Lulu Apiga Mnada Nguo Zake Kusaidia Wasiojiweza

Msanii wa filamu za Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ameuza  nguo zake kwa nia ya kusaidia watu ambao wanaishi katika mazingira magumu.

 

Siku ya Jumamosi, Januari 26, 2019 Lulu aliwakabidhi nguo  watu walionunua katika zoezi lake la kuuza baadhi ya nguo zake kwaajili ya kukusanya fedha ili kuwezesha project yake ya Save My Valentine, alilolenga kuwasaidia wasiojiweza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari, Lulu alisema kuwa kwa siku ile alikabidhi takribani nguo 36 kati ya 40 ambazo tayari zilikuwa zimeshapata wateja na kwamba mwitikio wa zoezi hilo umekua mzuri na unatia moyo kwa sababu watu wamepokea wazo lake vizuri na kumsapoti.

Mimi nina nguo nyingi sana, hivyo nilifikiria baadhi ya nguo kuzigawa bure kwa watu wasiyojiweza, lakini zipo nilizokuwa nikenda nazo kwenye events na shoo, nikaja na wazo baada ya kuona bora niziuze ili nipate pesa ya kuwasaidia watu wasiyojiweza ambao kwangu mimi nitasherehekea nao Siku ya Wapendandanao kama Valentine wangu, Februari 14.

Zoezi bado linaendelea, nitaposti tena jumatatu na watu wanaohitaji tutawasiliana ili wanunue. Ninafanya hivi kwa sababu nataka siku moja nikiondoka duniani niache alama ya mazuri niliyofanya, nimefanya mabaya mengi, nimepitia magumu mengi katika maisha yangu, lakini sasa hivi ni wakati wa kufanya angalau mema ili siku moja nikumbukwe kwa hiki ninachiokifanya”.

 

 

Lulu Adaiwa Kuwekewa Bodyguard Baada Ya Kuvishwa Pete

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amedaiwa kuwekewa ulinzi mzito na mume wake mtarajiwa Majizzo Baada ya kumvalisha pete.

Gazeti pendwa la Amani linaripoti kuwa tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.

Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone“.

Gazeti hilo lilithibitisha taarifa hizo wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.

Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.

Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa“.

Tangu ametoka gerezani miezi Michache iliyopita Lulu amekuwa na upepo wa bahati nzuri kwani amechumbiwa na Mpenzi Wake wa muda mrefu Majizzo na kumaliza kifungo chake rasmi.

Mama Kanumba Afungukia Ndoa Ya Lulu na Majizzo

Mama mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amefunguka na kusema yuko tayari kuhudhuria harusi Lulu endapo ataalikwa.

Mama Kanumba ambaye aliweka wazi chuki yake dhidi ya Lulu baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Marehemu Steven Kanumba ambapo alihukumiwa miaka miwili jela.

Mama Kanumba alifurahi baada ya kifungo cha Lulu lakini hivi sasa baada ya Lulu kuachiwa huru Mama Kanumba anafunguka na kusema wazi wazi kuwa hana chuki na Lulu na endapo ataalikwa Kwenye Harusi basi hatasita Kuhudhuria kwani hana kinyongo na Mrembo huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Mama Kanumba alifunguka haya:

Hapa duniani sina chuki kabisa na Lulu na mimi akili yangu kwa hivi sasa akili yangu imeegemea upande mmoja tu nao ni kumuomba Mungu tu maana yeye ndio anatoa haki sawa kwa tajiri na hata masikini pia”.

Lulu alivalishwa pete na mpenzi wake ambaye ni CEO wa EFM Majizzo ambapo ndoa yake inatarajiwa kufanyika Miezi ya mbeleni.

Lulu Afunguka Mazito Kuhusu Majizzo

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuongea mazito kuhusu mpenzi wake ambaye ni Mkurugenzi wa EFM, Majizzo.

Mwanzoni mwa wiki hii Majizzo alimvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi Lulu Ikiwa ni Miezi Michache tangu alipoachiwa huru kutoka kwenye  kifungo chake baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba.

Baada ya kuvalishwa pete Lulu alifunguka mazito juu ya mpenzi wake Ikiwa ni pamoja na kumshukuru kwa kuwa naye hata katika kipindi kigumu maishani mwake.

Lulu amesema kuwa mpenzi wake Msjizz amemvisha pete ya uchumba hivi karibuni  kama Baba kwake kwani ni mtu wa kuvaa uhusika tofauti tofauti hadi kumfanya ajisikie upendo wa Baba.

