Lulu Diva Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto Wake Kijijini

Mwanamuziki wa Bongo fleva Lulu Diva ‘Lulu Abbas’ au maarufu kama Diva Divanna amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbwa na skendo ya kutelekeza mtoto wake wa kumzaa mwenyewe kijijini kwao.

Habari za chini chini zilizo era zimedai Lulu Diva ana kula bata na kuishi maisha mazuri mjini lakini inasemekana kuacha mtoto wake kijijini kwao Handeni Tanga.

Mtu aliyetoa taarifa hiyo ni jirani ameiambia Global Publishers kuwa Msanii huyo alizaa mtoto huyo mwenye jinsia ya kike miaka Sita iliyopita huko Handeni Tanga lakini inadaiwa jambo hilo ni siri kubwa ya familia yake kwani hata mpenzi aliyekuwa naye hajui hili na hapendi kuliongelea:

Ninavyokwambia huyo Lulu alipozaa mtoto huyu alimuacha kwa mama yake kwa muda mrefu sana yeye akaja Dar, lakini kamwe huwezi kumsikia akimzungumzia mtoto wake huyo kwa mtu yoyote wala kusema aliwahi kuzaa”.

Lakini chanzo hiko cha habari kilizidi kutiririka kuwa kutokana na mtoto huyo kukaa na bibi yake kwa muda mrefu  hamjui kama Lulu Diva ni kama yake akimuona anamuita dada jambo ambalo limedaiwa kupendwa na msanii huyo.

Baada ya habari hizi kuenea gazeti hili lilimsaka Lulu Diva ili kumuuliza kama tuhuma hizo alizotupiwa na jirani yake zina ukweli wowote ambapo Lulu Diva alikana kuwa na mtoto na kusisitiza kuwa hajatelekeza mtoto kijijini ila amesema watu wengi wanamfananisha mdogo wake na mtoto wake.

Lulu Diva:Siogopi Kitu Nikitaka Kuachia Ngoma Mpya

Mwandada anaefanya vizuri sasa hivi na ngoma yake mpya ya amezoea , Lulu Abbas marufu kama Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amekuwa na ujasiri wa kuthubutu na kutokuogopa kitu chochote kila anapotaka kuachia ngoma yake mpya hata kama wapo watu watakaokaa wakamponda kuhusu nyimbo zake.

Akiongea na Dizzimonline, Lulu Diva ansema kuwa anaamini kuwa kama muziki ni mzuri siku zote ni lazima utaonekana tu hata kama wapo watu watakaa na kuanza kuongelea vibaya muziki huo.Diva anasema kwa kwa sasa ameshajifunza kufanya vitu bila kuogopa ni kitu gani kinachukua nafasi katika mitandao kwa kipindi hicho, hivyo kama anaamua kutoa nyimbo yake hana kinachomzuia.

Mimi siogopi kitu kama nataka kuachia ngoma yangu hata kuwe kunaendelea  nini katika mitandao ya kijamii  kwa muda huo wa sababu mimi ninaamini kuwa kama muziki wako ni mzuri  hakuna kitakachokufanya  usionekane  so nikuweka jitihada tu katika kazi  na maandilizi ni sumu peke yake.

Lulu Diva anasema kuwa kwa mwaka huu ameamua kuwakonga mashabiki zake kwa sababu amejipanga sana na anaayarajia kudondosha ngoma nyingi.

Kumekuwa na tabia ya wasanii wengi kuwa wanasubiria kama kuna kitu kikubwa kina-trend katika mitandao wakiogopa kuwa trending iyo inaweza kufanya muziki wao kufunikwa.

Lulu Diva Akana Tetesi Za Kunyang’anywa Mali Zote na Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva mwanadada Lulu Diva ameibuka na kukana tetesi za kunyang’anywa mali zote na mwanaume ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Siku za hivi karibuni Lulu Diva amekuwa akitawala vichwa vya habari kwa kasi ya ajabu huku akitawaliwa na skendo kadhaa huku moja wapo ya skendo ambayo imekuwa ikimuandama ni suala zima la mahusiano yake ya kimapenzi.

Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na tetesi kadhaa kuwa Lulu Diva ana uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo fleva kutoka katika kundi maarufu la WCB, Rich Mavoko ingawa yeye amekataa mara kwa mara mahusiano hayo lakini taarifa za mahusiano yao zimekuwa zilisambaa kila siku.

Kuna habari zilidai kuwa Lulu Diva ameachana na mpenzi wake wa siku nyingi anayeitwa Richard ambaye mapema mwaka jana aliweka wazi kuwa ametolewa mahari na yupo tayari kuolewa lakini siku chache zilizopita alikiambia kituo kimoja cha habari kuwa yeye na mpenzi wake wameachana na amesharudisha mahari.

Ingawa hakutaja sababu iliyopelekea wawili hao kuachana taarifa zilienea kuwa wamekata mahusiano yao baada ya Richard kugundua kuwa Lulu Diva ana mahusiano na msanii Rich Mavoko huku tayari akiwa kwenye mahusiano na yeye tayari.

Sasa siku ya jana taarifa zilidai kuwa Lulu Diva amenyang’anywa kila kitu alichonunuliwa na Richard ikiwemo nyumba aliyodai amenunua kwa milioni mia moja na gari la thamani taarifa ambazo jana hiyo hiyo alizipangua na kusema ingawa yeye na Richard wameachana lakini hajamnyang’anya kitu.

Kwenye mahojiano na East Africa Tv, Lulu Diva amezidi kufunguka haya kuhusu tetesi hizo:

Ni vitu ambavyo vimetokea lakini siwezi kuviongelea sana ila nakwambia jamaa siko kwenye mahusiano naye tena lakini nina imani tutakaa sawa kuhusu habari za kunyang’anywa vitu sio kweli sijanyang’nywa na hawezi kufanya hivyo ilikuwa ni ugomvi tu”.

 

Lulu Diva Anyang’anywa Mali Zote , ni Baada ya Kurudisha Mahari.

Siku kadhaa nyuma zilizopita Lulu Diva alikiri kurudisha mahari kwa mwanaume aliyetaka kumuoa huku akisema kuwa mwanaume huyo alikuwa akifata sana na kusikiliza maneno kutoka kwa ndugu zake ambao walikuwa hawataki yeye kuolewa katika familia hiyo, huku maneno  ya chinichini yakisema kuwa Lulu Diva alishindwa kuolewa kwa sababu mwanaume huyo aligundua kuwa Lulu Diva anatoka kimapenzi na msanii mweznie ambae ni Rich Mavoko.

Akifahamika kwa jina moja la Joho, mwanaume huyo ndie inaesemekana kuwa alikuwa akimpa lulu diva kila kitu alichokuwa akionekana kuwa nacho kama nyumba, gari na ela za kila siku lakini mwanaume huyo aliamua kubadilisha mawazo na kumpokonya kila kitu baada ya kuoa kuwa Lulu Diva hataki kuendeleza na kuheshimu mahusiano yao.

Lulu Diva ambae alikuwa akionekana na vitu hivyo , alipewa na mwanaume huyo ambae alikuwa akiishi  na kinyumba kwa zaidi ya miaka mitatu lakini wameshindwana na ameamua kuchukua vitu vyako.

Hata hivyo Lulu mwenyewe amekuwa akijitapa kuwa vitu hivyo vya thamani amepewa na kigogo mmoja wapo Tanzania.Akiongea na GPL, moja ya watu wa karibu wa Joho aliongea na kutoa siri ya lulu diva kwa kumuona muongo na kujitangazia kitu kisichokuwepo.

hivi unajua huyo lulu ni muongo sana,mbona gari analosema amepewa na kigogo  alipewa na rafiki yangu  joho na walikuwa wakiihsi nyumba moja  ila sasa wameachana na ninavyojua ni kwamba ameshalichukua gari lake.Hiyo yote ni baada ya kumshutukia kuwa lulu diva anatembea na msanii mwenzie rich mavoko.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, GPL iliamua kumtafuta msanii huyo na kumuuliza kuhusu ukweli wa tetesi hizo ambapo Lulu Diva alikiri kununuliwa gari na joho lakini sio hilo alilonalo sasa hivi.

