Zari Afunguka Kuguswa na Kifo Cha Mtoto wa Muna

Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amefunguka na kuweka wazi uchungu alioupata baada ya Muna kufika na mtoto wake usiku wa jana.

Mtoto wa Muna na Casto Dickson Patrick,  alifariki dunia siku ya jana Nairobi nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Zari ambaye na yeye ni mama wa watoto watano amefunguka na kuonyesha kuimizwa na Kifo Cha mtoto huyo na kuandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:

 

 

 

TANZIA- Mtoto wa Muna na Casto Dickson Afariki Dunia

Mtoto wa msanii na Mfanyabiashara Rose Alphonce Nungu maarufu kama Muna Love na Mtangazaji wa Clouds Tv Casto Dickson aliyekuwa anaitwa Patrick amefariki dunia siku ya jana.

Patrick ambaye alikuwa anaumwa miguu kwa muda  Alizidiwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kupelekwa nchini Kenya, Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kukaa hospitali kwa siku kadhaa usiku wa jana Zamaradi alitangaza kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa mtoto Patrick aliyekuwa ana miaka saba amefariki dunia.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kufika nchini siku ya Alhamisi kwa ajili ya maziko.

Mwenyezi Mungu ailaze mahakama pema peponi Amina.

Wasanii Waungana Kumsaidia Mtoto wa Muna

Mtoto wa msanii na muandaaji wa matamasha Muna love anejulikana kama Patric ambae mara ya kwanza alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya miguu na kumfanya mama ake kupitia katika majaribu yaliyomfanya muna kokoka na kumrudia Mungu ameanza kuumwa tena na kuonekana kuwa bado anahitraji uangalizi mkubwa wa  madaktari.

Mtoto huyo amabe anaonekana kugusa mioyo ya watu wengi katika tasnia ya sanaa , alianza kuwekwa katika mitandao ya kijamii siku ya jana huku watu wengi wakiandika maneno  ya masikitiko na yenye kutia faraja familia ya muna na ndugu zake kwa ujumla.

Hata hivyo wasanii wengi wameonekena kuguswa na tatizo hilo na kuamua kufanya harambee katika kitandao ya kijamii kupitia kurasa zao kwa ajili ya kuwaomba wadau na mshabiki kuchangia ili mtoto huyo aweze kusaidika katika matibabu yake.

Wema Havai Nguo za Ndani- Muna Love

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Muna Love amefungukia tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama kwa muda mrefu kuhusiana na urafiki wake na Wema Sepetu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi mbali mbali kuhusu sababu za kuvunjika urafiki wa Wema Sepetu na Muna.

Kama utakumbuka miaka ya nyuma Wema alikuwa na urafiki hasa na Muna walikuwa wanaonekana pamoja kila sehemu Lakini urafiki huo ulivunjika ghafla na kila mmoja alishika njia yake na kuendelea na maisha yake.

Lakini baada ya kugombana ilisemekana kuwa Wema aligundua kuwa Muna ni mshirikina na alikuwa anamuendea kwa waganga na kibaya zaidi ilisemekana kuwa Muna alikuwa anaiba nguo za ndani Wema (chupi).

Tuhuma hizo za kuiba nguo za ndani za Wema zilisambaa sana lakini juzi Kwenye mahojiano aliyofanya na Shilawadu ya Clouds Tv, Muna alikana tuhuma hizo na kudai hawezi kuiba nguo za ndani za Wema maana mtu mwenyewe havai nguo hizo.

Ngoja niongee ukweli kwa sababu nimeokoka nguo za ndani hizo ambazo wanasema alikuwa havai inakuaje nachukua nguo za ndani ya mtu ambaye alikuwa havai”.

Kwenye mahojiano hayo Muna alikiri kuwa hana tatizo na Tunda na hakutaka kabisa kuongea sana kuhusu mzazi mwenzake Casto Dickson.

Muna Kufuta Tatoo Kwa Zaidi ya Milioni Tano.

