Maimartha Amkingia Kifua Wema Kuhusu Jina la Tanzania Sweetheart.

Mtangazaji maarufu na mc kipenzi cha watu Maiamrtha wa Jesse amejikuta anashindwa kuficha hisia zake za hasira kwa mwanadada Hamisa Mobeto kwa kitendo chake cha kutaka kuitwa Tanzania sweeethaert jina ambalo alipewa Wema hapo awali kutokana na upendo alikuwa nao kwa watu.,

Maiamrtha anatoboa siri na kusema kuwa pamoja na mambo yote ambayo wema aliwahi kumfanyia hamisa katika maisha yake mpaka kufikia hatua ya kuwa anampa ela ya nauli na pesa ya kununulia pafyum na kumkaribisha nyumbani kwake kama mdogo wake lakini mwanadada huyo bado aliamua kumsaliti na kutembea na mwanaume wa dada yake na sasa anagombania jina.

Maimartah anasema kuwa pamoja na yote lakini Wema atabaki kuwa Sweetheart wa Tanzania na hatopata mshindani hata siku moja hivyo kama kuna watu wanamuonea wivu basi  wamuache.

Pamoja na maneno yote hayo, mapovu hayo pia yanaambatana na pongezi za wema za kutimiza miaka kadhaa  ambapo mwanadada huyo anasherekea siku ya september 28 mwaka huu huku akimwalika Van Vicker katika party hiyo.

 

Mapokezi ya Van Vicker Sio Mategemeo ya Wema

Sio kawaida kwa mwanadada Wema sepetu kupokea mgeni katika viwanja vya ndege kama ilivyotokea alfajiri ya leo kwa kuosekana kwa umati wa watu.Kama alivyokuwa akitoa taarifa ya ujio wa msanii huyo mkubwa kutoka Nigeria, alisema kuwa msanii huyo atakapo fika atakuja kupokelewa na watu mbalimbali kwa sababu ni mgeni wake.

Wema amekuwa moja ya watu wanaomamini kuwa na mashabiki wengi sana na kwa kuthibitisha hilo, utakumbuka ilivyokuwa wakati wa kumpokea mwanadada Omotola ambae aliwahi kuja Tanzania kwa mwaliko wa mwanadada Wema Sepetu jinsi ambavyo alipokelewa na watu wengi hasa Team Wema .

Hii inaweza kuleta maswali mengi sana kuhusu mashabiki wa Wema hasa wale wanaojiita Team wema kuwa walikuwa wapi kumpa sapoti msanii wao kama kweli wao ni Team Wema au ndio mapenzi yameanza kuisha.

Hali ilivyokuwa uwanja wa taifa ni tofauti na ile amsha amsha ya Wema kila anapokuwa na mgeni katika viwanja hivyo, hata hivyo siku ya shughuli bado hivyo tunaamini kuwa watajitokeza wengi kumsapoti katika siku yake ya kuzaliwa lakini pia katika uzinduzi wa filamu hiyo.

Wema Sepetu- Hamisa Hawezi Kuwa Tanzania Sweetheart, Ni Mimi Peke Yangu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka n kumnyooshea maelezo juu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ na kusisitiza pekee yake anaweza kuwa.

Kwenye mitandao ya kijamii Kumekuwa na mvutano kati ya mashabiki wa Wema na mashabiki wa Hamisa Mobetto ambapo wamekuwa wakigombani Jina la Tanzania Sweetheart na kila mmoja kudai staa wake anastahili kuitwa jina hilo.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Wema Sepetu Msanii wa filamu Wema Sepetu aka TZ Sweetheart amedai haoni sababu ya watu wengine kutaka kutumia jina hilo kwa kuwa yeye amekuwa akilitumia kwa muda mrefu baada ya kupewa na mashabiki wake.

