“Amber Lulu Ananiendea Kwa Waganga Kuniloga”- Amber Rutty

Msanii wa Bongo fleva aliyejizolea umaarufu kwa video yake chafu ya ngono kwenye Mitandao ya kijamii Amber Rutty ameibuka na kudai kuwa msanii mwenzake Amber Lulu anamuendea kwa waganga.

Amber Rutty na Amber Lulu wamekuwa hawana maelewano kwa muda mrefu ambapo kisa kilikuwa Amber Lulu aliona kama Amber Rutty anamuiga swaga zake kuanzia kumuiga jina na hata kumuiga tattoo zake alizochora mwilini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Amber Rutty amemtolea povu zito Amber Lulu na kudai amamuendea kwa waganga wa kienyeji kwa majaribio ya kutaka kumloga.

Amber Lulu amedai kuwa hawezi kumpenda Lulu kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa akijaribu kumshusha na kumharibia jina lake Lakini Baada ya kushindwa kwa njia hiyo sasa Hivi ameanza kumuendea kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kumloga asifanikiwe.

 

Amber Lulu Aanika Utajiri wake

Mrembo kutoka kiwanda cha Bongo fleva, Amber Lulu ameweka wazi kuwa ana pesa ambayo iko kwenye akaunti yake, pesa ambayo haitokani na mziki bali mishe zake za kimaisha.Amber Lulu anaamua kufunguka baada ya kuona kuwa

Akizungumza na mwandishi wa habari Lulu amesema “kwenye akaunti yangu kuna zaidi ya million 10 ambayo aitokani na mziki watu wajue hivyo”

Itakumbukwa kuwa Amber Lulu alianzia kwenye kuuza sura kwenye video za mastaa hapa bongo yaani (video vixen) na hatimae akaingia kwenye gemu ya mziki na ameshatamba na vibao vyake kama ‘Watakoma’ ‘Jini Kisirani na vingine kibao

Amber Lulu Alizwa Tena na Mapenzi

Mwanadada Amber Lulu ameonekana kuumizwa tena na maenzi ingawa  hajataka kuweka wazi kwanini kile alichkionyesha katika ukurasa wake wa instagram alikuwa akikimaanisha.

Katika ukurasa wake huo, mwanadada Amber Lulu aliweka  picha yenye kutukana kwa kiais kikubwa sana swala la mapenzi na kuonekana kama vile ni kitu ambacho kiemuumiza sana.

Katika ukurasa wake hata  baada ya kuweka picha hiyo mashabiki walianza kumuuliza kuhusu swala la kuyatukana mapenzi , na kwanini amekuwa akionekana kama mtu mwenye uchungu sana na swala hilo.

ikumbukwe kuwa  Amber Lulu alikuwa katika mahaba mazio sana na mwanaume wake prezzo kutoka kenya ambae alikuwa akimsifia kuwa ndie mwanaume mwenye kuma furaha muda wote tofauti na wale wa nyjma ambao walikuwa wakipa stress kila siku.

 

 

 

Amber Lulu Akiri Kutamani Mtoto Lakini Hali Ya Kiuchumi Inamzuia

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu ameibuka na kuweka wazi kuwa anatamani sana kuzaa Mtoto Wake mwenyewe lakini hali kiuchumi ineluctable kikwazo kwake.

Amber Lulu amekiri kuwa anatamani sana kuitwa mama Kama ilivyo kuwa kwa marafiki zake wengine na hata wasanii wenzake lakini hawezi kwa sababu anaona kabisa kuwa ramani hazisomeki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Amber alisema kuwa iwapo atapata mwanaume wa kuishi naye ambaye hana longolongo, ataanzisha naye familia lakini kwa sasa maisha yake ya kimapenzi hayaelewielewi.

Siyo kwamba sipendi watoto jamani lakini naona bado ramani haijasomeka kabisa maana siyo nazaa halafu hata ‘pampers’ ya kumvalisha mtoto nakosa, kitu hicho sikipendi kabisa, bado naangalia kwanza, kwani kuzaa sio fasheni”.

