Irene Uwoya Awakanya Wanaopiga Picha za Uchi.

Mwanadada Irene uwoya amefunguka na kuwashauri baadhi ya watu wanaodhani kuwa kupiga picha za uchi na kuweka katika mitandao ya kijami kunasaidia kuwapatia umaarufu kama ambavyo wadada wengi sasa wamekuwa wakifanya.

Irene anasema kuwa hata kama kuna mtu anataka kuwa msanii anatakiwa afuate misingi mizuri ya kuwa msanii kwa kufanya kazi nzuri na wala sio kupiga oicha za nusu utupu na kuweka katika mitandao ya kijamii kama inavyozoeleka.

Mimi nadhani kuna watu ambao wanashindwa kutambua swala hilo,una tofauti kati ya kuwa star na kufanya kitu unachokipenda mabacho kinaweza kukupelekea kuwa star moja kwa moja.

Irene Uwoya ni moja ya wasanii ambao waliwahi kupiga picha za nusu utupu na kuweka katika mitandao lakini kwa sasa ameonekana kubadilika kutokana na kutambua nafasi yake katika jamii lakini pia aliwahi kuitwa na TCRA na kuambiwa kuiomba jamii msamaha kwa makosa yake ya kuweka picha za uchi katika mitandao.

Irene Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Mama Watoto wa Aslay

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Irene Uwoya amefunguka kuhusu ukaribu alionao na aliyekuwa mpenzi wa Aslay, Tessy Chocolate.

Siku za hivi karibuni Uwoya ameonekana akiwa kribu sana na Mrembo ambaye amezaa na staa wa Bongo fleva Aslay, Tessy na kujionyesha kama ni mashoga kwa sasa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ameongelea ukaribu wake na Tessy, Uwoya amepasua kuwa pamoja na kwamba wanaonekana na ukaribu mkubwa lakini wawili hao wakikutana hawana muda wa kuongelea mabwana kama wengi wanavyofikiri:

Ni mtu ambaye tukikutana tunazungumza mambo ya biashara, lakini ishu zake za mapenzi huwaga sizijui, pia ishu kuhusu mahusiano yake ni privacy, huwa nikikutana naye hatuzungumzi masuala ya mapenzi kwa kwa sababu kila mtu ana wake”.

Sijui kwa sasa yupo na nani kwanza hayanihusu kabisa”.

Tessy baada ya kuachana na Aslay amekuwa akisemekana kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mfanyabiashara maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama Jembe ni Jembe, taarifa ambazo mwenyewe hajazithibitisha.

 

 

Baba Jokate Awataka Wema na Uwoya Wamuige Jokate

Baba mzazi wa Msanii na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate, Mzee Urban Costa Ndunguru amefichua siri nzito inayowafanya mpaka Wema Sepetu na Irene Uwoya Wasafikie malengo yao kisiasa.

Kwenye mahojiano na gazeti la ‘Amani’ Nduguru aliliambia Amani katika mahojiano maalum kwa njia ya simu hivi karibuni kuwa:

Mwanangu, Wema, Uwoya wote wana ndoto za kuwa wanasiasa na viongozi wa umma lakini hawa wawili kuna mambo yanawakosesha fursa.

Mimi Uwoya simfahamu sana, namsikia tu habari zake kwenye magazeti, lakini Wema namfahamu kwa sababu baba yake (marehemu Isack Sepetu) nimefanya naye kazi serikalini.

Matatizo yanayowakosesha nafasi za kufikia ndoto zao hawa watoto yako mengi lakini kubwa kabisa ni kuiacha misingi bora waliyolelewa na wazazi wao. Siri kubwa ya kufanikiwa hasa katika kutumikia watu ni kujiheshimu na kufanya mambo kwa siri, siyo kwenda kiholelaholela, unajivunjia heshima mwenyewe”.

Lakini pia Baba Jokate amewataka warembo hao wawili kuiga mfano wa Jokate:

Nimeona wanampongeza mwanangu kwa kuteuliwa kwake (kuwa DC), na mimi nasema wasiishie kumpongeza tu lakini waige tabia zake.

Jokate ni mwanangu, sisemi ni mkamilifu lakini ni msiri sana, vigumu kumuona kwenye jamii akifanya vitu vya ovyo, tabia hii naomba Wema na Uwoyawaiige itawasaidia kufikia ndoto zao za kuwa viongozi“.

 

Steve Amekuwa na Mchango Mkubwa Kwa Wasanii Hasa Muda Wa Matatizo- Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ameibuka na kumkingia kifua Msanii mwenzake Steve Nyerere dhidi ya tuhuma za utapeli na Kula pesa za Michango ya rambi rambi.

Stevw Nyerere alijikuta katika wakati mgumu baada ya kila mtu kumnyooshea kidole na kumnanga kuwa misiba ikitokea anakuwa mstari wa mbele na kuchanganya michango ambayo anaishia kuitumia.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Irene Uwoya amemtetea Steve na kudai mchango wake mi mkubwa sana kipindi cha matatizo kwani watu wanakuwa hawajui wafanye nini hivyo yeye huwapa mwongozo kama kiongozi.

Kama Steve asingekuwa mtu wa kujitoa na kusimamia hiyo misiba tusongekuwa tunatoa heshima za mwisho sasa imekuja imegeuzwa kuwa Steven anasubiria misiba ili afaidike kitu ambacho sio cha kweli kwa sababu akisimama Steve msiba umetokea anasimama kweli kwa sababu msiba ni kitu cha ghafla tunakuwa hatujajipanga kwaiyo Steve anakuwa na uwezo wa kushika simu na kufanikisha mambo mbali mbali”.

Irene Uwoya amesisitiza kuwa Steve ni mtu muhimu sana Kwenye jamii na kama akijiondoa katika shughuli za kujitolea kama hizo lazima atakumbukwa maana mchango wake ni mkubwa sana.

Uwoya- Hakuna Wa Kuziba Pengo La Kanumba

Muogizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kudai bado hajaona msanii mwingine anayeweza kuvivaa viatu vya staa wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba.

Uwoya amesema ameangalia sana mwenendo Kwenye tasnia hii kwa kipindi kirefu na Mpaka sasa hajaona bado msanii anayeweza kuwa hata nusu ya alivyokuwa marehemu Kanumba.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Uwoya amedai Kanumba ni staa aliyekuwa anajitoa ili kuifikisha Bongo Movies mbali, jambo ambalo hakuna anayelifanya kwa

Wakati mwingine alikuwa anatoa pesa yake mwenyewe mfukoni ili tu kufanya jambo la kuipeleka Bongo Movies mbali na kweli alikuwa ameanza kufanikiwa kuitangaza Tanzania duniani”.

Uwoya ameshawahi kucheza filamu nyingi sana na Marehemu Kanumba ambazo pia zimeweza kufanya vizuri zaidi.

Wasanii wengi wamekuwa wakidai tangu Kanumba sage dunia basi na tasnia hii nayo imelega kabisa kwani jitihada zake Kwenye tasnia zilikuwa za kweli kabisa.

Nimependa na Kukubaliana na Uchaguzi wa Jokate- Irene Uwoya

Msanii katika tasnia ya Bongo Movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa amependa na amekubali kabisa katika uteuzi wa Msanii mwenzake Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa wilaya.

Uwoya amefunguka hayo wakati alipokuwa anajibu barua ya wazi ya msanii Rado ambaye alimhoji kuhusu ushiriki wake katika siasa na kudai anaona kama Uwoya amestahili pia kuchaguliwa kuwa mbunge.

Kama utakumbuka mwaka 2015, Irene Uwoya aligombania nafasi ya Ubunge viti maalumu CCM na kusema ukweli alifanya vyema sana lakini Rado amemuuliza Uwoya kama anataka kuenda mbele kama Jokate je Dogo Janja anafaa kuwa kama mume wake?

