada ya tuhuma za Chiddi kuwa na uhusiano na wanawake wengine nje ya ndoa.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa alifunguka haya;

“Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa Mwenyezi Mungu. Sitoachana na wewe Kisa makelele ya wanadamu, nitaachana na wewe kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Unanipenda, unaniheshimu, unajishusha kuomba msamaha pale unapokosea  wakati wanaume wengine hawawezi kuomba msamaha hata wakikosea. Mume wangu nikikuelewa mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu. Maana anajitahidi huyo anayeitwa ILALA MJINGA kama ulivyomsave kwenye simu yako kusambaza msg kwenye magroup na kuwatumia waandishi ushahidi, jamani sitokaa nimuache mume wangu kwaajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamii. Amecheat Bill Clinton sembuse Rashid wangu? Nakupenda Rashid wa Shamsa Ford tupambane tuzidi tujenge familia yetu”.