Lulu Atangaza Rasmi Kuwa Yeye ni Simba

Mwanadada Lulu michael ametangaza rasmi katika vyombo vya habari kuwa yeye ni shabiki m,kubwa wa simba , ushabiki ambao aliupata kutoka kwa mama yake kwa sababu mama yake ni shabiki wa simba.

Lulu anasema alianza kuipenda simba kutokana na watu waliokuwa wakimzunguka hasa mama yake mzazi,.

Hata hivyo , Lulu aliyaongea hayo alipokuwa katika ziara yake katika kampuni ya habari ya mwananchi kabla ya mechi  ya simba na al ahly na kusema kuwa anawatakia kheri simba kufanya vizuri katika mechi hiyo huku akiwataka kutulia na kutokukata tamaa ya kufungwa magoli ,engi nyuma kuwafanye waumie na kushindwa kufanya vizuri.

Siwezi Tangaza Harusi Yangu Kwenye Mitandao :-Lulu

Mwanadada Lulu michael ambae kwa fununu zilizokuwepo hapo awali ni kwamba mwanadada hiuyo alienda kufungia ndoa yake nchini China amefunguka na kusema kuwa hakutaka na wala hatotaka ndoa yake itangazwe katika mitandao ya kijamii kwa sababu hilo ni swala ambalo sio lazima kila mtu kulijua hilo.

Lulu ameyasema hayo alipokuwa aktika tour yake kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwa ajili ya misaada atakayo itoa katika msimu huu wa valetine kwa watu wenye uhitaji katika jamii.

Lulu ambae pia aliwahi kusemwa kuwa mwanaume ambae anafunga nae ndoa amekuwa akimpiga na kumtesa sana kwa sababu ya pesa alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa maisha yakeya nyumbani yatabaki kuwa hivyo na wala hana haja ya kusema katika mitandao.

Lulu anasema kuwa tetesi zoozte hazina ukweli kuhusu ndoa yake na michakato ya harusi bado inaendelea.

 

Lulu Afungukia Tetesi Za Kuwa na Mimba

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa sio mjamzito na hata alipotoka gerezani hakuwa mjamzito.

Lulu alitoka gerezani mwaka jana Baada ya kutumikia kifungo kwa miezi kadhaa lakini Baada ya kutoka kuna tetesi zilisambaa kuwa ametoka mapema kutokana na ujauzito na pia alikuwa ameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Lakini siku ya Leo kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Lulu ameweka wazi kuwa hajawahi kuwa mjmzito kabisa bali alinenepa alipokuwa jela na kuongezeka karibia kilo 20.

Lulu amesema taarifa zilizowahi kusambaa kuwa alikuwa mjamzito hazily was za kweli bali alivyotoka jela alikuwa ameongezeka kilo 20 hivyo kupelekea mwili Wake kuwa mkubwa sana.

Lakini pia amefungukia tetesi za kugombana na Mpenzi Wake Majizzo ambapo amesema kuwa hawezi kuongea chochote kuhusu maisha yake binafsi:

Watu wanatengeneza vitu vyao ili wapate jambo kutoka kwako, watu wanatengeneza mambo yao, Mimi kuwa maarufu haimaanishi kila kitu katika miasha yangu lazima kiwe maarufu, hata mahusiano yangu yawe maarufu.

Juu ya hilo la kuvua pete Siwezi kukubali wala kukataa wacha waamini wanavyoamini”.

 

Dr. Cheni Baba Yangu Wa Sanaa- Lulu

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuongelea uhusiano wake  na muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni.

Kwa miaka mingi sasa Lulu ameonekana kuwa karibu sana na Dr. Cheni na sasa anafunguka na kuweka wazi kuwa ni mtu wa muhimu kwenye maisha yake.

Katika mahojiano aliyofanya na Kituo cha Times Fm, Lulu amefunguka na kusema kuwa watu wengi hawajui uhusiano Wake na Dr. Cheni Lakini yeye amemtaja kama baba yake katika Sanaa.

Watu wengi hawajui Lakini Dr. Cheni ni baba yangu wa Sanaa, tangu alipogundua kipaji changu Nikiwa na miaka mitano, amezidi kuwa mtu wa muhimu kwangu katika kuikuza na kuiendeleza Sanaa yangu”.

Lakini pia Dr. Cheni ameonekana na Lulu katika wakati ambao alikuwa anapitia kipindi kigumu ikiwemo wakati ambao aliwahi kupelekwa jela.

