Mpenzi Wa Hamisa Atajwa Kuwa Mcheza Mpira Wa Kikapu Nchini Marekani

Mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto alimuweka wazi Mpenzi Wake Mwishoni mwa wiki iliyopita Kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwa taarifa zaidi kutoka kwenye mitandao ya kijamii zinasema kijana huyo mtanashati anaitwa Josh Adeyeye ambaye Ana asili ya Nigeria lakini ni mzaliwa wa Marekani.

Josh anatajwa kuwa na umri wa miaka 25 na urefu wa futi 6.5 Lakini pia ni mchezaji wa Basketball na anatajwa kuwahi kucheza katika timu za NBA ingawa hivi sasa ni Free Agent.

Kwenye NBA amechezea timu Kama vile Dolphins, Maine Red claws.

Hamisa Mobetto Afunguka Haya Kuhusu Mpenzi Wake Mpya

Mwanamitindo na msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Hamisa Mobetto amemuanika mpenzi wake mpya Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuthibitisha mahusiano.

Baada ya tetesi kusambaa kwa muda wa siku kadhaa hatimaye Mobetto amefunguka mahusiano yake na Mwanaume ambaye ameweka Kupitia mitandao ya

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Hamisa ameweka picha yake akiwa na mwanaume huyo ambaye bado hajajulikana jina mpaka hivi sasa na kusindikiza kwa maneno yaliyosomeka:

Roho mkalia moyo ?…….. #Mymirindanyeusi #Mybiggiey #Naurefuwanguwotehapanimekuwamfupi ??“.

https://www.instagram.com/p/Bp8sjX-BUUG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=fgf4pw6gsl98

 

Hamisa Mobetto Amuanika Mpenzi Wake Mpya (video)

Mwanamitindo na msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto kwa Mara ya kwanza ameanika video zinazomuonyesha akiwa na mwanaume ambaye anasemekana kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Hamisa ambaye hivi sasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ameonekana kupata na penzi jipya kwani ameweka video zinazomuonyesha akiwa na Kijana mwingine huku wakiwa wameshikana mikono na hata baadhi ya video zimewaonyesha wakiwa wamebebana.

https://www.instagram.com/p/Bp6KT4YB095/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=s07nf6psfruv

Mpaka sasa Hamisa hajatoa tamko lolote kuhusu uhusiano wake na  kijana huyo lakini picha na video zimejieleza kuwa inawezekana akawa mtu wa kuziba pengo la Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Mama Mobetto Afungukia Penzi Jipya la Hamisa

Mama Mzazi wa mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga maarufu Kama Mama Mobetto amefungukia madai yaliyosambaa kwenye mitandao kumuhusu mwanaye Hamisa.

Mama Mobetto amefungukia madai kuwa mwanaye Hamisa Ana mwanaume mpya ambaye siyo Raia wa Tanzania na kusema kuwa, yeye kama mama hana taarifa ya kuwa mtoto wake huyo ana mwanaume mwingine kama inavyoelezwa mitandaoni.

Katika mahojiano yake na gazeti la Ijumaa Wikienda, Mama Mobetto ambaye ilidaiwa kuwa aliwahi kumweka mwanaume huyo kwenye ‘profile’ yake na kuandika kuwa anampenda mkwe wake huyo, alikana madai hayo. Alisema siku zote huwezi kuwazuia binadamu wakiamua kusema mambo yao hivyo naye hajali maneno ya watu.

Mimi kwa kweli sijawahi kumweka huyo mtu, lakini pia unajua kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii kila mtu anaongea lake. Kwa hiyo kama mtu huwaelewi, unaweza kupata tabu sana”.

Mambo ya mkwe yametoka wapi tena? Ninachojua sasa hivi Hamisa anapiga kazi tu na si vitu vinginevyo. Kwa sasa sihitaji mkwe wala sina maana siku akiwepo kila mtu atamjua tu, sidhani kama hiyo itakuwa ni siri”.

Tangu Hamisa aachane na Baba watoto wake Diamond Platnumz mapema mwaka huu amesema Hana mpango wa kujiingiza kwenye Mapenzi kwa sasa Bali anataka apige kazi ili aweze kuwalea watoto wake.

Maimartha- Siwezi Kuyumbishwa na Maneno Ya Watu

Mtangazaji mkongwe Maimartha wa Jesse ameibuka na kudai Kuwa hawezi kuyumbishwa na maneno ya watu ambao wamekuwa wakimsema na kumtukana kutokana na yeye kuwa mmbea kwenye mitandao ya kijamii kwani ndio kazi inayomuweka mjini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi, Mai alisema kuwa kila akitupia habari yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram watu wanamtukana na kumuita m’mbea, wengine wanadiriki kumwambia auze biashara zake lakini wanasahau kuwa kazi hiyo ameisomea na anahabarisha kama wengine wanavyohabarisha.

