Biashara Ziliniokoa Muziki Ulipotaka Kunizika

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ally timbulo ameweka wazi kuwa Biashara zake za ufugaji wa kuku ndio zilimuokoa kimaisha pale ambapo Muziki ulitaka kumzika  kiuchumi.

Timbulo ameweka wazi biashara yake aliyoanzisha ya kufuga kuku ndio imemfanya mpaka hivi sasa hategemei pesa za shoo peke yake kama wasanii wengine.

Kwenye mahojiano na , Timbulo alifunguka kuwa, aliamua kujishughulisha na mambo ya ufugaji baada ya kuona hawezi kukaa tu na kusubiria shoo maana kuna wakati zinakata kabisa hivyo hata pesa ndogondogo inakuwa ni shida.

Nina kuku 2,000 ambao nafuga na nina wauza kwa bei tofauti. Kuna wengine wanaanzia elfu 15 hadi elfu 40 kutegemeana na mbegu. Pia ninauza mayai, inanisaidia mimi na familia yangu”.

Wasanii wengi wamekuwa wakiishi katika maisha magumu wakati wakiwa na majina makubwa katika jamii hali iliyopelekea wengi wao kugeukia Biashara nyingine mbali na muziki.

Timbulo Adai Hataki Ukaribu na Wasanii Wenzake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Timbulo amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni msanii ambaye hataki sana ukaribu na Wasanii Wenzake.

Timbulo anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Sangoma’ amefunguka na kueleza sababu ambazo zinamfanya kutokuwa na ukaribu na Wasanii Wenzake wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Timbulo amekiri kuwa haonekani sana na wasanii wenzake akijichanganya kwa sababu hajawahi kupata mwaliko kutoka kwa wasanii hao.

Sionekani Kwenye events kama hizo za wasanii wengine kwa sababu sijaalikwa ila ningealikwa ningeenda na labda sijaalikwa kwa sababu mimi sijawahi kuwaalika lakini mimi utaniona Kwenye misiba ya wasanii wengine maana hakuna mialiko”.

Lakini pia Timbulo ameweka wazi kuwa hana ukaribu na Wasanii kwa sababu hataki mazoea sana na anataka kufanya kazi Kwenye sanaa kuliko mambo mengine Lakini pia amedai kuwa hawezi kuwa na ukaribu na wapinzani wake ambao ni wasanii wenzake.

Timbulo Amwaga Povu Kwa Wanaombeza Kwa Kumiliki Gari Aina Ya IST

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Timbulo amefunguka na kumwaga povu kwa mashabiki na wadau wote ambao wamekuwa wakimbeza baada ya kuona mafanikio yake yaliyotokana na muziki.

Timbulo amedai kusikitishwa na baadhi ya wadau wa muziki nchini Tanzania ambao wameonekana kushangazwa na  mafanikio yake baada ya kusikia kwamba kuna watu wanaona hastahili kumiliki vitu kama nyumba na magari.

Timbulo ambaye amekuwa akionekana mara kwa mara akianika mali zake Kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwemo nyumba na magari amedai anajiona anastahili kumiliki mali kama wasanii wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Timbulo amedai wasanii wa Bongo fleva  wanastahili kuwa na mali nyingi sio watu kushangaa yeye kumiliki gari kama IST.

Tunaona namna gani ambavyo tunajaribu kurudishana nyuma kwa sababu ukitazama namna ambavyo nimepambana mpaka kufikia leo, toka 2005 mpaka leo 2018, so ukiniambia leo si shahili kuwa hata na maisha ambayo naonekana nayo nakuwa roho inaniuma sana kwa sababu naona jinsi gani tunarudisha nyuma.

Sisi kama wasanii wa Tanzania tunastahili kuwa matajiri, tumefanya kazi kubwa sana, wenzetu mbele ngoma moja inabadili maisha yao, why mimi na ngoma zaidi ya 20 halafu mtu anashangaa mimi kulimiki IST”.

Siku za nyuma Timbulo ameshawahi kukumbwa na skendo ya Kuazima magari na kupiga picha ili kuonyesha kama ya kwake Kwenye mitandao tetesi alizozikana.

Timbulo Aomba Radhi Mashabiki, ni Baada ya Kukataa Kutoa Msaada.

