Jokate Mwegelo Azikingia Kifua Tuzo Za SZIFF

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye pia ni mlezi wa tuzo za sinema zetu ametoa pongezi kwa uongozi wa Azam ambao ndio  waandaaji wa tuzo hizo , na ametoa ushauri kwa wasanii walioshiriki katika tuzo hizo huku akiwahakikisha tuzo kubwa hutoka kwa mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa instargram, Jokate amesema anaamini Tuzo hizo zinachamsha tasnia ya filamu nchini, ambapo amesema yapo mapungufu machache yaliyojitokeza ni moja ya vitu vya kujifunza.

https://www.instagram.com/p/BuRWBgDnZxw/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1ijmoq1f5xm5m

Esther Kiama Atamani Nafasi Ya Jokate

Muigizaji wa Bongo movie Ester Kiama amefunguka na kuweka wazi kuwa ametokea sana kumtamania mrembo Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ester alidai kuwa, kwa sasa Jokate amekuwa ‘role model’ wake na anaamini siku moja atakuwa kama yeye.

Unajua nimejikuta natamani kuwamkuu wa wilaya flani hivi ingawa najua siyo mchezo kama watu wanavyofikiria. Kiukweli Jokate ndiyo amenifanya nitamani hivyo, navutiwa na utendaji kazi wake lakini pia anavyonyuka zile suti. Na mimi nimeshaanza kumuiga katika uvaaji”.

Miezi michache iliyopita Mrembo Jokate Mwegelo aliteuliwa na Raisi Magufuli na kuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na mara moja mrembo huyo ameonekana kufanya vizuri sana katika nafasi yake na kuwatumikia vyema wananchi.

Jokate Adhamiria Kuweka Urembo Pembeni

Muigizaji wa Bongo movie na pia Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amefunguka na kusema ameamua kuachana na mambo yote ya urembo na kuelekeza nguvu zake katika Wilaya yake ya Kisarawe.

 

Jokate ameweka wazi kuwa anataka kuweka pembeni mambo mengine yote na kuhakikisha anafanya kazi mwanzo mwisho hadi aone wilaya yake imebadilika na kuwa anavyotaka.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Amani, Jokate alisema kuwa mambo ya urembo na mengine yote aliyokuwa anayafanya, anayaweka pembeni kuhakikisha vitu muhimu vinavyotakiwa kuwepo Kisarawe vipo na vitakuwa vya kudumu hata kama yeye hatakuwepo.

Yaani mambo sijui ya kujiona mrembo huku kwangu mimi sina, sasa hivi yaani nataka kuona Kisarawe ambayo haina ziro, mimba za utotoni hakuna, unyanyasaji wa kijinsia umeondoka kabisa hata kama sitakuwepo madakarani“.

Jokate ameonekana kufanya vizuri sana kwenye nafasi aliyochaguliwa miezi michache iliyopita kwani Mpaka sasa ameshafanya mambo ya maendeleo katika Wilaya yake ya Kisarawe.

 

Jokate Atoa Adhabu kwa Taifa Stars Baada ya Kufungwa.

Mwanamitindo na mkuu wa wilaya ya Kisarawe mwanadada Jokate Mwegelo amefunguka na kuonyesha hisia na mapenzi aliyonayo katika muziki kwa kusema jinsi gni ameguswa na kufungwa kwa timu ta taifa ya Tanzania ya TaifaStars.

Taifa stars ambao jana walipotza mcheoz baada ya kufugwa bao 1-0 na kupoteza mchezo huo ambao mashabiki wengi walikuwa wameweka matumaini kuwa watashinda, wamemuangausha pia mwanadada huyo na kuamua kuwapaadhabu,

katika ukurasa wake jokate aliandika  kwa kuweka picha ya timu hiyo na kusema “kubangua korosho kunawahusu aiseee…”

Mwanadada Jokate ameuwa moja ya wasanii, wanamitindi na viongozi weny kuonyesha mapenzi sana latika swala zima la mpira hata kufikia hatua ya kusaidia vijana wenye vipaji.

Jokate Afurahishwa na Uteuzi wa Mh Rais.

Mwanadada mwanamitindo, mjasimiali, mwanasiasa na pia mkuu wa wilaya  wa Kisarawe ametoa yake ya moyoni baada ya mh Rais kufanya utezuzi wa viongozi wapya hivi karibuni huku akiwa na imani na uteuzi wa kijana Japhet Justice Sayi ambae bado kijana mdogo lakini kupewa nyadhifa kubwa serikalini.