 

 

Amber Lulu Afunguka Baada Ya Kupata Ajali Mbaya

Video vixen na msanii wa Bongo fleva mrembo Lulu Eugen maarufu kama Amber Lulu amefunguka mara baada ya kunusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia jana.

Siku ya jana Amber lulu aliweka wazi kuhusu ajali mbaya ya gari iliyomkuta ingawa alikiri kupata majeraha kidogo lakini uoga alioupata ulikuwa mkubwa zaidi.

Kwenye exclusive interview na Global Publishers, Amber Lulu amefunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametoka salama kwenye ajali hiyo iliyotokea juzi kati usiku wakiwa njiani kuelekea katika siku ya kuzaliwa ya msanii mwenzao, Messen Selekta.

Kwa kweli ilikuwa ajali mbaya sana, kwa sababu hata ukiiangalia gari tuliyokuwa tumepanda huwezi kuamini kama kuna watu wamepona, imeharibika vibaya, namshukuru sana Mungu kwa sababu nimetoka salama japo nina jeraha dogo mkononi”.

 

 

Amber Lulu Amsusuia Jina Amber Rutty

MwanadadaAmber Lulu amefunguka na kusema kuwa hataki tena kuitwa Amber kama ambavyo alikuwa akiitwa hapo awali kutokana na ukweli kuwa watu wanaokuja baaada yake wamekuwa wakilitumia jina hilo vibaya na kumchafua yeye na jina lake la Amber.

Maneno ya Amber Lulu yamekuja baada ya mwanadada Amber Rutty kukutwa na skendo ya kusambaza picha akiwa na mpenzi wake faragha na pcha hizo kufanya jina la Amber Rutty kuchafukliwa sana na habari hizo.

Amber Lulu anasema hata kaka mwanadada huyo anafanya mambo hayo kwa kiki ni vibaya na inachafua sana  taswira ya wanawake   na pia neno AMBER  linemkuwa likiwafanya mashabiki wajue kuwa ni jina lake hivyo kama ni kiki basi anamuachia jina lake mwanadada huyo.

wengi wamekuwa wakijua kuwa ni mimi na kwa hilo amekuwa akinivunjia heshima , na kwa sababu ya hilo naona ni bora kumuachia hilo jina la amber ahanagaike nalo yeye mwenyewe.

Pamoja na kwamba Amber rutty amekuwa akikiri kufaynya jambo hilo lakini pia alisema kuwa mpaa sasa hajui aliyefanya hivyo kutokana na kwamba simu iliyokuwa na video hiyo iliiibiwa.

Amber Lulu Anasurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya.

Mwanadada Amber lulu kutoka katika kiwanda cha bongo fleva amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya akiwa anaenleka katika party ya producer Mesen selekta .

Hata hivyo ambaer anaetamba sana na wimbo wake wa jini kisirani anasema kuwa anamshukuru Mungu kwa sababu mpaka sasa hali yake inaendelea vizuri.

Akiongea na waandishi wa habari Amber lulu anasema ” wiki hii imekuwa ya misukosuko kwangu sana,lakini jana kwenye mida ya saa 7 tulipata ajali tulikuwa tukielekiea kwenye birthday party lakini shukuru mungu tulitoka salama ingawa mimi nilibanwa sana mkono.

Mbosso Alinisaidia Nilipotaka Kubakwa-Amber Lulu

Video queen na Msanii wa Bongo fleva Lulu Eugene maarufu kama Amber Lulu amefunguka na kudai Msanii mwenzake Mbosso kutoka WCB alimsaidia alipotana kubakwa miaka ya nyuma.

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Mbosso, Amber Lulu ni mmoja kati ya wasanii ambaye amemposti Kwenye mitandao ya kijamii na kumtakia heri lakini Kwenye posti yake Amber Lulu amemshukuru Mbosso na kutoa siri nzito.

