Mr. Blue Ajutia Maamuzi Ya Kutoa Albamu

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Herry Sameer maarufu kama Mr. Blue amefunguka na kusema kuwa hakuna kitu kimemtia hasara kama kutoa Albamu.

Mr. Blue amesema kuwa hajawahi kupata faida kupitia albamu zake cha zaidi ni kwamba hakuna kitu kimemtia hasara kama kutoa albamu zake na kuzipeleka sokoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Mr. Blue alifunguka mambo haya:

Kusema Ukweli albamu hazilipi aisee kwa sababu albamu yangu ya kwanza nilipewa milioni na albamu yangu ya pili nilipata pesa ambayo nilinunua gari tu Lakini sasahivi single moja Lakini unaweza ukapiga mpaka milioni tano”.

Kutoa albamu kwa wasanii ni mafanikio makubwa sana kwani ndipo wanapotengeneza fedha kwa kuusa muziki wao Lakini kwa nchi kama Tanzania imekuwa tofauti kwani wasanii hawatoi kabisa Albamu kwa Kuhofia kupata hasara badala ya faida.

 

Mr. Blue Afungukia Ukimya Wa Darassa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amefunguka na kuvunja ukimya juu suala la Darassa.

Darassa amewahi kutoa wimbo ambao ulikuwa wimbo wa Taifa kwani ulioigwa kila kona na kukubalika kila kona anaweza Kuwa ndio msanii pekee kuandika historia hiyo.

Lakini tangu atoe hit Single yake Darassa amekuwa kimya sana jambo lililosababisha maneno kibao kuibuka Kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo tetesi za kuwa Msanii huyo amejiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya Kulevya.

Mr. Blue ameibuka na kuwataka watu wampe nafasi Darassa ya kupumzika kwani kilichotokea ni kuwa ameamua kupumzika kufanya Muziki kwa sas na Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Mr. Blue alifunguka haya zaidi:

Darassa mwenyewe ameamua kujipa break kwa sababu amefanya kitu kikubwa sana na mimi sidhani kama kuna tatizo lolote pale mtu anapotaka mapumziko kutoka kwenye muziki kwa sababu hata mimi nilishawahi kujipa break baada ya wimbo wangu wa Tabasamu lakini watu waliongea sana na kudai mimi ni teja lakini hii ndio kawaida ya binadamu kuongea kwa sababu wana midomo”.

Darassa ameshawahi kukana tetesi za kuwa yupo kimya kwa sababu yupo rehab na kusisitiza yupo kimya kwa sababu amechukua mapumziko baada ya mwanaye kuzaliwa.

Kwa ajili ya Familia,Yawezekana Mr blue Akaacha Muziki

Msanii Mr Blue amefunguka na kumshukuru sana mke wake ambae ni mama wa watoto wake kuwa kuwa amekuwa moja ya watu walioweza kumbadilisha sana mpaka kufikia ambapo alipo sasa hivi , sehemu ambayo hata yeye anaona kuwa amebadilika sana.

Mr Blue anasema kuwa kutokana na mchango mkubwa wa mke wake katika kumbadilisha, hata yeye amekuwa aifikiria jinsi gani anaweza kuifanya familia yake kuwa na furaha na anaona njia moja wapo ya yeye kufanya hivyo ni kukaa na kutulia hata  ikibidi kuacha muziki ili kumrudia mungu kwa ajili ya furaha yake , mkewe na familia yake pia.

Mr blue anasema kuwa mke wake ni swala tano , kitu kinachomsukuma zaidi yeye kutaka kutoka katika muziki ili kurudi na kuanza kuswali kutokana na msukumo mkubwa wa kidini kutoka kwa mke wake.

