Baba Lulu: Sipokei Posa Ya Mtu Kwaajili Ya Binti Yangu

Baba mzazi wa muigizaji wa bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayejulikana kama Mzee Michael Kimemeta amefunguka kuwa hataki posa kutoka kwa mwanaume yoyote.

Lulu ambaye kwa hivi sasa yupo kwenye kipindi kigumu kutokana na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba, lakini moja kati ya watu ambao wameonekana karibu kabisa na Lulu ni baba yake. Ambapo ni juzi tu Lulu alipokuwa anakimbizwa na waandishi wa habari Baba Lulu alichukua nafasi ya ubodigadi kumlinda binti yake.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Baba Lulu alifunguka yafuatayo kuhusu posa ya binti yake:

Unajua suala la ndoa ni la watu wawili yule anayeoa na yule anayeolewa, mwanaume yoyote atakayemleta Lulu sisi tutampa baraka zetu, suala la poss halipo kabisa kwenye msamiati wangu! Siuzi mtoto wangu wala sitaki posa yoyote posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayonipa”.

Baba Lulu alipoulizwa kama anajua uwepo wa mkwe wake anayeitwa Majjizo alisema hamfahamu kwani hajatambulishwa na binti yake lakini pia aliwasihi wananchi wasimuhukumu Lulu bure bali wasubirie sheria ichukue mkondo wake kwani mahakama ndio itakayoamua Kama Lulu ni Ana hatia ama hana hivyo amewasihi watu wasubiri hukumu ya mahakama itakayotolewa hivi karibuni ambayo itaamua hukumu ya Lulu.

 

 

 

Lulu Hana Utu Wala Ubinadamu Kwa Familia Ya Kanumba, Mange Amtolea Uvivu Lulu

Mchambuzi wa mambo ya siasa Mange Kimambi ameongelea tena kesi ya Lulu safari hii akiweka hisia zake wazi na kusema Lulu ameonyesha jeuri kwa familia ya Kanumba hasa mama yake mzazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amefunguka yafuatayo:

Ngoja niwe mkweli kwanini nimeshindwa kuwa na huruma kwa Lulu, ni sababu alivyoishi maisha yake kwa miaka mitano iliyopita, Hakuonyesha hata chembe ya kujutia kwa kilichotoke hasa kwa familia ya marehemu. Lulu alitakiwa atambue kuwa yeye ndio sababu marehemu hayupo duniani, angeonyesha ubinadamu utu hata kwa Mama Kanumba ambaye alikuwa anamtegemea kwa kila kitu, angalau angemjali yule mama, yote Tisa kumi Lulu kushindwa kwenda makaburini kwaajili ya Kanumba day? hapa ndo nilipomuona huyu msichana hana utu, hivi mtu unaanzaje kuwa na huruma kwa Lulu wakati yeye hana huruma kwa wale aliowasababishia majonzi? Hivi mmewahi kumsikia Lulu anafanya kumbukumbu ya Kanumba?

Mange pia hakuishia hapo aligusia suala la mauaji ya mpenzi wake mwingine aliyefariki baada ya Kanumba, Seki.

Kama Lulu angeonyesha ubinadamu kwa tukio hilo sidhani kama nisingekuwa upande wake ningesema amejifunza kitu, Ila mimi hakina kitu kinaniuma kama Lulu kuishi kama vile hana Deni kwa familia ya Kanumba yaani kama vile wasimghasi, Kanumba angekuwepo leo Mama yake asingekuwa anahangaika na daladala na Bajaji sahivi. Lulu anaenda mahakamani anachekacheka, anapiga picha na watu anachezea Simu kwa furaha yote wakati mama wa marehemu yupo mule ndani? Anapishana na mama Kanumba mahakani bila hats salami hiyo nifair kweli? Mama Wa marehemu yupo pale na majonzi yeye ndio kwanza anaenda pale na staili mpya ya rasta kichwani , kavaa high heels na kupanda migari mikubwa anaenda kumuonyesha mama aliyepauka kwa kupanda daladala tu ambaye mkikaa mnamuombea kwa Mungu? Akitoka mahakamani anaenda kupiga picha anabembea huku anakenua!  Hana utu wala ubinadamu huyo msichana period”.

