Jeshi La Magereza Lathibitisha Taarifa Za Uhuru Wa Lulu

Siku ya jana alfajiri kuna taarifa zilisambaa kuwa Muigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ameachiwa huru kutoka Kwenye kifungo chake.

Lulu alihukumiwa kwenda miaka miwili jela tarehe 13 mwezi Novemba baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Jeshi la magereza lilithibitisha Tetesi za Lulu kuachiwa huru baada ya kutoa barua rasmi Kwenye vyombo vya habari ikiujulisha umma kuwa Lulu ataendelea na kifungo cha nje.

.

Mastaa KIbao Wamkumbuka Lulu Siku Ya Birthday Yake

Siku ya jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mastaa kibao walimkimbuka kwa kumposti Kwenye mitandao ya kijamii.

Lulu alisheherekea siku yake akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo chake cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake movie star Steven Kanumba.

Mastaa kibao kama Kajala,  Wema, Aunty Ezekiel na wengine wamejitokeza na kumtakia birthday njema:

1. Wema Sepetu

2. Aunty Ezekiel

3. Shamsa Ford

4. Kajala Masanja

5. Lulu Diva

6.  Millard Ayo

.

 

Birthday ya Lulu Kufanyika Muhimbili

Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa  ya msanii Lulu Michael ambae kwa upande wake hatoweza kuifurahia sana kutokana na mazingira anayoyapitia kwa sasa ya kutumikia kifungo chake cha miaka miwili gerezani na kwamba hawezi kuungana na watu anaowapenda.

Hata hivyo familia yake kwa kushirikiana na watu wake wa karibu na baadhi ya mashabiki wameamua kufanya sherehe hiyo kwa kwenda katika hospitali ya taifa ya muhmbili na kusherekea sikukuu hiyo na wagonjwa waliopoa hospitalini hapo.

Wakionekana katika mazingira ya hospitali upand wa wagonjwa wenye vichwa vikubwa , wawakilishi wa lulu watatoa zawadi na misaada kidogo kwa wagonjwa hao kama kumshukuru Mungu kuendelea kumlinda lulu huko alipo na kumuombea ili aweze kuwa na afya njema tena.

Wasanii mbalimbali na watu wake wa karibu wameweza pia kukumbuka siku hii kwa kuweka pichazake katiia mitandao ya kijamii akiwepo Wema Sepetu pamoja na mpenzi wake Majizo.

Fancy wa Hamisa Amkumbuka Lulu Michael

Mtoto wa Hamisa Mobeto ambae jana ilikuwa ni kumbukumu ya siku yake ya kuzaliwa alionyesha huzuni kwa baaadhi ya mashabiki baada ya video iliyokuwa ikisambaa katika mtandao wa instagram ikimuonyesha mtoto huyo akiwa ameshika simu ya mezani  na kuanza kuigiza kama vile anaongea na  Lulu Michael ambae yeye amezoea kumwita aunty,

Fantacy na Lulu walikuwa na mahusiano mazuri kama ya mama na mtoto kutokana na upendo aliokuwa nao lulu michael kwa mtoto wa hamisa pamoja na kwamba lulu na hamisa  waliwahi kutoka kimapenzi na mwanaume mmoja.

Hata hivyo tangu kipindi cha mwanzo hamisa alishawahi kuthibitisha kuwa mtoto wake huyo alikuwa akimpenda na kumzoe sana aunty yake huyo kiasi kwamba hata yeye alihuzunika sana kwa sababu mtoto wake alikuwa akitumia muda mwingi kukaa na Lulu Michael.

Katika ukurasa wake wa instagram, majizo aliweka post hiyo ya mtoto wake huyo wa kike alizaa na Hamisa kipindi wakiwa bado wapenzi kabla ya kuachana na kuingia katika mahusiano na Lulu na kuandika”birthday girl ameshindwa kuvumilia imebidi aongee na aunty @elizabethlulumichael fake ..we miss you so much angalia mpaka @babyfancy anajiongelesha mwenyewe”

Dr. Cheni Amefunguka Mazito Kuhusu Maisha Ya Lulu Gerezani

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni  amefunguka mazito juu ya maisha ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ gerezani.