Lulu Michael Akataa Kuongelea Swala la Kupigwa na Majjizo

Kumekuwa na tetesi zilizosambaa katika mitandao kuhusu mwanadada Lulu Michael kupigwa na mwanaume ambae amemtolea mahali na kumvisha pete ya uchumba huku ndoa ikisemwa kunukia siku yoyote.

Mwanadada Lulu Michael amekataa kuzungumzia swala hilo huku akisema kuwa wengi wanaozungumzia na kusambaza taarifa  hawataki kuona anapiga hatua katika yale anayoyafanya kwa sasa lakini hawzi kuzngumzia swala hilo kwa sasa kwa sababu yuko na kampeni kubwa na yenye manufaa kwa jamii kuliko kitu chochote kwa sasa.

Kama umeshawahi kuona filamu za mapigano , mwisho wa siku utakuja kuona jinsi adui anavyojaribu kumuadaha sterling,  na hivyo ndivyo ninavyoyachukulia maneno haya.

Tetesi hizo zlianza hivi karibuni baada ya mwanadada huyo kuonekana hana pete ya uchumba aliyovishwa hivi karibuni na mume wake huyo mtarajiwa.

 

 

Lulu Atoa ofa ya Nguo kwa Mashabiki.

Mwanadada Lulu michael ameamua kutoa ofa kwa mashabiki wake kwa kutaka kugawa nguo zake nyingi zilizopo katbabtini huku akiwataka watu mbalimbali kumtumia picha ya nguo waliowahi kumuona nayo akiwa amevaa na kupendeza kisha yeye kuipenda ili aweze kugawa nguo hizo.

Mwanadada huyo ambae kwa sasa amekuwa nje ya mitadao amekuwa akitumia sana mtabada wake wa snap kwa ajili ya kupost kutokana pia na population ndogo iliyopo huko.

Akiandika katika ukurasa wak wa snap, lulu alisema kuwa ” kuna nguo yoyote uliwahi kuipenda  na ukatamani kuwa nanyo…oaky 2019 nitaanza kusafisha kabati langu ..who si ready ”

 

Makonda Athibitisha Lulu na Majjizo Kufungia Ndoa China

Mkuu wa moa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amefunguka wakati akimpa pongeza za kuamua kuchukua jiko kwa mc pilipili huku akijikuta akifunguka engi kuhusuwatru wake wa karibu anaowajua ambao pia wao katika kiwanda cha burudani.

Kama itakumbukwa , Mh huyo ndio alikuwa master mind wa  harusi ya msanii lulu michael na mpenzi wake majizo ambapo tunaambiwa kuwa wawili hao waliamua kwenda kufumga ndoa yao nchini china ambapo watrakuja huku kwa ajili ya kufanya sherehe tu.

Mwanadada Lulu Michael na majizo wamekuwa nje ya nchi kwa muda sasa huku taaarifa za wali zilidai kuwa walienda kwa ajili ya matembezi lakini mkuu wa mkoa katoboa siri.

Mh makonda aliamshauri Mc Pilipili kumshauri diamond kuacha kuhairisha ndoa kama alivyofanya kwa sasa kati yake na tanasha huku akisema kuwa swala lake la kumvisha msichana pete limewaumiza wengi aliwahi kuwa nao katika mahusiano.

 

Lulu Adaiwa Kuwekewa Ulinzi Mzito.

Tangu ametoka gerezani na hata kukitumikia kifungo chake cha nje na hata sasa amekimaliza na kuanza process za harusi, mwanadada Lulu Michael amekuwa aonekani sana kama zamnai alivyokuwa kila kona ya mtandao unamkuta yeye.

Mwanadada huyo kwa sasa anadaiwa kutembea na ulizni mkali wa bodyguard anaetembea nae kila mahali anapokwenda kwa ajli yaulizni na usalama wake.

Haijulikana sababu kubwa ya mwanadada huyo kutembea na mlizni lakini almekuwa akionekana katika baadhi ya matukio hayo makubwa ya harusi yake akiwa na mtu anaetembea nyuma yake kuhakikisha ulinzi wake.

Wakisimulia wale walioshuhudia siku ya kutolewa kwa posa yake. Lulu alionekana akija ukumbuni huku nyumba yake kukiwa na mtu wa ulizni aliekuwa akimuelekeza kila kitu cha kufanya hata kuwa nae karibu muda wote.

Hata hivyo mashabiki wake wanasema kuwa swala la kuwa na mlinzi ni kwa ajili ya ulinzi wake lakini kwa mashabiki ina wanyima uhuru kwa sababu hapo mwanzo walikuwa kila wakikutana nae wanaweza hata kupiga nae picha na kumkimbilia lakini tangu amekuwa na walzini imekuwa vigumu kwake kuwa karibu na mashabiki.

