Aslay Anatarajia Kumpa Kolabo Diamond

Mwanamuziki anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘natamba’ Aslay amesema anatarajia kumpa kolabo msanii mkubwa wa bongo fleva, Diamond Platnumz.

Aslay anayesifika kwa kutoa nyimbo mara kwa mara na sio bora tu nyimbo bali nyimbo zinazopendwa na mashabiki zake amesema kuwa anategemea kuachia nyimbo yake mpya hivi karibuni.

Mtayarishaji wa muziki hapa nchini, Shirko ambaye pia ndiye aliyeandaa nyimbo mbili za Aslay ambazo ni ‘natamba’ pamoja na ‘natamba’ amesema kuna uwezekano Mkubwa ambao wanatazamia kufanya ‘remix’ ya ngoma hiyo ambayo tayari inafanya vizuri ya ‘natamba’ na msanii pekee wanayemwangalia ili ashirikiane na Aslay kwenye wimbo huo si mwingine bali ni Diamond.

Diamond ambaye tayari na yeye anahit na wimbo wake wa ‘halelujah’ uliovunja rekodi na Kuwait msanii wa kwanza Tanzania kufikisha waangaliaji milioni moja kwenye mtandao wa Youtube ndani ya masaa kumi na tano. Pia na Diamond alishawahi kusema Kuwait angependezwa zaidi kama angepata nafasi ya kufanya kazi na Aslay kwaiyo bila Shaka utakuwa wakati mzuri kabisa kuwapa mashabiki zao kile kitu wanataka.

Aslay amezidi kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa youtube kwani kwenye wiki ya kwanza video ya wimbo huo kutoka alimtoa Diamond kutoka kwenye namba moja na kuishikilia kwa wiki kadhaa mpaka alipokuja kutolewa juzi na msanii kutoka wasafi Harmonize na wimbo wake wa ‘shululu’.

 

Aslay Azungumzia Wasiwasi Aliokuwa Nao Kufanya Kazi Mwenyewe.

Msanii anaefanya vizuri sasa katika muziki Aslay amefunguka na kuongelea wasiwasi aliokuwa nao kipindi anaanza kufanya muziki peke yake bila kuwa chini  ya Mkubwa Fella.Aslay ambae alianza muziki wake akiwa  na umri mdogo sana na wimbo wake wa kwanza wa  naenda kusema kwa mama akiwa chini y ameneja wake  Mkubwa Fella, baada ya muda meneja huyo alitengeneza band ambayo pia Aslay alikuwepo .

Hata hivyo baada ya kukaa katika band zaidi ya miaka mitatu , kundi ilo lilikuja likavunjika huku hakuna sababu ya msingi inayosemwa na mtu yoyote kutoka katika uongozi wa kundi ilo na kufanya Aslay sasa kuanza kufanya kazi zake.Hata hivyo Aslay amefunguka na kusema kuwa  baada ya kuvunjika kwa kundi aliwaza kuanza kazi peke yake lakini alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwani aliamini kuwa bila kuwa na mkubwa hatoweza kufanya kitu chochote katika muziki na akawaza kufanikiwa, lakini baadae alikuja kupata moyo baada ya kuongea na meneja wake mpya anaejulikana kwa jina la Chambuso na kuanza kufanya kazi mwenyewe.

‘Nilikuwa na wasiwasi sana kama tutaweza kusonga bila kuwa na mkubwa nyuma yetu,au menejiment yoyote nyuma yoyote,lakini baada ya hapo nilimtafuta Chambuso na yeye akaniambia kuwa tutaweza  kusonga mbele,hivyo tupige kazi,  na kweli tukaanza kupiga kazi na ninakumbuka yimbo yangu ya kwanza  ilikuwa inaitwa angekuona nilianza kuifanya peke yangu na  niliiachia katika tv na radio  mbalimbali,huo ndo wimbo unaonigusa  kutoka moyoni sana kwa sababu unaongelea maisha yangu  halisi kabisa“Aliongea Aslay

Aslay alikwa katika kundi la Ya Moto chini ya manejementi ya Mkubwa Fella na Chambuso lakini baadae kundi hilo lilikuja likavunjika ivyo kusababisha wasanii wote kusambaratika, hata hivyo wapo baadhi ya watu katika mitandao waliokuwa wakisema kuwa wasanii hao hawataweza kuendela vizuri katika muziki kwa sababu alikuwa akiwasimamia kimuziki ambae ndie Mkubwa Fella ndie alikuwa akilimudu kundi ilo lakini maneneo hayo yamekuja kuonekana ni tofauti baada ya Aslay kuweza kufanya kazi peke yake.