Ni miezi kadhaa tangu Lulu aende jela baada ya kuhukumiwa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Wiki iliyopita tuliona jinsi Dr. Cheni alivyomuwakilisha Lulu kwa kutoa msaada kwenye kampenzi ya Namthamini ya EATV. Dr. Cheni ni mtu ambaye siku zote amekuwa na ukaribu sana na Lulu hadi Lulu humuita Baba yake.

Kwa mara nyingine Tena Dr. Cheni amefunguka kuhusu maisha ya Lulu gerezani ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv amefunguka haya:

Kusema ukweli Lulu ni binti jasiri sana yaani sisi tuliokuwa nje tuna majonzi kuliko yeye mwenyewe yaani ukienda unamkuta ana furaha mtacheka naye mtafurahi kikubwa anasema tu niombeeni basi na kitu kikubwa Lulu huko jela anatizama sana mabinti anasema anawapenda sana mabinti wa Kitanzania”.

Lakini pia Dr. Cheni amesema kuwa Lulu  ana kawaida sana ya kutoa misaada ingawa hapendi kujitangaza Kwenye mitandao ya kijamii pia amedai Miezi michache kabla hajahukumiwa alienda kutoa msaada segerea.

 

Lulu Michael Atoa Msaada Kutokea Jela

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameguswa na kampeni ya kuchangia pedi kwa watoto wa kike na kutokea gerezani alipo kwa sasa ametoa msaada wake kupitia kwa mtu wake wa karibu Dr. Cheni.

Kituo cha televisheni cha EATV kinaendesha kampeni inayoitwa Namthamini ambayo inakusanya na kupokea michango ya pedi kwa ajili ya kuwapelekea watoto wa kike wa shule mbali mbali ambao hawana uwezo wa kununua pedi.

Mchango huo kutoka kwa Lulu umewasilishwa na Muigizaji wa Bongo movie Dr. Cheni ambaye pia ni mtu wa karibu wa Lulu ambaye amesema Lulu ameguswa sana na kampeni ile na ameamua kutoa kidogo alichoweza kuwa nacho.

Kwenye mahojiano na East Africa Tv, Dr. Cheni alizidi kufunguka haya kuhusu mchango huo:

Kwanza niwapongeze kwa hii program nimekuwa mfuaatiliaji na naamini itakuwa na ‘Impact’ kubwa kwenye jamii.

Kikubwa mimi Mahsein @drchenitz ni Muwakilishi, nimeleta ‘pic kadhaa za Pads ambazo zitakuwa msaada kwa Wasichana wakitanzania.

Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU), Ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo, yupo (jela)

Zaidi amesema niwaambie ANAWAPENDA saana na anawataka mabint wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia”.

Lakini Dr. Cheni alisema tetesi zito zilizokuwa zikisambaa kwa muda sasa kuwa eti Lulu hayupo jela bali alishatoka na kafichwa nchini Uganda jambo ambalo amesema ni tetesi tu mitandaoni.

Mama Kanumba Adai Anaogopa Maneno Ya Kejeli Kutoka Kwa Lulu

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ amedai kuwa anahofia Elizabeth Michael ‘Lulu’ atamtolea maneno ya kejeli pindi atakapotoka jela.

Miezi michache iliyopita Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.

Tangu Lulu amefungwa Mama Kanumba amekuwa akiongea mambo kadhaa kuhusu Lulu ambaye miaka michache nyuma alikuwa hana uhusiano naye mzuri sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Mwanaspoti, Mama Kanumba amefunguka na kudai kuwa hofu yake kubwa ni Lulu kumezeshwa maneno akitoka kuhusu na kuishia kumtolea maneno ya kejeli.

Mtoto wangu huyu anaweza kurudi mtaani na kushikwa masikio tena na watu kunifanyia vibweka kama alivyofanya awali, wala asithubutu wala kujihangaisha kwa kuwa iliyomshtaki ni Jamhuri hivyo anapaswa kuniheshimu. Hakuna neno lililoniuma kama siku aliyonipigia na kuniita kubwa jinga huku akiniambia haogopi polisi wala mahakama”.

Lakini pamoja na hayo Mama Kanumba amesisitiza kuwa hana bifu na Lulu wala kinyongo na atakuwa tayari kumtembelea jela kumsalimia kama ndugu zake watakuwa tayari.

 

“Lulu Akijishusha Kwangu Akaniomba Msamaha Nitamsamehe”- Mama Kanumba

Mama mzazi wa Marehemu Kanumba ameibuka na kuweka wazi kuwa hana kinyongo na Lulu endapo atakuwa tayari kujishusha na kumuomba msamaha basi atamsamehe.

