Ali Kiba Apiga Shoo Ya Kifalme Oman

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba ambaye Wiki iliyopita alipiga bonge la shoo nchini Oman amedaiwa kufanya bonge la shoo aambalo limetajwa kuwa la kifalme.

Gazeti la Ijumaa wikienda linaripoti kuwa Ali Kiba aliwasili nchini humo katikati ya wiki iliyopita ambapo ali­pumzika kwenye hoteli ya nyota tano kabla ya kukinukisha katika ukumbi wa hoteli hiyo aliyofikia ijulikanayo kwa jina la InterContinental, Muscat wikiendi iliyopita.

Ijumaa Wikienda lilizun­gumza na mmoja wa mameneja wa msanii huyo aitwaye Aidan Seif ambapo alipoulizwa kuhusu mafanikio ya shoo hiyo, alisema anamshukuru Mungu imefanikiwa na kwamba ni muendelezo wa Kam­puni ya Rockstar4000 kumuandalia Kiba pamoja wasanii wengine wa lebo hiyo shoo kubwa nje ya nchi.

Unajua bila Watanzania, Kiba muziki wake usingependwa nje kama hivi tunavyopokea mialiko kila kukicha, tunaomba waendelee ku­tusapoti. Kiba amefanya vizuri sana Oman, watu wameruka mwanzo mwisho hivyo nina amini picha kama hii itatokea maeneo mbalim­bali“.

https://www.instagram.com/p/BtqS7UXBgm_/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=hkewas2vl692

Ali Kiba Ndani Ya Ngoma Moja na Timaya Wa Nigeria

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amepata shavu la maana Baada ya kushirikishwa kwenye Albamu mpya ya Msanii wa muziki kutoka Nigeria Timaya.

Album mpya ya staa Timaya wa Nigeria inayoitwa Chulo Vibes’ ikiwa na jumla ya ngoma tisa ambapo imewashirikisha wasanii tofautitofauti akiwemo BurnaBoy,Machel Montano.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Timaya ameweka cover ya Album yake bila kutaja tarehe rasmi ya kuichia sokoni huku ngoma yake na Alikiba ‘Number One’ ikishika nafasi ya tano ndani ya Album hiyo.

https://www.instagram.com/p/BtkgvsoAKTG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=qumrgkjw6lre

Man Walter Achochea Bifu La Diamond na Ali Kiba Liendelee

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo fleva Man Walter ameibuka na kusema kuwa anatamani Bifu kati ya wasanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Ali Kiba lisiishe kabisa.

Man Walter amedai kuwa kuisha kwa bifu kati ya Ali Kiba na Diamond ni sawa na kuua timu za Simba na Yanga na hivyo kusababisha Kulia kaisa upinzani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Mwananchi, Man Walter ambaye ameshafanya kazi na wasanii hao wote wawili katika nyakati tofauti amesema Bifu hilo ndio Linapeleekea muziki kuwa mtamu.

Yaani Hawa wasanii wakipatana ni sawa na kutokuwepo kwa simba na Yanga, hivyo waacheni waendelee hivyo hivyo kwani ndio burudani yenye we”.

Pia Man Walter amefika mbali zaidi na kusema anahisi kabisa kama Bifu hilo litaisha kwa njia moja au nyingine basi ni wazi kabisa muziki wa Bongo fleva utadorora kabisa.

 

Ali Kiba Afunguka Baada Ya Kumzika Baba Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba amefunguka Baada ya kumzika baba yake mzazi aliyefariki siku ya jana.

Baba mzazi wa Ali Kiba na ndugu zake Abdu Kiba na Zabibu Kiba alifanikiwa Dubai siku ya jana kutokana na maradhi ya moyo ambayo yalizuka yanasemekana kumuandama kwa siku nyingi.

Mzee Saleh alizikwa siku ya jana katika makaburi ya Kisutu ambapo Maelfu ya watu wamiminika katika mitaa ya Kariakoo kwa ajili ya kumsindikiza baba mzazi wa msanii Alikiba ambaye amepoteza maisha.

Baada ya kumzika Baba Yake hatimaye Ali Kiba amefungukia msiba huo uliompata yeye na famili yake na kuandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Nawashukuru wote walioshiriki katika mazishi ya Mzee wangu, Na wale ambao hawakujaaliwa pia mimi na familia yangu tumefarijika sana Namuomba Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi na atupe subira katika kipindi hiki kigumu”.

 

Ali Kiba Athibitisha Mofaya Kuanza Kupatikana Jijini Dar

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na kibao cha cha ‘Kadogo’ Ali Kiba ametangaza rasmi kuanza kupatikana kwa kinywaji chake cha Mofaya katika mkoa wa Dar Es Salaam.