Yaani sitaki kukumbuka maana kipindi niko na joho alinitenda sana kiasi kwamba nilikuwa nikikesha nalia kila siku , alinifukuza kwenye nyumba nilikuwa ninakaa na hata  gari aliloninunulia alinipokonya ambapo kwa mtu yoyote lazima alifananishe kwa sababu ya rangi lakini ile ilikuwa BMW, na hii ni Jeep.

Lulu diva akiwa katika pozi na magari tofauti tofauti ya kifahari.

 

 

 

 

Baada ya Lulu Diva Kujitapa Kununua Jumba la Milioni 100, Inasemekana Kuna Mkono Wa Waziri Umehusika

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Mazoea’ ambaye siku chache zilizopita alijitapa kumiliki mjengo wenye thamani ya milioni 100 ambao alidai alinunua mwenyewe lakini kuna habari mpya zinazosema vinginevyo.

Siku chache zilizopita Lulu Diva aliuanika wazi mjengo wake mpya kwenye magazeti ya Global Publishers ambapo aliionyesha dunia nzima nyumba yake anayoishi kwa hivi sasa na pia gari lake la kifahari aina ya ‘Jeep’ analoendesha kwa hivi sasa.

Kwenye interview aliyoofanya na Millard Ayo Tv siku chache zilizopita Lulu Diva alifunguka haya kuhusu mjengo wake huo mpya:

Hivi vitu vyangu vyote nilivyonavyo nimenunua kwa kazi zangu za kimuziki lakini pia kuna kazi zangu nyingine nafanya kama biashara na kilimo na ile nyumba mliyoiona kwenye mitandao ya kijamii ikitrend ni yangu mwenyewe wala sijapangisha bali nimenunua ina vyumba viwili ipo maeneo ya Mbezi Beach nilinunua around milioni mia yaani haipungui milioni mia na kitu”.

Lakini sasa Global Tv online wanaripoti kuwa nyuma ya pazia kuna kigogo mmoja wa serikali ambaye jina kapuni ambaye amesimamia shoo nzima kuanzia kununua mjengo ule mpaka kuimalizia kuujenga lakini pia kigogo huyo pia amesimamia shoo ya gari analoendesha mrembo huyo kwa sasa.

 

Lulu Diva Ajiongezea Kalio La Kichina

Mwanamuziki wa Bongo fleva Mwanadada Lulu Diva amefungukia tetesi zinazomkabili hivi sasa kuwa anamiliki kalio feki au maarufu kama kalio la kichina.

Lulu Diva amekuwa akitrend katika siku za hivi karibuni hasa baada ya kutoa ngoma yake ya ‘Mazoea’ ambayo inafanya vizuri kwa hivi sasa Lakini pia Lulu Diva amekamata headlines baada ya muonekano wake kubadilika ghafla.

Mashabiki zake wengi wamegundua kwa uharaka kwamba kuna mabadiliko makibwa sana kwenye maumbile ya Lulu Diva hasa maeneo ya makalio ambapo kuna utofauti mkubwa na alivyokuwa huko siku za nyuma.Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Lulu Diva ameonyesha kuwashangaa watu wanaomsema kajiongeza kalio wakati mwili ni wake na yeye sio wa kwanza.

