Harmonize Awasaidia Walemavu Dar

Msanii kutoka katikakundi la WCB,Harmonize ameamua kuchukua uamuzi wa kuwasaidia watu wenye uhitaji hasa walemavu wanaoshindwa kutembea kwa kuwapa viti kwa ajili ya kutembelea.

Harmonize amefanya hivyo kwa watu hao akiamini kuwa hata watu hao pia ni mashabiki zake na wanahitaji kupata shukrani zake kwa fadhila ya kumsapotu kila siku katika maisha yake ya muziki.

Katika ujumbe alioandika mzito na mrefu Harmonize anasema kuwa amekuwa koja ya watu wanaosapotiwa sana na ni jukumu lake basi kufanya hivyo kwa watu wanaomjali pia.

Harmonize anakiri kuwa mwaka 2018 umekuwa mwaka wake wenye mafanikio sana hivyo haoni jasara kuamua kutoa shukrani na misaada kwa watu waliomfanya kufanikiwa katika mambo yake hasa muziki ambao kwake ni kazi.

Hii sio mara ya kwanza kwa msani Harmonize na hata kutoka WCB kuwa wakitoa misaada kwa wahitaji katika jamii.

 

Harmonize Awakumbuka Mashabiki Zake Kenya kwa Shukrani.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB Harmonize alimaarufu KondeBoy ametumia siku ya mwaka mpya kuwasifia na kutoa shukurani zake kwa mashabiki zake kutoka Kenya.Mashabiki ambao wamefanya mwaka wake wa 2018 kuwa na mafanikio kutokana na kupendwa sana kwa kazi zake katika nvhi hiyo.

Msanii huyo kutoka Tanzania ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwamwagia sifa nyingi mashabiki zake kutoka Kenya na kuandika maneno haya:-

INGAWA MIE NI MTANZANIA NA NUSU….!!! ILA NAJIVUNIA UWEPO WENU NDUGU ZANGU WA KENYA …!!!! I LOVE YOU ?? YOU CHANGED MY LIFE ? FROM TANZANIAN SINGER
TO EAST AFRICAN YOUNG STER
I LOVE YOU FROM MY HEART ❤
TULIIBADIRI TAREHE 31/12/2018
KUWA TAREHE 12/12/2018 NA TUKAIMBA HAPPY BIRHDAY KENYA…!!!! ❤ GOD

BLESS 254?? THANKS ALO NAAMINI 2019 ITAKUWA ZAIDII….!!! EAST AFRICA TO THE ?

Meneja Wa Harmonize Afunguka Kuitosa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize anayejulikana kama Mr. Puaz amethibitisha kuachana na Harmonize kwa like alichodai ni kukosa maelewano.

Licha ya Harmonize kuwa chini ya WCB Lakini pamoja na wasanii wengine wa label hiyo wana mameneja tofauti ambao wanasimamia kazi zao.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi la Mchanganyiko, Mr. Puaz alikiri kuacha kufanya kazi kama Meneja wa msanii huyo Lakini amekana kuwa na Bifu na msanii huyo wala Label ya WCB.

Ni kweli kwa sasa mimi na Harmonize hatufanyi kazi pamoja kwa sababu ya kupishana kauli; lakini haimaanishi mimi na WCB hatufanyi kazi au hatutafanya kazi.

WCB ni familia yangu ambayo ukaribu wangu na wao ulitokana na urafiki wangu na Diamond hivyo siwezi kuiacha, panapo kuwa na nafasi ya mimi kuhitajika kutoa mchango wangu nitaendelea kutoa kama mwanafamilia“.

 

Wasafi Festival Kuwashusha Wizkid na Mr. Eazi

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa staa wa muziki kutoka Nigeria  Wizkid kwa ajili ya kuperfom katika tamasha la Wasafi Festival.

Diamond Platnumz  amethibitisha hilo kupitia ukurasa wa Instagram baada ya ku-comment kwenye post ya Rayvanny ambayo alipost video fupi ikiwaoyesha Diamond na Wizkid muda mfupi baada ya kumalizika kwa tamasha kubwa la muziki la One African Music Festival lililofanyika Dubai wikiendi iliyopita.

Kwenye video hiyo Diamond alithibitisha kuwa atamshusha msanii huyo mkubwa Afrika kwenye tamasha hilo litakalofanyika Dar Es Salaam baada ya kuzunguka mikoa mingine.

Lakini pia na msanii Harmonize ameamua kuweka wazi meseji zake alizokuwa anawasiliana na msanii kutoka Nigeria akiomba kuja kushiriki angalau katika moja ya tamasha la Wasafi Festival Tanzania.