Baada ya kinywaji hicho kuhairishwa kuingia sokoni kwa miezi kadhaa tangu mwaka jana mwezi wa nne mpaka hivi karibuni hatimaye kinywaji hicho kimeingia sokoni rasmi.

Ali Kiba alitangaza habari hiyo njema Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika maneno haya:

Sasa Mofaya Energy Drink zimeanza kupatikana jijini Dar es Salaam kwa Mawakala Wakuu (main Distributors) :- :
Unaweza kuwasiliana nao kulingana na maeneo wanayopatikana.
:
Manzese. Magomeni. Ubungo. 0762841318 | 0717009035
:
Tabata. Ukonga. Segerea – 0717646022
:
Mbezi. Tegeta. Kawe. Mwenge. Salasala 0673207256
:
Kariakoo 0656990000| 0754990000| 0715629674
:
Kwa wateja wote wa rejareja mnaweza kuwasiliana na wakala wakuu kwenye number hizo . Mikoani kaeni tayari tunakuja karibuni, tunachukua order kutoka kwa wakala wakuu ( Distributors) kwenye number hiii 0755 333 302“.

 

Ali Kiba Kufanya Kolabo na Staa Kutoka Nigeria

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amethibitisha kufanya kazi na staa wa mkubwa wa muziki kutoka Nigeria anayejulikana Kama Enitimi Alfred Odom ’Timaya’.

Msanii huyo amempa shavu staa wa Bongo fleva Ali Kiba kwenye EP  yake ya ‘Chulo Vibes’ ambayo inategemewa kuingia sokoni ndani ya mwaka huu.

Tanya amethibitisha taarifa hizo ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika maneno haya:

My BROTHER @officialalikiba from TANZANIA came through on the EP. CHULO VIBES is ???”.

Ali Kiba Akumbwa na Tuhuma Nzito Za Wizi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amejikuta katika kitimoto Baada ya Msanii mkongwe wa Bongo fleva Domo Kaya kumtuhumu msanii huyo kwa wizi.

Tuhuma hizo zimekuja Baada ya Ali Kiba kutoa wimbo wake unaofanya vizuri hivi sasa ‘Kadogo’ ambapo ndani ya wimbo huo anasikika akitumia kidokezo cha ‘Yebaba’ ambacho Domokaya amedai amebuni yeye.

Domo Kaya amemuibukia Ali Kiba na kuwataka wasanii wengine wote hasa wapya kwenye tasnia ya Bongo fleva kuwa wabunifu kwenye kazi zao na sio kutegemea ubunifu wa wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Tv, Domo Kaya amesema kuwa haikuwa Vibaya kwa Ali Kiba kutumia neno hilo Lakini kiukweli alitakiwa kumuomba ruhusa kwanza:

Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi Lakini uombe kwa muhusika akupe baraka”.

Wimbo wa Kadogo wa Ali Kiba unaendelea kufanya vizuri na kumpa chati Msanii huyo.

Ali Kiba Adai Anacheza Moira Coastal Union Lakini Halipwi Kitu

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa ingawa amesainiwa kuichezea klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga lakini hawamlipi pesa yoyote.

Miezi michache iliyopita klabu hiyo ilitangaza kumsaini msanii huyo ambaye mbali ya kuimba Lakini pia ana kipaji kikubwa cha kucheza mpira wa miguu.

Lakini Baada ya miezi kupita tangu asainiwe na kutoonekana uwanjani Ali Kiba ameweka wazi kuwa yeye halipwi kuchezea klabu hiyo bali anacheza kwa sababu ya mapenzi aliyonayo kwa mchezo huo na timu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Ali Kiba amedai Kupitia kuchezea timu hiyo ameweza kukitangaza kinywaji chake cha Mo Faya Lakini pia na kuitangaza timu hiyo.

Mimi silipwi, sichezei kwa pesa, nacheza for fun napenda kucheza mpira. Vile vile nimeweza kuitangaza Coastal, nimeitangaza Mofaya zaidi. Vile vile Coastal wanaitangaza Mofaya hiyo nayo imenipa Milage sana kwangu mimi”.

Lakini pia Ali Kiba amesema yupo mbioni kuanza kuuza jezi  za Coastal Union zenye namba yake (7) na zitakuwa na saini yake na kukiingiza kinywaji cha Mo Faya Sokoni.

