Mapenzi na Ray ni Kitu Hakitawezekana :-Johari

Mwanadada johari amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba Ray amekuwa mpenzi wa Chuchu hans  kwa muda na hata kufikia kupata mtoto lakini hajawahi kuwa na mahusiano na ray kama ambavyo imekuwa ikitangazwa katika mitandao .

Kumekuwa na maneno kuwa kabla ya ray kuwa na mahusiano na chuchu alikuwa na mahusiano na Johari nadipo alipomuacha na kwenda kwa chuchu hans na kumuacha jihari na maumivu.

Hata hivyo, johari anasema kuwa hajawahi kuwa na mahusinao na ray na hata kama ingekuwaje icho ni kitu ambacho hakiwezekani na hakitawezekana kabisa maishani.

Chuchu hans na ray ambao kwa sasa mapenzi yao yanapumulia mashine wanaonekanakushindwana katika mapenzi na kwamba kwa sasa kila mtu yuko anaendelea na maisha yake.

Johari Apendezwi na Wasanii Wanaomwita Mlevi

Mwanadada mkongwe wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameeleza kukerwa na baadhi ya wasanii wenzake kumpa jina la mlevi na kudai wapo wengine wengi ambao wanalewa mpaka wanalala baa.
Akichonga na Za Motomoto News, Johari alisema anachukizwa na baadhi ya wasanii kumuona yeye ndiyo mlevi peke yake wakati akiamua kunywa huwa anakunywa kistaarabu na wala huwa hana ugomvi na mtu yeyote lakini anashangaa kujadiliwa kila kona kwa kuitwa mlevi.

Nashangaa sana kwa kweli, kunywa kwangu pombe basi wasanii wenzangu wananiona mimi ndiye mlevi kuliko wengine wote duniani wakati kuna watu kibao wanakesha na kulala baa wala hao wasanii hawawajadili sasa najiuliza ingekuwa nakunywa kwa hela zao ingekuwaje? Naomba waniache,” alisema Johari bila kuwataja majina wasanii hao.

Ikumbukwe kuwa hapo karibuni mwanadada huyo alilipotiwa kuwekewa  madawa katika kinywaji chake alipokuwa akipata kiywaji katika bar moja jijini Dar na kumuibia pochi yake iliyokuwa na vitu mbalimbali.

Johari Kufanya Maombi Baada Ya Kuandamwa na Mikosi

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula ameibuka na kudai kuwa ana Mpango wa kufanya maombi maalumu kwa ajili kuondoa mkosi ambao amedai umekuwa ukimuandama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari ameibuka na kudai ameamua kufanya maombi maalumu kutokana na mikosi ambapo amesema mwezi uliopita aliibiwa, alipata ajali ya gari hivyo kwake anaona si kawaida kwa hiyo anamuomba Mungu amuepushe na mabalaa ili aweze kumaliza mwaka vizuri.

Ulikuwa mwezi mgumu kwangu, nimepitia kwenye changamoto za mfululizo lakini namshukuru Mungu nipo imara. Nafanya maombi maalum Mungu aniepushe na mabalaa”.

Lakini pia mbali na kupatwa na majanga hayo mwezi uliopita kuna picha ziisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa amelewa chakari na taarifa kusambaa kwamba kwa hivi sasa ana tatizo la kunywa pombe kupindukia.

Johari Amtaka Hamisa Aachane na Diamond

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amempa somo mrembo Hamisa Mobetto kwa kumtaka aachane na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Johari amefunguka na kudai kuwa ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na staa hivyo anajua ni jinsi gani walivyo pasua kichwa hivyo anamshauri Mobetto aachane na Diamond.

Kwenye mahojiano  na Global Publishers, Johari amemtaka  Mobeto, asirudi kwa Diamond, bali angeendelea na maisha mengine maana kurudi ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.

Ningekuwa nimepata nafasi ya kumshauri Mobeto, ningemwambia asimrudie Diamond, lakini ndiyo hivyo nilisikia wako pamoja tena, ninachoweza kumwambia ni awe makini tu maana penzi na staa linaumiza sana. Kwani ni watu ambao hawatulii, atajikuta anajipotezea muda na baadaye kuja kujuta.

Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda”.

Johari alishawahi kuwa na uhusiano wa muda mrefu na staa wa Bongo movie Ray Kigosi lakini walikuja kuachana na Ray kuzaa na Chuchu Hansy.

