Aslay kakua Maswala ya Mapenzi Muachieni Mwenyewe.-Fela

Mkubwa fella amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea  kuhusu mahusiano ya Aslay na aliyekuwa mpenzi wake na kupata naeo mtoto mmoja kuachana na kwamba wawili hao kwa sasa wanaishi mbalimbali.

Mkubwa Felaa anasema kuwa kwa sasa aslay ameshakuwa kwaio anauwezo wa kuamua kufanya yale anayoweza kufanya kwa kuamua mwenyewe lakini kuhusu swala la ndoa yake Aslay mwenyewe hajamfata na kumuelezea kuhusu kitu icho kwaio hawezi kusema kitu juu ya swala  hilo.

mkubwa Fela anasema kuwa kwa sasa aslay amekuwa ‘ mtoto kakua , huu ni mwezi wa ramadhani kwaio ingekuwa mwezi wa kawaida tungeongea lakini yeye kakua na anajua kuna ubaya, kuna mazuri kuna nini,angekuwa na akili angekuja angenifuata na kusema baba kuna hili na hili ningejua tunamrekebisha wapi.

Aslay Athibitisha, Kufanya Kazi kwa Kujitegemea Kuna Faida Kubwa.

Msanii wa muziki wa bongo fleva , Aslay anasema kuwa kufanya azi kwa kujitegemea kuna utofauti mkubwa sana kuliko kufanya kazi kama kundi au kufanya kazi pamoja  kama ilivyokuwa kwake hapo awali.

Hata hivyo Aslay anasema kuwa pamoja na kwamba sasa hivi anafanya kazi peke yake lakini bado yupo karibu na wasanii wenzake waliokuwa wakiunda kundi lao la ya moto band lililovunjika mwaka uliopita.

Aslay anasema kuwa hakuna utofauti wala ugomvi kati yao na kama itatokea moja wao akitaka kufanya nae kazi atafanya nae lakini ameona kuna utofauti mkubwa sana kufanya kazi kama kundi na kufanya peke yake lakini pia anaamini kuwa kufanya kazi katika kundi ilikuwa ni moja ya safari yake ya kimuziki.

Itambulike kuwa hapo awali aslay na wenzake walikuwa wakifanya kazi pamoja kama kundi lakini baadae wwalikuja wakashindwana na kuanza kufanya kazi kila mmoja kwa kujitegemea.

 

Aslay Atoa Siri Yake Ya Kutoa Ngoma Kali Mara Kwa Mara

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amefunguka na kutaja siri ya mafanikio yake inayompelekea kutoa nyimbo kali kila siku.

Aslay alianza kupata umaarufu katika kundi la Yamoto Band miaka ya nyuma kidogo amezidi kung’aa Zaidi baada ya kuondoka katika kundi.

Aslay ameweza kuwa msanii pekee ambaye amekuwa akitoa nyimbo mara kwa mara na zote zimekuwa ni hit baada ya hit kitu ambacho hakiwezi kufanywa na wasanii wengi Bongo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Aslay amefunguka na kudai siri ya kuwa na nyimbo kali ni katika uandishi ambapo anazingatia kuzungumzia maisha halisi ya watu hasa ambao anaishi nao.

Mimi nikiwa naandika sana naangalia maisha ya kweli ambayo yanayotokea kila siku alafu mimi nimetoka uswazi hivyo naangalia vitu vingi vya uswahilini kwaiyo ni vitu ambavyo vinanipa mimi mashairi mazuri.

Lakini pia kuna baadhi ya mambo sio lazima yanitokee mimi yanaweza kuwatokea watu wengine ila cha muhimu viwe ni vitu vya Ukweli”.

Aslay atakuwa mmoja kati wasanii ambao watafanya show katika Tamasha la Sport&Music Festival mkoani Mwanza,

Amber Lulu- Aslay Ameshawahi Kufaidi Penzi La Wema Sepetu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Jini Kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kupasua kuwa Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshawahi kufaidi penzi la staa wa Bongo fleva Aslay.

Amber Lulu, ametoboa siri ya Wema Sepetu na Aslay kuwa wapenzi miaka ya nyuma lakini pia amedai waliwahi kuishi pamoja kinyumba kama mke na mume.

