Lulu Diva Aelezea maisha ya u-video Queen ni Mateso.

mwanadada Lulu Diva mabe kwa sasa anafanya vizuri sana katika maswala ya muziki hasa kwa wimbo wake mpya mabao amemshirkisha rich mavoko na kusema kuwa kwa sasa wimbo huo umemfikisha mbali sana kiasi kwamba anayaona mafanikio yake kama mmoja wa wasanii wa kike bora katika muziki Tanzania anasema kuwa hapendi kabisa kuyazungumzia maswala yake ya nyumba wa sasa.

Lulu diva ambae hapo awali aliwahi kuwa video queen kabla ya kuwa msanii wa muziki anasema kuwa hapendi kukumbuka maisha hayo ya kuwa video queen na kama mwandishi anataka kugombana nae basi amuulize kuhusu maswala hayo.

kwa kweli sitaki kusikia kabisa maswala ya u-video queen,ni kweli kuwa hayo ni mapito yangu na huko ndipo nilipotoka lakini sasa hivi nimeendelea na akili yangu yote ipo katika muziki ninaoufanya na uigizaji ndio ninaoufikiria zaidi.mtu unachukuliwa na kupamba wimbo wa mtu kwa malipo kidogo sana  na bado hicho kidogo unachokiangaika unakipta kwa manyanyaso.

Lulu Diva Adai Akikumbuka Alivyokuwa Video Queen Anatamani Kulia

Msanii wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa piga ya garagaza hawezi kuwa video queen tena  kwenye video za wasanii wengine.

Lulu Diva ni moja kati ya wasanii ambao kusema ukweli wametoka mbali kwani alianza kama muuza mgahawa baadae akaingia kwenye ulimwengu wa sanaa kama video vixen kwenye video za wasanii mbali mbali na mpaka sasa anafanya vizuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Vibes, Lulu Diva amesema  kwamba akikumbuka baadhi ya mambo kwenye u-video queen, muda mwingine hutamani hata kulia.

Kiukweli sitaki kusikia kabisa kuhusu mambo ya u-video queen, ni kweli ni mapito yangu na ndiyo huko nilikotoka, lakini kwa sasa ninaendelea na kuweka akili yangu yote kwenye muziki ninaoufanya na uigizaji huko ndiko ninafikiria zaidi.

Mtu unachukuliwa na kupewa kazi ya kupamba wimbo wa mtu kwa malipo kidogo, bado hicho kidogo chenyewe unakihangaikia na manyanyaso kibao”.

Wasanii wengi ambao waliwahi kuwa video queens kama vile Gigy Money na Amber Lulu wameponda sana kazi hiyo kusema haina pesa kabisa yaani wanaishia kupewa pesa ya nauli.

Lulu Diva- Kolabo na Rich Mavoko Imebadilisha Maisha Yangu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa wimbo wa Ona umempa mafanikio makubwa.

Lulu Diva aliachia Kolabo hiyo miezi miwili iliyopita aliyomshirikisha msanii anayesemekana kuwa mpenzi wake Rich Mavoko na amepata mafanikio makubwa baada ya utumbo hiyo kufanya vyema.

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alieleza kwamba nyimbo zake za nyuma zilikuwa ni nzuri na zilifanya vizuri lakini baada ya Wimbo wa Ona, umemfanya atambulike kwenye gemu la Bongo Fleva kama msanii mkubwa na kumpatia shoo za kila mara.

Wimbo wa Ona umenipeleka kwenye levo nyingine kabisa kiukweli. Kwa sasa na mimi ni miongoni mwa wasanii wakubwa, shoo zimeongezeka na hata hadhi pia”.

Kutokana na kufanya vizuri na  wimbo huo Lulu Diva ameonekana kwenye shoo mbali mbali akitumbuiza kama vile In Love and Money Tour ya Vanessa Mdee na Jux hivi karibuni.

Lulu Diva Azungumzia ONA ilivyobadili Maisha Yake ya Muziki

Mwanadada Lulu Diva amefunguka na kuelezea mafanikio yake ya muziki tangu alipoanza mpaka alipofikia sasa na kusema kuwa kwa sasa na yeye amekuwa akijiona kuwa ni msanii mkubwa sana kutokana na wimbo wake huu mpya wa sasa hivi.