Huku machozi yakimtiririka Lulu alifunguka:

Tokea nimeanza kuwa naye nimefeel upendo wa Baba Kwenye Maisha Yangu kwa sababu kuna muda anatoa character ya upenzi na Nini anakuwa kama Baba na kipindi kifupi kilichopita tulipita katika wakati mgumu sana lakini Tunashukuru Mungu”.

Ingawa mwaka huu ulianza vibaya kwa Lulu lakini unaelekea kuisha vibaya kwani Lulu amebakisha mwezi mmoja ili kumaliza kifungo chake cha nje na baada ya hapo inasemekana atafunga ndoa na Majizzo na kuna tetesi za ndoa kuwa Dubai.

Mastaa Wapunguze Kudanga Waige Mfano Wa Lulu- Sabby Angel

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bongo Movie Sabrina Omary maarufu kama Sabby Angel amefunguka na kusema anamkubali sana Lulu na ni mfano wa kuigwa na kuwataka mastaa waige mfano wa Lulu.

Kuanzia Siku ya Jumapili Lulu ametawala headlines zote baada ya kuvalishwa pete ya uchumba  na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye ni CEO wa EFM, Majizzo.

Sabby Angel  amefunguka na kumpongeza Lulu kwa jambo alilofanya kwani badala ya kudanga na kuhangaika ametulia na mwanaume mmoja na sasa wapo mbioni kufunga ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sabby Angel ameandika:

Nimefurahi sana Tena sana kuamka na kuona picha za posa ya Lulu, For real am so happy anaonyesha mwenendo mwema yaani she is a role model. Mwanamke lazima stara. Mastaa wengine wafuate Mfano. Sio kudanga tu na kiki. Kuwa kioo cha jamii lazima uwe Mfano kwani mabinti wengi wadogo hutangalia sisi na kufuata tunayofanya”.

Sabby Angel ametengeneza headlines baada ya kuolewa ndoa yake ya tano baada ya Kuachika mara nne tayari.

Lulu Afunguka Baada Ya Kuvishwa Pete (Video)

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka baada ya kufanyiwa bonge la surprise na mpenzi wake ambaye ni CEO wa EFM Majizzo.

Sherehe hiyo iliandaliwa na Majizzo maalum kwa ajili ya watoto wake, lakini mambo yalibadilika ghafla, ambapo wakati sherehe ikiendelea, watoto waliwaita mbele baba ambaye ni Majizzo na Aunt yao ambaye ni Lulu.  Shughuli ya kuvalishwa pete ikafanyika huku Lulu akiangua kilio kwa kutoamini surprise aliyofanyiwa na mpenzi wake huyo.

Lulu ambaye alionekana mwenye furaha kupitiliza amefunguka na kusema engagement hiyo ilikuwa bonge la suprise kwani hakujua kama kutakuwa na jambo kama hilo.

Hii ni video ya mahojiano aliyofanya Lulu mara tu baada ya kuvalishwa pete usiku wa jana:

https://www.instagram.com/p/BoYijxUBZnb/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=yzyk138znv2z

Lulu na Majizzo sasa wameamua kuweka mahusiano yao rasmi baada ya kuishi kwenye mahusiano hayo kwa siri na inaelezwa mipango ya ndoa inafanyika na huenda ikafungwa mwaka huu wakawa mke na mume.

Majizzo Amchumbia Rasmi Lulu (video)

Mkurugenzi wa Kituo cha televisheni na Redio cha EFM, Majizzo amemchubia rasmi mpenzi wake ambaye ni staa wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Tukio hilo la Lulu kuvalishwa Pete ya uchumba lilitokea siku ya jana Kwenye hafla ya chakula cha jioni ambapo Majizo alipiga goti na kumuomba kumuoa.

Majizo aliposti video hiyo Kupitia ukurasa wake Instagram na kuandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BoXKhaHF2t9/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1uqnbmblgb8aa

RC Makonda Amtaka Majizzo Afunge Ndoa na Lulu Haraka

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amefunguka na kumtaka mkurugenzi wa EFM, Majizzo afunge ndoa na msanii Elizabeth Michael haraka iwezekanavyo la sivyo atamfunga.

RC Makonda amefunguka hayo Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari kwenye tamasha la Komaa Concert jana jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kutokana na imani yake hataki kuwaona marafiki zake wanakuwa mabachela na kuahidi kuwafunga jela endapo watakiuka ahadi zao za kuoa.

