Barakah The Prince: Sina Ugomvi Wala Bifu na Alikiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai kuwa hana ugomvi wala bifu na msanii mwenzake Ali Kiba.

Ni wiki chache tu zilizopita Barakah alikuwa anafanya interview na kila kituo na stesheni mbali mbali za media na kudai kuwa Ali Kiba na uongozi wao wote wa Rockstar 4000 ulikuwa unamfanyia zengwe ili kuua mziki wake baada ya kujitoa kwenye label yao.

Barakah aliyesainiwa chini ya label hiyo ya Rockstar 4000 miaka michache iliyopita aliwashangaza watu wengi kwa kile alichodai kuwa anajitoa kwenye label hiyo kisa na mkasa ukiwa uongozi wa label hiyo ukiongozwa na Ali Kiba na Seven Mosha ulikuwa unamzuia kutoa kazi zake na akadai kuwa kwa mwaka mzima ameruhusiwa kutoa nyimbo moja tu.

Kinachojulikana ni kuwa Ali Kiba alishawahi kusema kuwa Barakah ni mtoto tu hana akili, na inasemekana kuwa aliyemfukuza Barakah Rockstar 4000 ni Ali Kiba kutokana na tabia alizokuwa nazo Barakah. Sasa inasemekana kuwa Barakah ameanza tena kujipendekeza kwa Kiba kwani amemposti Alikiba kwenye siku ya birthday na kumtakia maisha marefu lakini hakumjibu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kuptia kipindi cha Enews Barakah amedai kuwa hana ugomvi na bifu na Alikiba kama wengi wanavyodhani;

Mimi sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba kabisa wala sijawahi kufikiria kuwa na matatizo naye hayo matatizo ni midomo ya watu tu wanayatengeneza, mimi kutaka kuondoka kwenye kampuni yao ya kazi sio kwamba ndio nina ugomvi nao hii ni kazi tu naweza nikahama ofisi yoyote”.

 

Barakah The Prince Achoshwa na Longolongo Kaamua Kufungua Studio Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘sometimes’ amefunguka kuwa amechoshwa na longolongo za label mbalimbali alizofanya nazo kazi mwanzoni huvyo kufikia uamuzi wa kufungua label yake mwenyewe inayoitwa Bana Music.

Mwaka huu umekuwa mgumu kidogo kwa Barakah kikazi kwani aliondoka kwenye moja ya label kubwa Africa Rockstar 4000 kwa like alichodai ilikuwa inamchelewesha kutoa kazi zake. Baada ya kutoa wimbo wake mpya wa ‘sometimes’ Barakah aliingia tena kwenye mgogoro na label yake ya zamani kwa kile alichodai kuwa wanamfanyia hila ili kazi zake zisifanikiwe na pia alimtuhumu maneja wake wa zamani anayejulikana kama Seven kuwa anamharibia akaunti yake ya YouTube ili watu wasiangalie kazi zake.

Barakah ametangaza ujio wa label yake hiyo inayojulikana kama Bana Music Records, aliyoshirikiana na mwanamuziki mwenzake na pia mpenzi wake Naj.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Dizzim Online Barakah amefunguka kuwa ni kweli amekuwa akifanya kazi na watayarishaji na studio ambazo zinamhitaji na anazozihitaji kulingana na mahitaji;

Nimeamua sasa niliweke wazi kwa sababu watu wananionq nafanya kazi studio tofauti na wanajiuliza maswali mengi, Studio za Baba music zipo katika umaliziaji na hivi karibuni itaanza kufanya kazi na kutoa kazi zenye ubora. Kutoa kazi zenye ubora ndicho kitu tunazingatia na ninaamini utayarishaji wetu utazingatia kile ambacho mashabiki watahitaji kusikia”.

Lakini pia Barakah ameweka wazi kuwa mbali na kuwa mmoja wa waanzilishi wa studio hizo za Bana music, wapo wasimamizi wenye vigezo ambao wanasimamia label hiyo.

Barakah The Prince: Mimi Sio Mkorofi Nachukiwa Kwasababu ni Msemakweli

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Barakah The Prince anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘sometimes’ amefunguka na kudai kuwa yeye sio mkorofi kama wasanii wenzake wengi wanavyodai bali ni msema kweli.

Barakah amekuwa akishika vichwa vya habari wiki chache zilizopita baada ya kurushiwa tuhuma mbali mbali na wasanii wenzake na mashabiki zake ambao wamekuwa wakimkosoa mara ya mara.