 

Shepu yangu inapatikana Kariakoo? Hivi jamani unaanzaje kupata shepu kama hii Kariakoo haiwezekani kwanza  sio rahisi kama mnavyofikiria jamani hapana! Sijawahi hata siku moja kwanza mwili wangu nimepewa na Mwenyezi Mungu nimepewa na Mungu alafu kama makalio yangu yamekuwa jamani hamjui kama kuna ukuaji alafu sasa hivi napata vitu adimu nakula vizuri nalala vizuri napata mashabiki kila siku watu wanasapoti kazi zangu kwa nini nisinenepe ? Alafu isistoshe mimi nimenenepa sahivi lakini hii shepu ipo siku zote lakini hata kama ningetaka kubadilisha kitu kwa raha zangu mbona Michael Jackson alijibadilisha akawa mweupe kama mzungu kwa raha zake na akafa kwa time ambayo Mungu alimpangia”.

Mbali ya muonekano wake kuwavutia watu wengi lakini pia Lulu Diva alivutia watu wengi kwa nyumba yake anayoishi aliyodai ina thamani ya shilingi milioni mia moja lakini pia anamiliki gari la thamani aina ya Jeep.

Lulu Diva Arudisha Pesa ya Mahali Kwa Mume.

Msanii wa kike wa muziki nchini Lulu Diva amerudisha pesa aliyotolewa ya mahali kutoka kwa mpenzi wake ambae alipanga kufunga nae ndoa.Lulu Diva amerudisha pesa hiyo kwa mwanaume huyo aliedumu nae kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa habari zilizokuwa chini ya kapeti zinasema kuwa Lulu Diva alitakiwa kufunga ndoa tangu mwaka jana mwishoni lakini mwanaume huyo aliona kuwa haitawezekana baada ya kusikia tetesi kuwa mwanadada huyo anatoka kimapenzi na msanii mwenzie Rich Mavoko.

kama kuolewa basi mwanadada huyo alitakiwa kuolewa mwaka jana mwishoni lakini mwanaume huyo alibaini kuwa anatoka kimapenzi na msanii mwenzie rich mavoko, kwaio akaomba kurudishiwa mahali yake.

Hata hivo Lulu Diva alipigiwa simu na kuulizwa kuhusu swala hilo na alijibu kuwa ni kweli kuwa alirudisha mahali ya mwanaume aliyetaka kumuoa lakini sio kweli kuwa aligundua kuwa ana mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwao kuwa yeye sio mwanamke wa kuoa.

Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu,nikamrudishia mahali yake maana alikuwa akiwasikilza sana ndugu zake  ambao walikuwa hawataki anioe.

Hivi  karibuni Lulu Diva na Rich Mavoko wamekuwa wakionekana kuwa karibu sana na hata kuhisiwa kuwa waili hao watakuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Picha ya hivi karibuni ya Rich Mavoko na Lulu Diva

Lulu Diva Kufunga Ndoa Ya Kimya Kimya

Msanii wa kike bongo anaefanya vizuri kwa sasa Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa ndoa yake ipo karibuni lakini atafanya kitu cha kushangaza watu kwa sababu hatotaka watu wajue kwaio atafanya kimya kimya na watu watashtukia tu ameshafunga ndoa.

Lulu Diva anasema kuwa watu wengi wamekuwa wkifunga ndoa huku wakifanya kelel sana katika mitandao ya kijamii , lakini ndoa yake yeye ambayo itakuwa hivi karibuni hataki watu wajue wengi na itakuwa ya siri kwa sababu anaogopa sana maneno na macho ya watu.Lulu Diva anasema kuwa anachoshukuru Mungu mpaka sasa mipango yake ya ndoa iko poa na inaendelea vizuri kabisa lakini itakuwa kimya kimya.

Yaani ndoa yangu sitaki vurugu mbalimbali kbisa, watu watakuja wasikie tu kuwa nimeshafunga ndoa na nimeolewa, ninachoshukuru Mungu mpaka sasa hivi ni kwamba kila kitu kinaenda sawa kabisa kuhusu maandalizi ya ndoa yenyewe,kuna baadhi ya watu nitawachagua kidogo ili kuhudhuria harusi yangu .

Wasanii wengi wa bongo wameamua kuacha kuishi maisha ya kuiba iba na kuamua kuharalisha mahusiano yao kwa kufunga ndoa, kaama ilivyo kwa lulu diva hii itakuwa imetokea pia kwa wasanii wengine kwa mwaka huu wameamua kufunga ndoa na wapenzi wao.