Wiki iliyopita Amber Lulu alianika hadharani kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano pale alipoanika orodha ya wanaume ambao ameshawahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Amber Lulu ameweka wazi kuwa kipindi alipokuwa na Aslay alisikia pia alikuwa na Wema Sepetu aliyekuwa anaishi naye nyumba moja kitendo kilichofanya Mahusiano yao yasiwe serious:

Kipindi hiko nilikuwa undergrad nikawa nasikia Aslay alishakuwa na watu wengi nasikia alishakuwa na Wema Sepetu na wakakaa nyumba moja na wakapika na  kupakua halafu mimi kipindi hiko bado kabisa nilikuwa nanyapia nyapia”.

Amber Lulu amedai kuwa Aslay alikuwa ni fundi mzuri sana kunako mausuala ya sita kwa sita huku pia akitumia sifa hiyo kumtofautisha na Mbongo Fleva mwingini, Young D ambaye nae pia alikuwa mpenzi wake lakini hakuwa fundi sana kama ilivyo kwa Aslay.

Aslay- Pesa Ninayo Lakini Sina Utajiri wa Kutisha

Staa wa muziki wa Bongo fleva na hitmaker wa Natamba Aslay Isihaka amefunguka na kuweka wazi kuwa pesa anayo kidogo japo sio pesa kubwa kiasi hicho lakini angalau anayo.

Aslay ni moja kati ya msanii  ambaye amekuwa  akifanya  vizuri sana Kwenye ulimwengu huu wa Bongo fleva kwani amekuwa akitoa hiyo kwa kila nyimbo yake anayoweka mezani.

Hivi karibuni Aslay aliwekwa kundi moja na wasanii wakubwa kama Diamond na Ali Kiba na kusemwa na yeye anaingia Kwenye listi ya wasanii walio na mkwanja mrefu Bongo.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Tv, Aslay alisema kuwa hawezi kujisema ana hela kubwa lakini anayo pesa ya kubadilisha mboga ya kawaida:

Of course hela ya kubadilisha mboga ninayo Alhamdulilah siwezi nikasema sina nitakuwa naongopa hela ninayo lakini sina utajiri wa kutisha”.

Aslay alisemekana ana mkwanja mrefu sana baada ya miezi michache nyuma kununua ndinga la maana lenye viwango vyake aina ya BMW.

Penzi la Aslay na Mama Mtoto Wake Ladaiwa Kuvunjika

Kumekuwa na tetesi huko instagram kuwa msanii Aslay na mke  wake ambae amebahatika nae kupata mtoto mmoja kuwa kwa sasa hawapo tena pamoja na kwamba wawili hao  kila mmoja anafata ustaarabu wake kwa saa na inawezekana hata kukaa pamoja hawakai tena.

Wikiendi hii ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wawili ho huku siku zao zikiwa zimefatana  lakini kitu cha ajabu ni kwamba hakukuwa na shamrashamra za sherehe hiyo kwa wote wawili huku alsya hakutaka hata kuweka picha ya mzazi mwenzake huyo katika ukurasa wake wa instagram

Habari ziliozpo chini ya kapeti ni kwamba Aslay na Tessy hawako pamoja tena na kwamba mwanamke huyo alishaondoka nyumbani kwa aslay na sasa wapo katika mahuiano kama ya wazazi tu na sio vinginevyo.

Wasanii wengi wamekuwa na skendo za kuwa na mape nzi ya muda mfupi na pengine hata kushindwa kufikia muafaka wa ndoa kwa wapenzi wao huku swala kubwa likihusishwa na wivu wa mapenzi na kulewa umaarufu.

Aslay- Kifo Cha Masogange Kilizima Wimbo Wangu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Isihaka Nassoro maarufu kama Aslay amefunguka na kuelezea jinsi Kifo Cha marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ kilivyozima wimbo wake.