Barakah amesisitiza kuwa hajawahi kugombana na msanii yoyote ila kusema kwa ukweli ndio kunafanya watu kumchukulia kama mkorofi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Barakah amefungukia suala hili:

Sijawahi kumtukana au kugombana na msanii but ule ukweli wangu labda unamwambia mtu, unajua watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli anaweza akakuboa ukamwambia ukweli akakuchukulia tofauti kwa hiyo nadhani sana hiyo ndio ilikuwa inachangia, unajua wakati huu nimejitahidi ndio maana hata nimekaa kimya kwa muda mrefu sana , nimejaribu kukaa chini na watu wengi na kuzungumza nao na wamenipa canceling wakiwemo watu wakubwa kwenye entertainment”.

Mapema wiki hii Barakah aliingia kwenye bifu na mwanamuziki mwenzie Shilole kwa kile Shilole alichodai kuwa Barakah nimjeuri na mgombanisho lakini pia Barakah amegombana na uongozi mzima wa label yake ya zamani na Mc cater.

Shilole Amchana Barakah The Prince, Huku Mx Cater Adai Ana Stress

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Barakah the Prince amezidi kuwa katika kipindi kigumu wiki hizi chache tangu atoe wimbo wake mpya ‘sometimes’.

Tangu ametoa wimbo huo, Barakah amekuwa katika headline baada ya kudai kuwa label yake ya zamani Rockstar 4000 na Mx Cater wanamfanyia hila ili nyimbo yake mpya isivume wala kupata viewers YouTube.

Mapema wiki iliyopita Barakah alidai kuwa MX cater ambaye ni meneja wa wanamuziki Aslay na Shetta alimuomba password ya akaunti yake mpya ya YouTube kwa lengo la kumfanyia uchunguzi wa nani anamfanyia mchezo huo mchafu, lakini Barakah anadai baada ya kumuamini na kumpa password hali ile ikaanza kutokea tena kwenye akaunti yake mpya.

Barakah amedai kuwa habari za yeye kufanyiwa mchezo mchafu na MX carter amepewa na msanii mwenzake Shilole, jambo ambalo Shilole amelikataa kwa nguvu zote ambapo amedai kuwa Barakah ni muongo na mchonganishi.

Lakini kwa nini huyu mtoto anapenda kugombanisha watu? Na ndio maana haelewani na watu kwa sababu ya mambo yake anayoyafanya siyo vizuri kama unataka kuongea na mtu mfuate binafsi si mpaka upitie kwa mtu mwingine, yaani sikipendi nasema ukweli halafu yule ni mdogo wangu namheshimu, yule mtoto ajipange unajua sometimes unataka kiki lakini siyo za namna hiyo, ana dharau sana yule mtoto nasema hiyo dharau haitampeleka kokote, kwangu mimi hapati kiki bali nitamuharibia sitoi kiki kishenzi”.

Pia Shilole amezidi kusisitiza kuwa hajawahi kumwambia Barakah jambo kama hilo mara ya mwisho waliongea kwenye Simu ambapo Barakah alimuomba ampostie Nyimbo yake mpya, lakini pia Baada ya tuhuma hizo MX cater alikataa tuhuma hizo alizopewa na Barakah kudai Ana stress za nyimbo yake mpya kufeli.

Barakah The Prince Kuwashtaki Rockstar 4000

Msanii wa Bongo fleva Barakah the Prince ameshika tena headline baada ya kuweka wazi nia yake ya dhati ya kumshtaki Boss wake wa zamani Seven Mosha  pamoja na label nzima ya Rockstar 4000.

Barakah ameingia matatizoni na uongozi wake wa zamani, Rockstar 4000 na kumshutumu aliyekuwa boss wake. Baada ya kujitoa label hiyo ya Rockstar Barakah alitoa wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘sometimes’ lakini tangu wimbo huo ameweka wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube, Barakah amedai kuwa uongozi wake wa zamani umekuwa ukimfanyia vituko ilimradi asifanikiwe ambapo alisema walikuwa wanaifungia nyimbo hiyo ili nashabiki kutoka nchi za nje wasiiangalie.