Johari Akimbia Mjini, Aamua Kufanya Kazi Mikoani.

Mwanadada Blandina Chagula maarufu kama Johari amefunguka na kusema kuwa kwa sasa aanaanza kufanya kazi zake mikoani na sio dar tena kwa sababu kuna vipaji vingi mikoani hivyo ameamua kuznguka huko ili kuvitafuta na kufanya kazi.

Johari anasemakuwa kwa muda mrefu amekuwa Dar wakati kazi za sanaa sasa hivi zinalipa sana mikoani kwa sababu kuna vitu vingi vipya vinatakiwa kuonyeshwa ka mashabiki wao na ndio maana yeye ameamua kufanya kazi huko kuliko kukaa tu mjini.

Ni kweli muda mwingi sasa hivi nazunguka mikoani kwa ajili ya kufanya kazi huko,unajua kwa sasa hivi mikoani sanaa ndio inakuwa kwa kasi kwaio kwa mtu anaejielewa anaweza kutumia fursa hiyo katika kutafuta masoko huko  ili kupata fedha kuliko kungangania Dar tu.

Johari:-Sijawahi Kugombana na Chuchu kwa Sababu ya Ray

Mwanadada mkongwe katika tasnia ya bongo movie Jahari  Blandina Chagula amefunguka na kuzungumzia swala lililokuwa limesambaa kwa muda mrefu kuhusu yeye kugombana na Chuchu Hans kwa sababu ya ray na hawajawahi kugombana kabisa.

Johari ambae ilisemekana kuwa na mahusiano ya kimapezni na Ray kwa muda mrefu na kutengeneza kampuni ya uzalishaji wa filamu nchini ya RJ Company , aligombana na mwanamke mwenzake baada ya kusikia kuwa Chuchu Hans anatoka kimapenzi na Ray ambae alikuwa mpenzi wake yeye hivyo kutaka hata kuvunja kampuni ambayo ilikuwa ni ya umoja wao.

Akikanusha tetesi hizo katika Kikaangoni live ya EATV, Johari anasema kwa “Sijawahi kugombana na mtu yoyote, na sijawahi kugombana na chuchu kwa sababu ya ray, na hata tangu niingie kwenye sanaa siajwahi kugombana na msanii mwenzake hata mara moja.’

Uwezi kuzuia watu kuongea lakini sijawahi kugombana na mtu yoyote na hata siwezi kuzungumzia maswala ya watu, kwa sababu niko hapa kuzungumzia kazi zangu na sio kuzumgumzia watu wengine.

Hivi unavyoniona mimi nina muda wa kugombana kweli, na kwanini mimi nichukie Chuchu anapotoka na Ray. mimi sikuwahi kujuaswala la mimi kutembea na ray na hizo tetezi ni za uongo.Mimi na Ray hatujawahi kuwa wapenzi hata mara moja kwanza unavyoniuliza natumia nguvu nyingi kuelezea maisha ya watu wengine , sipendi kuongelea hivyo vitu.

Kwa kumaliza johari alikataaa kujibu maswali yote ambayo aliulizwa kuhusu mahusiano yake na ray, na hata kuongelea kuhusu Chuchu Hans.

 

Johari Afiwa na Mama Yake,Wasanii Wajitokeza Kumpa Pole

Msanii wa kike bongo movies nchi Johari Chagula amefiwa na mama yake mzazi siku ya tarehe 17 mwezi huu na msiba unafanyika nyumbani kwao jijini Dar Es Salam.Mama wa Johari ambae inasemekana kuwa alikuwa akiumwa kwa muda mrefu kidogo na kuwekwa hospitali kwa matibabu alipata umauti huo usiku wa kuamkia  siku ya jumatano.

Wasanii wengi wa filamu na muziki wamejitokeza kumpa pole msanii huyo kufuatilia tukio ilo la majonzi na la kusikitisha liliompa msanii mwenzao ,pia kwa ajili ya kumsindikiza mama wa Johari katika makao yake ya milele.