Msanii wa bongo fleva Timbulo awaomba radhi mashabiki na watanzania kwa ujumla baada ya wiki iliyopita kupigiwa simu na watangazaji wa kipindi cha Shilawadu na kumtaka atoe msaada kwa moja ya vijana ambao alishawahi kufanya nao kazi katika muziki wake anaejulikana kama Emma ambae ni dancer katika video mbalimbali.

Mcheza shoo huyo amabe hali yake inaonekana kuwa mbaya sana kiafya amethibitisha kuumwa kwa muda mrefu sasa akisumbuliwa na kifua kikuu na kwamba amekuwa akinywa dawa ambazo inahitajika ela nyingi kwa ajili ya kununua vyakula na ukitegemea yeye ndie aliyekuwa baba wa familia yake.

Emaa anasema kuwa amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo Alikiba ambae ndie amekuwa msanii anaemsaidia na kumpa ela mara kwa mara kwa ajili ya matibabu lakini hawa wengine wamekuwa wakimkwepesha na hata kumkatia simu zake.

Wakiwa hapo hapo kwa mgonjwa Soudy Brown na Qwisah waliamua kumpigia Timbulo ili kumuelezea hali ya kijana huyo ndipo msanii huyo alikuwa akiwajibu vibaya na kukata simu, lakini msanii huyo ameamua kuja na kuomba msamaha na kukubali kumsaidia kijana mwenzake.

Unajua emma mimi nimdogo wangu ukiachana na kufanya nae kazi za sanaa kwaio sikupaswa kutangazwa kila kitu kuhusu kumtembelea,kwa kuwa tunapaswa kushare kwa misaada zaid naomba mnisamehe kwa niliemkwaza  au kuguswa kwa namna yoyote ile , kwa sasa nimesafiri baada ya pasaka nitarudi na nitaenda kumuona mdogo wangu, nawapongezz sana shilawadu , wakati mwingine tunaonaga kama jamaa simu zao zinakuwa za umbea au udaku kumbe zingine zinakuwa na maana, kwasasa naomba tumchangie emma kwa kitu chochote kama una mia, mia tano elfu tano  kwa namba yake lakini pia unaweza kumpigia na kumpa pole.

Abdu Kiba na Timbulo Ndani ya Bifu Nzito Baada ya Kuibiana Nyimbo

Msanii wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amejikuta kwenye mvurugano na msanii mwenzake Timbulo baada ya kituhumiana kuibina mashairi ya nyimbo.

Wasanii hawa wawili waliingia katika mgogoro mkubwa sana Timbulo na Abdu Kiba baada ya wote wawili kujikuta wanaimba mashairi yanayo fanana huku Timbulo akimtupia lawama na kumuuliza kwa nini atumie mashairi yake.

Kizaazaa hiki kilianza baada ya habari kusambaa kuwa kuna rekodi ambayo imefanywa na Timbulo na kumshirikisha msanii mwingine anayeitwa Promise ambayo inafanana kabisa mashairi na nyimbo mpya ya Abdu Kiba inayoitwa jeraha.

Baada ya hapo kilichotokea ni kila mtu anamrushia mwenzake maneno na kumlaumu kwa kumuibia mashairi. Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Timbulo amefunguka na kusema anamlaumu Abdu Kiba kwa kumuibia mashairi yake:

Mengi yatasemwa lakini ukweli utabaki pale pale mimi ninavyozungumza najua ukweli na Abdu na yule mtu anayehusika kwenye huu wimbo anaujua ukweli anajua stori yake ilivyo alafu kitu ambacho kimenikera tangia mwanzoni ni pale nilipoona wimbo umetolewa halafu wamekosea wamesema wimbo unaitwa promise wakati mwenye wimbo anaitwa promise na jina la wimbo hata silikumbuki lakini mimi namlaumu Abdu maana like alichokiimba Abdu mimi ndio nimetunga mashairi yote aliyoimba”.

Baada ya kutupiwa lawama hizo AbduKiba alifunguka na kusema nyimbo ile kapewa na Promise ambaye ni mmiliki wa nyimbo hiyo na yale mashairi yote yaliandikwa na yeye mwenyewe lakini baadae Timbulo ndio aliomba kuimba mashairi hayo. Abdu Kiba alitoa povu zito huku akidai kuwa Timbulo amemdhalilisha kwa kumnyooshea kidole na kumtuhumu kwa wizi.

