Namkubali Sana Jay Dee Kuliko Msanii Mwingine:-Lady Jay Dee

Msaniii mkongwe wa muziki nchini  ambae alipata cheo cha kuwa dada mkuu katika muziki wa bongo lady jay dee amefunguka  na kudai kuwa katika kazi zake za muziki msanii anaemkubali kupita wote ni yeye mwenyewe na anawaheshimu sana baadhi ya wasaniii wakubwa na wakongwe nchi.

Lady Jay Dee ambae  ana haki ya kusema hayo kutokana na magumu mengi ya muziki aliyopitia mpaka sasa pamoja na changamoto za kuwa na wasanii wengi wa kike chipukizi lakini bado yupo katika game na anasimama vizuri anasema kuwa wasanii wengi wanafanya vizuri lakini kwake kuwa anajikubali mwenyewe zaidi kuliko mtu yoyote.

Namkubali sana lady jay dee kuliko wasanii wengine wote wa kike tanzania.ila pia ninawaheshimu sana Khadija Kopa na Patricia Hillary.

Mwandishi pia alipata bahati ya kumuuliza Jay Dee kuhusu tetesi zake za kukaa nje ya Tanzania na kuhamishia makazi yake nchini nigeria ambapo yupo mpenzi wake Spicy Music na hata kufanya kazi zake huko , lakini jJay Dee alisema kuwa Tanzania ndio nyumban, nigeria atakuwa anakwenda na kurudi tu kwa kuwa kila kitu chake alitengeneza hapa.

Kwenda na kurudi sawa lakini sio kuishi moja kwa moja huko,kwa aslimia kubwa sana maisha yangu yote nimeyajenga Tanzania, ila inawezekana ikibidi,

Mpaka sasa Jay Dee anaweza kuwa ndio msanii mkubwa wa kwanza wa kike mwenye album nyingi sana tanzania pamoja na kwamba jwa sasa wasanii wameanza kuwa na msimamo wa kutoa album lakini bado jay dee anaongoza kwa hilo.

 

Jay Dee Awatolea Povu Waliomwambia Ajui Kuvaa Kwenye Harusi ya Ay.

Mwanadada anaefanya vizuri katika muziki tangu miaka ya 90 mpaka kufikia hatua ya kumpachikwa jina la dada mkuu katika muziki Lady Jay Dee, amewatolea povu mashabiki ambao walimchamba na kumwambia kuwa amekosea kuvaa na kwamba hajui fashion  kutokana na kuvaa nguo nyeupe katika harusi ya msanii mwenzie Ay iliyofanyika wikiendi iliyopiat.

Lady Jay Dee ambae mara nyingi alishatamka kuwa hapendi kuendeshwa na hisia za mashabiki hivyo anataka kufanya kile ambacho yeye anajiskia anasema kuwa watu wamekuwa wakisema bila kuvaa uhusika wa kile kilichokuwa kinatokea au kufanyika, akijaribu kuweka mfanano wa wageni waalikwa wengine Lady Jay Dee anasema kuwa sio peke yake aliekuwa amevaa nguo nyeupe hivyo watu waache kuongea bila kuwa na uthibitisho.

katika ukuraa wake wa instagram , lady jay dee alitoa povu hili:haya wale mazwzawa wote ambao mlinichamba kuwa kuhusu kuvaa nguo nyeupe kwenye harusi ya watu..oooh kagooglee haya huyo google ni nani? ndo baba yenu au?haya na hao warembo wote waliovaa nyeupe vipi?mambo msioyajua  muwe mnayauliza kwanza kabla kuanza kubwata bwata..tusivae rangi ya harusi kisa nini..kisa google,,hebu mie..

Wasanii wengine wamekuwa wakikerwa na maneno ya mashabiki katika mitandao kwa kile wanachodai kuwa wamekuwa wakiongea na kuwataka  wasanii kufanya vile wanavyotaka wao wafanye.

 

Lady Jay D Ameongea Haya Kuhusu Nyimbo Zake Kupigwa Stop Kusikika Clouds FM

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ amefunguka kuhusu nini sababu hasa nyimbo zake kutopigwa na stesheni ya redio ya Clouds Fm.

Miaka kadhaa iliyopita Lady Jay Dee aliingia kwenye bifu kali na mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM, Ruge Mutahaba hali iliyosababisha kukatika kwa uhusiano kati yake na kampuni nzima ya Clouds Media Group hadi kupelekea stesheni kutopiga nyimbo zake tena.