Jokate amefunguka na kuona kuwa alichokifanya mh Rais ni jambo jema na kuwa amekuwa akionyesha vijana kuwa wanaweza kuleta mandeleo katika nchi na ndio maana ameazna kufanya kazi na vijana.

Katika ukurasa wake wa instagram, joate aliandika ”

Rais kaomba leo Ikulu uthibitishwe kijana mdogo uwe Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. – TADB. 
“Tunaamini kwa akili na uwezo wako mkubwa sasa wakulima watafutwa machozi yao na hili la korosho utalisimamia vyema. Sina shaka na uwezo wako kabisa. Mwenyezi Mungu aendelee kukuongoza . 
“Asante Mhe Rais kwa kuendelea kuamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu,” ameandika Jokate kupitia ukurasa wake wa Instagram leo.
Japhet Justine Sayi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo kabla ya jana Rais Magufuli kuelelekeza Waziri husika anayeshughulikia benki hiyo kumthibitisha Rasmi kuwa Mkurugenzi mkuu

Ali Kiba Amtumia Salamu Za Pongezi Jokate Mwegelo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba amemtumia salamu za pongezi Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa kazi nzuri anayefanya.

Ali Kiba ambaye ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Jokate katika siku za nyuma amefunguka kusema Jokate ni mmoja Kati ya viongozi wachapa kazi na kazi sake anazofanya zinaonekana.

Ali Kiba alifunguka hayo kwenye mahojiano na Big Chawa ambaye alimuuliza Kama anachochote cha kumwambia Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mrembo Jokate naye alifunguka:

Namwambia Afanye kazi na pia nimeona kazi zake anazofanya jinsi zinavyoenda vizuri kwa hilo ninampongeza”.

Lakini pia mahojiano hayo Ali kiba amekana taarifa kwamba nyimbo sake mbili alizozitoa mwishoni zimebuma na kudai anaona amefanya vizuri tu Kama siku nyingine.

Jokate Atengeneza Uadui na Manara Kisa Yanga.

Mwanadada ambae amekuwa akijihusisha na mambo megi sana katika jamii ikiwepo biashara, siasa fashion nahata mpira  Jokate Mwegelo ameamua kutuma salamu za  upinzani kwa mhasimu wake mkubwa mabe pia ni moja ya viongozi wakubwa kwa timu ya Simba Hajis manara kutokana na mchezo ambaeulichezwa wikiend hii kati ya Simba na Yanga.

Jokate ambae ni shabiki wa yanga anasema kuwa pamoja na kwamba yeye na haji ni marafiki lakini kwake hilo hatojali kutokana na uadui wako katika swala la upinzani wa kimpira mpaka pale dakika 90 zitakapo isha.

Jokate alisema “samahani sana Haji, Haji wewe ni rafiki yangu sana lakini inabidi utambue  na kukubali kuwa yangu ni timu bora kabisa ya taifa, tumepitia wakati mgumu sana na tunaamini  yatakweisha kabisa”Alisema jokate alipokuwa akiongea na Wasafi Tv.

Hata hivyo kabla ya mchezo huo, Jokate aliitabiria yangu kuifunga sima 3-0 lakini baada mchezo walitoka Droo.

Tuzo Za SZIFF Zimerudi na Jokate Ateuliwa Kuwa Mlezi

Tuzo za Sinema Zetu zinazorushwa na kituo cha Azam Tv Kupitia chaneli Ya Sinema Zetu zimerudi tena kwa mwaka 2018.

Global Publishers wanaripoti kuwa, Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, amesema taratibu zote za maandalizi kuelekea msimu huo mpya zimeshakamilika na kwamba zitaanza rasmi Januari Mosi, mwakani na kuhitimishwa Februari 23 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Uwasilishaji wa kazi hizo utaanza mara moja Oktoba Mosi, mwaka huu mpaka Novemba 30, mwaka huu, mchakato wote huo wa upokeaji wa kazi za wasanii utakuwa chini ya COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania, huku mwenyekiti wa jopo la majaji atakuwa ni profesa Martin Mhando kwani ndiye aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar,”

Katika hatua nyingine, Tido alimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kuwa ndiye wamempatia jukumu la kuwa mlezi wa tamasha la tuzo hizo litakalofanyika Februari 23, mwakani.

Tuzo hizo zilipofanyika mara ya mwisho zilionekana kupokelewa vizuri na wasanii na kuonekana kuondoa uhaba wa Tuzo Tanzania.

Diamond Amuunga Mkono Jokate Kupitia ‘Tokomeza Zero’

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameingia Mkono jitihada za Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo katika kuboresha elimu.

Wiki iliyopita Jokate alitangaza kufany harambee kwa ajili ya maboresho ya elimu katika Shule ya Minaki siku ya Jumamosi.