Ali Kuachia Nyimbo Mbili na Kinywaji Cha Mo Faya Kuingia Sokoni

Staa wa muziki wa Bongo fleva nchini Ali Kiba ameweka wazi mipango yake ya kufungia mwaka 2018 ambapo ametangaza ujio wa nyimbo mbili na kinywaji chake cha Mo Faya kuingia sokoni.

Ali Kiba amesema ngoma hizo ataziachia kwenye shoo yake kubwa ya kufunga mwaka na muimbaji maarufu Afrika, Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ikihairishwa hadi February, 2019.

Kupitia ukurasa wake Instagram, Ali Kiba ameandika maneno haya:

BREAKING & EXCLUSIVE NEWS!!!! Kuelekea kwenye show yangu kubwa ya mwaka #FungaMwakaNaKingKiba tarehe 29 December pale @nextdoor_arena – nitaachia “HITS” zangu mbili kabla mwaka haujaisha pamoja na kuizindua rasmi kinywaji changu cha #MofayaEnergyDrink.

Sema kuna mabadiliko ya tarehe ya show yangu na Mama Yvonne Chaka Chaka pamoja na King Of Best Melodies @bellachristian – kutoka December to February 2019, the month of Love ❤ :
Lakini sasa… siku hiyo ya tarehe 22 December 2018 si ndio FIESTA finale , so I’ll be performing katika Finale ya Msimu wa come back ya Fiesta na wanangu kutoka @kingsmusicrecords :
Na kumalizia mwaka basi tukutane Mombasa on New Year Eve tarehe 31 December —cheers to the New Year Mombasani ??!”.

 

“Ali Kiba Ndio Anatufundisha Muziki”- King’s Music

Wasanii waliosainiwa chini ya label ya Kings Music ambayo inamilikiwa na staa wa Bongo fleva Ali kiba wamefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii huyo ndio anawafundisha muziki.

Kundi hilo la wasanii ambalo linaundwa na wasanii kadhaa Kama Cheed, Killy na K-2GA na akiwemo kaka wa Ali Kiba, Abdu Kiba wamesema Msanii huyo ndio mtu anayewafundisha vitu vingi kuhusu muziki ikiwemo mpangilio wa nani aanze kwenye ngoma zao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati wanatambulisha ngoma yao mpya ‘Toto’, Abdu Kiba  amekiri kuwa kwa ukongwe wa Alikiba kwenye muziki lazima awaongoze.

Anayetupanga ni Alikiba yeye anajua vitu vingi kwenye muziki na ndio maana ana nafasi hiyo ya kushauri nani aanza na nani anafuata na nani atamaliza, kwahiyo Kings Music ni chuo cha muziki”.

Msanii mwingine wa Label hiyo Killy amesema tayari kwa nyimbo mbili ambazo wamezitoa ikiwemo Sina, zimeshawaletea mashabiki wa aina mbalimbali na majina yameanza kuwa makubwa.

“Bora Kufanya Kazi na Diamond Kuliko Alikiba”-Gigy Money

Video vixen maarufu na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford kwa jina la usanii Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ni bora kufanya kazi na Diamond kuliko Ali Kiba.

Gigy Money ambaye Hivi sasa anaonekana akiwa amejiunga pamoja na Kundi zima la Wasafi linaloongozwa na Diamond Platnumz ili kushiriki katika tamasha lao la Wasafi Festival.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Gigy Money ameibuka na kudai kuwa ameona kuna ubora mkubwa wa kufanya kazi na Diamond kuliko kufanya kazi na hasimu Wake Ali Kiba.

Ali Kiba anakunja sana kuliko Diamond  na siku ambayo tulienda kufanya wote shoo Kahama Ali Kiba alinitenga kabisa Backstage”.

Wiki mbili zilizopita Diamond Platnumz na Ali Kiba walifanya shoo zao usiku mmoja ambapo Ali Kiba alipiga shoo mkoani Shinyanga/Kahama na Diamond alipiga shoo yake mkoani Mtwara.

Ali Kiba Kupiga Shoo na Yvonne Chakachaka

Mwanamuziki katika tasnia ya Bongo movie Ali Kiba amefunguka kwamba atafanya shoo mbili za kufanga mwaka jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa na muimbaji mkongwe, Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Ali Kiba amesema atafanya shoo hizo kabla ya mwaka haujaisha:

Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika Funga mwaka na King Kiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya Desemba 2018.

1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es Salaam 22. December. 2018. Halafu 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018.”

Hii haikuwa mara ya kwanza Msanii kwa Ali Kiba kumleta Yvonne Chakachaka na kupiga naye shoo, ameshawahi kumleta na Kuperfom naye katika siku ya wanawake.