Lakini tangu miaka kumekuwa na maneno Mengi yamekuwa yakiongelewa kuhusu suala hili kwani tangu hapo nyuma hakuna hata nyimbo moja ya Jaydee ambayo inachezwa na Clouds FM. Kila upande ulishaonhea unahitaji msamaha yaani kumaanisha Jide na Clouds, lakini pia Jaydee alishatoa ruhusu ya wao kupiga nyimbo zake hapo nyuma pia.

Kwenye Interview aliyofanya na Dizzim Online Jaydee amesema hajawahi kukataza kituo hicho kucheza nyimbo zake na hata hivyo walisharuhusiwa na Seven lakini hakuna kilichofanyika.

Ilisemekana kuwa mimi ndio nilikataza  nyimbo zangu kupigwa jambo ambalo sio kweli Mimi sikukataza nyimbo zangu kupigwa na hakuna sehwmu yeyote niliyoandika nyimbo zangu zisipigwe, wao ndio waliamua kwasababu kuongea kwangu kule ndio nyimbo zangu zisipigwe. Baada ya hapo alisema akitoa ruhusa nyimbo zake zipigwe zitapigwa Seven akaongeq akatoa go ahead zipigwe je zilipigwa? Kwaiyo hapo sio tatizo langu inaonekaana dhahiri tatizo liko wapi na mtu anaweza kuongea kitu sio kwa kumaanisha”.

 

Lady Jay Dee Akiri Kumganda Spicy

Mwanadada mkongwe katika muziki Lady Jay Dee akiri kuwa kwa muda sasa tangu awe na mpenzi wake ameona kuwa ni muungano wenye kuleta mafanikio sana katika kazi zake za kimuziki ukiachana na mapenzi ambayo wamejiingiza.Mwanadada huyo amesema kuwa imekuwa ni mafanikio kwa sababu walipotoa remix ya wimbo wao wa together na mpenzi wake spicy ameona kuwa hana haja ya kutokumganda mwanaume huyo kwa sababu wanapofanya kazi pamoja zinakuwa na mafanikio zaidi.

hivi karibuni msanii huyo wa kike ametoa wimbo mwingine aliomshirikisha mpenzi wake huyo unaojulikana kwa jina la baby, na umefanya vizuri  na anaamini kuwa kuendelea kufanya kazi na spicy kutampeleka sehemu nzuri zaidi kwa sababu pia nu msanii mzuri.

nimeamua kumganda spicy, kwa sababu  ninaamini ni mwanamuziki mzuri na muungano wetu  huwa unafanya vizuri sana,angalia ngoma iliyopita na hii  utagundua kuwa  tunapokuwa pamoja na kufanya kazi pamoja  tunatengeneza kitu kizuri. -Alisema Jay Dee.

Lady Jay Dee yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mpenzi wake spicy ambae pia ni msanii kutoka nchini nigeria kwa zaidi ya mwaka sasa na kuamua kufanya kazi kwa pamoja kwa sababu wote ni wasanii na wanafanya vizuri katika kazi zao.

 

Nisipozaa Nitakufa Kwani? Lady Jay Dee Amtolea Povu Zito Shabiki Aliyemshauri Azae

Mwanamuziki mkongwe wa kike wa Bongo fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay Dee’ amemjia juu na kumtolea povu zito shabiki wake aliyemuombea kwa Mungu azae mtoto.

Lady Jay Dee amekaa kwenye sanaa ya muziki kwa kipindi kirefu sana labda kuliko msanii yoyote wa kike lakini moja kati ya vitu mashabiki wake hupenda kujua kuhusu yeye ni maisha yake binafsi.

Baada ya kuwa kwenye ndoa na mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G Habash kwa miaka kumi Lady Jay Dee aliomba talaka na kuachana kwa sababu zisizojulikana lakini tangu aachane na Gadner Jay Dee amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki kutoka Nigeria anayejulikana kama Spicy Music.

Moja kati ya vitu ambavyo huongelewa sana kuhusu Lady Jay Dee na maisha yake binafsi ni suala la kuzaa mtoto ambapo kumekuwa na teyesi nyingi kuwa hana uwezo wa kuzaa huku tetesi hizi zikizaliwa kutokana na kukaa kwenye ndoa kwa miaka kumi na zaidi bila kupata mtoto na umri wake kusemekana kuwa umeenda, Ingawa mwenyewe hajawahi kuliongelea suala hilo hadharani.