Aslay ameongelea jinsi wimbo wake wa ‘Kwa raha’ ulivyoshindwa kuvuma kutokana na kutoka kipindi kibaya ambacho ilikuwa ni msiba wa marehemu Masogange.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Aslay amesema kuwa ngoma hiyo aliitoa kama zawadi kwa mashabiki wake kwani ngoma yake ya mwisho kutoa rasmi ni Nibebe mara baada ya kubadilisha mfumo wake wa kutoa ngoma.

Kwa Raha nilitoa kama zawadi kwa sababu kuna ngoma inakuja kuitoa tena baadaye ila nasema ni ngoma yangu naipenda na namshukuru Mwenyenzi Mungu imeenda japo kuwa hapa kati imekutana misukosuko, Agness amefariki, kuna vitu kibao vimetokea lakini nashukuru ngoma hivyo hivyo inaenda“.

Aslay ni msanii mwenye mafanikio sana kiasi ya kwamba kila nyimbo anayotoa inafanya vizuri lakini  wimbo huu wa kwa raha haujafikia mafanikio wa nyimbo zake nyingine kutokana na kutoka wakati ambao kila mtu alikuwa na majonzi ya Masogange.

 

Aslay Afunguka Kuhusiana na Ndoa Ya Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay amefunguka na kuongelea ndoa ya staa wa Bongo wa fleva Ali Kiba iliyofungwa wiki iliyopita ambapo amesema haoni tatizo kwa Msanii huyo kuoa nje ya nchi.

Ali Kiba amemuoa mwanamke anayeitwa Amina Rikesh mwenye asili ya Kiarabu kutoka Oman lakini anayeishi Mombasa nchini Kenya.

Mashabiki walimtolea povu Ali Kiba kwa kitendo chake cha kuamua kwenda kuoa nje ya nchi wakati Tanzania kuna wanawake kibao jambo ambalo Ali kiba alijibu kuwa macho na moyo havina pazia.

Aslay ameipongeza na kusema watu wasishangae au kulalamika mtu kuamua kuoa nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kawaida tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aslay amewataka mashabiki zake wasilalamike kitendo cha yeye kwenda kuoa nje ya nchi kwani ni jambo la kawaida sana kutokea:

Kuoa ni jambo la kheri bwana na ni hatua kubwa sana nampongeza sana kaka mkubwa kwani sio jambo la mchezo hilo, lakini watu wanatakiwa kuelewa kuoa nje ya Tanzania ni jambo la kawaida tu kama mtu anavyotoka kwenye kabila lake na kuoa kabila lingine“.

 

Natamani Kushinda Tuzo Ya Heshima- Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana hivi sasa Aslay amefunguka kuwa anatamani sana kama atafanikiwa kupata tuzo basi apate tuzo ya heshima.

Aslay amekuwa akifanya vizuri kimuziki tangu atoke kwenye kundi la Yamoto Band, kila nyimbo ambayo amekuwa akitoa zimekuwa zikifanya vizuri kiasi ya kwamba amewekwa kwenye ramani ya wasanii bora wa Bongo fleva wanaofanya vizuri.

Pamoja na mafanikio hayo Aslay hajawahi kushinda tuzo yoyote hii inaweza Ikawa sababu ya ufinyu wa tuzo nchini ambazo zinatambua mchango wa wasanii mbalimbali na wadau.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv Aslay amefunguka haya kuhusu juu yake ya kuchukua tuzo Tanzania:

Nafikiri kuna tuzo nyingi sana zinatokaga Tanzania na mimi sijawahi kuchukua tuzo yoyote kubwa Tanzania lakini naamini siku nitakayopata tuzo ya heshima ndio nitajiona mimi nimekuwa msanii mkubwa na nitaweza kujishindanisha na wasanii wengine wakubwa”.

Lakini pia Aslay amefunguka kuhusu mipango yake ya kutoa Albamu ambapo ameweka wazi kuwa tayari nyimbo zake za kukaa kwenye Albamu zimeshatimia hivyo yupo kwenye michakato.

Aslay Agoma Tena Kufananishwa na Alikiba.

Msanii anaefanya vizuri sasa na wimbo wake wa sabalkheri aslay amewaomba mashabiki wake kuacha tabia ya kumfaninsha na kumlinganisha na Alikiba kwa sababu hawezi kabisa kulingana nae kwa chochote kwa sababu Alikiba ni msanii mkongwe na kazi yake ya kuupeleka muziki mbele imeshaonekana sio sawa na yeye ambae bado anatakiwa kufanya kazi kubwa ili kukuza muziki wake.