Lulu alifungwa miezi michache iliyopita baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia marehemu Steven Kanumba aliyekuwa naye kwenye mahusiano kwa kipindi hiko.

Kipindi chote wakati kesi inasikilizwa ni wazi kabisa Lulu na Mama Kanumba hawakuwa katika nafasi nzuri kwani walionekana wakipishana bila kusalimiana na hata Lulu alipohukumiwa kwenda jela Mama Kanumba alisema amefurahishwa.

Mama Kanumba alijiwa juu na watu hasa mashabiki za Lulu ndipo juzi alipofika kuwa hajawahi kumuombea Lulu mabaya na hana tatizo naye kwani alishamsamehe tangu zamani na hana kinyongo naye.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mama Kanumba amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo Lulu Akitoka jela akaenda kumuomba msamaha basi atamsamehe.

Lulu alihukumiwa na Jamhuri ilikuwa nje ya uwezo wangu iwe nilimsamehe au sikumsamehe sikuwa na uwezo wa kufuta kesi. Mimi sina kinyongo na Lulu alikuja mara ya kwanza nikamsamehe na kama akimaliza kifungo akiwa tayari kwa kuwa yeye ni mtoto mimi mtu mzima kwaiyo yeye anapaswa ajishushe kwangu akiwa tayari akinipmba msamaha mimi nitampokea”.

 

Mama Kanumba: Natamani Kwenda Kumuona Lulu Gerezani

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Mama Kanumba ameibuka na jipya tena huku safari hii anatamani kwenda jela kumuona Lulu.

Mama Kanumba hakuwa na uhusiano mzuri na Lulu kwani mpaka a nafungiwa walikuwa kama wana ugomvi fulani huku Mama Kanumba alidai sababu kubwa ni Lulu kumtupa mama huyo na kutomjali kwa lolote.

Miezi michache iliyopita Muigizaji wa Bongo movie Lulu Michael alifungwa gerezani kwa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.

Baada ya Lulu kufungwa Mama Kanumba hakusita kuonyesha furaha yake juu ya Lulu kufungwa na baadae alipoulizwa endapo ana mpango wa kwenda kumtembelea Lulu gerezani alisema hajui mpaka afanye mazungumzo na Mungu wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mwananchi Communications, Mama Kanumba ameibuka na kusema anatamani kwenda kumuona Lulu jela:

Tangu Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi ndio sababu, na kusahau ya the kwamba mimi nilishamsamehe kama binadamu na siye niliokuwa mlamlamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishitakiwa na serikali”.

Lakini Mama Kanumba amesisitiza kuwa yote yaliyotokea anamuachia Mwenyezi Mungu kwani yeye kufungwa hakuwezi kumrudishia mtoto wake ambaye amekwisha tangulia mbele ya hali.

Johari Aongelea Safari Ya Kwenda Kumuona Lulu Jela

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula amefunguka na kuongelea sababu zilizompelekea kutomtembelea Lulu gerezani mpaka leo ilhali alifungwa tangu mwaka jana.

Elizabeth Lulu Michael ‘Lulu’ alihukumiwa kwenda jela mwaka jana tarehe 13/11 kwa muda wa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Muigizaji wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba.

Tangu Lulu ametupwa jela kumekuwa na taarifa nyingi juu ya nini kinaendelea kwa Lulu huko Lupango. Wasanii wengi waliokuwa na ukaribu na Lulu wamedai ni vigumu kwenda Kumuona jela kwani kuna sheria za kwenda hivyo wengi wao hawajamuona.

Johari amefunguka Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, na kusema tangu Lulu amefungwa hajawa za kwenda Kumuona wala kumuuliza hali kwani anaogopa kumuongezea machungu.

Kiukweli tangu Lulu amefungwa jela sijawahi kwenda kumsalimia, kwa upande wangu naona unapokwenda kumtembelea ni sawa na kumuongezea machungu na ukweli zaidi hivyo mimi ndio naona na ndio maana nakuwa mzito kwenda”.

Lakini pia Johari amesema kiitendo kilichowapata wote wawili kumaanisha Kanumba kufariki na Lulu kufungwa kiliwaumiza watu wote lakini ana wacha Mungu.

