“Shilole Angetaka Kiki Angeenda Beach na Uchebe Wake na Kuvua Nguo Zote”-Nay Wa Mitego

Msanii wa MuzikiSana wa Bongo fleva Nay wa Mitego amemjia juu Msanii mwenzake Shilole baada ya kuingilia kati sakata la Muna na kumrushia maneno katika Interview mbali mbali.

Nay ameibuka na kumkingia kifua Muna na kumtolea povu Shilole na kudai anatafuta kiki Kupitia ishu ya Muna na hana lolote kingine linalomsumbua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nay wa Mitego alimuandikia ujumbe huu Shilole:

Shiloleeee Zainabuuu nadhani ulimiss tu Media dada yangu nadhani umefanikiwa kwa kiasi chake. Ulichokosea ni ishu uliyoingilia yaani gear  yako. Sioni alichokosea huyo unayemuita mdogo wako Muna ameongea mengi ambayo watu walitaka kujua nini kilichokuwa kinamsumbua Patrick.

Sasa ungetaka kiki mngeenda Beach na Uchebe wako mnavuana nguo zote alafu mbapiga picha halafu mnaposti bila hata caption halafu mtaona kiki yake ingekuwa noma.Lakini hili la Muna umejichoresha tu umeonekana ulikuwa unatafuta…..Mtazamo wangu tu”.

Sakata kati ya Muna na Shilole lilianza baada ya Muna kufanya Interview na kuweka wazi kuwa Casto ndiye Baba halali wa marehemu mtoto wake Patrick na mambo mengine ambayo yalionekana kutompendeza Shilole.

Ushauri wa Muna kwa Wanawake Wenzie

Mwanadada Muna love ameamua kutoa ushauri wa bure kwa wanwake wenzie wanaobeba mimba  za baba wengine na kuwapa wanaume wengine wazilee mimba hizo eti kisa wanaume waliowapa mimba wamekataa mimba zao.

Akiongea katika Press Conference aliyoifanya leo nyumbani kwake, Muna alisema kuwa wakati wa mazishi aliongea na casto na walikubaliana kuwa wayamalize matatizo yao na kukubali maiti kufikia nyumbani kwa peter kwa sababu tu walikuwa hawataki kugombana  na ndugu na walitaka msiba huo upite lakini sio kwamba mtoto Patrick ni mtoto wa Peter.

Muna anasema  Casto alimwambia “mama pati mimi na wewe tunaujua ukweli ila huwezi kuwabadilisha watu,nimekosea kwa nafis yangu naomba unisamehe kwa sasa hivi tujifanye wajinga tu ili mtoto haifadhiwe kwa sababu kosa tulilokosea ni kuandika jina la mtoto na jina la baba mwingine.

Baada ya kuongea hivi muna nawashauri wanawake wengine na kusema “mimi leo nakiri kwa wanawake wenzangu kuwa hata kama mwanaume mkiwa na mapenzi kiasi gani na una mimba ya mwanaume mwingine usikubali kumpa akalea tu.

Hata hivyo uamuzi wa muna kuongea na waandishi umepokelewa tofauti sana na watu mbalimbali huku wengi wwakisema imekuwa mapema sana kwake kuongea na waandishi kutokana na msiba mkubwa uliompata.

 

 

 

Shiloleh Amtolea Mapovu Muna “Utapata Tabu Sana”

Baada ya kuongea na waandishi wa habari, mwanadada Muna alisema mengi huku akisema kuwa anao uthibitisho wa kutosha kuwa mtoto wake patrick ni mtoto wa Casto na wala sio vinginevyo, huku akisema kuwa  hakuwahi kuwa na mahusiano na peter hata siku moja bali alikuwa akimchukulia kama baba yake na mtu wake wa karibu.

Kila mtu ameyapokea maneno ya Muna kwa hali tofauti lakini shiloleh ni moja ya watu walionhea mara tu  baada ya mahojiano hayo kuisha na kumshangaa sana muna kuwa amepata wapi nguvu ya kusimama na kuwaita waandishi wa habari mpaka kuja nyumbani kwake na kuongea kile alichokiongea .

Shiloleh anasema kuwa hata kama alichokiongea kina ukweli lakini hakupaswa kuonyesha au ku-prove chochote kwa mtu yoyote kwa sababu hata 40 ya mtoto wake ilikuwa bado haijafika.

Muna unaenda kuita press conference,ufanyiwe interviw for what, unafurahia nini, unawaia unawaambia nini na juzi tu umetoka kuzika mtoto wako.unataka kuthibitisha kuwa huyo mtoto ni wa casto hatutaki kujua, we dont need it…mimi ni dada yako kama ungekuwa na shda ungenifata tu kama unavyonifataga kwenye mengine…muna utapata tabu sanaa.

Shiloleh ameonyeshwa kusikitishwa sana na kitendo cha muna kumkana mume wake ambae amefunga nae mpaka ndoa kwa ujinga wake mwenyewe.

Muna Love Amkana Peter Kweupe, Asema Hakuwahi Kuwa na Mahusiano Nae.

Mwanadada Muna Love ameibua mazito baada ya kukana kumjua peter kama mume wake wa ndoa na kusem akuwa peter anamchukulia kama baba yake , kama rafiki yake na kama ndugu na wala sio tofauti na hapo.

Alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, Muna alisema kuwa   hata ile nyumba ya Mwananyamala ambapo anakaa peter  na ndipo ilipofikia maiti ya mtoto wake Patrick  ni ya kwake na kwamba haikuwa na hati bali leseni ya makazi tu wala sio vinginevyo.

nyumba ya mwananamala ni ya kwangu na kila kitu kinachohusu mwananamala ni cha kwangu na hata document ninazo ile numba haina hati ila ina leseni ya makazi,mimi peter nilipokuwa nakaa nae alikuwa kama rafiki na kama mtu wangu wa karibu tu , tuliamua kufanya msiba wa baba pale kwa sababu mimi nilikuwa katika mahusiano na mtu mwingine.

 

 

 

 

Muna Amtaja Baba wa Patrick kuwa ni Casto

Mwanadada muna love amewaita waandisi wa habari mapema leo nyumbani kwake kwa ajili ya kuongea nao kuhusu maswala yaliyokuwa yamezuka katika mitandao ya kijamii baada ya kutokea kwa msiba wa mtoto wake.

Muna anasisistiza kuwa pamoja na kwamba alikubali mtoto wake kufikia nyumbani kwa Peter lakini iyo aiwezi kubadilisa ukweli kuwa patrick ni mtoto wa casto na wala sio mtoto wa peter kama ilivyokuwa  ikieleweka hapo awali.

Muna anasema kuwa kwa sasa yeye ameokoka na hawezi kusema uongo kuhusu ukweli wa marehemu mtoto wake.

 nimeokoka na nina muamini Mungu, na bado nitaendelea kusimama kwenye ukweli kuwa Patrick baba  yake ni Casto

Mke Mwenzie na Muna Afungukia Mahusiano Yake na Peter

Wiki chache zilizopita picha za mume wa Muna Love, Peter Zacharia na mwanamke mwingine anayeitwa Rehem zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Picha hizo zilizowaonyesha Peter na Rehem wakiwa kwenye mahaba mazito kitandani zilisambaa na kusababisha maneno maneno ambapo Peter alikuja kuweka wazi kuwa aliyesambaza picha hizo ni Muna.

Rehema ameibuka na kuweka wazi kuwa zile picha hazina tatizo kwa sababu yeye na Peter wote ni watu wazima alafu Muna ndio alimuacha Peter.

Kwenye mahojiano na Global Publishers  Rehema amesema kwamba anamjua aliyezisambaza picha hizo ila kiufupi Muna atambue yule baba ni mtu mzima na yeye aliondoka kwa hiyo asingeweza kuvumilia kuishi bila ya kuwa na uhusiano.

Jamani Peter ni mtu mzima siyo mtoto, Muna atambue kuwa aliondoka kwake hivyo asingeweza kuishi mwenyewe“.

 

Peter Amtuhumu Muna Kwa Kusambaza Picha Zake Chafu Mtandaoni

Mzazi mwenza wa Muna anayejulikana kama Peter Zachariah amemjia juu mzazi mwenzake na kudai yeye ndiye mtu  aliyehusika kwa usambazaji wa picha zake Chafu Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Peter alidai kuwa anajua wazi anayezisambaza picha hizo mitandaoni ni Muna kwa nia ya kumchafua kwa sababu Aprili, mwaka huu alirudi nyumbani kwake Mwananyamala-Kisiwani na kujifanya kuwa anapanga vitu vyake ndani ya nyumba hiyo kumbe nia ni kunasa picha hizo.

Unajua chochote kinachoendelea hivi sasa najua wazi ni mpango wa Muna, anajitahidi kuufanya ili mimi nionekane wa ajabu baada ya kuona watu walivyonichukulia tofauti kwenye kipindi chote cha msiba wa mtoto wetu hivyo anataka kunichafua lakini mimi kwa hilo sitetereki“.

Peter amekiri alikuwa Kwenye Mahusiano na mwanamke huyo baada ya kuachana na Muna na kumtaja kwa jina la Rehema na kudai kuwa Muna anamfahamu mwanamke huyo.

Kinachonishangaza mimi Muna anataka kujifanya huyo mwanamke ni mpya kwake lakini sio kabisa, anajua kila kitu na jinsi alivyokuwa akitangatanga kwa wanaume tofautitofauti, mimi ningeishi vipi kama mwanaume? Nafikiri anajua fika kwa kufanya hivyo atanichafua mimi kumbe anajichafua yeye”.

Mgogoro wa Muna na mumewe ulijulikana hadharani hivi karibuni mara baada ya mtoto wao kipenzi Patrick kufariki nchini Kenya alipokuwa amekwenda kutibiwa.

Mara baada ya Patrick kufariki, mjadala mzito uliibuka mitandaoni ambapo kuna baadhi walisema baba yake ni Mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson aliyewahi kuwa mpenzi wa Muna lakini wengine wakasema ni wa Peter.

Muna alipotafutwa atoe neno kuhusu tuhuma hizo hakupatikana haraka. Siku chache zilizopita Muna alitangaza atafanya mkutano na waandishi wa habari na kujibu tuhuma zote.

Steve Nyerere Atangaza Kujivua Uongozi Wa Misiba

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere amefunguka na kutangaza kujivua Rasmi nafasi ya kiongozi wa misiba mbali mbali inayowahusu wasanii wa Bongo movie.

Steve amesema ameamua kujitoa katika nafasi hiyo kutokana na fedheha ambayo amekuwa akiipata kutoka kwa watu kutokana na nafasi hiyo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Steve Nyerere amedai kuwa amekua akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida”.

Steve Nyerere amekuwa akirushiwa tuhuma mbali mbali na watu ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa Kula rambi rambi ambapo juzi juzi ndugu wa Agnes Masogange walilalamika kuwa hawa kupokea rambi rambi tangu ichangishwe na Steve.

Muna Kuvunja Ukimya Kufuatia Kifo Cha Patrick

Muigizaji wa Bongo movie na mdau wa Muziki wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amesema yupo tayari kufunguka kufuatia Kifo Cha Mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, amesema kwamba atazungumzia kuhusu ugonjwa wa mtoto wake, alivyoanza matibabu mpaka kifo chake pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa yanatokea.

Nisikilizwe nachotaka kuongea toka mwanangu ameumwa mpaka kufariki sikuongea kitu, Ni watu tu walikuwa wanaongea na kunihukumu, wiki ijayo nitazungumza na waandishi kuweka sawa yote”.

Wiki iliyopita Mtoto wa Muna aliyeitwa Patrick alifatiki dunia lakini gumzo kubwa lilizuka Kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya kutojulikana nani hasa Baba wa mtoto.

Wanaume wawili walijitokeza kama Baba wa watoto ambao ni Peter aliyejitambulisha kama mume wa ndoa wa Muna na Casto ambaye alikuwa anajulikana kama ndio baba wa mtoto.

Mgogoro huo ulisabisha mvutano kati ya familia ya Muna naya Peter kuhusu msiba ufanyike wapi lakini baadaye wawili hao walikubaliana msiba ufanyike kwa Peter na ndipo ratiba ya mazishi ilivyoanza mpaka malaika huyo wa Mungu kuzikwa katika makabduri ya Kinondani jijini Dar es salaam.

Mainda Aitupia Lawama Mitandao Ya Kijamii Kwa Sakata La Msiba Wa Patrick

Msanii Mkongwe wa filamu za kibongo (Bongo movie) Ruth Suka maarufu kama Mainda, ametupa lawama zake zote kwa mitandao ya kijamii baada ya sakata la mazishi ya mtoto Patrick.

Mainda amefunguka na kudai isingekuwa uwepo wa timu timu Kwenye mitandao ya kijamii basi anaamini mtoto Patrick angezikwa vizuri bila ya mashabiki kuingilia Familia ya watu.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers. Mainda alisema anaamini watu wa mitandaoni wamechangia kwa kiasi kikubwa kuweka taarifa za upotoshaji kati ya Muna na mumewe Peter ambazo zimesababisha wawili hao washindwe kuelewana haraka.

Jamani hivi ni vitu gani? Ndiyo maana mimi sipo kwenye mitandao nina sababu kubwa sana. Kuna upotoshaji wa hali ya juu na kama isingekuwa mambo ya matimu haya kusingetokea mvutano mkubwa uliokuwepo na kusababisha mambo mazito kwenye msiba wa mtoto asiyekuwa na hatia kabisa“.

Mvutano mkubwa ulitokea hasa kwa sababu ya mgawanyiko wa kifamilia lakini baadae walifikia uamuzi sahihi na siku ya Jumamosi mtoto Patrick alipumzishwa kwa amani.

Wema Atangaza Rasmi Kumaliza Bifu Na Muna

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ametangaza Kumaliza rasmi bifu lake na aliyekuwa rafiki yake wa siku nyingi Muna Love ili waishi kwa Amani na Upendo.

Wema amefunguka hayo siku ya  Jumamosi, Julai 7, 2018 katika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar wakati wa kuaga mwili wa mtoto Muna, Patrick aliyefariki dunia Nairobi nchini Kenya, Julai 3 na kuzikwa siku ya Jumamosi katika Makaburi ya Kinondoni.

Pole zangu ziende kwa wazazi wa Patrick ambao ni Muna na Patrick, Muna ni rafiki yangu wa muda mrefu, nisingemjua Muna basi nisingemjua Patrick. Nilimpenda sana Patrick, japo sijabahatika kupata mtoto lakini nafahamu maumivu mnayopitia kwa kupoteza mtoto wenu“.

Muna pole sana, najua ulivyompenda Patrick, na mapenzi yako kwake ndiyo yametufanya hata sisi tuwe hapa leo, mimi huwa napenda sana watoto, najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, ninaamini Mwenyezi Mungu atakupa nguvu wewe na baba Patrick.

Ninaomba tuyaache ya mitandaoni, najua mtoto wenu atafurahi huko aliko akiona mnaupendo na hakuna mgawanyiko kama huu ambao tumekuwa tukiuona. Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda, yaliyopita si ndwele tugange yajayo”.

Miaka miwili iliyopita Wema na Muna waliongia Kwenye bifu zito Kwenye mitandao ya kijamii na hata kuvunja urafiki wao.

Mazishi Ya Mtoto Wa Muna, Patrick Peter (+picha)

Mtoto wa msanii wa Bongo movie na mdau wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love aliyeitwa Patrick Peter ameagwa rasmi siku ya Jumamosi katika viwanja vya leaders.

Patrick alifariki wiki iliyopita Nchini Kenya, Nairobi na kuzikwa siku ya Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni.

Hizi ni baadhi ya picha za mazishi ya Patrick Peter katika makuburi ya Kinondoni:

.
.
.

