Diamond atoa shukrani baada ya ‘Zilipendwa’ kutawala Kenya, Uganda, Tanzania na Oman

Wimbo mpya ya Diamond – ‘Zilipendwa’ amabayo aliwashirikisha wasanii wote wa Wasafi inatrend katika nafasi ya kwanza Kenya na Tanzania, nafasi ya tano Uganda na nafasi ya 28 nchini Oman.

Diamond amependezwa na jinsi ambayo wimbo huo unatrend hata kama wimbo pinzani ya Alikiba ‘Seduce Me’ bado iko na views mingi kwa YouTube.

Staa huyo wa Wasafi aliwashukuru mashabiki wake kwa kufanya ‘Zilipendwa’ kutrend na akawaomba kushare zaidi nchini mwao ili ipate views zaidi.

“Thank you Oman, Uganda, Kenya, and my Beloved Country Tanzania… #Zilipendwa (They Used to like) it’s a song which talks about all the Old Suff that people used to do ,to Eat, to like and used to Trend….. i know every country got it’s own #ZILIPENDWA… Can you please share with us, one from your Country…. full Video link in my BIO” Diamond aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram.

Ne-Yo amjumuisha Diamond kwenye tour yake ya Uingereza

Diamond atajiunga na Ne-Yo kwenye ziara yake ya kimuziki nchini Uingereza ambayo itaanza rasmi Septemba 13 jijini Manchester.

Mastaa hao wawili wamefanya kazi kimuziki pamoja awali, walishirikiana kuwachia wimbo ‘Marry You’ mapema Februari mwaka huu.

Ne-Yo alihairisha tour yake mara mbili baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi jijini Manchester nchini Uingereza.

Staa huyo wa Marekani sasa amethibitisha tour hio ya Uingereza na kutoa ratiba yake kamili inayoonyesha wapi na lini atakua.

Tazama wimbo wa Ne-Yo na Diamond hapo chini:

Elizabeth ‘Lulu’ Michael amchimba Diamond?

Diamond and Alikiba waliachia nyimbo zao ‘Seduce Me’ na ‘Zilipendwa’ siku moja Agosti 25. Alikiba ndo alikua wa kwanza kuachia wimbo wake kabla ya Diamond pia kuamua kuachia yake.

Hata hivyo ‘Seduce Me’ imepata views nyingi kwa YouTube kushinda ‘Zilipendwa’. Ngoma hio ya Alikiba iko na views milioni 2.3 kwa sasa ilhali ya Diamond iko na views milioni 1.5.

Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameonekana akimchimba Diamond kwa kitendo chake cha kuamua kuachia wimbo siku moja na Alikiba.

Katika ujumbe alioandika kwa Twitter, muigizaji huyo wa filamu ya Bongo alisema kuwa mtu akifanya kitu kizuri kwa nia mbaya hakifanikiwi kwa uzuri wote.

Ujumbe wa mrembo huyo inaonekana kama ushauri kwa Diamond ambaye alitoa wimbo wake kushindana na Alikiba lakini hajafanikiwa kumbwaga Kiba kwani wimbo wake unazidi kung’aa tu.

 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam atoa onyo kwa Alikiba na Diamond

Mhe Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, ametoa onyo kwa Diamond Platnumz na Alikiba kuhusu kushindana kwao kimuziki.

Makonda alikiri kuwa ushindani wa kimuziki baina ya Diamond na Alikiba unachangia kukuza muziki wa Bongo lakini hata hivyo alionya kuwa lazima wasanii hao wazingatie sheria na maadili ya jamii wanaposhindana.

Mhe Paul Makonda

“Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki. Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..,” Paul Makonda aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Alikiba na Diamond waliachia nyimbo zao mpya ‘Zilipendwa’ na ‘Seduce Me’ siku moja, Ijumaa Agosti 25. Tazama nyimbo hizo hapo chini:

“Mimi naibiwa haki yangu vipi?” Matonya adai wimbo mpya ya Diamond umeibwa kutoka kwake

Diamond na wasanii wote wa Wasafi waliachia wimbo mpya ‘Zilipendwa’ Ijumaa Agosti 25. Wimbo huo umezua utata kwani msanii Matonya anadai kuwa wimbo huo uliibwa kutoka kwake.

Matonya alitoa malalamiko yake kwenye mtandao wa Instagram ambapo alidai kuwa ana haki zake katika jina hilo la ‘Zilipendwa’. Staa huyo aliwai toa ngoma la jina hilo hilo zamani.

“Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini? Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/ kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila woga???? lakini haki itafata mkondo wake,” Matonya aliandika.