Mwijaku Afunguka Mengi Juu Ya Maisha Ya Lulu Gerezani

Moja ya watu maarufu katika tasnia ya sanaa na habari anaejulikana kama Mwijaku ambae aliweza kujulikana zaidi kutoka katika tamthiliya ya mahusiano iliyokuwa ikirushwa na Clouds Mv, amefunguka na kusema mengi juu ya maisha mapaya ya msanii Lulu Michael tangu amehukumiwa kifungo chake cha miaka miwili gerezani.

Mwijaku ambae amesimulia kila kitu na hali halisi ya msanii Lulu Michael amesema kuwa Lulu kwa sasa yupo katika wakati mgumu sana kiasi kwamba hata maisha anayoishi huku gerezani hakuna ambae anaweza kuishi kama vie watu wanavyofikiria.

Mwijaku anasema kuwa Lulu Michael amekuwa akijutia kila tukio lililotokea siku ya kifo cha marehemu Kanumba  na anasema kuwa anatamani hata asingpokea simu ya marehemu na kwenda nyumbani kwa marehemu usiku ule.

Hata hivyo bado Mwijaku anaendelea kusimulia na kusema kuwa Lulu anaishi maisha magumu na anasema kuwa ameshajutia na kujifunza sana kwa kila kilichotokea katika maisha yake ya nyumbani anayoishi sasa hivi. Mbali na yote msanii Lulu Michael amekuwa na wasiwasi sana hasa kuhusu maisha ya familia yake kwa sababu yeye ndie alikuwa baba na mama wa familia yake, anasikitika sana na maisha anayoishi mama yake,mdogo wake na baba yake kwa sasa kwa sababu hajui wanakula nini au kuvaa nini ilhali yeye aliyekuwa tegemezi lao hayupo tena kama zamani.

Lulu ametoa shukrani zake kwa wanaomuombea na wazidi kumuombea maana maisha ya huko sio mazuri , lakini pia anawaomba watanzania wote wamsamehe kwa kile alichokitenda ili atakapopata bahati ya kurudi uraini basi aishi maisha mapaya yenye amani.

Kwa kumalizia Mwijaku anasisitiza watu kuwa wawe na moyo ya kusameheana sana kwa kila jambo,tuwe na mioyo ya kuombeana na kukumbuka yale ya nyuma.

Mwijaku anaweza kuwa ndio mtu wa kwanza kwenda kumuona lulu michael tangu apelekwe gerezani na kuweza kuleta mrejesho wa kile alichokiona kuhusu maisha ya lulu gerezani,elizabeth lulu ichael alifungwa mwaka huu November 13, baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kama adhabu ya kitendo hicho.

Hamisa Amefunguka Kuhusu Bifu Lake na Lulu

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie, Hamisa Mobetto amemzungumzia muigizaji mwenzake Elizabeth ‘Lulu’ Michael aliyehukumiwa wiki iliyopita miaka miwili jela pamoja na uhusiano wao.

Siku za nyuma Hamisa na Lulu walikuwa na bifu kubwa tu ambalo lilitokana na wao kugombania mwanaume mmoja ambaye ni Majizzo. Hamisa alikuwa na uhusiano kwanza na Majizzo ambao ulipelekea kuzaa mtoto mmoja lakini baadae tena Majizzo aliachana na Hamisa na kuanzisha uhusiano na Lulu kitendo kilichopelekea mwanzo wa bifu la warembo hao wawili huku Hamisa akimtuhumu Lulu kwa kumuibia bwana ake hali iliyopelekea wawili hao kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Lulu kuhukumiwa Hamisa aliwashtua wengi baada ya kujishusha na kudai anamuonea huruma na hadi kufikia hatua ya kudai kuwa anampenda Lulu. Kitendo hiki kiliwaacha watu wengi midomo wazi na kwenye mahojiano na Millard Ayo alifunguka yafuatayo kuhusu uhusiano wake na Lulu:

Mimi kumposti Lulu ni kitu kidogo sana kwa sababu mwanangu Fantasy anapokuwa kwa baba yake Lulu naye anakuwepo ikimaanisha kuwa ni mama yake mdogo au mama wa kambo kwa mwanangu, lakini watu wanapenda tu kukuza mambo kwenye mitandao ya kijamii just because people don’t see each other doesn’t mean wana ugomvi mwisho wa siku mimi sina ugomvi na mtu na isitoshe nilivyo mposti Lulu ilikuwa ni kwa nia njema kabisa na kusema ukweli nimeumia Lulu kufungwa kwa sababu hata nilikuwa nikisafiri najua kabisa Fantasy nikimuacha na baba yake kunakuwa na mwanamke anamuangalia ambaye ni Lulu kwa sababu mimi siamini sana wafanyakazi wa ndani”.