Wasanii kadhaa wameunga Mkono jitihada hizo akiwemo Aliyekuwa mpenzi Msanii Diamond Platnumz ambaye Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka wananchi mbali mbali kushiriki siku ya kesho.

https://www.instagram.com/p/Bn-5ProhAVW/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=e0qllefy8n56

Jokate Aja na Tokomeza Zero Kisarawe.

Mwanadada Jokate amliyewahi kuwa mrembo wa miss tanzania lakini kutoka na juhudi alizoonyesha mh rais alimuamini na kumpa kiti cha ukuu wa wilaya ya Kisarawe anazidi kuonyesha nguvu na nia yake ya kutaka kuwasaidia vijana hasa katika kampeni yake mpya ya tokomeza zero katika wilaya ya kisarawe.

Jokate anasema kuwa kampeni ya kutokomeza wanafunzi wanaofeli katika shule za sekondari ilianza tangu 2017 hivyo anataka wadau mbalimbali sasa kutilia mkazo swala hilo ili kukamilisha azma hiyo.

ukimsaidia mtoto akaweza kupata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima,na mimi kuanzia sasa nataka tuanze  na kidato cha nne na sita tufute hizo zero na zisiwepo kabisa.

Jokate anasema kuwa nia yake kubwa ni kuwasaid awatoto katika elimu lakini pia inabidi kuweka mazingira safi kwa ajili ya kuepuka na kila kishawishi .

Jokate Amtaka Miss Tanzania Ajiandae na Matusi Ya Mitandaoni

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe na Aliyewahi kuwa mlimbwende wa Miss Tanzania Jokate Mwegelo amefunguka na kumuandaa kisaikolojia Miss Tanzania mwaka 2018 Queen Elizabeth na mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumapili Tanzania ilipata Miss mpya wa kuliwakilisha Taifa Mrembo Queen Elizabeth na mara moja mitandao ya kijamii ilianza kutoa maoni yao kuhusu Mrembo huyo.

Jokate ameibuka na kumuelezea balaa la mitandao ya kijamii na namna inavyoweza kumbomoa au kumjenga ambapo cha muhimu ni uajasiri kwani watu watakuwa na maoni mengi juu yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers , Jokate alisema baada ya kushinda, Queen Elizabeth amekuwa staa mpya kwa hiyo ategemee kusikia mengi kutoka mitandaoni.

Kikubwa unatakiwa kuwa tayari kupokea kila kitakachokuja kwako. Kwa sababu wakati mwingine unaweza kutukanwa kiasi kwamba ukatamani uachane na mitandao hiyo. “Lakini unatakiwa kufahamu hiyo ni hali ambayo inawakuta wengi wetu. Kwa hiyo kuwa mvumilivu na kwa upande wako itumie mitandao kwa manufaa ya jina na kazi zako”.

 

Jokate Mwegelo Ampongeza Miss Tanzania

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe na Mrembo Jokate Mwegelo amemtumia salamu za pongezi Mrembo ambaye ni Miss Tanzania mwaka huu Queen Elizabeth Makune.

Queen Elizabeth aliyezaa tajiri hilo mwishoni kwa wiki iliyopita na mara moja kulikuwa kuna gumzo kuzunguka ushindi wake ikiwemo zawadi aliyopata na hata waandaji wa Shindano hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate amemuandikia ujumbe huu Miss Tanzania mwaka 2018/2019:

https://www.instagram.com/p/BnkueosgAMU/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ctg7mnbl6wrb

Baba Jokate Awataka Wema na Uwoya Wamuige Jokate

Baba mzazi wa Msanii na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate, Mzee Urban Costa Ndunguru amefichua siri nzito inayowafanya mpaka Wema Sepetu na Irene Uwoya Wasafikie malengo yao kisiasa.

Kwenye mahojiano na gazeti la ‘Amani’ Nduguru aliliambia Amani katika mahojiano maalum kwa njia ya simu hivi karibuni kuwa:

Mwanangu, Wema, Uwoya wote wana ndoto za kuwa wanasiasa na viongozi wa umma lakini hawa wawili kuna mambo yanawakosesha fursa.

Mimi Uwoya simfahamu sana, namsikia tu habari zake kwenye magazeti, lakini Wema namfahamu kwa sababu baba yake (marehemu Isack Sepetu) nimefanya naye kazi serikalini.

Matatizo yanayowakosesha nafasi za kufikia ndoto zao hawa watoto yako mengi lakini kubwa kabisa ni kuiacha misingi bora waliyolelewa na wazazi wao. Siri kubwa ya kufanikiwa hasa katika kutumikia watu ni kujiheshimu na kufanya mambo kwa siri, siyo kwenda kiholelaholela, unajivunjia heshima mwenyewe”.