Aslay ameyasema hayo tena hivi karibuni baada ya kuona kuwa kuna watu wengi ambao wamekuwa wakisema kuwa kwa sasa ameshafanya vizuri na kukua kimuziki kiasi kwamba anaweza kufanya show na alikiba na bado akaweza kumfunika Alikiba akafanya show siku moja na watu wakajaa kwake na sio kwa Alikiba.

kama kuna masgabiki wanafanya hivyo basi wanakosea sana kwa sababu wasanii wanaonifananisha nao wameshafika level zingine kabisa.na mimi ninajitahidikufika level hizo siku moja , kwaio unavyonifananisha nao kwanza unania kisaikolojia,kwa sababu na mimi nitajiona kama nishafika  hatua zao kumbe bado sana.

ukisema kuwa umlinganishe aslay na alikiba utakuta kuwa unakosea vitu vingi sana kwa sababu yeye tayari alishaingia katika tuz mbalimbali ambapo sasa hivi hata akifanya show anajaza sana .

Aslay anasema kuwa kwa muda huu yeye so wa kujifananisha na mtu yoyoyte kwa sababu bado anataka kufanya kazi ambao itamfikisha katika level nyingine na kupiga hatua kama walizopiga wasanii wakubwa.

“Sina Mahusiano Ya Kimapenzi na Nandy”- Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva Anayezidi kufanya vizuri hivi sasa Aslay amefunguka na kusema hana Uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii mwenzake Nandy.

Kumekuwa na maneno mengi mengi ambayo yamekuwa yakisababishwa na ukaribu uliopo kati ya Nandy na Aslay ambapo mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii imesemakana kuwa wawili hao ni wapenzi.

Kwenye Interview aliyofanya Friday Night Live ya East Africa Tv, Aslay amefunguka na kusema ukaribu aliokuwa nao na Nandy ni wa kikazi tu sio zaidi ya hapo na amesisitiza kuwa yeye tayari ana mpenzi wake na familia.

Nafikiri watu wanaonifatilia watakuwa wanajua kuwa mimi nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy nipo naye kwenye kazi zetu za kimuziki tunazofanya hakuna kingine cha zaidi kinachoendelea kati yangu na Nandy”.

Nandy na Aslay wanakimbiza na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao umefikisha zaidi ya viewers milioni tatu YouTube kwa mwezi mmoja lakini pia wameshawahi kufanya ngoma nyingine iliyofanya vizuri siku za nyuma iliyoitwa Mahabuba.

Aslay Ampiga Marufuku Mke Wake Kuuza Sura .

Msanii anaefanya vizuri  hivi na vibao vyake kibao kikiwepo cha subakheri alichoimba na Nandy , Aslay amefunguka na kuonnhgelea uamuzi wake wa kumpiga marufuku mzazi mwezie kuwa anaonekana katika mitandao ya kijamii na kuuza sura.

Aslya amesema kuwa kwa sasa mwanamke wake hatakiwei kuonekana wala kujihusisha  na kuuza sura katika sehemu mbalimbali kwa sababu tayari ana kazi nyingine inayomuingizia kipato lakini pia yeye sasa ni mzazi na ana mtoto wa kulea kwaio hataki kumuona akiuza sura tena.

Akiongea kwenye FNL, Aslay amesema kuwa mzazi mwenzie huyo anaejulikana kama Tessy Chocolate alikuwa ni video vixen , lakini kwa sasa hawezi kuendelea na kazi hiyo kwa sababu kile alichokuwa akikitafuta katika kazi hiyo tayari ameshampatia.

hawezi kuendelea mimi ndio nimesema hawezi kuendelea,sidhani kama sasa hivi anapedna tena kufanya hiyo kazi, kwa sababu mara nyingi yuko na mtoto lakini pia kuna kitu nimempatia anafanya pia kinachomuingizia ela na kwasababu kule alikuwa anatafuta ela.-Alifunguka Aslay.