Kama ilivyo kawaida kwa mashabiki huwa hayakosekani ya kuongea ndivyo ilivyo kwa sasa kwamba inawezekana Aslay kuwepoa katika band ilikuwa inabana na kuficha kipaji chake, lakini baada ya kutoka ndio kazi na juhudi zake zinaanza kuonekana.

Aslay Aomba Hasifananishwe Na Alikiba

Msanii ambae kwa sasa hivi anafanya vizuri sana kwa katika kazi zake za muziki na amekuwa akiongoza kwa kutoa ngoma mpya kila siku na kupokelewa vizuri na mashabiki  wake amawataka mashabiki wake kutompambanisha na msanii mwenzie Alikiba au msanii yoyote ambae yeye anaona hajamfikia kiwango chake.

Katika mitandao ya kijamii  kumekuwa na tabia ya baadhi ya mashabiki kuweka mipambanisho ya wasanii mmoja na mwingine kitu kilichotokea pia kwa Alikiba na Aslay ambapo watu wanataka kuona ukali wa msanii Alikiba na msanii Aslay katika kutoa ngoma na je ni msanii gani anapendwa na mashabiki wengi,hata hivyo msanii huyo ameombwa kutokufananishwa na msanii alikiba kwa sababu kiwango chake na kiwango cha msanii Alikiba viko tofauti sana.

Akiongea na eNews ya EATV,Aslay anasema hata kama yeye kwa sasa anafanya vizuri lakini bado hawezi kufananishwa na msanii mkongwe kama alikiba ambae amekuwa mkongwe katika game kwa muda mrefu , kazi yake imekuwa ikionekana kimaifa lakini pia hata kipaji chake akiwezi kufananishwa na cha msanii alikiba ambae tayari alishapitia mambo mengi katika muziki na bado ana mambo mengi ya kujifunza kwa msanii mkubwa kama Alikiba.

“sio kitu kizuri kwa upande wangu kwa sababu alikiba kazi yake inaonekana na anafanya vizuri,kwahiyo ukisema  unanipamabnisha  mimi na alikiba itakuwa sio picha nzuri na sio  alikiba tu bali hata msanii yeyote msinipambanishe naye, ambaye tayari yupo level zingine” anasema Aslay

Aslay ambae kwa sasa anakuwa akifanya vizuri na vibao vyake vipya kama Pusha, Baby ,Likizo na hichi kipya cha Natamba amekuwa msanii aliyeshika kasi na amekuwa akifanya vizuri katika majukwaa.Aslay ambae kipaji chake kimeanza kuonekana tangu akiwa bado mdogo na baadae akaanza kuimba kwatika band ya Ya Moto Band,yeye ndie alikuwa msanii ambae alikuwa akionekana nyota kuliko wasani wengine.ingwa kwa sasa band aliyokuwa akifanyia kazi kuvunjika bado Aslay ameweza kuasimama peke yake na kuendelea kufanya vizuri zaidi kuliko wenzake wote.

Waliotaka Kumshusha Aslay Wamekwama Kwa Hili

Msanii wa Bongo Fleva anaefanya vizuri sana katika muziki kwa sasa na amekuwa akipendwa na mashabiki kutokana na uzuri wa nyimbo zake, Aslay ambae hivi karibuni amekuwa akitoa nyimbo mfululizo na kupokelewa vizuri kabisa na mashabiki  bila kujali interval ya wimbo mmoja na mwingine.