Siku chache zilizopita moja wa shabiki wa Lady Jay Dee aliandika kwenye ukurasa wa Lady Jay Dee kuwa anamuombea azae mtoto na anampensa sana maneno yaliyoelekea kumkera Jay Dee kwani alimtolea povu zito Sana:

Hivi hayo maswala ya kupata mtoto yanahusikaje hapa kwa mfano? Hivi si mngeniacha nipumua mtoto amekuwa mtoto kwani nisipopata itakuwaje kwani kwa mfano? Natakiwa nife au? na hii posti inahusikaje na mtoto? Jifunzeni kuwaachia watu maisha yao binafsi aisee mnanichosha zaeni nyie mjaze dunia inatosha”.

 

 

Lady Jay Dee:Nashinda Kutwa Nzima Nikisiliza Kazi Za Aslay

Sio wasanii wote ambao wamekuwa wakifunguka na kusema hisia zao  juu ya kazi za watu wengine tena hasa unapojua kuwa yupo katika kategoria moja ya kazi, hii imekuwa tofauti kwa mwandada lady jay dee ambae si zaidi ya mra moja amekuwa akisifia wasaniiw enzie kwa kazi nzuri wanazokuwa wanafanya.

hivi karibuni akiongea na moja ya magazeti pendwa ya habari nchi, mwanadada lady jay dee amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na kazi anazofanya msanii anaekuja kwa kasi sasa aslya ambae amekuwa akitoa nyimbo kila kikicha na zimekuwa zikifanya vizuri sokoni.

lady jay dee amesema kuwa kuna wakati unakuwa unaitaji kupumzika na kusikiliza muziki mzuri na mara nyingi amekuwa akishinda kutwa nzima akisikiliza muziki wa dogo aslay kwa sababu unamburudisha sana.

mimi ni mwimbaji lakini hii hainifdanyi mimi kushindwa kusikiliza kazi za watu wengine hata kidogo,ninahitaji burudani kutoka kwa wenzangu.kwa mfano ninaweza kutumia muda mwingi sana  wakati mwingine ninashinda hata kutwa nzima nikisikiliza muziki  wa aslay, anajua kuandika na  kuimba  kuimba nyimbo nzuri pia.

Lady jay dee ni mmoja wa wasanii wakongwe ambao wamekuwa katika game kwa muda mrefu na hajawahi kuwa mchoyo wa kusema kil wasanii wengine wanachofanya kama ni kizuri au kibaya.Hii hatakuwa mara ya kwanza kwa msanii lady jay dee kumsifia msanii huyo chipukizi ambae amekuwa akifanya vizuri anapokuwa jukwaani na nyimbo zake zimekuwa zikijulikana kila kona mpaka kwa watoto.

Hata hivyo Aslay ambae amekuwa akitoa nyimbo mfululizo  bila kuogopa kuchuja amesema kuwa kwa sasa amekuwa akitoa nyimbo mfululizo ili kutengeneza  album yake mwenyewe kwa sababu hawezi kuwa akiimba nyimbo za kundi ukizingatia kwa sasa amekuwa akifanya kazi  peke yake.

 

Lady Jay Dee Aongelea Uhusiano Wake na Mwana FA

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama Lady JD amefunguka kuhusiana na uhusiano mpya alionao na mwanamuziki mwenzake Mwana FA.

Lady JD na Mwana Fa waliwahi kiwa mahasimu wakubwa miaka ya nyuma kidogo lakino hivi karibuni wameweka tofauti zao pembeni na kuendelea na maisha kama marafiki.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa Lady Jay Dee alisema anashukuru kwa kitendo cha Mwana Fa kumsapoti katika kazi take mpya aliyoitoa hivi karibuni.

“Ni jambo jema sana msanii mwenzako anapo kusapoti, na ndio kitu wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu hivo mkae mkifahamu hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisapoti”.

Ili kuonyesha kwamba wako sawa na hawana tofauti baina yao tena Mwana Fa kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka kipande cha video mpya ya Lady JD unaojulikana kama ‘I miss you’  na kuhimiza watu wasikilize na kuangalia nyimbo hiyo.

Pia Lady JD aliendelea kufunguka kuwa;

“Ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri na kupendwa na mashabiki, Pia watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.