Ndugu wa Peter Wamshukuru Muna Kukubali Suluhisho la Mazishi.

Baada ya mgogoro wa muda mrefu na baadae kufikia muafaka wa sehemu ya kuzika na wapi mait ya mtoto itafikia, ndugu wa baba mzazi wa mtoto patrick wamefunguka na kumshuru sana muna kwa uamuzi wake aliofkia wa kukubali kila kitu kiende sawa ili kumpumzisha mtoto  huyo.

Muna ambae hapo awali alisema kuwa patrick sio mtoto wa Peter bali ni mtoto wa Casto alikataa maiti ya mtoto huyo kufikia kwa Peter mwananyamal na kutaka ifikie nyumbani kwake mbezi lakini baada ya kufanbya maongezi ya muda mrefu huku steve nyerer akishughulika na hilo muna alikubali kila kitu,

akiongea na waandishi, Bazo Peter, mdogo wake na Peter amefunguka na kumshukuru Muna kwa uamuzi huo na kumtia moyo pia “tunamshukuru sana Muna love kwa kuwa na utu na hali ya uelewa  bada ya kuonea nae kupitiamarafiki zake wa karibu na ndipo alipotuelewa na sasa tuna amani kabisa.

patrick atafikishwa Dar Es Salaam siku ya ijumaa na kupelekwa mochwari ya mwananyamala ambapo siku ya jumamosi wataaga mwili huo Leaders club na baada ya hapo wataenda kuzika katika makaburi ya Kinondoni.

Steve Nyerere Amwagia Povu Zito Muna

Muigizaji wa Bongo movie na kiongozi wa moja wa wasanii wa filamu nchini Steve Nyerere amewajia Muna na Familia yake juu ya sintofahamu zinazoendelea hivi sasa juu ya msiba wa mtoto wa Muna , Marehemu Patrick.

Steve Nyerere amemvaa mama wa mtoto huyo (Muna) na kumwambia aache kuwayumbisha watu badala yake aungane na mume wake wa ndoa (Petere Zacharia) ili kusitiri mtoto wao kwa heshima kuliko kuwafaidisha watu kwa mameneno na mifarakano yao mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Muna Muna Muna Muna Muna, naomba unisikilize popote ulipo, huu muda si wakufukua makaburi.
Wewe muna kwangu ni mama bora, ulimpenda mwanao ulisimama na mwanao mpaka kipindi cha mwisho. MUNGU akupe nguvu Muna.

Muna embu kaa tena chini jifikilie, ulitumia nguvu akili na maarifa yako yote na WATANZANIA wakatokea kukusapoti kwa namna moja ama nyingine. Kila mtu ameguswa na msiba wa mwanao ndani ya nchi na nje ya nchi, basi nakuomba Muna tumia busara sana weka utoto pembeni, Mweke shetani pembeni shilikiano na MUME wako wa NDOA kumpumzisha mtoto wenu.

“Matatizo yenu wekeni kando kipindi hiki kigumu Muna msiwape watu faida Muna, Naimani umeokoka basi kwenye hili kuwa na HOFU na MUNGU, sizani Muna kama aya tunayo yasoma mara mtoto wa huyu mara wa huyu, mara niliolewa nikiwa na mimba kama yanakujenga.

Bali nazani yanabomoa heshima yako.Dada nakuomba Fumba macho hili lipite nazani ata Patrick uko alipo analia kuona mfarakano huuuu. Msimtese mtoto uko alipo, tumieni busara sana .Baada ya maziko ayo mambo yenu mtaendelea nayo kwa sasa ushauri wangu ungana na family muweze kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili.

Washauri wa Muna nawaomba unganeni na family ya Peter kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili sisi wangine tupo pande zote ila atupendezwi na haya tunayo yaona nilizani ni muda muafaka wote kukusanyika mwananyamala kwa Peter kuhakikisha tunampumzisha kijana wetu asante“.