Ghorofa la Harmonize Lazua Gumzo

Msanii wa muziki Harmonize ameacha maneno midomoni mwa watu baada ya mwana muziki huyo  kuonekna akiwa katika moja ya hatua za ujezi wa nyumba yake kubwa lililopo maeneno ya tandale.

Jumba hilo ambalo ni ghorofa limeonekna bado katika kumalizia lakini kwa wale walioliona na kulithaminisha wanasema kuwa nyumba hiyo itakuwa kubwa sana kiasi kwamba litakapo isha litakuwa na kufuru kubwa.

Harmonize nae amekuwa akifanya mambo mengi yenye kuonyesha mafanikio yake huku akiwakumbuka hata watu wa nyumbani kwao kwa kuwajengea msikiti kwa udhamini wa bosi wake.

Watu wa karibu na ulipo mjengo huo walikiri kuwa mjengo huo mkubwa ni wa mwanamuziki Harmonize kwa sababu mara nyingi wamekuwa wakimuna mama wa msanii huyo akija kuongea na kusimamaia mafundi.

Jaguar Akerwa na Tabia Alioonyesha Harmonize.

Jumamosi iliyopita msanii kutoka Tanzania Harmonize  alikataa kupanda jukwaani Eldoret baada ya madai kuwa Promoter alishindwa kumlipa salio lake kama walivyokubaliana kwenye mkataba. Hata hivyo tukio hilo limemuudhi Mbunge wa Starehe Jaguar kutoka Kenya ambaye pia ni mwanamuziki. .
.
“Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi NAMSHTUMU sana Harmonize….wakenya wamemsupport sana, wamesupport wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu. Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuangalia mafans kwanza,” alisema Jaguar. .
.
Akiongea kwenye Mambo mseto na  Mzazi willy Jaguar ametangaza kuwa wiki ijayo anawasilisha mswada bungeni utakaohakikisha kuwa wasanii wa Kenya pia wanapewa nafasi na kulipwa pesa nyingi kama wanavyolipwa wasanii kutoka nchi za nje. Vilevile, ameongeza kuwa yeye na wabunge vijana watashikana na kuhakikisha kuwa broadcasters wanatii sheria iliyopitishwa kuhusu kucheza 60% Kenyan content.

Jaquar Amtolea Povu Zito Harmonize

Msanii Jaquar kutoka  Kenya ameibuka na kumtolea Povu Zito msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize Baada ya kushindwa kupiga shoo nchini humo.

Wikiendi iliyopita Harmonize alitakiwa kufanya shoo mjini El Doret nchini Kenya lakini alihairisha kufanya shoo hiyo Baada promota kushindwa kumlipa pesa waliyohaidiana.

Kitendo cha Harmonize kushindwa kupiga shoo kiliwauzi mashabiki wengi ikiwemo Mbunge wa jimbo la Starehe Jaquar ambaye kwenye mahojiano na Kipindi cha Mambo mseto alifunguka:

“Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi NAMSHTUMU sana Harmonize….wakenya wamemsupport sana, wamesupport wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu.

Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuanglia mafans Kwanza”.

 

Harmonize Aomba Radhi Baada Ya Shoo Yake Kubuma Nchini Kenya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika label ya WCB, Harmonize amejikuta katika wakati mgumu baada ya shoo yake iliyokuwa ifanyike siku ya jana El Derot nchini Kenya kutofanyika na hivyo kulazimika kuomba radhi mashabiki zake.

Sakata hilo lilitokea baada ya Harmonize kushindwa kupanda jukwaani kutumbuiza baada ya Promota aliyemleta kushindwa kumalizia mkwanja wake kama walivyopatana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika ujumbe wa kuwaomba radhi mashabiki ambao walitoa pesa nyingi kununua tiketi lakini wamejikuta wakikosa shoo kutoka kwa Harmonize;

BINAFSI NAJUA KIASI GANI PESA INATAFUTWA KWA UGUMU BUT KWA MAPENZI YENU MLIJITOA KUJA KUNI SUPPORT SIO KWASABABU MIE NI SPECIAL SANA….!!! NI KWA UPENDO WENU TUU ILA KILICHONISIKITISHA NI PROMOTERS KUCHUKUA PESA ZA WATU WASIO PUNGUA 4000K THEN WAKASHINDWA KUJA KUMALIZIA PAYMENT ILIYOBAKI NA KUKIMBIA HII INAUMIZA SANA…!! (1) NI DALILI YA KUNIVUNJIA HESHIMA NA UAMINIFU KWA MASHABIKI ZANGU (2) IMENIUMIZA KUONA WATU WALIOJITOA KULIPA VIINGILIO VYAO JUST FOR ME WANADHULUMIWA MWISHO KABISA…!!! NISEME SAMAHANI #ELDORET ?? NEXT TIME NITAHAKIKISHA TUMELIPWA DOO YOTE KABLA NI COME TRUST ME I’M SO….!!! DISAPPOINTED AND I LOVE YOU ❤ AND I WAS EXTRA READY ?? I DID#SOUNDCHECK AND EVERYTHING THIS IS TO BAD”.