Lulu Diva Amefunguka Kuhusiana Bwana Anayemgombania na Gigy Money

Msanii kike wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa, Lulu diva ameongelea bifu au ugomvi unaosemekana upo baina yake na msanii mwenzake anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Papa’ Gigy Money huku ikidaiwa Kisa kikubwa cha bifu hilo kikiwa ni mwanaume.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva na Gigy Money hawapikiki chungu kimoja hata kwa sekunde moja na hata wakikutana sehemu hawawezi kuzungumza lakini pia inadaiwa Kisa na mkasa ya uhasama huo ni kuwa kuna mwanaume ambaye warembo hao wote wawili wanamtaka kwa wakati mmoja kitu kinacho sababisha mikwaruzano.

Tetesi hizi zilizidi hasa hapa Kati baada ya warembo hao kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii, kwenye mahojiano na East Africa Tv kupitua kipindi cha Enews, Lulu Diva alikana kata kata taarifa hizo na kudai kuwa hana ugomvi na Gigy Money:

Amchukue bwana angu ampeleke wapi labda? Kwanza mi nawashangaa sana mimi sinaga ugomvi na Gigy Money na wala sijawahi kugombania naye bwana labda saa nyingine maneno yanavyo ongelewa inakuwa ni showbiz tu lakini mimi na Gigy Money tunajuana wenyewe ananipenda na mimi ninampenda yaani in short tunapendana na pia tunasapotiana kwenye kazi zetu mimi naimba nyimbo zake na vice versa yaani tupo fresh kabisa halafu isitoshe mwanaume wangu hana time na wait walio kwenye media mimi mwenyewe nimejuana naye kabla sijawa staa yaani Nina uhakika ningekutana naye wakati nimekuwa maarufu asingenitamani”.

 

Lulu Diva akatwa Kutumbuiza Fiesta Grand Finale

Msanii lulu Diva amesonyesha kilio chake kwa kuililia serikali iwafikilie wasanii ambao wataondlewa katika Fiesta ya mwisho itakayo fanyika jijini Ea es Salam mwaka huuu ikiwa ni kullele cha tamasha ilo ambapo kwa tamko la serikali tamasha ilo litapaswa kuisha saa sita usiku.

Akiongea na vyombo vya habari, mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds Media  Bw.Ruge Mutahaba alisema kuwa kwa ratiba hiyo ni lazima wapunguze idadi ya wasanii  watakao perfom siku iyo ili kuweza ku-balance muda unaotakiwa. Lakini bado alitoa tumaini kuwa kuna uwezekana wa kupata kibali cha kupitisha mud na ikitokea kibali kikapatikana basi wataweza  kuweka wasanii wote waliopangwa.

Lulu Diva ni mmoja wa wasanii ambao walokuwa wakinufaika na tamsha hilo kwa sababu kwanza ndio mara yake ya kwanza  kufanya show katika tamsha ilo amabpo alipata bahati  ya kutumbuiza katika baadhi ya mikoa iliyopita hapo awali lakini kwa sasa amethibitisha kuwa kutokana na mabadiliko hayo ya ratiba yeye pia ni mmoja wa wasaniiwaliokatwa kutumbuiza katika show hiyo kubwa ambayo kwake ingekuwa ni ‘dream comes true’ kwa kuifanya kwa mara ya kwanza kwenye mkoa mkubwa wa jijini Dar Es Salam.