Hamisa alifunguka hayo baada ya watu wengi kumuita mnafki baada ya kumuongelea vizuri Lulu lakini baadae alionekana kamualika kwenye sherehe yake Mama Kanumba ambaye anajulikana kama ni Hasimu Mkubwa wa Lulu.

Mama Kanumba: Nilikuwa Naumia Nikimuona Lulu Anakula Raha, Nimefurahi Alivyofungwa Sahivi Zamu Ya Familia Yake Kulia

Mzazi wa marehemu Kanumba, Mama Kanumba amefunguka kuhusu furaha aliyokuwa nayo baada ya muuaji wa mtoto wake muigizaji Lulu Michael kuwekwa ndani kwa miaka miwili.

Tangu hukumu ya Lulu mengi yamesemwa huku watu wakigawanyika na misimamo kutofautiana kwani kuna watu wanasema kuwa afadhali Lulu amefungwa na kuna wanaosikitika Lulu kufungwa kwa sababu ni binti mdogo.

Baada ya kifo cha Kanumba, Lulu alikuwa karibu sana na Mama Kanumba lakini baadae ghafla ule ukaribu ukaisha na kusababisha tetesi kuenea kuwa wawili hao wamegombana huku sababu ikiwa haijulikani.

Kwenye mahojiano ambayo Mama Kanumba alifanya na Global TV alifunguka yafuatayo:

Kwa kweli tunashukuru haki imetendeka kwaiyo kama familia ya Lulu wamelia mimi ninalia kila siku wao miaka miwili tu atatoka mimi mtoto wangu sitamuona tena yaani harudi tena, Baada ya hukumu kutolewa tulienda makaburini kufanya misa lakini mimi sherehe yangu nitaenda kuifanya kanisani kwa kutoa shukrani ya pekee. Kwa muda mrefu familia yetu imekuwa ikiumia tukimuona Lulu nakula raha anaenjoy anafurahia iiltuumiza sana kwa muda mrefu ni bora mtu usimuone lakini anaposti anavyokula raha kweli tulikuwa tunahuzunika sana, lakini kesi ilivyoanza tulitegemea kesi haki itatendeka na tunashukuru Mungu ametutendea kwa kweli”.

Mara ya kwanza hukumu ilivyotolewa hakimu wa Lulu, Peter Kibatala aliweka wazi nia yao ya kukata rufaa lakini habari zimeenea kuwa kutokea jela Lulu amekataa kukata rufaa badala yake ameamua kutumikia kifungo chake chote cha miaka miwili.

Kifungo Cha Lulu Watu Wamegeuza Ushabiki na Biashara- Belle 9

Msanii wa Bongo fleva anayejulikana kama Belle 9 amefunguka kuwa amesikitishwa na kifungo cha Lulu lakini yeye ameamua kukaa kimya juu ya suala ilo kwa sababu ameona watu wengi wamegeuza ushabiki.

Tangu kifungo cha miaka miwili cha muigizaji Lulu Michael kitangazwe siku ya Jumatatu mastaa mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti na hata wengine kubishana baada ya kugawanyika huku wengine wakiwa upande wa Lulu huku wengine wakiegemea upande wa Kanumba. Wasanii kama Mrisho Mpoto na Afande Sele wameingia katika majibizano makali mtandaoni baada ya kila mmoja kuegemea upande wake na kuamini anachotaka kuamini.

Belle 9 alipohojiwa na Millard Ayo Tv aliweka wazi hisia zake na kusema kuwa kwake yeye imekuwa ngumu kuongea chochote juu ya kesi hiyo siku hizo zilizopita kwani anaamini kuwa kuna wasanii wanashabikia kesi hiyo kwa sababu zao binafsi:

Unajua ishu ya Lulu ni ishu ambayo wakati inatokea watu wengi walionyesha sana ushabiki kwa upande fulani kwaiyo mimi nilivyoona ile hali ya kama kuna mgawanyiko na utimu sikupenda kuongea kitu kwa kweli kwa sababu ningeoneana kama naegemea upande fulani, Lakini kiukweli iliniuma kama msanii mwenzie kama mtu ambaye huwa anasapoti kazi zangu na tupo vizuri wakati wote hata tukikutana ni mtu ambaye tunapiga stori freshi tu lakini nilivyoona tu haya mambo ya ushabiki nikaona niache tu maana kuna watu huko mtaani wakiona umeegemea upande wa Lulu au upande wa Kanumba wanakutenga”.