Harmonize siyo msanii wa kwanza kuwanyooshea vidole mapromota feki kutoka nchini Kenya kwani miezi michache iliyopita tu msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage alilalamika na prom0ta feki pia.

“Wasanii Waache Unafiki”- Professor Jay

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva man mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amefunguka na kuwachana wasanii waache unafiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari katika siku za hivi karibuni, Professor Jay amesema kuwa unafiki kwa wasanii wengi Kwenye Bongo fleva ndio unapelekea wengi wao kukosa mafanikio mapema:

Nomba niwaombe sana Wasanii wa Watanzania, Unafiki ndio unatufikisha hapa tulipo, ukiona msanii mwenzako anaandaa kitu msapoti kwa njia zozote unazoweza kumsapoti ili kesho na wewe ukiwa na cha kwako na yeye aweze kukusapoti ingawa wasanii wa Bongo unaweza ukamsapoti ikifika zangu yako anakausha anasubiri mpaka anapokuja Tena anaomba umsapoti Tena sasa huo ni Unafiki “.

Lakini pia Professor Jay amezungumzia wimbo wake mpya aliomshirikisha Harmonize unaoitwa ‘Yatapita’ ambao una uhalisia wa maisha ya wengi ikiwemo Harmonize ambaye ameshapitia maisha magumu ikiwemo kuuza mitumba mpaka kukataliwa Kwenye BSS na sasa staa mkubwa Bongo.

Harmonize Amwagia Povu Zito Wolper Baada Ya Tetesi Za Kurudiana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amejikuta anamtolea povu zito aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper baada ya kusambaa kwa taarifa za Kurudiana.

Siku chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Harmonize wamerudiana baada ya Wolper kuposti jina la Harmonize.

Sakata hili lilianza baada ya Wolper kuposti picha kadhaa alizoziambatanisha na Jina la Raj ambalo lilikuwa ni Jina alilomuita Harmonize kipindi cha Mahusiano jambo lililoibua tetesi za wawili hao Kurudiana.

Lakini kabla ya Tetesi hizo kusambaa vizuri Harmonize alimjia juu Wolper baada ya kuulizwa na mashabiki zake kama kweli amemtosa Mzungu wake Sarah na kuamua kuwa na Wolper ambapo alijibu:

Anajitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe bila hata haya wakati tuma msiba wa ndugu yetu, na mwingine katekwa yeye analeta pombe zake hapa”.

Tangu Harmonize man wolper walipoachana wamekuwa maadui wakubwa huku mara kwa mara wakirushiana vijembe Kupitia social media na mara ya mwisho Harmonize alianika Orishas ya wanaume wote ambao Wolper alibanjuka nao.

Ndanda Fc wamshukuru harmonize kwa msaada aliotoa.

Msanii wa muziki Harmonize amewatoa kimasomaso wachezaji wa timu ya Ndanda fc baada ya kukwama katika hotel moja mjini singida walipokwenda kucheza mpira na timu ya Singida United na kufungwa goli 3-1 wiki iliyopita.

Hata hivyo wachezaji hao walikwamba hotelini hapo baada ya kuyumba kiuchumi lakini msanii huyo ambae ana mapenzi ya kweli na timu yake kutokea nyumbani Mtwara aliamua kujipiga na kutoa kiasi cha shilingi milioni tatu na laki tano kwa ajili ya kuwakwamua wachezaji na viongozi wao .

Wakitoa salamu zao za shukrani Timu hiyo ilimshukuru sana Harmonize lakini pia bila kuusahau uongozi wa msanii huyo amba ni Babu Tale na Diamond platinumz.

Harmonize Wa Bongo Star Search Alikuwa Mbovu- Master J

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo fleva mkongwe kabisa nchini Master Jay ameweka wazi kuwa Harmonize wa Bongo Star Search hakuwa mkali kama wa hivi sasa.

Sio Siri Harmonize ni moja kati ya wasanii anayefanya vyema sana hivi sasa katika tasnia ya Bongo fleva lakini kabla ya mafanikio haya Hatmonize alishawahi kushiriki katika mashindano ya Bongo Star Search.

Kwenye mashindano hayo Harmonize alitolewa na kukosolewa lakini miaka michache baadae alikuja kusainiwa na Wasafi Records na mpaka leo ni Msanii mkubwa Tanzania.

Siku ya jana Shindano la BSS lilitangazwa kurejea Rasmi na moja kati ya jambo ambalo liliulizwa sana kwa Majaji ni Ishu ya Harmonize ambapo Master Jay ameweka wazi kuwa Wakati Harmonize anashiriki BSS alikuwa Msanii mbovu.