Lulu Diva ambae mwanzoni alikuwepo katika orodha hiyo,  lakini baada ya tamko ilo alipokea ujumbe kuwa ameondolewa katika orodha kutokana na tamko la mkuu wa mkoa.Hata hivyo Lulu Diva anaiomba serikali kuwafikilia kwa sababu  kulipwa kwake kunategema watu wengine wengi nyuma yake na ukizingatia kuwa kwake ilikuwa ni kama ndoto kufanya show katika jukwaa kubwa kama hilo.

mwaka huu ndio mwaka niliotimiza ndoto yangu kwa  kutumbuiza kwa mara ya kwanza katika jukwaa la fiesta, ujira wangu  ninaoupata pale ninagawana na watu wengi sana nyuma yangu  kuna dereva, kuna make-up artist, na wengine wengi sana ndio maana ninaiomba serikali itufikilie sana sisi wasanii. Alifunguka Lulu  Diva

Tamasha la fiesta linategemea kufanyika tarehe 25 novemba katika viwanja vya leaders club na baadhi ya wasanii ambao mpaka sasa wapo katika orodha ni pamoja na Alikiba, Vannesa mdee, Madee, Fid Q, Weusi, Nandy, Ben Pol.

 

Lulu Diva Awachana Walikuwa Wakimwita Gumegume

Mwanadada Lulu Abas maarufu kama Lulu Diva  anaefanya vizuri katika anga za muziki wa bongo fleva amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwashangaa sana baadhi ya watu waliokuwa wakimwita gumegume kipindi cha nyuma na kwamba ni muhuni hawezi kutulia na mpenzi mmoja kitu ambacho yeye anasema kuwa wala haijawahi kuwa tabia yake.

Lulu Diva amesema kuwa kipindi anaanza mahusiano na mpenzi wake aliyenae sasa hivi , huku akikataa kutaja jina la bwana huyo watu wengi wakimkuwa wakimwita gumegume hasa marafiki zake na kumwambia kuwa hawezi kudumu nae kwa muda mrefu kwa sababu yeye ni gumegume hajazoea kukaa na bwana mmoja muda mrefu.

Akiongea na ijumaa wikienda Lulu Diva anasema kuwa watu hao kwa sasa akiwaangalia na akinagalia mahusiano yake yalivyofika mbali tangu walipokuwa wanaanza kuongea  anawacheka tu kwa dharau

kuna watu walikuwa wakiniita mimi gumegume na kwamba eti siwezi kukaa na mpenzi mmoja na nikadumu nae,kama nilivodumu na huyu mpenzi wangu wa sasa hivi.Ninawangaliaga alafu nawacheka kwa dharau-Alifunguka mwandada huyo machachari katika kazi yake.

Ingawa ni kweli kwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakishndwa kukaa na mpenzi mmoja kwa muda mrefu na hii inawezekana ikawa ni moja ya sababu ya marafiki zake kuwa wakimwita gumegume, hapo awali Lulu Diva alikuwa akitoka kimapenzi na msanii mwenzie Ney wa mitego ambapo walikuja kuachana na kuwa watu wa karibu tu.

wasanii wengi wamekuwa wakishindwa kudumu katika mahusiano ya mapenzi ma wenzi wao na kuwa wakiruka ruka kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine huku mbaya zaidi wakiwa wanatembea wasanii wenyewe kwa wenyewe na hii ndio maana inakuwa kazi kuwa na mahusiano ya kudumu ndani ya bongo hasa kwa wasanii wa muziki.

Lulu Diva Awaeleza Mashabiki wake Siri ya Urembo Wake

Mwanamuziki mrembo wa Bongo fleva Lulu Diva ameamua kuwapa mashabiki zake siri ya weupe wake, Lulu alifika hatua hiyo baada ya watu wengi kuingiwa na kasumba kuwa wasaani wengi wa kike au hata wa kiume wana tabia ya kujichubua na kuwa weupe.

Katika mahojiano wengi aliyoyafanya na East Africa radio katika kipindi chao cha Planet Bongo Lulu amekiri kuwa siri kubwa ya urembo wake na weue wake unaofanya kuwa mrembo ni kula matunda na mboga mboga.

Lulu alisema;

“Msanii unatakiwa kuanza kujibrand kuanzia mwili wako, ngozi yako, vitu unavyokula, naweza sema kuwa nakula sana mboga mboga na matunda na kuna baadhi ya vyakula vinasaidia ngozi kung’ara”.

