Shamsa Alezea Anavyokerwa na Wanaotukana Katika Mitandao.

MwanadadaSshamsa Ford amefunguka na kusema kuwa anawashanga sana wanaoingia katika mitandao ya kijamii na kuanza kutukana wakati wangeweza kufanya mambo ya maana kwa huo muda ambao wamekuwa wakitukana na kufanya yasiyowahusu.

Shamsa anasemakuwa mara nyingine huwa naona ni bora hata kutoka katika mitandao ya kijamii ili tu asiweze kukutana na maneno ya watu lakini ndio hivyo kazi zao zinawataka kuwa hivyo muda wote lakini njia anayotumia yeye  ni kuwa-block tu.

mimi kwakweli sipendi mtu anaetukana katika mitandao ya kijamii,watanzania tulivyokuwa sharp katika mitandao ya kijamii kutukana tungekuwa tunatumia huo muda kufanya vitu vya maana tungekuwa na maendeleo sana,kuna muda mwingine unaweza kusema ni bora hata ningetoka tu katika mitandao, lakini ndo hivyo hatuwezi lakini sasa unaona kama kikitokea kama icho basi  unam-block tu.

 

Shamsa Ford Ahaidi Kujituliza Kwenye Ndoa

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka kuhusu mipango yake ya kujituliza kama mwanamke hasa kwenye ndoa yake.

Shamsa ameweka wazi kuwa mambo yasiyo sahihi amefanya sana, lakini kwa sasa umefika wakati wa yeye kutulizana hasa kwenye ndoa .

Kwenye mahojiano aliyefanya na gazeti la Amani, Shamsa alisema kuwa, kutokana na kubadilika kitabia anatamani yeye na mume wake wawe mfano imara kabisa kwa jamii yaani waishi muda mrefu sana mpaka Mungu atakapowatenganisha.

Maisha siku hizi ni mafupi sana, ni muhimu mtu siku ukiondoka uache alama nzuri na ili hilo lifanikiwe ni muhimu kutulizana, jambo ambalo nimeamua kulifanya kwa sasa”.

Wasanii wengi wamekuwa wakiongelea kutulia na kuomba dua  hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

Shamsa Ford Atoa Povu Zito Kwa Watoa Misaada

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewatolea povu zito watu wote ambao wanatoa misaada kwa watu kisha kwenda kuwatangaza hapo baadae.

Shamsa Ford alimwaga povu hilo Kwenye ukuraaa wake wa Instagram kuashiria kukerwa na jambo hilo ambapo ameweka wazi kuwa ukiombwa unatangazwa mpaka unajuta kuomba msaada:

kila mtu anapenda kusaidiwa lakini kuna misaada mingine mpaka mtu unajuta kwann umesaidiwa. utafanywa tangazo kila sehemu,utasemwa na kusimangwa kila sehemu,utafanywa mtumwa,hata kama akikuudhi itabidi tu umchekee, Huyo mtoa msaada atajiona Mungu MTU kwamba bila YEYE maisha hayaendi, hapo bado hajakubania sehemu utasema yeye ndo mtoa RIZIKI. Misaada ya aina hiyo ni bora ikupite ufe na shida zako tu maana itafika sehemu utamsujudu yeye na kumsahau Mwenyezi Mungu ..”.

Shamsa hajamtaja mlengwa wa Dongo hilo lakini nina uhakika lililomuhusu limempata gizani.

Shamsa Ford Ajibu Tuhuma Za Kumfilisi Chidi Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amejibu tuhuma ambazo amekuwa akitupiwa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amemfilisi mume wake Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mfanyabiashara maarufu sana wa nguo na viatu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuwavalisha mastaa kibao ikiwemo Diamond na wengineo.

Lakini tangu Chidi afunge ndoa na Shamsa ameonekana kufulia kupita kiasi na haishi maisha aliyokuwa anaishi mwanzoni ambapo alikuwa anaonekana na duka kubwa na magari mazuri jambo lilipelekea watu wengi kumtuhumu Shamsa kamfilisi Chidi tangu amuoe.

Kwenye Interview na Enews ya EATV Shamsa amekana tetesi hizo na kuweka wazi kuwa maisha aliyokuwa anaishi Chidi siku za nyuma yalikuwa ni ya anasa na ujana mtupu hivyo walivyofunga ndoa alimsihi abadilike ili waweze kuweka akiba na hata kumsaidia kupunguza marafiki wasiokuwa na maana.

Lakini kuhusu duka kufilisika, Shamsa ameweka wazi kuwa walikuwa duka kubwa na la kifahari lakini walikuwa hawaingizi faida kubwa kwa sababu kodi ilikuwa kubwa hivyo akamshawishi mume wake wahamie Kwenye duka Dogo ili waweze kumudu kodi.

Lakini pia Shamsa ameweka wazi kuwa yeye sio mtu wa kupenda Show off kwa watu aonekane anaishi maisha ya kifahari ili Apate umaarufu Hapana anaishi kwa uahalisia wake kwa kile alichokuwa nacho kiukweli kabisa.

Mwanaume Kuchepuka Ndivyo Walivyoumbwa na Mungu: Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo fleva Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa mwanaume yoyote lazima achiti/ achepuke na wanawake wengine kwa kuwa ndivyo walivyoumbwa na Mungu.

Shamsa amesisitiza na kusema hakuna mwanaume ambaye hachepuki kila mwanaume lazima achepuke  na hakuna mwanaume ambaye anaweza kuwa na mwanamke mmoja tu.

Kupitia mitandao ya kijamii Shamsa ameandika maneno haya:

Mwanaume kucheat ndivyo alivyoumbwa na Mungu, hamna mwanaume ambaye hacheat Hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja. Bill Clinton alishawahi kuwa na kesi alicheat, Jay Z alikiri amemcheat Beyonce na uzuri wake wote na ustaa wake wote ule”.

Siku za nyuma kidogo mume wa Shamsa Chidi Mapenzi alishawahi kukumbwa na skendo ya kuchepuka na mwanamke mwingine mara moja Shamsa aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuachana naye wala hatokuja kumuacha mume wake kisa ana wanawake wa pembeni.

 

 

“Bongo Movie Wengi Hatupendani Hasa Wanawake”- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa wasanii wengi wa Bongo movie wanachukiana na kusababisha tasnia hiyo kushuka kila siku.

Shamsa amepasua chuki walionayo wasanii wengi kwa Wenzao hasa wanawake inasababisha kukoseshana madili ambayo yangeweza kuitangaza nchi kwa ujumla.

Kwenye mahojiano na Bongo Movie Shamsa amefunguka haya zaidi:

Ni kweli kwa sababu Bongo Movie wengi hatupendani, hasa wanawake hatupendi kuwa mabalozi wazuri kwa wanawake wengine, kwa hiyo mwisho wa siku zile chuki zinafanya isiendelee.

Lets say mtu anatoka nje anataka kufanya kazi na Shamsa, unaanza kuponda usifanye naye kazi, mwisho wa siku dili linaondoka wakati ngingefanya ningewakilisha wasanii wa Bongo na pia Tanzania, so chuki inasababisha kushuka kwa Bongo Movie”.

Kwa muda mrefu wasanii mbali mbali wa Bongo movie wamekuwa wakinyosheana vidole kuhusu nini hasa kilichosababisha kuzorota kwa tasnia hiyo kuliko kutafuta njia mbadala za kuokoa tasnia hiyo.

Harmonize Aliniumiza Alipoweka Jina la Mume Wangu:Shamsa

Mwanadada Shamsa Ford kutoka bongo movies amefunguka kwa mara ya kwanza akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kitendo cha Harmonize kuweka jina la mume wake katika list ya wanaume aliwahi kutembea nao Jackiline Wolper ilimuumiza sana kwa sababu ni mtu anaempenda.

Shamsa Ford amesema hayo siku ya uzinduzi wa filamu ya mama ya Aunty Ezekiel wikiendi iliyopita na kusema kuwa hata kama asingekuwa mke wake lakini swala  hilo lililmuumiza sana kwa sababu ni mambo yaliyopita tayari.

Ni lazima uumie kama binadamu na kwa sababu ni mtu unaempenda,lazima uumie tu na sio kwa mume tu hata kwa mtu ambae ni part ya maisha yako utaumia.

Siku chache zilizopita kulitokea mtafaruko kati ya harmonize  na aliyewahi kuwa mpenzi wake jackline wolper na ambapo harmonize kwa kutaka kumuhaibisha jackline aliamua kutoa idadi na majina ya wanaume aliwahi kutoka nao jacky kimapenzi ambapo kati ya majina hayo pia kulikuwepo jina la Chid Mapenzi ambae ni mume wa ndoa wa Shamsa Ford.

Shamsa Ford Amjia Juu Harmonize Kwa Kuingilia Ndoa Yake

Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa wa Shamsa Ford kwaiyo baada ya kusikia mumewe katajwa Kwenye orodha hiyo alishindwa kujizuia kwani alikuja juu bibaya mnoo na kumtaka Harmonize amkome mumewe na asimuingize Kwenye ugomvi wao.

Shamsa alienda kukomenti maneno haya Kwenye posti ya Harmonize:

Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu pls nisingependa kuona jina la mume wangu Kwenye huo ujinga wenu. Chidi kwenu anaweza akawa mshkaji kwangu mimi ni mume kulikuwa hakuna haja ya wewe kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tusichukuliane Poa”.

 

Shamsa Ford Awataka Mastaa Wenzake Waache Kuchukuliana Wanaume

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewajia juu mastaa wenzake kwa vitendo chao vya kuchukuliana mabwana/ Waume bila kujali jinsi vitendo hivyo vitakavyoumiza wengine.

Shamsa Ford amefunguka na kudai kuwa yeye binafsi hakuna kitu anachokiheshimu kama ndoa ya mtu au Mahusiano ya mtu mwingine kwaiyo hawezi kuingilia hivyo lakini anashangaa watu wanaokosa utu na Kuiba mabwana wa watu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Amani bila kuwataja majina, Shamsa alisema kuna baadhi ya mastaa wanajua wazi mwanaume anayemtongoza ni wa rafiki yake lakini akijua tu ana fedha yuko radhi hata ajifanye kama hamjui huyo rafiki yake ili mradi tu atembee naye.

Mimi jamani niko tofauti kabisa siwezi mwanaume wa rafiki yangu akanitongoza nikakubali ninaheshimu hilo lakini wengine wako radhi wakukane ili mradi tu apate fedha”.

Lakini pia Shamsa ameweka wazi kuwa yeye hana wasi wasi wa kuibiwa mume wake Chiddi Mapenzi kwani anamuamini mume wake kuwa ni mwaminifu.

Lakini pia siku za nyuma Shamsa alikwisha weka wazi kuwa hawezi kumuacha mume wake kwa sababu ya michepuko baada ya kujulikana alikuwa anachepuka.

 

Diamond Endelea Kuwatumia Hao Wanawake Maana Hawajielewi Lakini Kumbuka Kutumia Kondomu- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford Amefunguka na kudai kuwa sio kweli kwamba Diamond anawadhalilisha wanawake ambao wanatoka nao kimapenzi kwa kusambaza video zao mtandaoni.

Diamond alizua gumzo hili siku ya jana bada ya video zake kusambaa mtandaoni akiwa na Hamisa Mobetto chumbani wakikumbatiana na wakati huo huo akiwa na binti wa kizungu wakiwa pamoja chumbani pia Wakila denda na uchafu mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Shamsa aliulizwa nini maoni yake juu ya jambo hilo na alifunguka na kumtaka Diamond aendelee kutoka na wanawake tofauti tofauti kwa kuwa hawajitambui huku amtahadharisha kutumia kondom ili kuepuka magonjwa na zinaa.

Mwanaume hawezi kukufanya mwanamke ikawa chombo cha starehe inategemea mwenyewe na akili yako kama unataka kuchezewa utachezewa kama unataka kuwa mwanamke wa muhimu kwake utakuwa inategemea mwenyewe unajiweka wapi kwaiyo mimi siwezi kumlaumu Diamond kama anawatumia maana wenyewe ndio wameweka mazingira hayo kwa nini asitumie nafasi? Ila mimi namshauri Diamond awale tu hao wasichana ila akumbuke kutumia kondomu maana magonjwa mengi”.

 

 

Shamsa Ford Atishia Kumpeleka Baba Watoto Wake Kwa Makonda

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefungukia mipango yake ya kumbruza kwa Makonda Ex wake ambaye amezaa naye mtoto mmoja.

Shamsa ameweka wazi kuwa atampeleka mzazi mwenzie Dickson Matoke kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa ajili ya kudai haki ya kuhudumiwa mtoto wake.

Wiki iliyopita Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitangaza kuwa wamama wote waliotelekezwa na wanaume waliozaa nao waende ofisini kwake kwa ajili ya kuangalia msaada wa sheria watakaopata.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa sio kwamba hana uwezo wa kumhudumia mtoto wake lakini kuna wakati unaumia kuona baba wa mtoto yupo, anakula bata tu akiwa hajui hata kula ya mtoto wake inatoka wapi.

Dawa ya wanaume wa sampuli hii ni kuwapeleka tu kwa Makonda. Mimi watu watashangaa sana siku watakaponiona pale lakini ni kwa sababu wakati mwingine ukifikiria unajikuta unapatwa na hasira kuona mzazi yupo lakini kama hayupo vile”.

 

Mme Wangu Akioa Mke wa Pili Nadai Talaka:-Shamsa Ford

Mwanadada Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa endapo mme wake ataoa mke wa pili basi hiyo itakuwa ndio mwisho wa ndoa yake kwa sababu hawezi kuvumilia kuona mme wake anaenda kulala na mwanamke mwingine akijua kabisa kuwa leo sio zamu yake.

Akiongea na bongo 5 ,Shamsa anasema kuwa katika maisha yake ya ndoa na chid mapenzi hajawahi hata siku   moja kuingia katika mikiki miki na me wake zaidi ya kipindi ambacho mme wake alipata matatizo na kupeleka selo tu.

Labda kipindi kile mme wangu yuko ndani ndio kidogo nilipata tabu na nilisema niepeitia matatizo na niliandika post ya huzuni kidogo.lakini isjawahi kujutia ndoa yangu.

Namtaniaga nyumbanu siku zingine kuwa mme wangu oa basi mke mwingine , yeye ananiambiamaisha yangu tu me wapi, lakini hata kama dini inaruhusu kwakweli mimi nina wivu sana sitaweza kuvumilia najua kabisa leo sio zamu.na ikitokea siku ananiambia anataka kuoa mke wa pili nitamwambia tu talaka yangu na ndipo aoe mke wa pili.–Alifunguka Shamsa

Shamsa Ford:-Faiza Ally ni Mkurupukaji

Mwamamama Shamsa Ford amefunguka na kuongelea kuhusu swala lake kuongelea kuhusu madili ya makampuni mbalimbali ambayo yamekuwa yakienda kwa wasanii wa nje na sio kwa wazawa na mfano mzuri ni ile ya wiki iliyopita kuhusu Zari The Bossy alipokuja bongo na kusaini mkataba mkubwa huku wasnaii wakubwa  wa ndani wakiachwa.

Baada ya hayo Faiza alifunguka na kuongela lake lakini pia shamsa alifunguka na kuongea lake , sasa swali linakuja kuwa je wawili hao wanamahusiano gani mpaka kufikia hatua ya kukinzana katika mawazo hasa katika swala kama hilo.

mimi na faiza sio marafiki lakini nilimzoea kutokana na ukaribu wake na zama na mimi pia ni rafiki wa zamaradi, lakini pia nilikuwa naona anayoongea kuhusu single mothers kwa sababu hata mimi nilikuwa huko hivyo alikuwa akionge nina-feel kile anachoongea, lakini alipokuja kwenye hili niliona kawaida na kwa sababu nilishamzoea kuwa yeye ni mtu wa kukurupuka a, akikutupuka anaongea tu lolote analojisikia.

Sikutaka kumjibu kwa sababu pale uapoona mtu ameandika kitu kuhusu swala fulani basi liwe linahusu hisia zako lakini pia mimi ninapoandika basi niwe naheshimu hisa zako na zangu pia.kwaio haija haja ya kukosoa kwa sababu kila mtu na hisia zake.

Hatupaswi kutoleana amneno ambayo watu wanweza kuhisi labda tuna ugomvi , mimi ni mzazi na wewe ni mzazi kwaio inabidi tuheshimiane.-Alifunga shamsa alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari kutoka Ayo Tv.

Hakuna Mfanyabiashara Anaetaka Hasara Kisa Uzalendo-Shamsa Ford

Kulitokea maneno mengi sana hivi karibuni kuhusu mwanamama zari the bossy kutoka uganda kupat amkataba wa deal nono la kutangaza pampers za watoto huku katika mitandao ya kijamii watu walikuwa wakilalamika kwamba kwanini imekuwa hiyo wakati wasanii wengi wazawa wapo nchini, ina maana hakunanuzalendo wa hawa wazalishaji mpka kuchagua zari badala ya wasanii wengine wa kike .

Baada ya hayo yote , shamsa nae amefunguka na kutoa yake ya moyoni kuhusu lawama hizo ambazo zimekuwa nyingi katika mitandao ya kijamii kuhusu swala hilo.shamsa ansema kuwa kunavigezo na masharti mengi sana kampuni huyazingatia mpka kumchagua mtu kuwa balozi wa bidhaa zao.

morning my pipo naona watu wanalalamika kwa nini madeal yanapita tu kwa mastar wa bongo na wageni ndio wanapata nafasi hiyo.mimi nina mtazamao tofauti kabisa kuhusu hilo .kabla ya kumtafuta mchawi nani ni bora kwanza ujikague mwenyewe.ninaamini kil biashara ina conditions zake na kila biashara inahitaji faida.hakuna mfanya biashara atakaekubali kumchukua msanii wa bongo alafu baadae akubali kupata hasara.tusipinge ukweli kuwa sisi wenyewe tumevunja uaminifu na wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu wenyewe.tunapozungumzia  kuwa ambassador unazungumzia kubeba brand ya mtu, sasa nani anataka kuchafua brand yake kubebwa na mtu asieleweka, swala sio kujulikana tu swala ni kwamba unajulikana vipiwatu wanakutambua kwa lipi kisha akili kichwani mwako, ni vizuri kama tumeumia hivyo tujipange na kufukia mashimo  ili na sisi tuheshimike na  kuthaminika …niliowakera mnisamehe tu lakini inabidi tuishi kwa kuambiana.-Aliandika Shamsa Ford katika ukurasa wake.

 

Shamsa Ford Ahofia Kuachika ‘Mapenzini’ Kama Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Shamsa Ford amefunguka kuhusiana na mambo ya mapenzi na kuweka wazi uoga wake inapokuja suala la kuachwa.

Shamsa Ford Amekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri kwa wanawake wengine kuhusu masuala ya kudumu katika ndoa na ni juzi tu aliwaasa mastaa wenzake kujitahidi na kutoingiza ustaa Kwenye Mahusiano n ndoa zao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ambao ambao ameonyesha hofu yake kubwa endapo atakuja kuachana na mume wake mfanyabiashara maarufu Chiddi Mapenzi aliyefunga naye ndoa mwaka juzi.

Shamsa ameonyesha uoga wake lakini ameweka wazi anaogopa ua jeusi ambalo liliwekwa na Zari alipomtosa Diamond ili kuashiria penzi lililokauka au kuishiwa.

Mwenyezi Mungu niepushie na hili UA na huu uzee nitaenda wapi.. inatisha khaaaa”.

 

Zari aliweka rekodi na kulipa umaarufu UA hilo jeusi baada ya kulitumia kuvunja Mahusiano Yake na Diamond siku ya Valentine’s Day mapema mwaka huu.

 

Shamsa Atoa Siri ya Wasichana Kushindwa kudumu Kwenye Mahusiano.

Msanii wa bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kuweka wazi  sababu za wadada wengi wa mjini kushindwa kutokuolewa  wala kutokudumu katika mahusiano yao.shamsa anasema kuwa wadada wengi hasa wasanii wamekuwa na tabia ya kuingiza umaarufu wao katika mahusiano kitu kinachofanya washindwe kudumu katika mahusiano yao.

Nimegundua mahusiano mengi ya watu aarufu hayadumu kwa sababu  wengi wanataka ustar  hadi kwenye mahusiano , hata mtu wa kawaida akiwa katika mahusiano na msanii pia inakuwa kazi kwa mahusiano yao kudumu kwa sababu hiyo.

Hasa kwa wanawake tunaamini kabisa ustar ndio kila kitu katika mahusiano  na mwanaume , sijui ni kwa sababu hatuna elimu ya ustar au vipi, maana ingekuwa u-star shida Beyonce na Jay -Z wasingekuwa wamedumu katika ndoa maana hawa ndo ma-star wa Dunia.

Shamsa ni moja ya wasanii wachache wa kike walioweza kudumu katika ndo yao na mume wake tangu mwaka 2016 alipofunga ndoa.