Wasanii Wengi Wana Majina Makubwa Lakini Pesa Hakuna-Darassa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Darassa CMG ambaye amewahi kusumbua sana kwa ngoma yake ya Muziki ameibuka na kuweka wazi hali halisi ya wasanii wengi wa Bongo.

Darassa amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi Bongo wana majina makubwa na hata mashabiki wengi kwenye Mitandao ya kijamii Lakini kiuhalisia hawana pesa na wanaishi katika maisha magumu sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Darassa amezungumza mambo mengi sana ambayo ni shule kwenye maisha ya kawaida na Muziki wa Tanzania, lakini anakiri kuwa hakufaidika kwenye nyimbo alizotoa hapo  kama jinsi alivyokuwa maarufu.

Kwenye muziki wetu kutengeneza jina ni rahisi sana, lakini kutengeneza fedha ni kazi sana, mimi nilitaka kuwa kwenye daraja ambalo nalitaka lakini kuna ambao wapo wanaotaka kukuonyesha kuwa hicho unachofanya siyo sahihi, njia ya kupita ni huku”.

Baada ya kimya kirefu cha mwaka mzima hatimaye mwaka jana mwishoni Darassa aliachia ngoma yake ya ‘Acha Njia’ ambayo bado inafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya redio.

Darassa Ataja Sababu Iliyomfanya Akae Kimya

Msanii wa Bongo fleva aliyewahi kitikisa nchi na wimbo wake wa ‘Muziki’ Darassa CMG amefunguka na kuweka wazi sababu iliyompelekea kukaa kimya kwa muda wa mwaka mzima.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Kupitia mahojiano na  kipindi cha XXL cha Clouds Fmamefunguka kuhusu ishu ya ukimya wake wa mwaka mmoja ikiwemo tuhuma zilizokuwa zikiendelea mtaani juu yake baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye game ya Bongo Fleva.

Ni kweli nilikaa kimya sababu nilikuwa nimepata mtoto na muda wangu mwingi nilikuwa nautumia nikiwa nyumbani na hata hizo story ambazo zilikuwa zinaendelea juu yangu nilikuwa nazisikia nikiwa nyumbani kwangu huku nikiwa nimembeba mtoto wangu, Ilifika time watu walikuwa wanakuja kugonga nyumbani kwangu ili wanione je ni kweli yanayoendelea na ikawa inafika muda nafungua geti na nawauliza vipi mnaona nini”.     

Nimekaa ndani kwa mwaka mzima, Wasanii wengi wametoa ngoma zao na zimefanya vizuri, natumia fursa hii kumpongeza producer @abbah_process kwa kufanya ngoma nzuri ya Iokote, Watu wajue nimeanza kazi rasmi na ushindani utakuwa mkubwa”.

 

Darassa Ajibu Tuhuma Za Kutumia Madawa Ya Kulevya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye aliwahi kujizolea umaarufu na kibao chake cha ‘Muziki’ Darassa CMG ameibuka baada ya kimya kirefu na kukiri tuhuma zilizowahi kumkabili za kutumia madawa ya kulevya.

Miaka michache iliyopita Darassa alitoa bonge la ngoma lakini Baada ya mafanikio hayo alikuwa kimya kiasi cha kupelekea maneno kusambaaa kuwa msanii huyo amejitumbukiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Kwenye mahojiano aliyofanya Gazeti la Risasi Jumamosi, Darassa alisema kuwa mara baada ya kuachia Muziki aliamua kukaa kimya kwa ajili ya kuwa karibu na familia baada ya kupata mtoto wa kike.

Watu walikuwa wakiongea wanayojua wao. Ukweli nipo fiti, sijawahi kujihusisha na vitu kama hivyo. Ukimya wangu sasa hivi umefika mwisho na nimerudi rasmi”.

Darassa amekiri tetesi za madawa zilikuwa zinamuumiza sana ingawaje alikuwa Anajua kuwa hazina ukweli wowote.

Hivi sasa Darassa anafanya vyema na ngoma yake ya ‘Achia njia’ ambayo imeshika nafasi za juu katika chati za YouTube.

Darassa CMG Arudi Kwenye Sanaa Baada Ya Kimya Kirefu

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini na hitmaker wa ‘Muziki’ Darassa CMG ametangaza kurudi kwake kwa kishindo Baada ya kimya kirefu.

Baada ya kutoa ngoma kali kama ‘Muziki’, ‘Too much’ na nyinginezo Darassa aligubikwa na kimya kizito kilichosababisha kuibuka kwa tetesi mbali mbali ikiwemo kuhusishwa na madawa ya kulevya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa ameachia video hii kuashiria kurudi kwake kwenye gemu la Bongo fleva:

https://www.instagram.com/p/BrLMOQvHcHP/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1nmgqu6tsfhy9

Baada ya kuwa kimya sana tena ghafla kuna tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amejaaliwa kimya kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya taarifa alizozikana na kusisitiza kutokuwa na ukweli na kuweka wazi kuwa yeye yupo nyumbani akimlea Mtoto Wake.

 

Mr. Blue Afungukia Ukimya Wa Darassa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amefunguka na kuvunja ukimya juu suala la Darassa.

Darassa amewahi kutoa wimbo ambao ulikuwa wimbo wa Taifa kwani ulioigwa kila kona na kukubalika kila kona anaweza Kuwa ndio msanii pekee kuandika historia hiyo.

Lakini tangu atoe hit Single yake Darassa amekuwa kimya sana jambo lililosababisha maneno kibao kuibuka Kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo tetesi za kuwa Msanii huyo amejiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya Kulevya.