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya ametoa majibu kuhusu hilo ambapo ameweka wazi kuwa hana wivu wala tatizo na Jokate kuchaguliwa kwani anaheshimu maamuzi ya Raisi Magufuli.

Naamini sana katika maamuzi na mapendekezo ya mwenyekiti wangu wa Chama. Naamini sana na nimependa uteuzi wa Jokate kwa sababu baada ya kampeni na uchaguzi kuisha watu wengi tuliendelea na mambo yetu binafsi lakini ukifuatilia kwa ukaribu Jokate amepambana na amekuwa karibu sana na harakati za chama na haswa kushiriki katika shughuli za kijamii kwa haya na mengi zaidi nampongeza zaidi kwani amepanda mbegu nzuri ambayo amevuna mavuno mazuri hongera kwake Mheshimiwa Jokate Mwegelo”.

 

Hamisa na Irene Uwoya Waomba Radhi Kwa Picha Zao Za Utupu

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya na Mjasiriamali Hamisa Mobetto wameomba radhi baada ya kusambaa kwa picha zao za utupu Kwenye mitandao ya kijamii.

Kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) liliwapa onyo wasanii hawa wawili na kuwataka kuomba radhi baada ya kukiuka sheria za maudhui za mtandao.

Irene Uwoya aliomba radhi mbele ya waandishi wa habari baada ya kusambaa kwa video yake iliyomuonyesha akiwa nusu utupu mwezi uliopita na kuzua gumzo zito.

Lakini pia Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene aliandika ujumbe huu kwa nia ya kuomba radhi kwa mashabiki zake:

https://www.instagram.com/p/BlaPZRPn30Q/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=xx260oz7cz56

Lakini pia Hamisa Mobetto naye aliwaomba radhi Watanzania wote Kupitia vyombo vya habari Lakini pia aliandika ujumbe huu Kwenye ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BlaZbqplAl3/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=9scs819pluxg

Steve Nyererre Akerwa na Picha za Uwoya.

Msanii wa bongo movies Steve Nyerere ameonyesha kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya wasanii kutumia miili yao kama kiki katika sanaa hasa kwa kukaa uchi jambo ambalo limeuwa likifanywa sana na wakina dada katika tasnia ya sanaa.

Steve Nyerere anasema kuwa haamini hata kidogo kama msanii mkubwa kama Irene Uwoya anaweza kutumia mwili wake kuweka wazi kwa ajili ya kupata kiki katika mtandao ilihali swala hili linadharirisha sana hadhi yake  na watu wake wa karibu.

katika ukurasa wake wa instagram , steve nyerere aliandika “sitaki kuamini kuwa kiki inapatikana kwa kukaa uchi au ili uwe star  lazima ufanye kitu ambacho jamii na familia yako itakuwa wewe kama kituko na kitu cha ajabu basi wewe hapo ukajiona star , hapana hapo hata waliokuzunguka watakuona kituko.”

sifa ya msanii ni moja tu , msanii ni kioo cha jamii,kuburudisha na kuelimisha kupitia sanaa ama kipaji chake inapotokea mtu anafanya kinyume na katiba yetu huyo anatuchafua wote, hata wenye maadili wanaonekana walewale.

Wikiend iliyopita, mwana dada Irene Uwoya aliweka picha katika ukurasa wake wa instagram na Kuacha watu mdomo wazi baada ya picha hiyo kumuonyesha akiwa mtupu na sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi ilhali heshima yake katika jamii ni tofauti na yale anayoyafanya.

“Irene Hana Marafiki Wa Kweli, Shamsa Ford ni Mnafki” Mwijaku Amchana Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemwagia povu zito msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.

Siku ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.

Lakini Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:

Irene ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.

Halafu na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza mwenzake”.