Amber ameweka  wazi kuwa miaka ya nyuma Mbosso alishawahi kumsaidia alipokuwa anataka kubakwa Lakini pia hajawahi kumwambia mtu yoyote.

Kupitia ukurasa  wake wa Instagram, Amber Lulu ameandika:

Nuh Mziwanda Alivunja Mahusiano Yangu na Prezzo- Amber Lulu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ amefunguka na kudai kuwa Msanii wenzake Nuh Mziwanda ndiye sababu kubwa ya Penzi lake na Prezzo kufa.

Amber Lulu na Prezzo walikuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu lakini mapenzi yao yaliingia doa mara baada ya video iliyomuonyesha Nuh Mziwanda na Amber Lulu wakifanya yao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya  katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Amber amekiri kuwa kuna kipindi alikuwa karibu na Nuh Mziwanda na baadaye picha zake zilisambaa mitandaoni  wakiwa karibu wakijiachia kimahaba.

NUH NI MSHIKAJI TU ILA NDOA YANGU NA PREZZO ALIMAIND ILE KUKISIANA KISIANA NA NUH MZIWANDA JAPO NI MAKOSA TU KWAKUWA MIMI NI KIJANA NA YEYE YUPO MBALI MI NIPO HUKU MUDA MWINGINE NAHITAJI VITU VINGI LAKINI KUTELEZA KUPO  ILA NILIJITAHIDI SANA KUOMBA MSAMAHA SANA NIKAONA KAMA KANIKAZIA HIVI MWISHO WA SIKU NIKAONA NAOMBA MSAMAHA SANA KWAAJILI YA NINI NIKAONA FRESH TU KAMA UMEAMUA POA WACHA NIISHI MAISHA YANGU”.

Amber Lulu amesema hivi sasa ameamua kuwa Single ili apate muda wa kufanya kazi zake kwa uhuru bila kujali wanaume.

KWA SASA HIVI NIPO SINGLE SIHITAJI BOYFREND WALA MCHUMBA MUDA NINAOUPOTEZA KWAO NI BORA NIFANYE MAMBO YANGU ILA IKIFIKA MUDA NIKIMTAKA MTU NAMLIPA ARAFU TUNAMALIZANA FRESH SIHITAJI MUDA WA KUSUMBUANA WALA HUYO NUH HATA SIMTAKI YEYE MWENYEWE MAISHA YAKE YANAMSHINDA”.

Nuh Mziwanda Hawezi Kunitunza :-Amber Lulu.

Mwanadada Amber lulu  amefunguka nan kukanusha tetesi zinazondelea juu yake kuhusu mahusiano yake na msanii mwenzake Nuh mziwanda ambae hapo awali aliwahi kuwa na mahusiano na mwanadada shilole.

Amber Lulu anasema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu swala hilo na kusema kuwa hakuna kitu kama icho kinaweza kutokea kwa sababu hata familia yake inaweza kumshangaa kwa hilo.

Amber Lulu anasema kuwa sababu kubwa mabayo inamfanya aseme hawezi kuwa na mahusiano na Nuh Mziwanda ni kwa sababu hana pesa za kuweza kumtunza yeye na hata ndugu zake wakisiskia hivyo wanaweza kumshangaaa.

 

Najipendekeza Wasafi ili Niwe Msanii Wao :-Amber Lulu

Mwanadada Amber Lulu  amefunguka na kusema kuwa kwa siku nyingi amekuwa akitamani sana kufanya kazi na  wasanii wa kundi la WCB  kutokana na kujituma kwao kufanya kazi lakini pia kwa kazi zao nzuri ambazo kila mtu amekuwa akiziona .

amber lulu anasema kuwa na ndio maana amekuwa akikaa karib na WCB ili kujipendekeza ili siku moja wamuone ka kumchukua kama msanii wao.

wasafi wanajituma sana na wanajua sana muziki,  na ndio maana najipendekeza ili niwe msanii wao, magari yale yananitia sana uchizi.

Young Dee Akana Kuwahi Kuwa Kwenye Mahusiano na Amber Lulu

Msanii wa Bongo fleva Young Dee ameibuka na kumtolea maneno shombo aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu na kudai hajawahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.

Wawili hao waliingia Kwenye bifu zito siku za hivi karibuni na kurushiana maneno mazito na matusi Kwenye mitandao ya kijamii.

Young Dee ameibuka na kuweka wazi kuwa hajawahi kuwa Kwenye Mahusiano na Amber Lulu yaani hajawahi kuwa girlfriend wake bali alikuwa ni mtu aliyekuwa yupo kwa ajili ya kukutana naye kimwili kila muda anaotaka.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Young Dee amefunguka haya:

Amber hajawahi kuwa girlfriend wangu alikuwa ni bootycall wale watu unawapigia sana kumi usiku tu sasa unamuitaje Ex girlfriend wangu wakati sijawahi hata kukutana naye mchana”.

NIlikuwa nakutana na Amber kipindi kile nakunywa makonyagi tu siku hizi nimeacha pombe sina sehemu za kuktana naye maaana sio level zangu”.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa bifu lake na Young Dee lilianza mara baada ya Amber kukataa kuwa kwenye Mahusiano naye.

Bifu la Amber Lulu na Young Dee Lapamba Moto

Msanii wa Bongo fleva na hitmaker wa Bongo Bahati Mbaya Young Dee ameingia Kwenye bifu zito na aliyekuwa mpenzi wake na msanii mwenzake Lulu Eugenn maarufu kama Amber Lulu.

Bifu la Amber Lulu na Young Dee lilianza Siku za nyuma baada ya Amber kumtuhumu Young Dee kwa kumpa kipigo studio baada ya kumuona akiwa na mwanaume mwingine.

Amber Lulu alimtolea povu zito Young Dee baada ya picha zake za Harusi kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Amber rapa huyo hawezi kuoa kwa sababu hicho si kitendo rahisi na ukiangalia yeye mwenyewe sasa hivi anatamani kuolewa, hivyo kumtaka afanye muziki bila kutengeneza kiki kama anaweza.

Global Publishers lilimtafuta Young Dee Baada ya povu Amber ambapo Meneja alifunguka:

Young Dee hawezi akabishana na mtoto wa kike halafu hata hivyo huyo Amber Lulu hawezi akafanya muziki mzuri bila kufanya kiki na tena ukiangalia kiki zake nyingi ni lazima amtaje Young Dee, kwa sababu anajua kuwa brand kubwa hivyo anaona akimtumia lazima atoboe”.

Amber Lulu naye alifunguka tena kuhusu Young Dee ambapo aliendelea kumtolea shombo baada ya kusema anahitaji kuolewa kwani hawezi kuoa:

Niliongea vile kwa sababu najua Young Dee hawezi akatoa wimbo bila kufanya kiki, anadanganya watu kuoa wakati yeye mwenyewe anahitaji mtu wa kumuoa, halafu ukiangalia kiki ni kubwa kuliko wimbo anaotaka kuutoa yani kiufupi siku hizi muziki wake ushakufa labda ajipange upya“.

 

 

Amber Lulu Adaiwa Kumwaga Matusi Mbele Ya Mashekhe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Jini kisirani’ Amber Lulu amedaiwa kumwaga matusi ya haja mbele ya viongozi wa dini ambao walikuwa safarini.

Global Publishers wanaripoti kuwa Amber Lulu aliongelea maneno hayo machafu alipokuwa kwenye ndege anasafiri kutoka Mwanza kuja Dar Es Salaam ambapo Idadi ya mashehe waliosikia ‘domo’ la msanii huyo likimwaga mitusi ni saba, kibaya zaidi miongoni mwao alikuwepo Mufti wa Tanzania Abubakary Zuberi na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, mashehe wanaoheshimika.

