Sista Fey Amtolea Uvivu Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie Faidha Omary maarufu kama Sista Fey amemjia juu msanii mwenzake Steve Nyerere na kumuita mnafiki huku akimtuhumu kwa kusababisha mpaka yeye kukamatwa na kuwekwa ndani.

Sista Fey alikamatwa wiki chache zilizopita kutokana na kudaiwa kuanika maudhui mabaya kwenye mitandao ya kijamii lakini hivi sasa ameibuka na kumnyooshea kidole Steve Nyerere kama mtu aliyesababisha hayo yote.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Sista Fey alimwaga povu hili;

Hapa Tanzania hakuna msanii mnafiki kama Steve Nyerere kwani anakusema asubuhi jioni anajifanya rafiki yako ila namuombe kwa Mungu aendelee na unafiki wake na hivyo anavyojifanya mwema kumbe mnafiki tu”.

Steve anajifanya kimbele mbele zaidi ya viongozi wetu halafu mimi kama Fey najua hakuna nilichokukosea ila roho yako mbaya uliyotengeneza kwanini mimi nionekane sana Instagram kuliko wewe itakugharimu kwani kila mwanaadamu ana karama yake wewe karama yako kuiga sauti za viongozi wewe sio kiongozi”.

 

CCM ni Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.;-Steve Nyerere

Msanii Steve Nyerere amefunguka na kusema kwa ufupi kile kilichowafnaya wasanii wakaweza kuktana na  mh polepole katika ukumbi wa serena hotel siku ya jana.msanii huyu anasema kuwa lengo kubwa ilikuwa ni kuajdili changamoto za sanaa hasa kuangalia jinsi gani wasanii wanaweza kunufaika na kile wanachokifanya.

Steve anasema kuwa kazi zimekuwa zikiwafikia mshabiki ambao ni walengwa lakini hakuna manufaa zaidi na wasanii wamechoka na kufubaa kwa sababu hakuna faida ya kile wanachokifanya,

tulikuwa tunajadili mfumo wa kazi zetu ulivyo, na tulikuwa tunaangalia kuwa inawezekanaje kazi zinafika kwa mashabiki lakini wanaofanya kazi wanadhoofika.

Steve anasema pia anajua kuna watu watakaobezwa kwa sababu kikao kimefanywa na viongozi wa CCM lakini hawatajali kwa sababu wanachoamini ni kuwa CCM ndio mwakilkishi wa serikali kwa sababu serikali inaongozwa na CCM.

hatutajali kwa wale wanaobeza kwa sababu serikali inaongozwa na na ni chama hivyo wanaoona kuwa tumeitwa na  chama basi shauri zao.chama cha ni mapinduzi ni mwakilishi wa serikali kwa sababu Jamhuli ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na CCM.

Alichofanya Diamond ni Heshima kwa Wasanii Wengine :-Steve Nyerere.

Msanii a vichekesho nchini Steve nyerere amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba watu watakaa wakibeza kile alichofanya Diamond lakini ukweli utabaki kuwa alichofanyadiamond ni heshima kuwa kwa wasanii na kazi ya sanaa pia kuwa kuwa wasanii wanaweza kufanya kitu katika jamii.

Steve nyerere ambae amekuwa akiponda au kusifia bila kuogopa pale msanii anapokosea au kufanya vizuri  amesema kuwa kitu alichofanya Diamond inabidi kiwe mfano wa kuigwa hata kama  haitawezekana kufanya kwa kiwango chake.

Steve anasema “Huwezi kuzuia ukweli upite; Tumekuwa watu wakubisha bila sababu, Niambiwe ni 
nani alishawahi kujua waliomfanya awe wanaitaji msaada wake.Alicho kifanya Diamond ni HESHIMA kwa wasanii wengine, amefanya kwa Niaba ya Sisi WOTE.

Kama kuna MTU anabeza atakuwa DODOKI, Diamond ni mfano wa kuigwa, Kuna Watu walikuwa maarufu kuliko Diamond Ila waliishia sifa YA kujitapa mtaani na kudharau watu, MIMI KWANGU NAOMBA TUKUMBUKE TULIPO TOKA.Sanaaa ni KAZI, IFIKE Muda tujue ADUI wa sanaa ni Sisi wenyewe. Daimond songa umefungua milango ya huduma kwa JAMII KAKA

Hata hivyo steve nyerere amehaidi na kusema kuwa hata yeye atakuja kufanya vitu vikubwa sana zaidi ya alichofanya diamond kwa jamii yake.

Tunaheshimu Mamlaka Hata Kama Roho Haitaki :-Steve Nyerere.

Msanii wa filamu wa Tanzania na mchekeshaji marufu Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, amesema kwamba kitendo cha wasanii kujihusisha na siasa kwa wakati mmoja, ni kitendo ambacho hakiwezi kuzuilika kwao kwani wao wanatii mamlaka, hata kama rohoni mwako hautaki.

Akizungumza na EATV, Steve Nyerere amesema kwamba suala la kufanya kazi za chama kwa wasanii kwanza wao wenyewe wanajiingizia kipato, lakini pia wanaheshimu na kutii mamlaka iliyopo ya uongozi wa nchi. “Sisi tunaheshimu mamlaka, mamlaka ambayo inaongoza ni ya chama cha mapinduzi, kuna muda unaweza ukawa rohoni mwako hautaki, usishindane na watu wenye nguvu, vyama vyama vinawahitaji kwa sababu wana nguvu kwenye jamii, sio kama sisi tunalazimisha, zamani tulikuwa tunaenda kwenye hafla za kiserikali sio kwenye chama, vyama vilikuwa na wasanii wao kina Komba, sasa hivi unajikuta unaambiwa bei gani unahitaji, utakataa!? Kwanza unalipwa na unaambiwa nenda, ukienda unakutana na CHADEMA, si lazima usifie waliokulipa!? Huwezi kukataa”, amesema Steve Nyerere.

Kutokana na suala hilo Steve Nyerere amesema kwamba ni ngumu kuwatenganisha na siasa, kwani licha ya kwamba wao wanakuwa kazini, lakini pia kuna wengine ni makada wa vyama, hivyo wanapotumikia chama wanatakiwa watu waelewe kuwa wapo kazin

Steve Awaomba Wasanii Wote Wasimame na Wasanii Wenzao

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere ameibuka na kuwataka Wasanii Wenzake wote kuungana pamoja na kuwaombea msamaha wasanii wenzao.

Steve amewataka wasanii wote kwa jumla bila kujali wa muziki au filamu kuwa pamoja kumuombea msamaha msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama ambaye mpaka sasa yupo kituoni kwa kosa la uharibifu wa mali ya umma.

Maua na mtangazaji wa Clouds, Soudy Brown wanadaiwa kusambaza video mitandaoni ikionesha watu wanaokanyaga noti za shilingi elfu kumi ambalo ni kosa la kisheria.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Steve Nyerere amesema  anawaomba wasanii waungane kumuombea msamaha Maua kwani ni mwenzao.

Msanii yeyote ni kioo cha jamii, chochote atakachokifanya kinaweza kuwa na faida au hasara, kwa kile walichokifanya, mimi na wasanii wote bila kujali wa muziki au wa filamu tuwaombee kwa vyombo vyote husika kwa kuwa natumaini wamejifunza na naomba tu wapewe dhamana”.

 

Wasanii ni Wanafiki Wanasubiri Kutoa Pole Badala Ya Kusaidia”- Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere amefunguka na kutaka Wasanii Wenzake waache unafiki na kupaaza sauti sasa ili Soudy Brown na Maua Sama waweze kuachwa huru.

Maua Sama na Soudy Brown wamewekwa  ndani tangu siku ya Ijumaa mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuposti video clip iliyowaonyesha kundi la watu wakicheza wimbo wa Iokote wa Maua Sama huku wakirusha pesa na kuzikanyaga.

Steve Nyerere amewatolea povu wasanii Wenzake na kuwataka wajitoe kuwasaidia wasanii wenzao katika kipindi hiki cha shida badala ya kukaa kimya halafu kuja kutoa pole wakija kutoka hapo baadae.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Sisi wasanii ni waoga na wanafiki, limeanza kuhusishwa sijui kuna ugomvi na RC Makonda hawa wamekosea, sio wakitoka ndio tuanze kutoa pole, Ndio nilipanga kufanya hivi, Hapana muda ndio huu tuombe radhi kwa serikali vijana wetu wapewe dhamana”.

 

 

kijembe cha Steve Kilimlenga Hamisa Mobeto.

Kama siku mbili nyuma kuna habari ya Steve Nyerere kuongelea mambo ya uchawi na ushirikina ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii huku steve akisema kuwa mchawi mkubwa pekee ni mungu tu na wala sio binadamu kama watu walivyozoea.

Lakini katika kukaa saa na kuchunguza steve nyerere pia alisema kuwa ” wanawake wengi sana  wanaamini kuwa hawawezi kufanikiwa mpka wapate wanaume wenye pesa na wengine udirki hata kwenda kwa waganga wa kienyeji ili kupata wanaume hao wanaowahitaji

Kwa trending ya habari  ya wiki iliyopita habari kubwa iliyokuwepo katika mitandao ilikuwa ni swala la ushirikina ambalo alihusishwa hamisa mobeto na familia ya Diamond Platinumz huku ikisemekana kuwa hamisa amekuwa akimloga diamond ili aendelee kumpenda na kumpa pesa.

Swali linakuja je, kauli ya Steve nyerere haikuwa ni kijembe  kilicholenga kusistiza habar za uchawi za hamisa mobeto, na kwanini yamesemwa hayo baada ya kuvuma kwa skendo ya uchawi kwa hamisa Mobeto.

Yawezekana huo ni msumari wa moto steve nyerere aliamua kuupigilia kwa hamisa lakini bila kuwka wazi kuwa alikuwa akimlenga yeye.

Ninaamini Mchawi Mkubwa ni Mungu Pekee.;-Steve Nyerere

Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amefunguka na kusemakuwa wasichana wengi wamekuwa wakiamini kuwa kila unapotaka mafanikio basi njia rahisi ya kutusua ni kwenda kwa mganga kwa ajili ya kupata mafanikio wanayoyatafuta.

ninachoamini kuwa mchawi mkubwa ni Mungu pekee na kama utamwamini yeye basi unaweza kuushinda hata huo uchawi wenyewe,  na unaweza kuwasaidia wajinga wachache lakini mimi naamini kuwa ukimwamini Mungu utafanikiwa.

Mungu hana mwisho lakini uchawi una mwisho, na kama ukipiga magoti na ukamlilia basi unaweza kutusua kila kitu.

Steve anasema hayo alipokuwa akiongea na mtandao wa clouds na kusema kuwa kuna watu wengi wamekuwa wakitawaliwa na mambo ya ushirikiana kiasi kwamba hawawezi kufanya jambo lolote hata kama ni la kimaendeleo mpaka wamwambie kwanza mganga wao.

 

Mange Alipua Bomu, Asema Wastara na Steve Nyerere Waliwahi Kuwa na Mahusiano Hapo Nyuma.

Mwanaharakati Mange Kimambi amefunguka na kusema kuwa mwanamuziki na muigizaji wastara juma aliwahi kuwa na mhausiano ya kimapenzi hapo nyuma na msanii mwenzake seve nyerere lakini hakuna aliyewahi kujua na kwa sababu ilikuwa ni siri.

Wawili hao ambao wamenza kutukanana katika mitandao ya kijamii na kutishiana kutoleana siri mpaka za ndani imekuwa ni kama swala ambalo hakuna aliyetegemea kuwa lingeweza kufikia lilipofikia sasa.

Akiandika waraka mrefu wenye matuzi na kebehi nyingi mange kimambi amesema kuwa Steve Nyerere aliwahi kuwa na mahsuaino na mwanadada huyo lakini wastara  anajifanya kuwa ni mgonjwa wakati anaweza kutoka kimapenzi na wanaume tofautu tofauti ilhali hajali ugonjwa alaiona.

Wastara ambae ahap awali aliptajiwa mambo ya steve nyerere alimjibu kuwa mambo ya steve nyerere ni ya zamani kabla hata ahajapata ajali , akimaanisha kuwa ni kipindi ambacho alikuwa hajaolewa lakini mange alikanusha  na kusema kuwa ni kipindi hiki cha ugonjwa wake ndio alikuwa katika mahusiano na Steve Nyerere  na pia mdogo wake Alikiba pia.

Mama mbona unajitetea nimeanza kukutajia ya steve nyerere unaanza kujitia eeti ooh ya zamani, eti ni mambo ya miaka 10 iliyopita wakati steve ame**** wakati ukiwa umeshakatwa mguu…..Ma***a kilema wewe , …Ki**** hata kiwe na miaka20…..malaya mchafu wewe ume***** mpaka na abdul kiba hivyo ivyo na kigulu chako. unapenda sana watoto wadogo wastara.

Ujumbe Mzito Wa Steve Nyerere Kuelekea 40 Ya Mzee Majuto

Msanii wa filamu za Kibongo na mwanaharakati wa mambo ya siasa Steve Nyerere ametoa ujumbe mzito Ikiwa ni siku chache mpaka kufikia arobaini ya Msanii mkongwe Mzee Majuto tangu aage dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Amewaasa watu kumkumbuka Mungu siku zote za maisha yao kutokana na ukweli kwamba siku zetu za kukaa duniani ni chache na zinahesabika.

Tupo kwenye mapito ya kidunia sana,tunaishi kama tuna mkataba na Mungu hatuna hofu na Mungu,Tunasahau muda wa kuishi duniani ni mchache sana.

Tunasahau Muda Wa Ufufuo Wa Milele Inategemea Na Yale Mazuri Uliyofanya Ukiwa  Hai, Fedha ,Cheo ,Ustaa ,Vyote Mapito Pokea  Sikiliza Kataa Maskini Anapendwa Kusikilizwa Hata Kama Utakataa Jambo Lake“.

Mzee Majuto aliaga dunia tarehe 7 August mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alilazwa kwa muda mrefu Muhimbili na hata kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

“Nikifa Nizikwe na Ray na Awasomeshe Watoto Wangu”- Steve Nyerere

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanaharakati wa siasa Steve Nyerere ameibuka na kudai hawezi kuacha kusimamia misiba ya watu na msiba wake anataka msanii mwenzake ausimamie.

Steve ameibuka na hili baada ya sakata lake lililompata siku chache za nyuma baada ya kugubikwa na skendo ya kuiba pesa za Michango ya rambirambi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Steve amesema kitendo hicho cha kusimamia misiba kimeweza kwa namna moja au nyingine kumfanya pia awe karibu na watu wazito nchini ambao wanamuunga mkono kwenye kujitolea kwake.

Sitaacha kusimamia misiba ng’o, wanaosema waache waseme watachoka. Ninasimamia misiba kwa sababu ninafahamu na mimi ipo siku nitaondoka na watu watasimamia msiba wangu. Niseme tu wazi hata kama nikiondoka leo nataka Vincent Kigosi ‘Ray’ asimamie na kuwasomesha wanangu“.

Steve Nyerere amekana kabisa skendo za yeye kudhulumu pesa za rambirambi na kudai akikusanya basi hufikisha kwa wahusika.

Steve Nyerere Akubaliana na Uamuzi wa Katibu Kuhusu Wasanii Kutotumika Katika Kampeni

Msanii wa maigizo na vichekesho nchini, steve nyerere ameongelea majibu ya kile kilichosemwa na katibu mkuu wa CCM hivi karibuni kuhusu wasanii wa muziki  nchini kutotumika katika kampeni za CCM kama ilivyokuwa hapo awali .

Mwaka 2015 kipindi cha kampeni wasanii wa bongo movies na wasanii wa bongo fleva walitumiwa katika kampeni  katika mikoa mbalimbali lakini katibu mpya wa CCM anasema kuwa wamemaua kwa sasa wasifanya hivyo kutokana na heshima ya wasanii katika kufanya kazi zao.

Akiongea na EATV, steve nyerere anajibu kuwa  hawezi kuonelea chochote kuhusu swala hilo kwa sababu katibu mkuu ana nafasi kubwa sana katika chama na kama ameamua hivyo basi hawawezi kupinga kitu.

swala la  Bashiru siwezi kuliongelea kwa sasa , licha ya kuwa amesema hivyo lakini walifanya kazi kubwa sana na ndio maana tunawathamini, , siwezi kubishana na katibu mkuu kwa sababu yeye ana nafasi kubwa sana katika chama.

Hata hivyo steve anasema kuwa kwa sababu wanaheshimu sana maamuzi hayo wao kama wasanii hawatafanya lolote mpaka pale watakapoambiwa  cha kufanya hivo anawaomba wasanii wenzake wakae kimya na kuacha kujibizana na watu ambao wanaweza kuwabeza.

 

 

Wanaonitukana Wananipa Moyo wa Kufanya Vizuri Misibani :-Steve Nyerere

Msanii wa bongo movies Steve Nyerere amefumguka na kusema kuwa katika familia yoyote hamuwezi kuzaliwa mkafanana akili hata siku moja na yeye ni kati ya watoto waliozaliwa na kujua majukumu ya familia ukiachana na wale ambao watakuwa kazi yao ni kuwaumiza wazazi tu.

Steve anasema kuwa pamoja na kwamba amkuwa akitukanwa sana kuhusu swala la kujihusisha kwenye misiba na kwamba amekuwa akinufaika lakini kamwe hatoacha kujitolea kwa sababu moyo wake haumtumii kuacha kuwafanyia wengine mema.

hamuwezi kuzaliwa watoto saba alafu owte mkawa na akili timamu wapo watakaokuwa wanawatukana sana wazazi wenu, na wengine watatokea na kujua majukumu ya familia yao kwaio mimi ni moja kati ya wale watoto watoto saba wanaojua majukumu yao kwa familia ya watanzania.

na katika kitu pekee nashukuru ni kuwa wanaponitukana ndio wanazidi kuniongezea nguvu na moyo wa kufanya vizuri katika misiba.

Steve nyerere ambae mara ya kwanza aliona kama ni bora kuachana na kujitolea kwake lakini baadae alikuja kugundua kuwa endapo yeye atajitoa na kukaa pembni inapotokea matatizo ya misiba ya wasanii wenzao kuna kuna na mapungufu mengi sana.

Steve Nyerere Kufunga Ndoa na Wellu Sengo

Mchekeshaji na msanii wa Bongo movie Steve Nyerere ametangaza ndoa na binti Mrembo wa Bongo movie na mzazi mwenzake Wellu Sengo katika siku zijazo.

Global Publishers wanaripoti kuwa Steve Nyerere alitangaza habari hiyo njema Kwenye Ujumbe wa Alfa uliopo Morocco jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya harusi ya msanii mwenzake Jimmy Mafufu.

Katika hali ya utata Steve ametangaza ndoa na Wellu Sengo lakini tayari yupo Kwenye ndoa na mke wake na kudai kilichotokea baina yake na Wellu ni ajali kazini.

Siku ya harusi ya Jimmy Mafufu Steve Nyerere alisimama na kuongea ambapo alifunguka:

Samahani kwanza, naomba kuuliza, “hivi Wellu yumo humu? Mama ndoa yetu na sisi inakaribia anza kujiandaa”.

Baada ya Kauli hiyo iliyoashiria Steve yupo tayari kumuoa Wellu, Mke wa Steve alitoa Kauli yake juu ya suala hilo na kudai:

Steve ataenda popote lakini atarudi tu, kuna wadada wenye maisha magumu wanataka kuwa na maisha bora ndiyo maana wanamsumbua sana mume wangu“.

Miezi michache iliyopita Steve Nyerere alikiri kufanya makosa kuzaa nje ya ndoa na Wellu lakini akasema hana mpango wa kumuoa:

Ni kweli nimezaa na Wellu lakini watu lazima wajue kwamba kuzaa na mtu siyo kuoa, hivyo sidhani kama nitamuoa Wellu“.

 

Hakuna Msiba Wenye Faida ;-Stev Nyerere

Msanii wa muziki wa bongo movies stebe nyerere ambae kila siku amekuwa akijitoa kufanya analoweza ili kuwaistiri watu mbalimbali wanaokumbwa na misisna lakini wasanii wanaofariki kuweza kushughulikia mazishi amfunguka  baada  ya kuwepo kwa maneno mengi kuhusu kujihusisha kwake katika misiba.

Akiongea na Clouds media mapema leo, steve nyerere anasema kuwa alikuwa amekaa pembeni kwa muda kuangalia jinsi waliokuwa wakifanya kazi hiyo kama wanaweza na amegundua mapungufu mengi yanavomlazimu kuendelea kujitolea kufanya shughuli hiyo.

Hata hivyo Steve anasema kuwa hawezi kuacha kujitolea kufanya kazi  hiyo kwa sababu ya maneno ya watu.

Mimi sitaacha kusimamamia misiba ya watu kwa  sababu ya maneno ya watu, nilikaa pembeni lakini baadae nikagundua kuwa utendaji kazi hauridhishi, nimeamua nirudi,kuna baadhi ya watu kazi yao kuchuruza maji kama dodoki lakini nataka kuwaambia kuwa hakuna msiba wenye faida.

Steve amekuwa akisemwa kuwa amekuwa akijihushisha katika misiba kwa sababu amekuwa akipata pesa katika misiba hiyo pale zinaapochangishwa pesa kwa ajili ya matatizo hayo.

 

“Sitaacha Kusaidia Kwenye Misiba” Steve Afungukia Skendo Ya Kula Rambirambi

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere amefunguka na kuongelea skendo ambayo imekuwa ikitengeneza headlines juu ya Kula rambi rambi za misiba anayochangia.

Katika wiki hizi chache Steve amekuwa akitawala headlines za mitandao ya kijamii kwa tuhuma za kutumia rambi rambi za misiba anazozikusanya kwa matumizi yake binafsi.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani juzikati mara baada ya kujitoa kuratibu msiba wa mchekeshaji Amri Athuman ‘King Majuto’, Steve alisema suala hilo halimuumizi kichwa kwa sababu kutoka ndani ya nafsi yake anaamini kwamba hachakachui fedha.

Angalia wasanii wenzangu wengi sasa hivi wameonesha kuniunga mkono hivyo sitaacha kusaidia pindi misiba inapotokea kwani wamenitia moyo kwamba ninastahili kuwaunganisha katika matatizo“.

Wasanii kadhaa kama Faiza Ally, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya na wengineo walijitokeza na kumkingia kifua Steve juu ya tuhuma hizo na kudai ni mtu anayejutoa Kwenye matatizo ya watu na tuhuma za kuiba rambi rambi si za kweli.