Enock Bella Amtolea Povu Beka Flavour

Mwanamuziki Enock Bela amejikuta akimtolea povu msanii mwenzake Beka Flavour na kudai kuwa msanii huyo hawezi kumsaiida kitu chochote kwa sababu wote wapo katika level moja hivyo hana uwezo huo.

Enock anasema kuwa hata akiangalia haoni msaada gani beka anaweza kumpa kwa kumsaidia kama ambavyo amekuwa akijinadi katika interviews kuhusu swala la yeye kumsaidia msanii mwenzake zaidi anaona kama vile anatafuta kiki.

simshangai beka kuzngumza hivyo maana naona kama vile na yeye anatafuta ugali tu,sidhani kama anaweza kunipa msaada mkubwa wowte katika muziki ili niweze ku-survive kama anavyosema  kwa sababu mimi na yeye tunalingana.Vitu vingine watu wapo kwa ajili ya kujitafutia faida tu  na kuongea mambo mabayo hayawezi kufanyika.

Enock pia anasema kuwa hakuna ukweli owowte kuwa amefulia  kwa sababu anangoma nyingi sana zaidi ya album ambazo ataanza kuzitoa hivi karibuni.Enock anasema  hawezi kuacha mufanya muziki wa kwa sababu muziki ndio maisha yake.

Aslay Kumsaidia Enock Bella Kimuziki Kwa Kolabo

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kumshika mkono na kumsaidia Msanii mwenzake kutoka Yamoto Band Enock Bella.

Aslay alikuwa mmoja wa wasanii waliounda kundi la Yamoto Band lakini baada ya kundi hilo kuvunjika miaka michache iliyopita kila msanii alishika njia yake.

Baada ya kila msanii kuendelea na kazi zake binafsi Aslay alionekana kupata mafanikio makubwa zaidi lakini pamoja na Beka Flavor ambaye pia amekuwa anafanya vyema na Mbosso aliyesainiwa WCB amekuwa anafanya vizuri pia.

Lakini Enock Bella aliyekuwa maarufu kwa kuimba bezi kwenye Yamoto amekuwa akisuasua tofauti kabisa na wenzake kwani ameshatoa nyimbo kadhaa ambazo hazijafanya vizuri kabisa.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Aslay amefunguka na kukiri kuwa kuna jitihada anafanya kwa ajili ya kumsaidia msanii mwenzake Ikiwa ni pamoja na kolabo hivi karibuni:

Ndio Enock Bella yupo na ninaongea naye na pia Bado Yupo Kwenye grupu moja kwaiyo bado tuna ukaribu na kuna jitihada tunafanya kwaiyo inshallah siku is nyingi mashabiki wataona kitu kutoka kwetu ingawa siwezi nikakiongelea sana”.

Enock Bella alitangaza kusainiwa kwenye label iliyopo nchini Uganda mwaka jana mwishoni lakini baada ya muda mfupi akatangaza kujitoa.

Enock Bella Akiri Kufelishwa Kwa Kukosa Uongozi Wa Maana

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyejipatia umaarufu katika kundi la Yamoto Band Enock Bella amefunguka na kusema jambo pekee linalopelekea kusua sua Kwenye muziki ni kwa ajili ya kukosa uongozi wa maana.

Enock Bella amekuwa ndio msanii pekee kutoka katika kundi la Yamoto ambaye amekosa mafanikio kulinganisha na waaanii wenzake kama Aslay, Beka Flavor na Mbosso ambao wamepata mafanikio makubwa.

Bella anafunguka na kusema sababu pekee inayomfanya mpaka hivi sasa anasua sua hana ngoma za kutosha ni kukosa management ya maana ya kumsimamia ipasavyo.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Enock Bella amfunguka haya kuhusu suala hilo:

Mara nyingi kinachonifelisha kama Enock ni kuwa active katika kazi zake kwa sababu ya menejimenti ninazozipata mara nyingi huwa mbovu.