Unajua utangazaji ni sawa na umbea, mimi nahabarisha watu kwa staili yangu na sitokoma kazi hii labda watu wafiche mambo yao lakini hivi hivi sikomi, ni kazi kama kazi nyingine”.

Mai amemwaga povu hilo baada ya siku za hivi karibuni kuingia matatizoni na baadhi ya mashabiki wa wasanii mbali mbali hasa Hamisa Mobetto baada ya kuivalia njuga ishu ya Hamisa kuwa na mpenzi mpya.

“Hamisa Anapata Mafanikio Baada Ya Kuachana na Diamond”-Mama Mobetto

Mama mzazi wa mwanamitindo na msanii Hamisa Mobetto anayejulikana kama Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa kilichokuwa kinamkwamisha mwanaye ni mapenzi lakini baada ya kuachana nayo mambo yanamnyookea.

Hamisa Mobetto aliachana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz ,miezi michache iliyopita na tangia hapo amekuwa akipata madili makubwa kama ubalozi wa makampuni na hata kutoa wimbo wake wa kwanza unaozidi kufanya vizuri kwenye Youtube.

Siku chache baada ya Hamisa kuonekana akifanya shoo nchini Marekani mama Mobetto ameibuka na kuweka wazi kuwa mwanaye amefanikiwa baada ya kuyaeweka kando mambo ya mapenzi yaliyokuwa yanampotezea muda na kuamua kupiga kazi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mama Mobetto amesema siri kubwa ya mwanaye kuonekana mambo kumwendea vizuri baada tu ya kuachana na Diamond ni kwa sababu amekuwa msikivu kwa kila jambo analomwelekeza.
Aliendelea kusema kwamba amekuwa akimshauri na kumwelekeza Mobeto mambo mengi sana yanayohusiana na maisha na anamshukuru Mungu kwani kwa sasa amekuwa ni mtoto msikivu sana na ameona faida yake kwani amekuwa akipata kazi mbalimbali nje ya nchi.

Namshukuru Mungu sana kwa kila jambo kwani mwanangu baada ya kuachana na ishu za mapenzi amekuwa msikivu, anasikiliza na kuzingatia kile ninachomwambia kama mama yake na ndiyo maana anafanikiwa na anazidi kutusua kila siku”.

 

Hamisa Mobetto Anunua Gari Jipya (video)

Mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amezidi kung’aa kwani ameanika gari lake jipya alilonunua katika siku za hivi karibuni.

Kupitia ukuarasa wake wa snapchat, Hamisa amejirekodi akipiga picha na kuonyesha gari lake jipya ambalo halina hata palte number ambalo ni aina ya Toyota Vanguard.

https://www.instagram.com/p/Bpi8AonlKm1/?utm_source=ig_web_copy_link

Hamisa amezidi kung’aa kimaisha kwani hivi sasa yupo chini Marekani kwa ajili ya show akiwa na msanii muimbaji Christian Bella.

 

Mobetto Apata VISA Ya Marekani Baada Ya Zari na Wema Kupigwa Chini

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva  Hamisa Mobetto amewabwaga mahasimu wake wakubwa Zari The Bosslady na Wema Sepetu na Kufanikiwa kupata visa ya kwenda Marekani.

Hamisa amewaacha mbali Zari na Wema baada ya kujipatia VISA yake ya kuingia nchini Marekani kwa ajili ya kupiga kazi.

Miezi michache iliyopita Wema Sepetu alitangaza kuwa atakuwa nchini Marekani kwa ajili ya kufanya appearance Kwenye Tanzania day lakini hilo halikufanikiwa baada ya kunyimwa VISA ya kwenda nchini humo.

Lakini vivyo hivyo ilikuwa kwa Zari ambaye Miezi michache nyuma alitangaza kuwapeleka Tiffah na Nillan kwa Diamond aliyekuwa nchini Marekani Kwenye ‘A Boy from Tandale Tour’ lakini baadae ilishindikana baada ya Zari kunyimwa VISA ya kuingia nchini Marekani.

Hamisa ameonekana kuwashinda mahasimu wake hao kwani hivi sasa yupo njiani kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya appearance katika miji mbali mbali.

 

 

 

Mbasha Akiri Kumkubali Wema, Amponda Mobetto

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ameibuka na kudai Wema Sepetu ndio Tanzania Sweetheart pekeee na sio vinginevyo.

