Wema Sio Mtoto ila Hajielewi:-Mh Shonza

Naibu waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo,Juliana Shonza amepinga kauli ya Wema Sepetu kusema aliyokuwa akiyafanya ni utoto baada ya kuvuja kwa video zake za faragha.Watu wengi wamekuwa wakimuonea huruma mwanadada huyu na kusema kuwa inawezekana kuwa bado anahitaji msaada na msamaha kujifunza

Akiwa mbele ya mwandishi Waziri Shonza amesema “Wema hana utoto wowote bali nikushindwa kujielewa na hivyo baada ya baraza la sanaa adhabu nyingine bado kutoka TCRA”

Aidha Waziri Shonza amesema kama Wizara nayo itamchukulia adhabu na kuwataka wadada wenye tabia za kukaa utupu mitandaoni kuacha tabia hizo mara moja.

hata hivyo tangu kutokea kwa tukio hilo, wema amekuwa akipokea adhabu tofauti  kutoka katika mashirikisho mbalimbali ya filamu huku TCRA wakimfungulia kesi .

Ray C Amtumia Ujumbe Mzito Wema Sepetu

Msanii mkonwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameibuka na kumuandikia ujumbe mzito msanii wa Bongo movie Wema Sepetu ambaye amefungiwa kufanya sanaa ya maigizo kwa muda usiojulikana.

Siku chache Wema alijikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya kuachia video iliyomuonyesha akipata wakati wa faragha na mpenzi wake baada y ahilo Wema aliomba msamaha lakini aliishia kufungiwa kufanya filamu kwa muda usiojulikana.

 

Baada ya sakata hilo Ray C ameibuka na kumpa ujumbe wa kumpa moyo katika kipindi hiki kigumu anachokuwa anapitia.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram, Ray C amesndika;

Nakumbuka 2006 Mange alinipigia Simu akaniambia anakuja nyumbani na mshiriki mmoja atakaeperform wimbo wangu kwenye kipengele cha Vipaji kwenye mashindano ya urembo ya (Miss Indian Ocean)na inabidi tumvalishe kama mimi nikamwambia sawa!walipofika nyumbani Kwangu nilimwangalia wema juu mpaka chini na alivyo mrefu,nikamwambia Mange huyu anashinda Miss Tanzania,nakumbuka alikuwa mwembamba,mrembo na mwenye aibu and I was like Wow!!!!

Anyway kiufupi Nakupenda mpaka leo Wema,Maisha ni Kama milima!wewe bado ni mdogo sana na una nafasi ya kuwa utakacho!pamoja na yanayoendelea sasa bado moyo wangu una imani na wewe kuwa utasimama tena zaidi ya juzi jana na leo na Utakua.Never give up!

Dunia inaweza kukubadilikia kutoka kuwa kipenzi cha watu na kuwa Public enemy number one!Its normal!!!Its ok!ila kumbuka Familia yako ndio kila kitu!Please usihuzunike ukajiona wewe ndo mkosaji dunia nzima maana kila binadamu ana majanga yake ni Mungu tu ndio mkamilifu ingawa sio sababu ya kutufanya kurudia makosa over and over again!

Nakupenda na nina imani na wewe!Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na natamani kumuona Wema Mpya.Lots of  love @wemasepetu ”.

 

Ray Kigosi-Wema Anastahili Adhabu Ya Kufungiwa

Msanii mkongwe wa sanaa ya Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’  amefunguka na kuweka wazi kuwa msanii mwenzake Wema Sepetu anastahili kabisa adhabu aliyoipata ya kufungiwa kufanya filamu kwa miaka miwili.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Sammisago Tv, Ray ameweka wazi kuwa ni sawa tu kwa adhabu aliyoipata Wema kwani kitendo alichofanya hakikuwa kizuri kabisa hasa kama msanii ambaye ni kioo cha jamii;

Wema alistahili mkupewa adhabu ya kufungiwa unajua tatizo la Watanzania wanapenda tuambiane vitu vya kusifiana sifiana tu lakini tusiseme pale mtu anapokosea kwaiyo mimi nikiwa kama msanii mkongwe ambaye nimekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu nasema kabisa kuwa Wema alikosea sana sana kwa sababu ukiangalia Wema ni Brand kuna watu wengi wengi sana ambao wanamuangalia hao wanaomuangalia wafanye nini yeye ni kioo cha jamii  kimsingi kabisa amefanya kosa lakini tumeshamuona Wema akiomba msamaha mara nyingi sana imefika wakati sasa abadilike”.