Siku chache zilizopita baada ya Aslay kutoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Natamba, na kuanza kufanya vizuri katika channel ya Youtube, iliripotiwa kuwa wimbo huo umefungiwa katika channel iyo kuwa hauruhusiwi kuonekana public kwa watu bali watazamaji lazima wawe juu ya miaka 18, kwa sheria za channel iyo iliwataka waangaliaji kujisalili na kufuata masharti ndipo waweze kuona au kuupakua kutoka katika account hiyo.

Hata hivyo, baada ya kufuatilia kwa muda na baadhi ya watu wake wa karibu kuangaika, wakishirikiana na bosi wake anaejulikana kama MxCarterm alitatua tatizo hilo na kuwajulisha mashabiki wake katika ukurasa wake wa instagaram.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram baada ya kutatua tatizo ilo, MxCarter aliandika”usiyempenda karudi” huku akiweka picha ya msanii huyo.

Akaunti hiyo ya msanii Aslay inaonekana kuwa hacked na watu wasiojulikana huku lengo lao likiwa halijajulikana , lakini kitendo kama icho kinafanya kutokuonekana kwa musiki huo kwa mashabiki hivyo kushusha idadi ya mashabiki,Aslay kwa sasa amekuwa akifanya vizuri sana katika kazi zake pamoja na kuvunjika kwa kundi lao la Ya Moto Band ambalo lilikuwa pia lilikuwa likifanya vizuri, lakini hata baada ya kuvunjika kwa kundi hilo , Aslay amekuwa akikaririwa akisema haijamfanya hashindwe kuendelza muziki wake.

Hivyo kama kuna watu walikuwa na lengo la kufanya muziki wa Aslay kushindwa kuwafikia mashabiki , basi swala hilo halijafanikiwa.Pia tunatoa pole kwa msanii huyo kwa maswahibu hayo yaliyomkuta.

 

Huu Ndio Ushauri Wa Mama Ashura Kwa Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amezidi kupanda chati katika chati mbalimbali za redio na televisheni kupitia nyimbo zake zinazofanya vizuri sana kwa hivi sasa.

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu TV Mama Ashura amekuwa mmoja kati ya watu waliompongeza na kumpa ushauri Aslay, kupitia ukurasa wake Instagram Mama Ashura alimuandikia ujumbe huu;

“Nimeona niongee na mdogo wangu Aslay, kiukweli unafanya vyema na inaonekana unajua unachokifanya, muziki unaujua na pia kipaji unacho Big up Sana!”.

Pia aliendelea kufunguka kuwa;

“Kama ilivyotokea kwa wasanii wenye uwezo kama wako, waliposifiwa sana wakajisahau na kudhani kuwa wameshawini wakajikuta majina yamebaki juu alafu kazi zipo chini. Spirit yako nazidi kuiona kila siku nakutabiria miezi michache ijayo tutakuona kwenye level za kimataifa zaidi, lakini kuwa makini na baadhi ya mashabiki ambao sasa wanakuja kwako kwa wingi kutoka kila mahali kuna wengi ni fake fans ambao hata ukiboronga utasikia Aslay kaboronga vizuri na makofi wanakupigia badala yAslay.ukosoa ili uendelee kufanya vizuri  yangu ni hayo tu naendelea kufurahia natamba bonge la songi.

Aslay anatamba na wimbo wake wa ‘natamba’ ambao kwa sasa unashika chati sana na video ya wimbo huo umempindua Diamond na wimbo wake wa hallelujah huko YouTube alipokuwa anaongoza na kwa sasa anaongoza Aslay.

 

 

Sababu Za Aslay Kutoa Nyimbo Mpya Kila Siku

Ile tabia ya bandika bandua kwa Aslay haiwezi kukoma kwa kipindi hiki kwa sababu kadri watu wanavyozidi kusema kuhusu tabia ya baadhi ya wasnii kutoa nyimbo mpya kila siku ndo kwanza yeye anazidisha.Aslay ambae kwa sasa nafanya vizuri kabisa katika muziki na amekuwa akitoa nyimbo mfululizo na zote zinapokelewa vizuri na mashabiki wake.