Alipohojiwa na kituo cha televisheni cha  East Africa, Barakah aliongelea ishu hiyo na kuweka wazi hatua za kisheria atakazochukua:

Nilijaribu kutengeneza YouTube account mpya ili niachane na ile ya mwanzo kwa sababu ilikuwa na matatizo na Rockstar walikuwa wanaing’ang’ania lakini baada tu ya kuweka video yangu mpya mayo ikaanza matatizo kama ile video ya mwanzoni viewers wanashuka badala ya kupanda kwaiyo hapa kuna watu wawili wanaoweza kufanya hivyo aidha ni watu wa Mxcarter au Seven kutoka Rockstar, na siwezi nikaongelea tena hili suala kwa sababu kesi ilishafunguliwa polisi tunasubiria kwenda mahakamani”.

Barakah alikosa maelewano na label hiyo ya Rockstar iliyokuwa inasimamia kazi sake za kimuziki baada ya kuamua kujitoa kwa kile alichodai walikuwa wanafanya uzembe na kazi zake hata hivyo Barakah amewasihi mashabiki zake wasikate tamaa kwani ataachia nyimbo nyingine hivi karibuni.

Barakah the Prince Afunguka Kuhusu Utapeli Anaofanyiwa na Alikiba na Timu Yake Nzima

Mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘sometimes’, Baraka Da Prince amefungukia hujuma anazofanyiwa na label yake aliyojitoa hapo nyuma ya Rockstar 4000.

Rockstar 4000 ni label ya mziki inayosimamia wanamuziki mbali mbali katika kazi zao mwaka 2016, Alikiba alipewa cheo cha kuwa mkurugenzi wa label hiyo baada ya kusimamiwa na label hiyo kwa miaka sita mfululizo mwaka huo huo Alikiba alimsaini Barakah de prince Rockstar baada ya kuhama label kadhaa, lakini mapema mwaka huu Barakah alitangaza kuondoka kwenye label hiyo na kusababisha maneno mengi kuzuka.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Liliommy, Barakah amefunguka kuwa aliondoka Rockstar sio sababu za kimaslahi na pia changamoto anayoipata tangu kuondoka kwenye label hiyo;

Mimi niliondoka Rockstar sababu ya utoaji wangu wa kazi. Unajua Rockstar wamenifata nifanye nao kazi tayari mimi ni star na nina mashabiki wengi sana sasa tangu nianze kufanya nao kazi nimetoa nyimbo moja tu ‘nisamehe’ kwa miaka miwili kwaiyo hicho ndo kilichotokea nina nyimbo zaidi ya hamsini ndani lakini nimeishia kutoa nyimbo moja kwa miaka miwili nikashindwa kuvumilia hilo suala”.

Pia Barakah amelezea ni jinsi gani label yake hiyo aliyoihama imekuwa ikikwamisha jitahada zake zakuinua muziki amedai wamekuwa wakitumia nguvu waliyonayo katika kuharibu jitihada sake hasa kwa huu wimbo wake mpya ambao amedai tangu ameuweka YouTube waangaliaji hawaongezeki na pia amedai kuwa kuna nchi za nje kama Dubai wamekuwa hawauoni wimbo huo YouTube kitu alichodai kuwa nihujuma inayofanyika katika kumfelisha.

Barakah The Prince Afunguka Kuhusu Kumwagana na Naj na Mpango Wa Kutoa Nyimbo Mpya Kila Wiki

Mwanamuziki wa Bongo fleva wa kujiita Magufuli wa Bongo fleva, Barakah the Prince amefunguka kuhusu tetesi za yeye kumwagana na mpenzi wake na mwanamuziki mwenzake, Naj na pia afafanua mpango wake wa kuwa anatoa nyimbo mpya kila baada ya wiki moja.

Barakah anayetamba na wimbo wake mpya wa ‘Sometimes’ amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Naj kwa kipindi kirefu sasa ambapo siku za nyuma walikuwa ni kawaida yao kuposti picha mtandaoni wakiwa pamoja au kila mmoja kumposti mwenziye lakini ghafla taratibu hiyo ikapotea na ndipo wengi walidhani kuwa watakuwa wamemwagana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Barakah alifunguka yafuatayo kuhusiana na ishu hizo:

Napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa wimbo wangu wa ‘sometimes’ ndio wimbo wa kiwango cha chini katika listi ya nyimbo nitakazotoa ambazo ntaanza kutoa kila wiki, yaani kila wiki ntakuwa naachia ngoma mpya kwa sababu mashabiki zetu tunakuwa tunawaangusha kwasababu wanataka kila siku wawe wanasikiliza nyimbo mpya alafu pia nyimbo zikiwa nyingi inatupa changamoto wasanii ya kufanya kazi nzuri zaidi, unajua zamani nilikuwa naweza kutoa nyimbo moja kwa miezi sita sahivi nabadilisha utaratibu kwa sababu mashabiki wamebadilika na mziki ni biashara kwaiyo inabidi niangalie wateja wangu”.

Barakah pia aliongelea uhusiano wake na Naj:

Sasa mimi nasapotije kazi yake ya mziki wakati na yeye ni mwanamuziki anahitaji yeye mwenyewe kupromote kazi yake, kwanza kazi na mapenzi haviwezi kuingiliana hata siku moja nilimsapoti kwa kazi yake ilipoishia ndo hapo hapo kwani ile ni page yangu mimi mwenyewe nataka kuposti vitu vingine mbali na Naj, tukiwa Nyumbani tunaonyeshana mapenzi sio lazima tuonyeshane Instagram, lakini hajanimwaga Mimi nikimwagwa kila mtu atajua kwasababu ukinimwaga nataka uwe adui yangu mi sijaachana na Naj tungekuwa tumeachana Mimi ningesema yule sio mpenzi wangu lakini bado tuko wote ila kwa sasa yupo nyumbani kwao London”.

 

Sina Tatizo Wala Ugomvi Wowote na Barakah the Prince- Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amefunguka na kukataa kuwepo kwa bifu lolote baina yake na msanii mwenzake Barakah the Prince.

Tetesi za wawili hao kuwepo na bifu zilienea baada ya Barakah kujitoa kwenye Label iliyokuwa inamsimamia ya Rockstar 4000 na baada ya muda mchache Ommy kujiunga, Label hiyo ambayo pia inamsimamia msanii Alikiba. Kutokana  na kitendo hicho cha Barakah kujitoa na muda huo huo Ommy kujiunga kilitafsiliwa na wengi kama walijiona hawataiva kwenye chungu kimoja hivyo mmoja wao akaamua kujitoa kwenye label hiyo.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka yafuatayo;

“Sidhani kama Barakah labda alitoka sababu mimi nimekuja hapana, kwanza naamini mi na Barakah tunafanya miziki tofauti yaani hatuna sehemu yoyote tunayoweza kusema hii inaweza ikatokea mkwaruzano, na tunaheshimiana yule ni mdogo wangu namkubali naamini ni moja ya watu wenye kipaji kukubwa kwa hapa Tanzania na kapambana kutengeneza jina lake”.

Ommy Dimpoz pia aliendelea kufunguka;

“Kilichomfanya aondoke Rockstar siwezi kukizungumzia na siwezi kujua ni nini, nafikiri yeye mwenyewe na label wana majibu sahihi zaidi. Siwezi kusema kama nahisi kuna pengo sababu wakati yeye yuko Rockstar mi sikuwepo kwaiyo wenyewe ndo wanaweza kujibu kama kuna pengo la Barakah au hakuna na pia mahusiano yangu mi na Barakah ni ya siku nyingi kabla hajaenda Rockstar yaani tupo sawa tu hatuna tatizo hata kidogo”‘

Ommy Dimpoz kwa sasa anatamba na nyimbo yake ya Cheche ambayo inashikilia namba moja kwenye stesheni za redio mbalimbali na pia kwenye mtandao wa youtube.

Barakah: Mimi ni Magufuli Wa Bongo Fleva Kutokana na Misimamo yangu Thabiti

Mwanamuziki wa bongo fleva Barakah The Prince amesema yeye ni sawa na Raisi Magufuli kwenye gemu ya  bongo fleva kwa kuwa ana misimamo na itikadi ambazo wengi hawazipendi.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa radio, Barakah amesema misimamo yake na kwa jinsi ambavyo hapendi kuona anaonewa, ndio sababu ya watu kutomkubali na ndo sababu ya kuhama hama kwenye uongozi.

Barakah amesema siku zote mtu akiwa na misimamo yake na mitizamo yake binafsi lazima watu watakuona mbaya, huku akimtolea mfano Raisi Magufuli jinsi alivyo na msimamo katika harakati zake za kutetea wanyonge, kitendo ambacho kinapingwa na watu wengi sana katika jamii.

Barakah amekuwa mmoja kati ya wasanii ambaye wamekuwa akikosolewa sana kwenye mitandao ya  kijamii kutokana na maneno yake na misimamo yake hasa akiwa anawaongelea wasanii wenzake.’