Lakini pia alikanusha tetesi za kuwa waliachana na mama mtoto wake na kusema kuwa taarifa hizo sio za kweli.

Beka Fleva: Mbosso Hajanitetemesha, Aslay Nayeye Acha Tushindane

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya Kiben10 amefunguka na kusema hajatetemeshwa na ujio mpya wa msanii Mbosso kutoka WCB lakini pia Aslay atashindana naye tu.

Beka fleva, Aslay, Mbosso na Bella waliunda kundi la Yamoto band waliojipatia umaarufu miaka ya nyuma lakini baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa kundi hilo liliishia kuvunjika na kila mmoja alishika njia yake na kuanza solo careers.

Wasanii wote wamekuwa wakifanya vizuri na kukubalika na kila mmoja wao amekuwa akidai hakuna uhasama kati yao na kila mmoja anamtakia heri mwenzake na mafanikio.

Lakini pia Beka fleva ameongelea tetesi za yeye kukasirikia mafanikio ya Mbosso kusainiwa WCB na hivyo kusababisha kutohudhuria halfa yake ambapo amedai alichelewa kupata taarifa za shughuli hiyo hali iliyopelekea kushindwa kufika.

Beka fleva amefunguka kuwa alivyoona Utambulishi wa Mbosso kwenye bonge la hoteli la Hyatt Regency na baadae kijamii uwanjani Mwembeyanga hakutetemeshwa hata kidogo ndio kwanza alifurahi kuona mafanikio ya mwenzake lakini pia amesema anafurahia ushindani wake na Aslay kwani unaleta mziki mzuri.

Kisa Mama , Aslay Amliza Mama Yake Nandy.

Wikiendi hii inaweza kuwa ni wikiendi ya kihistoria katika swala la muziki , hii ni baada ya kufanyika kwa show kubwa iliyojulikana kama Aslay , Nandy na Marafiki huku lengo kubwa ikiwa ni kuwaburudisha wpenzi wa muziki hasa katika kusherekea siku ya wapendao  Ambayo ilifanyika February 17.

Akiwa anataka kutumbuiza wimbo wake unaokwenda kwa jina la mama, Aslay aliamua kumfuata mama na baba yake Nandy ambao pia walikuwepo katika show hiyo ili kuwakumbatia ikiwa ni kama ishara ya kuwaheshimu wazazi hao huku akiongea na kusema kuwa anatamani sana hata yeye mama yake angekuwepo katika show hiyo.

Huku akielekea katika meza hiyo, Aslay alikuwa akisema”kwa heshima kubwa napenda kwasimamaisha wazazi wa nandy ana nngependa wawe wazazi wangu pia, ninafuraha kuona wazazi wanawasapoti watoto wao,hsa mama na ninapomuona ninfarijika kwa sababu hata mimi nilitamani mama yangu angekuwpo hapa lakini hayupo.ninawaomna muwaheshimua sana wazazi hasa mama.

Hata alipokuwa akiimba wimbo huo watu wengi walionekana kuwa na huzuni kwa sababu ya msanii huyo kutoa lilipo moyoni mwake kuwa angetamani siku kama hiyo mama yake angeona mafanikio ya kazi yake kwa sababu walihangaika sana wote ili yeye awepale alipo.

Mama yake Aslay alifariki mnamo mwaka 2015, ambapo kwa histori aya maisha ya Aslay huwa anaumia sana anapokuwa akikumbuka au kuliongele atukio hilo kwa sababu mama yake alikuwa akimsaidia na kumfariji sana katika kufanya kazi lakini ilikuwa ni kama mshumaa uliozimika kwa sababu mama yake hajapata kuona mafanikio yake.

Aslay Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuiba Daftari la Nyimbo la Yamoto Band

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana kwa hivi sasa Aslay Isihaka amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea tetesi zilizosambaa mtandaoni kuwa aliiba daftari la nyimbo za Yamoto Band.

Habari hizi zilienea mtandaoni mwaka jana baada ya Kundi la vijana la Yamoto Band kuvunjika. Aslay alikuwa mmoja kati ya wasanii waliounda kundi hili ambalo lilivuma kwa miaka mingi.