Wiki iliyopita msanii huyu alitoa wimbo mwingine mpya alijulikan kama ‘natamba’, wimbo ambao  baada tu ya kutoka ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya mashabiki kuonekana kuuelewa sana,wimbo huu.Hivyo Aslay amuamua kufunguka na kutoa sababu za ya yeye kutoa nyimbo mpya kila siku.

Akiongea na EA Radio katika kipindi cha Planet Bongo  Aslay alisema kuwa kwa sasa inambidi atengeneze nyimbo zake mwenyewe ili aweze kuepukana na kuimba nyimbo za band katika show kwa sababu kwa sasa afanyi kazi na band”tangu nimetoka kwenye band nimekuwa  nikifanya kazi peke yangu, nategemea show zangu  na nyimbo zangu tu sio nyimbo za band tena,ndio maana nafanya kutoa nyimbo nyingi,ilimradi hata nikipata show  niwe natumia nyimbo zangu” alisema Aslay

Ikimbukwe kuwa Aslay alikuwa katika kundi la Ya Moto Band lililokuwa likiundwa na vijana wanne lakini kundi ilo kwa sasa limevunjika na kila mtu anafanya kazi peke yake huku yeye Aslay akiwa chini ya meneja  wake Chambuso na Maromboso ikisemekana kuwa amesajiliwa katika Lebel kubwa  kabisa Tanzania ya Wcb, wengine bado wapo kimya.

Hata hivyo Aslay anaonekana kujiamini na kile kitu anafanya na anasema kuwa ni kwasababu kazi zake nzuri na zinapokelewa vizuri na mashabiki, neno ambalo sio mara ya kwanza kwa msanii huyu kulisema”kingine natoa kazi nyingi kwa sababu ni nzuri,kazi nzuri ikikaa  ndani huwa naagopa  kwa sababu naogopa  idea ya kugongana , kazi nzuri ukitoa leo na nyingine ukatoa kesho watu watapenda tu kwa sababu ni nzuri”  alimalizia Aslay.

Hivi karibuni msanii huyo ametoa nyimbo kama ‘mhudumu’, ‘pusha’,’likizo’ na ‘baby’ na zote zinafanya vizuri sokoni.

Fella Hamiliki Muziki,-Chambuso Aongea.

Ya Moto Band ni moja ya kundi kubwa la muziki lililokuwa limeteka sana hisia za mashabiki wa Bongo Fleva nchini kutokanana kazi nzuri waliyokuwa wakiifanya  katika muziki , kundi hilo  ambalo liliundwa na vijana wadogo waliokuwa wanachipukia kimuziki lakini walikuwa wakifanya vizuri. kKwa bahati mbaya kundi ilo lilikuja kusambaratika na vijana wote kuanza kufanya kazi kwa kujitegemea huku Aslay akiwa chini ya menejenti mpya  ya Chambuso.

Kabla ya kundi ilo kuvunjika lilikuwa likiongozwa na Chambuso pamoja na Mkubwa Fela na kuunda lebel iliyokuwa ikijulikana kama Mkubwa na wanawe  na moja kati ya kundi lililoundwa lilikuwa ni Ya Moto Band, ambalo hivi sasa limekufa.Hata hivyo baada ya kundi kuvunjika Chambuso aliamua kuanzisha lebel yake mpya  na  alipomchukia Aslay kama msanii wake.

Kumekuwa na  tetesi zinazoendelea  kwa baaadhi ya watu wakisema kwa endapo msanii akitoka kwa Mkubwa Fellla basi na muziki wake umekufa, Chambuso anakanusa maneno hayo na kusema kuwa“Wanaosema kwamba muziki upo kwa  peke yake, kwamba ukianzia kwake na ukatoka basi hautaweza kufanya vizuri tena, wanakosea na hakuna kitu kama hicho”