Mimi Jina langu ni Wema, Tanzania Sweetheart ni Jina ambalo nimepewa na mashabiki zangu kutokana na mapenzi yao kwangu kwa hiyo hatuwezi kuwa Ma- Tanzania Sweetheart wawili kila mtu Awe na Jina lake halafu kuna Tanzania Sweetheart mmoja tu mbona majina yako mengi jamani”.

Wema na Hamisa wamekuwa Kwenye bifu  ya muda mrefu huku Wema akimtuhumu Hamisa kwa kumsema vibaya kwa watu.

Van Vicker Kuwasiri Kesho Kwenye Birthday ya Wema.

Msanii mkubwa kutoa Nigeria Van Vicker anatarajiwa kuwasili mwisho wa mwezi huu  nchini tanzania huku dhumuni kubwa likiwa ni kuhudhura kumbukumbu ya siki ya kuzaliwa ya mwanadada wema sestu na pia kufanya uzinduzi wa filamu kubwa iliyowahi kutangazwa sana katika mitandao.

Filamu hiyo ambayo imewakutanisha wema na Van Vicker ilitangazwa sana hapo kipindi cha nyuma lakini haikutoka , hivyo msanii huyo anapokuja sasa atafanya pia uzinduzi wa filamu hiyo.

Akiongea na EATV Wema anasema kuwa van vicker atawasili jijini saa 10 alfajiri na kupokeklewa na watu mbalimbali akiwepo yeye mwenyewe, ikifuatiwa na kumpepeleka sehemu kwa ajili ya kupumzika huku wakifanya maandalizi ya siku husika  ambayo ni september 28 .

Wema anasema kuwa Van Vicker atatembezwa katika vituo mbalimbali vya habari kwa ajili ya interviews, lakini pia katika siku yake hiyo anatarajia kuona viongozi mbalimbali pia wakiwepo katika shughuli hiyo kubwa.

hii ni mara ya pili sasa Wema Sepetu kuleta msanii kubwa kutoa nigerai ambapo mara ya kwanza alimleta Omotola Ajalade Ikende.

Wema Sepetu Kuja na Biashara Nyingine Baada Ya Lipstick na Perfume

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu anadaiwa kujaribu tena Bahati yake katika ulimwengu wa ujasiriamali baada ya Tetesi za kutaka kufungua duka lake jipya hivi Karibuni.

Wema ambaye ameonekana Kupitia mitandao ya kijamii akiwa nchini China na dada yake anadaiwa ameenda huko kwa ajili ya kufunga mzigo wa kuuza Kwenye duka lake jipya.

Wema anatarajiwa kufungua duka lake la Pili baada ya duka lake kwanza alilokuwa anauza perfume na lipstick kufungwa Habari za chini chini zinadai duka hilo litakuwa maalumu kwa ajili ya kuuza nguo za watoto.

Duka hilo linatarajiwa kuitwa ‘Little Sweetheart’ na kuna baadhi ya marafiki wa karibu wa Wema wameonekana kumpongeza Msanii huyo kwa hatimaye hiyo aliyopiga.

 

Wema Sepetu Kuja na Event Ya Mwaka ‘Birthday Bash’

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amefunguka na kutangaza shughuli yake ambayo ameitangaza kama ‘Birthday Bash’ itakayofanyika tarehe 28 Septemba.

Wema ametangaza kuwa  tiketi za ‘Birthday Gala’ zitaanza kuuzwa rasmi kuanzia kesho (Jumamosi) huku bei elekezi zikiwa ni 50000 kwa tiketi moja na kwa meza ya watu 10 ikiwa ni tsh 500,000.

Mrembo huyo atafanya matukio mawili kwa pamoja, uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Dad’ alioshirikiana na Van Vicker kutoka Nigeria pamoja na kusherekea birthday yake ambayo ameiita Bithday Gala.

https://www.instagram.com/p/BnsOyVsn9pO/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=167grqmk00rzg

Mobetto Hawezi Kuwa Tanzania Sweetheart ni Wema Peke Yake-Maimartha Jesse

Mtangazaji maarufu na mfanyabiashara Maimartha Jesse ameibuka na kumkingia kifua Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu na kudai hakuna kama yeye.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na mjadala Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Hamisa Mobetto amekuwa akipambanishwa na Wema Sepetu na watu hata kusema title ya Wema ya Tanzania Sweetheart anatakiwa apewe Mobetto kwani ndio anapendwa kuliko Wema.

