‘Wengi walikushauri utoe mimba yangu lakini nakushuru kwa kunipa mtoto’ Rayvanny amwandikia mchumba wake ujumbe huu

Rayvanny na mchumba wake wamebarikiwa na mtoto wa kiume, Jaydan. Taarifa za kupata mtoto zilitolewa na Rayvanny kupitia Instagram.

Muimbaji huyu wa Wasafi alimpongeza mchumba wake kwa kumuandikia ujumbe ambao umeewacha wengi wakitamani mapenzi yao. Hata hivyo, Rayvanny aliweza kuweka wazi kuwa wengi walikuwa wakimsihi Fahyma kutoa mimba yake kwa sababu ya umri wake mdogo.

Lakini kwa sababu aliamua kuiweka na kuzaa Rayvanny amemfungulia roho kupitia instagram na kuandika kusema….

Rayvanny na mchumba wake
Rayvanny na mchumba wake

Kuna Kuachana, kugombana,kutengana lakini kuacha yote hayo Swala Kubwa Sana Ulilolifanya Ambalo sitoweza kulisahau ni Kunipa @jaydanvanny kwenye maisha yangu.Maana Ungweza Kutoa Mimba lakini Ulikua Na nia njema na mwanao .Wengi walikushauri Utoe wakasema unajiharibia Future wakasema bado mapema lakini haukua tayari kumpoteza Mwanao. @fahyma_ @jaydanvanny We love you son #Youngparents?

Ishara tosha Idris Sultan ni mkali wao katika Mitindo ya Fashion

Aliyekuwa mshindi wa Big Brother na mchekeshaji nchini, Idris Sultan ni mmoja wa Wanaume ambao wanajitambua katika Mitindo ya Fashion

Ingawa Idris Sultan siku hizi amekuwa kimya, picha zake huongea mengi kumhusu. Kupitia mtandao wake wa Instagram Idris Sultan huwaacha wengi wa kimmezea mate kwa sababu ya fashionable taste yake.

Ni mtu ambaye akivaa suti unatamani kumtazama mara kadhaa kwa sababu ni mtu ambaye huwa anapendeza. Kama huniamini tazama hizi picha Zake.

Sanaipei Tande awasihi wasanii wa Kenya kuandika nyimbo zenye ‘content’ za kuelimisha jamii

Sanaipei Tande sasa hivi ameanza kurudi kwenye muziki baada ya kuchukua break ya muda mrefu. Ata hivyo bado sauti na nyimbo zake ni za kutoa nyoka pangoni.

Hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya ‘Amina’ ambao aliuachia wiki chache zilizopita. Sanaipei amekuwa akiupromote kupitia interview za radio na Televisheni. Ata hivyo aliweza kuzungumza na Bongo 5 ambapo alifunguka kusema kuwa wasanii wa Kenya wamepoteza muelekeo wa nyimbo zao.

Sanaipei Tande
Sanaipei Tande

Na kama wasanii ni jukumu letu kuleta mambo kama haya machoni mwa watu, ila kuimba tu bila maana inasaidiaje jamii!

Aliendelea kwa kusema kuwa wasanii wanapaswa kuachia muziki wenye maudhui. Sanaipei anahisi kuwa wasanii wakipoteza muelekeo kwenye nyimbo zao basi pia Jamii iankosa watu wa kuielekeza.

“Lazima pia tutengeneze miziki ya kuelimisha watu wetu na ‘Simama Imara’

Aliongeza kusema kuwa hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya May.

Tazama picha za ‘pacha’ wake Wema Sepetu

Inasemekana kila mtu duniani anafanana na mwingine japo hawana uhusiano wowote kijamii.
Wakati mwingi,mtu hutupiwa picha akaambiwa,’angalia mbona huyu mnafanana?’

Wema Sepetu
Wema Sepetu

Na sio jambo geni,imetokea mara nyingi hata hapa Tanzania,ila, mrembo Lisa Deedee aka `Tuerny’ amejipatia umaarufu baada ya kusemekana kuwa ni pacha wa kipenzi cha wengi Tanzania,Wema Sepetu,unakubali,hasa huo mwanya?

Tuerny
Tuerny

Tuerny anasema,’Nakumbuka mwaka 2012 niliweka picha mtandaoni, mama akanitumia sms kwamba ninafanana na Wema, nilishtuka lakini tangu hapo akawa kama amebariki hicho kitu. Nilishangaa kila sehemu niliyokwenda watu wananiambia nafanana na Wema.’

Tuerny msichana anayefanana na Wema Sepetu
Tuerny msichana anayefanana na Wema Sepetu

Mrembo huyu amesema kuwa,hajawahi kukutana na Wema ila hapo nyuma watu walipoanza kunifananisha naye, alifurahi akawa ana-comment kwenye picha zake kwenye mtandao wa Instagram.

Kipindi hicho,akawa ananisifia naye anamjibu, lakini kutokana na maneno ya watu kama ilivyo kawaida ya wabongo na issue ya kutoleana povu,akachukia na kunipotezea…Tuerny amedai.

Kuna beef? Idris Sultan na Harmonize wachanana mitandaoni ya kijamii

Inaonekana kuwa Idris Sultan na Harmonize wameanza beef ambayo imewaacha mashabiki kama wameduwaa bila kujua ni yupi watampa support kwa kuwa wawili hawa ni mastaa wakubwa Bongo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Idris Sultan alionekana akimtania Harmonize bila kujua kuwa muimbaji huyu hapendi mchezo. Idris aliandika kusema,

Ogopa rapa wako anapo kiki kuliko wewe. Inabidi mbadilishane wewe ndo uwe rapa.

Harmonize naye hakuchelewa kumjibu Idris Sultan huku akimchana kuwa anaskia kuwa amewekwa na mwanaume mwenzake na kuwa hakuwa na pesa anavyojigamba. Kupitia Twitter Harmonize aliandika kusema….

Nasikia unalala Mbezi kwa mwanaume mwenzio daa huruma. Kwani ulishindaga shilingi ngapi South…??? Mbaya zaidi nasikia unamarinda.

Idris naye kupitia Instagram alimjibu kwa kuposti picha hii na kuandika..

Idris Sultan

Acha nicheke tu, ntafanyaje sasa. Kumpiga nzi risasi ntamuonea maskini. Huyu ni makofi tu ??? #MarindaNimekuaSketiYaShule …. KARIBU KIUMENI ??

Harmorapa awataja mastaa ambao waliompa jina analolitumia sasa

Rapper wa Tanzania, Harmorapa, kwa sasa hivi ni mmoja wa watu maarufu Afrika Mashariki. hii ni kwa sababu ya jina lake na pia nyimbo anazoziachilia.

Kabla ya kuwa staa mkubwa rapper huyo hakuwa anatumia jina hilo lakini baada ya kujitokeza na alikutana na mastaa kadhaa waliomshauri kutumia jina analotumia sasa.

Akizungumza katika show ya Bongo Dot Home cha Times FM, Harmorapper alisema kuwa Roma na Mr T-Touch ni watu ambao walimsihi kutumia jiona la Harmorapa na pia kwa sababu anafanana na mwimbaji wa Wasafi records, Harmonize

“Baadhi ya mastaa wakubwa katika muziki wa hapa Bongo nao walinishauri nijiite hivi, akiwemo brother Roma Mkatoliki na Mt T-Touch,”

Hapo mbeleni rapper huyu wa Tanzania alikuwa akifahamika kama Jembe la Kusini, jina ambalo ata mimi kama shabiki wake naona halingeweza kumake kwa hii industry.