Chambuso anasema kuwa mfano mkubwa ni kutoka kwa aslay ambae ametoka kwa mkubwa fella na sasa hivi anafanua vizuri na kazi zake za kimuziki “Mbona Aslay  anafanya vizuri sana na hayupo kwa Fella? Msisahau kwamba hata yeye huu muziki alizaliwa na akaukuta, kivipi ishindikane msanii kutoboa  kisa hafanyi kazi naye, hicho kitu sikiamini.”anaongezea Chambuso

Hata hivyo maneno ya meneja mpya wa Aslay yanaweza kuthibitika kwa sababu tangu aslay amekuwa na menejiment mpya amekuwa akifanya vizuri na kila siku amekuwa akitoa nyimbo mpya ambazo zinapendwa sana na mashabiki, hivyo kufanikiwa kimuziki kwa msanii itategemea na nidhamu na juhudi anazokuwa nazo msanii binafsi katika kuifanya kazi yake ya sanaa.Tangu kuvunjika kwa kundi ilo Aslay ndio anayesikika sana katika muziki akifatiwa na  Beka ambae pia ametoa wimbo mpya wa Libebe na  Sikinai hivi karibuni.

 

Sitegemei kushuka kimuziki-Aslay

Mwanamuziki wa Bongo Fleva  ambae hivi karibuni amekuwa akitoa nyimbo nyingi kwa mfululizo na nyimbo zote kupokelewa vizuri na mashabiki , Aslay amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa wala hategemei kabisa kushuka kimuziki kwa sababu anaamini nyimbo zake ni nzuri na anaamini nyimbo zake zinapendwa sana.Aslay ambae hivi karibuni mashabiki walimpachika jina la Chris Brown wa bongo  na majina mengine lukuki amesema kuwa kwa upande wake muziki ameanza tangu akiwa mdogo hivyo amekuwa nao hategemei kuchuja katika kazi hiyo.Pamoja na kuvunjika kwa kundi lao lililokuwa linatikisa sana nje na ndani ya nchi kundi la ya Moto Band bado anasema kuwa hiyo kwake haiwezi kuwa sababu kwani wakati anaanza muziki alianza peke yake.

“Nilianza muziki nikiwa peke yangu  na nilikuwa mdogo kiumri , enzi zile za naenda kwa mama  ila niliweza kufanya vizuri  kwaiyo kuingia kwenye kundi na kutoka  sioni kama nitashindwa kufanya  niendelee na muziki nwangu ” anasema Aslay

Kwa Aslay kuvunjika kwa kundi hakuumaanishi kuwa ndio mwisho wa kazi zake kwa sababu anaona hakuna kilichobadilika kabisa, na anaongezea kwa kusema kuwa “kwa sababu naona ni kama zamani tu,ndio maana nafanya vizuri tu , naachia ngoma kila kukicha na ngoma zangu  kali na zinapendwa , mashabiki hawawezi kuzichoka  kwa sababu mimi ni msanii mzuri najua nini ninachokifanya  na sitegemei kushuka kimuziki.”

aslay ameanza kufanya kazi peke yake baada ya kundi lao lilikuwa likifanya vizuri  kundi hilo lilikuwa likijulikana  na kufanya vizuri katika vibao vyake kama  nitakupwelepweta, Cheza kwa Madoido, Niseme Nisisema na Su waliomshirikisha mwanadada  Ruby, kundi ilo lilikuwa likiundwa na Enock Bella, Maromboso na  Beka Flavour pamoja na Aslay mwenyewe.

Aslay ambae sasa ni baba wa mtoto mmoja anavuma kwa nyimbo mpya kwama Pusha, Baby, Mhudumu, na  Likizo ambazo zote zimetolewa kwa kufuatana na zote zinafanya vizuri katika vituo vya radio na televisheni lakini pia mashabiki wamempokea vizuri katika jukwaa la fiesta tamasha linaloendelea sasa hivi nchini.

Lady Jay Dee: Mimi ni Shabiki Mkubwa wa Aslay

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva nchini Lady jay dee ambaye ni mkongwe wa mziki huo tangu miaka ya 90 ambaye pia anaweza kuwa mmoja kati ya wasanii bora wa kike Afrika Mashariki nzima kutokana na ukongwe wake na kutochuja kwenye fani na kuweza stahimili kukaa kwenye chati kwa miaka yote hiyo.

