Ali Kiba na Mkewe Amina Wamkaribisha Mtoto Wao Wa Kwanza

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba na mke Wake Bi. Amina Khaleef hatimaye wamefanikiwa kupata Mtoto wao kwanza.

Ali Kiba ametangaza habari hiyo njema Kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo ameweka mkono na mguu wa Mtoto huyo kuonyesha ujio Wake siku ya jana.

Ali Kiba ameweka wazi kuwa Mtoto Wake huyo ni Jinsia ya kiume. Huyo ni Mtoto wa nne wa Ali Kiba Lakini atakuwa ni Mtoto wa kwanza kwa mkewe Amina.

“Mimi na Mke Wangu Amina Tunatarajia Kupata Mtoto Mwakani”-Ali Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke Wake Amina Khaleef wanatarajia kupata Mtoto wao kwanza mwakani.

Baada ya fununu za muda mrefu hatimaye Ali Kiba ameweka wazi kuwa mke Wake Amina ni mjamzito na wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza mwakani Baada ya kufunga ndoa mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Radio Jambo ya Nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA , Ali Kiba alifunguka haya kuhusu ujauzito wa mke wake:

Katika dini yetu tunaamini ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise, atakua Mtoto wangu wa nne” 

Lakini pia Kiba ameweka wazi kuwa huyu atakuwa ni Mtoto Wake wa nne kwani tayari ana Watoto watatu na wanawake wengine aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano siku za nyuma.

“Tangu Nimeoa Mabinti Wamepunguza Usumbufu”- Ali Kiba

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa tangu ameoa Miezi michache iliyopita anaona mabadiliko makubwa kwani mabinti wamekuwa hawamsumbui kama alivyokuwa single.

Kama ilivyo kwa wasanii wengi maarufu ni kawaida kwa warembo kujigonga kwao kutokana na labda umaarufu au hata pesa ambazo wanakuwa nazo na Ali Kiba aliwahi kukiri kukutana na changamoto kama hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Al Kiba amefunguka kuwa tangu amefunga ndoa amebadili tabia yake na kwa saaa anamuheshimu sana Mke wake.

Lakini pia Kiba amekiri kuwa usumbufu  aliokuwa anaupata kutoka kwa mabinti ambao walikuwa wanamtongoza umepungua kabisa kwa sababu wanajua hivi sasa ameoa.

Ali Kiba ameweka wazi hata kwa upande wake binafsi amebadilika kwani amekuwa akijiheshimu na kumuheshimu Mke wake tofauti na  alivyokuwa kabla hajaoa ambapo wasichana walikuwa wanamsumbua wakijua ya kwamba labda wanaweza  kupata nafasi ya wao Kuolewa kitu ambacho kwa sasa hakipo kabisa.

Esha: Jokate Usinichukie Mimi Ni Bendera Fuata Upepo

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameendelea kumtolea povu zito mwanadada Jokate Mwegelo huku akimsihi asimchukie kisa Ali Kiba kuoa kwani yeye ni bendera fuata upepo tu.

Siku chache zilizopita Esha alimtuhumu Jokate kwa kumchukia kisa na mkasa alihudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mkewe Amina Mombasa nchini Kenya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Esha amedai kuwa  amesikia kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba mwanamitindo huyo anamchukia kwa sasa kutokana na kuwa karibu na Kiba kwenye harusi yake na mrembo Amina Khaleef.

Kama ni kweli Jokate atakuwa ananichukia kisa mpenzi wake wa zamani Kiba kuoa kama watu wanavyosema, basi atakuwa ananichukia bure“.

Lakini pia Esha ameweka wazi kuwa sio kosa lake kwani yeye ni kama bendera fuata upepo anafanya alichokuwa anaelekezwa kwani haikuwa harusi yake:

Mimi ni kama bendera tu nafuata upepo kwa hiyo wa kumchukia ni Kiba mwenyewe aliyeamua kumuacha yeye na kuoa mtu mwingine, na wala si yeyote yule ambaye yupo karibu na Kiba”.

Tangu Ali Kiba Afunge ndoa aliyekuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo hajaposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii.

Esha Buheti Amlipua Jokate na Kudai Anaona Wivu Baada Ya Alikiba Kuoa

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kumtupia tuhuma nzito mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ baada ya kudai kuwa tangu amehudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na Amina mrembo huyo amekata naye mawasiliano.

Esha ni mtu ambaye ana ukaribu sana na familia ya Ali Kiba na hata kwenye harusi ya Ali Kiba alionekana mwanzo mwisho akishitiki kwani alienda hadi Mombasa.

Hapo nyuma kuna taarifa ilisambaa kuwa Esha ndiye aliyemtafutia mchumba huyo Ali Kiba (Amina) ingawa mwenyewe alishakataa na hata Ali Kiba na Amina waliweka wazi walikutana wenyewe Kwenye ndege.

Kwenye mahojiano na Shilawadu  Esha anadai kuwa tangu ahudhurie ndoa ya Ali Kiba basi Jokate kama kama kamkasirikia kwani zamani alikuwa anaangalia status zake WhatsApp lakini saivi ameacha.

Mimi na Jokate tukiongelea kuhusu kukutana basi tulikutana kama mara tatu tu lakini kama yeye ananichukia ni yeye tu lakini mimi siwezi kumchukia kwa sababu sio mimi niliyeoa aliyeoa ni Ali kiba, ingawa kabla alikuwa ana view status zangu lakini tangu niende Mombasa sijaona aki view tena Lakini sikuhangaika kuangalia kama ameniblock au vipi”.

Jokate hajaonekana aliposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii tangu harusi ya Ali Kiba hivyo pia hajajibu tuhuma hizi.

Ex wa Ali Kiba Sabby Angel Amtolea Povu Zito Staa Huyo

Muigizaji wa Bongo movie Sabby Angel ameibuka na kumtolea povu zito Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba baada ya kauli tata aliyoitoa kuhusu warembo wa Bongo.

Sabby Angel alishawahi kukiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ali Kiba siku za nyuma kidogo ameshindwa kuvumilia na kumpa ukweli Staa Huyo aliyeoa hivi karibuni.

Hivi karibuni Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ali Kiba alifunguka kuwa sababu ya yeye kuwaacha warembo wote wa Bongo na kwenda kuoa Kenya ni kwa sababu wasichana wengi wakibongo wanaendekeza vigodoro na wengi sio wasomi.

Sabby Angel ameonekana kukasirishwa na kauli hiyo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani na ameandika ujumbe huu:

Ni jambo la Kheri kwa Ali K kuoa lakini sijapenda comment yake eti kusema eti Tanzania hakuna wanawake wasomi wa kuoa.

Bonafsi kama mtu umeamua kuoa we oa tu kwa manufaa yako lakini sio kukashifu wanawake wote. Kwani hapo wakati anatoka na hao wanawake wa Kitanzania hauona hayo mapungufu? Kwani watu wanaoa vyeti? Wanaoa kukimu mahitaji yao binafsi na kuzaana?.

Hiyo ni kumaanisha hata wazazi wetu wa kike na hata mama yake ni wale wale it is very immature”.

Ali Kiba alifunga ndoa na binti kutoka Mombasa Kenya wiki chache zilizopita.

Ali Kiba- Nilivyokutana Tu na Amina Nilijua Nataka Kumuoa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka kwa mara ya kwanza kukutana na mke wake Bi. Amina Khalef alijua wazi kuwa ndiye mwanamke wa kuoa.

Kwenye Interview Baby kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Amina ameweka wazi kuwa yeye na Ali kiba walikutana Kwenye ndege na wakabadilishana namba na kuwa marafiki:

Mara ya kwanza kukutana na  ilikuwa kwenye ndege na hatukuzungumza mara ya pili Kaka yangu binamu ndiyo alinikutanisha nae maana walikuwa marafiki sana na hapo ndiyo tulianza urafiki wetu kabla ya kufika hapa tulipo“.

Hata hivyo, Bi. Aminah amesema kuwa Alikiba ndiye aliyeanza kumtamkia kuwa anampenda na yeye akamwambia kama ni kweli aende kwa wazazi wake akajitambulishe.

Ali Kiba na yeye ameweka wazi kuwa alivyokutana na Bi Amina mara moja akajua yule ndio mke wa kuoa hivyo mara moja akamfuata gavana wa Mombasa Joho akamwambia anataka kuoa.

Yeah Joho ni mtu ambaye aliniongoza sana kwenye maswala ya msingi, kama nilivyokuwaambia kwenye maswala ya dini, mimi na mke wangu tulikutana Nairobi, tukajuana tukaanza kuwasiliana.

Tulivyokuwa marafiki na Hassan nikamwambia kaka kuna msichana anakaa hapa, akaniambia kama ni kuoa basi process zifuatwe nilipoonja Mo Faya tu!, nikaoa hapo hapo,

Bongo Movie Wamwaga Povu Baada Ya Kukosa Mualiko Kwenye Harusi Ya Alikiba

Wiki iliyopita ilikuwa ni harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mpenzi wake Amina Khalef iliyofanyika Kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Global Publishers inaripoti kuwa Wasanii wa Bongo movie wamemjia juu Ali Kiba kwa kitendo cha kutowaalika Kwenye harusi yake.

GP inaendelea kudai kuwa Msanii mmoja maarufu ameibuka na kudai wameumizwa na kitendo cha kutengwa kabisa Kwenye shughuli hiyo:

Yaani harusi ilipopita, tukafanya tathimini na kuangalia idadi ya watu waliohudhuria. Tukagundua wengi ni mastaa wa Bongo Fleva, watangazaji na wadau wengine wasiohusiana na Bongo Muvi.

Kwa kweli tukagundua jamaa ni mbaguzi. Hakuwa fair, alipaswa kuwaalika angalau mastaa wachache wa Bongo Muvi kuonesha ushirikiano, mbona sisi kwenye mambo yetu huwa tunaalika watu wote?”.

Inadaiwa gazeti la Amani lilifanya uchunguzi na kugundua Kinabalu waraka ulioandikwa na wasanii hao, uliosomeka hivi:

Sisi Bongo Muvi tumekuwa tukishiriki matukio mengi ya wasanii wa Bongo Fleva iwe harusi, misiba na hata maradhi, lakini kwa tukio la AliKiba tumejiuliza sana, wasanii kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel, JB, Dk. Cheni, Ray, Richie, Gabo nk. ambao hata wachache chini ya hapo walifaa kualikwa.

Tulimuona Esha Buheti lakini najua yule ni mwana familia kwa upande flani, sijajua ni kipi kimetokea kiasi cha kutokualikwa sisi, lakini kwenye video zao wamekuwa wakitualika ili tupendezeshe video zao, na hata kututaja ndani ya nyimbo zao,”

Lakini pia gazeti hilo liliwahoji wasanii kadhaa ili kupata mtazamo wao juu ya hilo na waliongea haya:

Aunt: Nisingependa kabisa kuongelea kuhusu hilo.

Wolper: Kwa kweli sikupewa mualiko lakini pia nilikuwa naumwa.

Steve Nyerere: Siwezi kulalamikia kutoalikwa kwenye harusi japo najua hayo mambo ya utimu yanaweza kuingia.

Ali Kiba alipotafutwa kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo hakuweza kupatikana.

Ali Kiba Azindua Kinywaji Chake Siku Ya Harusi Yake

Staa wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amezindua rasmi kinywaji chake cha Energy siku ya jana katika hoteli ya Serena ambapo ndipo reception yake ya harusi ilifanyika.

Ali Kiba ametangaza Habari hiyo kuwa amekuwa balozi rasmi wa kinywaji kinachoitwa Ali Kiba Mofaya Energy Drink ambacho kimesindikizwa kwa picha yake kwenye chupa.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Ali Kiba atakuwa balozi wa bidhaa kadhaa mbali na fani yake ya muziki.

Lakini pia mashabiki zake wote waliokuwepo Kwenye ukumbi huo walipata nafasi ya kuonja kinywaji hicho kwani kilipatikana kwa kila mmoja aliyekuwa Ukumbini humo.

Tazama Picha Za Harusi Ya Alikiba na Abdu Kiba

Siku ya jana tarehe 29/04  Staa wa muziki wa Bongo fleva AliKiba na alitimiza sherehe ya mwisho ya ndoa yake na mrembo kutoka Mombasa Amina Lakini pia harusi hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Serena Hotel.

Lakini pia kilichovutia watu wengi haikuwa tu sherehe kwa ajili ya Ali Kiba na mkewe Lakini pia mdogo wa ALikiba Mwanamuziki Abdul Kiba ambaye na yeye alionekana na mke wake Ruwayda.

Harusi hiyo ilirushwa Love Kwenye chanel ya Azam na pia ilihudhuriwa na mastaa mbali mbali kama vile Mama Salma Kikwete, Ummy Mwalimu, Idris Sultan, Vanessa Mdee na Mimi Mars na wengineo.

Hizi ni baadhi ya picha za harusi hiyo:

 

Zabibu Kiba Amtaka Wifi Yake Awe Mvumilivu Kutokana na Kazi Ya Ali Kiba

Jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kabisa kwani ilikuwa ni ndoa ya Ali Kiba na mpenzi wake Amina ndoa iliyokuwa gumzo jiji zima.

Ndoa hiyo ilifungwa nyumbani kwa wazazi wa  Amina huko Mombasa nchini Kenya na baadae sherehe ilifanyika usiku katika ukumbi wa Diamond Hall na kurushiana live Azam Tv.

Dada wa Alikiba amayejulikana kama Zabibu Kiba amemfungukia mazito wifi yake huyo na kumtaka kikubwa awe mvumilivu hasa kwa sababu kazi ya Ali Kiba ni Mwanamuziki kazi yenye changamoto:

Mimi namkaribisha Amina nyumbani namkaribisha kwenye familia yetu kikubwa ni uvumilivu hasa kwa sababu anakuja kazi ya mumewe na changamoto ni nyingi na nafikiri alishaanza kukutana nazo na sidhani kama zitamshinda na sisi kama familia tumemkubali na tu nampenda kama alivyopendwa na mume wake 

Ujumbe Wa Diamond Kwa Ali Kiba Baada Ya Kuoa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameweka bifu pembeni na kumpongeza msanii mwenzake Ali Kiba baada ya kufunga ndoa siku ya jana.

Diamond na Alikiba wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu ambapo lilisababisha kugawa mashabiki zao lakini hivi katibuni Diamond aliweka wazi kuwa hana bifu na Ali Kiba.

Jana ilikuwa siku ya shamra shamra kwa Alikiba kwani alifunga ndoa mjini Mombasa Kenya na mkewe Bi. Amina na ilikuwa ni harusi iliyozua gumzo sana Kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond hakuona hiyana kumpongeza Ali Kiba na alimtumia ujumbe wa pongezi Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Wadau nimeambiwa King Kiba kaoa leo mumfikishie salamu zangu za ndoa njema na maisha yenye furaha Amani na baraka tele”.

Baada ya kumtumia ujumbe huo pia Mama mzazi wa Diamond na familia yake wote walimposti Ali Kiba na kumpongeza.