Yaani nafesli sana katika menejimenti lakini nikipata menejimenti inayojitambua nakujua muziki ni nini na dhamani ya msanii ipo wapi wanaweza wakashangaa Watanzania”.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya kuachana na na menejimeti iliyokuwa inamsimamia kutoka nchini Burundi.

Enock Bella Kulikwaa Dili Kubwa Burundi.

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambae hivi sasa anatamba na kibao chake kikubwa kama Sauda na bado kidogo amefanikiwa kulamba dili kuwa na moja ya kampuni kubwa nchini burundi kwa kutaka kusimamia kazi zake za kimuziki.

Enock bella ambae tangu kufa kwa band ya  ya moto amekuwa akifanya kazi mwenyewe huku akiwa ni moja ya wasanii waliokuwa wakisema kila siku kuwa wanatamani sana uongozi wa Ya Moto uendele kuwasimamia .

Wakati wa kusainishana kwa mkataba huo kati ayke na kampuni hiyo inayojulikana kama  chakor music group, meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa lengo lao kubwa ni kutaka ku-push muziki wa tanzania kufanya vizuri na kuendelea kukua .

Tumeingia Tanzania kusaka vipaji vya muziki na tumekuja tukaona kuwa Enock Bella  anauwezo mkubwa na kazi zake tumezifuatilia tumeziona  ana sauti nzuri, anajua kuimba na  ana muziki mzuri.Tunaamini kuwa tutafika nae mbali kwa sababu  ana radha nzuri na tofauti ya muziki wake  katika kuimba na kutunga pia.

Kwa upande wa Enock pia amefunguka na kusema kuwa ni faraja kubwa tena hasa baada ya kuvunjika kwa kundi la ya moto.

Sikujua kama kazi ninayoyafanya inapenya hadi mbali kiasi hicho.namshukuru mungu kwa chakor kuniona na pia  kwa kupata management yangu mpya.naamini kuwa sasa muziki wangu utafika mbali zaidi  na nitafanya vizuri kulio hata vile nilivyokuwa nikifanya mwanzo

Ninai-miss Menejiment Yangu ya Zamani:-Enock Bella

Msanii kutoa kundi la Ya moto Band Enock Bella amefunguka na kuongelea kwa jinsi gani ambavyo anatamani sana menejimenti yake ya zamani ambayo ilikuwa ikiwamiliki wasanii wote wanne wa kundi la Ya Moto band kuendelea kuwaongoza na kuwa natamani sana kundi lao lingeendelea kufanya kazi pamoja kwa sababu wametoka mbali.

Enock Bella ambae kwa sasa ameachia ngoma yake mpya ya ngoja kidogo anasema kuwa pamoja na kuwa alikaaa kimya kwa muda mrefu  lakini anashukuru Mungu kwa sababu mashabiki zake wamempokea vizuri na ngoma yake inaonekana kufanya vizuri.

mapokezi ya wimbo wangu yamekuwa mazuri sana,mara ya kwanza nilijua sauti yangu ni ya kawaida sana kwaio nyimbo haitakuwa nzuri lakini kumbe sio.wengine walisema kuwa kwanini nipo kimya, labda nimekufa kimuziki au nilikuwa nabebwa sana na kundi , nilikuwa natembelea nyota lakini sio kweli.

kwa sasa nina fight mwenyewe wala sina uongozi kwa sababu wao wanaokuja na kufanya  kazi na mimi lakini wamekuwa wanashindwa makubaliano yenu, kwaio hakija mtu tukaelewana vizuri basi tutafanya kazi.

ninaimiss sana menejiment yangu ya zamani, ningependa sana ya moto band iendelee kuwepo kwa sababu imenifundisha vitu vingi, ndo imenitengeneza mimi, imenifanya niwe hapa niwe hapa.

Ya moto band ilikuwa ikifanya vizuri sana katika muziki lakini ndoto za vijana hawa wanne zilikuja kuvunjika baada ya kundi hili kusambaratika huku kukiwa na sababu zisizoeleweka

 

Enock Bella Amefungukia Tuhuma za Aslay Kuiba Daftari La Nyimbo za Yamoto Band

Aslay ni mmoja Kati ya wasanii anayefanya vizuri sana kwa hivi sasa mafanikio anayopata ni wasanii wachache wanaoweza kufikia ukitegemea kwa mtindo wake wa kutoa nyimbo kila baada ya muda mfupi.