Mwanamuziki huyo amekiri kipaji cha Aslay na kusema  kuwa anamkubali, Aslay ni msanii anayekuja kwa kasi ya ajabu sana katika mziki huu wa Bongo fleva. Aslay ambaye amejitoa katika kikundi cha Yamoto Band hivi karibuni amekuwa akitoa nyimbo nzuri kutokana na staili yake hiyo ya kuimba nyimbo zake kwa hisia kali. Aslay tangu ameanza kufanya muziki kama Solo Artist ameweza kufikisha views milioni kumi katika chaneli yake ya Youtube.

Lady Jay Dee alieleza haya alipokuwa katika kipindi cha THE PLAYLIST wakati ambapo alitakiwa kuchagua nyimbo tano anazozipenda ambapo mojawapo ilikuwa nyimbo ya Aslay “Muhudumu” na kufunguka kuwa  yeye ni shabiki mkubwa wa msanii huyo na muziki wake na kwasababu ana melodies za kipekee na nzuri sana kwenye nyimbo zake.

Lady Jay Dee ametoa nyimbo yake mpya inayoitwa “I miss you” inayofanya vizuri redioni na pia Aslay naye ana nyimbo kadhaa zinazofanya vizuri alipoulizwa kuwa endapo watashirikiana kufanya kazi mbeleni alijibu kuwa atafurahi ikiwa hivyo.

Aslay akataa kuwepo kwa Bifu kati yake na Beka

Mwanamuziki wa kizazi kipya Aslay Isihaka akataa kuwepo  kwa bifu kati yake na mwanamuziki mwenzake kutoka Yamoto Band Beka. Wanamuziki hao walisemekana kuingia kwenye ugomvi mara baada ya kundi hilo la Yamoto band kuvunjika na kila mtu kuanza kuimba mwenyewe.

Baada ya kutengana kwa kundi hilo habari za kutoelewana baina ya wanakundi hao zilianza kuenea na ushindani baina yao ulianza  ambapo Aslay alikuwa akiachia nyimbo mpya basi na Beka anaachia nyimbo nyingine hali iliyopelekea tetesi hizo kuzidi kukua katika mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano aliyoyafanya Aslay hivi karibu alikataa kuwepo kwa bifu baina yao na kusema yafuatayo:

“Mimi Beka ni mwanangu halafu hatuna tofauti yoyote hadi naondoka huku ananibless mwanangu fanya kitu,ila kuna watu wanatengeneaz genge kwa msanii yoyote anayetoka Yamoto lakini everything is good.watu wanadai mi nataka kumfunika Beka ila sio kweli mi natoa nyimbo kwa maslahi yangu mwenyewe alfu mi siwezi kuwa na na bifu na Beka kwa sababu mi ndo nimempokea Beka na nimemlea na ninamuombea kwa mwenyezi Mungu aendelee kufanikiwa”.

Aslay alikuwa msanii kiongozi na mwenye kipaji ndani ya Yamoto band ambayo iko chini ya Mkubwa Fela ambaye pia ni meneja wa Diamond, baada ya kujitoa kwenye kundi hilo lilisababisha mpasuko hadi watu kudhani kuna ugomvi baina ya wasanii hao. Kwa sasa Aslay ni mwanamuziki wa kujitegemea na anatamba na nyimbo zake zinazofanya vizuri kwenye chati mbalimbali nchini.

Aslay apagawisha jukwaa la fiesta Arusha,nyimbo zake zote zaimbwa.

Ikiwa imepita siku moja tu tangu tamasha la fiesta lizinduliwe rasmi tarehe 9 septemba ,mkoani Arusha ambapo tamasha ilo hujumuisha wasanii wengi wakubwa na wachanga  nchi Tanzania na hata nje ya nchi,msanii kutoka Tanzania aliyekulia kwenye muziki tangu akiwa na umri mdogo ameacha historia ya kuliteka na kulitawala jukwaa .Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha “pusha”.

