Cathy Ajivunia Uamuzi Wa Kutokutoa Mimba na Kuwa na Mtoto Mkubwa Sasa

Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya Bongo movie Sabrina Rupia maarufu kama Cathy amewashangaza watu wengi Baada ya kumuonyesha Mtoto Wake wa kwanza.

Cathy alizua taharuki Baada ya kuweka wazi Siri yake kuwa ni mama wa Mtoto mkubwa tu wa kiume ambaye anaitwa Issa mwenye umri wa miaka kumi na Sita kwa sasa.

Kijana huyo aliibua mshtuko hivi karibuni baada ya mama yake  huyo kuanika picha wakiwa pamoja na watu kujiuliza Cathy alimzaa akiwa na umri gani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Cathy ameweka wazi kuwa alimzaa mtoto wake huyo akiwa na miaka 16 hivyo hivi karibuni ndiyo yalikuwa mahafali yake ya kuhitimu digrii ya kwanza ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Huyu ni mtoto wangu wa kwanza, nilimpata nikiwa na miaka 16, namshukuru Mungu sikumdhuru kama mabinti wengi wanavyofanya wakipata mimba za utotoni, sasa nafurahia yaani ndiye huyu tumekua wote, nampenda sana, ni mwanangu, ni kaka yangu, ni mshauri wangu, kifupi ndiyo kila kitu kwangu“.

Ni kawaida kwa mastaa kuficha watoto wao na kudanganya kuwa hawana watoto kwa kuhofia umri wao halisi kujulikana mfano ni mastaa Kama Johari Chagula na Lulu Diva ambao wameshawahi kupata  skendo za kuficha Watoto.

Monalisa Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Uganda

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu Kama Monalisa amepata tuzo nyingine kutoka nchini Uganda Kupitia Sanaa yake ya maigizo.

Monalisa amejipatia Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.

Baada ya kutangazwa kupata tuzo hiyo jana tarehe 08/11/2018 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.

Bi. Fissoo ametoa pongezi hizo ofisini kwake ambapo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako”.

Lakini pia Monalisa alifunguka Baada ya kupokea salamu hizo za pongezi kutoka kwa Bifu ya Fulani Tanzania:

Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha”.

 

Tanzia: Muigizaji Mkongwe, Mashaka Afariki Dunia

Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama ‘Mashaka’ aliyewahi kuigiza katika kundi la Kaole Sanaa group miaka ya nyuma amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi, Oktoba 20, 2018.

Abdallah Ditopile ambaye ni mtoto wa marehemu amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema baba yake aliugua ghafla usiku ndipo wakamkimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu na Ilipofika asubuhi hali yake ikabadilika, madaktari walitupatia rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili Tawi la Mloganzila, wakati tukijiandaa kuita ambulance, akakata roho, baba ametutoka katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.

Mashaka alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Presha pamoja na kisukari ambapo jana alizidiwa gafla na kukimbizwa hospitali ya Amana, madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu ikiwa pamoja na kumuwekea mashine ya kupumulia ya oksijeni.

Mashaka amezikwa siku ya Jumapili oktoba 21 Katika makaburi ya Kinyerezi jijini Dar Es Salaam.

Mwenyezi Mungu Ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

Odama Afunguka Mazito Baada Ya Kuzushiwa Kifo

Muigizaji wa Bongo movie Jeniffer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amenena mazito baada ya kuzushiwa Kifo katika mitandao ya kijamii.

Wiki hii kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuna taarifa ilisambaa kuwa Msanii huyo ameaga dunia taarifa zilizowashtua watu wengi sana.

Odama akielezea kilichotokea ame-screenshot picha za matangazo na kuyaposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kujamii na kuujulisha umma kuwa habari hizo sio za kweli.

Baada ya sakata hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Odama amefunguka na kusema anamshukuru Mungu na Kifo hupangwa na yeye tu na sio mwanadamu:

KIFO KIPO NA HAKUNA ATAKAEKIKWEPA… KILA BINADAMU ATAONJA MAUTI NA KUKAMILIKA KWA MAISHA YETU HAPA DUNIANI…. LAKINI PIA HATA KAMA HUMPENDI MTU UNAMCHUKIA IWE ALIKUTENDEA UBAYA AU UMEAMUA TU KUMCHUKIA SIO VIZURI KUMUOMBEA KIFO TENA UKAONA HAITOSHI BASI UNAWEKA MATANGAZO MITANDANDAONI…. NAKUSHUKURU WEWE ULIEAMUA KUFANYA HILI.. NAJUA UNANIONGEZEA UMRI WA KUISHI.. NA NIKUAMBIE TU KUA MIMI NI MZIMA WA AFYA NA NINAISHI KWA KUDRA ZA MUNGU.. NITAKUFA TU PALE SIKU YANGU ITAKAPOFIKA MUNGU ATAKAPOAMUA KUNICHUKUA LAKINI SIO KWA KUTAKA WEWE…. SIJUI NILICHOKUKOSEA MPAKA KUFIKIA KUNITANGAZIA KIFO… NAKUOMBEA MAISHA MAREFU ILI UENDELEE KUNIONA NIKIVUTA PUMZI YA MUNGU…. BINADAMU SISI LAITI TUNGELIJUA KUA SI KITU KABISA TUNGEACHA CHUKI ZISIZO NA SABABU…. ASANTE MUNGU KWA KILA KITU“.