Alikiba aeleza kwanini Barakah The Prince alitemwa na lebo ya Rockstar4000

Barakah The Prince alikua amesainiwa Lebo ya kimataifa la Rockstar4000 kabla ya kuihama lebo hio. Alikiba ni mmoja wa wakurugenzi katika lebo hio la Rockstar4000.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio, Alikiba alifunguka na kusema kwa Barakah The Prince alitoka Rockstar4000 kwasababu ya utovu wa nidhamu.

Barakah The Prince na Alikiba

Kiba alieleza kuwa hakufurahishwa na vitu ambavyo Baraka alikuwa akifanya kwani aliona kuwa mwimbaji huo hakua na heshima kabisa.

“Baraka hayupo Rockstar, alitoka sababu za kukiuka vitu ambavyo hakutakiwa kufanya, Baraka nimemjua baada ya kuwa naye Rockstar400, lakini kiukweli sikufurahishwa na vitu ambavyo alikuwa akifanya, nadhani nilikuwa nikiona kama ni utoto lakini si utoto tena, ni kutokuwa na heshima nikaona haina haja, na mimi nikiwa kama mtu mzima sitakiwi kugombana na mtu mdogo inatakiwa umuache dunia imfunze kidogo, au kama kuna kitu ambacho amefanya au kalishwa sumu basi akapewe dawa itoke,” alisema Alikiba.

 

Barakah the Prince afungua YouTube mpya baada ya kuvurugana na lebo linaloongozwa na Alikiba

Alikiba alipandishwa cheo na kuwa mkurugunzi wa label ya RockStar4000 iliyokua imemsimamia Barakah the Prince kabla ya msani huyo kuondoka hivi karibuni.

Barakah The Prince alianza maisha yake mapya akiwa na label yake ya Bana Music baada ya ndoa yake na kampuni ya RockStar4000 kuvunjika.

Staa huyo ametangaza kwa mtandao wa kijamii kuwa anafungua akaunti mpya ya YouTube na kuiacha ile ambayo aliyokuwa akiitumia akiwa katika label ya RockStar4000.

“Ndugu zangu nitawatangazia soon YouTube channel yangu mpya kuna zawadi zenu kama 5 hivi…basi na hii itadondoka ndugu zangu,” aliandika Barakah Instagram.

Hatua hii ya Barakah the Prince imezua madai kuwa RockStar4000 imekataa kupea Barakah akaunti yake ya YouTube ya zamani.

 

Dynamic afunguka kuhusu mchango wa Barakah The Prince kwa maisha yake

Msanii Hamadi Abdulhemed maarufu kama Dynamic amefunguka na kusema kuwa Barakah The Prince amemsaidia sana katika muziki na hata shoo anazofanya.

Dynamic alimsifu sana Barakah The Prince kwa mchango wake, alisema pia Barakah hana kujiskia kwingi kama watu wengi wanavyosema.

“Nimeshapanda na Barakah kwenye shoo kubwa mbili, sijui kwa wengine labda wanaoona anajisikia kwangu hayupo hivyo. Ni mtu poa sana na nimekuwa nikishirikiana naye mara kwa mara kwenye muziki,” Dynamic alisema akiongea na Over Ze Weekend.

Barakah The Prince amsifu sana Diamond kuliko Ali Kiba akilinganisha mchango wao kwa muziki

Barakah The Prince anatambua kuwa Diamond and Ali Kiba ndo ndume katika ulingo wa muziki Tanzania. Lakini mwimbaji huyo amekiri kuwa Chibu Dangote ndo ndume kamili.

Barakah aliwataja wasanii watatu ambao wako na mchango mkubwa kwenye muziki; Diamond, Ali Kiba na Ommy Dimpoz.

Akiongea na Bongo 5, Barakah alimsifu sana Diamond ambaye alisema ameweka mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wote nchini.

“Kwa mfano Bongo kwa mtu kama Ommy Dimpoz, Ommy ni package kabisa ya staa, Diamond ni package na Alikiba ni package iliyokabilika ambayo unaona kabisa huyu ni staa kakamilika. Kwa hiyo kwenye muonekano pia hususan mavazi na mwili lazima mtu uwe makini sana. Diamond ni miongoni mwa mtu ambaye anaowasanua sana watu kwenye vitu, nani alitegemea kama Diamond anaweza kuja na Chibu perfume? Hakuna mtu aliyetegemea, lakini jamaa kaka kafikiria watu wanapenda sana kunukia.

Baraka The Prince

“Nampongeza sana Diamond, ni mtu ambaye anatumia nafasi yake aliyopo sasa hivi vizuri. Kwa hiyo sitaki kusema kuwa watu wengi wanafanya kwa kuwa yeye kafanya, no lakini uyeye anaweza akawa anawapa watu mioyo ya kuthubutu. Unajua mtu mpaka kurizki na kuweka hela yake nyingi kwenye brand ya nguo au nini, ujue hapo umerizki na biashara ina mambo mawili, kuna kunyanyuka na kuna kuanguka.

“Mtu mpaka uweze kurizki lazima uone mfano kwa mtu, huwezi kurizki tu, kwa hiyo yeye ni miongoni mwa watu wanaowapa watu moyo na kuona kumbe kitu hiki unaweza kukifanya na kitu hiki na kikawezekana na tukabiga mitonyo na maisha yetu yakawa mazuri,” Barakah alisema.

 

 

Barakah the Prince: Sijasimamiwa na Ali Kiba

Barakah the Prince ni miongoni wa wasanii wachache kutoka Tanzania ambao wako chini ya usimamizi wa kampuni ya RockStar4000.

Hivi juzi Ali Kiba aliteuliwa kuwa mkurugenzi katika kampuni hio ya RockStar4000.Hata hivyo Barakah amedhibitisha kuwa yeye hasimamiwi na Ali Kiba.

Akiongea na kipindi cha 5 Selekt ya EATV, Baraka The Prince alitoa ufafanuzi kuwa yeye ni msanii anayesimamiwa kazi zake na kampuni ya RockStar4000 na si kusimamiwa na Ali Kiba.

“Mimi sitaki sana kuzungumzia sana juu ya Alikiba kuwa Director wa RockStar4000 kwani kipindi ambacho yeye anaingia mikataba mimi nilikuwa Nairobi na wao walikuwa Afrika Kusini na sijapata nafasi kusikia chochote hivyo kwa sasa bado sijui vizuri hilo jambo, siwezi kulizungumzia japo nafahamu maana naweza kuzungumzia nikazungumza nikasema jambo lisilo la kweli. Ila nimefurahi sababu Alikiba ni kaka yangu na naishi naye vizuri na najua kuwa kazi itakwenda vizuri. Mimi ni msanii wa RockStar4000 na si msanii wa Alikiba hilo watu naomba waelewe,” alisema Barakah The Prince.

 

Ali Kiba akiri kuwa Barakah The Prince ako na akili za kitoto

Wambeya wanasema kuwa urafiki baina ya Ali Kiba na Barakah The Prince unadidimia kwasababu ya bifu kati ya Baraka na Ommy Dimpoz.

Inasemekana kuwa ukaribu wa Dimpoz na Ali Kiba umechangia kuzorota kwa urafiki baina ya Kiba na Baraka kwasababu Dimpoz na Baraka hawali sahani moja kwa sasa.

Barakah The Prince na Ali Kiba

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Ali Kiba alikiri kuwa Barakah The Prince ako na akili za kitoto ndio maana kuna maadhi ya mambo yanaibuka kwamba haelewani na baadhi ya wasanii wenzake.

“Mimi nadhani ni utoto tu, nadhani ni umri tu lakini Baraka yupo vizuri, ni mtu anayesikiliza na ana rekebishika. Muda mwingine labda umri ndio unampeleka lakini muda mwingine mtoto akifanya jambo unamwambia. Ni mdogo wetu tutamwelimisha na sidhani kama anamchukia Ommy Dimpoz labda ni maneno tu ya mtaani,” Ali Kiba alisema.

 

Barakah the prince afunguka kuhusu kufeli kwa wimbo wake mpya

Baada ya kuachaia wimbo wake mpya ‘acha niende’ msanii wa bongo Barakah the Prince almefunguka kudai kuwa amegundua kuna vitu kadhaa ambazo zimefanya wimbo wake kutofanya vizuri Kama nyimbo zake za hapo awali.

Akizungumza na kipindi cha Enewz cha EATV Barakah the Prince alisema kuwa aliwachia wimbo wake wakati kulikuwa na mambo mengi yanaendelea. Msanii huyo alisema,

Barakah The Prince
Barakah The Prince

Hali ni ngumu kweli kwa wasanii, nyimbo nyingi ambazo zimetoka hivi karibuni zimeshindwa kufanya kusema kweli hata wimbo wangu haujafikia kwenye malengo ambayo nilijiwekea wakati natoa ai hata nikilinganisha na nyimbo zangu zilizopita.

Hata hivyo amejipa moyo wa kufanya nyimbo zingine hivi karibuni.