Kila msanii wengi amekuwa na maoni yake juu ya sakata la Wema wapo ambao wamemchana laivu kuhusu kosa lake lakini wapo ambao wamemkingia kifua kama vile Wolper.

Wema Afungiwa Miaka Miwili Kutofanya Sanaa.

Chama cha filamu  Kinondoni  TFDAA kimemfungia kufanya kazi  zozote za filamu mwana dada Wema Sepetu kwa muda wa miaka miwili kuanzia tamko jilo kutolewa mpaka litakapotimia miaka miwili ijayo.Adhabu hiyo ni muendelezo wa adhabu zinazoendelea kutolewa na mamlaka mbalimbali kumlenga wema baada ya kusambaza video zinazoenda kinyume na maadili ya jamii.

Chama icho kimeenda mbali zaidi na kusema kuwa kwa muda huu  vyama vingine havipaswi kumsikiliza msanii huyo akiwa anakuomba misamaha na kupuuza misamaha anayoomba .Msemaji wa kamati ya chama icho anasema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kamati ya maadili kukaa chini na kufikia muafaka huo.

Chama icho kinasema kuwa ni matumaini yao kuwa BASATA pia watamuongezea adhab mwanadada huyo kutofanya kazi kwa muda ili kuonyesha kujifunza kwake mwa muda wa miaka miwili ili aweze kujirekebisha.

Mpaka sasa BASATA wamepeleka kesi mahakamani kwa ajili ya kushughulikia kesi hiyo inayomkabili Wema sepetu  ya utovu wa nidhamu na uchapishaji video zenye maudhui ya kingono.

Wema Kupambana na TCRA Mahakamani.

Mamlaka inayohusika na ufatiliaji wa sheria za mitandao nchini TCRA wameamu kumfungulia mwanadada wema sepetu shitaka baada ya kufaya kosa la kuchapisha video chafu katika mitandao ya kijamii na kufanya kitendo cha ukiukaji wa maadili katika mitandao ya kijamii.

Shitaka hilo lenye kesi namba  KJN/RB.13607/2018 kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono mtandaoni., huku kesi iyo ikiwa imefunguliwa katika kituo cha olisi cha kijitinyama jijini da es salaam.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mwanadada Wema Sepetu aliomba msamaha kwa kosa lake hilo na kukiri kukosea na kukosea mashabiki pamoja na serikali kwa ujumla.

Hata hivyo utekelezaji wa kufungua kesi kwa TCRA kumetokana na kutakiwa kufuatwa kwa sheria za mitandao ambazo kila mara wamekuwa wakipiga kelele inabidi zifuatwe.

Hata hivyo wataalamu wa shetia wamesema kuwa kwa kosa la Wema , endapo kesi hiyo itapelekwa mahakani na kukutwa na hatia itamgharimu wema kufungwa kwa kifungo cha miaka 7 au faini ya milioni 20 au vyote kwa pamoja.

Ukaribu na Wema Sepetu Wamponza Diana Kimary

Msanii wa fialmu za Bongo movie mrembo Diana Kimary amefunguka na kuweka wazi kuwa hajali manneo ya watu ambayo yamekuwa yakusemwa kuhusu yeye kuwa na ukaribu na Wema Sepetu ambapo amedai hajali na acha waendelee kumnanga lakini hawajui maisha yake halisi.

Diana Kimary ameonekana kuwa karibu sana na Wema Sepetu ambapo amekuwa akimuita dada lakini ukaribu huo umekuwa ukiibua maneno mengi sana  kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea kusemwa sana na mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Diana alisema kuwa watu wengi kwenye mitandao ya kijamii hawajui kabisa maisha halisi ya mtu zaidi ya kukisia na kumsema vyovyote wawezavyo ndio maana hawafuatilii.

Unajua ni hivi wamenisema sana hapa katikati lakini hawajui kamwe maisha yangu na uzuri najitambua havinisumbui kabisa najua nini nataka maishani mwangu kwa hiyo hata kama wakinitukana ni sawa kwa vile siwalipii bando”.

Diana amekuwa na ukaribu na Wema kwa kipindi sasa ambapo ukaribu huo umemfanya hadi kujichora tattoo yenye jina la Wema.

 

Mume Mtarajiwa wa Wema Atajwa Kumdhulumu Wema Pesa

Mwanadada Wema Sepetu anasemwa kuwa katika kipindi kigumu kwa sasa kwa kile kilichodaiwa kuwa mume wake mtarajiwa aliesemekana kuwa anataka kumuoa hivi karibuni alifikia hatua ya kumdhulumu pesa zote ambazo nyingine zilikuwa na lengo la kumfanya afungue biashara yake mpya ambayo alikuwa akiitangaza.

Wiki iliyopita Wema alioomba msamaha kwa mahsbiki pamoja na serikali baada ya kuvujishwa kwa pichaa kiwa faragha na mpenzi wake huyo , lakini wema alionekana kuwa na kitu alitaka kusema lakini alikuwa akisita kila mara.

Hata hivyo baada ya kuchunuza sana , watu wake wa karibu na Wema walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari wanasema kwa sasa wema yupo katika wakati mgumu kutokana na kuwa mwanaume huyo ambae alimuamini kuwa anaweza kumuoa hakuana na lengo la kumuoa zaidi ya kutaka kiki na kumtapeli pesa.

 Wema yuko katika wakati mgumu sana, ni kweli wema aliingia katika mahusiano na huyo bwana ambae kwa kifupi anaitwa PCK , ila amemtapeli mamilioni ya pesa na kwa sasa mwanaume huyo anatafutwa na jeshi la polisi-Alisema mtoa habari huyo ambae ni mtu wa karibu na wema ila hakutaka kujulikana.

Ikumbukwe kuwa kipindi wema anaanza mahusiano na mwanaume huyo watu waliosemwa kuwa walikuwa wamedhulumiwa na mwanaume huyo walikuwa wengi huku wengine wakisema kuwa wamemfungulia kesi polisi lakini wema hakujali maneno hayo.

Wema Achukuliwa Hatua Kali na BASATA Baada Ya Kuvujisha Picha Chafu

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amejikuta katika upande mbaya wa sheria za nchi baada ya kuvujisha picha zake za faragha alizokuwa na mpenzi wake PCK.

Pamoja na kuomba radhi siku ya jana kuhusiana na picha hizo chafu Kwenye mitandao ya kijamii lakini tayari BASATA wameamua kumchukilia hatua kali Wema pamoja na wasanii wote walioachia picha chafu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni.

Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya  filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pamoja na Wema kusambaza na video zake chafu Lakini pia Gigy Money amedaiwa kuachia picha yake chafu Lakini pia video vixen Amber Rutty ameachia video yake ya ngono Mtandaoni.

“Wema Anasumbuliwa na Pepo La Ngono”- Mwijaku

Muigizaji maarufu wa Bongo movie anayejulikana kama Mwijaku ameibuka na kudai kwamba Msanii mwenzake Madam Wema Sepetu anasumbuliwa na pepo la ngono.

Mwijaku amefunguka hayo alipokuwa anaongelea skendo inayomuandama Wema Sepetu hivi sasa ya kusambaa kwa picha na video akiwa faragha chumbani na mpenzi wake anayeitwa PCK.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo, Mwijaku ameibuka na kudai anaamini kabisa Wema atakuwa na pepo la ngono kwa sababu mambo anayofany sio ya kawaida kabisa:

Wema inawezekana sio umaarufu wake unaomsumbua kuna kitu kingine tu kinamsumbua nacho ni pepo la ngono, nisikufiche naongea leo niko hai mpaka nakufa kama hatatibiwa pepo la ngono tutaona anaenda vizuri kesho anaaibika.

Lakini pia leo hii mambo anayefanya Wema hawezi kupata investor serious aka invest Kwenye Wema Sepetu Brand   Kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuwekeza kwa mtu ambaye anakuaibisha yaani endorsement zote atapoteza na kuishia kujirudisha nyuma”.

Tangu kusahau kwa video hizo chafu Wema Siku ya jana ameita mkutano na waandishi wa habari na kuomba radhi kwa yote aliyofanya.

Nimefunga Jalada la Upuuzi, Ujinga na Utoto :-Wema

Mwanadada Wema Sepetu  alipokuwa kiomba msamaha mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwa mama yake leo. alifunguka na kuonekana mwenye kujuta juu ya kile kilichotokea  hivi karibuni baada ya video chafu kusambaa akiwa faragha na mpenzi wake.

Wema anasema kuwa kwa sasa amefunga jadala la ujinga na upuuzi katika maisha yake na ataanza kujiweka kama mtu aliyekuwa na anaetambua majukumu yake katika jamii.

ninaomba radhi marafiki zangu,ndugu zangu na wale wote wanaonisapoti kwa ujumla.lakini zaidi namuomba msamaha mama yangu ambae amekuwa akiumia zaidi,hakuna marefu yasiyo na ncha, nimnefunga jalada la utoto , jalada la ujinga na jalada la upuuzi, naomba radhi kwa haya yaliyotokea,

Wema anasema kuwa takuwa akionekana mtu wa jabu sana kama jatoonekana kujali kwa sababu tangu siku ya tukio mpaka muda anongea hakuwa sawa kwa kila kitu.

Wema Aita Waandishi wa Habari, Aomba Radhi Mashabiki na Serikali.

Mwanadada Wema sepetu amewaita waaandishi wa habari mapema leo nyumbani kwake na kuongea nao huku dhumuni lake kubwa ikiwa ni kuataka kuombamsahama kwa mamalka husika na mashabiki zake wote kutokana na video chafu iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa faragha na mume wake mtarajiwa.

Wema anasema kuwa amekiri kosa hilo na hawezi kutaja sababu ya kwanini alifanya hivyo zaidi ya kujutia kosa hilo kwa sababu amedahlilisha watu wengi na kuwaumiza hasa wale wanaompenda ikiwepo mama yake mzazi.

Naomba radhi kwa hili liliotokea, naomba radhi kwanza kabisa kwa serikali yangu kupitia mamlaka ya TCRA , naomba radhi kwa bodi yangu ya filamu na pia naomba radhi kwa familiayangu, ndugu jamaa na marafiki, naomba radhi kwa wale wote wanaonipenda .

nawaomba radhi wadogo zangu ambao wamekuwa wakiniangalia kama kioo kwao, lakini zaidi namuomba radhi mama yangu mzazi , najua nimewadharirisha wengi na wala siko hapa kutoa sababu ya kile nilichokifanya  kwa sababu haitabadilisha kile kilichotokea lakini pia sihitaji kumlaumu mtu yoyote kwa lililotendeka kwa maana kosa ni kosa.

Wema Achafua Hali ya Hewa na Video Yake Chafu

Mwanadada Wema sepetu amechafua tena hali ya hewa katika mitandao ya kijamii baada ya video chafu akiwa na mwanaume aliyetangaza kuwa ni mume wake wakiwa faragha na kuonyesha uchafu wao hadharani kitu ambacho hakikupaswa kuwa sahih kwa wema .

Video hiyo ambayo imesikitisha mashabiki wengi ukiachana na hapo awali  ilipovuja siri kuwa Wema amekuwa na mahusiano na Dogo janja,  mashabiki na wote wanaompenda wema wameonekana kukatishwa tamaa na msanii huyo kutokana na ukweli kuwa hawakutegemea kitu kama icho kingewezwa kufanya na msanii huyo ambacho kipo kinyume na maadili.

Hata hivyo kwa wema amekuwa akionekana hajakli swala hilo wala mamo yanayosemwa katika mitandao juu yake.

 

Mobetto Apata VISA Ya Marekani Baada Ya Zari na Wema Kupigwa Chini

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva  Hamisa Mobetto amewabwaga mahasimu wake wakubwa Zari The Bosslady na Wema Sepetu na Kufanikiwa kupata visa ya kwenda Marekani.

Hamisa amewaacha mbali Zari na Wema baada ya kujipatia VISA yake ya kuingia nchini Marekani kwa ajili ya kupiga kazi.

Miezi michache iliyopita Wema Sepetu alitangaza kuwa atakuwa nchini Marekani kwa ajili ya kufanya appearance Kwenye Tanzania day lakini hilo halikufanikiwa baada ya kunyimwa VISA ya kwenda nchini humo.

Lakini vivyo hivyo ilikuwa kwa Zari ambaye Miezi michache nyuma alitangaza kuwapeleka Tiffah na Nillan kwa Diamond aliyekuwa nchini Marekani Kwenye ‘A Boy from Tandale Tour’ lakini baadae ilishindikana baada ya Zari kunyimwa VISA ya kuingia nchini Marekani.

Hamisa ameonekana kuwashinda mahasimu wake hao kwani hivi sasa yupo njiani kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya appearance katika miji mbali mbali.

 

 

 

Wema Sepetu Adai Hana Mpango Wa Kumuacha Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie staa Wema Sepetu amefunguka na kusema pamoja na mashabiki wake kutokwa na povu zito baada ya yeye kumuanika mpenzi wake lakini yeye ndio amemchagua.

Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuanika picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake amayejulikna kama Patrick Christopher ‘PCK’ ambapo mashabiki zake wengi walionekana kuchukizwa na Mahusiano hayo.

Wema na Mpenzi wake PKC

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema amesema  kuwa yeye ana uamuzi wake binafsi wa kufanya anachotaka kwenye maisha yake, lakini anashangaa watu wengine wanamuingilia mpaka kwenye maisha yake binafsi na kutokwa povu.

Yaani watu wametokwa na povu kama lote, kisa tu mimi kumuonesha mwanaume wangu, sasa hata wakiungana dunia nzima kunisema, kama nimeshampenda watanibadilisha vipi“.

Watu wengi wamejitokeza na kumshauri Wema aachane na yule mwanaume kwani haendani naye hata kidogo jambo ambalo limeonekana kumkera Wema.

Wema Awapa Pole Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mume Wake Mtarajiwa

Mwanadada Wema Sepetu ambae wiki iliyopita aliacha gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumuweka wazi mwaaume ambae alijulikana kwa jina la Patrick christopher na kusema kuwa huyo ndio mume wake mtarajiwa.

Baada ya kuweka picha hizo wakwa faragha na mume wake huyo , watu walianza kuongea maneno mengi katika mitandao huku baadhi ya mahasimu wake wakijitahidi kutafuta mabaya ya wema na hata ya mwanaume huyo na kuyaweka hadharani.

Hata hivyo Wema haonekani kujali maneno yoyoote anayosema kuhusu mwanaume huyo na amesema kuwa hata kama wataungana dunia nzima kwake ni kazi bure tu hivyo waache kuongea maana hakuna kinachosaidia .

Akiongea na waandishi wa habari Wema anasema “yaani watu wametokwa na povu kama lote kisa mimi kumunyesha mume wangu tu, sasa hata wakiungana dunia nzima kunisema kama nimeshampenda watanibadilisha vipi”

Mwanaume huyo amekuwa akikoselewa sana na hata kuonyeshwa baadhi ya vitu kama kuwa na familia na watoto alipwatelekeza, lakini pia inasemekana kuwa mwanaume huyo ambae ni raia wa Burundi amekuwa akitafutwa huko kwao kwa kosa la utapeli.

Jacqueline Wolper Ahaidi Kupambana na Marafiki Wanafki

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper ametoa neno kwa marafiki wote ambao wamekuwa na tabia za kinafki na kuhaidi kupambana nao.

Wolper amefunguka na kudai siku akimkamata mtu ambaye wanafahamiana vizuri akiwa anamsema kwenye Mtandao wa Instagram atafurahia shoo kwa atakachomfanya.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Wolper kama mtu mnajuana na ukaona amekosea ni vyema ukamfuata mwenyewe na kumwambia kuliko kuandika unavyotaka Instagram kwani huo ni unafiki.

Siamini kabisa mtu mwenye mapenzi ya dhati na wewe anaweza kukuandikia ujumbe kwenye Instagram. Mimi huo ninauita unafiki na siku nikimkamata mtu wa aina hiyo atanijua“.

Siku chache zilizopita Wolper aliingia kwenye mgogoro na msanii mwenzake Esha Buheti baada ya kuamua kumsema Wema Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo Wolper alidai hajapenda na kumtaka Esha amfuate pembeni na kumsema Wema badala ya kumsema Instagram.