Harmonize aliyekuja Kwenye BSS miaka ile alikuwa mbovu iko wazi kabisa hata mimi nimeweka ile clip Kwenye page yangu yaani Harmonize aliyekuja Kwenye BSS siyo huyu wa leo anayefanya vizuri”.

 

Harmonize Ajivunia Kwangaruu Nchini Kenya.

Msanii wa muziki kutoka katika kundi la WCB anajivunia kufanya vizuri kwa wimbo wake wa kwangaru ambao alimshirikisha bosi wake Diamond Platinumz.

Harmonize ambae yuko nchini humo kwa ajili ya kufanya tour ya wimbo huo anasema  katika kila sehemu anayofanya show anaona kuwa na mwitikio mkubwa na mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.

Harmonize anafurahi zaidi anapoona kuwa kila anapopanda jukwaani kuimba wimbo huo , mashabiki wamekuwa wakiuimba mwanzo mwisho, kitu kinachompa matumaini zaidi.Na hata baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa wimbo huo ndio wimbo wa mwaka.

 

Harmonize Kupita Tena na Dully Sykes

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize, ameweka wazi nia yake ya kupita tena na kufanya kazi na Msanii mwenzake Dully Sykes.

Harmonize ametangaza ujio wa  ngoma yake inayokuja hivi karibuni aliyomshirikisha Msanii mkongwe wa Bongo fleva Prince Dully Sykes.

Harmonize ameweka wazi kuwa mashabiki wajiandae mkao wa kul kwa sababu ngoma hiyo itakuwa kali kupita maelezo.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika posti hii kuhusu ujio wa ngoma hiyo:

Lakini ngoma hii mpya haitakuwa Kolabo ya kwanza kati ya Harmonize na Dully Sykes kwani siku za nyuma walishawahi kutoa wimbo wa ‘Inde’ uliofanya vizuri kabisa.

Sijawahi Kufikiria Kuishi Maisha Haya -Harmonize.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini kutoka katika kundi la wcb, Harmonize amefunguka na kusema kuwa katika maisha  yake hakuwahi kuwaza kusihi maisha kama anayoishi sasa hivi ambavyo alivyokuwa akiishi maisha magumu na maisha mazuri aliyonayo sasa.

Harmonize amefunguka na kusema kuwa miaka mitano aliyokuwa  nayo huko nyuma hakuwahi kuwaza kuwa kama leo kutokana na kwamba alikuwa tu anafanya biashara ndogondogo,

miaka mitano iliyopita nilikuwa ninafanya baishara ndogo ndogo hapa hapa kariakoo,nilikuwa machinga mwenye shida, tabu ,  suluba nilizokuwa napitia kila siku.mungu mwenyewe ndio alikuwa anajua , hata ukiangalia 90% ya wimbo wangu wa matatizo ilikuwa ni maisha yangu ya nyuma.sina utajiri wowote lakini kwa afadhali niliyoipata naona mwenye bahai sana.

Maisha ninayoishi sikuwahi kufikiria kama nitaweza lakini pia nina mshukuru mungu kwa kunipa nafasi ya kukumbuka ndugu zangu niliyowaacha maeneo haya.

Harmonize Athibitisha Hana Bifu na Harmorapa wala Harmo Junior.

Msanii wa muziki anaefanya vizuri kwa sasa katika anga za muziki, Harmonize amethibitisha hana bifu na wasanii Harmorapa wala Harmo junior wasanii mabao wamekuwa wakitumia majina yake amabayo yeye ndi aliyetambulisha majina hayo katika anga za muziki wa bongo fleva.

Ingawa kitendo hicho kimeshtua wauwengi kutokana naukweli kwamba ingewezaka kabisa harmonize alitakiwa kuwa na chuki wa wasanii hawa kutokana na kutumia majina yake lakini hakuwa na kinyongo nao ingawa kwake ni mara ya kwanza kufanya hivyo lakini inaonyesha upendo fulani kwa wasanii hawa.

Harmonize anafunguka na kusema kuwa anafurahi kuona watu wana kuwa na tamaa ya jina lake kwa sababu hayo ni mafanikio kwake.

Katika ukurasa wake  wa instagram , harmonize aliandika, mwiko kukata tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule, kwa sababu safari yako ya mafanikio ni ndefu sana.utakutana na changamoto nyingi sana kuna matusi , uonevu na kadhalika….. pale unapokata tamaa utakuwa pia umewavuna moyo watu wengi sana…mwenyezi mungu ni wa aabu sana na hajawahi kukosea katika hii Dunia, maisha ni kombolela…God bless you my twin brothers.