Akiongea na waandishi wa habari Jokate alitoa maneno ya faraja kumpa pole msanii mwenzake na kusema kuwa kilichobaki kikubwa kwa sasa ni kumuombea mama ambae anafarijika anapoona wasanii wengine wameenda kumpa pole mwenzao.

sis wote njia yetu ni moja , kikubwa ni kwa dada yetu Johari pole sana pole pole sana,lakini tnaendelea kumtumaini mungu maana mungu akikuita hauwezi kukataa.tumekuja wasanii wengi kwa ajili ya kumpa pole na kumpumzisha mama ayke na nina uhakika huko alipo mama anafurahi kuona wasanii tupo pamoja nae.

nae drcheni pia aliyekuwepo katika msiba pia aliongea na kulelezea majonzi yake kwa msiba huo na kusema.

Mungu ampe subira tu awe na moyo wa subira kwa sabau kuondokewa na baba kuna tofauti yake na kuondokewa na mama pia kuna tofauti yake kila mtu anajua , kuondokewa na mama ni kitu kikubwa sana tunajua machungu yake, tuendelee kumuombea Johari.

Nae Dogo Janja na mwenzie Irene Uwoya walionyeshwa pia kusikitishwa na msiba huo na kusema kuwa hili limekuwa pigo kubwa kwa Johari , kwa muda huu anahitaji sana ukaribu na watu ili aweze kukaa sawa.Hata hivyo Dogo Janja anasisitiza kumshukuru mungu kwa kila jmabo kwa sabau katika dini kifo pia ni ibada hivyo swala lililopo ni kumuombea marehemu.

 

Johari Afunguka Kuhusu Kukaa Kimya Baada Ya Hukumu Ya Lulu,Amwaga Chozi

Watu wengi walimposti katika mitandao ya kijamii ikiwa ni kama njia ya kuonyesha  na kuguswa kwao na  machungu yao baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha miaka mwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia katika mauaji ya msanii aliyekuwa maarufu ndani na nje ya Tanzania marehemu Steven Kanumba.Lakini wapo baadhi ya watu wa karibu kabisa ambao hawakutaka kuonyesha kitu chochote katika jamii , mmoja wapo ni Johari Chagula.

johari chagula amabe pia ni msanii wa bongo movies alikuwa ni mtu wa karibu kabisa na marehemu kwa sababu walikuwa wmetoka mkoa mmoja na walikuwa wakishirikiana karibia katika kila hali na marehemu, yeye pia hakutaka kupost kitu chochote katika mitandao ya kijamii anayojihusisha nayo, hata hivyo alipoulizwa johari hakusita kufunguka kile alichokuwa nacho moyoni.

Johari anasema kuwa sio kila ananepost basi ni kweli anakuwa na maumivu ya kile kilichotokea wengine wanapost tu ili kuonyesha wameguswa lakini laa, lakini pia sio lazima kila maumivu yake ayaonyeshe kwa watu kuwa ameumia inawezekana akawa ameumia lakini ameamua kuvumulia moyoni mwake mwenyewe.

Nadhani kama mtu kitu kinakuuma zaidi unaweza ukakaa tu ukawa unaumia na nafsi yako,sio umuonyeshe kila mtu au uanze kuposti,na sio kwamba nikiweka katika instgram basi yule mdogo wangu vinaweza kumfikia na akajua kuwa johari ameniposti zaidi sana itakuwa inaongeza vitu vingi kwa jamii na kumuumiza na kuniumiza zaidi ndani ya moyo wangu.Huzuni yangu iko ndani ya moyo wangu

Kuguswa nimeguswa sana kwa sababu mimi nipo pande zote mbili , Lulu ni mdogo wangu ameazna tuko nae wote pale kaole, na Kanumba ni kaka angu tuetoka wote Shinyanga nyumbani, kwaio kuguswa nimeguswa sana lakini kinapokuja kitu kama hiki sio lazima nikaposti ili kila mtu nae ajue kuwa nimeguswa au nimeumia sana.wengine labda wamepsti ila wamepost unafiki tu.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu kauli ya baba wa marehemu kuhusu kuwa hukumu hiyo ni ndogo sana , Johari anasema kuwa baba anatakiwa ashukuru Mungu tu kwa sababu haujui kesho yako , tunachopaswa ni kuwa na imani tu na sio kitu kingine.

Baba atambue kuwa Kanumba alikuwa mwanae lakini pia hata Lulu pia ni mwanae kwaio ningemuomba tu aweke imani yake mbele na kumuomba Mungu kwa sabbau ukisema hukumu haikumstaili wakati hata angepewa miaka kumi na akaimaliza miaka yake akirudi anakuwa huru bado.- Alimalizia Johari