Lakini pia Baba Jokate amewataka warembo hao wawili kuiga mfano wa Jokate:

Nimeona wanampongeza mwanangu kwa kuteuliwa kwake (kuwa DC), na mimi nasema wasiishie kumpongeza tu lakini waige tabia zake.

Jokate ni mwanangu, sisemi ni mkamilifu lakini ni msiri sana, vigumu kumuona kwenye jamii akifanya vitu vya ovyo, tabia hii naomba Wema na Uwoyawaiige itawasaidia kufikia ndoto zao za kuwa viongozi“.

 

Sikuwahi Kufikiria Kuwa Mkuu wa Wilaya, Nilitamani Ubunge:-Jokate

Mwanadada Jokate Mwegelo ambae kwa sasa ameanza rasmi kazi yake mpya ya kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kisawasawa na kishindo na kuwa karibu na wananchi wake  aliwahi kusikika siku ya kuapishwa kwake akisema kuwa hakuwahi kabisa kuwaza kuwa angeteuliwa na Mh Rais kuwa mkuu wa wilaya.

Jokate ambae hapo awali aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika chama tawala na hata baadae kuenguliwa atika moja ya vyeo vikubwa katika UVCCM, amesema kuwa hata baada ya kutolewa huko alikuwa amekaa kimya kumbe pia Mungu alikuwa akimtayarishia jambo kubwa na zuri zaidi.

Jokate anasema kuwa bado anamshukuru sana mh rais kwa kumuona na kumuamini lakini nafasi hiyo hakuwahi kuifikiria wala kujua kama angeweza kuipata.hata hivyo baada ya kutolewa katika cheo hicho alikaa kimya muda mrefu bila kuonekana katika mitandao ikiwa ni njia yake ya kujitafakari  na kujua nini anataka kufanya.

sikuwahi kufikiria kama ningekuwa mkuu wa wilaya , lakini nashukuru kwa hshima kubwa aliyonipatia mh rais.Nafasi niliyokuwa natamani kwenye siasa ni kugombea ubunge.sikutegemea wala kufikiria swala la ukuu wa wilaya.

Mh. Jokate Aanza na “Operation Jokate ” Kisarawe.

Mwanadada mrembo na mwanamitindo Jokate Mwengelo ambae hivi karibuni aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe, ameanza kazi rasmi katika wilaya hiyo huku akianza kwa kishindo kikubwa kwa Operation Jokate ambayo inalengo la kuondoa wavamizi  katika mapori na hifadhi za taifa.

Kampeni hiyo ambayo Jokate ameanza nao inalengo la kuondoa wafugaji wanaotumia vibaya hifadhi za taifa kwa ajili ya ufgaji kitu ambacho ni kinyume na taratibu.

Zifuatazo ni picha zinazomuonyesha Mh Jokate akiwa na watendaji tofauti tofauti walikuwa wakitekeleza jukumu hilo.

Licha ya Kuwa Mkuu wa Wilaya,Jokate Akiri Kutoachana na Uanamitindo.

Mwanadada Jokate Mwegelo ambae hivi karibuni aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe  amesema kuwa hawezi kuacha kuwa mwanamitindo kama wengi wanavyodhania kwa sababu tu yeye ameteuliwa kushika nafasi fulani katika serikali.

Jokate anasema kuwa  watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa itakuwaje kuhusu kazi yake ya uanamitindo hasa baada ya kupewa cheo kingine serikalini, lakini anachoamini kuwa hiyo ni kazi yake hivyo hawezi kuacha kazi hiyo.

jamani mimi bado membo kwaio siwezi kuacha kufanya kazi na wabunif mbalimbali kwa sababu ya kuwa mkuu wa mkoa. na kwa sababu bado navaa, nitaendelea kuvaa nguo , vitenge, na nguo mbalimbali zinazobuniwa ila tu kwa sasa lazima kuwe na utaratibu maarum wa kuvaa lazima nibadilike kidogo.

lakini pia ikumbukwe kuwa kuna mitindo na urembo mbalimbali kama mafuta, wanja, na urembo ni lazima tuendelee nao kwa sababu tu ni maisha yetu ya kila siku.na sio kwamba nitakuwa ninashiriki sana lakini nitafanya pale kwa uweoz wangu, kwa mfano kama nguo niliyovaa sasa imebuniwa na mwanamitindo kutoka hapa nchi , sasa ntaachaje kuvaa, nitaendelea kusapoti mitindo na huu ukuu wa  wilaya wangu.