Timbulo Aamia Kwa diamond, Mashabiki Wamshangaa

Msanii ambae kwa sasa amekuja na kibao chake kipya kinachojulikana kama vibaya , timbulo ameamua kufunguka yale anayo-feel kwa msanii mwenzie mkubwa duniani Diamond Platinumz huku akisema kuwa moja ya nyimbo za Diamond ulikuwa umefanana sana na wimbo wake ambao aliacha kuutoa baada ya kuona msanii huyo ameutoa.

Timbulo anasema kuwa alikuwa akiupenda sana wimbo wa Utanipenda ambao na yeye pia alitaka kuutoa lakini aliumi sana alipoona wimbo hio Diamond ameutoa, lakini ilikuwa ni copy yake.

Mimi niliwahi kumtamani Mond katika wimbo wa Utanipenda ,nilikuwa nimepotea kwenye game sijatoa ngoma muda mrefu sana , nilivyomsika jamaa kitu amekifanya kwenye ule wimbo ni copy ya  kile kitu na mimi pia nilikuwa nimeimba na kutamani kukifanya , kwanza nilipenda sana lakini baadae niliumia kwa sababu it was my sort.

Kwanza kwa namna kubwa sana  kuanza story sasa nikaanza kupita na meleody zangu  lakini ile story yenyewe aliyoimba yeye  alafu ukija kitu alichokuja  kukifanya kwenye  video, melody, maandiko kila kitu cha kwenye ule wimbo  it was perfect kwa upande wangu

Hata hivyo baada ya msanii huyo kuyaongea hayo mashabiki wake na mashabiki wa Diamond ambao wanajua muziki wa wasanii wote wawili wamemjia juu Timbulo na kuwambia kuwa aache kutafuta kiki kupitia mgongo wa Diamond kwa sababu hawezi kujifananisha na Diamond hata kidogo na hizo habari za wimbo wa Utanipenda sio kweli kuwa Diamond anaweza kufanya copy yake hata mara moja.

Mashbaiki hao waliendelea kusema kuwa wamekuwa wakimshangaa msanii huyo kwa sababu hivi karibuni alikuwa akisema kuwa Diamond kufanya kolabo na wasanii wa nje  sio kitu kizuri na kinaua muziki wa bongo , iweje leo aseme kuwa alikuwa anaupenda sana wimbo  Utanipenda wa msanii huyo huyo tena.

Mo Music Ndani Ya Bifu Zito na Timbulo

Mwanamuziki wa bongo fleva aliyetamba na vibao kama ‘basi nenda’ No music amefunguka na kudai kuwa anahisi kuwa Timbulo ana bifu naye kwa sababu amekuwa hapokei Simu yake akimtafuta.

Mo music alikuwa chini ya management ya Timbulo na McDenis lakini baada ya muda alihama na kuhamia management nyingine lakini baada ya kuhama aliamua kumaliza bifu na msanii mwenzie Timbulo lakini cha ajabu ameshangaa kuona kuwa anampotezea na kukataa kupokea Simu yake ili waweze maliza tofauti zao.

Mo music ameyaongea hayo kwenye mahojiano na Lilommy ambapo alifunguka mambo yafuatayo;

Kwanza mimi sijawahu kuwa na bifu na Timbulo maana mimi sijawahi kumchunia ila mwenzangu nimejaribu sana kumtafuta nimejaribu sana kumpigia Simu lakini anakuwa hapokei simu yangu lakini mimi namheshimu sana Timbulo maana ni moja ya watu wameweza kunisaidia mimi kuwa Mo music na pia ni kaka yangu alafu isitoshe amewahi kuwa kwenye gemu kuliko mimi kwaiyo kilichotokea ilikuwa ni misunderstanding kati yangu na yeye mimi nilikosea lakini na yeye pia alikosea baadhi ya vitu ambapo kuna mambo aliyazungumza kwenye media badala ya kunitafuta mimi kama mdogo wake tuyamalize wenyewe kwangu mimi niliona kama ameni disrespect kwa kweli”.

Timbulo alipotafutwa ili aongelee ishu hiyo alifunguka na kudai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Mo music ila kama kweli hajamkosea ni kwanini ameenda kumuomba radhi redioni?Timbulo amedai kuwa tangu Mo music amehama uongozi amekuwa akitafuta kiki kupitia jina lake.