Papii Kocha Atangaza Kurudi Bendi Yake Ya Ngwasuma

Msanii wa muziki wa Dansi nchini Johnson Nguza Viking ‘Papii Kocha’ amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kurudi katika bendi yake ya Ngwasuma.

Papii Kocha ametangaza kujiunga na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliyokuwa akiitumikia kabla ya kupatwa na majanga ya kifungo cha maisha na baadaye kupata msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Papii Kocha alisema kuwa hafikirii kujiunga na bendi nyingine yoyote zaidi ya kurudi kwenye bendi yake hiyo ya zamani kwani bado anaipenda.

Kwa sasa nafanya kazi ya muziki kwenye maonesho mbalimbali nikiwa na baba (Babu Seya) kama wasanii binafsi lakini nikishatulia vizuri natarajia kurudi FM Academia na sifikirii kujiunga na bendi nyingine tofauti na hiyo“.

 

Pappii Kocha Afungukia Tetesi Za Kubambikiwa Mtoto

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Johnson Nguza Viking maarufu kama Pappii Kocha amefungukia tetesi ambazo zimekuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii ambapo mashabiki zake wamehoji endapo yule ni Mtoto Wake.

Oktoba 28 mwaka huu Pappii Kocha alimuweka hadharani Mtoto Wake ambaye alimzaa mara tu Baada ya kutoka gerezani kwa msamaha wa raisi mapema mwaka huu.

Wapo waliojifanya wanajua kukokotoa mahesabu kwa kumhesabia siku alizotoka jela na kulinganisha na muda wa kubeba mimba kisha kujipa majibu kuwa mtoto huyo si wake kwamba huenda amebambikiwa, lakini wapo waliompongeza na kutaka kumjua mwanamke aliyezaa naye.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Papii Kocha alikana tetesi hizo na kusema kuwa Mtoto Yule ni wa kwake na ana uhakika huo:

Unajua nini? Mimi nilitoka jela Desemba 9, mwaka jana ambapo Desemba 9, mwaka huu (kesho) nitakuwa natimiza mwaka mmoja, na siku niliyotoka nilipokelewa na mama mtoto nikabahatika siku hiyohiyo kumpa ujauzito hivyo naamini mtoto wangu ni wa halali kabisa na niwatoe wasiwasi”.

Papii Kocha tayari ana Mtoto wa kike ambaye ana umri wa miaka 18 aliyemzaa kabla ya kwenda jela Lakini hivi sasa Papii Kocha amekataa kumuweka wazi mwanamke aliyezaa naye.

Papii Kocha Atangaza Kupata Mtoto.

Msanii wa muziki wa dansi papii kocha ametangaza katika ukurasa wake wa instagram kuwa siku ya leo amebahatika kupata mtoto wa kike .Papii kocha ambae kwa sasa ana zaidi ya mwaka mmoja uraiani baada ya kutoka jela alipokwekwa kwa kifungo cha maisha lakini alitolewa kwa msamaha wa rais.

Ikumbukwe kuwa kipindi papii anakwenda jela aliacha mke na mtoto mmoja wa kike, mtoto ambae mpoaka sasa ameshafikia umri wa utu uzima na kumkuta mke wake tayari alshaolewa na mwanaume mwingine.

Papii kocha atakuwa anatimiza idadi ya watoto wa wili wa kike ambae wa kwanza alimpata kabla hajakwenda gerezani, hatahivyo mama wa mtoto huyo bado hajuajulikana na hakutaka kumtangaza.

Wanawake Weupe Sio Ugonjwa Wangu:-Papii Kocha

Msanii wa muziki wa siku nyingi Papii Kocha kutoka familia ya viking amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake sifa kubwa ya mwanamke anyoipenda sio ra kwa sababu wanawake wenye rangi nyeupe kwake sio kitu hata kidogo.

Papii Kocha ameyasema hayo alipokuwa kaifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuhakikisha kuwa pamoja na kwamba mwanamke  huyo anaweza kumtongoza yeye lakini haimaanishi kwamba atamkubali kwa sababu ranngi nyeupe sio ugonjwa wake.

mwanamke mweupe hata anitongoze kwa njia gani huwa siwezi kumuelewa tu,maana rangi nyeupe sio ugonjwa wangu

papii kocha ambae alikuwa grezani kwa takribani miaka 14 na kuiacha familia yake ya mke na mtoto uraiani aliporudi alikuta mke wake tayari amekwisha olewa na mwanaume mwingine.

Papii Kocha Ajivunia Mtoto Wake

Msanii wa muziki wa dansi nchini, Papii Kocha anasema kuwa amekuwa akijivunia sana mtoto wake wa kike  aliyemwacha akiwa mdogo pindi anakwenda jela baada ya kupatwa na kesi iliyotakiwa kuwagharimu maisha yao wakiwa huko.

Papii ambae baada ya kukaa jela kwa zaidi ya miaka 14 wamtoka jela  kwa msamaha wa raisi lakini moja ya vitu ambavyo vilimshangaza ni kumuona binti yake ambae alikuwa mdogo kipindi hicho kuwa mkubwa na mtu mzima kabisa.

Papii anasem akuwa kwake ni jambo la kujivunia na kumshukuru sana Mungu kwa kumtunzia binti yake na kumkuta akiwa salama na siku zote binti yake ni sifa yake.

Papii Atamani Kupanda Mwendokasi, Ashangazwa na Uwepo wa Mitandao ya Kijamii.

Ni miaka 14 tangu walipopata hukumu yao na kukaa gerezani kwa muda wote huo, kipindi hicho hakukuwa na mambo mengi ambayo wameyakuta sasa hivi yanaendelea katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia .Akiongea na Leo Tena ya Cloud Radio, Papii Kocha amefunguka na kuelezea mshangao wake aliokuwa nao baada ya kutoka gerezani baada ya kukaa muda wote huo.Katika vitu alivyokuwa akishangaa ni   uwepo wa mabasi ya  mwendokasi.

Nilipotoka jela nimeona vitu vingi sana vimebadilika, nimeshangaa sana kuona mabasi ya mwendokasi ila sijayapanda ila natamani sana kuyapanda , ninaogopa watu tu watakuwa wengi na maswali yatakuwa mengi.

Akiendelea kuelezea kuhusu vitu vingi alivyovikuta amesema pia  anasema kuwa mwaka 2003 wakati wanahukumiwa hakukuwa na mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, whatsaap  na instagram lakini sasa hivi ametoka ameikuta ingawa hawezi kuitumia kunawatu wamekuwa wakimsaidia lakini ni mizuri.

Kweli hakukuwa na mitandao ya kijamii , tulikuwa tunatumia simu zile kubwa za twanga pepeta lakini kwa sasa kutumia hii mitandao ndugu zangu ndo wananisaidia nimeipenda mitandao ni mizuri sana.kuna mtu ananisaidia kutumia lakini whatsapp natumia mwenyewe.

Papii Kocha anasema kuwa mambo mengi yamebadilika sana hata kasi ya maendeleo ni kubwa sana kulinganisha na walivyokuwa wameacha na hata baadhi ya maeneo yamekuwa kama nje ya nchi .

Papii Kocha Amefungukia Mapenzi Yake Kwa Mwanaye

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Papii Kocha aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na wimbo wake wa ‘Seya’ amefunguka na kusema hakuna kitu kinachompa Faraja na ushujaa kama kumuangalia mtoto wake.

Papii Kocha alitumikia kifungo jela kwa takribani miaka minne na katika kipindi hiko chote alimuacha binti yake aliyemtaja kwa jina la Asha uraiani akiwa mdogo sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la ‘Amani’ Papii Kocha amekiri kuwa kwa kipindi chote alichokaa gerezani kwa miaka kumi na nne hakupata muda mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia gerezani lakini kwa sasa ameona afanye kila analoweza ili mwanaye aweze angalau kufaidi matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu.

Unajua sijakaa na mtoto wangu kwa Kipindi kirefu sasa na hivi sasa ndio anafaidi matunda kutoka kwa baba yake hivyo ni lazima nifanye kazi kwa jasho jingi ili ayafaidi matunda yangu”.

Lakini pia Papii Kocha amewasisitizia mashabiki zake kumiminika kwa wingi kwenye Show yao inayotarajiwa kufanyika tarehe 10 machi katika ukumbi wa King Solomon Hall.

Papii Kocha na Babu Seya Kupiga Bonge la Show ‘Vikings Night’

Wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo fleva waliowahi kutamba na kibao chao cha ‘Seya’ Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Papii Kocha wanampango wa kufanya bonge moja la show itakayoitwa ‘The Vikings Night’.

Wasanii hao Baba na mwana waliokuwa jela kwa miaka zaidi ya 10 kwa mashtaka ya kubaka, ambapo walifanikiwa kuonja ladha ya uraiani mapema mwaka jana siku ya uhuru 9 disemba ambapo walitoka jela kwa msamaha wa raisi.

Tangu warudi uraiani miezi mitatu iliyopita wasanii hawa wanatarajiwa kufanya Show yao kubwa ya kwanza baada ya kuachiwa huru ingawa wameshafanya shoo chache hasa visiwani Zanzibar shoo hii inatarajiwa kuwa kubwa zaidi.

Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 10 machi katika ukumbi wa King Solomon Hall. Papii Kocha ameshatoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Waambie ambao Mpaka sasa tayari unafanya vizuri sana.

Aunty Lulu Atoa Ofa Kwa Papii Kocha.

Mwanadada aliyewahi kujipatia umaarufu wake kwa kazi ya utangazaji ambae pia haachi kuwa na drama za mara kwa mara, Aunty Lulu amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kumpa ofa msanii wa muziki papii kocha kwa muda wot mpaka asahau maisha ya jela aliyoyapitia.

Aunty Lulu anasema kuwa amemuona papii kocha na ameona jinsi ambavyo amekuwa akipendeza na kuwa mpya hivyo yuo tayari kumpa penzi litakalomfanyua asahau shida na mateso aliyokuwa ameyapitia kipindi yupo jela.

Aunty Lulu ambae amejisifia kuwa anajua sana kupenda amesema kuwa yuko tayari endapo msanii huyo atakubali kumpatia nafasi.

Unajua mimi najua kupenda,endapo nitampatia penzi papii kocha mbona atasahau kabisa alipotoka.Yeye akubali tu mbona sijawahi kuona mahusiano yake,naamini kwa kipindi alichokaa jela kama angekuwa na mwanamke angekuwa tayari ameshajitokeza siku nyingi.-Alifunguka Aunty Lulu.

Jitihada za kumtafuta papii kocha ziligonga mwamba baada ya simu ya msanii huyo kutokupatikana ili kujulishwa taarifa hizo.

Papii kocha na baba yake walikuwa wasanii wa muziki waliofanya vizuri kwa muda mrefu lakini kazi zao zilisimama baada ya kukaa jela kwa muda mrefu kwa kosa la kulawiti watoto , lakini mwaka 2017 mwishoni wasanii hao walipokea msamaha wa rais na kuachiwa huru.

wasanii hao sasa hivi wamepanga kurudi kwa kasi ya ajabu huku wakiwa chini ya studio ya Wanene Entertainment huku wakipokea msaada na uangalizi wa wizara ya habari na michezo ili waweze kuimarika kimuziki.