Pia Belle 9 aliwasihi wasanii wasigeuze kifungo cha Lulu kama njia ya kufanyia bishara au upepo fulani wa trending ili tu waonekane mbele za watu kuwa bado wapo kwenye ramani.

Mange Kimambi: Jaji Ametenda Haki Lulu Kufungwa, Big Up Kwake

Mwanaharakati wa Siasa Mange Kimambi amefunguka mapema leo mara baada ya hukumu ya Lulu kutoka na kuhukumiwa miaka miwili jela, Mange amedai Lulu amestahili hukumu hiyo.

Tangu kesi hii imeanza Mange amekuwa muwazi na kusema anatamani Lulu afungwe ili tu ajifunze kidogo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Mimi ningekuwa hakimu ningemkuta na hatia ya kuua bila kukusudia, Ila ningempa adhabu ndogo tu ya mwaka mmoja au miaka miwili jela. Mtu kafariki wakati wa ugomvi na aliyekuwa anagombana naye alikimbia that means kuna kitu alifanya bila kukusudia kilicho sababisha  hicho kifo, anyways kila mtu na Bahati yake”.

Baada ya Jaji kutangaza hukumu yake na kusema miaka miwili Mange alifunguka kuwa anafuraha kuwa haki imetendeka na sheria imekata pande zote:

Breaking News…Lulu amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela..Jaji ametenda haki Big up Jaji Lumanyika umetenda haki!! Sio kama nimefurahi Lulu kufungwa ila nilichotaka kuona nihakuna double standards, nilitaka kuona haji inatendeka na Lulu anstahili hiyo miaka miwili jela labda itampa muda wa kufikiria ni kwa jinsi gani matendo yake yalivyo muumiza Mama Kanumba na famili yake labda akitoka atakuwa more humble. Lakini pia mwanasheria wa serikali achukuliwe hatua za kinidhamu afukuzwe kazi alijaribu sana kumbeba Lulu ili amsaidie kushinda kesi”.

Mara baada ya kesi hiyo kuisha Lulu alitupwa jela na Mama Kanumba aliongea na Waandishi wa Habari huku akishukuru Mungu kwa haji kutendeka lakini Mama Lulu alionekana akiondoka mahakamani huku akiwa ameshikiliwa kwa sababu ya kukosa nguvu.

Lulu Michael Amehukumiwa Miaka Miwili Jela Kwa Kumuua Bila Kukusudia Kanumba

Siku ya leo muigizaji Lulu Michael aliwasili mahakama kuu kwa ajili ya kusikiliza hatma ya kesi yake ambapa Jaji wa Kesi hi to Jaji. Rumanyika amemhukumu miaka miwili jela.

Jaji Rumanyika aliiambia mahakama katika uamuzi wake amemkuta Lulu na hatia kuwa alimuua Kanumba ingawa hakukusudia kumuua kwa maana ilikuwa ni bahati mbaya ambapo aliongea maneno haya:

Ushahidi wa mazingira ni ushadi ambao mshtakiwa alikuwa kuwa yeye ndio mtu wa mwisho kuwa na marehemu ambapo mshtakiwa alikuwa na marehemu kwa miezi minne, ushadi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, pia mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, maelezo ya dokta Josephine sio maelezo ya cheti cha hospitali hayakuwa na hadhi ya hospitali…”.

Baada ya maelezo hayo Jaji alitangaza kuwa baada ya kupitia ushahidi na maelezo ya pande zote mbili amemkuta mshtakiwa ana hatia ya kuua bila kukusudia na hivyo kumpa kifungo cha miaka miwili jela.

Baada ya hukumu hiyo wakili wa Lulu, Peter Kibatala amefunguka na Kudai Kuwait Wana mpango wa kukataa rufaa juu ya kesi hiyo kwa kile walichodai sio haki kwa hukumu ile.