Inadaiwa sakata hilo lilianza baada ya Amber Lulu kuanza kugombana na mtu aliyekaa naye siti moja baada ya kuomba Msanii huyo ahamishwe siti basi kusikia hivyo Amber Lulu alianza kuporomosha matusi mazito kwa Abiria mwenzake.

Kwa nini nikakae Kuna mtu kalipa milioni humu …(tusi zito)” sauti za “astaghfirullah” zikasikika kuashiria kuna watu walikuwa wakiomba msamaha kwa Mungu.

Kuashiria kwamba aliyekuwa akiombewa msamaha zaidi hajitambui akaporomosha tusi tena, kisha akanyanyuka kama mtu anayesema “mtanifanya nini?” Akaaga kwa sauti:

“Naenda chooni nilikirudi huko nataka kumjua aliyeniambia nihamie nyuma… (tusi zito tena) sauti za “astaghfirullah” zikafuatia”.

Haikujulikana kama ni ulevi au ndiyo akili za msanii huyo imepinda alianza kufanya mambo ambayo hayakuwa ya kawaida kwani alipotoka maliwatoni maziwa yake yalikuwa nje na hata sehemu nyeti za mwili zikionekana.

Mwanaume wa Kuishi na Mimi Anahitaji Kuwa na Akili Hata Kama sio Mvumilivu : Amber Lulu

Mwanadada kutoka katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Amber Lulu  siku ya august 02 alikuwa akitambulisha nyimbo yake mpya katika ofisi za Clouds Media, amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye yupo single lakini anataka mwanaume mwenye akili.

Ambaer lulu ambae hapo awali aliwahi kutangaza na kusema kuwa yuko single baada ya kuachana na mwanamuziki Prezzo , anasema kuwa hataki mwanaume mvumilivu yeye anataka mwanaume mwenye akili ili aweze kuishi nae kwa sababu hata yeye ana akili nyingi sana.

Niko single kwa sasa na nafasi iko wazi kabisa, lakini mwanaume ambae nina mtaka inabidi awe na akili sana za kuishi na mimi, maana kuishi na mtu na mimi inahitaji akili sana hata kama hatokuwa na uvumilivu.;-Alisema Amber lulu.

 

 

 

Amber Lulu Asema Hataki Tena Kupoteza Muda kwa Sababu ya Mwanaume.

Tangu mwanadada Amber Lulu atangaze kuwa single hajataka kubadilisha msimamo wake kuwa hataki tena na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote kwa sababu anachoamini kuwa kwa muda wote aliwahi kuwa katika mahusiano kulikuwa kuna kupotezeana kwa wakati kati yake na wanaume wake.

Amber Lulu ambae alikuwa katika penzi zito na msani kutoka kenya prezoo walikua kuachana ghafla baada ya kusambaa kwa picha za mwanaume huyo akiwa na mwanamke mwingine, kitu kilichomuuma sana Amber Lulu, na kuamua kutangaza kuwa yuko single.

Amber Lulu  ameuambia mtandao wa Pro24Djs kwamba amepotezewa sana muda na wanaume ambao hawana msimamo katika mapenzi.

“Kama kutoka kimapenzi na mtu ambaye hajui thamani yako, ndio kitu ambacho huwa nakifikiria kwasababu nimepoteza sana muda,” alisema Amber Lulu. “Huwaga hicho kitu kinaniumiza sana,  muda ambao nilikuwa naupoteza na nguvu ambazo ningeziweka kwenye muziki wangu ningefika mbali sana,”

Aliongeza, “Ndio maana watu wanasema ni bora mtu akupende kuliko umpende, kwa sababu ukimpenda inakuwa ni shida. Vitu kama hivyo vimenipelekea kufanya vitu vya ajabu, unakuwa na watu ambae haujawataka, inakuwa kama ni hasira kwahiyo imenifanya nisitamani kumuona mwanaume yeyote katika macho yangu,”