Bifu la Lady JD na Mwana Fa lilikuwa kubwa lililogawanya mashabiki ambapo waliandaa shoo siku moja lakini Jay D aliishia kujaza ukumbi na Mwana Fa aliishia kupiga ukumbi mtupu na pia kuna tetesi Jay D alimuimbia wimbo wa Yahaya Mwana Fa.

Lakini tunafurahi kuona Wasanii hawa wameamua kumaliza tofauti zao kwani wote ni wasanii wazuri sana.

Mashabiki Wanapendelea Zaidi Nyimbo Za Mapenzi-Lady JD

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Lady Jay Dee amefunguka kuhusiana na sababu za yeye na wanamuziki wengi kupendelea zaidi kuimba nyimbo za mapenzi.

Lady Jay Dee amesema kuwa sio kweli anaimba sana mapenzi bali ni mashabiki zake ndio wanapenda.

Lady Jay Dee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘I miss you’ amesema hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha TBC ambapo alifunguka;

“Mashabiki wanasikiliza wanachokipenda zaidi kwa hiyo nafikiria ndio watu huwa wanapenda mapenzi siyo kwamba mimi ndio huwa naimba mapenzi sana”.

Pia katika mahojiano hayo Lady Jay Dee alifunguka kuhusu ongezeko kubwa la wasanii wa kike katika mziki wa Bongo fleva;

“Nafurahi sana kwa sababu kwa kipindi kirefu kumekuwa na uhaba wa wasanii wa kike na kila tunapoenda tunaulizwa kwa nini wanamuziki wa kike si wengi lakini kwa sasa kuna unafuu mabinti wameongezeka, wamejitokeza”.

Mwana FA Ampa Shavu Jay Dee Kwenye Wimbo Wake Mpya

Ni ya kama miaka mitano imepita tangu wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini, mwanadada Lady Jay Dee na Mwana FA  walipofanya kazi ya pamoja ilikuwa ikijulikana kama “Hawajui’, kazi ambayo ilifanya vizuri sana kama muziki wa bongo, wasanii hao ni  kati ya wasanii wa kwanza na wakongwe kabisa waliwahi kuafanya vizuri na wanaendelea kufanya vizuri mpaka sasa katika tasnia hii ya muziki.Hata hivyo kuna kiprind kirefu kimepita ambapo wasanii hawa wawili walikuwa wakionekana katika bifu zito ilhali hakukuwa na sababu ya wazi kwa bifu lililokuwa likiendelea kati yao, kiasi kwamba walishindwa hata kuendelea kufanua kazi pamoja.

Hivi juzijuzi msanii wa kike Lady Jay Dee alitoa wimbo wake mpya wa” I miss you’, ambao kwa sasa unafanya vizuri katika vituo mbalimbali  vya Radio na Televisheni, lakini jambo la kufurahisha zaidi ni pale msanii Mwana FA alipoamua kupost katika ukurasa wake wa Instagaram na kuonyesha support  kwa msanii huyo wa kike kwa kutoa wimbo wake mpya,akiwa kama msanii mkubwa na anaependwa ma kufuatwa na watu wengi nchini na hata Duniani, Mwana FA kupost kazi ya Lady Jay Dee ianongeza idadi ya mashabiki hata kwa Lady Jay Dee pia na ni njia moja kubwa na nzuri ya kufanya wimbo wake mpya uendelee kujulikana na watu wengi zaidi.

Post ya Mwana FA kwa Lady Jay Dee

Sio hivyo, lakini jambo kubwa zaidi hii inaonyesha kuwa kumbe wawili hao walishamaliza tofauti zao na wamefikia hatua nzuri ya kuanza kusaidiana tena katika muziki.Hata hivyo baada ya kupostiwa kwa wimbo huo katika ukurasa wa Mwana FA naLady Jay Dee alijibu kwa kuandika “more blessings

Ukiachilia mbali na Mwana FL wasanii wengine walionekana kufurahishwa na ujio mpya wa lady Jay Dee n pamoja na Proffessa Jay, pamoja na msanii AY.Hata hivyo mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na hatua kubwa ya wasanii hawa kuonekana kuwa pamoja tena na kumaliza tofauti zao ili waweze kuendelea kufanya kazi pamoja hatimaye kukuza muziki wa tanzania ilhali wao ni wasanii wakongwe kabisa katika muziki.