Lulu diva anasema kuwa wimbo wa ona ambao amemshirikisha Rich Mavoko ambao kwa sasa umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na tv umekuwa moja ya mafanikio yake makubwa na anaona kabisa kuwa kwa sasa amepiga hatua kubwa kutokana na hilo.

Wimbo wa ona umenipeleka kwenye levo nyingine kabisa, kwa sasa mimi ni miongoni mwa wasanii wakubwa ambao kila siku shoo zinazidi kuongezeka tu  na hata hadi yangu pia.

 

 

Lulu Diva Akiri Kulaumiwa Sana Kwa Kuiba Madanga Ya Watu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Ona’ amekiri kuwa wanawake wengi wamekuwa wakimlaumu kwa kuiba wanaume wao (madanga).

Lulu  Diva amekiri kwamba ameshakutana na tuhuma nyingi kutoka kwa wanawake kadhaa ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa kuwachukulia wanaume zao.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha ‘Now you Know’ Lulu Diva amefungukia tuhuma hizo na kusema haya:

Nimeshakutana na hizo kesi sana unakutana na mtu anasema “Unatembea na bwana angu umemchukua” sasa mimi najiuliza mwanaume anachukuliwaje? Anachukuliwa au anakuja mwenyewe”.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva Anatembea na mwanaume mwenye pesa Chafu na hata ilisemekana kuwa mwanaume huyo ni Kigogo wa serikalini tetesi ambazo mwenyewe amezikataa mara kwa mara.

 

 

Lulu Diva Adaiwa Kufaidi Penzi La Bill Nas

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Bill Nas.

Global Publishers wanaripoti kuwa wasanii hao wawili wamekuwa na ukaribu wa ajabu na wameonekana wakionyeshana Mahaba hadharani bila kujali macho ya watu.

Gazeti hilo linaripoti kuwa lilimpata mtu ambaye alitoa taarifa hiyo ambapo alifunguka:

Walianza kama masihara, tukajua labda Rich Mavoko ndiyo anakaa kwa Lulu kumbe ni Bill Nas bwana, juzi walikuwa tena pamoja wakielekea mkoani sijui mkoa gani lakini picha zao za kujibebisha zinamaanisha“.

Baada ya Tetesi hizo na kusindikizwa na picha kadhaa Kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha ukaribu Global Publishers lilimsaka Lulu Diva ambaye alimwaga povu hili:

Hivi jamani mtu kuongozana na mwanaume ndiyo kutembea naye? Mbona mnataka kuniharibia kwa mtu wangu niliyekuwa naye?“Bill Nas ni mshikaji   wangu wa kawaida tu, juzi (Jumamosi iliyopita) tuliandaliwa shoo ya pamoja huko Iringa, tukiwa njiani tulikuwa tukipiga mapicha picha kama mtu na rafiki yake, nashangaa watu wanageu-zageuza maneno”.

 

Lulu Diva Awatupia Dongo Zito Mavideo Queen

Mwanamuziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anayefanya vizuri na kibao chake cha Ona, ameibua bifu zito na wauza nyago Kwenye video za wasanii (Video queen au video vixens).

Lulu Diva amewatupia Dongo Zito wale mavideo Queen wote ambao wanaacha kazi zao na kuamua kuongi Kwenye muziki wa Bongo fleva ambapo amedai sasa wameshapotea.

Lulu Diva alifunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers amesema kwamba, anaona kila dalili za wanadada ambao walikimbilia kwenye muziki wakitokea kwenye u-video queen wakipotea wote kwenye gemu jambo linalomfanya kujihisi kubaki bila mpinzani.

Wote wamepotea, siwezi kuwataja kwa majina nisije kuzua ya kuzua lakini sasa hivi hakuna video queen anayethubutu kubaki kwenye gemu zaidi yangu“.

Imekuwa kawaida kwa wasichana ambao wanafanya kazi kama mavideo Queen kujiingiza Kwenye Muziki ambapo wenyewe wamekuwa wakikiri kuwa mara ya kwanza walikuwa hawapati maslahi yoyote mfano wa mavideo Queen wanaofanya vizuri Kwenye Bongo fleva ni Gigy Money, Amber Lulu na wengineo kama Haitham.

Siwezi Kupata Mtoto Sasa Hivi Labda Miaka 5au 6 Inayokuja:Lulu Diva

Mwanadada Lulu Diva amefunguka na kusem kuwa hatokaa kubadilisha msimamao wake wa kupata mtoto sasa hivi kwa sababu hana  mpango wa kupata mtoto kwa sasa kama ambavyo alishasema tangu hapo awali,

kuna kipindi cha hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa lulu diva alishapata mtoto huku awali lakini mtoto huyo amemuacha kwa mama yake na kwamba hataki watu wajue kama anamtoto, kitu ambacho lulu diva mwenyewe alikanusha na kusema kuwa amekuwa akiakaa na watoto wa ndugu zake wengi kwaio hana mtoto wala hategemei kupata mtoto kwa sasa.

kama mtoto nilishasemaga kuwa siwezi kupata mtoto sasa hivi labda miaka 5 au 6 inayokuja not now , maana sio kitu cha kukimbilia.

Akiongea na waandishi wa habari alipkuwa katika ufunguzi wa car wash ya perfect chrispin, Lulu Diva anasema kuwa kwa sasa amejikita kuwekeza zaidi katika kilimo kwa sababu kuna mashambe mengi ya mama yake ambayo ameachiwa na marehemu baba yake kwaio akiwa kama mtoto mkubwa kwenye familia yao ameona ni bora kuyafanyia kazi mashamba hayo.

Lulu Diva- Sina Mpango Wa Kuzaa Kwa Sasa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Huba’ Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto kwa hivi sasa labda baada ya miaka mitano.

Kama utakumbuka siku mwezi uliopita wakati Lulu Diva anasheherekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) CEO wa WCB Diamond Platnumz alianika wazi uhusiano wake na Rich Mavoko na kumtaka Lulu Diva Azae naye mtoto.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi za Lulu Diva kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko ingawa wawili hao wamekuwa wakikataa na hata kuficha lakini wamebambwa pamoja mara kadhaa.

Kwenye mahojiano ambayo Lulu Diva alifanya na Sam Misago Tv, ameweka wazi licha ya kuwa Diamond alimtaka azae mtoto hivi karibuni na yeye akakubali hjamaanisha atazaa siku za hivi karibuni kwani hana mpango wa kuzaa mpaka miaka mitano ipite.

Mbona mimi kila siku ninasemaga siwezi kupata mtoto sahivi labda miaka mitano sita huko na kuendelea sio sasa hivi kabisaaa”.

Lakini pia Lulu Diva aliendelea kukataa kuongelea Mahusiano Yake na Rich mavoko huku akidai hayo ni maisha yake binafsi na asingependa kuyaani

Lulu Diva Adaiwa Kutupiwa Jini Baada Ya Kuiba Mume Wa Mtu

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Homa’ Lulu Diva amedaiwa kutupiwa jini/ shetani baada ya kuiba mume wa mtu.

Habari hii inaripotiwa na Global Publishers ambapo inadaiwa kuwa ubuyu huo ulitolewa na mtu wa karibu wa Lulu Diva ambapo amedai kuwa alitupiwa jini hilo na mke wa mtu baada ya kumuiba mumewe miaka kadhaa iliyopita.

Chanzo hiko cha habari kimedai kuwa tangu ametupiwa jini hill amekuwa akipata mikosi mitupu na wanaume hiyo ikidhihirishwa na mahari yake aliyotolewa kurudishwa kwa mwanaume.

Baada ya tetesi hizo Ijumaa Wikienda ilimsakaa Lulu Diva na alifunguka mazito haya:

Kwanza naomba niseme huyo aliyewaambia nishamjua maana mimi mwenyewe nilimwambia alafu isitoshe mimi nilitoa siri hiyo kwa sababu kila mipango yangu ya ndoa ikikamilika kunatokea jambo na mwanaume anasema ana mambo yake mengine. Hapo kama sio kupigwa juju ni nini? Hilo la kwamba aliyenipiga juju ni mume wa mtu ni siri yangu”.

Lulu Diva Kutoa Album Itakayomshirikisha Cardi-B

Mwanadada sext lady amefunguka na kukiri kuwa kwa sasa nyimbo na muziki unazidi kuendelea hivyo wanaitaji kwenda na mfumo mpya ambao wasaniiwengine wameshaanza kuufuta wa kutoa nyimbo zao kwa mfumo wa album na hata yeye yuko njiani kufanya hivyo.