“Mimi na Mke Wangu Amina Tunatarajia Kupata Mtoto Mwakani”-Ali Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke Wake Amina Khaleef wanatarajia kupata Mtoto wao kwanza mwakani.

Baada ya fununu za muda mrefu hatimaye Ali Kiba ameweka wazi kuwa mke Wake Amina ni mjamzito na wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza mwakani Baada ya kufunga ndoa mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Radio Jambo ya Nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA , Ali Kiba alifunguka haya kuhusu ujauzito wa mke wake:

Katika dini yetu tunaamini ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise, atakua Mtoto wangu wa nne” 

Lakini pia Kiba ameweka wazi kuwa huyu atakuwa ni Mtoto Wake wa nne kwani tayari ana Watoto watatu na wanawake wengine aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano siku za nyuma.

Ali Kiba Ndiye Msanii Pekee Asiyehitaji Kiki Wala Matusi Kujaza Shoo-Mange Kimambi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mwanamama Mange Kimambi ameibuka na kumpigia  saluti staa wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai kuwa hakuna Kama yeye Bongo nzima.

Mange ameongea hayo Baada ya shoo iliyofanyika Wiki iliyopita mjini Kahama kujaza nyomi la ajabu pamoja na kwamba Ali Kiba hakuipigia promo shoo Ile Kama ilivyokuwa kwa Wasafi Festival na Fiesta.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

Ujumbe huo umeonekana Kama Dongo kwa mpinzani wa Ali Kiba Diamond Platnumz na tamasha lake la Wasafi Festival ambao walionekana kutoa promo ya nguvu Lakini pia Fiesta ambayo ilikuwa katika majobizano na Wasafi.

WCB Watangaza Mdhamini Wa Wasafi Festival, Ali Kiba Atupwa Kule

Msanii wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ametangaza kinywaji rasmi kitakacho dhamini Tamasha la Wasafi Festival linalotegemewa kuanza tarehe 24 November.

Mpaka siku ya jana ilikuwa inaaminika kwamba Ali Kiba kupitia kinywaji chake cha Mo Faya ndio watakuwa wadhamini rasmi wa Wasafi Festival hii ni Baada ya Diamond kukubali mwaliko wa Ali Kiba kudhamini tamasha hilo.

Siku mbili zilizopita Diamond alitangaza kuwa kinywaji Fulani ndio kitadhimini kinywaji hiko ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika:

Management imenambia kuna Kinywaji kesho kinaingia Rasmi onboard kama Mdhamini Mkuu wa #WasafiFestival2018 …Labda nikitaarifu tu kuwa kijiandae kutengeneza Storck za kutosha maana sio tu kunywewa, bali hata wengine watataka kukiogea kwa promo ntayokipa…. “.

Lakini jambo hilo limekuwa tofauti kwani usiku wa jana Diamond ametangaza kuwa kinywaji rasmi kutakacho dhamini Tamasha la Wasafi Festival ni Pepsi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqNo1pehxso/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=irbye9kwk5xm

Mpaka sasa bado haijajulikana Kama Ali Kiba Kupitia Mo Faya bado atadhamini tamasha hilo au ndio basi katupwa kule lakini hawajatoa mrejesho wowote.

Zabibu Kiba Afunguka Kuikacha Ndoa Yake Sauzi na Kurudi Bongo

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Ali Kiba, Zabibu Kiba amefunguka na kuanika sababu za kumuacha mume wake Abdi Banda nchini Afrika ya Kusini na kuamua kurudi Tanzania mwenyewe.

Zabibu na mume wake Abdi Banda walihamia SA ambako anacheza soka la kulipwa, miezi michache iliyopita Mara tu Baada ya kufunga ndoa lakini ghafla Zabibu ameonekana kurudi Tanzania na kumuacha mumewe SA.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Vibes, Zabibu alisema amekuwa akipata maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali kwamba imekuwaje amemwacha mumewe Afrika Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

Sioni kama kuna tatizo mimi kurudi mapema Bongo maana ndiyo nyumbani kwa wazazi ila sababu kubwa ni kwamba Kusini na kurudi Bongo ambapo alisema amerudi kwa sababu kibali cha kuishi nchini humo ‘viza’ kiliisha muda wake.

Viza yangu ilikuwa hainiruhusu kuendelea kukaa Afrika Kusini kwa muda mrefu kwa hiyo kuna mambo nimerudi kuyaweka sawa kisha nitarudi tena kwa mume wangu kuendeleza mahaba kama kawaida”.