Naomba mungu ipo siku najua nitaacha muziki kabisa na mimi nipumzike na kutulia kabisa , umri unakwenda pia,sio utani siwezi kusema ni officil lakini kama mke wangu atataka nifanye nitafanya kwa sababu nina mpenda sana.  -Alisema Mr Blue alipokuwa akiongea na Bongo5

Mr. Blue Athibitisha Kukimbilia Afrika Ya Kusini

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Kherry Sameer Rajabu maarufu kama Mr. Blue amethibitisha kuwa amekimbilia nchini Afrika ya Kusini kwa ajili kufanya shoo.

Baada ya kutoonekana Bongo kwa muda mrefu hasa kutofanya shoo za ndani kwa muda mrefu Blue ameweka wazi kuwa ameamua kwenda kwa Madiba ili kubadilisha muelekeo kwa muda.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Mr Blue anayebamba na Ngoma ya Mbwa Koko alisema kuwa, kuwepo Kwa Madiba kumemfanya kujisikia tofauti na kuonesha hilo, juzikati alipafomu katika Jiji la Durban na kupata shangwe za kutosha kwa mashabiki wanaofutalia muziki wake.

Nipo huku (Kwa Madiba) ikiwa ni muendelezo wa kazi zangu ambazo nimekuwa nikizifanya nje. Kwa sasa nimeamua kuwekeza nguvu zaidi kupiga dili za nje ya Bongo kama ambavyo nilikuwa nafanya ndani. Si vitu vigeni kwangu, lakini kwa sasa nahitaji kuipeleka kazi yangu next level zaidi.”

Wasanii wengi wamekuwa wakibalisha makazi yao ili kuoata nafasi za kupiga kazi zaidi wasanii kama Ray C na Mr. Nice wamehamisha makazi yao nchini Kenya lakini pia Diamond yupo nchini Marekani kwa mwezi mzima kwa ajili ya kupiga Tour yake ya ‘A boy from Tandale’.

Mr. Blue Awainulia Mikono Ali Kiba na Diamond

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khery Sameer  au maarufu kama Mr. Blue amewainulia mikono mastaa wa Bongo fleva Diamond na Ali Kiba.

Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa anaona kabisa kuna vitu vya Ziada vinavyowafanya Ali Kiba na Diamond wazidi kupata mafanikio katika tasnia hii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mr Blue amesema wanamuziki wengi chipukizi hutamani kuwa kama wawili hao bila kufahamu mbali na kufanya muziki wanajituma, wana nidhamu na wana malengo ya kufika

Unajua wengi hutamani kuwa kama fulani kwenye muziki hasa watu wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kama Diamond na Kiba, lakini bila kufahamu kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na vitu vya ziada mbali na kuimba kawaida.

Kwa ushauri wangu, wanamuziki chipukizi waangalie ni vitu gani vya ziada wanavyo wanamuziki wanaotamani kuwa kama wao wavifuate na wataweza kufika kule wanako kuhitaji”.

Ni wiki chache tu zilizopita Mr. Blue alikana taarifa za  kuwa ana bifu na Diamond baada ya tetesi za muda mrefu zilizodai hivyo.

Mr. Blue- Sina Tatizo na Diamond Ila Kuna Watu Wanataka Tuwe na Bifu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Khery Sameer  maarufu kama Mr. Blue amefunguka na kudai binafsi hana tatizo lolote na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz bali kuna watu wanataka wawatengenezeee bifu.

Kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa Diamond na Mr Blue wana bifu kutokana na mara kadhaa Mr Blur amesikika akimtupia madongo mazito Msanii huyo.

Lakini juzi Mr. Blue amethibitisha kuwa hana tatizo lolote na Diamond na hata akauposti Wimbo Mpya wa Diamond #Iyena na kuupa promo.

Lakini pia Kwenye Interview aliyofanya na Wasafi Tv, Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo na Diamond kwani alianza kumsapoti tangu akiwa underground:

Ukikaa na Diamond ukamuuliza atakwambia kuwa mimi nimeanza kumpa sapoti tangu mwanzoni Wakati Diamond hajulikani na waandishi wa habari, hajulikani na mtu yoyote.