Lulu Diva anasema kuwa baada ya kuamua kufanya hivyo, msanii wa kwanza wa nje ambae anataka kufanya nae kazi atakuwa ni Cardi-B ambae anatarajia kumuweka album yake ya kwanza.

Lulu Diva anasema kuwa kufanya kazi kwa mfumo wa labum kuna leta hshima kwa msanii lakini pia kunaweka  historia ya muziki wa msanii, hivyo basi anaamua kumuweka mwanadada huyo kwa sababu anaamini kuwa atamsaidia kutangaza muziki.

Najianda kufanya album kama ambavyo wasanii wakubwa wanavyokuwa wanafanya,na hivi karibuni tu nitafanya kama wasanii wengine wakubwa duniani wanavyofanya, album yangu itasheheni wasanii wengi na wakubwa ndani na nje ya nchi  na nina mpnago wa kumshirikisha Cardi -B , nitafurahi sana kama kazi zangu zitakuwa ni za kimataifa.

 

Lulu Diva- Sitaki Kupambanishwa na Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya muziki wa mduara Lulu Diva ‘Diva Divana’ ameibuka na kusema hataki kufananishwa na msanii mwenzake Shilole.

Lulu Diva amewataka mashabiki ambao wanafananisha rekodi zake na na miondoko ya nyimbo za Shilole waache kumpambanisha naye kwani hataki beef naye.

Lulu Diva amefunguka hayo Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, ambapo amedai anamheshimu Shilole kama dada yake hivyo hatopenda kuwa na beef naye:

Hapana Jamani hakuna mtu ambaye anapotezwa kila mmoja anaimba mziki wake na mimi Shilole namheshimu kama dada na anafanya mziki wake wa kwake peke yake yaani hata ukiangalia mziki anaofanya na mziki wangu ni vitu viwili tofauti ni watu tu wanatengeneza vitu ili waweze kutuchonganisha”.

Lulu Diva aliendelea kumwagia Sifa Shilole huku akisisitiza hataki bifu naye:

No mimi namheshimu sana as a sister she is a legend ameanza mziki kabla yangu anajua vitu vingi kwenye gemu kabla yangu kwaiyo wasitengeneze hiyo kitu mpaka mimi nikawa kuna kitu nataka kujua kuhusu mziki nikashindwa kumfuata kwa sababu ya maneno kwaiyo naomba hivyo vitu visiwepo mimi nafanya mziki wangu mimi kama mimi”.

 

Hamisa Mobetto na Lulu Diva Kupamba Steji Moja Nchini Uingereza

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Amezoea’ Lulu Diva atapanda steji moja Hamisa Mobetto katika uzinduzi wa Lipstick zake nchini Uingereza.

Mzazi mwenza wa staa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamusa Mobetto anatarajia kuzindua rasmi lipstick zake zinazojulikana Kama “Charmed Cosmetic”.

Kwenye uzinduzi huo utakaofanyika tarehe 5 Mei 2018, utasindikizwa na burudani toka kwa Lulu Diva ambaye ametoa wimbo wake mpya hivi karibuni unaoenda kwa jina la Huba.

Hamisa alitangaza habari hiyo njema kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliandika:

 

United Kingdom get ready. Business marketing my charmed cosmetics lipstick launch coming soon. Live performance by the sexy Lulu Diva. We come for serious business”.

 

Lulu Diva Akanusha Kuishi Kwa Kudanga.

Msanii wa kike wa miondoko ya mduara Lulu Diva hivi karibuni amekuwa akikumbwa na tetesi nyingi  za kutupa mtoto mara za kuishi mjini kwa kutegemea wanaume na vitu vingine vingi.hata hivyo msanii huyo amefunguka na kusema kuwa sio kweli kuwa amekuwa akiishi kwa kudanga kwa sababu maisha mazuri kwake yamekuwepo kwa muda mrefu.

Kwanza kabisa mimi maisha ninayoishi ni mmazuri kabla hata sijawa  hata mwanamuziki, nilikuwa hivi hivi tangu zamani.mimi ni msichana niliyehangaika sana kutafuta maisha , nilishawahi kuwa waiter, nikafanya baaadhi ya biasghara.nimeshahangaikia sana pesa yangu na wala sijawahi kudanga, tangu zamani nilikuwa nahangaikia sana maisha yangu tangu zamani.