 

Lulu Adaiwa Kuwekewa Bodyguard Baada Ya Kuvishwa Pete

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amedaiwa kuwekewa ulinzi mzito na mume wake mtarajiwa Majizzo Baada ya kumvalisha pete.

Gazeti pendwa la Amani linaripoti kuwa tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.

Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone“.

Gazeti hilo lilithibitisha taarifa hizo wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.

Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.

Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa“.

Tangu ametoka gerezani miezi Michache iliyopita Lulu amekuwa na upepo wa bahati nzuri kwani amechumbiwa na Mpenzi Wake wa muda mrefu Majizzo na kumaliza kifungo chake rasmi.

Lulu Athibitisha Kukutana na Mungu Live

Mwanadada Lulu Michael amefunguka na kutangaza kuwa alikutana na mungu live hasa baaada ya kukutana na matatizo makubwa katika maisha yake katika umri wake mdogo.

Akijibu moja ya pongezi alizokuwa akipewa na ke wa Mh Paul Makonda hasa baada ya kufanikisha zoezi kubwa katika maisha yake wikiendi iliyopita ambapo mpenzi wake alikwenda nyumbani kutoa mahali.

Mwanadada huyo amekuwa katika wakati mgumu mara nyingi hasa kutokana na makubwa aliywah kutapitia ikiwemo ya kufungwa gerezani akiwa na umri mdogo na hata kuwa na historia ya kuwa na kesi ya mauaji .

Lulu anasema kuwa kwa jinsi ambayo amekuwa akikutana na Mungu live katika maisha yake anaamini kuwa hakuna kinachoweza kumshinda katika maisha haya ya kawaida.

Lulu Michael Atolewa Mahali na Mchumba Wake.

Mwanadada Lulu Michael ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu kutoana na kuwa na kesi ya kuua bila kukusudia, wiki iliyoisha alianza kuonekana katika mitandao ya kijamii hasa baaada ya kuweka moja ya post zake kaika mitandao ya kijamii .

Lakini moja ya habari kubwa  ya kufurahisha ni kwamba mwanadada huyo kwa sasa anatarajia kufunga ndoa siku yoyote hasa baada ya matukio ya kuhararsiha ndoa hiyo yakifuata moja baada ya jingine.

Mwezi uliopita mwanadada huyo alivalisha pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi majizo na sasa wiki iliyopita mwanadada uyoa ametolewa mahali na mwanaume huyo kuashiria kuwa siku yoyote wawili hao wanatarajia kufunga ndoa.

Mwanadada huyo ambae mashabii wake wamekuwa wakimsubiri kwa hamu sana kumuona akiwa katika mitandao na kufanya yale aliyokuwa aktafanya hapo nyuma amekuwa kimya sana tangu ametoka gerezani na inawezekana baada ya hayo ameona ni bora kubadilisha maisha yake kabisa.

Lulu Avunja Ukimya Baada Ya Kumaliza Kifungo Chake

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu hatimaye amevunja ukimya tangu alipomaliza kifungo chake na kutoa shukrani zake za dhati kwa watu wote.

Mwaka jana Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka mieili jela Baada ya kukutwa na hayo a ya kumuua Bila kikusudia aliyekuwa Mpenzi Wake marehemu Steven Kanumba.

Lakini Baada ya kutumikia kifungo chake kwa miezi kadhaa Lulu alipata  msamaha wa kipunguziwa kifungo na kupewa kifungo cha nje ambacho ametumikia na kumaliza Wiki hii.

Baada ya ukimya mrefu kwenye mitandao ya kijamii hatimaye Lulu amefunguka na kuandika haya katika ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BqO4xVJHf3d/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=fuqi471bjk50

Msemaji wa Magereza Akanusha Uhuru wa Lulu Michael

Huku taarifa za habari za furaha zikianza kusambaa katika vyombo mbalimbali kuhusu msanii Lulu Michael kuwa huru baada ya kusemekana kuwa kifungo chake kuisha lakinimsemaji wa magereza amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa lulu bado ni mfungwa kama wafungwa wengine na kifungo chake kitakapoisha atakuwa hurulakini si sasa.

Msemaji huyo anasema kuwa kwa kawaid ahaweiz kuwa huru kama hajafata utaratibu wa magerezawa kuachi wa huu hata kama hakuwa akiishi gerezani kwa kipindi cha muda mrefu kutokana na kutumikia kifungo chake cha nje.

