“Rayvanny Alivyofungiwa Nilikuwa Napata Mawazo Sana”- Fahyma

Mpenzi na mama Watoto wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma ‘ Fahyvanny’ amefunguka na kuweka wazi Furaha yake Baada ya Rayvanny kufunguliwa na BASATA.

Fahyma amekiri kufurahishwa na kitendo cha baba mtoto wake huyo kusamehewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwani ishu hiyo ilikuwa inamnyima usingizi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Fahyma alisema katika kitu kilichokuwa kinampa mawazo na kukosa kabisa usingizi ni kufungiwa kwa baba mtoto wake huyo lakini kwa sasa anaishukuru Basata kwa kuwahurumia na kuwafungulia kuendelea na kazi kama kawaida.

Kufungiwa kwa Rayvanny kulikuwa kunanipa mawazo sana maana nilikuwa nawaza maisha yetu yatakuwaje na tulikuwa hatujui msamaha utatoka lini lakini tunashukuru Mungu wamesamehewa na mwisho wa siku maisha mengine yanaendelea, nitaendelea kumhimiza asirudie kosa tena”.

Rayvanny na Diamond Platnumz walifungiwa na BASATA Baada ya kupandishwa stejini na kuperfom wimbo wao wa ‘Mwanza’ ambao ulikuwa umepigwa stop kwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Fahyma Adai Haoni Sababu Ya Wimbo Wa Rayvanny Kufungiwa

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyvanny ameibuka na kumkingia kifua Mpenzi Wake kuhusu sakata la BASATA kufungia nyimbo yake ya Mwanza.

Siku chache zilizopita Rayvanny na Diamond waliachia nyimbo yao mpya lakini muda mchache Baada ya kuachiwa BASATA waliifungia kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Fahyvanny amedai wimbo wa mzazi mwenziye uliofungiwa ni kwa ajili ya kuburudusha vijana na sio watoto kwa hiyo ziwekwe sheria ambazo zitawapa wasanii uhuru wa kubuni vitu vizuri kwa kuwa sio wote wameuelewa wimbo huo kutokana na ubunifu uliotumika.

Nimejisikia vibaya sana kwa sababu ni kazi ya mume wangu halafu ni kazi ambayo naipenda sana, lakini pia wamepoteza pesa nyingi na muda kurekodi halafu wanafungia wimbo kirahisi tu, wanaposema wimbo hauna maadili huwezi jua kila mtu anaposikiliza anakuwa ana mtazamo wake.

Mimi sioni tatizo kwenye huo wimbo kwa sababu umetungwa kwa ubunifu wa hali ya juu mbona nchi za wenzetu hawana haya mambo jamani tena kama Nigeria wanaandika kabisa kuwa muvi hii ni kwa ajili ya watu walio juu ya miaka kumi na nane”.

Baada ya wimbo huo kupigwa stop kupigwa BASATA iliwatoza WCB faini ya milioni 9 na kukataza kabisa wimbo huo kupigwa sehemu yoyote nchini na kuwakataza wasanii kuperfome wimbo huo stejini.

“Nagombana Sana na Rayvanny Ila Ndio Nishampenda Simuachia”- Fahyma

Mpenzi na Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma au Fahyvanny amefunguka na kuweka wazi Siri ya kudumu kwenye Penzi kwa muda mrefu.

Tofauti na mastaa wengi Rayvanny na Fahyma ndio kapo ya WCB ambayo imedumu kwa muda mrefu na hii ni tangu walipoanzisha mahusiano miaka michache iliyopita Baada ya kukutana kwenye moja ya video za Rayvanny ambapo Fahyma alikuwa video queen.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Fahyma alisema kwamba, watu wengi huwa wanahisi yeye na mzazi mwenzake hawagombani kitu ambacho si kweli, huwa wanagombana mara nyingi ila upendo na uvumilivu ndivyo vinawafanya waendelee kudumu mpaka sasa.

Kuna watu huwa wanafikiri mimi na mzazi mwenzangu hatugombani, kitu ambacho si kweli huwa tunagombana sana tu, ila sema binafsi nilishaamua kutulia naye, nampenda basi inatosha na ndiyo maana hamjawahi kusikia nina bwana mwingine zaidi yake“.

Rayvanny alishatangaza ndoa na Fahyma na hata kumpeleka kumtambulisha nyumbani kwani Mbeya mwaka jana.

Rayvanny Ahofia Kuibiwa Mpenzi Wake na Wanaume Wakware

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa kutoka WCB, Rayvanny amefunguka na kuweka wazi kuwa anahofia wanaume wakware washiriki wakamuiba mpenzi wake Fahyma.

Siku za hivi karibuni Rayvanny amekuwa akiwa mstari wa mbele kujulisha watu wote kuwa anampenda mpenzi wake Fahyma kwani amekuwa akimposti mara kwa mara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata ni siku chache tu zilizopita ambapo Rayvanny aliweka wazi mipango yake ya kutaka kumuoa mpenzi wake baada ya kuandika kwamba hivi karibuni atamchukua jumla jumla mrembo ambaye amemzalisha mtoto mmoja, Jayden.

Jana Kupitia ukurasa wake Instagram Rayvanny amemtahadharisha mpenzi wake juu ya kuwa makini na wanaume wakware ambao watajaribu kumtongoza na kuharibu penzi lao:

Itaniuma sana siku Pumbavu wakiniibia…..Mama jilinde ukipewa hi tu wewe Buloooock……..maana wanaanziaga mahali”.

Rayvanny Afuata Nyayo za Diamond na Kutangaza Ndoa

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny amefuata nyayo za Bosi wake Diamond Platnumz aliyetangaza kufunga ndoa mwaka huu ambapo na yeye amesema tegemea kuona ndoa yake  hivi karibuni.

Diamond aliwashangaza watu siku chache zilizopita baada ya kumuomba Baraka mama yake mzazi na kumuhaidi kuwa atafunga ndoa mwaka huu hasa kwa sababu ameachana na mpenzi wake Zari mwezi uliopita.

Lakini inaelekea Rayvanny amefuata nyayo hizo hizo kwani na yeye ameibuka na kusema kuwa na yeye anatarajia kumuoa mpenzi wake na mama watoto wake Fahyma.

Taarifa hiyo imekuja siku chache baada ya wapendanao hao kutoka mkoani Mbeya nyumbani Kwa Rayvanny ambapo walienda kwa ajili ya shughuli zao za kifamilia.

Kupitia mtandao wa Instagram Rayvanny aliweka picha yake akiwa katika vazi la suti na kuandika “Bwana Harusi” naye mpenzi wake Fayvanny hakubaki nyuma na akuamua kujibu kuashiria wapo katika michakatao hiyo ya ndoa.

Ohh bby I can’t wait for the day & you will be mine forever (sooooooon) @rayvanny ”.

Aliandika Rayvanny akiashiria ana mpango wa kufunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Abdu Kiba Amefunguka Baada ya Video Yake na Fahyma wa Rayvanny Kusambaa Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye pia ni maarufu sana kwa sababu ya undugu alionao na staa wa Bongo fleva Ali Kiba, amefunguka na kuongea kwa mara ya kwanza kuhusiana na video iliyomuonyesha yeye na mke wa Rayvanny.

Kipindi cha nyuma kidogo kuna video ambayo ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Abdu Kiba na baby mama wa Rayvanny anayejulikana kama Fahyma au Fahyvanny wakiwa wamepozi wanapiga stori.

Inajulikana wazi kuwa Rayvanny yupo WCB na Diamond ni bossi wake lakini pia inajulikana kuwa Ali Kiba na Diamond ni paka na panya hivyo hiyo inapelekea makundi haya mawili kuwa na bifu hivyo ilipotokea Rayvanny na Fahyma wameachana kisha video yake na Abdu Kiba ikasambaa mtandaoni maneno mengi yalisemwa kutokana na ushindani wa kimuziki uliopo baina ya Ali Kiba na Abdu Kiba dhidi ya timu nzima ya WCB.

Baada ya sakata hilo Abdu Kiba Amefunguka Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Tv ambapo amedai kuwa anamjua fahyma tangu zamani sana na ile video ni ya kitambo kipindi hicho  fahyma alikuwa shabiki wake.

Nilimjulia yule msichana alikokuwa anafanya kazi kule Tv One na tulikuwepo tunafanya Interview ya television na kati kati ya Interview tukarekodi ile video na kipindi kile alikuwa ni shabiki wangu mkubwa lakini hiyo ilikuwa zamani kabla hajawa na Rayvanny nahisi lakini tangu amekuwa kwenye Mahusiano naye sijawasiliana naye”.

 

Rayvanny na Fahyma Hawajaachana Bali Walipishana Kauli- Babu Tale

Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka kuhusu sakata lilitokea kati ya msanii kutoka WCB Rayvanny na Mama watoto wake Fahyma.

Siku chache zilizopita Rayvanny na mpenzi wake Fahyma walitawala headlines na kutrend kwenye mitandao ya kijamii baada ya wawili hao kurushiana maneno na kupelejea watu kudhani kuwa labda wawili hao wameachana.

Tetesi za michepuko kuhusishwa kwenye ugomvi huo zilitawala hasa baada ya Rayvanny kuanza kurusha picha za wasichana wengine lakini kilicho washangaza watu wengi ni kitendo cha wawili hao kugombana na kuamua kuachana kwenye Instagram.

Babu Tale ambaye ni Meneja wao alifunguka na kudai sio kweli kuwa wawili hao wameachana ila tu kilichotokea ni walipishana kauli na kutoelewana kidogo.

Kwenye interview na Soudy Brown kupitia kipindi cha XXl cha Clouds, Babu Tale alifunguka yafuatayo:

Kusema ukweli hata mimi naona mnachoona nyie mitandaoni nikimuuliza vipi kunani anacheka tu namwambia hapa kuweni makini mmezaa msilete ujana kwenye maisha ya ndoa hata kama mkiwa hamjaoana lakini mtoto wenu bado mdogo kwaiyo manya mzaha au mnapogombana kuweni making lakini mwenyewe akaniambia hawajagombana walipishana kauli tu Mimi nikamshauri awe makini tu lakini ndio mapenzi ya mastaa hayo ila baadae nawaona wanaongea kwenye video call ila mimi sijataka kuwaaingilia maana nisije kuwa naletewa kesi kila siku bure”.

 

Harmonize Amshauri RayVanny Amsamehe Mpenzi Wake Fahyma

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB, Harmonize ameingilia kati na igomvi unaoendelea mtandaoni kati ya msanii mwenzake kutoka WCB Rayvanny na mzazi mwenzie Fahyma.

Siku ya Jumatatu Rayvanny na Fahyma walianzisha balaa mtandaoni na kutrend baada ya kulete matatizo yao mtandaoni na Rayvanny kumtosa mama mtoto wake huyo na kumwambia aache kutumia jina lake.

Kisa cha Rayvanny kumtosa Fahyma hakijajulikana lakini kumekuwa na tetesi kuwa mini mkata kamba aliyeingilia penzi lao ni michepuko ingawa haijajulikana sana ni nani kati yao mwenye michepuko kwani kila mmoja ameonekana kumtupia lawama.

Mpaka hivi sasa hakuna taarifa kabisa ya uhakika kuhusu nini kinaendelea lakini tangu Jumanne Rayvanny amekuwa akilalamikia kitendo cha kumkosa mwanae Jaden, yaani inavyoelekea Rayvanny na Fahyma hawako wote na Fahyma ndo yuko na mtoto wao.

Sasa Jana rafiki wa Rayvanny na msanii mwenzie Harmonize aliibuka na kumpa ushauri na kumuomba wayamalize matatizo yao yanayowakabili na waweze kumlea mtoto wao:

Lakini hapana kaka tusifike huko mtoto anahitaji matunzo ya baba na mama tumlaani shetani kwani mwenzio kateleza”.

Baada ya Harmonize kuandika maneno hayo kwenye ukurasa wa Rayvanny wa Instagram watu wengi walitafsiri maneno hayo kama Fahyma ndiye mwenye makosa kwani Harmonize alikuwa anamuombea msamaha, lakini badala yake Rayvanny alipuuza maneno yake na kumwambia Harmonize aache unafki