Dogo Janja aliweka wazi kuwa hakukerwa na picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake.

Shamsa Ford Aibuka Kumtetea Uwoya Baada Ya Picha Yake Ya Utata Kusambaa

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kumkingia kifua Msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake ya utata kusambaa mtandaoni.

Siku ya jana Irene Uwoya alitengeneza headlines baada ya kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha maungo yake nje ndani ya nguo ya kuogelea.

Watu walimjia juu Uwoya baada ya picha ile kusambaa ingawa mwenyewe alijitetea kuwa alikuwa yuko Beach na lile ni vazi la kuogelea hivyo haoni tatizo.

Shamsa amemtetea Uwoya na kuweka wazi kuwa haoni kama kuna kosa yeye kuvaaa vile hasa ukiangalia alikua mazingira ya baharini hivyo kuvaa vazi la baharini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa maandiko ujumbe huu:

Picture zako zote nzuri mama umependeza sana, mimi nachojua mtu unavaa kutokana na location unayoenda, sasa sidhani kama Ir

Kuna wengine wanavaa en anaweza akavaa hivi halafu akaenda ofisini. Sasa mtu yupo beach mlitaka avae dira.

Mumewe amemsifia amependeza sasa nyie wapembeni mnasema amekosea mnajisumbua, kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake binafsi na Mungu. Tusiishi kwa kuhukumiana maana wa peponi hawajulikani.

hadi dira beach lakini matendo yake ukiyashuhudia unaweza ukatoa mbio. Tatizo lako wewe dada Iren ni hilo umbo ndo limewakosesha amani watu.Ungekuwa na flatscreen maneno yasingewatoka hebu kafanye operation upunguze Gushepu“.

 

Uwoya Awapa Pole Waliosema Picha yake Mpya ni Mbaya Mitandaoni

Kumekuwa na picha iliyosambaa katika mitandao huku wengi wakiiisema picha hiyo kwa mitazamo tofauti kuwa haina maadili na kwamba mwanadada ireen uwoya yuko uchi kutokana na picha hiyo inayoonesha maungo yako.

Baada ya picha hiyo kusambaa sana kila mtu aliweza kuongea lake lakini Irene Uwoya mwenyewe aliamua kuwajibu na kuwatolea povu katika mtandao kwa kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kwa kila anachokifanya mpaka anashindwa kuua ni kitu gani bora cha kuweka katika page yake ili kiwafurahishe mashabiki wake.

ukivaa ngu kawaida ooh ana kidogoro,nikimpost mume ooh ana kigodoro,nisipompost kwanini haumpost haumpendi ..nikivaa nguo ya ufukweni niko uchi mimi mke wa mtu…sasa nasema poleni sana kwa wale iliyowauma..siku nyingine nitawashirikisha nikitaka kupost-Aliandika Irene katika ukurasa wake  wa instagram.

Baada ya hapo alitafutwa na leo tena ya clouds tv na kusema hivi “sijaona tatizo kwa sababu nimevaa nguo hii na nimeenda ufukweni,pale nilikuwa ufukweni labda waniambie walitaka nivae nini’

Irene Uwoya Aapa Kutoifuta Tatoo Ya Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakuja kuiguta tatoo ya marehemu Masogange aliyekuwa rafiki yake kipenzi.

Agnes Masogange aliaga dunia mwezi uliopita baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa pumu enzi za uhai wake yeye na Uwoya walikuwa marafiki wakubwa sana.

Mara baada ya tu ya Agnes kufariki Irene Uwoya alienda kucheza tatoo Kwenye mkono wake kwa ajili ya kumkumbuka shoga yake huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na  Ijumaa Wikienda Uwoya amefunguka kuwa aliichora tatoo hiyo kwa kuwa ni jambo lililotoka moyoni mwake na lilitokana na uchungu aliokuwa nao wa kupitiliza kwa rafiki yake huyo hivyo hawezi kuifuta.

Nitaanzaje kuifuta? Ni kitu ambacho nime-kichora mwen-yewe, tena cha kumbukumbu muhi-mu kwenye maisha yangu, jamani itaendelea kudumu kwenye mkono wangu daima“.

 

Tatoo ya Agness Haukuniuma Kama Tatoo Nyingine:-Uwoya

Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kuelezea kuwa aliamua kuchora tatoo yenye jina la Agness kama kumbukumbu ya rafiki yake huyo kipenzi lakini anasema kuwa katika tatoo zake zote , tatoo hiyo haikumuuma kama tatoo zingine na wala hakupata maumivu yotote.

Irene anasema kuwa aliamua kuchora tatoo hiyo kuonyesha kuwa rafiki yake huyo ataendelea kuishi katika maisha yake kutikana na mapezni ya kweli waliokuwa nayo  kipindi rafiki yake huyo alipokuwa hai.

Nimechora tatoo ya Masogange lakini sikuhisi maumivu kama niliyowahi kuyapata nachora tatoo nyingine mwilini mwangu , nafkiri tu labda kwa sababu ya uchungu mkubwa niliokuwa nao,na nilchora tatoo hiyo ili kila siku ninapoiangalia ninapata amani ya moyo.

 

Kwa Mara ya Kwanza Irene Aongea Alivyoguswa na Kifo cha Masogange

Msanii wa kike wa bongo moviea  Irene Uwoya amefunguka na kuongea kwa mara ya kwanza tangu msiba wa marehemu Agness Masogange ulipotokea na mpka aulipoisha huko kijijini kwao.Irene ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa masogange aliuonekana kuumia sana na msiba huo kwa sababu alikuwa rafiki yake wa karibu sana na ndie alikuwa mtu wake wa kila siku katika maisha yake.

Katika ukurasa wake wa instagram, Irene Uwoya aliandika” Siku zitapita na miaka itapita lakini nitakukumbuka daima,rafiki wa kweli na mwenye mapenzi ya dhati moyoni…najua hata ningetangulia mimi najua ungefanya kama nilivyofanya mimi…nitaendelea kukulilia kwa machozi ya ukimya na kutabasamu kwa tabasamu la huzuni kwa kwuweza kutimiza ndoto yako japo hukufanikiwa kuiona..wewe ni mwanamke shujaa !!!pumzika kwa amani …i will always  love you.

Siku moja kabla ya mazishi ya masogange, Irene uwoya alichora tatoo yenye jina la Agness kama njia ya kuendelea kukumbuka urafiki wake na masogange.

Uwoya Achora Tatoo ya Agness

Mwanadada Irene Uwoya aamua kufanya maamuzi magumu baada ya kuamua kuchora Tatoo yenye jina la rafiki yake kipenzi alifariki wikiendi hii Agness Masogange ikiwa kama ishara ya kutotaka kumsahaua kabisa katika maisha yake.

                                           

Wawili hao walikuwa watu wa karibu sana na hata kufichiana mambo mengi na katika msiba huo irene uwoa alikuwa akionekana mwenye majonzi na hasiye taka kuamini kitu kama hicho kingeweza kumtokea katika maisha yake na rafiki yake.

Kila mtu ameguswa kwa naman ya tofauti kuhusu swala la msiba lakini kwa Irene ameona kuwa njia pekee ya kumuenzo rafiki yake huyo ni kwa kuamua kuchora taoo yenye jina lake.

Nimemzidi Dogo Janja Kila Kitu Labda Yeye Kanizidi Dhambi:- Uwoya

Msanii wa bongo movie nchi irene uwoy amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.

Irene Uwoya ameyasema hayo leo alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena  cha Clouds Radio  alipokwenda yeye na mumewe huyo.Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu  hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.

Ni kweli nimemzidi  umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata, 
Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo

Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio ela bali ni mapenzi ya dhati.

Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa.