BASATA Wakanusha Tetesi Za Kumuita Wema Sepetu

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha tetesi za kumuita na kumhoji staa wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kusambaza Mtandaoni picha na video zenye utata.

Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuachia picha na video za yeye na mpenzi wake huku video ikiwaonyesha wawili hao wakiwa wanapeana mabusu moto moto na picha ikiwaonyesha wakiwa chumbani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kuna tetesi zilisambaa kuwa kutokana na picha hizo chafu Wema Sepetu ameitwa na BASATA kwa ajili ya kufika katika ofisi zao taarifa ambazo kwa saaa BASATA wamezikataa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Afisa Habari BASATA, Agness na kukanusha taarifa hizo huku akidai kama mwanadada huyo anaenda Basata ni kwa mambo yake binafsi sio kwamba aliitwa.

Sio kweli Wema ameitwa Basata, hata sisi tunasikia hizo habari na kuihusisha na mambo yake ya kwenye mitandao, sisi kama Basata atu-deal na maisha binafsi ya wasanii labda afanye tukio katika kazi ya sanaa ndio tunaweza kumuita,Kama ni mambo ya mtandaoni TCRA ndio wenye mamlaka”.

BASATA ni sehemu ya wasanii, ni wazazi wa wasanii, kama anakuja sisi tutampokea na kuzungumza naye hukusu sanaa yake na namna ya kujiweka kama msanii lakini mpaka sasa hatuna taarifa kama anakuja lakini akija sawa tutampokea”.

 

Esma Platnumz Amkingia Kifua Wema

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumkingia kifua Wema Sepetu kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya juzi Wema alimtambulisha mpenzi wake mpya ambaye amedai ndiye atakuwa mume wake mtarajiwa lakini moja kwa moja hali ilibadilika kwani mwanaume yule ameshawahi kumtukana Wema.

Mashabiki mbali mbali wa Wema walimshauri avunje Mahusiano na mwanaume yule na wapo hata Mastaa Wenzake ambao walimshauri atulie kwani mwanaume yule tayari ana wake wawili.

Lakini Esma ameibuka na kumpa sapoti Wema na kulpongeza kwa maamuzi  yake na kumtaka kufanya  kile ambacho moyo wake umeridhia na kama anataka Kuolewa na yule mwanaume basi ruksa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma ameandika maneno haya kwenda kwa Wema:

Go go Mu forever wiii cha muhimu ukiwa naye uko happy, ifike mahali tuheshimu hisia za watu jamani tutapangiana maisha mpaka lini? Insta imekuwa sehemu ya watu kutuchagulia maisha watu tuishi vipi khaaa Wema ngoja na mimi nikitoe kibabu changu”.

 

Mama Wema Afungukia Mahusiano Ya Wema na Diamond

Mama Mzazi wa staa wa Bongo Movie Wema Sepetu, Mariam Sepetu amefunguka na kuongelea uhusiano wa binti yake Wema na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wema na Diamond waliwahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu kwa miaka ya nyuma lakini tetesi za wao Kurudiana hazijawahi kuisha.

Katika interview aliyofanya na Gazeti la Amani, Mama Wema alifunguka mara baada ya mwanahabari wetu kumuuliza kama atakuwa tayari kupokea posa ya Diamond kama atajirudi na kuomba nafasi nyingine kwa bintiye, alisema wawili hao imebaki stori.

Wewee, sikiliza nikwambie bwana, Wema na Diamond kwa sasa wamebaki kuwa marafiki tu. Haiwezi kutokea tena wakarudiana. Mimi ndiyo namjua Wema vizuri, ana moyo wa aina yake ndiyo maana unaona pamoja na kuwa wameshaachana lakini bado wanakuwa karibu, wanashirikishana mambo yao kiroho safi.

Wema ana maisha yake sasa hivi, Diamond ana yake, kamwe hawawezi tena kurudiana“.

Hivi sasa itakuwa ngumu kwa Wema kurudi kwa Diamond kwani tayari Wema ana mpenzi wake ambaye amekwisha tangaza naye ndoa Lakini pia Diamond na yeye ana wanawake wake wengine.

Esha Buheti Amchana Wema Kwa Picha Chafu Alizovujisha

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kumchana Msanii mwenzake Wema Sepetu baada ya kuvujisha picha na video chafu zinazomuonyesha yeye na mume wake mtarajiwa.

Siku ya jana Wema alitengeneza headlines baada ya kumtambulisha mwanaume anayetambulika kama Patrick na kusema ndiye mume wake mtarajiwa lakini baada ya kuposti video iliyowaonyesha wawili hao wakibusiana ilizua gumzo zaidi.

Esha Buheti ambaye ni rafiki mkubwa wa Wema alishindwa kuvumilia na kumuandikia barua ya wazi ambapo amemchana laivu na kumtaka aache kufanya mambo ambayo yanamuaibisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esha Buheti aliandika ujumbe huu:

Wema ametangaza uhusiano na mwanaume ambaye anasemekana tayari ana wake wawili Lakini pia kijana huyo ameshawahi kumrushia maneno ya kejeli Wema na Familia yake Kupitia mitandao ya kijamii.

Wema Afunguka Tetesi Za Kufaidi Penzi la Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuongelea skendo nzito inayomuandama hivi sasa ya kufaidi Penzi la Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku ya jana Mange Kimambi alidai kuwa  Wema  na Dogo Janja walikutana mkoani Arusha ambapo walikuwa nyumbani kwa rafiki yao lakini mambo yaliwazidi na kujikuta wanafanya yao.

Wema ameibuka kukataa tetesi hizo na kumtuhumu Mange kwa kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli wowote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika maneno haya:

Wema amekana tetesi hizo na kumuanika mwanaume mwingine ambaye amedai atakuwa mume wake mtarajiwa.

Wema Adaiwa Kuvunja Ndoa Ya Irene Baada Ya Kuchepuka na Dogo Janja

Staa wa filamu za Bongo Movie Wema Sepetu amekumbwa na skendo ya mwaka baada ya kudaiwa Kuvunja ndoa ya Msanii mwenzake Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja.

Wema Sepetu amejikuta katika wakati mgumu baada ya stori kutoka kwamba yeye na mume wa shoga yake Irene Uwoya ambaye amewahi kukaririwa akimuita shemeji kudaiwa kubanjuka.

Mange Kimambi ameripoti kuwa Wema na Dogo Janja walifanya mapenzi wakati Dogo Janja yupo na Uwoya.

Mange ameweka wazi kuwa alipata taarifa za Wema na Dogo Janja kufanya yao siku chache zilizopita lakini kwa kuwa anampenda Dogo Janja akaamua kumpotezea na hata kumtafuta na kumtaka kuhandle privately.

Lakini baada ya kutibuana na Wema jana Mange aliamua kumwaga ubuyu huo ambapo Mange amedai Wema ndiye alimuomba unyumba Dogo Janja.

 

Baada ya kuweka sakata hilo wazi Uwoya alionekana kumshukuru Mange kwa kumpa taarifa hiyo kwani tayari ndoa yake na Dogo Janja imekuwa  ikionekana kusuasua.

 

Wema Amuanika Hadharani Mpenzi Wake Mpya

Muigizaji wa Bongo movie supastaa Wema Sepetu amemuanika hadharani mwanaume ambaye yupo naye Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa.

Wema alizua gumzo zito baada ya kumposti mwanaume huyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘My future husband’ akimaanisha mume wangu mtarajiwa.

Wema amekaa muda mrefu bila watu kumtambulisha mwanaume wake kwani alishazoea kuwapost wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano,kipindi cha hapa katikati watu walihisi mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na muigizaji kutoka nchini Ghana ambaye amefanya nae Movie waliyoitambulisha mwezi wa tisa ambayo inajulikana kwa jina la D.A.D, na maswali hayo aliulizwa kwenye mahojiano yake mbalimbali na vyombo tofauti vya habari ila wema alikataa lakini leo ameweza kumuweka hadharani mwanaume wake.

Lakini pia mwanaume huyo ameonekana akikomenti Kwenye page ya Diamond na kumpa taarifa ndoa yake na Wema inafanyika tarehe 25.

Zari Aamua Kumuiga Wema Kwa Hili

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amemuiga Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu kwa jina.

Ikiwa jina la Tanzania Sweetheart bado lina utata ambapo Wema Sepetu na  Hamisa Mobetto bado wako vitani kwa ajili ya Jina hilo na Zari naye ameibuka na lake.

Zari na yeye ameamua kumuiga kwa kujiita Uganda’s Sweetheart. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Snapchat, Zari aliweka picha yake na kuambatanisha na maneno hayo ya Uganda’s Sweetheart hali ambayo ilisababisha gumzo mitandaoni.

Mh! Bi dada naye kaona amuige Wema kwa kujipa jina la Sweetheart, makubwa,” alichangia mmoja wa wadau wa mtandao wa Instagram baada ya kipande hicho cha picha kusambaa.

Hata hivyo Zari hakutoa maelezo yoyote kama kujiita vile ilikuwa ni kwa ajili ya utani au kweli alimaanisha kutaka kuwa Uganda Sweetheart.

Mama Wema Adaiwa Kumfanyia Vurugu Bwana Wa Wema

Mama mzazi wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Miriam Sepetu maarufu kama Mama Wema amedaiwa kumfanyia bonge la varangati mwanaume ambaye alikuwa  mpenzi wa Wema, R.a.h.u.r.

Global Publishers wanaripoti kuwa Mama Wema ambaye hakuwa akifurahishwa sana na uhusiano wa bintiye na ‘mkwewe’ huyo, aliibuka nyumbani hapo kwa mwanaye na kumtolea uvivu baada ya kuona jamaa si mtu wa maana.

Inaripotiwa kuwa siku ya tukio Mama Wema alienda nyumbani kwa Wema maeneo ya Salasala lakini alipofika hakumkuta mwanaye zaidi ya yule mwanaume na inadaiwa baada ya muda umeme uliisha na Mama Wema alipoona kijana yule hana mpango wa kununua alimtimua na kumfanyia bonge la varangati.

Baada ya sakata hilo gazeti hilo lilimsaka Mama Wema ili kupata ukweli wake ambapo alifunguka haya kwa upande wake:

Hakuna mwanaume yeyote ambaye Wema amenitambulisha hivyo ndiyo maana nilimtimua. Naona na kuyasikia haya mambo kwenu waandishi, lakini hakuna mtu ambaye mimi namfahamu yupo na mwanangu”.

Lakini pia mwanaume ambaye alikuwa katikati ya sakata hilo alisakwa na kufunguka ambapo amekana kabisa taarifa hizo:

Si kweli kwamba mimi nimegombana na huyo mama kwa sababu eti ya luku, mimi nashindwa kununua luku ukiniangalia? Huyo mama hakutaka niwe karibu na mwanaye kwa madai sijui hayuko vizuri anaumwa”.

GPL pia wameripoti kuwa Wema na mwanaume huyo kwa sasa wameachana na Wema tayari yupo na jamaa mwingine ambaye hataki kabisa kumuweka hadharani.

Mbasha Akiri Kumkubali Wema, Amponda Mobetto

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ameibuka na kudai Wema Sepetu ndio Tanzania Sweetheart pekeee na sio vinginevyo.

Emanuel amesema hayo baada ya kuibuka kwa mjadala mzito katika siku za hivi Karibuni baada ya mashabiki kutaka kumvua cheo cha Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu na kumvalisha Hamisa Mobetto.

Katika Interview yake na Gazeti la Ijumaa, Mbasha alisema kuwa kwa upande wake, Tanzania Sweetheart kati ya warembo hao wawili, ni Wema kwani ndiye anayestahili na hilo halina hata mjadala.

Hilo jina linamfaa aliyekuwa nalo tangu zamani (Wema), kwani ndiye aliyepewa hilo jina, kwa hivyo acha tu aendelee nalo kwa sababu ndio linampendezea”.

Siku za hivi Karibuni Mbasha aliingia katika vita kali na mashabiki wa Mobetto baada ya kuweka picha yake akiwa anapaa na ungo kufuatia tuhuma za uchawi.

Wema Sepetu- Nina Kitu Cha Ziada Ambacho Wengine Hawana

Muigizaji wa Bongo movie Madam Wema Sepetu ameibuka tena katika jitihada za kulitetea Jina lake la Tanzania Sweetheart na kusema ana kitu ambacho wengine hawana.

Kwa wiki kadhaa sasa Wema amekuwa Kwenye vita kali katika harakati za kutetea Jina lake la Tanzania Sweetheart ambapo hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashabiki kudai hana vigezo vya Jina hilo Tena na kutaka Hamisa kuwa Tanzania Sweetheart.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la  Risasi Jumamosi, Wema amesema  hawezi kustaafu kutumia jina hilo kwa sababu wakati anapewa na mashabiki wake wa jijini Arusha, hakuambiwa kama kuna kustaafu hivyo jina hilo ni lake na ataendelea kulitumia.

Kwani kuna kustaafu? Sasa nani mwingine atumie jina hilo wakati Tanzania Sweetheart ni mmoja tu? Kwanza akianza kulitumia mtu mwingine mashabiki watakubali? Kila kitu kinaenda na mazoea, watu wamenizoea mimi na nitabaki kuwa mimi tu na hakuna kama mimi“.

 

Aunty Ezekiel Ajibu Tuhuma Za Kumlipizia Kisasi Wema

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amejibu tuhuma ambazo zinemuwndama baada ya kutoonekana katika sherehe ya shoga yake mkubwa Wema Sepetu.

Gazeti la zamani linaripoti kuwa watu wa karibu wa Aunty wamedai Msanii huyo hakufika Kwenye Sherehe kwa ajili kumlipizia kisasi Wema ambaye hakufika Kwenye hafla yake siku za nyuma na sio k amna nguo yake kiharibika kama alivyosema mwanzoni.

Hakuna cha nguo kuharibiwa wala nini sema Aunt kaamua kumlipizia kisasi Wema kwa sababu naye hakuenda kwenye uzinduzi wa filamu yake iitwayo Mama,” 

Baada ya Tuhuma hizo Aunty aliyafutwa na gazeti hilo na alifunguka na kusema:

Sikuwa na sababu yoyote ya kunifanya nishindwe kufika kwenye sherehe ya Wema kwani nimeshirikiana naye hatua zote lakini kilichonikuta ndiyo hicho cha nguo na wala sijamlipizia chochote.

Kwangu alichelewa tu na mwisho tulionana na picha alipiga, watu wanafananisha tukio la Idris ndiyo fundi alimharibia nguo Wema hakufanikiwa kufika”.

Wema alipotafutwa alifunguka na kusema anaamini Aunty hakufika kwa sababu ya dharura na sio kingine:

Aunt aliniambia kuwa hatoweza kufika kwa kuwa amepata dharura lakini tulishirikiana katika kila kitu sasa anilipizie kisasi kwani mimi nina tatizo naye jamani! Dharura ni kawaida kwa binadamu na nilimwelewa”.

 

Aunty Ezekiel Ataja Sababu Ya Kutoenda Kwenye Sherehe Ya Wema

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameweka wazi sababu ya kutoonekana Kwenye Birthday party ya rafiki yake kipenzi Wema Sepetu iliyofanyika siku chache zilizopita.

Siku ya Jumapili kulikuwa kuna bonge la party ya Birthday ya Wema Sepetu ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao lakini kati ya watu hao mtu ambaye alikosekana ni rafiki kipenzi wa Wema ambaye ni Aunty Ezekiel.

Aunty kutohudhuria kulizua maneno mengi ikiwemo watu kufikiri labda wawili hao hawana maelewano.

Kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari Katika usiku wa Jibebe Challenge, Aunty amefunguka na kusema sababu iliyomfanya asihudhurie ni kukosa nguo ya kuvaa.

Kilichotokea ni kwamba kila kitu ambacho kilifanyika tulishirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho yaani kuanzia kutoa kadi mpaka mwisho Lakini pia mwishoni fundi akaharibu nguo yangu ikabidi nilale nyumbani hamna kingine”.

Aunty Ezekiel amekana tetesi za kuwa hajahudhuria sherehw ya Wema kwa sababu amemlipizia kwa sababu kama utakumbuka siku za nyuma Kwenye uzinduzi wa movie ya Aunty ya ‘Mama’ Wema naye hakuhudhuria uzinduzi huo Mlimani City akasema nguo yake iliharibiwa na fundi.

“Sina Bifu na Mobetto Lakini Nampenda Wema”-Diana Kimary

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary amefunguka na kudai hana bifu wala hamchukii Hamisa Mobetto ila tu anampenda sana Wema Sepetu.

Diana Kimary ambaye siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na Ukaribu sana na Wema ameweka wazi kuwa watu wengi wanadhani yeye ana bifu na Mobetto kwa sababu yuko na Wema jambo hilo sio la kweli.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Diana ambaye hivi sasa yupo karibu na Wema alisema watu wengi wanajua ana bifu na Mobeto, lakini wanashindwa kuelewa anapoweka vitu vyake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram havilengi kumsema mtu.

Simchukii na wala sina tatizo na Hamisa (Mobeto)kama watu wanavyotengeneza kwenye mitandao, bali wakiona namuweka Wema ni kwa vile nina mapenzi kama yote kwake pia hata nikiandika ujumbe simsemi mtu”.

Wema na Mobetto wametajwa kuingia katika bifu zito kwa sababu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ ambapo mashabiki wamedai wamemvua Jina hilo Wema na kumvalisha Mobetto jambo ambalo Wema amepingana nalo.

Rc Makonda Amtetea Wema Kuwa Tanzania Sweetheart Amtaka Mobetto Awe Buguruni Sweetheart

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Mh. Paul Makonda ameibuka na kumkingia kifua Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu na kusema analistahili Jina la Tanzania Sweetheart na sio Hamisa Mobetto.

Kwa wiki chache zilizopita Wema Sepetu amekuwa akifanya interviews mbali mbali na amekuwa akibainisha kuwa yeye ndiye Tanzania Sweetheart na sio Mobetto kama mashabiki zake ambavyo wamekuwa wakilazimisha.

Siku chache zilizopita akiwa katika Birthday Bash ya Wema iliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City, Makonda aliweka wazi kuwa Wema ndiye Tanzania Sweetheart pekee ila kama wengine wanalitaka hilo Jina wanaweza kuwa Buguruni Sweetheart.

Wema ni Tanzania Sweetheart kwa sababu kuna vigezo, na kwanza hujiiti Jina mwenyewe, watu wanakupa Jina kama alivyopewa na Baba yake na mama yake Jina Tanzania Sweetheart wengine wanaweza kuwa Buguruni Sweetheart sio dhambi au Manzese Sweetheart”.

Vita kali ya Jina la Tanzania Sweetheart ilianza baada ya mashabiki Mtandaoni kusema wanamvua Jina hilo Wema na kumpa Mobetto kwa sababu Wena amepoteza umaarufu wake na kuwachukiza mashabiki zake kwa matendo yake ya mitandaoni.

Matukio Katika Birthday Party ya Wema Sepetu.

Halima yahaya moja ya wasanii walioalikwa ktaika usiku wa party hiyo.

Jacob Steven nae alikuwepo.

Waandishi wakimsubiri Wema ashuke wenye gari tayari kwa kuinga ukumbiki.

 

 

Mama Wema akizungukwa na waandishi wa habari.

Van Vicker ambae alisafiri kutoka Nigeria  kumsapoti Wema.

Van Vicker na Wema wakiingia ukumbini.

Wema akionekana mwenye furaha.

Wema akiwa na Van vicker