Marafiki zake aliwataja na kuwataka waoe mara moja ni pamoja na Majizzo, Leo Mutuz, Meya wa Kinondoni na kuhaidi kuwafunga endapo hawatafanya hivyo.

Nina ndoa kubwa tatu lazima nizisimamie na wasipooana nawafunga, moja ni Majizzo unajua mimi ni mkristo kwenye Biblia inasema wengine wataokolewa kwa moto. Sasa Majizzo tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu wameshakuja nyumbani tumeshafanya vikao vingi vya kupanga harusi.

Lakini kuna harusi nyingine ya Meya wa Kinondoni nimemwambia na yeye asipooa namfunga. Lakini kuna Lemutuz naye asipooa namfunga. Kwa hiyo kuna watu watatu hawa lazima mipango yao ya harusi ikamilike mwaka huu na waoe”.

Tangu Lulu atoke jela Kumekuwa na tetesi kuwa yeye na mpenzi wake Majizzo wapo katika mipango ya kufunga ndoa na hata Makonda alikuwa wa kwanza kutangaza Ndoa hiyo.

 

Hamisa Mobetto Atoa Baraka Zote Ndoa Ya Lulu na Majizzo

Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa hana kinyongo na kutoa baraka zote kwa ajili ya ndoa ya Lulu na Majizzo.

Hamisa amewahi kuwa kwenye Mahusiano na Majizzo siku za nyuma na  kuzaaa naye mtoto mmoja ameweka wazi kuwa hivi sasa hana matatizo na Majizzo wala Lulu hivyo kwake ni Poa tu wakifunga ndoa.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema kuwa hana kinyongo na Lulu kama ambavyo watu wanasema kwa kuwa mapenzi yake na Majizzo yalishakwisha siku nyingi.

Mimi na huyo anayetaka kumuoa tulishamalizana, hivyo hakuna tena hata chembe ya mapenzi zaidi ya uhusiano wetu wa kulea mtoto.

Kwa maana hiyo sina shida kusikia Lulu anaolewa na siku ya sherehe nikipewa kadi nitakwenda“.

Tangu Lulu atoke jela Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa yeye pamoja na mpenzi wake Majizzo wanategemea kufunga ndoa hivi karibuni na taarifa hiyo ilithibitishwa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda.

RC Makonda Atangaza Ndoa Ya Majizzo na Lulu

Mkui wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza rasmi kuwa Muigizaji wa Bongo movie Lulu Michael na Mkurugenzi wa EFM Majizzo watafunga ndoa hivi karibuni.

Kumekuwa na tetesi nyingi tangu Lulu atoke gerezani wiki chache zilizopita ikiwemo kuwa ni mjamzito na kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Majizzo.

Hatimaye Paul Makonda amethibitisha taarifa hizo baada ya kuandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ni mwenye kati wa shughuli hiyo ambayo itafanyika hivi karibuni lakini hajweza kutaja tarehe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram RC Makonda kaandika maneno haya:

Nikiwa mwenyekiti wa  kamati ya Harusi ya bwana Majizzo na Bi Elizabeth Michael (Lulu) nimeupitisha huu wimbo wa Mrisho Mpoto na Harmonize kuwa ndio winbo rasmi wa Harusi yao, kuhusu tarehe za harusi endelea kufuatilia 92.5 Dodoma”.

Mpaka sasa Maharusi Watarajiwa hawajathibitisha taarifa hizo.

Lulu alifungwa jela mwaka jana mwishoni baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia marehemu Steven Kanumba.

Majizzo: Lulu Wewe ni Mtu Wa Muhimu Kwangu

Mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa Kituo cha televisheni cha TV E na kituo ch redio cha EFM Francis Siza maarufu kama Majizzo amezidi kumkumbuka mpenzi wake Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Ikiwa leo ni siku ya kusheherekea kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Lulu ambaye yupo gerezani Majizzo amemkumbuka Lulu kwa kumuandikia ujumbe mzito wa kumkumbuka.

Lulu alifungwa miezi kadhaa iliyopita baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake na nguli wa filamu za kibongo Steven Kanumba.

Majizzo amemuandikia ujumbe huo mpenzi wake Lulu Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemtaka awe jasiri Lakini pia amemuhaidi kuwa yeye ni mtu muhimu sana maishani mwake: