Tattoo Mpya Ya Irene Uwoya Yazua Gumzo

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amezaa gumzo kwenye mitandao ya kijamii Baada ya kuanika tattoo yake mpya aliyochora katika siku za hivi karibuni.

Siku ya jana Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene alianika tattoo yake mpya aliyochora kwenye maeneo ya pans kwa nyuma kutokana giographia ya sehemu tattoo ilipo mara moja ilisababisha gumzo.

 

Kuna baadhi ya mashabiki walimjia juu Uwoya kwa kuacha sehemu kubwa ya maungo yake wazi hasa kwa sababu tattoo hiyo ameichora maeneo ya mapaja karibia ya makalio huku wengine hata wakihoji ni nani aliyepata bahati ya kumchora tattoo.

Mpaka sasa Uwoya hajaweka wazi maana ya tattoo hiyo ambayo amechora bastola.

Mungu Nisamehe Naenda Kuiba Mume wa Mtu :-Irene Uwoya

Mwanadada Irene Uwoya ameacha guzo katka mitandao baada ya kuweka picha na caption inayoashiria kuwa kuna kitu anaenda kukifanya na anakijua anakifanya kwa makusudi ikiwa kama swala la kulipiza kisasi kwa kile alichowahi kufanyiwa yeye.

Irene anasema kuwa anajua kuwa anakwenda kuiba mume wa mtu lakini anaomba kusamehewa na Mungu kwa sababu hata yeye wakati wa kwake wanamuiba hakusema kitu alinyamaza kimya.

Ikumbukwe kuwa Irene alikuwa mke halali wa Dogo Janja lakini walikuja kuachana baada ya skendo ya mume wake huyo kusemekana kuwa alitoka kimapenzi na wema sepetu.

Picha Za Irene Uwoya na Ommy Dimpoz Zazua Mazito

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya amekuwa  anatrend sana Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuvunjika kwa ndoa yake na staa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku ya jana Uwoya amerudi Kwenye headlines kwa ajili ya picha zake alizopiga na msanii mwingine wa Bongo fleva Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ambaye alikuwa mgonjwa kwa Miezi kadhaa baada ya kufunyiwa upasuaji wa koo nchini Afrika ya kusini.

Siku ya jana wawil hao wamezua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wakiwa pamoja baada ya kila mmoja kiposti picha hizo Kwenye kurasa zao za Instagram.

Mashabiki wengi wa Uwoya walimtaka aanzishe Mahusiano na Ommy na kudai ndio anaendana naye kuliko hata Dogo Janja.

Wawili hao hawajaweka wazi sababu ya kuonekna pamoja kama ni wako ktika harakati za kuleta project ya pamoja au ni Mahusiano.

Uwoya Adaiwa Kuteketeza Milioni 15 Ndani Ya Siku Moja

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya adaiwa kutumia shilingi za Kitanzania Milioni 15 kwa siku moja kwa ajili ya Kula bata tu.

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya alikodi boti kwa mamilioni kisha kuijaza vyakula na vinywaji vya bei mbaya ambavyo navyo viligharimu mamilioni Uwoya alifanya pati hiyo ambayo ilianza muda wa saa 5:00 asubuhi hadi jioni huku akipewa sapoti na baadhi ya wasanii wenzake akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na mama mlezi wa Bongo Muvi, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ huku wengine wakipewa mwaliko, lakini hawakuweza kufika.

Kutokana na jeuri ya fedha anayoionesha, Uwoya hivi sasa anadaiwa kutoka na bwana wake mpya ambaye ni raia wa Nigeria. Ilisemekana kwamba jamaa huyo ndiye anayemuwezesha kila kitu Uwoya hivyo Dogo Janja ni wazi kwamba ndiyo  basi tena.

Baada ya taarifa hizo gazeti la Risasi lilimsaka Uwoya ili kumhoji kuhusiana na taarifa hizo ambapo aligunguka:

Niliamua tu kufanya kwa ajili ya mashabiki wangu na timu yangu kwa jumla na ilinigharimu kama zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania maana boti yenyewe kuikodisha kwa siku nzima ni kama shilingi milioni tano na hizo nyingine (shilingi milioni 10) zilitumika kwa ajili ya vinywaji na chakula”.

Uwoya alipohojiwa kuhusu kuhusika kwa  tajiri wa Kinigeria alikataa kabisa na kudai ni pesa yake mwenyewe imefanya hayo yote.

Irene Uwoya Amtamani Juma Nature,

Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa katika watu anaotamani sana kufanya nao kazi ya sanaa hasa kuigiza ni msanii wa bongo fleva Juma Nature kwa sababu hata hivyo hajawahi kufanya nae kazi yoyote  tangu ameanza kazi yake ya sana.

Irene ameongea hayo alipokuwa akiongea na Times Fm na kusema kuwa moja ya sifa kubwa ya kutamani kufanya kazi na juma anature ni kwa sababu muoekana wa msanii huyo ni uhusika tosha katika kufanya kazi ya kuigiza .

Kama kuna msanii wa bongo fleva natamani kufanya  nae kazi ( movie) basi ni Juma Nature,  maana jinsi alivyo tu tayari anakuwa ameshava uhusika.

JUma nature alikuwa moja ya wasanii waliwahi kufany avizuri sana hapo miaka ya nyuma na mziki wake kupendwa sana na vijana.

 

 

Wanasema Anaumwa Kwa Ajili Yangu, Sijawahi Sikia Ugonjwa wa Mapenzi :-Uwoya

Mwanadada Irene uwoya amejikuta akimwaga povu katika baadhi ya mahojiano yake na station mbalimbli hasa wanapotaka kila mara kumuuliza kuhusu mahusiano yake na msanii dogo janja aliefunga nae ndo mapema mwaka huu na kusemekana kuwa ndoa hiyo kwa sasa imeota mbawa.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu wawili hao huku ikisemekana kuwa  ndoa ya wawili hao imevunjika kwa sababu irene amepta mwanamue miwngine mwenye pesa kumzidi Dogo janja na ndio maana kumekuwa na kutokuelewana kwao.

Hata hivyo ,Dogo janja aliwahi kulazwa hospitali na kusemwa kuwa sababu kubwa na msanii huyo kulazwa na kutokana na stress zinazotokana na kuumizwa na mapenzi, akijibu swali hilo Irene anasema ‘

wanasema kuwa anaumwa kwa sababu yangu, basi hayo ni makubwa .sijawahi kusikia mtu ana umwa ugonjwa wa mapenzi, ina maana mimi ndo huwa natesa watu je mimi huwa siteswi, maana kila mtu uwoya uwoya… ina maana kila siku katika mapenzi mimi ndio  natesa watu, ina maaana mimi ni tesatesa au mimi chinjachinja wa mapenzi.

Ni kweli kuwa mimi ni mkali lakini huyo mwanaume atakuwa na ugonjwa wake miwngine tu.

Uwoya Afunguka Kuolewa Tena

Mwanadada Irene  Uwoya hivi karibuni aliropitiwa kuwa amechana na mwanamme aliefunga nae ndoa ili kufunga ndoa na tajiri mwingine kimya kimya, Irene ambae alifunga ndoa mapema mwaka huu inasemekan kuwa ndoa hiyo na msanii dogo janja imeota mbawa na wawili hao kwa sasa hawapo tena pamoja.

Hata hivyo Uwoya aliulizwa kuhusu tetesi za kuolewa na mwanaume mwingine , lakini alikataa na kusema kuwa hakuna kitu kama icho watu wamekuwa wakiongea tu.

Hapana , hakuna kitu kama icho,mimi nilikuwa kwenye sherehe jana,kwanza siwezi kuongelea mambo yangu ya ndani kias icho labda kama kuna mambo mengine.

hata hivyo tetesi za kuolewa tena kwa uwoya zinakuja baada ya mwanadada huyo kuonekana kuwa ameachana na mume wake lakini bado amekuwa akionekana mitandaoni akienda sehemu mbalimbali za gharama na kuvaa nguo za gharama sana kitu mabacho hakikuwepo hapo awali alipokuwa kwenye ndoa.

Irene Uwoya Amkwapua Bodyguard Wa Diamond

Muigizaji wa filamu za Kibongo Irene Uwoya ameonekana akiwa na Bodyguard maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Mwarabu Fighter.

Mwarabu Fighter alijizolea umaarufu alipokuwa mlinzi binafsi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz lakini aliacha kazi kwake mapema mwaka huu baada ya kutibuana.

Uwoya ambaye amekuwa akitengeneza sana headlines Kwenye mitandao ya kijamii siku mbili hizi amerusha video iliyomuonyesha akiwa na Mwarabu fighter kazini.

Uwoya kuonekana na Bodyguard kama Mwarabu Fighter kumezidi kuzusha tetesi za kuwepo Mkono wa Kigogo ambaye anasimamia maisha ya gharama anayoishi Uwoya kwa hivi sasa.

Baadhi ya wasanii ambao wameonekana na walinzi wao binafsi katika siku Hizi za karibuni ni pamoja na Jacqueline Wolper na msanii wa Bongo fleva Barnaba Boy.

Irene Uwoya Adai Bata Zake Zinasimamiwa na Management Yake

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Irene Pancras Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa uongozi wake mpya ndio unahakikisha anaishi maisha mazuri.

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya amekuwa akila bata kwenye viwanja vya gharama kubwa ikiwemo mahoteli makubwa huko Dubai, Zanzibar na mikoani hivyo kuibua maswali kwa mashabiki wake kuwa ni mapato ya filamu tu au?

Mbali na matanuzi na shopping za nguvu, Uwoya amekuwa akibadili magari makali huku akiendelea na ujenzi wa klabu yake ya gharama kubwa ya Last Minute iliyopo Sinza- Mori jijini Dar.

Kwenye mahojiano man gazeti la Ijumaa Uwoya aliulizwa kuhusu matanuzi hayo na endapo kuna mtu mwingine zaidi ya Mumewe Dogo Janja anasimamia ambapo  alifunguka:

Hakuna mtu, unajua sipendi kuweka mambo yangu hadharani. Haya ndiyo maisha yangu, ni kawaida.

Kuhusu nguo mpya kila siku Ni mimi tu nimeamua kupendeza. Kama ni kubadili nguo mimi nguo ninazo nyingi sana, sema zamani nilikuwa navaa, lakini sipigi picha. Nadhani hii ishu ya kuvaa na kuposti mtandaoni ndiyo inafanya watu waone ni nguo mpya”.

Lakini pia Uwoya alitoa siri ya kuwa na Management kwa sasa ambayo inahakikisha anajijengea image ambayo anayo kwa sasa kama Msanii:

Kuna siri watu wengi hawaijui. Kwa sasa mambo yote yanasimamiwa na menejimenti yangu. Menejimenti ndiyo inanifanyia kila kitu ambacho watu wanaona ni jeuri ya fedha”.

Kutokana na maisha anayoishi hivi sasa Uwoya kuna tetesi zilikuwa zinadai kuna Kigogo mmoja mwenye pesa ndefu ndio anasimamia lifestyle ya Uwoya kutokana na ukweli Mumewe Dogo Janja hawezi kumfanyia mambo makubwa.

Uwoya Atiwa Mbaroni Baada Ya Kukutwa Anakunywa Baa Usiku Wa Manane

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya na wasanii wenzake kama Tausi Mgedela, Idris Makupa ‘Kupa’, Hamis Changale ‘Mtanga walijikuta mikononi mwa polisi Mkoani Mbeya.

Wiki iliyopita kuna stori ilitrend kuwa Uwoya na Wasanii Wenzake walikamatwa mkoani Mbeya walikoenda kufanya shughuli za kijamii lakini kuna taarifa zilidai walikamatwa na sasa inadaiwa kuwa walikamatwa baa Usiku wa manane.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii hao walikamatwa usiku wa Jumamosi iliyopita ya Septemba 22 kuamkia Septembea 23, mwaka huu baada ya kukutwa wakinywa pombe baa jijini Mbeya wakiwa wamevuka muda wa baa kufungwa. Kwa kawaida sheria zinaonesha kuwa baa inatakiwa kufunguliwa saa 10:00 jioni na kufungwa saa 5:00 usiku, lakini wao hawakujali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ulrich Matei amefunguka:

Walikamatwa na Polisi wa doria baada ya kukutwa baa wakiendelea na mambo yao wakati muda wa kufunga baa umepita. “Tuliwakamata na tulitaka wao ndiyo wawe mfano bora kwa jamii kwa sababu ni kioo cha jamii. “Lakini sikutaka kulikuza jambo hilo kwa sababu lilitokea wakati taifa lipo kwenye msiba mzito uliotokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kule Ukerewe.

Hivyo niliona jambo hilo lisituondoe kwenye maombolezo, kwa hiyo tuliwapa elimu na kuwaachia, lakini liwe ni funzo kwa wengine. “Ni marufuku kunywa pombe muda wa kazi na ni marufuku kupitiliza muda wa kufunga baa.”

RPC Mbeya Athibitisha Kukamatwa Kwa Uwoya na Wenzake.

Wikiend iliyopita kulisambaa kwa taarifa kuwa msanii Irene Uwoya na Tausi walikamatwa na polisi baada ya kuktwa katika kiwanja kimoja cha starehe muda mabao sio kwa kuendeleza starehe. Hata hivyo taarifa zilikuwa zikisema kuwa wasanii hao walitoka polisi hapo kwa dhamana.

Habari za kuaminika zinasema kuwa ni kweli wasanii hao walikamatwa na hawakuwa wawili tu bali walikuwepo na wengine kama Mtanga na Kupa  ambao walikutwa katika kiwanja kimoja wakinywa pombe muda ambao ulikuwa ni wa kufunga.

Hata hivyo mtioa habari anasema kuwa wasanii hao walikamatwa na kulala lupango mpaka siku ya pili jion ambapo mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Fadhili  anaesemekana kuwa ndio aliwaalika katika shoo jijini Mbeya aliwatoa kwa dhamana na kuachiwa huru

Baada ya hapo GLP Waliamu kumtafuta mhusika kituon hapo ndipo walipoongea na afande matei amabe alikiri na kusema “ni kweli tulimtia mbaroni, Irene, tausi na wenzake hao,walikamatwa na polisi wa doria baada ya kukutwa bar wakiendelea kunywa wakati muda wa kufunga ulikuwa umeshafika, tuliwakamata kwa sababu tukitaka wao pia wao mfano mzuri kwa wengine kwa sababu wao nikioo cha jamii.

lakini tliona hakuna haja  ya kulikuza kwa sababu taifa lilikuwa katika masikitiko makubwa ya janga a MV Nyerere, lakini watu watambue kabisa ni marufuku kunywa pombe muda wa kazi au kupituliza muda wa kufunga.

Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuelezea Mahusiano Yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kuzua gumzo siku za hivi karibuni.

Uwoya na Diamond walitengeneza headlines mwishoni  wa wiki iliyopita baada ya Diamond kumposti Mrembo huyo Kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuweka caption yoyote jambo lililozua maswali mengi.

Pamoja na maneno ya hapa na pale ilikuja kujulikana kama Diamond alikuwa amemlipa Uwoya kwa ajili ya ku host Shindano la Jibebe challenge ambalo lilifanyika siku ya Jumapili.

Pamoja na hayo bado Kumekuwa na tetesi kuwa Wawili hao wana mahusiano ya zaidi ya kikazi ilihali Uwoya ni Mke wa Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.

Kwenye mahojiano na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) Uwoya amesema kuwa alichukulia kitendo Cha Diamond kumposti  kawaida ingawa watu walitafsiri vibaya lakini hana Mahusiano na Msanii huyo zaidi ya urafiki wa kawaida:

Sioni kama ni tatizo kwa sababu aliposti tu picha ambayo mtu mwingine anaweza akaposti. Watanzania wanapenda tu kufikiria vitu, ku-judge wanavyoweza wao, haikuwa tatizo kwangu”.

Siku ya Jumapili Kwenye Biko Jibebe Challenge  Irene Uwoya ndiye alikuwa host wa tukio hilo. Shindano hilo lilianzishwa na Diamond baada ya kutoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Jibebe ambao ameshirikiana na Mbosso na Lava Lava.

Diamond Adaiwa Kumnyapia Nyapia Irene Uwoya

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amerudi tena kwenye headlines akihusishwa na mwanamke mwingine ambapo safari hii Malkia wa Bongo movie Irene Uwoya.

Siku ya jana Diamond aliwashangaza mashabiki zake baada ya kuposti picha ya Irene Uwoya katika ukurasa wake wa Instagram bila kuambatanisha na ujumbe wowote hali iliyopeleka mashabiki hao kukosa majibu.

Baadhi ya watu walimjia juu Diamond kwa kitendo kile na kudai anakuwa anakosea kwa sababu Irene ni mke wa mtu lakini pia anakuwa anamkosea heshima Dogo Janja ambaye ni msanii mwenzake lakini pia ni mume wa halali wa Uwoya.

Lakini pia kuna baadhi ya mashabiki walimvaa Uwoya kwa kitendo chake cha kulike picha ile ya Diamond kumaanisha kuwa anafurahia attention ile anayoipata kutoka kwa Diamond na hata kumwambia anamuonea mume wake Dogo Janja kwa sababu ni mdogo kwake.

Diamond tena alienda kulike na kukomenti makopa kopa kuonyesha amekubali tena picha nyingine iliyopostiwa na Uwoya. Kitendo hiki kimetafsiriwa tofauti tofauti na watu kwani wapo waliosema Diamond anafanya hivyo ili kupata kiki, ingawa hakuna aliyesema kitu chochote yote haya ni mawazo ya mashabiki.

Ikumbukwe siku za nyuma kuliwahi kusemekana kuwa Diamond ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Uwoya.

Picha za Uwoya Akila Bata Dubai Zageuka Gumzo Mtandaoni.

Mwanadada Irene Uwoya wiki iliyopita alianza kuonekana yupo Dubai akiwa kama amekwenda kwa ajili ya kupata mapumziko ya peke yake nchini humo, hata hivyo mwanadada huyo amekuwa akionekana kuwa na furaha na kufurahia mapumziko yaeke ingawa katika mitandao ya kijmaii kumekuwa na meneno mengi yanayoendelea katika mitandao kuhusu mwanadada huyo.

Moja ya sababu kubwa ya mwanadada huyo kuandamwa na mashabiki ni kutokana na kwamba alikuwa akionekana yuko peke yake katika mapumziko hayo na kwamba kwanini hajakwenda Dubai na mume wake dogo janja .

Lakini baadae mwanadada huyo alikuja kuonekana katika picha ya pamoja na mwanaume mmoja ambae inasemekana kuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Irene uwoya lakini bado mashabiki hawakutaka kuamini na kuendelea kumshambulia mwanadada huyo.

Kama ilivyo kawaida katika mitandao ya kijamii , mashabiki wamekuwa wakisema mengi kuhusu Irene uwoya huku wakisema kuwa ndoa yake imeanza kuota nyasi na kwamba mwanaume aliyeenda nae Dubai ndie mpenzi wake wa sasa.

Hata hivyo dogo janja hjafungika wala irene mwenyewe kuhusu  tuhuma hizo  zinazoendelea zidi yake.Uwoya amekuwa moja ya wasanii wa kike wanaongoz kusema vibaya katika mitandao ya kijamii.

Gigy Money Amtolea Uvivu Irene Uwoya.

Msanii wa bongo fleva na ‘video vixen’ nchini, Gigy Money amefunguka na kumchana muigizaji wa filamu, Irene Uwoya kuwa umri wake umeshaisha wa kutengeneza ‘skendo’ za kuvaa na kupiga picha za nusu utupu na ndio maana anawasii watu wengine kuwa kama yeye.
Gigy ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kupita takribani siku tano tokea mwanadada Irene Uwoya alipotoa kauli yake, ya kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia ‘skendo’ za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu.
“Ana haki ya kuongea hivyo Irene, kwasababu ameshamaliza ujana wake wa kufanya vitu vya hivyo na anajua faida na hasara zake, ila sisi bado tutaendelea hadi pale tutakapoona imefikia tamati, ndio nasi tutaacha na kuwa kama yeye”, amesema Gigy.
Mbali na hilo, Gigy Money amesema mitandao ya kijamii imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatambulisha katika jamii, jambo ambalo likapelekea na wao kuonyesha kipaji chao cha uimbaji walichokuwa nacho baadhi ya watu.
“Kinachoimba sio mavazi, mimi ninaamini kwenye kipaji zaidi kuliko kitu chochote. Lakini kama tungeanza kwenye muziki wasingetufahamu hadi hii leo na ndio maana kila mtu ana njia yake ya kujisogeza pahali fulani. Kwa hiyo waangalie u-serious wa mtu, vitu vingine ni ‘brand’ tu”, amesisitiza Gigy.

Gigy Money ni miongoni mwa wanadada walioweza kujipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, kwa vituko vyake anavyovifanya kila kukicha bila ya kuhofia kitu chochote kilichopo mbele yake.

Irene Uwoya Awaonya Wanaopiga Picha za Uchi.

Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kuwakanya wasanii wa hasa wa kike kuwa kitendo cha kupiga pich za uchi na kuweka katika mitandao ya kijamii haina umaana wowote kwa sababu kutafuta kiki kupitia swala hilo  linashusha heshima ya mtu.

Mimi nadhani watu hawajui kuwa kuna tofauti ya kuwa star, na kufanya kitu ambacho unakipenda lakini kikakupelekea kuw star.Mimi nawshauri tu watanzania kama unataka kuwa muigizaji ni bora kufuata misingi mizuri tu lakini sio kupiga picha za nusu utupu na kuweka katika mitandao ya kijamii.wanaopiga picha za utupu wanajidhalilisha tu kwakweli.

Mwanadada huyo hivi karibuni pia alikumbwa na skendo ya kuweka picha katika mitandao ya kijamii ambazo hazikuwa za kupndeza na kuitwa BASATA ambao alitakiwa kuomba msamaha Umma  kwa kitendo hicho.