 

Lulu Amekutwa na Hatia Ya Kuua Bila Kukusudia

Muigizaji Lulu Michael aliyekuwa anatuhumiwa kumuua bila kukusudia mpenzi wake Steven Kanumba amekutwa na hatia.

Lulu aliyewasili mahakamani hapo asubuhi ya leo kusikiliza shauri ya kesi yake ambayo ilikabidhiwa kwa baraza la wazee.

Wazee wa Baraza ambao pia ni washauri wa mahakama kuu kanda ya Dar es salaam, wamekubaliana kuwa Lulu ameua bila kukusudia.

Mzee wa kwanza  Alisema:

Nimeridhika na ushahidi uliotolewa kwa pande zote mbili, Elizabeth ameua bila kukusudia kutokana na marehemu kuwa na mwili mkubwa”.

Mzee wa pili pia Alisema;

Naweza kusema kuwa Elizabeth hakuua kimakusudi aliua bila kukusudia”.

Mzee wa tatu pia alimalizia;

Lulu ameua bila kukusudia”.

Baada ya majibu hayo ya baraza la wazee Jaji Sam Rumanyika anategemea kutoa hukumu yake tarehe 13 Novemba mwaka huu.

Bado haijajulikana kwa sheria za Tanzania Lulu atapata hukumu gani mpaka sasa lakini anweza akapata kifungo cha miaka kadhaa jela au hata faini.

Kesi Ya Lulu Yaendelea Kuunguruma Leo, Hatma Yake Mikononi Mwa Baraza La Wazee Kesho

Kesi ya muigizaji wa bongo movie Lulu Michael ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake na mpenzi wake marehemu Steven Kanumba, imeendelea kusikilizwa leo mahakama kuu ambapo Askari Polisi Sargent Nengea amesoma maelezo aliyomwandikisha daktari wa Kanumba Josephine Mshumbisi.

Siku jana iliamriwa ya kuwa askari polisi aliyemuandikisha maelezo daktari wa Kanumba anatakiwa kufika mahakamani hapo kusoma maelezo hayo kutokana na kwamba Daktari Mshumbisi kuwepo nje ya nchi kwa sasa. Haya yafuatayo ni baadhi ya maelezo ambayo Askari polisi huyo alisoma;

Mmoja wa wateja wangu, marehemu Steven Kanumba kwa mara ya kwanza alikuja kwangu mwaka 2011 kwa ajili ya kutoa sumu mwilini. Marehemu alikuwa na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka sana”.

Polisi detective Sargeant Nengea alimalizia kusoma maelezo hayo yaliyotolewa na aliyekuwa daktari wa marehemu Steven Kanumba wakati wa uhai wake.

Baada ya kumaliza kusikiliza maelezo hayo ya upande wa daktari jaji aliamuru kuwa siku ya kesho tarehe 26 octoba, wazee wa baraza watakaa chini na kuamua na kujadili kama Lulu ana hatia ya hiyo kesi inayomkabili au hana.

Itambuliwe kuwa endapo lulu atakutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba na baraza hilo la wazee basi anaweza akahukumiwa kifungoo cha kuanzia miaka nane mpaka maisha jela.

Kesi ya Lulu Yaendelea Kuunguruma ( Tazama Video ya Lulu Akitimua Mbio Mahakamani)

Kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili muigizaji Lulu Michael imehairishwa mpaka tarehe 25 Oct siku ya kesho ambapo shahidi ambaye ni mke wa Dr. Slaa, Dr. Josephine Mshumbusi kutofika mahakamani kutoa ushahidi.

Josephine Mshumbusi alikuwa mmoja wa madaktari waliomtibu marehemu Kanumba, ameshindwa kufika mahakamani siku hii ya leo kutokana na kwamba yuko nje ya nchi na hivyo kusababisha mawasiliano kuwa magumu, hivyo mahakama ikawa imeomba maelezo ya bi. Josephine  yaliyoandikwa polisi siku ya tukio hivyo siku ya kesho inategemewa askari aliyeandika maelezo hayo kufika mahakamani na kutoa ushahidi huo.