Mr. Blue ameibuka na kuwataka watu wampe nafasi Darassa ya kupumzika kwani kilichotokea ni kuwa ameamua kupumzika kufanya Muziki kwa sas na Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Mr. Blue alifunguka haya zaidi:

Darassa mwenyewe ameamua kujipa break kwa sababu amefanya kitu kikubwa sana na mimi sidhani kama kuna tatizo lolote pale mtu anapotaka mapumziko kutoka kwenye muziki kwa sababu hata mimi nilishawahi kujipa break baada ya wimbo wangu wa Tabasamu lakini watu waliongea sana na kudai mimi ni teja lakini hii ndio kawaida ya binadamu kuongea kwa sababu wana midomo”.

Darassa ameshawahi kukana tetesi za kuwa yupo kimya kwa sababu yupo rehab na kusisitiza yupo kimya kwa sababu amechukua mapumziko baada ya mwanaye kuzaliwa.

Darassa Akana Taarifa Za Kupotea Kisa Madawa Ya Kulevya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na hitmaker wa ngoma ya ‘Muziki’ Sharifa Thabeet maarufu kama Darassa amekanusha taarifa za kupotea kisa matumizi ya madawa ya kulevya.

Baada ya kuhit sana na ngoma yake Darassa alikuja kupotea ghafla na mara moja kuna tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Darassa amejiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kwa muda mrefu alikuwepo Rehab.

Global Publishers wanaripoti kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu maripota wao walifika katika eneo analoishi ambapo lilikutana moja kwa moja na Darassa mwenyewe akiwa amembebelea mtoto wake wa kike huku hali yake kiafya ikiwa safi tofauti na inavyoenezwa.

Huyu ndiye mwanangu, maneno yamesemwa sana lakini huyu ndiye aliyenifanya kukaa chini kwa muda na kulea,” alisema Darassa huku akimbembeleza mwanaye huyo mwenye miezi kadhaa.

Lakini pia GPL wanaripoti kuwa baada ya Kuchonga na kukanusha Tetesi za madawa ya kulevya Darassa  aliwatembeza maripota katika mjengo wake wa kifahari:

Hii hapa ni studio yangu, maisha yangu yote yapo hapa, huwezi kunikuta nikitamba studio yoyote, vitu vyote napikia hapa”.

 

Ben Pol- Tetesi Za Darassa Kutumia Madawa Ya Kulevya Sio Za Kweli

Mwanamuziki wa Bongo fleva Darassa alibamba sana siku za nyuma na kibao chake cha ‘Muziki’ ambacho kilikuwa ni kikali balaa lakini siku za hivi karibuni sifa hiyo njema aliyokuwa nayo imekumbwa na wingu baya.

Tetesi za Darassa kujiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya zilisambaa kama moto wa kifuu baada ya picha yake tata kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kuzua sintofahamu.

Ben Pol ni moja kati ya watu wa karibu wa Darassa na hata amefanya naye kolabo mbili ambazo ni Muziki na sikati Tamaa.

Kwenye Interview ambayo Ben Pol amefanya na Clouds Tv, amesema hamsini taarifa hizo kwani anawasiliana naye karibia kila siku.

Kusema kweli siamini, sina element yoyote inayonifanya niamini chochote kuhusiana na hizo tetesi kwa sababu ili mtu uweze kusema kitu lazima uwe na element ambazo umeziona lakini mimi hamna element.

Mimi tunaongea masaa mawili, saa zima kwenye simu, video call sometime kwa hiyo sioni kuna element ya hicho kitu”.

Wasanii wengi walikuwa wanafanya vizuri tumeona jinsi wanavyoteketea kisa matumizi ya madawa ya kulevya ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri maisha yao mfano mzuri ni Q Chillah,Ray C na Chid Benz na wengineo.

‘Hasara Roho’ ya Darassa kuvunja rekodi ya ‘Muziki’?

Iwapo kuna msanii ambaye anatamba Afrika Mashariki sasa ni Darassa. Miezi mitano iliyopita msanii huyu sliachia wimbo wake wa Muziki na kwa mara ya Kwanza alivunja rekodi ambazo wasanii wengi waliokuwa wamemtangulia hawajafika bado.

Muziki ilitazamwa mara mara 7,859,849 kupitia mtandao wa YouTube na nyimbo yake mpya Hasara Roho inaonyesha kuwa inafuata mtindo huo kwani kwa imeangaliwa mara 933,776 ndani ya wiki mbili.

Hata hivyo hapo awali wengi wa mashabiki waske walihisi kuwa nyimbo hii yake haikuwa na tofauti kubwa na Muziki lakini inaonekana kuwa wanaipenda pole pole tu. Video ya wimbo huo hata hivyo ni wa hali ya juu na ndio maana mashabiki wengi wanaendelea kuonyesha wanaikubali.

Darassa ana huzuni sana na ni kwa sababu ya mambo haya yanayotendeka Tanzania

Darassa CMG ana huzuni mingi na ni kwa sababu ya mambo yanayoendelea Tanzania wakati huu.

Hana furaha hata kamwe.

Anaogopeshwa na future ya nchi na mambo yanavyoendeshwa kwenye serikali and anaogepea watoto na wanawake wataangamia siku zijazo.

Huu ndio ujumbe alio utoa kwenye instagram yake:

BABA MUNGU SHUKA WEWE UENDESHE NCHI YETU! BORA TUPOTEE SISI NI SAWA!!!! vip kuhusu watoto wadogo na wanawake!!!! Future ya nchi inaogopesha na huitaji macho kuona hili ? sina chama wala upande m1 kwenye shilling!!! maana sijui hata nani anatupenda kweli sisi wananchi na atakua tayari kututhamini! ???