Aslay  hivi karibuni amefululiza kutoa nyimbo nyingi,na licha wa upya wa nyimbo izo bado mashabiki wake walionekana kuimba nyimbo zote tena bila kumpa nafasi msanii huyo kuiba na kipaza sauti,mashabiki walionekana kuwa na mzuka wa kila nyimbo alikuwa anaianzisha kitu kilichamfanya Aslay kushindwa kabisa kuimba muda mrefu,lakini hii ni dalili tosha kuwa msanii Aslay amekuwa akikubalika na kufatiliwa na mashabiki wake kwa ukaribu sana.Aslay alisikika akiwaambia mashabiki zake kuimba hadi kiitikio huku mashabiki wakionekana kuwa na shangwe la kutoka katika kila wimbo aliimba hadi wimbo mpya uliotoka hivi juzijuzi wa pusha.

Hata hivyo kwa hivi karibuni Aslay ameonekana kulitawa vizuri jukwaa na kupokea shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki wake akiwa jukwaani mfano mzuri ni katika tamasha la hivi karibuni la  usajili wa  tigo fiesta na show ndogo iliyoandaliwa mkoani Mtwara na kituo cha television cha clouds Tv show  inayojulikana kama ‘jiwe la mwezi’  yenye lengo la kutoa zawadi kwa msanii alifanya vizuri kwa mwezi huo,huku mashabiki wakionekana kumpa sapoti kubwa alipokuwa jukwaani.

Hongera kwake bwana Aslay tunaamini mafanikio haya yataendelea kwa show zote za fiesta zijazo na matamasha mengine pia.keep it up!

Beka Flavour: Mimi ndiyo Justine Beiber wa Bongo

Msanii aliyekuwa katika kundi ya Yamoto Band – Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa yeye ndo Justine Beiber wa Bongo.

Akiongea na E-Newz ya EATV, Beka alisema kuwa yeye sasa ameachana na mambo ya kiki kwasababu anataka kuboresha muziki wake.

“Siku hizi hamna muziki wa maneno mengi na kiki sema mimi nilikuwa naona vile vitu vilikuwa vinaendelea mtandaoni. Ukweli hamna kitu kama hicho mimi nafanya muziki wangu binafsi halafu ninaamini ni wakwangu, mimi ndiyo Justine Beiber wa Bongo,” amesema Beka Flavour.

Beka Flavour

Staa huyo pia aliwakashifu wanahabari kwa kumliganisha na Aslay ambaye alikuwa naye Yamoto Band. Beka alisema kuwa yeye hafanyi muziki ya ushindani na kuongeza kuwa hana tatizo na msanii wowote wa Bongo.

“Wanatakiwa watusapoti, siyo poa wanavyoandika wanatushindanisha halafu mimi sifanyi muziki wa ushindani na miaka 100 siwezi nikafanya muziki wa ushindani sina tatizo na msanii yeyote kutoka Tanzania.”

 

Beka Flavour: Aslay si msanii mkubwa kwamba mimi nimuogope. Ali Kiba ndo anaweza

Msanii Beka Flavour sasa anavurugana na Aslay kuonyesha ubabe katika muziki. Bifu yao ni kama ile ya Ali Kiba na Diamond igawa bado haiwezi.

Ubishi kati ya Beka Flavour na Aslay unadhihirika jinsi wanavyoachia nyimbo zao zikifwatana. Akiongea na eNewz, Beka Flavour alisema hawezi kumruhusu Aslay kutoa ngoma bila yeye kuachiza nyimbo zake zishindane na za hasimu wake.

“Nimepanga kuachia wimbo mpya wiki mbili zijazo lakini kama Aslay akiachia tena kazi mpya sitaweza kumvumilia na mimi nitaachia mashine ili zipambane mbele kwa mbele maana mimi nimeshapanga ratiba zangu na siwezi kuzivunja,” Beka Flavour alisema.