Hapo inaonyesha wazi kuwa sina chuki na Diamond wala sina tofauti naye yoyote kama ningekuwa na chuki ningemzuia tangu anaanza kutoka hata nyie msingekuwa na kazi”.

Lakini pia Mr Blue aliendelea kufunguka:

Kinachonichekesha kunishangaza ni pale watu wanapooana nimemsapoti akiwa na mafanikio wanataka nianze kumkandia kitu ambacho hakiwezekani. Mimi Diamond ni mdogo wangu wakati anatoka sikuwahi kuwa na bifu naye wala tofauti naye, kuna I wanaotaka kutuingiza katika tatizo mimi na Diamond”.

 

 

Mr. Blue Anyoosha Mikono kwa Diamond Platinumz.

Kwa muda mrefu msanii Kheri Sameer (Mr Blue) amekuwa yupo kwenye bifu zito na Diamond Platnumz Simbaaaaaaaa ,mara kwa mara Blue amekuwa akimponda Diamond Platnumz lakini waswahili husema jibu la mjinga ni kumkalia kimya tu ipo siku ata erevuka,na siku zote kama unajua unajua tu watu watapiga kelele mwisho wa siku watanyoosha mikono bila kupenda.

Sasa bhana Diamond a.k .a mzee wa minyoosho anazidi kuwanyoosha tu watu , na mmoja mmoja anaanza kunyooka , alianza kunyooka ,Richi Mavoko,akafuatia H-baba ,akaja Baraka the Prince sasa zamu ya Mr Blue naye kanyooka bila kupenda ,Ha ha ha ha team Kiba inazidi kusambaratika tu, hapo amebaki Tundaman na adui kuu Ally Kibanio

Yani Blue kanyooka haswaaa ,tena kasindikiza na Caption Mungu ni mwema maana alijijua alichokuwa anakifanya ni kitendo cha kijinga ,kapitwa na fursa nyingi kwa kitendo chake cha kumchukia Diamond.

Mr. Blue: Kuanzia Leo Sitaki Tuzo Yoyote Kutoka Tanzania

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Mr. Blue amefunguka na kusema kuwa anaumua sana kuwa mpaka leo hii na ukongwe wake kwenye gemu lakini hana tuzo hata moja lakini pia amekiri kuwa kuanzia leo hataki tena Tuzo kutoka Tanzania.

Mr. Blue ni moja kati ya wasanii wachache waanzilishi wa mziki wa Bongo fleva ambaye alianza kuimba tangu enzi hizo mziki huo unaanza anza lakini cha kusikitisha msanii kama huyu mpaka leo hii hana tuzo hata moja ya hapa nchini wala ya nje ya nchi.

Mr. Blue amefunguka keen he mahojiano na Planet Bongo ya East Africa na kuelezea jinsu alivyokatishwa tamaaa kwa muda mrefu na uamuzi alioamua kuchukua juu ya hilo:

Kusema kweli huwa nafurahi nikipita mtaani naona bado heshima ipo kutoka kwa mashsbiki wa kweli lakini naumia sana ninapo ona sina tuzo yoyote kabatini mpaka leo alafu ninachoumia sio kukosa tuzo peke yake pia kuona mpaka leo hwajanitafutia category ya muziki ninaofanya kwa sababu ukizungumzia marapa wanaofanya hip hop Tanzania mimi siwekwagi kwenye bongo fleva swekwi sasa moans najiuliza mimi ni nani mpaka najiona nipo tu. Kwaiyo kuanzia sahivi sikubali Tuzo yoyote kutoka Tanzania yaani nikipewa nakataa ila Tuzo za nje ya nchi poa tu”.

Hivi sasa Mr. Blue anatamba na wimbo wake wa ‘Mbwa koko’ uliofanikiwa kukamata chati kwenye mtandao wa YouTube na kupelekea kuwa namba moja kwa muda wa wiki nzima.

Mr.blue Hana Beef na Diamond Platinumz.