 

Ugonjwa Uliomuua Mtoto Patrick Wabainika

Siku ya Jumanne usiku mtoto wa Muna aliyekuwa anaitwa Patrick aliyekuwa na miaka 8 aliaga dunia hospitalini alipokuwa anatibiwa Nairobi nchini Kenya.

Global Publishers wanaripoti kuwa katika harakati za kutaka kujua nini hasa kilimuua mtoto huyo walianza kuongea na Muna ambaye yupo nchini Kenya kwa hivi sasa ambapo alifunguka:

Kinachomsumbua mwanangu ni uvimbe kwenye ubongo na hajaamka kwa siku sita huku akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’ hivyo tunasubiri aamke ndipo madaktari waangalie kama watamfanyia operesheni au la“.

Muna alifunguka hayo kabla ya taarifa za Kifo chake.

Lakini pia Daktari ambaye amewahi kumtibu mtoto na yeye alifunguka kuhusu ugonjwa wa mtoto:

Dk Chale alisema uvimbe kwenye ubongo kitaalamu huitwa ‘Brain Tumour’ ambao unaweza kuwa wa kawaida au kansa na husababishwa na njia kuu mbili; moja ni ubongo wenyewe na pili kutokana na viungo vingine.

Katika njia ya kwanza ni kwamba inawezekana ugonjwa huu ukarithi kutoka kwa familia kama baba au mama amewahi kuwa na matatizo hayo basi lazima na wengine warithi. Sababu nyinginezo ambazo zinachangia ni maambukizi ya virusi wa ugonjwa huo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, sababu za kimazingira ambayo mtu anaishi, kemikali za viwandani, vipodozi, chakula, dawa na nyingine nyingi.

Katika njia ya pili ya viungo vingine hutokana na kama mtu ana kansa ya mapafu, kizazi, matiti, figo, tezi dume hizi huweza kusa babisha uvimbe kwenye ubongo. Dk Chale aliendelea kufafanua kuwa uvimbe kwenye ubongo kwa upande wa watoto mara nyingi huwa ni kansa na siyo wa kawaida ndiyo maana huua haraka sana na hawawezi kupona maana uvimbe huwa chini ya ubongo na siyo kwa juu kama inavyokuwa kwa watu wazima.

Mwenyezi Mungu aendelee kufika za roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

Muna Amtaja Casto Kama Baba Wa Mtoto Ahaidi Kumuumbua Peter

Muigizaji wa Bongo movie na mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Muna Love amefunguka na kuweka wazi kuwa Baba wa mtoto wake Marehemu Patrick ni Casto Dickson.

Kauli hiyo imekuja baada ya utata kutanda kuhusu nani ni Baba wa mtoto baada ya mwanaume mwingine anayeitwa Peter kujitambulisha na kudai kuwa yeye ndio Baba wa mtoto.

Marehemu Patrick na Peter

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Muna ameweka wazi kuwa hataki utata huo anachotaka ni kumzika mtoto wake na kumtaja Casto kama Baba na msiba utakuwa nyumbani kwake Mbezi:

Jaman jamani ?????? naomba nimzike mtoto wangu ???? vaeni viatu vyangu. Kuna siri kumbwa amjawahi kuijua nawaomba nimzike mtoto wangu alafu ndiyo mnitukane. Mimi ?????? naumia jamani, namuheshimu Peter siwezi kuweka kitu hapa maana nitamwaibisha….Siwezi kumsema Casto maana yeye anajua wapi alikosea, nawaombeni jamani, naomba nataka kumzika mwanangu. Miaka miwili nahangaika na Paty wangu ????????, nimalize kumzika niongee.

Nnyiwe wanawake mnaonihumuku, vaeni viatu vya siri nilizohifadhi… baba wa mtoto ni Casto, inatosha ????????, nitukaneni mimi nife ila Paty ni kiongozi alieniongoza nione maisha mapya na nimjue Mungu… Nitalia milele mimi.

Paty wangu????????leo wanakugombania mwaanangu, natamani urudi mara moja??????????… Mwanangu ntaleta ijumaa na ntamzika Jumamosi?????, msiba uko kwangu Mbezi Beach“.