“Sina Sababu ya Kusema Namuhurumia Kapata Matatizo Shauri Zake”. Amefunguka Faiza Baada ya Sugu Kufungwa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally ambaye amejipatia umaarufu zaidi kutokana na kuwa mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Uhusiano wa Sugu na Faiza sio mzuri siku zote kwani ni mara nyingi wamekuwa watu wa kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii huku Faiza akimtuhumu Sugu kwa kukataa kumlea mtoto wao na kupelekea vita kali kati yao.

Siku ya Jumatatu Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano Jela baada ya kukutwa na hatia na mahakama ya hakimu mkazi Mbeya ambapo Sugu alihukumiwa kwa kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi na lugha ya fedheha dhidi ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. J.P Magufuli.

Baada ya hukumu hiyo hatimaye mzazi mwenza wa Sugu, Faiza amefunguka kuhusiana na hukumu hiyo na kusema amechukizwa na kitendo hicho kilichofanyika maana hakikuwa cha haki kabisa.

Faiza amesema hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Radio 5 ambapo amedai kitendo hicho kimemuuma kama mzazi mwenzake ingawaje maisha yake yanakuwaga magumu zaidi Sugu akiwa uraiani.

Nikimuangalia kwenye maisha yangu namuona kama adui ambaye hana neno kwangu, kwaiyo mimi sina sababu ya kusema sijui namuhurumia sijui kapata matatizo shauri zake, Hayo matatizo kwa kweli naona akiwa uraiani maisha yangu yanakuwa magumu sana, sijali japo siombi akae jela hivyo lakini saa nyingine naona inabidi aah sijali kwa kweli”.

 

Wolper Amsifia Faiza Kwa Picha Yake Ya Uchi Adai Asijali Maana Wabongo Washamba

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Jacqueline Wolper ameibuka na kumpa tano rafiki take Faiza Ally kwa picha ile ya uchi na kudai asijali maana wabongo ni washamba tu kwa kutoelewa maana ya picha ile.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Faiza aliwashangaza watu wengi baada ya kuamua kurusha picha iliyomuonyesha akiwa uchi kabisa huku sehemu zake za siri zikiwa wazi wakati akizaa leba mtoto wake wa kiume. Baada ya pica hiyo kusambaa ilizua gumzo sana na kusababisha picha hiyo kuenea mtandaoni kama moto wa kifuu.

Baada ya picha hiyo watu wengi walimjia juu Faiza huku mastaa wa mziki kama Snura akimuomba Faiza aitoe picha ile kwa kuwa ilikuwa haimdhalilishi tu yeye kama mwanamke bali wanawake wote maana mambo yanayotokea leba yanapaswa kuwa ya siri kabisa.

Wolper alipohojiwa na kituo kimoja cha habari ili aweze kupima uzito kwenye suala linalo-trend hivi sasa ambalo ni picha ya uchi ya Faiza, Wolper alidai anawashangaa wait wanaomponda Faiza aliyeposti picha hiyo hivi karibuni kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati yeye amevutiwa sana na kitendo hiko na iko siku atamuiga.

Wabongo ni washamba sana ushamba ndio unawasumbua sio kitu kingine kabisa, sioni ubaya wa ile picha hata kidogo eti katudhalilisha sasa pale kamdhalilisha nani? Mimi nimefurahi mno na binafsi ipo siku nitamuiga endapo nitajaaliwa kupata mtoto wangu mwenyewe”.

 

Picha Ya Uchi Ya Faiza Imemponza Polisi Wameingilia Kati

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally amejikuta katika wakati mgumu baada ya picha aliyoweka mtandaoni akiwa uchi anamzaa mtoto wake kumuweka matatani na jeshi la polisi.

Wikiendi iliyopita Faiza alitawala headlines zote baada ya kuamua kuweka mtandaoni picha iliyomuonyesha akiwa uchi leba anazaa. Watu wengi walishangazwa na kujiuliza kuwa ni kwanini Faiza aliamua kufanya kitendo cha fedheha kiasi kile huku wanawake wengi hadi  mastaa kama Snura walimuomba acute kwani anawadhalilisha wanawake wenzie lakini Faiza kuonyesha kuwa hajali alisema baadae angerusha video kabisa inayomuonyesha wakati anazaa.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Faiza kufanya vitendo kama hivi kwani alijipatia umaarufu kwa kuweka picha za uchi au picha zinazomuonyesha akiwa amevaa nusu uchi mtandaoni.

Baada ya kuenea kwa kasi kwa picha hiyo siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza aliwaeleza mashabiki zake kuwa namba yake haitakuwa ikipatikana kwa muda kwani polisi wamezichukua kwa uchunguzi zaidi:

Wateja wangu Simu yangu itakuwa haipatikani kwa muda kwani polisi wamezichukua na sijui watakaa nazo kwa muda gani kwa iyo mliotuma pesa zenu kwa ajili ya mzigo msijali ziko katika mikono Salama na mizigo yenu itafika kwa wakati”.

Baada ya hapo baba watoto wa Faiza aliweka wazi kuwa yeye ndio anatuma taarifa katika mitandao ya kijamii kwani Faiza hayupo. Mpaka sasa hawajaweka wazi ni mini Faiza ameambiwa na polisi.