“Maisha Yangu Yanategemea Bongo Movie” Kilio Cha Shamsa Ford Kwa Wadau

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameirudish mada ya Bongo movie mezani huku safari hii akilia na wadau mbali mbali wa Sanaa na kuwasihi waifufue Bongo movie maana maisha yake yanategemea kazi hiyo.

Kwa miaka hii ya karibuni sio siri bali Bongo movie imepotea sio sawa sawa na ilipokuwa miaka mitano iliyopita ambapo kazi zilikuwa zinafanyika na mashabiki wa kununua filamu hizo walikuwepo lakini sasahivi hakuna mashabiki.

Shamsa Ford akiwa mmoja ya wasanii waliopata umaarufu kupitia kuigiza filamu hizo za Bongo movie amejikuta akisononeka na sekta hiyo ilipofikia kwani sasa haisikiki kabisa na waigizaji wengi wanajaribu kupenya kwenye Bongo fleva na wengine kujiingiza kwenye biashara nyingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shamsa ameandika ujumbe ambao amewataka wakongwe wa tasnia, madirector na hata wadau mbali mbali kufanya jambo ambalo litasaidia kufufua fani hiyo:

Jamani Johari Chagula, JB, Richie Mtambalike, Ray Kigosi, Cloud tafadhali jamani fanyeni kitu nyie ndio wenye Bongo movie please irudisheni kupitia nyie imetusaidia wengine kupata ajira na kuendesha familia zetu sasa hivi Bongo movie ilipo naumia kwa sababu Mimi ni mmoja wa watu ambaye naishi kuitegemea Bongo movie sio kama wale wanaosema hawaishi kwa kutegemea movie…please nawategemea wadau was”.

 

Shamsa Ford:Naheshimu Sana Ndoa Yangu

Msanii wa filmu tanzania Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hawezi kufanya upumbavu wa kuharibu ndoa yake kwa mabo ya kijinga au kumkazwa mume wake .Shamsa amesema kuwa kama na yeye angekuwa anataka kujivika ustaa na kuacha kuheshimu ndoa yake mpaka sasa angekuwa ameshaachika kama wasanii wengi wa kike wanavyoachika na kushindwa ndoa.

Shamsa anasema kuwa alipoamua kuolewa aliamua kujishusha kabisa na kufanya yale yanayotakiwa katika ndoa kwa sababu aliamini kabisa kama angeendekeza ustaa basi ndoa ingekuwa ilishamshinda siku nyingi.Shamsa anasema kuwa katika ndoa kuna vitu lazima mwanamke uvilinde na ndio maana hata yeye ameweza kudumu na kuachana na mambo ya usanii.

Siwezi kufanya ujinga wa kuichezea ndoa yangu hata siku moja,kwani ndoa ni kitu adimu sana kwaio unapokipata lazima ukilinde na kukitunza vizuri sana.kama ni ustaa nauacha mlangoni, ninpoingia nyumbani kwangu nayaacha yote la sivyo ndoa yangu isingedumu hata siku moja.

Shamsa aliolewa mwaka juzi na moja ya watu wanaopendezesha wasanii jijini Chidi Mapenzi na amedumu katika ndoa hiyo tangu amefunga ndoa.

 

 

Shamsa Ford Akatazwa Kutumia Mitandao ya Kijamii na Mumewe.

Msanii wa bongo movie Shamsa Ford ambae amolewaa miaka miwili iliyopita, amefunguka na kuthibitisha kuwa mume wake alimwambai aache kutumia mtandao wa kijamii hasa instagram ili kuepusha shari na matusi kutoka kwa mashabiki.Shamsa Ford ambae kwa sasa amekua haonekani sana katika mitandao ya kijamii  huku sababu ikisemekana kuwa sababu ni kukatazwa na mume wake chid mapenzi.

Mtu wa karibu na Shamsa Ford alisema kuwa shamsa alikatazwa kutumia mitandoa hiyo kwa sababu alikuwa akitumia muda mwingi katika mtandao wa instagram na kuweka poicha na hata muda mwingine alikuwa akiambulia matusi kutoka kwa mashabiki kitu ambacho kimekuwa  kikimkera sana mume wake na kumfanya amkataza kuweka picha  na kutumia mtandoa huo.

Kampuni ya habari ya GPL,liliamua kumtafuta Shamsa Ford ili aweze kusema juu ya hilo ndipo nae alipokiri kuwa ni kweli mume wake alimwambaiaache kutumia mtandao huu kwa muda mpaka pale atakapomruhusu tena “kwa sasa naishi kwa amani sana, mana nimepumzika na matusiya kwenye mitandao sitaoni tena.sijui mume wangu aliona nini mpaka aliamua kuniambia  mpaka atakaponiruhusu kurudi tena.”

Shamsa Ford na chid mapenzi ni moja ya couple ya watu maarufu walioweza kufunga ndoa na kudumu bila kuwa na skendo wala maneno ya hapa na pale kuhusu ndoa yao, ilhali inafika muda mpaka Shamsa anatumia muda wake kuwashauri wanawake wengien kuingiakatika ndoa na jinsi ya kuishi na mume vizuri.

Madhaifu mengi ya wasanii yamekuwa yakionekana kupitia mitandoa na wamekuwa wakikumbana na matusi mengi katika mitandao hiyo.Muda mwingine kwa kujua au kutokujua mashabki hujikuta wakimu-attack msanii na kumtukana bila kujua sababu ya vitu vinavyotokea.

Shamsa Azidi Kuwakaosoa Wanawake Wapenda Ela.

Msanii wa filamu za bongo nchi Shamsa Ford ameendelea kula sahani moja na wanawake wenzie ambao wamekuwa wakipenda kuolewa na wanaume wenye ela bila kujali kuwa maisha siku zote yanatafutwa.hivi karibuni  Shamsa Ford aliandika caption ya kumpongeza msanii mwenzie wa kike Shiloleh kwa kuamua kufunga ndoa na mwanaume wake ambae watu walijua hawezi kufunga nae ndoa kutokana na wadhifa mdogo aliokuwa nao mwanaume huyo.

Katika pongezi zake Shamsa Ford hakusita kuwaambia watu hasa wanawake wenzie kuwa ndoa ni uvumilivu na sio kutaka kuolewa na mwanaume mwenye ela bila kujua pa kuzitafuta.Hata hivvo Shamsa alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kusubirI kupewa kila kitu na mwanaume.

Akiongea tena na GPL hivi karibuni, Shamsa Ford anasema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakijisahau kuwa sasa hivi maisha yamebadilika , kikubwa ni kuangalia jinsi gani mwanaume uliyenae anakupenda na amekuwa na msimamo na wewe na sio kuwaza kuwa mwanaume mzuri katika maisha ni yule mwenye ela.

Wanawake wengi wamekuwa wanafikiria vibaya kuwa wao wanapaswa kuolewa na wanaume wenye hela tu, na uwezo mkubwa wa kifedha lakini kumbe sio kweli,kikubwa ni kuangalia mwanaume uliyenae anakupenda na amekuwa na msimamao na mapenzi na wewe sio fedha. Alisema Shamsa Ford

Shamsa Ford aliolewa na mwanaume aliyenae sasa hivi mwaka huu , mwanaume ambae ni mfanya biashara wa nguo jijini na Shamsa amekuwa kipaumbele katika kumsaidia mwanaume wake katika biashara hiyo.

Shamsa Ford Awatolea Povu Waliomchamba Baada ya Kusema Uwoya Mzuri Kuliko Wanawake Wote Bongo movie

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewatolea povu mashabiki wote wanaomsema vibaya baada ya kusema kuwa Irene Uwoya ndiye mwanamke mzuri kuliko wanawake wote kwenye tasnia ya Bongo movie.

Siku ya Jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo movie Irene Uwoya kama kawaida mastaa wenzake wengi walimtumia salami za kumtakia kheri mmoja kati ya watu hao ni rafiki yake Shamsa Ford.

Shamsa aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kumwagia sifa kibao kuwa ni mzuri kuliko wanawake wengine wa Bongo movie, baada ya kusema hivyo mashabiki walimjia juu kwa maneno na mateso.

Shamsa alishindwa kuvumilia maneno hayo na kuwatolea povu hili:

Yani Jana kusema huyu mwanamke ni mzuri kuliko wanawake wote wa Bongo movie imekuwa shida. Yaani mpaka mnanitumia msg za matusi? Binadamu nyie ni watu wa ajabu aisee….huo ndio ukweli mbishe mkatae kwa upande wangu na ninyi wote mnakubali moyoni machoni mnakataa huyo ndio mzuri. Hana kasolo hata moja kea vitu vya muonekano. Amejaaliwa na mwenyezi Mungu kuanzia juu mpaka chini. Mimi huwa nalionaga kama jini akipita lazima ustuke. Wanawake kusifiana ni ngumu lakini mimi huwa siwezi kuacha kumsifia mtu. Narudia tena Irene ni mwanamke mzuri na mwenye mvuto kuliko wanawake wote wa Bongo movie”.

Baada ya kusema hayo watu walizidi kumjia juu Shamsa huku wakitaja wasanii wengine wa Bongo movie kama Wema, Jennifer Kyaka, Wolper, na kudai kuwa ni wazuri kuliko Irene.

Shamsa Awaasa Wanawake Waolewe Waache Kusubiria Wanaume Matajiri, Waige Mfano Wa Shilole

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kuwashauri wanawake waige mfano wa Shilole na kuolewa badala ya kukaa na kusubiri kuolewa na mwanaume tajiri.

Shamsa aliongea hayo alipokuwa anampa hongera Shilole baada ya ndoa yake na Uchebe. Shilole aliolewa wiki iliyopita na Uchebe ambaye ni fundi magari na kusababisha watu wengi kumsema.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa Ford alifunguka yafuatayo:

Hongera mamy umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza mwenyezi Mungu cha muhimu uwe mke bora wa Kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana Inshallah mtazikana karibu kwenye chama mama…Sasa nyie mnaosubiri matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubiri sana mpaka uso utaota sugu uzuri na ustar una mwisho wake itafika kipindi hata nzi hatokusogelea”.

Ingawa Shamsa hakutaja majina lakini dongo like aliliekekeza kwa wasanii wenzake ambao hawataki wanaume kuolewa na wanaume wa kawaida bali nia yao ni kupata wanaume wenye pesa lakini wanaume wale wenyewe wanawaita madanga wengi wako wameoa tayari na wanafamilia zao

 

Shamsa Ford Ampa Darasa La Ndoa Shiloleh

Mwanadada mrembo anaejihususha na bongo movies lakini pia ni mjasiriamali maarufu baada ya kuijingiza huko baada ya kuolewa na mpenzi wake Chid Mapenzi, amefunguka na kumsahuri mwanadada Zuwena maaarufu kama Shiloleh jina la kisanii juu ya maisha ya ndoa aliyoyaanza hivi karibuni.

Shiloleh amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu kidogo anaejuliakana kwa jian la Uchebe wiki iliyopita ndoa ambayo ili-trend sana katika mitandao baada ya kuwashangaza watu wengi amabo walihisi kuwa ndoa hiyo haitaweza kufungwa kutokana na migogoro iliyojitokeza hivi karibuni baada ya kuvuja picha zikimuonyesha mwanadada huyo akiwa na mpenzi wake wa zamani ambae pia ni msanii mwenzie Nuh Mziwanda .

Shamsa Ford  akitumia uzoefu wa ndioa yake aliyofunga mapema mwaka huu amemshauri Shiloleh  kutulia katika ndoa yake  na kuachana na sifa za kuwa maarufu kutokana na usanii wake bali atulie ili kuweza kufaidi matunda ya ndoa yake.

Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa ameamua kufunguka kuhusu swala ilo na kumpongeza kwa uamuzi aliouchukua

Hongera sana mama umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu cha muhimi uwe mke bora wa kitanzania kwa mumeo na ustar uache pembeni ‘mumuweke Mungu mbele yenu,uvumulivu na kuheshimiana Inshallah mtazikana,karibu kwenye chama mama …sasa nyie mnaosubiri matajiri wawaoe wakati matajiri wana wake zao  mtasubiri sana mpaka uso  uote sugu,uzuri  na ustar uana mwisho wake  itafika muda hata inzi hakusogelei. HONGERA MAMA

Alichokiandika shamsa ford katika ukurasa wake wa instagram

Mwisho huu w mwaka umekuwa mwaka mzuri kwa baadhi ya wasanii ambao wameamua kuachana na ukapela na kujiingiza katika maswala ya familia.PONGEZI NYINGI KWA SHILOLEH NA MUME WAKE.

 

Muda Wa Kanumba Kuondoka Duniani Ulikuwa Umefika- Shamsa Ford

Msanii wa filamu za Bongo fleva, Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa muda wa Kanumba kuishi duniani ulikuwa umefika ndio maana akatangulia mbele ya haki kwa wakati ule.

Siku ya Jana Elizabeth Michael almaarufu kwa jina lake la uigizaji kama Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika mahakama kuu ya Tanzania baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukisudia mpenzi wake na muigizaji mwenzake Steven Kanumba miaka mitano iliyopita.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa watu mbalimbali wakiwemo mastaa wamejitokeza kutoa michango yao ya hali na mali huku kila mmoja akionekana kusikitishwa na kitendo hiko.

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford pia amefunguka kwenye mahojiano na Millard Ayo na kueleza yaliyo moyoni mwake na kusisitiza kuwa Kanumba  alipoteza maisha ile siku kwa sababu ilikuwa imeshaandikwa iwe hivyo.

Kusema ukweli baada ya kusikia Lulu amefungwa miaka miwili jela nilijisikia vibaya sana kwa sababu naamini atakuwa katika wakati mgumu sana huko alipo lakini mwisho wa ukiangalia kila linalotokea kwa mwanadamu basi ujue mwanyezi Mungu amelipanga kwaiyo kuna njia sahihi ambayo Mungu anampeleka na ndio maana anampitisha kote huko kwa cha msingi kwake ni kuwa jasiri lakini kiukweli nilimuonea huruma sana ukiangalia yule bado ni biinti mdogo sana mwenye ndoto nyingi na ukiangalia muda katika maisha ni kila kitu”.

Lakini pia Shamsa alimuongelea Kanumba ambaye anaaminika kuwa ameacha pengo kubwa sana katika tasnia hii ya filamu na kudai kuwa anaamini kuwa Kanumba alikufa siku ile kwa sababu siku yake ilikuwa imefika kwaiyo watu wasipende sana kumuhukumu mtu kilichobaki ni kumuombea tu mwenzetu ambaye tuko naye duniani.

 

 

Haya Ndio Majuto Ya Shamsa Ford Katika Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai moja ya jambo analijutia maisha yake yote ni kitendo cha kukataa kusoma shule pale alipokuwa mdogo.

Shamsa Ford alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amedai kuwa anaumia kila akikumbuka nafasi aliyochezea alipokuwa mdogo kwani Mama yake alimbembeleza sana arudi shule akasome ndio aendelee na kuigiza;

Mama yangu alinikazania sana nisome kwa bidii wakati nipo shule ila nilipomaliza form six nikaona inatosha counter book nikaona zito ila scipt nikaona nyepesi…Natamani ningerudisha siku nyuma ningesoma kwa bidii hata kama ningetaka kuwa muigizaji basi ningekuwa muigizaji wa kimataifa with knowledge. Moja kati ya vitu vikubwa vinavyoturudisha nyuma bongo movie ni elimu. Mtu aliuesoma na asiyesoma ni vitu viwili tofauti sasa sisi wengi wetu hatuna elimu kabisa wengi wao ni darasa la 7,5,2,6 wengine ndio kabisaa alijifunza kusoma na kuandika tu. Nakumbuka mwaka juzi nilimuona msanii wa Nigeria Genevieve Nnaji akiojiwa CNN nikatamani niwe mimi. Wenzetu wamesoma ndio maana wametupita vitu vingi sana”.

Shamsa aliendelea kufunguka mazito kuhusiana na hali halisi ilivyo kwa Bongo movie na filamu zao kwa ujumla;

Yaani huku Bongo movie kumejaa umbea, chuki, roho mbaya, ushirikina. Mtu hata kama hujawahi kumkosea lakini akikaa na watu wanaokuchukia atakusema vibaya, lakini pia ukijitenga useme uishi kivyako utaambiwa unaringa na vikao vya kusengenywa utawekewa juu! Yote hayo ni kwa sababu ya ukosef wa Elimu ndio maana watu wanaweza kupoteza muda kwa vitu vya kijinga. Mwenyezi Mungu nisaidie nimsomeshe mwanangu kwa nguvu zangu zote aje awe mtu wa muhimu kwenye hii dunia na sio Bongo Movie”.

Siku za hivi karibuni tasnia nzima ya bongo mo vie imekuwa ikiandamwa na visa vya kufeli katika kuburudisha huku watu wengi wakithubutu hata kusema kuwa kwa sasa Bongo movie imekufa kabisa.