Ingawa mpaka leo hii haijajulikana nini has a sababu kibwa iliyofanya mpaka kunsi hill kuvunjika lakini kikubwa kinachisemekana ni masuala ya maslahi yaani uongozi wao ulikuwa hauwapi walichokuwa wanastahili na kusababisha kundi hilo kuvunjika.

Lakini mara tu baada ya kundi hilo kuvunjika na kila msanii kuanza kufanya kazi binafsi Aslay alidhihirisha uwezo wake wa kuimba kwani alianza kung’aa mara moja na alianza kuachia nyimbo zake kwa fujo na nyimbo zake zote zilishika namba moja kwenye chati mbali mbali.

Baada ya kuona kuwa katika muda mfupi ambao Aslay amekuwa peke yake amekuwa akitoa nyimbo nyingi kiasi like ndipo tetesi zilanza kusambaa kuwa Aslay aliiba daftari la nyimbo la Yamoto band lililokuwa na by nyimbo zilizo andikwa na wasanii wotenwakundi hilo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5 Aslay amekana tuhuma hizo na kuhakikishia watu kuwa nyimbo zote anazoimba ni zake:

Hizo tetesi za mimi kuondoka na daftari la Ya Moto Band zilikuwa ni tetesi tu unafikiri zilikuwa na ukweli wowote hapana hazina ukweli yalikuwa ni maneno tuu yaliyoanzishwa na mashabiki ili mradi tuu kuchekesha watu na mimi nilivyoona nilicheka tu maana nilijua ulikuwa ni utani kutoka kwa mashabiki”.

Aslay amekiri kuwa tangu ameondoka katika kundi la Yamoto Band ametoa nyimbo kama kumi na sita na sababu kubwa iliyomsukuma kutoa nyimbo nyingi katika kipindi kifupi ni ili akifanya shoo zake asitumie nyimbo za Yamoto.

 

Enock Bella Amefungukia Tuhuma za Aslay Kuiba Daftari La Nyimbo za Yamoto Band

Aslay ni mmoja Kati ya wasanii anayefanya vizuri sana kwa hivi sasa mafanikio anayopata ni wasanii wachache wanaoweza kufikia ukitegemea kwa mtindo wake wa kutoa nyimbo kila baada ya muda mfupi.

Lakini mafanikio Kama haya lazima yaje na changamoto kadhaa kwa upande wa Aslay changamoto hiyo ni bendi yake ya zamani ya Yamoto Band iliyovunjika miezi michache iliyopita na kupelekea vijana waliokuwa wanaunda bendi hiyo kutengana.

Baada ya kuvunjika kwa bendi hiyo na Aslay kama solo artist, maneno maneno yalianza chini kwa chini ambapo moja kati ya habari zilizosambazwa na watu wasiojulikana na kushika kasi ya ajabu hivi sasa za kumchafua Aslay ni kuwa kitu pekee kinachompa Aslay mafanikio baada ya kuondoka Yamoto na kuwa na nyimbo nzuri kila siku ni kwa sababu wakati anaondoka Yamoto band aliiba daftari la nyimbo la Yamoto ambalo alishirikiana na wenzake kuandika.

Enock Bell ambaye alikuwa kwenye bendi ya Yamoto na Aslay amefungukia tuhuma hizo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha  East Africa:

Unajua uzuri nchi yetu haijamkataza mtu kuongea kila mtu akijisikia kuongea anaongea chochote anachoweza kukifikiria lakini kiukweli ni kuwa Aslay bahati nzuri Mwenyezi Mungu kamjalia kitu chake cha kipekee ni msanii ambaye unaweza ukamwekea biti tu akafree style nyimbo nzima kwaiyo Ana uwezo wa kuandika nymbo hata nne kwa siku mbili anaweza kupangilia mashairi yake vizuri kwa muda mfupi na yakawa makali kwaiyo sio kweli kuwa aliiba daftari la Yamoto kwanza hatukuwa na daftari lolote”.

Enock alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa sababu pekee watu wanasambaza habari hizo ni baada ya kuona Aslay anatoa nyimbo kali kila siku lakini amedai hicho ni kipaji chake tu na sio wizi.