Emanuel amesema hayo baada ya kuibuka kwa mjadala mzito katika siku za hivi Karibuni baada ya mashabiki kutaka kumvua cheo cha Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu na kumvalisha Hamisa Mobetto.

Katika Interview yake na Gazeti la Ijumaa, Mbasha alisema kuwa kwa upande wake, Tanzania Sweetheart kati ya warembo hao wawili, ni Wema kwani ndiye anayestahili na hilo halina hata mjadala.

Hilo jina linamfaa aliyekuwa nalo tangu zamani (Wema), kwani ndiye aliyepewa hilo jina, kwa hivyo acha tu aendelee nalo kwa sababu ndio linampendezea”.

Siku za hivi Karibuni Mbasha aliingia katika vita kali na mashabiki wa Mobetto baada ya kuweka picha yake akiwa anapaa na ungo kufuatia tuhuma za uchawi.

Wema Sepetu- Nina Kitu Cha Ziada Ambacho Wengine Hawana

Muigizaji wa Bongo movie Madam Wema Sepetu ameibuka tena katika jitihada za kulitetea Jina lake la Tanzania Sweetheart na kusema ana kitu ambacho wengine hawana.

Kwa wiki kadhaa sasa Wema amekuwa Kwenye vita kali katika harakati za kutetea Jina lake la Tanzania Sweetheart ambapo hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashabiki kudai hana vigezo vya Jina hilo Tena na kutaka Hamisa kuwa Tanzania Sweetheart.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la  Risasi Jumamosi, Wema amesema  hawezi kustaafu kutumia jina hilo kwa sababu wakati anapewa na mashabiki wake wa jijini Arusha, hakuambiwa kama kuna kustaafu hivyo jina hilo ni lake na ataendelea kulitumia.

Kwani kuna kustaafu? Sasa nani mwingine atumie jina hilo wakati Tanzania Sweetheart ni mmoja tu? Kwanza akianza kulitumia mtu mwingine mashabiki watakubali? Kila kitu kinaenda na mazoea, watu wamenizoea mimi na nitabaki kuwa mimi tu na hakuna kama mimi“.

 

“Sina Bifu na Mobetto Lakini Nampenda Wema”-Diana Kimary

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary amefunguka na kudai hana bifu wala hamchukii Hamisa Mobetto ila tu anampenda sana Wema Sepetu.

Diana Kimary ambaye siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na Ukaribu sana na Wema ameweka wazi kuwa watu wengi wanadhani yeye ana bifu na Mobetto kwa sababu yuko na Wema jambo hilo sio la kweli.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Diana ambaye hivi sasa yupo karibu na Wema alisema watu wengi wanajua ana bifu na Mobeto, lakini wanashindwa kuelewa anapoweka vitu vyake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram havilengi kumsema mtu.

Simchukii na wala sina tatizo na Hamisa (Mobeto)kama watu wanavyotengeneza kwenye mitandao, bali wakiona namuweka Wema ni kwa vile nina mapenzi kama yote kwake pia hata nikiandika ujumbe simsemi mtu”.

Wema na Mobetto wametajwa kuingia katika bifu zito kwa sababu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ ambapo mashabiki wamedai wamemvua Jina hilo Wema na kumvalisha Mobetto jambo ambalo Wema amepingana nalo.

Rc Makonda Amtetea Wema Kuwa Tanzania Sweetheart Amtaka Mobetto Awe Buguruni Sweetheart

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Mh. Paul Makonda ameibuka na kumkingia kifua Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu na kusema analistahili Jina la Tanzania Sweetheart na sio Hamisa Mobetto.

Kwa wiki chache zilizopita Wema Sepetu amekuwa akifanya interviews mbali mbali na amekuwa akibainisha kuwa yeye ndiye Tanzania Sweetheart na sio Mobetto kama mashabiki zake ambavyo wamekuwa wakilazimisha.

Siku chache zilizopita akiwa katika Birthday Bash ya Wema iliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City, Makonda aliweka wazi kuwa Wema ndiye Tanzania Sweetheart pekee ila kama wengine wanalitaka hilo Jina wanaweza kuwa Buguruni Sweetheart.

Wema ni Tanzania Sweetheart kwa sababu kuna vigezo, na kwanza hujiiti Jina mwenyewe, watu wanakupa Jina kama alivyopewa na Baba yake na mama yake Jina Tanzania Sweetheart wengine wanaweza kuwa Buguruni Sweetheart sio dhambi au Manzese Sweetheart”.