Beka Flavour

Staa huyo hata hivyo alisema Aslay sio msanii mkubwa wa kumuangalia wakati anafanya kazi zake, alidai kuwa Ali Kiba ndiye kioo chake Tanzania.

“Mimi natoa nyimbo zangu kulingana na jinsi ambavyo nimepanga ratiba yangu na uongozi wangu. Sijashindwa kuachia wimbo eti kwa sababu Aslay katoa ngoma mpya ila matatizo niliyopata ya kupelekwa polisi ndiyo yaliyonifanya nisogeze vitu mbele. Aslay siyo msanii mkubwa kusema kwamba mimi nimuogope au nimfikirie. Hapa nchini msanii mkubwa ni Alikiba na ndo kama kioo najitazama lakini siyo Aslay. Mimi natazama wasanii wakubwa nje ya nchi lakini siyo ndugu yangu,” Beka Flavour alifunguka.

 

Aslay aeleza kwanini hawezi kubali kusainiwa Wasafi

Dogo Aslay ambaye yuko katika lebo ya Mkubwa na Wanawe amefunguka na kusema kuwa hawezi kubali kujiunga na lebo ya Diamond Platnumz – Wasafi.

Staa huyo wa Yamoto Band ambaye ameanza kutoa nyimbo zake binafsi amesema kuwa malengo yake yamezidi kuwa msanii wa Wasafi ya Diamond.

Aslay

Aslay alieleza kuwa mipango yake ni kufikia kiwango cha Diamond na Ali Kiba kwa hivyo hawezi kusainiwa na Wasafi kama anataka kufikia malengo yake.

“Kusainiwa WCB hapana, kwa sababu mimi nina ndoto za kuwa zaidi ya WCB au kuwa zaidi ya kitu kingine chochote, naamini nitakaza nitafika hizo sehemu, naweza kusema nina ndoto za kufika kama alipofika Chibu, nina ndoto za kufika kama alipofika Ali Kiba. Inabidi nikaze niwe mimi kama mimi nitafute njia ya kutoboa nifike level hiyo, yaani sio yeye pekee yake mtu yeyote, wakisema wanisaini siwezi kukubali sasa hivi”  Aslay alisema katika kipindi cha XXL ya Clouds FM.

 

Aslay avutwa kwenye mgogoro baina ya Diamond na Ali Kiba

Aslay sasa ni miongoni mwa wasanii ambao wamejipata pabaya kwa kuonekana kujihusisha na Ali Kiba.

Msanii huyo wa Yamoto Band alisemekana kuwa eti atatoa wimbo na Kiba hivi karibuni, madai ambayo yanaonekana kuwa uvumi tu.

Meneja wa Aslay, Chambuso, amemtetea msanii wake huyo kuwa hajawahi kuwa na ukaribu wowote na Ali Kiba.

Akiongea katika kipindi cha FNL, Chambuso amesema hakuwa na wimbo wowote ambao Aslay ameurekodi na Ali Kiba kama inavyosemwa na baadhi ya watu.

Chambuso pia aliogezea kuwa hakuna tatizo lolote kati ya Aslay na kundi la WCB.

 

Aslay: Sivuti bangi

Aslay amefunguka kuhusu mtindo wake wa maisha na jinsi anavyo nawiri kama solo artist. Msanii huyo alieza kuwa bado yuko Yamoto Band hata kama anatoa nyimbo zake pekee yake.

Watu wengi wanadhani Aslay ametoka Yamoto Band lakini ukweni ni kwamba hakuna msanii yeyote ambaye amekihama kundi hilo.

Yamoto Band

 

Akiongea na Times FM 100.5, Aslay alisema kuwa Mkubwa Fella amewakubali kila msanii wa Yamoto Band kufanya kazi kivyake. Aslay mwenyewe ashaachia nyimbo tatu kama solo artiste.

Aslay pia aliuliza maswali kuhusu mtindo wa maisha yake, mtangazaji wa Times FM alimuuliza kama huwa anavuta bangi.

“Hapana sivuti bangi, sinywi pombe” Aslay alimjibu.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=xBaR9hiu3lk