Lulu Diva pia amekanusha stori kuwa amechukuliwa na pedeshee  ambalo limemuweka mjini na kumpa kila kitu

Lulu Diva – Siishi Mjini Kwa Kudanga Maisha Yangu Mazuri Tangu Zamani

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyegeukia miondoko ya mduara Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi haishi mjini kwa kudanga kama watu wengi wanavyomzushia bali anapiga kazi na mpenzi wake ni mwanaume wa kawaida.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na maneno mengi sana ambayo yamesemwa kuhusiana Lulu Diva ambapo inasemekana kuwa malo zote alizokuwa nazo ambazo ni gari aina ya Prado na nyumba ya kifahari anayoishi Mbezi Beach vyote amepangishiwa na lake.

Kwenye Interview aliyofanya na Times Fm  Lulu Diva amekataa habari hizo na kudai kuwa maisha yake ni mazuri kabla hata hajawa Mwanamuziki:

Kwanza kabisa mimi maisha yangu ninayoishi na jinsi ambavyo nipo ni toka sijawa mwanamuziki nilikuwa na maisha haya sema mimi ni msichana ambaye nimehangaika sana nimeshafanya kazi hotelini nikawa waiter na biashara zote nimefanya kwaiyo nimehangika sana pesa yangu kwaiyo sijawahi kudanga hata siku moja Maisha Yangu mazuri ninayoishi nimeyafanyia kazi wala sijawahi kudanga”

Lulu Diva pia ameikana stori ya kwamba anachukuliwa kimapenzi na pedeshee ambalo linamuweka mjini na ndio linalompa kila kitu bali amedai mwanaume ambaye ni mpenzi wake ana maisha ya kawaida sana hana utajiri wa kiivyo.

 

Natamani Kupata Mtoto Lakini Sina Mpango Kwa Sasa.-Lulu Diva

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Lulu Diva amefunguka na kuzungumzia tetezi zinazoendelea kusamba juu yake kuhusu swala la kutelekeza mtoto wake kijijini na kwamba kutokana na umbali wake  na mtoto imefikia hatua mtoto huyo amekuwa akimwita dada badala ya mama.

Lulu anasema kuwa watu hawajui kuwa hata yeye anatamani mtoto kwa sababu ni baraka kutoka kwa mungu  na   kwamaisha ya sasa hivi kuwa na mtoto ni kuwa na dili kubwa sana kwa sababu anaweza kuwa ambasador wa kampuni flani hivyo ikakusaidia katika malezi pia.

Nimeona hizo taarifa sana katika mitandao lakini sio kweli kuwa mimi nimetelekeza mtoto,kwangu pia ni suprise kwa sababu kutoka kwa mwenyezi mungu mtoto ni zawadi na kwa maisha ya sasa hivi kutupa au kukana mtoto ni ushamba kwa sababu anaweza kuwa balozi wa mabenki , au kampuni flani.

Hata hivyo Lulu Diva anasea kuwa amekuwa akitamani kupata mtoto lakini hana izo plani kwa sasa kwa sababu muda wa kuzaa kwake bado.

Mimi mwenyewe natamani mtoto lakini sina mpango kwa sasa hivi  naona muda bado ila sina mtoto anaeniita dada.nina watoto wa mama zangu wadogo ambae nilimlea na sasa hivi yuko zanzibar, pia kuna mtoto wa dada yangu na wengine wengi ambao wamekuwa wakija kwangu na mimi nina kaa nao na kutoka nao.

Lulu anasema kuwa watu wamekuwa wakisema kuwa  anamficha mtoto mara hamjali mtoto wake lakini hiyo sio kweli lakini anategemea kupata mtoto baada ya miaka mitano.

Kwa sasa sina plani za kupata mtoto kwa sababu niko kwenye plani za kutafuta baba,labda baada ya miaka mitano.na hata mwennzangu nikimuuliza namuona hana muda kwa sasa.

Lulu Diva alipoulizwa kwanini anasubiri muda mrefu hivyo mpaka muda wa kupata mtoto na yeye alijibu.

Tunahitaji kuwawekea na kuwatengeneza mazingira mazuri watoto wetu,sio tunazaa tu kwa sababu tuna uwezo wa kuzaa.