Tazama wimbo huo hapo chini:

Steve Nyerere atoa ushauri wake kuhusu bifu mpya kati ya Diamond, Alikiba na Ommy Dimpoz

Diamond Platnuz, Alikiba na Ommy Dimpoz wamekua wakitupiana maneno yenye mafumbo katika mitandao ya kijamii tangu Diamond aliposhirikishwa katika remix ya ngoma ya Fid Q ‘Fresh’.

Diamond alisema kwa wimbo huo kuwa hawezi kulinganishwa na Alikiba kisha Kiba naye akamjibu kwa fumbo kuwa yeye bado ndo mfalme.

Diamond tena aliweka wimbi nyingine kwenye account yake ya Instagram ambayo aliwachimba Alikiba na Ommy Dimpoz. Baada ya Diamond kuweka wimbo huo kwa Instagram, Ommy Dimpoz pia aliweka picha Instagram akiwa na mama mzazi wa Diamond na kuandika ujumbe wenye utata:

Ommy Dimpoz na mamake Diamond

“BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU

Salam zako nimezipata mwanangu Hivi kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa langu mimi nini???? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?

#UnanioneaKwaKuaSijuiKurap?

#SijuiNaMimiNimkatae??

#KamaYeyeAlivyomkataaWaMobeto

#YaniUnamkataaMjukuuWangu??

#UnakubaliKuleaWatotoWa5SioWako

#UmerogwaWWSioBureMwanangu

#NilikuwaNajuaNimezaaSIMBA

#KumbeNimezaaKIMBA

#DavidoNaeAnalalamiKuhusuENEKA

#UmeletaJanjaJanjaKwenyeFallOnU

#NnaedhalilikaMimiBabaYaKo??

#UtakujaKuniuaKwaPreshaJomoniiii?

#HayaNendaKatungeVesiNyingine?

#RahaYaVitaUsichagueSilaha

#BABAMALKIA

 

Steve Nyerere sasa ameingilia kati na kutoa ushauri wake, somo ujuembe aliondika kwa Instagram hapoo chini:

“NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA.”

Steve Nyerere

 

Diamond aagiza tani 100 za karanga kutoka kwa wakulima

Staa wa Wasafi Diamond Platnumz anapanua biashara yake ya karanga. Hit maker huyo wa ‘Eneka’ ameagiza tani 100 ya karanga kutoka kwa wakulima nchini.

Diamond alitoa ombi hilo kupitia account yake ya Instagram:

FURSA KWA NDUGU ZANGU WAKULIMA WA KARANGA…. sasa waweza kutuuzia karanga mbichi nyeupe zenye rangi ya kwenye picha hapo, Maarufu kama Super Quality Small size….

Kuna nafasi ya kununua hadi Karanga Tani mia moja (Tani 100) kwa kila Mwezi… Usafi na Ubora wa karanga zako ndio nguzo ya kwanza sisi kuweza kuzinunua karanga zako….Wasiliana nasi kwa namba hizi +255714993724 @diamondkaranga #NogewaJirambe ?? MAZINGATIO:

  1. Karanga ndogo Nyeupe (Super Quality Small Size)
  2. Ziwe Safi sana sana.
  3. Zifungwe katika ujazo wa kilo 20 kwa kiloba.
  4. Tunanunua kwa Bei kati ya tsh 2300 – tsh 2700 kwa kilo.
  5. Maitaji yetu ni tani 100 kwa mwezi.
  6. Piga simu: +255-714-993-724

Alikiba aonyesha kukerwa na hatua ya Diamond kuamua kumchimba

Diamond alimchimba Alikiba kwa remix ya wimbo ‘Fresh’ remix. Staa huyo wa Wasafi alitumbia fumbo kumpiga teke Alikiba kwa wimbo huo; alisema kumcompare na Cinderella (Alikiba) haiwezi kuwa fresh.

Alikiba pia alitumia lugha ya mafumbo kumjibu Diamond baada ya hit maker huyo kusikika akimchimba katika remix ya ngoma ‘Fresh’ remix.

“The KING ll always Be a KING. je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu ?? #KingKiba,” Alikiba aliandika kwa mtandao wa Twitter.

Skiza ‘Fresh’ remix hapo chini:

Diamond: Hauwezi kunicompare na Alikiba

Diamond amemchimba Alikiba kwa remix ya wimbo ‘Fresh’. Diamond ambaye alirap kwa wimbo huo, alisema kumcompare na Cinderella (Alikiba) haiwezi kuwa fresh.

Soma mistari ya Diamond kwa wimbo ‘Fresh’ hapo chini:

Niliposikia beat tu nikatamani nifanye verse/ Nikamcheck Ngosha akaniambia simba mbona fresh/ Upesi upesi nikaandika nimurde kesi/

Na sasa ngoma kitaani imenuka kama kinyesi/

I started young kabla sijaitwa Chibudenga/

Enzi hizo naitwa Domo eti siku hizi lips Denda/ Baba Tiffa mnaniita Baba Nillan/

Nasikia naitwa Baba Abdul, kuna mambo mitaani /

Mzuka ukipanda ukate viuno kama Vanga/

Kwa beat ya Kubanda inayobakwa na muuza karanga/

Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi/ Kunicompare na Cinderella haiwezi kuwa fresh/ Simba kutoka mbuga ya Tandale/

Naona swala wanaforce tuwe sare sare/

Viuno vidogo wanataka pensi ya Pepe Kalle/

Si walitaka kiti, nimewapa hadi kitanda wakalale

 

Tazama video chini:

Diamond aeleza sababu ya Alikiba kuwa kwa ofisi yake

Watu wengi wanadhani kuwa Diamond anamchukia Alikiba lakini hii si ukweli wa mambo. Diamond hana chuki na mpinzani wake kwani ata ako na picha ya Alikiba kwa ofisi yake.

Akiongea na Cloud FM, Diamond alieleza sababu ya Alikiba kuwa kwa ofisi yani ni kuwa yeye anawatambua wasanii wote wa Bongo ambao wana mchango mkubwa kwa muziki wa Bongo Flava.

Diamond akiwa kwa ofisi yake na msanii Willy Paul kutoka Kenya. Nyuma yao ni picha kadhaa za wasanii mbalimbali wa Bongo Flava

“Ile siyo ofisi ya Diamond, Rich Mavoko, Harmonize, siyo ofisi ya Tale, ni ofisi ya muziki wa Bongo Flava ambayo imeweka kuona ni kwa namna gani inaweza kuinua muziki wa Bongo Flava. Bongo Flava haikuletwa hapa tu pekee yangu na wana WCB lakini kuna wasanii tofauti tofauti wana mchango wao katika muziki wa Bongo Flava, so tumeweka baadhi ambao wanamchango, tulitamani tuweke wengine wengi lakini nafasi isingetosha, tumechagua wachache ambao wana mchango,” amesema Diamond.

 

Diamond na Alikiba kumenyana Nigeria katika tuzo la AFRIMA 2017

Wasanii kadhaa wameteuliwa katika vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRIMA 2017. Diamond na Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao waliteuliwa katika tuzo hilo ambalo huandaliwa Nigeria.

Diamond na Alikiba wameteuliwa katika kundi moja; Best Male Artiste, Eastern Africa. Tazama listi hio hapo chini:

Best Male Artiste, Eastern Africa

Diamond Platnumz –Eneka (Tanzania)

Sinishaw Legesse – Selam (Ethiopia)

Qritiqual- Malika (Kenya)

Kibrom Birhane – Eskista (ft Nassmbu Barasa)  (Ethiopia)

Henok Mehari Brothers – irkir Yishala (Ethiopia)

Alikiba – Aje (ft M.I)  (Tanzania)

Octopizzo – TBT (Kenya)

Mura K.E – Excuse My Language                (Kenya)

 

Best Female Artiste, Eastern Africa

Julianna Kanyomozi – I Am Still Here (Uganda)

Chess Nthussi – Give it to You (Kenya)

Victoria Kimani – Giving You (ft Sakordie) (Kenya)

Lady Jaydee – Sawa Na Wao (Tanzania)

Venesa Mdee – Cash Madam (Tanzania)

Wayna Wondersonn – You are not Alone (Ethiopia)

Nandy – One Day (Tanzania)

Hii ndo sababu Diamond alirejea Tanzania kwa upesi baada ya kuzika mamake Zari

Diamond alisafiri kuelekea Uganda kwasababu ya mazishi ya mama mkwe wake ambaye aliaga dunia Alhamisi wiki jana akipata matibabu hospitalini.

Mamake Zari – Halima Hassan alizikwa Ijumaa kulingana na itikadi za Kieslamu ambayo inasema wafu wanafaa kuzikwa chini ya masaa 24 baada ya kifo.

Mama mkwe wa Diamond alizikwa Kalama, mji ambao uko katikati ya Uganda. Baba Tiffah alihudhuria mazisho hio huko Kalama.

Diamond akiwa kwa mazishi ya mama mkwe wake

Staa huyo hata hivyo aliabiri ndege kurudi Tanzania siku hio hio ya Ijumaa baada ya mwenda zake kuzikwa. Diamond alirejea Tanzania kwa upesi kwasababu alikua na show Jumamosi pale Leader Club.

“Mitihani ni sehem ya Maisha na Huletwa na Mwenyez Mungu , na Siku zote huletwa kwa sababu, na ndiomaana tumefunzwa kushukuru kwa kila jambo….. Allah nakushkuru kwa yote, Nakushkuru kwa kunifikisha Uganda na Kumaliza kila jambo salama….Naomba pia Uniongoze katika safari yangu hii ya sasa ya Kuelekea Dar es Salaam….na unitie nguvu siku ya kesho nikiwa kazini pale Leader Club… ? @mama_dangote,” Diamond aliandika.