Shamsa Ford Awatolea Povu Mashabiki

Msanii wa bongo movies Shamsa Ford  ameonyesha kukasirika na kuwatolea mapovu mashabiki wake ambao wamekuwa wakimsema vibaya kuhusu yeye kukaa dukani kwa mume wake nakuwa anauza duka badala ya kuajiri kijana.

katika ukurasa wake wa instagram mashabiki wengi wamekuwa wakitoa maoni yao huku wakimsema kuwa yeye ni mbahili kwa sababau tangu ameolewa amekuwa akikaa dukani kwenye duka la mumewe badala ya kufanya shughuli nyingine  huku wakimsahuri atafute kijana wa kazi.

Hata hivyo Shamsa alionekana kukera na baadhi ya maoni hayo ya washabiki na kuwaomba wasimpangie maisha na hata hivyo anayo haki ya kukaa katika duka analomiliki mume wake kwa sababu ni la kwake pia,

Unajua kuna watu wananishangaza sana , wananiambia si nitafute  mtu akae dukani halafu mimi nifanye nini sasa muda huo?alihoji shamsa ford kwa mashabiki wanaokuwa wanamzonga kila siku katika mitandao.

Hata hivyo Shamsa aliongezea na kusema kuwa wengi wa wasanii hasa wakike wamekuwa na tabia ya kuolewa na kukaa tu nyumbani wakitaka kuletewa kila kitu kutoka kwa wanaume lakini yeye hajazoea kitu hicho kwaio hawezi kabisa kukaa nyumbani kama wao wanavyotaka

mastaa wengi  wa kike wamezoea kulala , sasa mimi siwezi unapopata  fursa ni lazima uitumie ipasavyo.

Msanii huyo wa kike ShamsaFford alifunga ndoa na mumewe Chid Mapenzi mwaka uliopita, Chid Mapenzi ni moja ya wafanyabiashara wakubwa sana wa nguo jijini Dar Es Salam akiwavalisha wasanii wengi wa muziki na filamu pia hata watu maarufu.

Hata hivyo baada ya kuolewa na mwanaume huyo Shamsa Ford alijikita zaidi kumsaidia mumewe katika kazi ya kukaa dukani na kuhudumia wateja lakini baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimjia juu na kutaka msanii huyo atafute kijana wa kuuza dukani na aachane na kazi hiyo ya kuuza duka kitu ambacho Shamsa mwenyewe amekataaa na kusema hawezi kukaa nyumnbani ilhali duka la mumewe ni la kwake pia.

Imekuwa ni kitu cha kawaidia kwa baadhi ya mashabiki kuwa wanatoa maoni juu wa wasanii wao kuhusu maisha yao binafsi badala kujikita zaidi katika sanaa.

Shamsa Ford afunguka kuhusu skendo ya ujauzito

Msanii wa Bongo Movies, mrembo na ambae anafanya vizuri katika tasnia hii ya filamu  kwa muda mrefu ,mwanadada Shamsa Ford amefunguka na kusema ukweli kuhusu tetesi zinazizidi kusambaa mitandaoni kuhusu yeye kuwa mjamzito , Shamsa ambae  amefunga ndoa hivi karibuni ikiwa ni kama  mwaka tu umepita  tangu ndoa yao na mumuwe   Chid Mapenzi  ameamua kusema ukweli  na kukanusha kuhusu tetesi hizo,Shamsa amekanusha kabisa taarifa izo na kusema kuwa hayo ni maneno ya watu tu katika mitandao wakitaka kumzushia kuhusu taarifa hizo.

“am not pregnant, mimi kweli kabisa sina  mimba” aliongea Shamsa  huku akicheka.

Kwa muda sasa kumekuwa na  tetesi mitandaoni huku watu wakisema kuwa Shamsa  ni mjamzito ,lakini Shamsa anakataa na kusema kuwa labda kwa sababu amekuwa akionekana mnene sana kwa muda sasa ndio maana watu wameanza kuhisi kuwa yeye ni mjazito,lakini unene wake ni kwasababu amejiachia na kula sana.

Hata hivyo Shamsa anaongezea kuwa inawezekana watu wanashawishika kuwa yeye ni mjamzito kutokana na picha zake alizopost hivi karibuni ambapo moja inamuonyesha amevimba uso kidogo na huku nyingine ikimuonesha akiwa  na mtoto wake wa kwanza wa kiume ikiwa na caption ya kusema anatamani kupata mtoto mwingine maana huyo aliyenae ameshakuwa.

Shamsa anaongezea kwa kusema kuwa watu wengi wamezoea kuwa mtu akishaolewa basi kinachofuata ni mimba na mtoto,lakini kwa upande wao bado hawajapanga kuzaa kwa sasa bado wanatafuta maisha mungu akujalia basi watapata mtoto “mimba ni jambo la kheri,kwanini nifiche,..nikipata basi Inshallah ”

Alipoendelea kuulizwa na mtangazaji wa kipindi cha eNews cha EATV ,kwamba kwanini watu wanasema wanamuona hadi anaenda kliniki Shamsa anasema hajawahi kwenda kliniki na ikitokea amepata mimba hawezi kufika  na kwasababu mimba inakuwa basi tumbo haliwezi kufichika.

Shamsa ameolewa ni mwaka mmoja  umepita tangu akiwa amefunga ndoa yake na kwa sasa anamtoto mmoja wa kiume anaeitwa Terry, na kama kweli Shamsa ni mjamzito basi tunamtakia afya njema yeye na mtoto wake.

Shamsa Ford atoa onyo kali kwa vijana wanaofugwa na kinamama wanaowazidi umri

Muigizaji wa filamu za Bongo Shamsa Ford amewasuta vijana ambao wanaingia kwenye mahusiano na kinamama wanaowazidi umri.

Staa huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hio kwani anasema vijana wanakua wazembe na kuishi kutegemea kulishwa na kufanyiwa kila kitu bila ya wao kutoa jasho.

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki. Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah,” Shamsa Ford aliandika kwa mtandao wa Instagram.

 

Shamsa Ford aeleza kwanini hawezi ruhusu mumewe kumuongezea mke mwenza

Muigizaji wa filamu za Bongo Shamsa Ford amefunguka kuhusu kinyongo alichonacho ikikuja kwa swala la mumewe kuoa mke wa pili.

Akiongea kwenye FNL, Shamsa alisema kwamba hataweza kukubali mume wake kuongeza mke wa pili kama hataweza kumpa sababu maalum.

Chidi Mapenzi na Shamsa Ford

Mrembo huyo aliyekua kwenye uhusiano wa kimapenzi na Nay wa Mitego kabla ya kuolewa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ alieleza kuwa anaamini anamtosheleza mume wake kwa kila kitu na kuwa Rashidi hana sababu ya kutaka kuoa mke wa pili.

“Wivu nilionao siwezi kukubali kuongezewa mke wa pili hata mume wangu (Rashid) anajua kwa sababu yeye mwenyewe ana wivu sana na mimi. Ukweli kabisa nahisi ninaweza hata kufa kwa presha nikiongezewa mke wa pili. Inabidi kwanza kabisa kabla ya kuniomba aoe, anatakiwa anipe sababu za msingi kwannii anaamua kufanya hivyo na ikiwa sababu zinamashiko na mimi nikazielewa basi nitamruhusu kwa kuwa dini inasema hivyo kwa sababu pia ni ibada. Lakini kama hazina msingi siwezi kukubali kwa sababu naamini namtosheleza kwa kila mtu na sina kasoro yoyote,” Shamsa alisema.

 

 

Malkia wa filamu Shamsa Ford amaibisha mpenzi wake wa kitambo – Nay wa Mitego

Rapper Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameaibishwa hadhani na Shamsa Ford – mpenzi wake wa kitambo.

Apo awali ilisemekana kuwa Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapper Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20 2017.

Nay wa Mitego ndo alisemekana kuwa chanzo cha habari kuwa mpezi wake wa kitambo Shamsa Ford atakuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’

Shamsa Ford na Nay wa Mitego walipokua bado wanapendana

Malkia huyo wa filamu hata hivyo amemkana Nay wa Mitego na kumaibisha hadharani. Akiongea na Bongo 5, Shamsa Ford alisema kuwa hajui chochote kuhusu show hiyo kwasababu Nay wa Mitego hajawai mwambia lolote kuhusu show hilo.

“Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live. Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote,”alisema Shamsa Ford.