Katika interview aliyofanya na Global Publishers, Maimartha amesema hakuna na hatatokea mrembo mwingine anayependwa na kukubalika kama Wema hivyo wanaompigia debe Mobeto kwamba ndiye anayekubalika sana kwa sasa wanajisumbua tu.

Wema ndiye Tanzania Sweetheart, hakuna wa kufanana naye na hatatokea mwingine kama yeye, hii ni namba nyingine, wanaosema Mobeto anamzidi ni waongo na hawajafanya tathmini zao vizuri, Wema anapendwa na kila mtu kuanzia watoto hadi wazee“.

Pamoja na kutokea kupingwa na kuchukiwa na mashabiki siku za hivi karibuni mpaka kutakiwa kuacha kujiita Tanzania Sweetheart Mrembo Wema Sepetu amegoma kuachia jina hilo na kusisitiza yeye ndio Sweetheart wa East Africa nzima.

Wema Sepetu Adaiwa Kumwaga Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ametudi Kwenye headlines ambapo anadaiwa amemwaga aliyekuwa mpenzi wake anayeitwa kwa jina la Lawrence Masanja maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama R.A.H.U.R.

Global Publishers wanaripoti kuwa kuvunjika kwa penzi hilo kulitokana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Wema kumng’ata sikio kuwa jamaa aliyenaye hafai na akiendelea naye atakuja kujuta.

Chanzo cha karibu cha Wema kimetiririkia gazeti la Ijumaa Wikienda:

Wema kaamua kumwaga manyanga kwa yule jamaa yake, mwenyewe alishaanza kushitukia kuwa kaingia ‘cha kike’ na hata watu wake walipomtonya kuwa jamaa siyo hakuona ugumu kumtosa. Sasa hivi nasikia ana jamaa mwingine”.

Baada ya Tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Wema ili kupata ukweli kutoka kwake na alikiri kuwa yeye na mwanaume huyo hawapo wote:

Jamani huyo mtu siko naye na sidhani kama itakuwa ni vyema nikimuongelea kwa sababu sihitaji kufanya hivyo ila kwa kifupi hayupo katika maisha yangu”.

Mahusiano ya Wema yalisemekana kuingia doa wiki chache zilizopita baada video zilizomuonyesha Wema na Diamond wakiwa na ukaribu wa ajabu kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Napenda Kupigwa na Mpenzi Wangu- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie supastaa Wema Sepetu ameacha watu midomo wazi baada ya kutoa Kauli ya kwamba anapenda sana pale mwanaume ambaye yupo naye kimapenzi anampiga.

Wema amedai kuwa anapokuwa Kwenye mahusiano anakuwa anaona raha pale mwanaume wake anapompiga japo kidogo pale anapokosea.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wema Sepetu aliyasema hayo hivi karibuni kwenye sherehe ya kuzaliwa ya meneja wake, Neema Ndepanya iliyofanyika nyumbani kwa Wema, Salasala jijini Dar ambapo aliulizwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusu aina ya mwanaume anayependa kuwa naye

Napenda mwanaume anipe kipigo kidogo siyo mwanaume mnaishi miaka yote, halafu hata kukupiga kofi kidogo hakupigi”.

Wema ameshawahi kusema aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliwahi kumpa kipigo cha nguvu kiasi ya kwamba alimuachia majeraha mwilini.

 

Mrembo Aliyechora Tattoo Ya Jina La Wema Afunguka

Msanii wa Bongo movie anayejulikana kama Diana Kimary amefunguka na kueleza sababu hasa za kuchora Tattoo ya Jina la Msanii Wema Sepetu Kwenye mwili wake.

Siku ya jana Diana alitengeneza headlines baada ya video iliyomuonyesha akiwa amechora tattoo hiyo kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea gumzo.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Diana amefunguka kuhusu Tattoo hiyo na kusema ameamua kumchora Wema kwa sababu mbali na urafiki Lakini pia ni dada yake na anampenda Sana.

Nampenda sana Wema kwa sababu amekuwa dada mzuri kwenye Maisha Yangu”.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Tanzania sweetheart Wema Sepetu kuchorwa Kwenye mwili wa mtu kwani miaka ya nyuma Kajala Masanja alishwahi kuchora Tattoo kubwa yenye Jina la Wema lakini baada ya ushoga kuisha aliifuta.

Mange Amtupia Wema Tuhuma Nzito Za Kwenda Kwa Waganga Kama Mobetto

Mange Kimambi ameingia Kwenye bifu zito na msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya sakata la uchawi la Hamisa ambalo lilishika kazi baada ya voice note kuvujishwa mtandaoni.

Mange na Wema walianza kurushiana maneno baada ya Mange kumtuhumu Wema kwa kushabikia kesi ya Mobetto ambapo Mange alimwambia Wema asishabikie sana kwani yeye mwenyewe ameshawahi kupata skendo za waganga.

Baada ya maneno hayo kusemwa ndipo vita ya maneno na matusi ilianza kwani Wema alikataa kuwa hajawahi kwenda kwa waganga hata siku moja na kuweka posti hii:

https://www.instagram.com/p/BnUKOienUro/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1swhan939ccq1

Mange alimjia juu Wema juu ya tuhuma za Kwenda Kwa Waganga na kuweka video ya miaka ya nyuma ambayo Mama Wema aliongea na kukiri mtoto wake ana tabia za kwenda kwa waganga:

https://www.instagram.com/p/BnUWEWHlxF5/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=imnibw87yviy

Mange Amkingia Kifua Mobetto Dhidi Ya Familia Ya Diamond Kufuatia Tuhuma Za Uchawi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa na mdau wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi amemkingia kifua Hamisa Mobetto baada ya familia ya Diamond kumuandama na skendo za ushirikina.

Mama Diamond na Esma Platnumz wamemtuhumu Hamisa kwa uchawi ambapo wamedai kuwa alienda kwa mganga kwa nia ya kumloga Mama Diamond na Esma ili wampende na aolewe na Diamond.

Mange ameibuka na kumtetea Hamisa dhidi ya tuhuma hizo na hata kuwatupia maneno ya shombo familia ya Diamond na Wema Sepetu ambaye pia ameonekana kumsema na kumtupia vijembe Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BnMqWQFFRTt/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1d4duzu19snyf

Mama Wema Akanusha Mwanae Kuchumbiwa.

Pamoja na kwamba katika mitandao ya kijamii kumekuwa na maneno mengi kuhusu mwanadada Wema Sepetu kuchumbiwa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Rahur lakini  wema hakuwahi kuthibitisha hilo, mama mzazi wa mwanadada huyo ameongea na kukanusha swala hilo kuwa yeye kama mama hajui chochote kuhusu ilo.

Mama yak Wema Sepetu amesema kuwa mitandaoni kumekuwa na mambo mengi sana kiasi kwamba hakuna taarifa zinazoweza kutolewa zikawa na ukweli  wowote kuhusu swala hilo.

Mimi sitambui kabisa kama kuna mchumba eti amekuja kwangu na ametaka kumchumbia  na kwamba tayari tuko katika taratibu za ndoa , icho kitu sio cha kweli na maana mimi ndio mzazi mwenyewewatu wasikazanie kusikiliza vitu vya mitandao na ukizingatia kuwa mitandaoni kuna mambo mengi sana.ni bora kupata uhakika wa jambo lolote kutoka kwa mhusika mwenyewe.

Wema Sepetu Athibitisha Kuwa Hali Ya Ommy Dimpoz ni Njema

Msanii wa filamu za Bongo Movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa hali ya Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz imeendelea kuwa vizuri tangu taarifa zake za kuzidiwa kuvuma.

Siku ya Jumamosi taarifa za Ommy Dimpoz kuzidiwa na kulazwa ICU zilisambaa kama moto wa kifuu na kusababisha taharuki kubwa miongoni wa mashabiki zake.

Wema ambaye ana Ukaribu mkubwa na Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi baada ya kuwasiliana na Ommy anaamini anaendelea vizuri na hakuna kibaya kitakachotokea:

https://www.instagram.com/p/Bm9N1eJH2vo/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=sov38uq6c8e3

Taarifa za Ommy kupelekwa ICU zilipingwa na uongozi wake wa label ya Rockstar 4000 ambao waliweka wazi kuwa Msanii huyo anaendelea vizuri tu na matibabu.

Baba Jokate Awataka Wema na Uwoya Wamuige Jokate

Baba mzazi wa Msanii na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate, Mzee Urban Costa Ndunguru amefichua siri nzito inayowafanya mpaka Wema Sepetu na Irene Uwoya Wasafikie malengo yao kisiasa.

Kwenye mahojiano na gazeti la ‘Amani’ Nduguru aliliambia Amani katika mahojiano maalum kwa njia ya simu hivi karibuni kuwa:

Mwanangu, Wema, Uwoya wote wana ndoto za kuwa wanasiasa na viongozi wa umma lakini hawa wawili kuna mambo yanawakosesha fursa.

Mimi Uwoya simfahamu sana, namsikia tu habari zake kwenye magazeti, lakini Wema namfahamu kwa sababu baba yake (marehemu Isack Sepetu) nimefanya naye kazi serikalini.

Matatizo yanayowakosesha nafasi za kufikia ndoto zao hawa watoto yako mengi lakini kubwa kabisa ni kuiacha misingi bora waliyolelewa na wazazi wao. Siri kubwa ya kufanikiwa hasa katika kutumikia watu ni kujiheshimu na kufanya mambo kwa siri, siyo kwenda kiholelaholela, unajivunjia heshima mwenyewe”.

Lakini pia Baba Jokate amewataka warembo hao wawili kuiga mfano wa Jokate:

Nimeona wanampongeza mwanangu kwa kuteuliwa kwake (kuwa DC), na mimi nasema wasiishie kumpongeza tu lakini waige tabia zake.

Jokate ni mwanangu, sisemi ni mkamilifu lakini ni msiri sana, vigumu kumuona kwenye jamii akifanya vitu vya ovyo, tabia hii naomba Wema na Uwoyawaiige itawasaidia kufikia ndoto zao za kuwa viongozi“.

 

Wema Aingilia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amejikuta Tena katika headlines za social media baada ya kuingilia kati bifu linalo trend hivi sasa kati ya Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Zama na Mobetto waliingia Kwenye bifu hili baada ya kutifuana kuhusu mshono wa vazi alilovaa Zamaradi Kwenye 40 ya mtoto wake wiki chache zilizopita.

Zamaradi aliandika waraka mrefu wa kurasa tatu ukieleza namna alivyosikitishwa na maneno yanayosambaa mitandaoni kuwa alipewa mshono na Mobeto kwa lengo la kushonewa, lakini akauchukua na kwenda kuushona kwa mtu mwingine huku akimwaga chati zote za WhatsApp walizokuwa wakitumiana.

Lakini pia kwa Mobeto naye aliibuka na kupinga vikali waraka huo. Wakati hayo yakiendelea, Wema kupitia ukurasa wake alinunua ugomvi kwa kuandika; Tuendelee ama tusiendelee’.

Meneja wa Wema, Neema Ndepanya naye hakukaa kimya, aliingilia kati na kumkingia kifua Wema kwa kuandika waraka wake. “Kiki za kuchafuana zilishapitwa na wakati, hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa mnafiki, yaani nachukia mtu anajifanya kila wakati anaonewa yeye tu,”

.