Msanii wa  muziki nguli Bongo Mr.Blue amefunguka na kukanusha maneno yanayosambaa katika mitandoa kwa muda mrefu  ya kusema kuwa yeye na msanii mwenzie wa muziki Diamond Platinumz wako katika beef zito linalowafanya washindwe kufanya kazi za muziki kwa pamoja.

Mr.Blue amesema kuwa yeye na Diamond walishawahi kufanya kazi mbili  hapo nyuma labda kwa sasa wafanye tena lakini sio kweli kuwa  yeye na Diamond wana beef linalowafanya washindwe kushirikiana.mMr blue anasema kuwa kwa sababu watu wamekuwa wakizusha kuhusu beef lao basi kama kuna uwezekano watafanya kolabo tena ili kuthibitisha kuwa hakuna beef kati yao.hata hivyo anasem akuwa kitu kikubwa kinachowafanya washindwe kufanya kolabo ni kwa sababu wote ni wasani wakubwa na kunakuwa na u-busy kati yao wa kushindwa kukutana.

ni mtu nilishashirikiana nae  sio kitu cha kushangaza kwamba  labda kusema haitawezekana kufanya nae kazi pamoja,lakini unajua shida mnapokuwa wasanii wakubwa kila mtu anakuwa busy  kwa upande wake lakini ikija kufanyika kolabo kati yangu na yake basi inakuwa kitu kizuri sana kwa sababu tutawaonyesha raia kuwa hatuna beef lolote.

kwa kwelie sina tatizo lolote na diamond , ni mdogo wangu ninamuheshimu na ninaheshimu hustle zake, na amekuwa mfano wa kuigwa kwa watu.hayo mambo mengine tusiyachukulie sana serious.

Diamond na Mr blue walishawahi kufanya kazi kwa pamoja kama katika  nyimbo ya BBM  ambao waliimba wakiwa na msanii mwenzao ambae sasa hivi ni marehemu , Ngwea.na pia wimbo wa Dimaond  ambao unajulikana kama kiss to the lady .

Wasanii wengi wanakuwa na beef na migogoro isiyokuwa na maana inayowafanya washindwe kufanya kazi pamoja na kukuza soko la muziki, Mr.Blue anasisitiza kuondoa tofauti zinazotokea kati ya wasanii ili kukuza muziki wa Tanzania.

kwa upande wa diamond kumekuwa na tetesi nyingi za yeye na wasanii wengi kutokuwa na maelewano mazuri ambapo wasanii kama bob junior, alikiba ambao wamekuwa wakishindwa kukaa meza moja na kuzungumza yakaisha na kurudi kufanya kazi pamoja.

Qboy Msafi azidi kutamba na Kamoyo kolabo yake na Mr. Blue

Mwana mitindo mashuhuri aliyejitosa katika mziki,Qboy Msafi anazidi kuonyesha kuwa anaweza kufanikisha hata baada ya kuambiwa kuwa hawezi.

Wengi walimponda kwenye mitandao wakisema kuimba hatoweza lakini kila kuchapo Qboy anazidi kujituma na kuachia nyimbo nzuri.

Diamond Platnumz aliwahi kusema kuwa alimshauri ajitume zaidi katika fani ya nguo na mitindo badala ya kuimba.

Ukiwa makini utagundua anakua kwa kasi na katika kila kazi mpya, mashairi yanazidi kuwa mazuri na hata kuimba anaimarika na kumakinika.

Itakumbukwa Qboy Msafi alikuwa katika lebo ya mziki ya Wasafi na alitoka baada ya kufanya kosa lidogo ambalo hakukusudia lingezua uamuzi uliotolewa.

Pale WCB aliwahi kusema kuwa alikuwa kama yupo shuleni anasoma na sasa amehitimu.

“Mimi nikiwa Wasafi ni kama vile mtu akiwa chuo baadae akahitimu masomo, sasa nafanya mambo yangu tu kibao” alisema pale Radio Maisha mapema mwakani,nchini Kenya.