Mwanadada mjasilimali na muigizaji Rose Alphonce amefunguka na kudai kuwa atatumia zaidi ya milioni tano kufuta tatoo zilizopo mwilini mwake , Muna ambae alisema kuwa kwa sasa ameokoka hivyo tatoo hizo zimekuwa zikimnyima amani sana anatamani kuzifuta tatoo hizo na anaona kabisa kuwa ni lazima azifute.

Muna anasema kuwa mpaka sasa hivi ana michoro kama mitano mwilini mwake huku tatoo iliyopo shingoni ndio kubwa kuliko zote lakini alishafanya mpango wa kuuliza sehemu ambayo angeweza kufuta tatoo hizo na kuambiwa kuwa inawezekana kufutwa kwa milioni tano.

Tayari nimeshaulizia kwa wataalamu huko thailand,ambao watanifuta bila kupata madhara yoyote na wameniambia kuwa hizo zingine ndogondogo  zitakuwa ni chini ya milion 2.1.

 

Baada ya Uokovu,Tatoo Zinamtesa Munalove .

Msanii wa maigizo nchi, Muna Love amekiri kuwa tatoo alizochora mwilini mwake kipindi hajaokoka zimeanza kumtesa kwa sababu hata mtoto wake wa kiume amekuwa akimpigia kelele kila siku kuhusu kuziondoa tatoo hizo.

Muna ambae mara ya kwanza alikuwa katika mambo ya kidunia na baadae alipata matatizo makubwa yeye na mwanae yaliyoyafanya kuokoka na kumrudia mungu, anasema kuwa  anatamani kuzifuta tatoo hizo na kuondoa kabisa.

Mtoto wa kiume wa Muna ambae pia ameokoka amekuwa akimsumbua mama yake huyo kuzifuta tatoo hizo  kwani zinaenda kinyume na maadili ya uokovu.

                                           

                                                 Muna akiwa na mtoto wake.

 

Muna Awajibu Wanaomsema Kuhusu Ulokole na Tatoo Zake

Msanii wa bongo movies ambae pia ni mjasiliamali Rose Alphonce maarufu kama Muna amefunguka na kuwashangaa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimsemak kuwa anajifanya ameokoka wkati aamejaa tatoo katika mwili wake tena zinaonekana.

Mwanadada huyo ameonyeshwa kuwashangazwa na watu wanaomsema hivyo na kuwajibu kuwa kwa upande wake tatoo hizo haoni kama zinamsumbua chochote na swala la yeye kuokoka kwa sababu aliyyafanya hayo akiwa dhambini na sasa ameokoka kwaio anachoamini Mungu hatohesabu hayo makosa yake ilhali aliyafanya kipindi ambacho alikuwa hajatubu.

Muna anasema kuwa katika imani wanaamini kuwa mtu anapoamua kuokoka mungu aangalii makosa ya nyuma bali imani yake ya kuamua kuokaka na kurekebisha yake yaliyopita na kuwa mpya kwaio tatoo haziingiliani na swala la kuokoka.

Sidhani kama Mungu anaangalia tatoo zangu,ninachojua hatoangalia dhambi zangu bali atanipokea  na kufuta kila kitu changu ambacho kimekifanya  nyuma.kwasabau kama tatoo nishachora nyingi na hakuna njia ya kuzikwepa kabisa na kwasababu  nimetubu naamini kuwa Mungu atanisaidia.

Muna ambae kwa sasa anaonekana kujiweka karibu zaidi na Mungu na kusema kuwa ameokoka , ameonekana kuwa katima maombi muda mwingi na hata posti zake zimekuw zikithibitisha hivyo.

 

Muna Ahaidi Kufunga Mpaka Hukumu Ya Lulu Itakapokwisha

Muna , akiwa ni kama ndugu kwa Lulu Michael alijitolea kwa hiari yake kuwa dada wa hiari wa Lulu tangu kipindi wanaigiza wote kipindi wapo kaole sanaa group,  Muna amekuwa karibu na familia ya Lulu kwa kipidi chote cha raha na shida na sana sana   katika kipindi hiki cha miwsho cha kesi ya Lulu mpaka anapata hukumu yake. Pamoja na kwamba Muna  alikiri kuwa alikuwa na mgonjwa hospitali lakini bado Muna aliweza kuhudhuria katika kesi hiyo  kila siku ili kumfariji mdogo wake huyo.

Akiongea na waandishi wa habari, Muna alielezea jinsi ambavyo ameipokea hukumu ya mdogo wake Lulu kwa masikitiko ukizingatia ndie ndugu na rafiki wa karibu aliekuwa nae kwa kipindi kirefu na tangu wajuane hawajawahi kugombana,lakini pia Muna bado anajipa moyo na kusema kuwa hukumu ya miaka miwili kwa Lulu ni moja ya jaribu tu ambalo Mungu ameamua kumpitisha Lulu huku akimundalia mema zaidi mbele ya safari yake.

Unajua mimi namuamini sana mungu na ninaamini ilo  ni moja ya jaribu tu  ambalo Mungu ameamua kumpa Lulu lakini ipo siku litapita tu na lulu atarudi katika maisha yake ya zamani.-Aliongea Muna kwa kujipa matumaini makubwa

Lulu na Muna katika picha za pamoja

Hata hivyo kwa masikitiko makubwa kabisa Muna anasema kuwa atakumbuka sana kipindi amvacho alikuwa na Lulu,na kufanya mambo mengi kwa pamoja kwa shida na raha lakini leo anafanya peke yake, mbali na hayo muna amehaidi kufunga kwa sala kwa siku zote ambazo Lulu atakuwa hukumni ili kumuombea.

Nitakumbuka nyakati zote nilizokuwa na yeye kipindi yupo uraiani,lakini kuanzia siku aliyopewa hukumu kazi yangu ni moja tu  kufunga na kuomba kwa ajili yake.-Alimalizia Muna

Wapo wengi walionekana kuguswa na hukumu ya Lulu lakini pia Muna akiwa kama mwanafamilia na rafiki wa karibu wa Lulu Michael anaamini kuwa ndugu yake huyo anahitaji maombi ya muda mrefu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazomkabili kipindi atakapokuwa gerezani ukizingatia wengi waliotoka huku wamekuwa wakielezea ugumu wa maisha ya kutokuwa huru.

 

Muna Azungumzia Ugumu Anaoupata Kwa Kesi Ya Lulu

Mwanadada mrembo anaejihusisha na uigizaji na  mjasiriamali   Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kuongelea ugumu na kipindi kigumu anachopitia kwa kipindi hiki tangu kesi ya mdogo wake wa hiari Elizabeth Lulu Michael  imeanza.Muna Love amesema kuwa kwa kipindi hiki amekuwa na kazi kubwa  ya kuuguza mtoto wake ambae amelazwa muhimbili  kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa na pia amekuwa akitakiwa kuoekana mahakamani ili kumsaidia na kumfariji mdogo wake Lulu Michael katika kesi ya mauaji inayomkabiri iliyokuwa ikisikilizwa mahakamani.

Akizungumza na Star Mix ya Global  , Muna ambae tangu kesi ya msanii mwenzie na mdogo wake huyo ianze amekuwa akonekana mahakamani bila kukosa anasema kuwa kwa takribani miezi miwili sasa amekuwa akimuuguza mwanae pale muhimbili lakini pia ana ndugu yake ambae pia anahitaji uwepo wake , hivyo inabidi aweze kufanya kotekote ingawa inakuwa inampa ugumu kidogo.