 

“Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kupasua kuwa habari ya wasanii wa Bongo movie  kama Wema, Aunty, Shamsa, Faiza, Maimatha na Wolper Kwenda Kwenye party ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu.

SIku chache zilizopita Kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, Babu Tale aliwaalika Bongo Movie kwa ajili ya kwenda South Africa Kwenye party ya Tiffah South Africa Lakini mara moja Zari aliwapiga stop.

Baada ya mgogoro wasanii hao kila mmoja ameonekana kughaili Kwenda huku wengine wakidai kulikuwa hakuna Safari bali ilikuwa ni kiki tu.

Gazeti la Amani, liliamua kuwasaka baadhi ya mastaa waliokuwemo kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja aliongea la kwake kama ifuatavyo;

Faiza Ally alisema kuwa alijua wazi kuwa hatakwenda kwa sababu Zari ‘alishamblock’ siku nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mimi baada ya kutangaziwa vile tu nilijua siwezi kwenda kwa sababu Zari alishaniblock siku nyingi, sasa huwezi kwenda kwa mtu ambaye alishakublock na alivyosema maneno yale ndio kabisaaa”.

Maimatha wa jesse alidai kuwa hawezi kwenda kwa sababu hakuipenda tabia ya Zari kuwaambia kuwa watakwenda kumchafulia nyumba.

Sikuipenda kabisa tabia ya Zari, yeye angeacha akaona kama kweli tutaenda au la lakini kabla hata siku hajizafika akajibu palepale, ya nini kwenda? Nimemshangaa maana hajui kama kwake tungeenda ingekuwa na faida sana hata kujitangaza kibiashara“.

Shamsa Ford yeye alidai kuwa anachojua lile tangazo la wao kwenda Sauz kwenye sherehe ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu wala hakukuwa na ukweli wowote.

Unadhani mchezo kuwasafirisha watu wote wale, ile ilikuwa ni sehemu ya kiki tu, wala siendi mimi”.

 

Dude Ashauri Wasanii Wapewe Elimu

Muigizaji wa Bongo movie Kulwa Kikumba maarufu kama Dude ameitaka serikali iwasidie elimu wasanii ili waweze kuelimika katika masuala ya uwekezaji.

Dude amedai mambo ya wasanii kupata matatizo au inapotokea wanaugua wanakosa pesa za kutibiwa mpaka kufikia hatua ya kuchangiwa pesa na serikali ni la Kutia Aibu badala yake wapate elimu ya uwekezaji.

Kwenye mahojiano na Za Motomoto News Dude amesisitiza suala la wasanii kuugua na kushindwa kujilipia gharama za matibabu nje ya nchi limekuwa likimuumiza mno hivyo kuiomba Serikali kuwaboreshea mazingira ya kazi zao na kupatiwa elimu ya uwekezaji kwa hicho kidogo wanakichopata.

Tunaiomba Serikali ituboreshee mazingira ya kazi zetu maana tunateseka sana hasa pale tunapopatwa na magonjwa yanayohitaji matibabu ya nje ya nchi au hata hapa nchini. Pia tupate elimu ya uwekezaji kwa fedha hizi kidogo tunazopata maana hatuna elimu hiyo pamoja na bima ya afya”.

Siku chache zilizopita Msanii mkongwe wa Bongo movie Mzee Majuto alikosa kabisa pesa za matibabu mpaka kufikia hatua ya kuchangiwa na serikali ili akapate matibabu nchini India.

Batuli: Nitairudishia Heshima Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Yobnesh Yusuf maarufu kama Batuli amefungka na kusema ana mipango ya kuirudisha tasnia hii ya Bongo movie kwenye chati.

Kiuweli kabisa Bongo movie imepoa sana kwani ni tofauti na miaka mitano nyuma ambapo kila mtu alikuwa anatazama filamu za Bongo movie lakini hivi sasa hakuna kitu.

Lakini Batuli amekiri kuwa pamoja na Tasnia ya Bongo movie kupoteza muelekea yupo tayari Kupiga na kufanya na kupona kwa ajili ya kuifufua na kuhakikisha anaitudisha pale ilipokuwepo kwenye chati.

Batuli amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo amekiri Bongo movie imepoteza mwelekeo kutokana na kazi mbovu walizokuwa wanazitoq ambazo hazikuwa na viwango sahihi na baada ya kufanya uchunguzi wamejipanga kuwaletea Watanzania kazi bora kabisa.

Filamu au tamthiliya ni biashara kama zilivyo nyingine na biashara yoyote lazima uangalie soko linataka nini kwa sababu wakati tulionao sasa ni tofauti na ule wa zamani, mashabiki wanataka kazi bora na siyo uchafu kwenye runinga zao hivyo nitarudisha heshima ya Bongo Muvi kutokana na kazi ninazokuja nazo”.

Kumekuwa na jitihada nyingi za wasanii mbali mbali wa Bongo movie kuongea kuhusiana na mipango ya kuhakikisha Bongo movie inarudi pale ilipokuwepo na mashabiki pia ni muhimu kutoa sapoti kwa kazi nzuri.