Baada ya kuachia ‘Karorero’ na remix yake akiwa na Naiboi ambaye ni msanii kutoka Kenya, Qboy na usimamizi wa timu yake wamepiga hatua kubwa kwa muda mfupi sana na hivi karibuni mafanikio yake yatawaacha wengi vinywa wazi.

Baada ya wimbo wake Unaanzaje, ambao ulifanya vizuri pia,Qboy Msafi sasa amemshirikisha mkali wa kutoka zamani Mr. Blue kwenye Kamoyo.

Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wazuri na wakali zaidi nchini Tanzania na hata Africa ya Mashariki.

Kamoyo ni wimbo mzuri sana na ujumbe wake unaendana na hisia na maisha ya watu wengi.

Dude limeandaliwa na Mr. T Touch pamoja na Davy Marchords.

Video ya kolabo hii ni kazi yake Lucca Swahili.

Akipiga kazi kwa kasi hii na ubora huu,basi atazidi kwenda mbali kimziki.

Mashabiki wameupokea vizuri wimbo huu.

 

Moyo Niliokuwa Nao Mimi Ni Wa Msaada-Mr.Blue

Msanii mkongwe wa bongo fleva ambae ana historia ndefu katika muziki huku akianza muziki katika umri mdogo mpaka sasa ameshakuwa mtu mzima na bado amekuwa akifanya vizuri katika kazi yake, Mr. Blue amefunguka na kusema kuwa yeye ana moyo wa kusaidia sana na mpaka sasa ameshafanya kolabo na wasanii zaidi ya kolabo 600, na bado yuko tayari kuendelea kufanya kolabo ilimradi kukuza muziki na kipaji cha msanii mchanga anaetaka msaada wake.Akiongelea swala ilo na kuhusu yeye kurudia maneno katika baadhi ya kolabo za wasanii Mr.Blue anasema inaweza kutokea bahati mbaya kwa sababu amefanya kolabo nyingi hivyo anaweza kusahahu kama alishawahi kufanya kitu icho kwenye nyimbo nyingine kabla.

“juzi nilikuwa nimekaa nahesabu kolabo nilizofanya tokea nimeanza game,zinafika kolabo mia sita, kuna huyo sijui katokea wapi na huyu na yule,kwaio kurudia sometimes inaatokea maana sijui niliimba kwa nani na nani kwa kuwa kuna ubinadamu pia, hivyo ukiona nimeimba wimbo afu nimerudia baadhi ya maneno ni vizuri tukae mimi na yeye tubadilishe, ila sipendi kumfanyia mtu kitu hasiridhie maana mpaka nimeingiza sauti yangu manake tumekubaliana.ila kama nimekosea hata kidogo ni kesi ya kibinadamu,moyo niliokuwa nao mimi ni wa msaada. Alifunguka Mr. Blue

Hata hivyo katika mahojiano hayo ya eNews ya EATV, Mr. Blue aliombwa kujibu tetesi zinazosambaa kuwa hajawai kurudisha fadhila kwa producer aliwahi kumsaidia na kumtoa kwenye muziki kipindi yuko chini mpaka sasa amekuwa msanii mkubwa lakini hajawahi kurudi kwa Amma G,”hapana mi nakataa G-lover hawezi kusema hivyo,kwa sababu hata akisema hawezi kusema nataka fadhila , nooh namjua G, G mi namwita dady na yeye ndie alienikuza kwenye game, ”

Hata hivyo Mr. blue anasema kuwa pamoja na kuwa Amma G alikuwa anamsaidia lakini hakuwahi kupewa ela na producer huyo hivyo basi kutokana na kipaji chake yeye kuwa special ndio maana alimchagua yeye na kwenda kurekodi, hivyo msanii huyo anasema kuwa producer huyo alikuwa akijilipa kutokana na kipai alichokuwa nacho yeye.