Msemaji wa magereza anayasema hayo baada ya kuona kuwa taarifa za kuwa huru kwa mwanadada huyo zimesambaa sana katika mitandao ya kijamii, “taratibu nadhani anazifahamu kwa sababu lazima kuna utaratibu wa kufuatwa kabla ya kuwa huru,  na hata kama yuko kifungo cha jje kuna utaratibu anafuata pia kama wafungwa wengine tu hata kama ni mtu maarufu , kile ambacho lulu anafanyiwa ni kama anaweza kufanyiwa mfungwa mwingine yoyote yule...”

Msemaji huyo anasema kuwa kama ilivyo kwa wafungwa wengine kuwa hawakutangazwa kipindi anawekwa ndani na ndivyo itakavyo kuwa akiwa anatoka, na hata kama alikuwa na kifungo cha nje haimaanishai kuwa anatakiwa kuondokea huko huko uraiani bali anapaswa kurudi magereza na kufuata taratibu za kumaliza kifungo na ndipo atakapokuwa hur na maisha yake ya nje..

Lulu Amaliza Rasmi Kifungo Chake

Mwanadada Elizabeth Michael amemaliza rasmi kifungo chake alichokuwa akitumikia kwa muda saa akiwa nje na November 12 ndio ilitakiwa kuwa huru kwa kukimaliza kifungo hicho.

Mwanadada Lulu ambae alikuwa nje akitumia kifungo cha nje huku akipangi wa kufanya kazi mbalimbali za kijamii amekuwa huru kuanzia sasa na kwamba hata zile kazi alizokuwa akifanya za kijamii itakuwa zimefika kikomoe kuanzia sasa.

Lulu alihukumiwa kifungo cha jela baada ya kukitwa na kesi ya kuua bila kukusudia kwa mwanamaigizo mwenzake Steven Kanumba mabae alikuwa ni mpenzi wake pia walipokuwa wakikorofisha  na kumsukuma kwa bahati mbaya na kuuumia sehemu za kichwa.

Mwanadada Lulu anaingia uraia tena akiwa tayari amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi Majizo ambao walitangaza ndoa hiv karibuni.

Majizzo Atangaza ujio mpya wa Lulu

Mchumba wa mwanadada Lulu michael amefunguka na kuweka bayana ujio mpya wa mpenzi wake huyo kwa kuweka kipande kidogo cha picha inayoonekna kuwepo jikoni kwa sasa  .

Huku ikiwa ni zaidi ya mwaka sasa tangu mwanadada Lulu Michael awe kimya katika mitandao ya kijamii na pia katika televisheni tangu alipokumbwa na hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudia, mwanadada lulu michael amekuwa akisubiriwa kwa hamu na kila shabiki yake.

katika ukurasa wake wa instagram Majizo aliandika”back to bussiness “

Mwanadada Lulu michael anarudi katika tsnia akiwa tayari amesubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki zake.

Kifungo cha Lulu Chabakiza Siku 40.

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ’Lulu’, amebakiza siku 40 kumaliza kifungo chake huku akielezwa kuwa mtiifu kipindi chote.

Lulu alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela, baada ya Novemba 13, mwaka jana kuhukumiwa na mahakama kuu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa gwiji wa filamu, Steven Kanumba.

Hata hivyo, Aprili 26 mwaka huu, msanii huyo aliye kwenye orodha ya wadada wanaojua kuvaa  hapa Bongo alibadilishiwa adhabu hiyo na kuwa ya kifungo cha nje.Kutokana na hilo, alipangiwa kazi ya kufanya usafi katika Wizara ya Mambo ya Ndani iliyopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam aliyoianza tangu Machi 14 mwaka huu.

Katika siku za mwanzo gazeti la Mwananchi lilipata picha akiwa ameanza kutumikia kifungo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Probesheni na Huduma za Jamii, Charles Nsanze, amesema katika kipindi chote hicho Lulu amekuwa akitekeleza majukumu yake bila kukosa. “Amekuwa mmoja wa wafungwa wenye nidhamu ya hali ya juu na hakuna siku aliyokosa kuja na kufanya kazi kama alivyopangiwa,” amesema Nsanze alipoulizwa kuhusu utumikiaji adhabu wa msanii huo ulipofikia hadi sasa.

Kifungo cha Lulu kilipaswa kuisha Machi mwakani endapo asingebailishiwa adhabu ya kifungo gerezani na kuwa kifungo cha nje baada ya kupata msamaha wa Rais.Magereza ilifafanua kwamba ina utaratibu wa kutoa msamaha wa theluthi moja ya kifungo na msanii huyo alinufaika baada ya kuonyesha tabia njema.