Hapo Jana wakili wa mshtakiwa, Peter Kibatala aliomba mahakama ikubali kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na bi. mshumbusi ambaye yupo nje ya nchi kwa sasa lakini mahakama ilikataa ombi hilo na ikasema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushadi huo na kuagiza askari aliyeandika ushahidi huo awepo mwenyewe.

Baada ya kesi hiyo kuairishwa leo asubuhi Lulu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutimua mbio huku waandishi wa habari wakimkimbiza ili kupata picha hizo tafadhali tazama video hiyo hapa.

 

 

Marehemu Kanumba Alikuwa Ananipiga Kila Siku Akilewa, Amejitetea Lulu Mahakamani

Kesi inayomkabili muigizaji wa bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji Steven Kanumba, bado inaendelea kuunguruma katika mahakama kuu.

Kesi hiyo iliyoanzwa kusikilizwa wiki iliyopita, imeendelea leo mahakamani ambapo kwa Mara ya kwanza Lulu amepanda kizimbani kwaajili ya kujitetea dhidi ya kesi inayomkabili. Asubuhi hii Lulu amejitetea kuwa yeye hakumuua Kanumba bali alidondoka mwenyewe na hakumsukuma kama watu wengi walivyodai. Lulu amesema:

Nilipofika kwa marehemu Kanumba nilimkuta yupo kwenye dressing table, Nilikaa kitandani kwa Kuwait hapakuwa na sehemu ya kukaa, Mara nyingi marehemu alikuwa akilewa ananipiga ila sio kwa akili zake, nilikuwa nataka kutoka na marafiki zangu lakini marehemu alinikataza alikuwa hataki nitoke na marafiki zangu lakini nilipomwambia nataka kutoka na marafiki zangu alinikimbiza mpaka nje akiwa na taulo bila ndala, na mimi nilikuwa naogopa kupigwa alipoona simu yangu inapigwa alihisi ni mwanaume anapiga akasema kwanini naongea na Simu ya mwanaume mbele yake? Marehemu akaingia uvungumi akatoa panga akasema Leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja, Baada ya hapo Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa, nilivyoona hivyo nilitoka nikaelekea chooni na kupiga makelele Lakini baada ya mufa mchache nilisikia kishindo kama mtu anafungua mlango nilivyorudi nikamkuta amelala nikajua amejiganyisha nikaanza kumwambia watu wakija nawaambia jinsi ulivyonipiga na panga, nilimwambia Seth, akajaribu kumwamsha hakuamka akasema anaenda kumuita  daktari alivyosema hivyo mi nikaogopa nikaondoka nikaona asije akaamka akaanza kunipiga”.

Pia Lulu aliendelea kujitetea;

Niliondoka nikawasha gari nikaelekea coco beach, huko cocobeach sikuenda kuonana na mtu nilenda mwenyewe kutuliza akili yangu Ghafla meseji zikaanza kusambaa watu kuniuliza wa nasikia Kanumba kafariki, nikachukua Simu nikampigia rafiki yake na Kanumba kumuuliza Kanumba amelazwa hospitali gani? Akaniambia usjie hospitali we niambie uko wapi tuonane Bamaga tulivyokutana akawa kama anataka kuongea na mimi lanini ghafla polisi wakaja kunikamata na kunipeleka kituoni Osterbay, nilijua Kanumba kafariki huko huko polisi”.

Pia Lulu amejitetea Kuwa yeye hakusababisha kifo cha  Kanumba bali yeye ndio aliyepigwa na kuumizwa na marehemu  kutokana na yeye Lulu kuwa na umbile dogo lakini pia marehemu alikuwa na panga.

 

Lulu Ang’ara Kwenye Uzinduzi wa Tuzo za SZIFF

Mwigizaji Lulu Elizabeth Michael amezidi kung’ara jana usiku baada ya kuhudhuria tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF).

Lulu amepata bahati ya kuchaguliwa kuwa balozi wa tuzo za SZIFF ambazo ni tuzo zitakazo husisha waandaaji na wadau wa filamu Tanzania. Ni tuzo za filamu kupitia televisheni zenye nia ya kuleta mapinduzi ya katika soko la filamu nchini Tanzania.

Kama kawaida ya Lulu kupendeza alitokelezea huku akiwa ameng’aa zaidi na kuvutia kutokana na gauni lake alilovaa na hata make up yake aliyopakwa.

Hizi ni picha za Lulu katika uzinduzi uliofanyika jana usiku:

.
.
.

 

Nyota Za Warembo Hawa Zazidi Kung’aa Zaidi (picha)

Katika kuonyesha kuwa kweli wanajitihada ya kazi wanazofanya warembo Elizabeth Michael ‘Lulu’,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Jokate Mwegelo wamekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwa ujumla kutokana na jitihada zao na uwezo wao wa kufanya kazi na zikaonekana na jamii.

Haya ni baadhi ya mafanikio waliyofikia warembo hawa ambao wanahitaji pongezi:

  1. Vanessa Mdee
Vanessa kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram leo hii ametangaza kuwa ataungana na hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam ambapo atakuwa Balozi wa Hoteli hiyo, hayo ni mafanikio mazuri sana kwa Vanessa na anastahili pongezi. 

2. Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwania Tuzo za Vjana 100 wenye ushawishi mkubwa Africa(100 Most Influential Young Africans) kama Mfanyabiashara kupitia kampuni yake ya Kidoti. Hivi sasa Jokate yupo nchini Marekani kwaajili ya kushiriki Mkutano unaojulikana kama Forbes Under  30 Summit kwaajili ya kukutana na Vijana Wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

3. Elizabeth Michael

Elizabeth Michael kupitia Azam TV amechaguliwa kuwa Balozi wa Tamasha la tuzo za filamu kwa upande wa Africa Mashariki ikimaanisha kuwakilisha Tasnia ya Filamu za Bongo Movie katika Tuzo hizo.

Wanawake wote hawa warembo wamethubutu na wameweza na ni vyema kuwapongeza mara kwa mara katika Jamii Zetu.

Elizabeth Michael “Lulu” afunguka kuhusu mipango yake ya ndoa

Staa wa sinema za Kibongo ambaye pia alikuwa msanii wa kwanza kuigiza akiwa umri mdogo Elizabeth Michael “Lulu”, na msanii ambaye amekuwa akikumbwa na skendo mbalimbali , kwa mara ya kwanza ameweka wazi kila kitu kwani mashabiki wake wengi wamekuwa wamekuwa wakiongea mengi kuhusu yeye kuolewa Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Lulu aliweka wazi kuwa anashangazwa na watu wanavyomtabiria ndoa kila siku ikiwa yeye mwenyewe hajaweka wazi aliendelea kusema:

“Nafurahi kweli kusikia hizo habari, hivi mtu anawezaje kila siku anakutabiria ndoa? sasa nazungumza mwenyewe kama Lulu, hakuna kitu kama hicho, kwani ndoa anapanga Mungu kama ipo ipo tu”.

Pia Lulu aliweka wazi kuwa yeye kuishi maisha mazuri kwa kuvaa mavazi mazuri na kujiremba sio lazima kuwa na mwanaume mwenye pesa wa kumuwezesha kama watu wengi wanavyodhani  bali ni yeye mwenyewe kujishughulisha na shughuli zake nyingi anazofanya ambazo watu hawazioni.

kuna tetesi nyingi ambazo hutokea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Lulu ni mjamzito, Lulu ameweka wazi kuwa anashangazwa na jinsi watu wanavyo mzushia kuwa ni mjamzito na ilhali yeye mwenyewe hajaweka wazi ila ni watu wachache wanaotunga habari hizo. Kwenye swala kuwa na familia hapo baadae Lulu alisema:

“Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa na familia hasa watoto, lakini kwa sasa naona bado wangu haujafika siku ikifika endapo Mwenyezi Mungu atanijaalia basi ntafurahi kuwa mama”.

Lulu ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya wasaanii wa Bongo movie anayefanya vizuri sana amekuwa kivutio kwa watu hasa kwa mavazi yake ya kupendeza na kuvutia huku wengi wamejikuta  wakikumkubali kama msanii anayevaa vizuri Bongo movie.

Kauli ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael kuhusu upendeleo na uchawi

Elizabeth Michael ametoa ujumbe maalum kwa mashabiki wake kuhusu mapendeleo na uchawi. Staa huyo wa filamu ya Bongo alitoa mawaidha yake kwa kusema kuwa kibali ndo huwezesha mtu kunawiri kwa anachofanya wala sio mapendeleo ama uchawi kama baadhi ya watu wanavyoamini.

Soma ujumbe alioandika Elizabeth hapo chini:

Umeshawahi kukutana na watu wa aina hii;

1.SHULENI; Mwanafunzi nayependwa sana Na waalimu na staffs wa shule…anaaminiwa zaidi Hata kwenye baadhi ya mambo muhimu ya kishule…Ila kwa wenzake anaonekana kama hastahili na anapendelewa.

2.KAZINI; Mfanyakazi anayependwa na kuaminiwa zaidi na boss na aina ya watu flani wakubwa katika ofisi/taasisi/kampuni…Huyu inawezakana sio bora kuliko wengine pengine ni mwenye kiwango cha chini kabisa lakini anasikilizwa na kushiriki kwenye mambo makubwa au yupo kwenye nafasi kubwa kuliko wanao onekana wanastahili.

Huyu sasa anaonekanaga mchawi tuna atahusishwa na mahusiano na story nyiiingii feki.

3.FAMILIA; Mtu anayeaminiwa sana Na familia na hakuna majadiliano au maamuzi yoyote yatafanywa na familia bila uwepo wake…Huyu kama amebarikiwa uwezo wanafamilia wengine watasema anapewa hiyo nafasi kwasababu ya uwezo wake kama Ana maisha ya kawaida ataonekana anapendelewa.

4.MAHUSIANO; Mke/Mume/Mchumba anayeonekana hafai kwa mwenza wake…Labda ki muonekano,umri,uwezo,historia au chochote tu lkn muhusika ndo anamuamini na kumpenda…Huyu sasa anaonekana mwanga maana kwenye uchawi tunaonaga amevuka

Hizo ni baadhi tu ya jinsi watu wengi tunavyoona vitu katika makundi hayo….Ila ki KIUHALISI na KIROHO hakuna upendeleo wala uchawi bali kuna kitu kinaitwa KIBALI(Kwa wakristo watanielewa zaidi)

Mtu yoyote aliyepewa KIBALI NA MUNGU anaoneka kama mtu anayependelewa katika mambo mengi au mtu anayetumia nguvu ya ziada kufanikisha mambo yake…ni kwasababu ukiwa na KIBALI unauwezo wa kuingia/kutoka mahali pagumu kuingilika/kutoka kwa uwezo wa ki binadamu,unaweza kukaa/kushirikiana na watu wakuubwa ambao kwa uwezo wako binafsi usingeweza kukaa/kushirikiana nao,una uwezo wa kuwa katika nafasi ambazo unaonekana hustahili kuwepo….Yaani kiufupi ukiwa na KIBALI UNAWEZESHWA KUYAWEZA YASIYOWEZEKANA katika hali ya kawaida

Nashukuru MUNGU kwa kuwa mmoja kati ya wengi waliopata KIBALI chake…Mambo mengi yaliyopita,yaliyopo na yanayoendelea kutokea kwenye maisha yangu yanathibitisha KIBALI chake.

 

Elizabeth ‘Lulu’ Michael amchimba Diamond?

Diamond and Alikiba waliachia nyimbo zao ‘Seduce Me’ na ‘Zilipendwa’ siku moja Agosti 25. Alikiba ndo alikua wa kwanza kuachia wimbo wake kabla ya Diamond pia kuamua kuachia yake.

Hata hivyo ‘Seduce Me’ imepata views nyingi kwa YouTube kushinda ‘Zilipendwa’. Ngoma hio ya Alikiba iko na views milioni 2.3 kwa sasa ilhali ya Diamond iko na views milioni 1.5.

Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameonekana akimchimba Diamond kwa kitendo chake cha kuamua kuachia wimbo siku moja na Alikiba.

Katika ujumbe alioandika kwa Twitter, muigizaji huyo wa filamu ya Bongo alisema kuwa mtu akifanya kitu kizuri kwa nia mbaya hakifanikiwi kwa uzuri wote.

Ujumbe wa mrembo huyo inaonekana kama ushauri kwa Diamond ambaye alitoa wimbo wake kushindana na Alikiba lakini hajafanikiwa kumbwaga Kiba kwani wimbo wake unazidi kung’aa tu.