Diamond na mamake wakiwa wanarejea Tanzania

 

Diamond na mamake walivyowasili Uganda kwasababu ya mazishi ya mamake Zari (Video)

Diamond Platnumz tayari amewasili nchini Uganda kumfariji mkewe Zari Hassan ambaye alimpoteza mamake mzazi Alhamisi asubuhi.

Mamake Zari – Halima Hassan aliaga dunia akiwa anapata matibabu katika Nakasero Hospital jijini Kampala. Mwendazake alifariki kutokana na maradhi ya moyo.

Staa huyu wa wasafi alisafiri Uganda na mamake Sanura Sandra Kassim na meneja wake Babu Tale. Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond aliwasili Uganda.

 

Diamond aomboleza kifo cha mama mkwe wake

Zari alimpoteza mama yake mzazi Halima Hassan ambaye aliaga dunia mapema leo Julai 20 akipata matibabu katika hospitali jijini Kampala.

Mama mkwe wa Diamond Platnumz alilazwa Nakasero Hospital kwa takribani wiki tatu hivi, alikua anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Wiki chache zilizopita, Diamond alizomewa na mashabiki wa Zari kwa kukosa kumtembelea mama mkwe wake hospitalini alikokuwa amelazwa.

Diamond na Zari na mama zao

Diamond ata hivyo ameomboleza kifo cha mamake Zari. Staa huyo wa Wasafi aliomba Mungu aweke roho yake marehemu mahali pema peponi.

“Mwenyez Mungu ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi Amini….” Diamond aliandika.

 

Diamond aonyesha jumba lake ambalo liko Nairobi

Diamond tayari anamiliki majumba ya kifahari jijini Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini. Hit maker huyo pia ako na jumba lingine Nairobi.

Baba Tiffah ni miongoni mwa wasanii wenye utajiri mkubwa Afrika. Staa huyo wa Wasafi anapata mapato kutoka kwa muziki wake na biashara anazofanya.

Utajiri wa Diamond unadhihirika kwa majumba ya kifahari anayomiliki Tanzania na Afrika Kusini. Diamond alitumia bilioni kadha kununua jumba jijini Johannesburg.

Diamond akiwa kwa makao yake jijini Johannesburg, Afrika Kusini

Diamond amesisimua watu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akionyesha jumba lake jijini Nairobi, Kenya kwenye video.

“My apartment in Nairobi, call me Mr. Naseeb when am on these type of mission, not Diamond,” Baba Tiffah aliandika kwa video yake.

Tazama video hio hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=kwqyKzPZAVk

 

Barakah The Prince amsifu sana Diamond kuliko Ali Kiba akilinganisha mchango wao kwa muziki

Barakah The Prince anatambua kuwa Diamond and Ali Kiba ndo ndume katika ulingo wa muziki Tanzania. Lakini mwimbaji huyo amekiri kuwa Chibu Dangote ndo ndume kamili.

Barakah aliwataja wasanii watatu ambao wako na mchango mkubwa kwenye muziki; Diamond, Ali Kiba na Ommy Dimpoz.

Akiongea na Bongo 5, Barakah alimsifu sana Diamond ambaye alisema ameweka mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wote nchini.

“Kwa mfano Bongo kwa mtu kama Ommy Dimpoz, Ommy ni package kabisa ya staa, Diamond ni package na Alikiba ni package iliyokabilika ambayo unaona kabisa huyu ni staa kakamilika. Kwa hiyo kwenye muonekano pia hususan mavazi na mwili lazima mtu uwe makini sana. Diamond ni miongoni mwa mtu ambaye anaowasanua sana watu kwenye vitu, nani alitegemea kama Diamond anaweza kuja na Chibu perfume? Hakuna mtu aliyetegemea, lakini jamaa kaka kafikiria watu wanapenda sana kunukia.

Baraka The Prince

“Nampongeza sana Diamond, ni mtu ambaye anatumia nafasi yake aliyopo sasa hivi vizuri. Kwa hiyo sitaki kusema kuwa watu wengi wanafanya kwa kuwa yeye kafanya, no lakini uyeye anaweza akawa anawapa watu mioyo ya kuthubutu. Unajua mtu mpaka kurizki na kuweka hela yake nyingi kwenye brand ya nguo au nini, ujue hapo umerizki na biashara ina mambo mawili, kuna kunyanyuka na kuna kuanguka.

“Mtu mpaka uweze kurizki lazima uone mfano kwa mtu, huwezi kurizki tu, kwa hiyo yeye ni miongoni mwa watu wanaowapa watu moyo na kuona kumbe kitu hiki unaweza kukifanya na kitu hiki na kikawezekana na tukabiga mitonyo na maisha yetu yakawa mazuri,” Barakah alisema.