Vita kali ya Jina la Tanzania Sweetheart ilianza baada ya mashabiki Mtandaoni kusema wanamvua Jina hilo Wema na kumpa Mobetto kwa sababu Wena amepoteza umaarufu wake na kuwachukiza mashabiki zake kwa matendo yake ya mitandaoni.

Diamond Alitaka Kunioa Mke Wa Pili, Nilikuwa Tayari- Hamisa

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa amekiri kuwa wakati anaanzisha Mahusiano na Diamond, tayari Diamond alikuwa Kwenye Mahusiano na Zari na walikuwa wamezaa watoto.

Kwenye Interview yake aliyofanya akiwa nchini Kenya, Mobetto amefunguka haya:

Wakati nakutana na Diamond nilijua kuna Zari na nilimuuliza, akasema mimi ni muislam na uwezo wa kuoa hata wanawake wawili,” alisema Mobetto. “Na mimi nipoo tayari hata kama ningekuwa nimeolewa halafu mume wangu anataka kuoa mke wa pili ningemruhusu“.

Hamisa alibeba mimba ya Diamond wakati akiwa Kwenye Mahusiano na Zari jambo lililoleta mtafaruku na kupelekea kuachana kwao mwishowe.

Baada ya Diamond kuachana na Zari alikuwa Kwenye Mahusiano na Mobetto Tena lakini Mahusiano hayo yaliingia doa kwani Hamisa ameishia Kwenye ugomvi mkubwa na Familia na Diamond na kuishia kuachana naye.

Wema Sepetu- Hamisa Hawezi Kuwa Tanzania Sweetheart, Ni Mimi Peke Yangu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka n kumnyooshea maelezo juu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ na kusisitiza pekee yake anaweza kuwa.

Kwenye mitandao ya kijamii Kumekuwa na mvutano kati ya mashabiki wa Wema na mashabiki wa Hamisa Mobetto ambapo wamekuwa wakigombani Jina la Tanzania Sweetheart na kila mmoja kudai staa wake anastahili kuitwa jina hilo.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Wema Sepetu Msanii wa filamu Wema Sepetu aka TZ Sweetheart amedai haoni sababu ya watu wengine kutaka kutumia jina hilo kwa kuwa yeye amekuwa akilitumia kwa muda mrefu baada ya kupewa na mashabiki wake.

Mimi Jina langu ni Wema, Tanzania Sweetheart ni Jina ambalo nimepewa na mashabiki zangu kutokana na mapenzi yao kwangu kwa hiyo hatuwezi kuwa Ma- Tanzania Sweetheart wawili kila mtu Awe na Jina lake halafu kuna Tanzania Sweetheart mmoja tu mbona majina yako mengi jamani”.

Wema na Hamisa wamekuwa Kwenye bifu  ya muda mrefu huku Wema akimtuhumu Hamisa kwa kumsema vibaya kwa watu.

Mange Kimambi Amshauri Hamisa Asirudi Kwa Diamond Adai Ana Gundu

Mwanaharakati wa Mambo ya siasa Mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa Mobetto asithubutu kurudi tena  kwa mzazi mwenzake Diamond Platnumz kwa madai kuwa ana gundu.

Hamisa aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz waliachana Mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa.

Lakini baada ya kuachana Hamisa aliingia kwenye mgogoro na Familia nzima ya Diamond ambao waliishia kumtangaza kama mchawi mara baada ya kuwaendea kwa mganga.

Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa asirudiane Tena na Diamond kwa madai kuwa familia nzima ya Diamond ilikuwa inampa gundu tu kwani sasahivi tangu ameachana nao amekuwa akipata madili mengi ya ubalozi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BoGFxI6larV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1o9n4uzj4l67d

Mama Mobetto Afungukia Wimbo Wa Mwanaye

Mama mzazi wa Mwanamitindo Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga amefunguka kuhusu wimbo mpyawa binti yake ‘Madam Hero’ ambao ameshitiki Kwenye video.

Mama Mobetto amefunguka kuwa ameamua kuigiza kama mama kwenye wimbo wa kwanza wa mwanaye huyo wa Madam Hero kwa ajili ya kuweka baraka zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  Ijumaa Wikienda, Mama Mobetto amesema kwamba hakuna jambo linalompa faraja kama kuona wimbo huo wa mwanaye unaongoza kwa sababu alipoamua kuigiza kama mama kwenye wimbo huo ilikuwa ni kuubariki ili ufanye vizuri.

Alichokuwa anakitaka mwanangu ni baraka pekee kutoka kwangu kama mzazi na hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa”.

Wimbo mpya wa Mobetto umeendelea kufanya vizuri kwa kushika chati ya juu Kwenye mtandao wa Youtube.