“Wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayepanga na kupangua,” Harmorapa ambia watu wanaomuongela vibaya

Staa na rapa wa Tanzania, Harmorapa hivi majuzi aliweza kufunguka kuhusu watu ambao wanamtusi na kumuongelea vibaya tangu awe maarufu.

Rapper huyo ambaye amekuwa akifanya vizuri Tanzania na Afrika Mashariki kupitia nyimbo zake hivi sasa ndiye anayepata kiki kubwa Bongo na anavyoonekana, Harmorapa atakuwa na umaarufu kama wa Diamond Platnumz iwapo ataendelea kurelease projects ambazo watu watapenda.

Hata hivyo, akizungumza na Bongo 5 rapa huyu alisema kuwa habebwi na kiki na kuwa kazi yake ndiyo inafanya awemaarufu kwa hivyo wanomchukia wanafanya kazi bure na kuwa ataendelea kuachilia nyimbo zake kama kawaida.

“Watu ambao wanahisi Harmorapa hatodumu kwenye game kwanza wanakosea halafu pia naweza nikasema kwamba wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayepanga na kupangua,”

Aliendelea kwa kusema kuwa…

“Kama mimi binafsi nimejipanga sana vya kutosha. Unajua kwamba maneno yao mimi hayanivinjii chochote ni ile sawa na kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo. Wanavyoniongea mimi ndo wananipa power na wananipa maujuzi na wananipa kuweza. Ni wao wananiweza mimi kuweza na kukaza ilmradi niweze kufanya kazi nzuri.”

Harmorapa  pia amehaidi mashabiki wake projects kubwa ambazo ataachilia mwaka huu.

Tiffah Dangote amependeza zaidi na mavazi ya kiume ya kakake Nillan?

Mtoto wa kwanza wa Diamond Platnumz, Tiffah Dangote, wikendi hii aliwafurahisha wengi alipovalia nguo za mdogo wake, Nillan na kuposti picha kuwaonyesha mashibiki wake.

Kupitia mtandao wa Instagram, mamake Tiffah aliposti picha za Tiffah akiwa amevalia mavazi ya kiume na kwenye caption akaandika alikuwa ameazima nguo za Nillan alizozivaa wakati wa #40 photoshoot.

Rocking @princenillan shirt and hat from his #40 photoshoot. Everything from #BABYSHOP

Mashabiki wengi walimpongeza mtoto huyu kwa fashion sense yake huku wakisema kuwa amependeza sana na nguo hizi. Tiffah Dangote ambaye atafikisha miaka miwili mwezi wa Agosti ameonekana kuwa mtoto ambaye anataste nzuri ya mavazi na inaweza kuwa mamake, Zari Hassan, ndiye anayemfunza mtot huyu kuwa a fashion icon wa watoto maarufu Tanzania.

Kwenye picha hizi mpya, Tee pia amaonekana pia kufanana na baba yake sana. Angalia picha za Tee kama amevalia nguo za mdogo wake hapa.

Tiffah's tomboy look
Tiffah’s tomboy look
Tiffah apendeza na mavazi yake ya tomboy
Tiffah apendeza na mavazi yake ya tomboy

New Video: Harmonize aachia video yake mpya aliyomshirikisha mpenzi wake kama video vixen

Msanii wa Tanzania Harmonize ameachia mpya video ya wimbo wake mpya Niambie aliofanya miezi 6 baada ya Matatizo.

Harmonize ambaye anafanya kazi chini ya uongozi wa Wasafi records amefurahisha washabiki kwa wimbo huu uonawagusa kidani maana ameimba kuhusus mapenzi, kitu ambacho mashabiki wa bongo hupenda.

Katika video yake, Harmonize alimshirikisha mpenzi wake wa dhati, Jacqueline Wolper. Kwa kufanya hivi, mashabiki wengi wameachwa wakifikiria kuwa mapenzi yake na Wolper ni ya kiki.

Hata hivyo, alifutilia maneno haya mbali alipokiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuwa kuna wakati alipogombana na mpenzi wake lakini sasa wamesuluhisha kila kitu.

“Kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa, lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi. Sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki,”

Hata hivyo, tazama video yake mpya hapa.