Lakini mafanikio Kama haya lazima yaje na changamoto kadhaa kwa upande wa Aslay changamoto hiyo ni bendi yake ya zamani ya Yamoto Band iliyovunjika miezi michache iliyopita na kupelekea vijana waliokuwa wanaunda bendi hiyo kutengana.

Baada ya kuvunjika kwa bendi hiyo na Aslay kama solo artist, maneno maneno yalianza chini kwa chini ambapo moja kati ya habari zilizosambazwa na watu wasiojulikana na kushika kasi ya ajabu hivi sasa za kumchafua Aslay ni kuwa kitu pekee kinachompa Aslay mafanikio baada ya kuondoka Yamoto na kuwa na nyimbo nzuri kila siku ni kwa sababu wakati anaondoka Yamoto band aliiba daftari la nyimbo la Yamoto ambalo alishirikiana na wenzake kuandika.

Enock Bell ambaye alikuwa kwenye bendi ya Yamoto na Aslay amefungukia tuhuma hizo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha  East Africa:

Unajua uzuri nchi yetu haijamkataza mtu kuongea kila mtu akijisikia kuongea anaongea chochote anachoweza kukifikiria lakini kiukweli ni kuwa Aslay bahati nzuri Mwenyezi Mungu kamjalia kitu chake cha kipekee ni msanii ambaye unaweza ukamwekea biti tu akafree style nyimbo nzima kwaiyo Ana uwezo wa kuandika nymbo hata nne kwa siku mbili anaweza kupangilia mashairi yake vizuri kwa muda mfupi na yakawa makali kwaiyo sio kweli kuwa aliiba daftari la Yamoto kwanza hatukuwa na daftari lolote”.

Enock alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa sababu pekee watu wanasambaza habari hizo ni baada ya kuona Aslay anatoa nyimbo kali kila siku lakini amedai hicho ni kipaji chake tu na sio wizi.

 

Enock Bella Azidi Kujitamba Kwa Sauti Yake Ya Kipekee

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Enock Bella amejivunia na kudai sauti yake ya kipekee anaweza kuitumia vyovyote atakavyo.

Enock Bella aliyejipatia umaarufu kutoka katika kundi maarufu la Yamoto Band lililovunjika miezi michache iliyopita. Kwenye kundi hilo alikuwa na wanamuziki wenzake mbali mbali kama vile Aslay, Beka flavour ambao tofauti take Kati ya hawa wotee ni sauti zao Enock alijizolea umaarufu kutokana na sauti yake nzito na bezi.

Kwenye mahojiano na kituo cha redio aliyofanya hivi karibuni Enock alisisitiza kuwa anaamini kuwa sauti yake inamsaidia kwa sababu ya upekee wake na pia amesisitiza kuwa Sababu tu ya bezi lake haimaanisha inamzuia kuimba kama wasanii wengine:

Sauti yangu Ina uwezo wa kufanya kitu chochote, halafu nimejua kugundua kwamba kupitia sauti yangu ya bezi naweza kutengeneza mziki mzuri ambao unaishi ndio maana nikaweza kufanya kitu kikubwa kama hiki”.

Alipokuwa kwenye kikundi cha Yamoto Enock alikuwa anaimba baadhi tu ya sehemu zilizohitaji sauti kubwa tofauti na wasanii wenzake waliokuwa wanaweza kuimba sehemu yoyote. Lakini Enock Bella alikataa tuhuma hizo na kudai utofauti wa sauti yake ndio utafanya afanye mziki mzuri zaidi, hivi sasa Enock Bella anatamba na wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘Sauda’.

Enock Bella Alitafuta ‘kiki’ Kwa Kudanganya Ameoa

Msanii wa Bongo fleva Enock Bella aliyepatia umaarufu kupitia katika kundi la Yamoto Band kutokana na kuwa na sauti nzito kabisa ametuhumiwa kwa kitendo chake cha kudanganya mashabiki zake ameoa na kusambaza picha za harusi mtandaoni ilimradi tu apate kiki.

Imekuwa ni jambo la kawaida sasa kwa wasanii wa Bongo fleva na Bongo movie kutengeneza kitu kinachoitwa ‘kiki’ ambacho kitu kinachotokea ni wasanii hawa hutengeneza skendo feki ambazo ni mbali na muziki wao na hivyo kuwavuta watu au mashabiki na kisha kutoa kazi zao ili zipate media attention. Wasanii hawa hutangaza ndoa feki, hudanganya kuwa ni wajawazito na hata hudanganya kuwa wana uhusiano na mastaa wenzao ilimradi tu watu wavutiwe.

Sasa msanii Enock Bella aliyesifika kwa kuimba kwa bezi alipokuwa Yamoto, ilidaiwa kuwa baada ya kundi hilo kuvunjika alitoa nyimbo ambayo haikufanya vizuri hivyo alimua kuwa atakapotoa nyimbo yake ya pili atengeneze kiki hiyo.

 

Alipohojiwa na kituo cha televisheni cha East Africa Enock Bella alifunguka yafuatayo kuhusiana na tuhuma hizo;

Unajua zile picha za harusi zilizo trend zilikuwa ni project tu ilibidi zitumike kwenye video ya Sauda lakini baadae zile picha zilitolewa kwa maana zisitumike tena maana director alisema tubadilishe kwa sababu wasanii wengi walishatumia harusi kwenye video zao ili kuleta utofauti ilikuwa lazima tutafute utofauti fulani kwaiyo baadaye zile picha zikawepo tu bila kazi kwaiyo watu wangu wa karibu wakanishauri zile picha tuziachie tu ili ziwe za kutafuta attention ya watu”.

Pia Enock Bella amekiri kuwa hajafunga ndoa bali zile picha zilitumika kwa ajili ya kutafutia kiki ili nyimbo yake ipae zaidi.

Msitegemee Kuiona Yamoto Band Kama Zamani- Enock Bella

Msanii kutoka katika kundi lililovunjika la Yamoto Band amefunguka na kudai kuwa mashabiki wao wasitegemee kuwaona wanakundi hao wanafanya kazi pamoja muda wowote kuanzia sasa.

Enock Bella alipokuwa anafanya mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa amefunguka kuwa pamoja na watu wengi kudai kuwa bendi hiyo imekufa lakini yeye hana taarifa hizo bali anachojua kuwa wamepeana nafasi ili kila msanii aweze kufanya kazi kivyake kwanza ila endapo kama kuna siku akiitwa au wakihitajika kupiga shoo kwa pamoja basi hatakuwa na neno bali ni kwenda na kushiriki na wenziye.

Enock Bella ambaye kwa sasa anafanya muziki wake kama msanii wa kujitegemea ameweka wazi kuwa kwa sasa kundi hilo kurudi kama zamani itakuwa ngumu ila kama ikitokeaa kufanya kazi ya mara moja basi watafanya makubaliano fulani ila kwa sasa kila msanii anafanya vizuri mwenyewe;

Sifikirii kwa sasa hivi labda kwa baadae ila kwa sasa kuiona Yamoto Band kama zamani kwa muda huu ambao tunao kwa sasa kusema kweli nitadanganya ila kwa baadae kinaweza kutokea chochote kile ila sio kwa sasa ila baadae naomba tuamini kuwa inaweza ikawezekana”.

Enock Bella ambaye ametoa wimb wake wa kwanza tangu ahame ya Yamoto ameonekana yupo mbali kidogo kulinganisha na wenzake kama Aslay ambaye anafanya vizuri na ametoa jumla ya nyimbo kumi na tatu tangu ahame bendi hiyo, pia wasanii wengine wanaofanya vizuri ni Becka Flavour ambaye anazidi kukimbiza katika jukwaa la Fiesta.