Lady Jay Dee Aikataa Rockstar 4000 ya Alikiba

Baada ya kusambaa kwa  taarifa za Lady Jay Dee kujitoa kwenye Label kubwa Africa ya Rockstar 4000 imbayo pia inawasimamia Ali Kiba na Ommy Dimpoz mapya yaibuka.

Akiongea na Bongo 5 mtu wa karibu wa msanii huyo amedai, Jide hajawahi kusaini mkataba na label hiyo kwa maana hakuna picha zilizowahi kuonyesha mkataba  huo, alikuwa anafanya kazi na Seven Mosha ambaye ni boss wa label hiyo Kama rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa anamsaidia kazi katika mziki wake.

“Nafikiri kaamua ka Continue reading “Lady Jay Dee Aikataa Rockstar 4000 ya Alikiba”

Kwa Hali Ilivyo Sasa Tanzania ni Wazi Amani Haipo sio Kama Zamani- Lady Jay Dee

Msanii Mkongwe Wa Bongo fleva Judith Wambura au maarufu kwa jina lake la usanii kama Lady Jay Dee amefunguka na kusema kwa hali ilivyo sasa Tanzania in wazi amani haipo sio Kama kipindi cha nyuma na kudai kuwa hali hiyo inaleta hofu miongoni mwa wananchi.

Lady Jay Dee aliyasema hayo katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni ambapo aliulizwa nini mtazamo wake kutokana na kinachoendelea nchini aliongelea ukosefu amani hasa vitendo Kama kupigwa risasi kwa Mbunge Wa Singida Mh. Tundu Lissu na pia Meja mstaafu Wa JWTZ Vincent Mritaba kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni wazi amani ya nchi haipo.

Lady Jay Alisema;

Ni kweli Tanzania hakuna amani kwa  sababu kitendo cha Mtu kupigwa risasi hadharani kinatishia amani ukizingatia kuna wasanii wengine walikuwa wanatekwa unaogopa, sehemu yenye amani vitu kama ivyo havipo, na kitendo cha Meja mstaafu Wa JWTZ  kupigwa risasi inatosha kabisa kuonyesha Tanzania Amani haipo naweza kuwa sina la kusema nikaishia kusikitika tu”.

Aidha Lady Jay Dee amesema kuwa matukio hayo yanaleta picha mbaya kwa nchi kwa kuonyesha tunakoelekea sio kuzuri, kwani nchi yetu ya Tanzania inasifika kea uwepo wake Wa Amani na Upendo na Umoja pia na mshikamano.

Lady Jay Dee: Mimi ni Shabiki Mkubwa wa Aslay

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva nchini Lady jay dee ambaye ni mkongwe wa mziki huo tangu miaka ya 90 ambaye pia anaweza kuwa mmoja kati ya wasanii bora wa kike Afrika Mashariki nzima kutokana na ukongwe wake na kutochuja kwenye fani na kuweza stahimili kukaa kwenye chati kwa miaka yote hiyo.

Mwanamuziki huyo amekiri kipaji cha Aslay na kusema  kuwa anamkubali, Aslay ni msanii anayekuja kwa kasi ya ajabu sana katika mziki huu wa Bongo fleva. Aslay ambaye amejitoa katika kikundi cha Yamoto Band hivi karibuni amekuwa akitoa nyimbo nzuri kutokana na staili yake hiyo ya kuimba nyimbo zake kwa hisia kali. Aslay tangu ameanza kufanya muziki kama Solo Artist ameweza kufikisha views milioni kumi katika chaneli yake ya Youtube.

Lady Jay Dee alieleza haya alipokuwa katika kipindi cha THE PLAYLIST wakati ambapo alitakiwa kuchagua nyimbo tano anazozipenda ambapo mojawapo ilikuwa nyimbo ya Aslay “Muhudumu” na kufunguka kuwa  yeye ni shabiki mkubwa wa msanii huyo na muziki wake na kwasababu ana melodies za kipekee na nzuri sana kwenye nyimbo zake.

Lady Jay Dee ametoa nyimbo yake mpya inayoitwa “I miss you” inayofanya vizuri redioni na pia Aslay naye ana nyimbo kadhaa zinazofanya vizuri alipoulizwa kuwa endapo watashirikiana kufanya kazi mbeleni alijibu kuwa atafurahi ikiwa hivyo.