“Yaani najiona kabisa kama huu mwaka ni wangu,maana pale Muhimbili wameshanizoea kabisaa.Nimekaa muda mrefu nikimuuguza mwanangu mguu lakini ukiachana na mgojwa huyo pia  naangaika na upande wa pili kwa mdogo wangu Lulu mpaka nachanganyikiwa” alisema Muna Love

Kesi ya Lulu ambayo ilianza kusikilizwa mahakamani tangu Oktoba 19 inayohusu mauaji ya msanii mwenzie mkongwe ambae pia alikuwa ni mpenzi wake Steven Kanumba , iliendelea kwa muda wa takribani wiki mbili ambapo mashauri ya mwisho na hukumu yanatarajiwa kutolewa Novemba 13.Muna amekuwa ni mmoja wa watu wa karibu katika kumfariji Lulu kwa kipindi hiki kigumu ambacho anapitia na amekuwa nae bega kwa bega kila siku wanapokwenda mahakamani.

Ukiachana na wote kuwa wasanii katika tasnia moja, Lulu Michael na Muna Love wamekuwa marafiki na watu wa kakribu kama ndugu kwa muda mrefu na kusaidiana kwa mambo mbalimbali .Watu hawa wamekuwa kama ndugu sasa.

Muna pia alishawai kuwa rafiki wa karibu wa Wema Sepetu lakini mambo hayakuwa mambo na waligombana na kurushiana maneno katika mtandao wa instagram na kusababisha mahusiano yao kuvunjika

 

Bifu La Young Dee Na Dogo Janja,Chanzo ni Muna

Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoko kati ya wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva yaani Young Dee na Dogo Janja ambapo katika kufatilia sababu inaonekana ni yale maneno ambayo Young Dee aliyaongea yaliyokuwa yanamuhusu Dogo Janja na Young Killer Msodoki kuwa yeye (Young Dee) ni mkubwa kimuziki hivyo hataki kabisa kusikia watu wakimfanisha na wasanii hao wawili ambao kwake anawaona bado wachanga hawajamfikia kiwango chake. Young Killer alinyamzaza na hajaonekana kuongea chochote kuhusu ili lakini Dogo Janja hakuweza kuvumilia na kuamua kujibu maneno ya Young Dee na kumwambia kuwa hata yeye hawezi kulinganishawa  msanii kama yeye ambae anavuta unga, kabisa hawezi kuongea na ‘mteja’.

Bifu limeendelea na kuwa kubwa mpaka baadhi ya wasanii waliamua kuingia nakuwashauri kuyamaliza mambo hayo, kati ya wasanii hao ni pamoja na Nikki wa Pili.Lakini jana msanii wa muziki wa singeli Sholo Mwamba nae aliamua kufunguka kuhusu bifu ilo huku akiamua kumwaga ubuyu hadharani kuhusu sababu ya wasanii hao kugombana ni mwanamke.

Akiongea na eNews ,Sholo Mwamba ambae alikuwa chini ya menejiment ya Muna Entertainment alifunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye na Muna hawafanyi kazi pamoja na sababu sio kwamba yeye alichokwa na Muna bali yeye alimchoka Muna, alipoulizwa sababau ya yeye kumchoka meneja wake alijibu “Kitu ambacho mimi kiliniuzi na nilikichoka kwa Muda ni kitendo cha sisi wanaume kufanya kazi na kutafuta ela  afu tukienda pale  kwa muna tunakuta madogo wengune wamekaa kwenye makochi wamejiachia, sisi wahuni tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu bosi anatumia na wajinga”aliongea Sholo Mwamba

hapo wote vingasti tu, tunawakuta pale kwa bimkubwa wanajiachia achia tu, Dogo Janja, Young Dee, wanagombana wanagombania demu, ila sisi tunakuja kwa bosi tunawakuta hayo mambo ya kugombana ni miyeyusho tu” aliongezea Sholo Mwamba

Hata hivyo Sholo pia anaonekana ana wivu wa mapenzi kwa Muna Love na kufikia hatua ya kusema ” namshangaa bosi si angenipa hata mimi, akinipa sisemi, tunakula kimyakimya”