Luu Diva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaoitwa  ‘Give it to me’ ameamua kuweka wazi swala hilo kwani watu wengi wamekuwa wakiwashutuma wasanii kwa kutumia mikorogo ili wawe weupe kwa kuamini kuwa ndio wanakuwa warembo zaidi.

Lulu Diva aeleza kwanini mwanaume atakaye muoa atatoa idadi ya ngombe anazotaka yeye

Lulu Diva amesema kuwa yeye ndo ataambia mwanaume atakaye muoa idadi ya ngombe anazopaswa kutoa. Muimbaji huyo alisema hadhani kuwa kuna mwanaume yeyote ambaye anaweza kataa kutoa ngombe anazotaka yeye.

Mrembo huyo anadai kuwa uzuru wake ndo chanzo cha yeye kupewa kitu chochote anachotaka na wanaume. Akiongea kwa kipindi cha Uhondo cha E FM, Lulu Diva alieleza kuwa yeye ni mrembo kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi.

Lulu Diva

“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua. Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.

Lulu Diva aeleza ukweli kuhusu madai kuwa anashiriki mapenzi na Jaguar

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anadaiwa kushiriki mapenzi na msanii Jaguar kutoke nchi jirani ya Kenya.

Jaguar ni meneja wa mrembo huyo kutoka Tanzania lakini kuna wale wanaodai kuwa wasanii hao wawili wanashiriki mapenzi chini ya maji.

Jaguar

Lulu Diva hata hivyo aliambia Star Mix kuwa wambeya wametunga tu hadhiti kuwa yeye na Jaguar ni wapenzi ilhali wao wanahusiana tu kikazi.

“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo,” Lulu Diva aliambia Star Mix.

Lulu Diva

 

Hawa ndio wasanii wa Bongo ambao Lulu Diva anawakubali

Lulu Diva ambaye anajulikana kupitia mziki wake hivi karibuni aliwataja warembo wawili kutoka Tanzania ambao yeye anazitambua kazi zao.

Akizungumza kwenye interview, Lulu Diva alisema kuwa Vanessa Mdee na Lady Jaydee ni wasanii ambao wameweka bidii kwenye kazi zao. Aliendelea kuwasifu kuwa wawili hao wameipa Tanzania sifa kutokana na kazi zao za kuridhisha.

Lulu Diva pia alimtaja Beyoncé na Celine Dion Kama wanawake ambao anafurahia kazi zao za kimziki. Akiongea katika interview Lulu alisema,

“Kimataifa namuangalia sana Beyonce na Celine Dion. Nikimuangali Beyonce naangalia hadi life style yake anayoishi, nikimuangalia Celine namuangalia hata the way anavyoimba, anavyoweza ku-control sauti yake. Beyonce kuanzia swagger anavyoimba, anavyocheza jukwaani, anavyocheza mwenyewe kwenye video zake, mavazi hata life style yake akiimba nakubali sana.”

“Kwa sasa kunilinganisha na akina Amber Lulu na Gigy Money ni dharau kubwa, si levo zangu, tazama muziki wanaofanya na muziki wangu” Lulu Diva

Lulu Diva amepanda cheo na sasa hataki kuwa analinganishwa na video vixen wengine kama Amber Lulu and Gigy Money.

Mwanadada huyo aliyekuwa video vixen hapo awali sasa hataki kamwe kuekwa kwenye levo moja na watu wengi kwa sababu anafanya mambo makubwa.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Lulu alisema ni kweli wapinzani wake wote hao wanafanya muziki kwa sasa kama anavyofanya yeye lakini bado levo zao si kama zake maana yeye yupo chini ya uongozi unaosimamia kazi zake za kimuziki na umemuwezesha kupata kolabo nje ya nchi na Mzimbabwe Jah PPrayzah.

“Kwa sasa kunilinganisha na akina Amber Lulu na Gigy Money ni dharau kubwa, si levo zangu, tazama muziki wanaofanya na muziki wangu”  alimalizia.